You are on page 1of 7

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Ref. Na EA.7/96/01/H/56

9 Julai, 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 599 kwa ajili ya Katibu mkuu
Wizara ya maliasili na Utalii kama zilivyorodheshwa katika tangazo hili.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.


i.
ii.
iii.

iv.
v.

vi.

Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45


Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya

kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho


hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

vii.

viii.

ix.
x.

xi.
xii.
xiii.
xiv.

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

Computer Certificate

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

Picha moja Passport size ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

Testmonials, Provisional Results, Statement of results, hati matokeo za


kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24 Julai, 2015
Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa


Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya ajira kwa
kuingia sehemu iliyoandikwa Recruitment Portal)
MUHIMU; Waombaji kazi wote mnatahadharishwa kujiepusha na
matapeli wanaojitambulisha kama watumishi wa Sekretarieti ya ajira
kuomba Rushwa kwa baadhi ya waombaji kazi ili kuwapangia vituo
vya kazi.

1.0 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II - NAFASI- 111


Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi
Kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na vibali vya kukamata wanyama
hai
Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori
Kudhibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na kuhakikisha kufuatwa kwa
maadili katika kutumia wanyamapori
Kudhibiti matumizi haramu ya wanyamapori
Kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya uhifadhi wanyamapori
Kuhakikisha viwango vya kukamata wanyama hai kwa ajiri ya biashara na ufugaji
Kufanya kazi za kuzuia ujangili
Kukusanya taarifa na takwimu za uhifadhi
Kutekeleza kazi za uhifadhi katika Mapori ya Akiba
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori kutoka Chuo Kikuu
kinachotambuliwa na serikali
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D. kwa mwezi.
2.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II NAFASI 30
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
kulinda Nyara za Serikali
Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
Kusimamia matumizi ya magari ya doria
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kutunza takwimu zao
Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
Kudhibiti moto katika hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake

2.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya
Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha
Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

3.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (TECHNICIAN) NAFASI 87


Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

1.1 MAJUKUMU YA KAZI


Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya
Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya
Uhifadhi wa Wanyamapori (Technician Certificate in Wildlife Management)
kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo kingine
kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B2 kwa mwezi

4.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA III (BASIC TECHNICIAN) NAFASI 346


Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

1.4 MAJUKUMU YA KAZI


Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
Kusimamia shughuli za uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
Kulinda binadamu na mali zake dhidi ya Wanyamapori
Kukusanya na kulinda Nyara za Serikali
Kufanya usafi na ulinzi wa kambi
Kusimamia uingiaji na utokaji wa watu na mali zao kwenye hifadhi
Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na
kukusanya takwimu zao
Kusimamia taratibu za kusafirisha wanyamapori hai na nyara nje na ndani ya
Nchi
Kudhibiti wanyamapori waharibifu
Kudhibiti moto kwenye hifadhi
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
1.5 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Astashahada ya
awali ya Uhifadhi wa Wanyamapori (Basic Technician Certificate in Wildlife
Management) kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.6 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B1 kwa mwezi

5.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 10


1.7 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandika na kutunza register zinazohusu shughuli za uhasibu.
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
1.8 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au Foundation Level kinachotolewa na


NBAA
1.9 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
6.0 AFISA UTALII DARAJA LA II - NAFASI 15
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na
wadau wote
Kutoa leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii
Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii
Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi
Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau katika uendeshaji wa biashara ya utalii
Kuandaa kaguzi mbalimbali za wakala wa utalii
Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli
Kukagua hoteli, loji na migahawa
Kujibu na kufuatilia malalamiko yanayotolewa na watalii
Kutoa ushauri wa kitaalaam kwa wakala wa utalii
Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/ vituo nchini vya kuingilia/
kutoka kwa wageni
Kutunza kumbukumbu za vitabu/ majalada ya maktaba ya utalii
Kutayarisha taarifa za kila mwezi ya takwimu ya watalii walioingia nchini na
mapato yaliyopatikana
Kufanya tafiti ndogo survey kwenye hifadhi za Taifa na maeneo
Kufuatilia kwa karibu na kushirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo
vinavyotoa mafunzo ya utalii nchini
Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii
Kutayarisha ripoti ya robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima
Kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya sekta kwa kufanya savey
Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kufuatilia utekelezaji wa
maazimio
Kupitia miongozo inayohusu Tourism Facilitation Committee
Kuratibu shughuri za kubuni vivutio utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii
utalii
Kutayarisha na kuhakiki vivutio vya utalii nchini
Kuitisha mikutano/ semina za uhamasishaji kuhusu uendeshaji utalii
Kushiriki katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii

Kushirikiana na Mashirika? Taasisi mbalimbali za mazingira katika shughuri


zihusuzo utalii na mazingira
Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje

6.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wenye Shahada/ Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii, Hoteli,
Uhusiano wa kimataifa, Biashara (masoko) au Sheria (Commercial law) kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na serikali
6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.

X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.