You are on page 1of 20

www.annuurpapers.co.tz au facebook:annuurpapers@yahoo.

com

Sauti ya Waislamu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1205 SAFAR 1437, IJUMAA , NOV. 27 - DES. 3, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Ujio wa 'ukafiri' katika dini...

Wazanzibari wapaza sauti
White House Washington

Mtihani wa kwanza kwa Rais Magufuli
Dini sasa kufundishwa kama taaluma…
Yadaiwa ‘Ibada’ hazijengi mshikamano
Masheikh wasubiriwa kupitisha muswada

Kwa haya ya Afande Msangi…

Zanzibar
inaelekea
kubaya
Baada ya Karume kuwavusha salama…
Wanaelekea kutangatanga Jangwani
Saamiriyyu wanawavuruga

MAALIM Seif Sharif Hamad.

ALHAJ Mzee Ali Hassan Mwinyi.

ANNUUR NEW.indd 1

DKT. Aman Abeid Karume.

DKT. Ali Mohamed Shein.

WA Z A N Z I B A R I
tutafakari
na
k u j i h a d h a r i .
T u m t a m b u e
‘ S a a m i r i y y u ’
tumuepuke.
“Hatutoi Nchi kwa
K a r a t a s i . Wa k i t a k a
wapindue”, ni kauli za
akina ‘Saamiriyyu’.
Hao ni pamoja na wale
ambao wanatuambia
kuwa katika watoto
pacha, ‘yule wa
Jamhuri’ halali, ila
mwenzie ‘Zanzibar’,
mwanaharamu.
Bila uamuzi wa busara
na kurejea kwenye haki
na ukweli, tutaonja joto
ya jiwe la Bani Israil.
Kutangatanga
Jangwani miaka arobaini
tukitafuta ‘nchi’,
Amani na Maendeleo,
hatutaipata.
Tu t a z a m a k a t i k a
Idhilali na hatutapata wa
kutunusuru wala kuona
mlango wa kutokea.Uk.9

11/26/2015 6:13:19 PM

Makala

2

Mafundisho ya Qur’an Aal Imran: 64

Fethullah-Gulen

SEMA enyi watu wa
kitabu njooni kwenye
neno lililo sawasawa
katikati yetu na kati
yenu – nalo ni kwamba
tusimwabudu yeyote
isipokuwa Mwenyezi
Mungu na tusikishirikishe
naye kitu chochote, na
wa s i f a n ye b a a d h i ye t u
kuwafanya baadhi kuwa
wa u n g u , k i n y u m e c h a
Mwenyezi Mungu” [AaliImrani 64].
Kuufanya msimamo laini
mbele za watu wa kitabu ni
amri katika amri za Qur’an.
Siyo watu wa kitabu tu, bali
Mwenyezi Mungu mtukufu
alimwamrisha Mussa (a.s.)
aseme maneno laini kwa
Firauni;
“Sema naye maneno
laini huenda akaonyeka au
akamcha Mwenyezi Mungu”.
[Twaha 44]
Kwa msingi huo, maneno
magumu hayana nafasi kabisa
katika Uislamu au kulaumu
kwa nguvu kuwalaumu
watu katika kuwaita kwa
Mwenyezi Mungu.
Na aya iliyo juu ni
k i e l e l e z o k i k u b wa c h a
maneno laini yaliyokaribu
na nyoyo za watu na maneno
yenye kuvutia katika kutoa
ujumbe. Iwapo tutaufikiria
Uislamu kuwa ni ngome
a m b a y o i m e z u n g u s h wa
kuta zinazojengeka katika
mipaka ya Mwenyezi Mungu,
hapana shaka kwamba kuna
milango mingine ya ngome
hiyo na kuna njia nyingi
sana kwa idadi ya viumbe
zinazowezesha kufika
kwenye milango hiyo. Na
unasimama Uislamu na
njia yake maalumu kwa
kuwakumbatia watu katika
njia yoyote katika njia hizo na
katika kituo chochote katika
vituo hivyo ili kuwarahisishia
kuingia katika mmoja katika
milango hiyo. Kwa hakika
kutokuwa wazi kwa hatua
hizi au kutolielewa jambo hilo
kumewaongoza baadhi ya
watu huko nyuma na mpaka
sasa bado kunaendelea
kuwaongoza kwenye makosa
yanayojulikana.
Aya hii inawapokea watu
wa kitabu, katika kimoja
c h a v i t u o v ya n j i a h i z i
na inajisogeza kwao kwa

