You are on page 1of 6

HOTUBA YA IJUMAA 22/05/2015

AHLULBAYT NDIO SILAHA PEKEE YA KUPAMBANA NA UGAIDI WA


FIKRA DUNIANI
Akihutubia katika Swala ya ijuma iliyoswaliwa leo katika Msiki wa Ghadir
Kigogo, Dar es Salaam Mawlana Sheikh Hemedi Jalala ametoa mkono wa
pongezi kwa Waislamu wote duniani na hususan Imam wa Zama (ATF) na
kiongozi wa Waislamu dunia Sayyid Ali Khamenei kwa Munasaba wa Kuzaliwa
Imam Mtuharifu na Kingozi wa Vijana wa peponi Shahidi wa Karbalaa Hussein
ibn Ali ibn Abii Twalib (sa) ambaye kuzaliwa kwake kunanasibiana na Tarehe
Akiorodhesha baadhi ya matukufu ya Imam Hussein (as) amesema kwamba
huyu ndiye shahidi wa Karbalaa vita vilivyopiganwa baina ya Haki na Batili,
Imam hussein ni imam miongoni mwa maimamu 12 waliotajwa na Mtume
katika hadithi maarufu ya Vizito viwili (Hakika mimi nawaachieni vizito viwili
Kitabu cha mwenyezi Mungu na watu wa nyumba yangu), Hussein ni yule
ambaye mtume anamtambulisha katika Hadithi zake kuwa ni miongoni mwa
Viongozi wa peponi, Hussein ni mtoto wa pili (2) katika watoto wa Mtume
(s.a.w.w) akitanguliwa na kaka yake Imam Hassan (as). Hussein ni miongoni
watukufu wanne (4) walioshiriki katika tukio Maarufu la kihistoria la Mubahala
(Maapizano) na wakristo wa Najran tukio ambalo Allah

(sw) analihadithia

katika Quraan "Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikilia ilimu


hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wake
zetu na wake zenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha
tuombe

kwa

unyenyekevu

tutake

laana

ya

Mwenyezi

Mungu

iwashukie waongo (3:61)


Mawlana Sheikh Jalala amesema ukitaka kufahamu utukufu wa Imam hussein
ni kulisoma vizuri tukio la Maapizano (Mubahala) na hususani radiamali ya
maneno ya Askofu wa kikristo alifajiri palipo pambazuka na kumuona mtume
akija huku katika mikono yake akiwa amembeba Hussein na mkono mwingi
1

akimshika mkono Hasaan, Fatima akiwa nyumba yake na Imam Ali akiwa
nyuma ya Fatuma, alipoona nyuso za watu watano hawa watoharifu wakiwa
upande wa Mtume (saww) katika maapizano hayo
Kiongozi wao Askofu na kusema

ndipo

alipopaza sauti

'Enyi Wakristo! Hakika Mimi naona

nyuso ambazo kama wao watanyanyua mikono yao na kuomba


Mwenyezi Mungu ili auhamishe Mlima kutoka mahali pake, basi bila
ya shaka Atauhamisha mlima huo. Hivyo basi, Msifanye Maapizano
nao, vinginevyo mtaangamia, na hakutabakia Mkristo yoyote juu ya
uso wa

Ardhi, mpaka siku ya ufufuo.

Moja ya nyuso hizo ni uso wa

Hussein huyu tunayesherehekea kuzaliwa kwake alisistiza Mawlana Sheikh


Jalala.
Hussein ni mmoja kati ya watu watano (5) waliofunikwa na Mtume (saww)
katika Shuka (Kisaa) la kiyemeni kisha Mtume akawaombea dua ikawa
sababu ya Allah (sw) kuwasafisha na kuwatoharisha na maovu na machafu
yote kama anavyotufunulia Allah katika (33:33) Hakika Mwenyezi Mungu
anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na
kukusafisheni baarabara. Hussein ni miongoni mwa Watano hao walio
twaharishwa na Kuzuiwa na Maovu na Machafu. Hussein ni miongoni watu
watu wa nyumba ya Mtume (saww) waliotajwa katika Quraan (42:23)
Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi kwa Watu wa
Nyumba yangu.
Hussein huyu amelelewa katika mikono ya Mtume, Sheikh Jalala akasema
kama ni Taasisi ndipo alilelewa Hussein, basi Meneja alikuwa Bi fatma Zahraa
(as), Msimamizi alikuwa Imam Ali (as) na Kichwa/ mkuu alikuwa ni Mtume
(saww), Je fikiria Taasisi hii imemtoa mtoto wa aina gani? aliuliza samahati
Sheikh jalala. Sheikh akaongeza kuwa taasisi hii ya Malezi na ubora wa
waleaji ndio iliyomfanya Mtume kutoa hakikisho kuwa Hassan na Hussein
wawili hao ni viongozi (Maimamu) wakiwa wamesimama (wakipewa
kuongoza) au hata wakiwa wamekaa (wasipopewa kuongoza). Mtume

