You are on page 1of 9

Sababu Tisa kwanini CCM itashinda katika Uchaguzi Mkuu Jumapili

hii, Oktoba 25
Na January Makamba
Tarehe 25 mwezi huu Oktoba, Watanzania watapiga kura kumchagua
rais wao wa tano, wabunge na madiwani. Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
umekuwa na msisimko mkubwa zaidi tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
siasa za vyama vingi mwaka 1995. Mengi yamendikwa kuhusu uchaguzi
huu, hususan kutokana na hisia kwamba safari hii Upinzani una nafasi ya
kukiondoa madarakani moja ya vyama vikubwa na vyenye muundo bora
barani Afrika, chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM). Matukio
mbalimbali kuelekea uchaguzi huo yameleta shauku inayoweza
kutengeneza hadithi ya kusisimua.
Nikiwa sehemu ya Timu ya Kampeni ya CCM,na kwa manufaa ya wote
ambao wangependa kuwa na mtizamo tofauti, ninatoa sababu 9 kwanini
tunaamini kuwa CCM itaibuka mshindi na kwanini Dkt John Pombe
Magufuli atakuwa Rais ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Ugombea ‘fyongo’ (flawed) wa Edward Lowassa
Ilishabainika kuwa uchaguzi huu ungekuwa mgumu kwa CCM bila
kujali nani angekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Upinzani. Lakini
matokeo ya uchaguzi huu yalielemea upande wa CCM pale Upinzani
ulipomchagua Lowassa kuwa mgombea wao. Ni rahisi kwa CCM
kuchuana na Lowassa kuliko laiti mgombea wa Upinzani angekuwa
Dkt Wilbrod Slaa, ambaye ndiye aliandaliwa kuwa mgombea kabla ya
‘ukusukumwa kando’ na nafasi hiyo kupewa Lowassa. Slaa alikuwa na
uadilifu katika maeneo mengi, na aliaminika. Kwa Lowassa, ni vigumu
na inanyima raha kuchuana na mfumo aliyoshiriki kujenga na ambao
ulikuwa sehemu ya maisha yake hadi Agosti mwaka huu alipohamia
Upinzani. CCM ilikuwa na nafasi ya kumpitisha Lowassa kuwa
mgombea wake wa nafasi ya urais. Hatukufanya hivyo kwa sababu
rahisi tu kwamba ingekuwa vigumu mno kumkabidhi kwa wananchi
mgombea wa matarajio ya baadaye ambaye ni kiashirio cha yale
yasiyowaridhisha wananchi kuhusu CCM. Kuna wanaoamini kuwa
uchaguzi huu ni mgumu kwa vile Lowassa ndiye mgombea wa
1