ANNUUR NEW.indd 2

uso wenye bashasha na
maneno matamu mazuri
na inawaambia: “Njooni
kwangu – elekeeni kwangu”
Wakati inapowasemesha
hivyo, inawaambia: Kwa
hakika lile ambalo ninawaita
kwenye hilo si jambo jipya
juu yenu na si kitu ambacho
hamkijui, bali kitu hicho ni
kile ambacho mmekwisha
kukijua na mmekizoea
huko nyuma. Isipokuwa
kinawezekana kwenu
mkawa mmekisahau au
mmekikumbuka, kwa fursa
ya makosa”.
Na mfano wa miito kama
huu, unajenga daraja kati
yetu na watu wa kitabu na
unazigusa nafsi zao kwa
upande ambao wanaliwazika
nao. Utaratibu huu katika
kulingania kwenye Uislamu
ni muhimu sana. Mnaweza
mkauita kwa msemo ambao
ulienea katika masiku
haya kwa kuita “Njia ya
majadiliano”. Ndiyo kwa
hakika wito wa Uislamu
kwa watu wa kitabu, kwenye
nukta ambayo imezoeleka
kwao kunawezekana
kuufupisha wito huo katika
tamko moja fupi, kwa sababu
Qur’an imetaka kwao kitu
kimoja tu nacho ni kulivuka
daraja hili linaloonekana
mbele ya macho yao na kufika
kwenye mlango huu. Pindi
tutakapoyaweka mambo
yote pembeni kwani tamko
“Sawaa – lililo sawa sawa –
peke yake linaelezea eleweko
hili la kina ambalo ni laini na
ukunjufu wa kifua na raghba
katika kujenga madaraja ya
kipekee na sifa za daraja hili.
Hapa
tunaona
k wa m b a Q u r’a n b a d a l a
ya kuzungumzia kuhusu
kujishughulisha na
kulitolea taarifa jambo
ambalo limethibitishwa,
inajishughulisha na
kulionyesha lile ambalo
limekanushwa mbele ya
macho. Kwa hiyo inaingia
katika maudhui haya kwa
sura ifuatayo: Kwanza ni
kwamba watu wa kitabu
walikuwa wanamjuwa
Mwenyezi Mungu, kwa
m f u m o wa o m a a l u m u ,
isipokuwa ni kwamba
baada ya kupita kwa zama
nyingi, vumbi lilipanda juu
ya maarifa haya ambayo
yalipoteza mtizamo wake na
upya wake. Kwa sababu hiyo,
lilikuwa ni jambo la lazima
kusimama upya kazi ya
kusafisha na kutwaharisha.
Itakapokamilika kazi hii,
zitadhihiri katika hali ya
kuwa wazi mbele ya macho
yote. Na kunawezekana

kuona kazi hii ya usafishaji
katika sentensi hii.
“Tusimwambudu yeyote
asiyekuwa Mwenyezi
Mungu”.
Maana ni kwamba,
Uislamu unaanza kila kazi
kwa kitendo cha kusafisha
na kutwaharisha. Kwa hiyo
huzisafisha akili na fikra
zenye makosa na mambo
ya kiovyo na unayasafisha
macho na kupondoka na
wakati inapotaja kwa kusema
“A s i ye k u wa M we n ye z i
Mungu”, Qur’an inasimama
kabla ya kukitolea taarifa
kitu ambacho ni chanya.
Inasimama na kazi ya kifikra
na kazi ya kiakili, bali huenda
ikasimama na kazi ya kifursa
upya. Kwa msingi huo, aya hii
badala ya kusema :
“Na tufanye hivi na vile”
inasema; “Tuacheni tusifanye
kitu kadha”.
Ndiyo, watu wa kitabu
b a a d h i ya o wa l i p o t o k a
kwa sababu ya kupita kwa
zama nyingi wakaelekea
kwenye kumshirikisha
Mwenyeiz Mungu,
wakaanza kumhusisha
Mwenyezi Mungu mtukufu
na watoto wanamume na
watoto wanawake, mfano
wao, mfano wa wale wenye
kuabudu masanamu na
wakaingia pia katika mambo
yasiyoeleweka ya makosa
mfano wa kusema kwamba:
moja ni tatu, na tatu ni moja.
Wakawapa wana wazuoni
wao na watawa wao uwezo
wa kimungu. Mfano wa
kukubali toba ya ushirikishaji
na mengine katika ibada.
Na msemo ambao amekuja
katika aya kuhusu kufanya
kwao wanawazuoni wao
na watawa wao waungu
kinyume cha Mwenyezi
Mungu, unafungamana
na mambo ya maisha ya
kila siku, na unathibitisha
kwamba wao hawamiliki
haki ya kuweka sheria. Kwa
msingi huo, Qur’an inaanza
kwa kuzisafisha nyoyo na
akili na kuzitwaharisha na
kumshirikisha Mwenyezi
Mungu mtukufu na kuelekeza
ibada kwake yeye peke yake
tu. Kunapasa kuwa swala na
swaumu na Hijja na zakat,
ni kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu. Na kutolewa sadaka
na wanyama wanaochinjwa
kwa ajili yake peke yake.
Hapa wanaweza kusema
watu wa kitabu kwa urahisi
kabisa kwa “hakika sisi yote
haya tunayafanya katika
njia ya Mwenyezi Mungu.”
(Maelezo juu ya aya hii
yataendelea wiki ijayo.)

