You are on page 1of 9

Na MARY GWERA, MAHAKAMA YA TANZANIA

Hivi karibuni, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande


Othman, alifanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua
shughuli za Mahakama katika mikoa ya Tabora na Shinyanga.
Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika mikoa tajwa ililenga katika
kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mikoa hiyo
ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama
kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji
haki nchini.
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na
Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea
hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia
kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika
utendaji kazi wa kila siku.
Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Naibu Msajili-Mahakama ya
Rufani (T), Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama
Kuu anayeratibu Mahakama Kuu, Mtendaji wa Mahakama za
Wilaya na Mikoa na Mtendaji wa Mahakama za Mwanzo nchini.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania,


akisalimiana na Mhe. David Mrango, Jaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Tabora pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Kanda hiyo
na Viongozi wakuu wa Mkoa waliokuja kumpokea alipowasili
mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi, mwenye sare ni Bi. Suzan
Kaganda, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye
alianza rasmi ziara yake mkoani Tabora tarehe.25.02.2015 alipata
nafasi ya kukagua na kuongea na Watumishi wa ngazi mbalimbali
za Mahakama katika mkoa huo ambapo katika vikao mbalimbali
alivyofanya na Watumishi hao ikiwa ni pamoja na Wahe. Majaji na
Mahakimu, Mhe. Jaji Mkuu alisisitiza mara zote juu ya utendaji
kazi kwa kujituma ili kubadili taswira ya Mahakama kwa wananchi
ambao ndio wadau muhimu wa Mahakama.
Akiongea na Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Tabora Mhe.
Jaji Mkuu alieleza kufurahishwa na kasi ya usikilizaji na
umalizwaji wa mashauri katika Mahakama za Mwanzo mkoani
Tabora. Awali; katika taarifa yake kwa Mhe. Jaji Mkuu,
2

Mhe.Yolanda Mallya, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya


Mwanzo Tabora Mjini alimtaarifu Mhe. Jaji Mkuu juu ya mkakati
waliojiwekea wa kumaliza mashauri ya aina yoyote kwa kipindi
kisichozidi miezi sita.
Aidha Mhe. Jaji Mkuu alitumia ziara hiyo ya kikazi kuwaeleza
Watumishi juu ya mikakati ambayo Mahakama imejiwekea katika
kuhakikisha kuwa huduma ya utoaji haki inaboreshwa nchini.
Kwa
hivi
sasa
Mahakama
ya
Tanzania
imejiwekea
mikakati/vipaumbele ambavyo vinalenga kuboresha huduma ya
utoaji haki nchini, na malengo haya inabidi yafanyiwe kazi na kila
mmoja wetu kwa maana ya kila Mtumishi na mdau wa Mahakama
awajibike katika kufikia malengo yetu ya kuboresha huduma ya
utoaji haki nchini. Alisema, Mhe. Jaji Mkuu.
Alivitaja vipaumbele hivyo mbele ya Watumishi kuwa ni;
Uboreshaji wa Masjala za Mahakama; katika hili Mhe. Chande
alisema kuwa Masjala ndio kitovu katika
utendaji kazi wa
Mahakama na kusisitiza kuwa Masjala inabidi ziimarishwe na
kuboreshwa kwa kuzingatia umuhimu wa nyaraka za kesi
mbalimbali zinazohifadhiwa.
Uimarishaji wa ukusanyaji wa takwimu; hili pia ni eneo ambalo
limewekwa kama kipaumbele katika maboresho Mahakamani, Mhe.
Jaji Mkuu alisema Mahakama pia imejipanga vyema kuhakikisha
inakuwa na takwimu sahihi za kesi mbalimbali zilizopo katika
Mahakama mbalimbali nchini ili kuangalia ni sehemu ipi
inayohitaji nguvu zaidi katika kushughulikia mashauri/kezi za
muda mrefu. Alitoa mfano kuwa katika kipindi cha miaka miwili,
wamebaini baadhi ya Kanda kama Tabora, Mwanza, Dar es
Salaam, kuwa na mashauri mengi ya muda mrefu na tayari jitihada
za dhati zimeshafanyika kwa kuwa na vikao maalum (special
sessions) kwa ajili ya kumaliza kesi hizo, hatua hiyo imefanikiwa
kiasi kikubwa kupunguza mashauri ya muda mrefu Mahakamani.
Matumizi ya TEHAMA; Aliongeza kuwa kwa sasa Mahakama
imejielekeza katika Matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) katika kusajili kesi za ngazi mbalimbali
zinazoandikishwa/zinazoletwa Mahakamani.
3