Upinzani. Sisi twaamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa mgumu
mara kumi zaidi laiti Lowassa angekuwa ndiye mgombea wetu.
2. Upinzani umesalimisha ajenda yake ya kupinga ufisadi
Kipindi cha miaka 10 iliyopita kimetawaliwa na matukio mbalimbali
ya kuwabainisha mafisadi na kuwachukulia hatua. Vyombo vya
habari, taasisi za kiraia na Bunge vimefanya kazi nzuri kushughulikia
suala hilo. Rais Jakaya Kikwete ameweka historia kwa kuamuru ripoti
za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kupatikana kwa
wananchi na kujadiliwa kwa uwazi Bungeni. Waziri Mkuu aliyekuwa
madarakani, si mwingine bali Lowassa, alijiuzulu kwa sababu ya
kashfa ya rushwa. Mawaziri kadhaa walitimuliwa kazi na manaibu
waziri wawili wanatumikia vifungo jela. Huu ni uwajibikaji wa hali ya
juu japokuwa kuna wanaoweza kudhani ni hatua ndogo. Umma
umeamka.
Upinzani ulijenga hadhi yake kwa kuongelewa sana kuhusu ufisadi.
Kilele cha Upinzani kilijiri mwaka 2007 katika mikutano mkubwa wa
hadhara ambapo walitangaza majina 10 ya watu waliowaita mafisadi
wakubwa zaidi, katika kilichokuja kufahamika kama Orodha ya Aibu
(List of Shame). Lowassa alikuwa kinara kwenye orodha hiyo.
Ilitarajiwa kuwa Uchaguzi Mkuu huu uwe ‘hukumu’ kwa CCM kuhusu
ufisadi. Upinzani ulitarajiwa kuitumia ajenda ya ufisadi ambayo
inawagusa watu wengi. Lakini ghafla, kwa kumteua mwanasiasa,
ambaye kwa jitihada zao wenyewe Wapinzani, amefahamika zaidi
kwa ufisadi, iliwalazimu kuzika ajenda hiyo. Kilichofuata baada ya
hapo ni kituko na kichekesho. Wale mashujaa wa mapambano dhidin
ya ufisadi walijikuta wakilazimika ‘kulamba matapishi yao.’ Wengi
wao waliokuwa mahiri katika mitandao ya kijamii walilazimika kufuta
historia ya baadhi ya waliyoyaandika mtandaoni walipokuwa
wakikemea ufisadi, lakini si kabla ya maandiko yao kunaswa kwa
‘screenshots.’ Ulikuwa ni ukweli wa kushangaza. Ni Dkt Slaa na
Professa Ibrahmi Lipumba, viongozi muhimu wa Upinzani tangu
miaka ya Tisini, walioamua kujiuzulu nyadhifa zao kwa kukerwa na
uamuzi wa Upinzani kumpokea Lowassa.Matokeo yake, Upinzani
walijikuta wakichana kadi yao turufu- ajenda dhidi ya ufisadi. Ni nadra
2

kwao kuongelewa suala hilo, na wanapojaribu kufanya hivyo, ni kwa
kujitetea tu.
Jioni moja mwezi Agosti, nilimwona Mbunge wa Upinzani, Peter
Msigwa, katika mdahalo kwenye runinga. Aliongelea kitu ambacho
kilijumuisha mtizamo wa Upinzani kwa muda huo, na kiliniacha hoi.
Alisema, kabla hawajampokea Lowassa, walifanya utafiti wao, na
“ufisadi sio ajenda muhimu kwa taifa letu.” Alidai kwamba wenye
ushahidi
kuhusu
ufisadi
wa
Lowassa
wajitokeze
hadharani.Alionekana kusahau kuwa walipomtaja Lowassa katika List
of Shame, walitangaza hadharani kuwa wana ushahidi. Muda si mrefu
uliopita, CCM ilikuwa ikiwaomba Wapinzani kuleta ushahidi kila
yalipojitokeza madai ya ufisadi dhidi ya viongozi wa chama na serikali
allegations were leveled against the party and its leaders.
Haikupendeza kuingiza hoja za kisheria katika masuala ya kimaadili.
Upinzani sasa umeamua kwa hiari yao kuchukua ‘chembemoyo’
wakati ambapo viongozi wa CCM wanaongelea ufisadi kwa ujasiri na
msisitizo.
Uchaguzi huu Mkuu ni muhimu sana kwa Upinzani. Kimsingi, unaweza
kuwa na madhara makubwa. Endapo watashindwa hapo Jumapili,
‘watapotea’ kwa muongo mzima ujao. Ndio maana inashangaza kuona
wamechukua uamuzi wa kukimbia ajenda yao kuu ya kupambana na
ufisadi ambayo iliwatambulisha na kuwaimarisha. Na kuwapa nguvu
kukubalika kwa wapigakura. Kuona wanatarajia kushinda ni miujiza
mkubwa.
3. Mabadiliko ambayo kamwe huwezi kuyaamini
Ukizinguka jijini Dar es Salaam utakutana na mabango ya Upinzani
yanayodaia “Ni Muda wa Mabadiliko.” Lakini ukisikiliza mikutano yao
ya kampeni, ni porojo na hasira tu. Wasemaji wakuu katika mikutano
hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani na kada wa muda mrefu wa CCM,
Frederick Sumaye na Lowassa mwenyewe. Kwa pamoja, wamekuwa
wana-CCM na katika nyadhifa za juu serikalini kwa zaidi ya miaka 50.
Kwa hiyo inasikitisha kusikiliza kauli zao – zinazokosa imani na
kupalizwa na aibu – wakipambana na mfumo walioshiriki kujenga,
uliojenga tabia zao za kisiasa, na ambao walikuwa wakiusifu miezi
mwili tu iliyopita.
3