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 27
B

M

W

A

K

A

W

A

T

E

M

B

O

A

K

A

S

S

I

M

J

U

M

A

N

A

M

A

B

D

A

L

L

A

S

A

L

U

M

B

I

B

R

A

H

I

M

A

L

I

S

A

O

B

I

L

A

L

H

I

S

H

A

M

U

O

Z

U

B

E

Y

R

A

W

A

M

N

L

2

H

A

M

Z

A

A

B

U

B

A

K

R

6

A

B

U

T

A

L

I

B

U

M

A

R

8

S

A

H

A

B

A

25

35

45

40

20

30

A

U

S

T

R

A

L

I

A

1

0

0

0

MASUALA
1.Walioshi na Mtume (SAW) wakiwa wa Islamu wanaitwaje? Jawabu:
Sahaba.
2.Mwaka aliozaliwa Mtume (SAW) waitwaje? Jawabu: Mwaka wa Tembo.
3.Ami yake Mtume (SAW) jina lake. Jawabu: Abu Talib
4.Mtume Muhammad (SAW) alipomuoa Bibi. Khadija alikuwa na umri
gani na Bibi Khadija akiwa na umri gani? Jawabu: 25 Mtume (SAW) 40 Bi.
Khadija.
5.Jina la ami yake Mtume Muhammad (SAW) aliouwawa katika vita vya
Uhud. Jawabu: Hamza
6.Majina ya watoto wa kiume wa Mtume Muhammad (SAW. Jawabu:
Kassim, Abdalla, Ibrahim.
7.Chakula alacho mnyama Panda. Jawabu: Bamboo.
8.Mnyama Kangaroo maarufu anaonekana nchi gani? Jawabu: Australia.
9.Millennium 1,000 au 10,000 au 1,000,000. Jawabu: 1,000
10.Mwanadamu ana mbavu ngapi? Jawabu: 2

N

A

T

I

O

N

O

F

I

S

L

A

M

A

L

M A

I

D

A

A

Y

A

3

M

A

A

W A

H

I

D

N

A

U

R

U

M

C

S

J

U

M A

A

L

K

H

A

M I

S

U

I

J

U

M

A

M O

S

I

N

A

K

A

L

B

A

Q

A

R

A

Y

A

125 45

3

6

A

S

A

12 56 24 35 33 23 33 43 11

22

I

A

N

D

I

O

B

A

S

I

O

570 CE 4

B

L

A

C

K

M

U

S

L

I

M

I

A

K

U

A

K

W A

K

A

S

I

N

MASUALA
1.Uislamu ni dini: (i)Inayopungua idadi kila siku (ii) Inakua kwa
kasi, (iii) Ina idadi kubwa Asia.
2.Uislamu unaruhusu kuoa mpaka wake wangapi? 1, 4, 0.
3.Mtume Muhammad kazaliwa mwaka 570 CE, 670 CE, 622 CE.
4.Vugu vugu la Waislamu Weusi Marekani linajulikana kama,
Nation of Islam, Black Muslim, Elijah Muhammed.
5.Waislamu walio wengi wanaonekana barani Africa, Asia, Ulaya?
6.Mtume (SAW) alikuwa hana mke mwengine alipoishi na Bibi
Khadija binty Khuwayld. Ndio au Sio?
7.Mtume alikuwa na umri wa miaka mingapi alipofariki mama
yake? 3, 6, 12.
8.Uislamu una pinga haki za mwanamke na inasisitiza
ukandamizwaji wa Wanawake. Ndio au Sio?
9.Quran imeteremshwa kwa kipindi cha miaka 23, 33, 43.
10. Aya ipi ilioelezea kuwa “Leo nimekukamiliishieni Dini
yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni
UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila
ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu

Jee Unajua?

1. Misikiti 10 yenye haiba duniani wa mwanzo ni AlHaram uliopo Makka ukifwatiwa na Al-Masjid an-Nabawi
uliop Madina, Al-Aqsa-Palestina, Hassan II-Morocco, Sultan
Omar Ali Saifuddin-Brunei, Masjd Zahir-Malaysia, Masjid
Faisla-Islamabad/Pakistan, Taj ul uliopo Bhopal nchini India,
Masjid Badshaihi uliopo Lahore Pakistan na MAsjid SultaSingapore: http://www.wonderslist.com/10-most-beautifulmosques-in-the-world/
2. Nchi 10 zenye Waislamu wakazi wengi duniani
inayoongoza kuwa na idadi kubwa ni nchi ya Indonesia
ikifwatiwa na Pakistan, India, Bangladesh, Misri, Nigeria,
Iran, Uturuki, Algeria na Morocco: http://malaysiandigest.
com/features/555150-10-countries-with-the-largest-muslimpopulation-in-the-world.html au link hii: http://www.
mapsofworld.com/world-top-ten/world-top-ten-countrieswith-largest-muslim-populations-map.html
3.
Nchi inayoongoza kuwa na Waislamu wengi barani
Afrika kwa asilimia (%) inayoongoza ni Mauritania ikiwa na
asilimia 100, ikifwatiwa na Libya 99.8, Algeria 99.7, Comoro
98, Sudan 97, 96 Djibouti, 95 Niger, Misri 95: http://www.
muslimpopulation.com/africa/
4. Katika nchi za Ulaya Albania inaongoza kuwa na
asilimia kubwa ya Waislamu ikiwa na idadi ya asilimia 79.9
(%) ikifwatiwa na Bosnia Heregzovinian 60.06, Macedonia
34.9: http://www.muslimpopulation.com/Europe/