kuthibitisha mapenzi yake Kwa Hussein amenukuliwa akisema Mimi


nampenda Hassan na Hussein na nyinyi muwapende
Sheikh Jalala akasema kwa yeyote anayetaka kumfahamu vizuri Mtume na
Imam Ali (as) na Amsome kwa ufasaha Imam Hussein hatopata tofauti
yoyote baina yao na kuthibitisha hilo ni kauli yake mwenyewe mtume
aliposema Hussein anatokana na mimi na Mimi natokana na
Hussein Akafafanua sheikh kuwa sehemu ya kwanza ya kauli hii Hussein
anatokana na Mimi ni rahisi kuelewa kwani hussein ni Mtoto wa Imam Ali
ambaye ni ndugu wa Mtume na Mama yake Ni Fatma Zahraa (a) ambaye ni
mtoto wa pekeee wa Mtume. Virozo ni katika sehemu ya pili Iweje mtume
atokane na Hussein? Kisha Mawlana sheikh jalala akafafanua kuwa Mantiki
ya Maneno hayo ni kuwa ukimtizama hussein, Tabia yake, Siasa yake na
Misimamo yake ya Dini, Upole na wema wake Kwa wajane na Masikini wake,
Uchamungu na Unyenyekevu wake kwa Mwenyezimungu. Ushujaa wake
mbele ya Makafiri, maneno yake hayana tofauti na ya mtume na hii ndio
maana ya maneno na mimi natokana na hussein.
Kisha Sheikh Jalala akawaeleza waumini kuwa baada ya mtume kufa Imam
Hussein alibaki chini ya Mikono mitoharifu ya Imam Ali na hapa alichukuwa
mafunzo na Malezi chini ya Imam Ali, haupati tofauti yoyote ya Maisha
aliyoishi Imam Ali (a) na yale aliyokuwa nayo hussein, Matukio ya kihistoria
yanatukumbusha kuwa ni katika kipindi hichi ambacho Imam Ali aliwatoa
watoto wake wawili kwenda kumhamia khalifa wa Tatu Othman ibn Affan pale
alipokuwa amezingira ili kuwawa, Ni imam Ali (a) aliyewaamuru wanawe
akiwemo Hussein kumplekea Maji ya kunywa Othman Ibn Affan pale ambapo
watu walipomzuia maji ya kunywa. Ni hussein na hassan walioshiriki bega
kwa bega na Baba yao katika Vita vya Qaasitin na Maarikini mpaka ukatia
khpofu moyo wa imam Ali juu ya hatari ya kuuwawa wanawe isije ikawa
mwisho wa kizazi cha Maimamu.

Baada ya kufa Imam Ali (as) Imam hussein alibaki chini ya Uangalizi wa Kaka
yake imam Hassan (as) ambaye mbali ya Matatizo ya Utawala wa Muawiya
Ibn Abii Sufiani, lakini Imam hussein alidumu katika kumsaidia kaka yake
mpaka

pale Mauti

yalipompata

kwa

Kuwekewa

sumu na

watumishi

waliotumwa na Muawiya ibn Abii sufian.


Kisha Mawalana Sheikh Hemedi Jalala akazungumzia Masuala yanayojiri leo
Duniani na Kuwatanabaisha waumini kuwa yote yanayotokea leo Duniani
Majibu yake yaliyo sahihi ni kwa watu kumfahamu Imam Hussein kwa
ufasaha, bali watu kuwajua Watu wa nyumba ya mtume ndio suluhisho la
kudumu. Akisistiza alisema leo kama Dunia inataka Uislamu wa kweli, kama
tunataka Amani ya kweli, Utengamano na Wanaadamu wote, Ushirikiano
Mapenzi ya dhati lazima tushikamane na Ahlulbayt watukufu. Aliongeza na
kusema leo dunia inakabilia na tatizo kubwa la Ugaidi wa Kifikra, Watu
wamesomeshwa na kulelewa katika Vyuo vikuu wakijengwa kifikra kupitia
Mitaala iliyoratibiwa barabara na kusimamiwa kwa uhodari wa hali ya juu na
kwa gharama za mabilioni ya fedha za waislamu. Lengo ni kumjenga mtu
ambaye anaamini kuwa yoyote anayetofautiana naye kifikra ni kafiri na
Damu yake kumwagwa ni Tiketi ya kupata pepo. Huu ni Ugaidi wa kifikra.
Tumeona Video zilizosambazwa na Makundi ya ISIS na ISIL wakiwachinja zaidi
makumi kwa mamia ya Wakristo huko Libya, Iraq na Syria kosa lao nini?
Aliuliza Sheikh na Kujibu kosa lao ni hawakubaliani na Fikra za ISIS na ISIL,
Tumeona Maelfu ya ndugu zetu masunni wakiuwawa huko Iraq na Syria kosa
lao ni kutokubaliana na fikra za Magaidi wa ISIS na ISIL, na hata wanapowaua
ndugu zangu Mashia katika miji ya Iraq na Syria sababu ni hiyo hiyo tu
kutofautiana kifikra.
Ebu jiulize Maktaba za Dini, Turathi za kihistoria tunazoshuhudia katika
vyombo vya habari zikichomwa na kulipuliwa kwa Mizinga ya Mabomu,
Maktaba, Vitabu vya Dini na nyumba za Ibada Makaburi ya Maswahaba wa
Mtume kufukuliwa na kuteketezwa, maeneo ya kumbukumbu za historia nayo
yana makosa gani? Ahaa! Utagundua kuwa lengo la Makundi haya ni kufuta
4