Kutokuwa wakweli na kuweka mbele maslahi binafsi kwawatuma
kudai kuwa CCM haijafanya chochote katika miaka miaka 50 iliyopita.
Inapotokea viongozi wawili waandamizi wa chama na serikali kwa
zaidi ya miaka 30, wote wakiwa walioshika Uwaziri Mkuu, kudai kuwa
hakuna chochote kilichofanyika katika miaka 50 iliyopita,
wajihukumu wenyewe. Si kwa muundo, mwonekano au ukweli,
wanasiasa hao wanasimamia mabadiliko. Yayumkinika kuhitimisha
kuwa mabadiliko wanayoongelea ni kuhusu kubadili chombo
kilichowaingiza madarakani, mabadiliko ya sare tu za chama. Hawana
habari na mabadiliko ya maisha ya wananchi wa kawaida. Wapigakura
wameanza kushtukia ukweli huo.
4. Migogoro na mkanganyiko ndani ya UKAWA
Huko nyuma, kila ulipojiri uchaguzi, Upinzani ulijaribu kuunganisha
nguvu ili kuing’oa CCM madarakani.Na kila mara jitihada za
ushirikiano zilishindikana. Mwaka 2014, mjadala kuhusu Katiba Mpya
kuataka serikali tatu uliwapatia ajenda ya kuwaunganisha pamoja.
Kisha wakaamua kutafsiri ushirikiano huo kuwa wa kisiasa,
wakaafikiana kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais na
kugawana majimbo.
Baada ya hapo kukajitokeza unafiki wa wazi. Kuonyesha kuwa
matamanio yaliwekwa mbele ya kanuni zilizopatikana kwa jitihada
ngumu, chama ambacho jina lake linajumuisha maneno ‘demokrasia’
na ‘maendeleo’ kilitemea mate mchakato wake chenyewe wa
kidemokrasia na mshikamano kupata mgombea wake wa urais, na
kukurupuka kumpitisha kada wa muda mrefu wa CCM ambaye
jitihada zake kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho tawala
ziligonhga mwamba.
Waliamini kwamba uamuzi wa Lowassa kuhama CCM ungekiathiri
chama hicho tawala, wakitarajia vigogo kadhaa wangemfuata huo
Upinzani. Badala yake, ujio wake huko ukapelekea kuondoka kwa
wanasiasa wawili waliokuwa nguzo muhimu kwa Upinzani, Dkt Slaa
na Prof Lipumba.Kadhalika, wanachama wengine muhimu waliohama
na kujiunga na chama cha ACT- Wazalendo, ambacho hakikujiunga na
UKAWA.
4

Kana kwamba hiyo haitoshi, makubaliano ya UKAWA kusimamisha
mgombea mmoja kila jimbo yalikumbwa na mushkeli katika majimbo
kadhaa na kupelekea malalamiko yaliyosababisha ugumu katika
kampeni za Lowassa.
Huko Masasi, mgombea mwenza wa Lowassa, Juma Duni, alilazimika
kuokolewa jukwaani baada ya waliohudhuria mikutano wake wa
kampeni kupiga kelele kuwa wataipigia kura CCM. Katika jimbo la
Nzega, Lowassa alilazimika kuendesha ‘kura ya sauti’ kuwauliza
waliohudhuria mikutano wake wa kampeni wanamhitaji mgombea
gani kati ya wawili wa UKAWA waliokuwa wanachuana. Mpango
mzima wa ushirikiano miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA
umekwenda mrama.CCM sasa ipo katika nafasi nzuri ya kujinyakulia
majimbo ambayo vinginevyo yangekwenda kwa wagombea wa
Upinzani.
Lakini kilele cha unafiki wa UKAWA ni hiki. Umoja huo uliundwa ili
kutetea Katiba Pendekezwa iliyoshauri muundo wa Muungano wa
serikali tatu. Kanuni hiyo ya msingi iliwekwa kando pale UKAWA
walipomchagua mgombea wao wa tiketi ya urais, Lowassa, ambaye
alikuwa mtetezi mkubwa wa muundo wa Muungano wa serikali mbili.
Kwa wengi wasioendeshwa na propaganda, uamuzi wa kutelekeza
suala la msingi lililopelekea umoja wa vyama hivyo, kwa ajili tu ya
imani ya kufikirika ya kushinda urais, yaashiria uchu wa madaraka na
sio mabadiliko yanayohubiriwa kwa wananchi.
5. Lowassa kushindwa kufanya kampeni nchi nzima
Lowassa anaonekana kutokuwa na uwezo wa kusafiri kwa urefu na
upana wa Tanzania kufanya kampeni. Mara nyingi amekuwa akitumia
usafiri wa anga kwenda mikoani ambako hufanya mikutano mikubwa
kwenye makao makuu ya mikoa, kutembelea majimbo mawili au
matatu ya jirani kwa helikopta, na kurejea jijini Dar es Salaam. Huko
Tanga, kwa mfano, alifanya kampeni katika majimbo matatu tu kati ya
tisa mkoani humo. Mkoani Ruvuma, alifanya kampeni katika majimbo
matatu kati ya tisa, Kigoma majimbo mawili kati ya manane, na Kagera
majimbo matatu tu.
5

