You are on page 1of 3

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI CHA UMOJA WA


MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA
YA AFRIKA KUFANYIKA TANZANIA
Bunge la Tanzania, wiki hii litakuwa mwenyeji wa Kikao cha 67
cha Kamati ya Utendaji ya Umoja wa Mabunge ya Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Madola [Commonwealth
Parliamentary Association (CPA)] wa Kanda ya Afrika
kitakachofanyika katika Hotel ya Ledger Plaza, Kunduchi
Beach, jijini Dar es Salaam Tanzania kuanzia tarehe 17 hadi 21
Machi, 2015.
Kikao hicho ambacho kitakuwa mahusisi kwa ajili ya kupitia
bajeti ya Umoja huo ya mwaka 2016 na kufanya tathimini ya
maandalizi ya Mkutano wa 46 wa CPA Afrika unaotarajiwa
kufanyika Mjini Nairobi, Kenya mwezi Agosti, 2015,
kitatanguliwa na vikao vitatu vya kamati ndogo za CPA Afrika
kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi, 2015 kabla ya kufanyika kwa
kikao kikuu cha Kamati tendaji tarehe 21 Machi, 2015.
Vikao hivyo vitatu vya kamati tendji vitakavyotangulia ni
pamoja na:
Kikao kidogo cha Kamati ya Wabunge wanawake wa
CPA Afrika [Commonwealth Women Parliamentarians
(CWP)] kitakachofanyika tarehe 18 Machi, 2015
1

Kikao kidogo cha Kamati ya Mipango na Fedha na


Kikao kidogo cha kamati ya Wawakilishi wa Kanda
vitakavyofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 20 Machi,
2015

Aidha kikao hiki cha 67 cha Kamati ya Utendaji ya CPA Afrika,


kitafanyika chini ya uenyekiti wa Mhe. Lindiwe Maseko (Mb)
kutoka Bunge la Afrika Kusini ambaye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati hiyo na kitahudhuriwa pia na:
Rais wa CPA Kanda ya Afrika Mhe. Justin Bedan Njoka
Muturi (Mb) ambaye pia nis Spika wa Bunge la Kenya
Makamu wa Rais wa CPA Kanda ya Afrika Mhe. Santi Bai
Hanoomanjee (Mb) ambaye pia ni Spika wa Bunge la
Mauritius
Mweka Hazina wa CPA Kanda ya Afrika Mhe. Request
Muntanga Mbunge kutoka Bunge la Zambia
Mwenyekiti wa CWP kanda ya Afrika Mhe. Lucia Witbooi
kutoka Bunge la Namibia
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya CPA
Afrika Mhe. Anne Makinda (Mb) ambaye pia ni Spika wa
Bunge la Tanzania
Katibu wa CPA Kanda ya Afrika Dkt. Thomas Kashililah,
ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania
Wawakilishi 6 kutoka Kanda za Afrika ambazo ni Kanda ya
Kati, Kanda ya Mashariki, kanda ya Kusini mwa Afrika
(Wawakilishi 2) na Kanda ya Magharibi (Wawakilishi 2)
Pamoja na wawakilishi 18 kutoka matawi yote ya CPA
Afrika ambayo ni:
Botswana

Ushelishel
Cameroon
i

Siera
Ghana
Leone
Kenya

Afrika
Lesotho
Kusini
Malawi

Swaziland
Mauritius

Uganda
Mozambique

Zambia
Namibia
Nigeria

Rwanda
2

Na
Mwenyeji
Tanzania

Umoja wa Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya


Madola [Commonwealth Parliamentary Association (CPA)]
uliundwa mnamo mwaka 1948 ukijumuisha nchi mbalimbali za
Jumuiya ya Madola.
Jukumu kubwa la Umoja huu ni kuyaunganisha Mabunge ya
Nchi Wanachama katika kuimarisha uwezo wa Wabunge na
Watumishi wa Nchi husika kuhusiana na masuala mbalimbali
yanayohusu Utawala Bora, Demokrasia na Haki za Binadamu.
Huu ni Umoja wenye jumla ya Mabunge 170 na Wabunge
wapatao 17,000 kwa hapa Afrika Umoja huu una jumla ya
matawi 18 ambayo ni Mabunge ya Nchi Wanachama na Matawi
madogo 45 ambayo ni Mabunge ya majimbo ya baadhi ya
nchi. Bunge la Tanzania ndio makao makuu ya Sekretariati
kwa Bara la Afrika.
Imetolewa na:

Dkt. Thomas Kashililah


Katibu Mkuu
Sekretariat ya CPA - Kanda ya Afrika
DAR ES SALAAM
16 MARCH 2015.