11/26/2015 6:13:22 PM

3
Na Mwandishi wetu
Washington-Mzalendo.
net

M S H I N D I
wa uchaguzi
atangazwe.”
“ M a a m u z i
ya
Wazanzibari
yaheshimiwe.” “Bila haki
hakuna Amani.”
Wakati vikao vya siri
v ya k u t a f u t a s u l u h u
ya m z o z o wa k i s i a s a
visiwani Zanzibar vikiwa
vikiripotiwa kuendelea,
juhudi za kuupatia
ufumbuzi mzozo huo
zimefika Ikulu ya Marekani
(White House).
Wanachama wa Jumuia
ya Wazanzibar wanaoishi
nchini Marekani (ZADIA)
kutoka majimbo tofauti
nchini humo, wakionyesha
m a b a n g o ya o m n a m o
Novemba 21 waliandamana
hadi kwenye Ikulu ya nchi
hiyo ikiwa ni katika juhudi
za kutafuta uingiliaji kati
wa kimataifa ili kuupatia
suluhisho mzozo huo.
Akizungumza na
waandishi wa habari mbele
ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti
wa Jumuiya hiyo iliyoandaa
maandamano hayo Bw.
Omar Haji Ali, alisema
kuwa maandamano
h a y o ya m e k u j a i k i wa
ni juhudi za Jumuiya
hiyo kutafuta uingiliaji
kati wa kimataifa katika
kuukwamua mgando wa
kisiasa visiwani Zanzibar.
Bw. Omar Haji, alisema
kuwa maandamno hayo
pia yalikuwa na lengo la
kumkumbusha Rais Barack
O b a m a wa M a r e k a n i ,
kutekeleza ahadi yake
ya kuilinda demokrasia
Barani Afrika.
“Katika hotuba yake
aliyoitoa kwenye Makao
Makuu ya Umoja wa Afrika
mapema mwaka huu, Rais
Obama alisema “... pale
ambapo raia hawawezi
kutekeleza haki zao, basi
ulimwengu una jukumu
la kukemea. Na Marekani
itafanya hivyo, hata
kama wakati mwengine
itakuwa inauma...”, Bw.
Ali alikumbusha k wa
kunukuu matamshi ya
Obama.
Aliongeza kuwa
Wananchi wa Zanzibar
wameshindwa kutekeleza
haki yao kwa zaidi ya nusu
karne sasa na kwamba,
wakati umefika sasa kwa
u l i mweng u k uch ukua
jukumu lake.
“ Wa k a t i u m e f i k a
sasa kwa Marekani
siyo tu kukemea, lakini
pia kuchukua hatua za
kivitendo ili kuhakikisha
kuwa sauti za Wazanzibari

ANNUUR NEW.indd 3

Habari

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Wazanzibari wapaza sauti
White House Washington
Kura zao, maamuzi yao yaheshimiwe
Mshindi wa uchaguzi mkuu atangazwe

zinasikilizwa na
kuheshimiwa,” alisema.
Mwenyekiti huyo wa
ZADIA alipoulizwa ni hatua
gani watakazochukuwa
iwapo Serikali ya Marekani
haikuchukua hatua yoyote
kusaidia kumaliza mgando
wa k i s i a s a Z a n z i b a r ,
alisema wana imani na
Rais Obama na tayari
wa m e m f i k i s h i a b a r u a
ya malalamiko yao na
wanachosubiri ni jibu lake.
Alisema, imani yao ni
kuwa atachukua hatua
madhubuti, hususan
ikizingatiwa kuwa
Ubalozi wa Marekani
nchini Tanzania ulikuwa
wa kwanza kutoa taarifa
kuelezea kuwa uchaguzi
wa Zanzibar ulikuwa wa
haki na huru.
Aliongeza kuwa iwapo
hali itaendelea kubaki
kama ilivyo, basi ZADIA
itaelekea kwenye Umoja
wa Mataifa.
Katika maandamano
hayo yaliyowashirikisha
pia wapenda amani na
demokrasia kutoka sehemu
mbalimbali ulimwenguni,
waandamanaji walibeba
mabango yaliyokuwa na
maneno kama vile “Mshindi
wa uchaguzi atangazwe”,
“maamuzi ya Wazanzibari
yaheshimiwe”, “bila
haki hakuna amani’ na
mengineyo.
Aidha waandamanaji hao
walipaza makelele wakidai,
“tunataka matokeo yetu ya

uchaguzi..”
Akizungumza na
Swahilivilla, raia mmoja
wa Marekani aliyeshiriki
kwenye maandamano hayo
alisema, “Nilimpeleka
mwanangu kwenda
kusoma kule, bado ana
mapenzi na Zanzibar