Kwa sasa Mahakama ina mfumo ambao unawezesha kubaini idadi


ya mashauri yaliyofunguliwa katika ngazi mbalimbali za
Mahakama nchini, katika hili Wataalam wetu wa Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (IT) walizunguka takribani nchi nzima
kuwaelekeza Makarani wetu jinsi ya kusajili kesi kwa njia ya
Kompyuta, na hili pia limeleta mafanikio kwa kiasi kikubwa kwani
takwimu na taarifa nyingine za Mahakama zinatumwa makao
makuu kwa urahisi zaidi, alisema Mhe. Jaji Mkuu.
Mafunzo; Mhe. Jaji Mkuu alitaja kuwa Mafunzo pia ni mojawapo ya
eneo lililowekewa msisitizo lengo likiwa ni kuwaendeleza kitaaluma
Watumishi wa Mahakama kwa Mafunzo ya muda mrefu na muda
mfupi ili kuwapa ujuzi na ufanisi zaidi katika utendaji kazi wa kila
siku. Alibainisha kwa miaka miwili (2) sasa, Mahakama imeweza
kusomesha takribani Watumishi 457 katika mafunzo ya muda
mrefu, na watumishi takribani 763 wameendelezwa katika mafunzo
ya muda mfupi. Aliwataka Watumishi kuchukua fursa hiyo
kujiendeleza kwani kwa sasa Mahakama inatoa nafasi kwa kila
Mtumishi wake kujiendeleza kitaaluma.
Uboreshaji wa Miundombinu: miundombinu hii ni pamoja na
majengo ya Mahakama, vitendea kazi n.k, Mhe. Jaji Mkuu alisema
pia katika kuboresha huduma zake Mahakama imejipanga katika
kuboresha miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kujenga majengo
ya Mahakama na kukarabati majengo yaliyochakaa.
Tatizo kubwa ambalo Mahakama inakabiliana nalo ni uchakavu
wa miundombinu yake, kwa hili tuko mbioni kuhakikisha
Mahakama inakuwa na miundombinu bora zaidi, tumejipanga
kuboresha ikiwa ni pamoja na kujenga Mahakama Kuu katika
mikoa yote ambao haina majengo, taratibu zinaendelea na kwa
mwaka huu tumepanga kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika
mikoa ya Kigoma, Lindi, Morogoro, Musoma/Mara etc, na kueleza
kuwa Mahakama kuu Shinyanga iko mbioni kukamilika kwa ajili
ya kuanza kazi rasmi, alieleza.
Uboreshaji wa hali ya Wafanyakazi wa Mahakama; Hili pia ni moja
kati ya eneo ambalo limepewa kipaumbele katika maboresho
yanayoendelea kufanyika ndani ya Mahakama; Mhe. Jaji Mkuu
4

