You are on page 1of 3

Wazimbabwe waja kujifunza kilimo cha Tumbaku

Tanzania
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Wadau wa zao la tumbaku kutoka Zimbabwe, wako
nchini Tanzania kwa ajili kujifunza pamoja mambo
mengine, mbinu bora ya kulima zao hilo, ikiwemo
mafanikio ya kilimo cha mikataba kati ya wakulima na
wanunuzi.
Msafara huo wenye wajumbe sita, kutoka Bodi ya
Tumbaku na Masoko ya nchi hiyo (TIMB), ulitembelea
makampuni yote ya ununuzi wa zao hilo hapa nchini,
ambayo yote yana makao makuu yake Mjini Morogoro,
ikiwemo Kampuni ya Tumbaku Tanzania(TLTC) na
Kiwanda cha Kusindika Tumbaku Tanzania (TTPL)
ambayo ni kampuni dada ya TLTC.
Makampuni mengine yaliyotembelewa ni Premium
Active Tanzania, Alliance One and JTI- Leaf Services.
Ujio wa wazimbabwe umekuja wakati wadau wa zao hilo
kusini mwa Jangwa la Sahara, ambapo zaidi ya watu
milioni
10
huishi
kwa
kutegemea
zao
hilo,
wamekubaliana kimsingi kubadilishana uzoefu kwenye
sekta hiyo, ikiwemo mbinu za upandaji miti na
kuboresha uhakika wa chakula miongoni mwa jamii ya
wakulima wa zao hilo.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa
Sheria na Uhusiano wa TLTC na TTPL, Bw Richard
Sinamtwa alisema kilimo cha mikataba nchini kina
manufaa makubwa kwa wadau, wakiwemo wakulima.
Alifafanua kuwa kutokana na kilimo hicho, wakulima
hujipatia mamilioni ya fedha kwenye zao hilo,huku taifa
likiingiza fedha za kigeni sambamba na kuhakikisha zao

lenyewe linalimwa kwa kufuata misingi ya kilimo bora.
Aidha, alisema kwa mtindo huo, zao linakuwa halina
madhara kwenye mazingira, mambo ambayo ni vigezo
muhimu kwenye uuzaji wazao hilo kwenye soko la
dunia.
Kwa mujibu wa Sinamtwa, kilimo cha mikataba hapa
nchini kinaenda sambamba na sera ya serikali
inayowataka wakulima kujinunulia pembejeo zao, huku
soko la zao hilo likisogezwa kwa mkulima kwa bei
ambayo
inaafikiwa
na
kwenye
chombo
kinachotambulika kisheria.
“Maafikiano ya bei hufanyika kabla ya mkulima
hajapanda zao lake.Ukitazama huu mfumo wetu,
utagundua kwamba ni wa kipekee hapa Afrika, kwani
kwingineko wanatumia mtindo wa mnada, hivyo wakati
mwingine kusababisha usumbufu kwa wakulima
ikiwemo mikasa ya soko ya dunia” alisema.
Alieleza kwamba, mfuko huo unaungwa mkono na
serikali, ambapo kupitia Benki Kuu, hutoa dhamana kwa
taasisi za fedha ili ziweze kutoa mikopo kwa wakulima
wa tumbaku, na hivyo kuifanya sekta ambayo ilikuwa
haikopesheki, kuwa yenye kuaminika na kwamba
kiwango cha urejeshaji mikopo kimekuwa cha
kuridhisha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TTPL, Bw David
Crowhurst ugeni huo umepata nafasi ya kujionea namna
zao
hilo
linavyopokelewa
kiwandani
kwake,kuchambuliwa mpaka linavyopangwa kwenye
gredi mbalimbali.
“Wamejionea pia namna tulivyofanya uwekezaji, yaani
baada ya ubinafsishaji na jinsi tulivyoweza kukibadilisha
kiwanda kilichokuwa cha umma kuwa chenye mitambo

ya kisasa.Pia tuna programu nzuri ya usalama mahala
pa kazi na jinsi tulivyoweza kuzalisha ajira kwa wingi,”
alisema
Kwa upande wake, Meneja wa Ufundi TIMB Bw. Blessing
Dhokotera aliushukuru uongozi wa TLTC na TTPL kwa
mafunzo hayo akisema walijionea kiwandani hapo
kimewafungua macho.
“Pamoja na kwamba Zimbabwe inaongoza kwa
uzalishaji wa tumbaku ya mvuke katika Afrika, lakini
bado tunayo mengi ya kujifunza Tanzania, hususani
namna ambavyo TTPL inavyosindika zao pamoja na
kilimo cha mikataba kinavyoendeshwa na TLTC na eneo
la upandaji miti,” alisema.
TIMB ni bodi ya udhibiti na ushauri wa tumbaku nchini
Zimbabwe, huku ikiratibu pia masoko ya na takwimu ya
zao hilo nchini humo.
Kwa mujibu wa Bw Dhokotera jumla ya kilo za tumbaku
Milioni 195.7 zimeuzwa mwaka huu nchini humo tangu
msimu huu uanze mwezi Machi. Kiasi ambacho ni sawa
na Dola za Marekani Milioni $577.