Kinyume chake, mgombea wa CCM, Magufuli amekuwa barabarani
tangu Agosti 23, huku akipumzika kwa siku tatu. Anatumia usafiri wa
gari, akitembelea kijiji baada ya kijiji, na kufanya mikutano kati ya
minane hadi 12 kwa siku. Aina hii ya kufanya kampeni ‘kwa rejareja’
inabaki kuwa nguzo pekee ya kujihakikishia ushindi kwenye uchaguzi
mkuu nchini Tanzania, hususan katika maeneo ya vijijini ambayo
usikivu na kuonekana kwa vyombo vya habari ni mdogo. Wakati
Lowassa anavutia wahudhuriaji wengi katika mikutano yake katika
miji mikubwa, Magufuli anajipatia wahudhuriaji wengi katika kila
kona ya Tanzania. Kama idadi ya wahudhuriaji katika mikutano hiyo
ya kampeni inamaanisha wingi wa kura, basi kwa hakika CCM
itashinda. Lakini tofauti na Upinzani, CCM haidanganyiki na wingi huo
wa wahudhuriaji katika mikutano ya kampeni. Rekodi ya mahudhurio
makubwa ilikuwa ikishikiliwa na Agustino Lyatonga Mrema,
mgombea maarufu wa kiti cha urais kwa tiketi ya Upinzani mwaka
1995 (ambaye pia alijiunga na Upinzani akitokea CCM). Hata hivyo
alishindwa kwenye uchaguzi huo. Sie twategemea kitu kingine.
6. Mfumo imara wa CCM katika uhamasishaji kuanzia ngazi ya chini
kabisa.
Katika Tanzania, vyama vichache mno vinavyoweza kuchuana na
uwezo wa CCM kuhamasisha wananchi. Wakati Wapinzani huhadaiwa
na ‘mahaba’ wakati wa kampeni za uchaguzi, mahudhurio makubwa
kwenye mikutano yao ya kampeni na vichwa vya habari magazetini,
CCM hutumika nguvu yake ya kimuundo na kuwasha ‘mashine zake za
kisiasa,’ kuanzia ngazi ya mtaa (ujumbe wa nyumba kumi) kwa nchi
nzima. Kimuundo, jumiya ya wanawake wa CCM (UWT) pekee ni
kubwa kuliko Chadema, chama kikuu cha upinzani. CCM Haihitaji
kusafiri ili kufanya kampeni. CCM ipo kila mahala, ikifanya kampeni
katika makundi madogo, vijijini na mitaani, kila siku na mbali ya upeo
wa vyombo vya habari. Kwa wanaofahamu muundo wa chama hicho,
ushindi kwake si jambo la kushangaza.
Kwenye miaka ya 1950s, wakati wa harakati za kusaka uhuru kutoka
kwa mkoloni, uwezo wa TANU kuhamasisha ulikuwa nguzo muhimu
kwa Tanganyika kupata uhuru wake.CCM imerithi vinasaba vya TANU.
Mwalimu Nyerere aliijenga CCM kuwa imara kwa nyakati kama hizi.
Mwaka jana, huku umaarufu wake ukiwa umepungua, CCM ilimudu
6

kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa kwa asilimia 80 dhidi ya umoja
Huohuo wa Upinzani inaokabilina nao katika uchaguzi huu
Mkuu.Tofauti haipo kwenye nini kinachoonekana kwenye vyombo
vya habari au mitandao ya kijamii bali jinsi gani makada wa chama
hicho tawala walivyofanya uhamasishaji katika kila mtaa na kijiji.
Uchaguzi huo wa serikali za mitaa, ambao hufanyika mwaka mmoja
kabla ya uchaguzi mkuu, hutoa dalili nzuri kuhusu matokeo ya
uchaguzi mkuu.
7. Umahiri wa Dkt Magufuli
Mwaka jana, baadhi ya waandishi wa habari walikiri kwamba ni
vigumu mno kumshambulia na kumshinda Dkt Magufuli. Ana rekodi
imara ya usafi, uchapakazi na anayetaka kuona matokeo sahihi.
Hajawahi kuvutiwa na harakati za kisiasa, na ilikuwa mshangao
alipotangaza kuwania urais. Na alipotangaza, hakufanya mbwembwe
wala kijitangaza kwenye vyombo vya habari. Alizingatia kanuni za
chama kwa ukamilifu. Dkt Magufuli analeta kumbukumbu za
mgombea mwingine aliyekuwa hajulikani mwaka 1995 - Benjamin
Mkapa. Wakati umaarufu wa CCM ukiwa chini, huku ikikabiliwa na
upinzani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu aliyehama kutoka chama
hicho tawala, CCM ilimchagua turufu yake ambayo ilikuwa ngumu
kuikabili.Miaka 20 baadaye, ikikabiliwa na upinzani wa Waziri Mkuu
maarufu wa zamani aliyehama chama hicho na kujiunga na Upinzani,
CCM imefanya tena ‘vitu vyake.’ Siku zote, CCM hujua ‘kufanya pigo la
haja.’
8. Ufanisi wa CCM katika maeneo ya vijijini
Mimi ni Mbunge wa jimbo lisilo mjini, lenye idadi ya wastani ya
wapigakura. Mwaka 2010, katika uchaguzi ulionekana kuwa mgumu,
CCM ilishinda jimbo langu kwa asilimia 80., na kitaifa kwa asilimia 61.
Hivi sasa, tunatarajia ushindi wa CCM kuwa wa asilimia 90 hivi.
Tanzania ina majimbo kadhaa yaliyo kama jimbo langu. Upinzani
hupenda kuwapuuza wananchi katika majimbo yasiyo ya mijini, kama
jimbo langu, kwa kudai kuwa wanaichagua CCM kutokana na ujinga
wao. Wasingeweza kukosea zaidi ya hivyo.