kumbukumbu zote za mwanadamu na Dini, Kufuta Ukweli wa Dini za Mungu


Mmoja, Ukweli ni kutaka kuwatawala watu kifikra, fikra zote sahihi zipotezwe
ibaki fikra moja tu, fikra kuwa yeyote asiyekubaliana na Uwahabi
(ISIS/ISIL) sio binaadamu tena hana Dini damu yake ni halali
kumwagwa mali yake ni halali kutaifishwa. Hakuna sehemu kuna
Usalama Duniani iwe Bara la Ulaya, Arabuni hata Afrika, hakuna Nchi iliyo
salama na hapa niwatahadharisha na Viongozi wa Tanzania kuwa Macho na
makundi haya ambayo yanavaa Ngozi ya kondoo yakidi ni Waislamu na huku
ndani yake wakiwa na ngozi ya chui (Magaidi wauwaji wakubwa).
Kisha Sheikh Jalala, akatoa Suluhisho kwa kusema, Kupigana na Ugaidi wa
kifikra unahitaji kuwa na Hazina ya Silaha za Kitaaluma za kuikomboa fikra.
Na kuwa hupat katika dunia ya leo mafunzo ya kukomboa fikra kama yaliopo
kwa watu wa nyumba ya Mtume. Hivyo suluhisho pekee la Amani ya kweli ya
dunia na Vita ya fikra ni kuwaelekea na kushikamana na watu wa nyumba ya
Mtume (saw). Sheikh akawaasa waumini kwa kuwataka kutambua kuwa
Wafuasi wa Ahlulbayt leo duniani wanabeba nyadhifa na Majukumu makuu
mawili jukumu la kwanza ni kuwa Imam wao wa zama aliye hai na anawataka
waisaidie dunia kuwa yenye Amani, upendo na utengamano na jukumu la pili
ni kwa dini yao ya uislamu, Wafuasi wa Ahlulbayt wanadhima mbele ya
Mwenyezi Mungu (sw) kutumia Mafunzo ya Maimamu wao na vipawa vyao
kupambana na Ugaidi huu wa Fikra.
Aidha aliwataka waislamu wote Masunni kufuta fikra kuwa siku moja
wanaweza kuwafanya Mashia wote wawe Masunni au Mashia kudhania kuwa
wanaweza kuwafanya masunni wote kuwa Mashia hili halitawezkana mpaka
siku ya kiama. Masalafi kudhania siku moja watatubadili sote Masunni na
Mashia kuwa masalafi hili haliwezekani ni ndoto ya Mchana, Tofauti zetu
kama Unaamini Uislamu ni kufuga ndevu nyingi na kukata suruali hili
halikuzuii kukaa na yule asiyefuga ndevu na anayevaa suruali ndefu Sheikh
aliuliza Je Ndevu nyingi zinatatizo gani au zinazuia nini kuzungumza na mtu
asiye na ndevu? Lazima watu wakae wajadiliane, wazungumze hatari
5

zinazowakabili na changamoto za Maisha yao. Mwisho akatoa Mshangao


wake kwa Tukio liliotokea hivi karibuni pale moja ya nchi za Africka mashariki
zilipoanza kampeni ya kuandaa Hafla za kuwakutanisha Maimamu na
viongozi wa dini tofauti tofauti kujadili matatizo na chngamoto za jamii zao.
Kirozo ni pale moja ya nchi inayojiita ya kiislamu sasa hivi imeanza kuchukua
vijana wa Kiislamu wa nchi hiyo na kuwapeleka katika vyuo vile vya
kuwaathiri kifikra na kuwafundisha Ukafiri wa Mashia na Uhalali wa kumwaga
damu zao. Akasisistiza kuwa haya yote ni kukosa kumjua na kuyaishi
mafundisho matukufu ya Imamu Hussein, Imam ambaye Kwa tabia njema,
muamala na wasiokuwa Waislamu, msaada kwa wajane

ni sifa alizokuwa

amejipamba, akisifiwa kuwa alikuwa akiamka usiku wa manane na zigo la


chakula akigawanya katika nyumba za wajane, Hakuna kama yeye katika
Uchamungu na kujidhalilisha mbele ya Allah. Mwisho aliwausia waumini
kusoma kwa makini moja ya dua zake Maarufu kama dua ya Arafa ili
wathibitishe

kiwango

cha

uchamungu

wake

na

kiwango

alichokuwa

akinongona kwa udhalili mbele ya Mola wake


Alihitimisha hutuba yake kwa kuwapa mkono wa hongera na fanaka kwa
Waislamu wote kwa kukumbuka kuzaliwa Imam Hussein.