“Mshindi
wa u c h a g u z i
atangazwe.”
“Maamuzi ya
Wazanzibari
yaheshimiwe.”
“Bila haki hakuna
Amani.”
na amenisimulia habari
nzuri za amani, utulivu na
ukarimu wa watu wake.
Amekuwa akifuatilia hali
ilivyo, na kwa hamasa
kubwa alipopata habari
za maandamano haya,
akaniomba tuje kuwaunga
mkono Wazanzibari katika
kudai haki yao”
“ T u t a f a n y a
maandamano kuitaka
S e r i k a l i ya M a r e k a n i
kuingilia kati na kuweka
shindikizo kwa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ili mshindi
aliyeshinda atangazwe na
serikali ya umoja wa kitaifa
i u n d we Wa z a n z i b a r i ,
washirikiane wajenge nchi
yao,” alisema mmoja wa
Wazanzibari anayeishi

Marekani.
Wananchi wa Zanzibar
wa l i p i g a k u r a k a t i k a
uchaguzi mkuu wa Oktoba
25 mwaka huu, lakini
Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) Bw. Jecha Salum
Jecha, baadae Oktoba
28 alitangaza kufutwa
uchaguzi huo Mkuu
visiwani humo katika hatua
za mwisho za majumuisho
ya kura, kitendo ambacho
wa t a a l a m u wa S he r i a
wamesema kuwa
kinakwenda kinyume na
Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona
kuwa hatua hiyo ya
Bw. Jecha ilikuja wakati
asilimia kubwa ya
matokeo yaliyokuwa
yameshatangazwa
yalikuwa yamempa
ushindi mgombea wa urais
wa Zanzibar kutoka chama
cha upinzani CUF, Maalim
Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa
kwa uchaguzi huo ambao
wachunguzi wa nje na
ndani waliulezea kuwa
ulikuwa wa haki na huru,
kimezua mtafaruku wa
kisiasa visiwani Zanzibar,
na juhudi za ndani na nje
zimekuwa zikifanyika ili
kumaliza mgogoro wa
kisiasa visiwani humo.
N o v e m b a
1 9
Wazanzibari wanaoishi
nchini Uingereza walikuwa
wa m wa n z o k u f a n ya
maandamano katika nchi

za nje, wakidai haki ya
k u t a n g a z wa m s h i n d i
katika uchaguzi mkuu
wa Zanzibar uliofanyika
Octoba 25 mwaka huu.
Maandamano hayo
yaliandaliwa na Jumuiya
ya Z a n z i b a r We l f a r e
A s s o c i a t i o n ( Z AWA) ,
ambapo wazanzibari hao
kutoka maeneo mbalimbali
katika miji ya nchi hiyo
wa l i k u s a n y i k a k a t i k a
eneo Downing Street,
iliko Ofisi ya Waziri Mkuu
wa U i n g e r e z a , D a v i d
Cameron na uongozi huo
kukabidhi barua yao yenye
malalamiko ya kutaka suala
la Zanzibar lishughulikiwe.
Wa z a n z i b a r i h a o
walivalia nguo za rangi
nyekundu na buluu,
huku wengine wakiwa
wamebeba mabango yenye
maandishi mbalimbali na
picha za Mgombea Urais
wa tiketi ya Chama Cha
Wananchi (CUF) Maalim
Seif Sharif Hamad,
wa l i o n e k a n a wa k i wa
n a f u r a h a wa k a t i wa
maandamano hayo.
Maandamano hayo
yamefanyika kwa lengo la
kuongeza shinikizo kwa
mamlaka ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania
kuchukua hatua za haraka
ya kuhakikisha Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
i n a k a m i l i s h a k a z i ya
kutangaza matokeo ya
uchaguzi huo.
B a r u a
h i y o
iliyowasilishwa na Rashid
Ali, ambaye ni kiongozi
w a Z AWA w e n y e w e
wanaamini kwamba suala la
Zanzibar litashughulikiwa
ili wananchi wa Zanzibar
waweze kuendelea na
maisha yao ya kawaida.
Mwakilishi wa ZAWA,
Hassan Khamis alisema
wa m e a m u a k u p e l e k a
barua kwenye ofisi za
Waziri Mkuu wakiamini
suala hilo litashughulikiwa
ikiwa pamoja na serikali ya
Tanzania kuchukua hatua
madhubuti na za haraka
katika kushughulikia suala
hilo ambalo limewaweka
wazanzibari roho juu.
“Tunaumia tukisikia
ndugu zetu wa Zanzibar
wana mgogoro mwengine
uliotokana na uchaguzi
kwa sababu ni miaka
mingi kulikuwa na hali
kama hiyo miaka mitano
nyuma kukatafutwa
Maridhiano lakini sasa
tunarejea nyuma miaka
15 iliyopita, haipendezi na
pia inatutia sisi wasiwasi
ambao tupo mbali na
ndugu zetu,” alisema
m m o j a wa wa n a wa k e
walioandamana.