7

Popote walipo, watu hupiga kura kulingana na mahitaji yao. Mwaka
2000, vijiji vinne tu katika jimbo langu ndivyo vilikuwa na umeme.
Leo, vijiji 44 vina umeme. Japo hatujaweza kutoa huduma zote kwa
kiwango cha kumfurahisha kila mtu, lakini hali halisi yaonyesha wingi
wa wanafunzi mashuleni, walimu zaidi, madaktari na manesi zaidi,
zahanati nyingi zaidi zimejengwa, huduma za mawasiliano ya simu
zinapatikana kwa wingi, barabara nyingi za lami, nk. Porojo kuwa
hakuna kilichofanyika Kwahiyo wapigakura wasiichague CCM
haieleweki katika maoneo hayo ambay kimsingi ndiyo yenye
wapigakura wengi. Na wagombea wa CCM wanaposema watafanya
zaidi
ya
waliyokwishafanya,
kwa
kuzingatia mafanikio
yaliyokwishapatikana, wananchi wanawaamini. Hotuba za kampeni ni
mwonekano na mantiki.
Chaguzi sio kuhusu ahadi tu bali jinsi gani ahadi hizo zitaandaliwa na
kutekelezwa. Jukwaa ambalo kila chama kitanadi ajenda zake za
uchaguzi hujengwa wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama husika.
Yahitaji mtu kuangalia tu uzinduzi wa kampeni za za Lowassa na
Magufuli. Lowassa aliongea kwa dakika 9 tu - akiahidi, pamoja na
mambo mengine, kuwaachia huru wabakaji (sio kama ninazusha hili)
wanaotumikia vifungo vyao na watuhumiwa ugaidi wanaosubiri kesi
zao. Bila kujali alikuwa na malengo gani wakati anatoa ahadi hizo,
makosa hayo hayastahili msamaha wa rais. Kwa upande wake,
Magufuli aliongea kwa dakika 58, akielezea kwa undani ajenda za
maendeleo katika nyanja za elimu, ajira, afya, ufisadi, huduma za maji,
na miundombinu. Kuanzia hapo, kwa muda wote wa kampeni,
mwenendo umekuwa hivyo, kwa uzito wa ujumbe kwenye hotuba
zake na muda wa kuhutubia
Wanaohudhuria mikutano ya Dkt Magufuli huondoka katika mikutano
hiyo wakiwa na matumaini na wenye nguvu. Kwa upande mwingine,
wahudhuriaji katika mikutano ya Lowassa huondoka wakiwa
wamekanganywa. Siku ya kupiga kura, wapigakura wanamkumbuka
jinsi mgombea alivyoonekana na alivyoongea, na jinsi walivyojisikia
walipomwona jukwaani. Kwa kigezo hiki, ni bora ningekuwa upande
wa Magufuli.
9. Uongo, uongo na takwimu
8

Tanzania haina utamaduni wa kura za maoni kupima nafasi za
wagombea katika uchaguzi. Tuna utaratibu wa muda mrefu wa kupata
maoni ya wananchi katika maamuzi makubwa ya kisera – kuingia
mfumo wa vyama vingi vya siasa, marekebisho ya Katiba, na
kadhalika. Mwaka 2005, kulifanyika kura ya maoni, iliyobashiri
ushindi mkubwa kwa CCM. Na kwa hakika, CCM ilishinda kwa asilimia
80. Mwaka 2010, kura ya maoni iliyoendeshwa na kampuni ya IpsosSynovate iliashiria kuwa idadi ya kura za CCM ingepungua hadi kufikia
asilimia 61. CCM ilipinga matokeo ya kura hiyo ya maoni ikidani kuwa
yalikuwa kiasi kidogo sana. Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama
yalivyotabiriwa katika kura hiyo ya maoni. CCM ilipata asilimia 61 ya
kura zote.
Hivi karibuni, kura mbili za maoni zilichapishwa. Zote zilifanywa na
taasisi huru zinazoheshimika. – Twaweza and Synovate-Ipsos tenazote zikijihusisha na utafiti wa kusaka maoni. Taasisi mbili tofauti,
zilizotumia mbinu tofauti za kufanya utafiti, katika nyakati tofauti,
matokeo yaleyale. CCM itashinda kwa asilimia 62 ya kura zote.
Inaruhusiwa, na kwa yumkini ni jambo zuri, kupingana na sababu hizi
tisa za kwanini CCM itashinda. Lakini namba zina tabia ya
ukandamizaji. Ndio mwelekeo wa kura huwezi kubadilika. Lakini kwa
kuzingatia yote yaliyokwishaongelewa kuhusu kinachodaiwa kuwa
ufuasi mkubwa kwa Upinzani, basi muda huu ingetarajiwa tuwa
tunajadiliana kuhusu ufuasi wa wengi kutoka Upinzani kuelekea
CCM– na sio kutarajiwa ufuasi wa wengi kutoka CCM kuelekea
Upinzani. Na ndiyo, kura za maoni zaweza kukosea, na tusiwekee
mkazo sana.Lakini hoja hii sasa ndiyo hupendelewa zaidi na upande
unaelekea kushindwa kwenye uchaguzi.
January Makamba ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM, na msomaji wa Kampeni za CCM

9