aliwaeleza Watumishi wa Mahakama Tabora kuwa uboreshaji huu


unaangalia upatikanaji wa stahili za Watumishi kwa wakati ikiwa
ni pamoja na nauli za likizo, madeni mbalimbali, uboreshaji wa
mishahara ya watumishi suala ambalo linaendelea kufanyiwa kazi.
Masuala/Matatizo yote yanayohusiana na watumishi tayari
tumeshayabaini, kwahiyo hivi sasa, tunashughulikia masuala yote
kwa wakati mmoja, mfano, kulipa nauli za likizo kwa watumishi
wanaokwenda likizo kwa mwaka husika na kwa wakati mmoja,
alifafanua Mhe. Jaji Mkuu.
Aidha Mhe. Jaji Mkuu aliongeza kuwa suala Maadili na nidhamu
pia limewekewa kipaumbele, alisema kuwa kuna baadhi ya
Watumishi wa Mahakama hawana nidhamu na maadili katika
utendaji kazi, hali hii imesababisha kuwa Mahakama nzima
kutupiwa lawana juu ya utendaji kazi wake.
kuna baadhi ya Watumishi ya watumishi wa Mahakama hawana
maadili na nidhamu hali hii inachafua taswira nzima ya
Mahakama, lazima tuongeze uadilifu, Watanzania wanataka
Watumishi wanaotoa haki, wanaoaminika ili kila mwananchi
aridhike, alisema.

Baadhi ya Watumishi wa Mahakama wa Mkoa wa Tabora wakiwa


katika Mkutano na Mhe. Jaji Mkuu (hayupo pichani) alipoongea
nao juu ya masuala mbalimbali ya kiutendaji alipokuwa kwenye
ziara ya kikazi mkoani humo.
Mapema akimkaribisha, Mhe.Jaji Mkuu katika Mahakama Kuu
kanda ya Tabora, Mhe. Amir Mruma, Jaji Mfawidhi- Mahakama
Kuu (Kanda ya Tabora ambayo inajumuisha mikoa ya Shinyanga,
Kigoma na Simiyu) alimueleza Mhe. Jaji Mkuu kuwa, Mahakama
mkoani Tabora imejiwekea mikakati yake ya kumaliza mashauri ya
muda mrefu ili kwenda sambasamba na maboresho yaliyoridhiwa
na Mahakama nchi nzima ambayo ni kuboresha huduma ya utoaaji
haki nchini.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiongea


na Wahe. Majaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora
alipotembelea Kanda hiyo katika ziara yake ya kikazi.
(kulia,mwenye tai nyekundu) ni Mhe. Amir Mruma, Jaji MfawidhiMahakama Kuu Kanda ya Tabora, pembeni yake (wa kwanza kulia)
ni Mhe. Sam Rumanyika, Jaji, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora,
(wa kwanza kushoto kutoka upande wa Mhe. Jaji Mkuu) ni Mhe.
John Utamwa, Jaji-Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, (katikati), ni
Mhe. David Mrango, Jaji-Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, (wa
kwanza kushoto) ni Mhe. Leila Mgonya, Jaji Mahakama Kuu Kanda
ya Tabora.
Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu alifanikiwa pia kukutana na
kuongea na Wadau mbalimbali wa Mahakama wa mkoa wa Tabora
kama, Polisi; Polisi, Magereza, Mawakili wa Serikali na wa
Kujitegemea, PCCB n.k ambapo alieleza jitihada ambazo Mahakama
inafanya katika kuboresha huduma zake na kuwataka kuonyesha
7

ushirikiano katika kufanikisha upatikanaji haki kila mmoja katika


eneo lake.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo, Sikonge


(aliyenyoosha mkono) akimuonyesha Mhe. Jaji Mkuu kiwanja cha
Mahakama ambacho kitajengwa Mahakama ya Wilaya. Katika
ziara yake mkoani Tabora, Mhe. Jaji Mkuu alipata nafasi pia ya
kutembelea Mahakama ya Mwanzo Sikonge.
Akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Jaji
Mkuu pia alipata nafasi ya kuongea na Watumishi ambapo
aliongelea juu ya vipaumbele vya Mahakama katika kuboresha
huduma zake, akisisitiza kuwa kila mtumishi wa Mahakama ni
chachu katika kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama, hivyo kuna
haja kila mmoja kwa nafasi yake aliyopo afanye kazi kwa bidii na
hatimaye kufikia lengo la kutoa huduma bora.

MWISHO

You might also like