11/26/2015 6:13:22 PM

4

Tahariri

AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM.
E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk
Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

www.annuurpapers.co.tz

Baraza la Mawaziri kigezo
isiwe ukongwe serikalini

R a i s k u m t e u a Wa z i r i
anayepimika kwa matokeo
ya utendaji wake na wenye
maono thabiti juu ya taifa
lake ni bora na vizuri zaidi.
Mtendaji wa serikali bora,
a n a ye p i m a m a t o k e o ya
utendaji wake na mwenye
maono thabiti juu ya nchi
yake, ni dhahiri ataweza
kutatua na kupunguza kero
nyinyi zaidi, kuliko yule
atakayeteuliwa kwa ‘mazoea’
na ambaye amedhihirisha
kufanya kazi kwa ‘mazoea’
huko alikopita.
Katika ulimwengu
wa s a s a wa u s h i n d a n i ,
ulimwengu unaomlazimu
kila mtu kusaka kwa udi
na uvumba mafanikio kwa
ajili ya mustakabali mzuri
wa maisha yake, familia na
jamii kwa ujumla. Viongozi
wanatakiwa kuacha
kuongoza kwa mazoea, lakini
pia Watanzania wanatakiwa
kuacha kuchagua viongozi
wao kwa mazoea.
Habari za kujuana katika
kusaka watu wa kuongoza
taifa au katika utendaji
serikalini na katika jamii
k wa u j u m l a , h a b a r i z a
kupeana nafasi kwa kigezo
cha ‘huyu ni mwenzetu’ ,
ametumikia chama muda
mrefu nk. ni chanzo cha
uzembe na sababu kubwa
ya kuua taifa kiuchumi
na maendeleo ya jamii na
hatimaye kudhoofisha ustawi
wa wananchi wengi.
Ukiacha sintofahamu
iliyopo Zanzbar, tayari
Tanzania kumeshafanyika
Uchaguzi
Mkuu,
waliochaguliwa, hususan
Rais, wabunge na madiwani.
Hawa tunaweza kusema ni
viongozi waliochaguliwa na
wananchi wenyewe na kwa
namna moja au nyingine,
watakuwa wakiwajibika
moja kwa wananchi
waliowachagua.
Lakini wapo viongozi
n a wa t e n d a j i wa k u b wa
wa serikali, ambao pamoja
na kwamba wengine
wanatokana na hao hao
wabunge, lakini wanapewa
m a m l a k a ya k i u t e n d a j i
serikalini na Rais.
Kwamba Rais anateua
Mawaziri na Manaibu Waziri
watakaokuwa wanamsaidia
kazi. Wao ndio watakaokuwa
wapangaji, waidhinishaji,
watendaji, wafuatiliaji na
wasimamizi wa rasilimali
za serikali zinazoelekezwa
kwa ajili ya maendeleo ya
wananchi.

ANNUUR NEW.indd 4

Hapa ndipo tulipoona
kuna haja ya kupasemea japo
katika kiwango cha kutoa
maoni yetu.
Kwa wale ambao
watabahatika kuteuliwa
kuwa Mawaziri au Manaibu
M a wa z i r i , k wa h a k i k a
wanapaswa kuacha mara
moja kutekeleza majukumu
yao kwa mazoea. Na mwanzo,
ishara aliyokwisha kuonesha
Mheshimiwa Rais, huenda
ikaleta mageuzi makubwa
katika utendaji wa serikali.
K wa m t a z a m o w e t u ,
tuliona kwamba viongozi
wetu waliotangulia,
walikuwa wakiteua wasaidizi
wao kwa mazoea. Yaani
kigezo cha uteuzi mara
kadhaa kimeonekana kama
ni ‘uswahiba, fadhila, ufariki,
udugu, ukanda, ukereketwa
wa kiitikadi na hata wakati
mwingine udini umetumika
kwa kificho.
Na tunapozingatia kuwa
m a z o e a h u g e u k a k u wa
kawaida, tuna maana wengi
wa Mwaziri wa serikali
zilizopita walizoea kufanya
kazi kwa hiari zaidi na
hakuna aliyewabughudhi
hata pale walipovurunda.
Ndio maana tumeshuhudia
wakati mwingine watendaji
hawa wakiitwa ‘mizigo’ na
kusababisha serikali kuitwa
dhaifu nk. Kwa kuwa
pamoja na kupewa nafasi,
walishindwa kabisa kutoa
matokeo yaliyokusudiwa.
Badala yake waliingizia
serikali katika hasara.
Awamu hii kuna haja ya
Rais John Pombe Magufuli,
kuepukana na yale mazoea
ya kuteua watendaji kwa
mazoea na kisingizio kikawa
n i u z o e f u n a u k o n g we
serikalini. Kwamba mtu
fulani amekaa muda mrefu
akitumikia serikali au
chama itoshe kuwa tiketi ya
kuteuliwa.
Tunadhani msingi wa
mtendaji mzuri anayeteuliwa
na Rais ni matokeo ya kazi
yake na si uzoefu wa kukaa
serikalini au katika chama
kwa muda mrefu bila kupima
matokeo.
Tunaamini kabisa kwamba,
wengi wanaotenda kwa
mazoea, ndio wanaofanya
ufisadi kwa taifa letu kwa
kuwa wamebweteka ndani
ya mfumo zaidi ya miaka 40,
hawakuwa na matokeo na
hakuna aliyehoji.
Tunaamini kazi kama ndio
msingi mkuu wa maendeleo
na mafanikio. Na kwa kupitia

kazi bora ndio tutaweza
kujenga jamii bora na yenye
m a e n d e l e o . Tu n a a m i n i
kwamba kazi ndio italeta
maendeleo binafsi na ya jamii
kwa ujumla.
Hatuamini kwamba kuna
njia ya mkato ya kufikia
m a f a n i k i o ya k u d u m u
ambayo haihusishi kazi.
Hatuamini kwamba misaada
inaweza kutuletea mafanikio
kama Taifa, kama watendaji
hawatakuwa tayari kufanya
kazi kwa ubunifu na kupima
matokeo ya kazi zao.
Hakuna kikwazo kikubwa
cha mafanikio kwenye kazi
kama kufanya kazi kwa

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015
mazoea. Watendaji wabunifu,
waliopata nafasi kwa umahiri
wao, ni hamasa mpya katika
utendaji wa serikali na mara
zote wanakuwa na shauku
ya kufanya kazi ili kuendelea
kuweka rekodi ya mafanikio.
Ni matarajio yetu kwamba
Rais Magufuli, safari hii
hatakuwa Rais wa kulipa
watu fadhila, si waliofanya
naye kampeni, wala hatajali
wale alikuwa amezoeana nao
katika Baraza la Mawaziri
lililopita.
Tunakumbuka wakati
wa kufunga kampeni kule
M wa n z a , R a i s m s t a a f u
alisifia sana kituo kimoja

cha televisheni kwa
kumsaidia sana kumpigia
kampeni, hivyo akamshihi
Magufuli katika ufalme wake
asimsahau Bosi wa huyo wa
vyombo vya habari.
Tu s e m e t u k w a m b a ,
u t e n d a j i h u p i m wa k wa
matokeo. Bila shaka Rais
Magufuli anawajua watendaji
wanaojali matokeo, wateue
utasalimika.
U k i f u a t a u s h a u r i wa
‘usimsahau fulani’ wakajaa
maswahiba, ‘mwenzetu’,
utaunda serikali ya walipwa
fadhila nawe utaishia
kukarabati serikali kipindi
chote cha miaka mitano.

Mtihani wa kwanza kwa Rais Magufuli
Na Mwandishi Weti

SERIKALI imetoa
‘mwongozo’ wa ufundishaji
na ujifunzaji wa somo la dini
ambao unaondoa masuala ya
ibada.
Mwongozo huo na ‘sera’
hiyo mpya ya ufundishaji
wa Somo la Dini kwa watoto
wa shule za msingi, utakuwa
mtihani wa mwanzo kwa
Rais Dr. John Pombe
Magufuli kwani ni jambo
ambalo lilikwisha kupingwa
na Wakristo na Waislamu
l i l i p o l e t wa n a s e r i k a l i
zilizotangulia.
Mwongozo huo ambao
utatumika katika kuandaa
mitaala ya usomeshaji wa
Somo la Dini katika elimu
ya msingi (darasa la I-VI),
unaelekeza kuwa “Somo
la Dini lifundishwe kama
taaluma na si ibada.”
Hoja ya serikali ni
kuwa ibada haiwezi
kuwaunganisha Watanzania
wa dini tofauti, bali kuwaletea
chuki, mifarakano na hata
kuleta uvunjifu wa Amani.
N a k wa m a a n a h i y o ,
kinachotakiwa sasa ni Somo
la Dini kufundishwa kwa
lengo la kuwaunganisha
Wa t a n z a n i a we n ye
Imani tofauti za kidini ili
kuwafanya wapendane na sio
kuwafanya wanafunzi kuwa
‘wachamungu’ kwa mujibu
wa dini zao.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizopatikana kutoka
Islamic Education Panel,
chombo kinachohusika na
kuandaa mitaala na vitabu
vya usomesjaji wa Somo
la Dini ya Kiislamu, hivi
sasa serikali kupitia Taaasisi
ya Elimu Tanzania (TET)
ishasambaza mwongozo huo
kwa wadau wa Elimu na hivi
karibuni kitaitishwa kikao
cha kuupitisha na kuubariki
mwongozo huo.
Wadau
muhimu
wanaotarajiwa kuitwa katika
kikao hicho ni taasisi kuu za
Kiislamu na zile za Kikristo.
Awali kulifanyika kikao
ambapo taasisi hizo zilipewa
kabrasha la Mwongozo huo
na kuambiwa kwamba mara
baada ya uchaguzi mkuu
wataitwa tena ili kuupitisha.
Hata hivyo, taarifa kutoka

Islamic Education Panel (IEP)
zinasema kuwa, katika kikao
cha awali, ambapo wadau
kutoka taasisi za kidini
walishiriki, mpango huo wa
serikali ulipingwa.
S e r i k a l i i k a s h a u r i wa
kuacha suala la nini
kifundishwe, waachiwe
wenye dini.
Kwa upande wake
Islamic Education Panel
wa m e m wa n d i k i a b a r u a
Kaimu Mkurugenzi, Taasisi
ya Elimu Tanzania, wakijenga
hoja za kutokukubaliana na
mpango huo.
“Baada ya kupitia kwa
makini mwongozo uliotajwa,
tumegundua kuwa unalenga
kuweka mfumo wa watoto
wetu wadogo wa shule
za msingi wa dini tofauti
wafundishwe dini moja.
Kwa msingi huu na kwa
kuitakia mema nchi yetu,
tunapinga mwongozo huu
wa ufundishaji na ujifunzaji
wa somo la dini katika elimu
ya msingi (darasa la I-VI) ”
Imeanza barua ya IEP
kuweka hoja ya msingi ya
pingamizi inayofichua lengo
linalokusudiwa kabla ya
kunyumbulisha sababu
nyingine.
Kuhusu hoja kuwa Somo
lifundishwe kama taaluma,
IEP wamesema kuwa “ni
jambo lisilowezekana
kumfundisha
mtoto
mdogo taaluma ya dini bila
kumfundisha ibada.”
Na kisha kusisitiza kuwa
watoto wasipofundishwa
Ibada, haiwezekani
kuwajenga kimaadili kwa
sababu “ibada na kumuabudu
Mwenyezi Mungu ndio

msingi wa maadili.”
“Watoto wadogo wa shule
ya msingi kufundishwa elimu
ya dini ili wawe waumini
wazuri wa dini kwa mujibu
wa imani zao ni jambo jema,
ambalo litawaimarisha pia
kuwapenda na kuwahurumia
watu wengine, hata kama sio
raia kwani wote ni waja wa
Mwenyezi Mungu.”
Imesema sehemu ya barua
ya IEP kwa Mkurugenzi
Taasisi ya Elimu ambayo
imenakiliwa kwa Baraza
la Maaskofu, Jumuiya ya
Kikristo Tanzania na Katibu
Mkuu, Wizara ya Elimu.
Barua hiyo ya hivi karibuni
ikaongeza kuwa ni jambo
lisilokubalika, mwalimu
Muislamu kuwafundisha
watoto wadogo wa shule ya
msingi wa Kikatoliki Elimu
ya dini ya Kikristo au
kinyume chake, kwa hoja tu
kwamba anaifundisha kama
taaluma.
IEP iliongeza hoja hiyo kwa
msingi kwamba kama Somo
la Dini litafundishwa kama
taaluma, ina maana anaweza
k u c h u k u l i wa m wa l i m u
Muislamu akafundisha
somo la Dini ya Kikristo na
kinyume chake.
Ikasisitizwa katika barua
hiyo kwamba “Mwalimu
mahiri wa wa Elimu ya Dini
ya Kikatoliki, lazima awe
Mkatoliki mzuri anayeakisi
mafundisho ya dini hiyo”, na
sio tu mwalimu japo akijua
Biblia vizuri lakini si mfuasi
wa dini hiyo.
Na kwamba mwalimu
wa namna hiyo atakuwa
anafundisha mambo
a s i y o ya a m i n i n a h i v y o
hawezi kumuathiri mtoto
kimalezi.
Katika hoja ya serikali ya
kuhusisha dini na uvunjifu
wa Amani, IEP wanatoa hoja
kuwa machafuko mengi
yanayosababisha uvunjifu
wa Amani na hata ukitizama
hapa nchini, ni kwa sababu
za kisiasa.
Wanasema, matukio mengi
ya uvunjifu wa amani na
hata watu kupoteza maisha,
yaliyojiri nchini baina ya
2010 na 2015, yametokana
na uchochezi na mihemko
ya kisiasa.

Inaendelea Uk. 9

11/26/2015 6:13:23 PM

Habari za Kimataifa

5
Na Shaaban Rajab

W

AKATI wazee wa
Tanzania wakiishi
maisha ya taabu
katika uzee wao, wakiishi
bila kuwepo huduma
za matuinzo za serikali,
wakikosa hata huduma za
matibabu licha ya kuwepo
mpango wa matibabu
bure kwa wazee, waja
wazito na watoto, serikali
ya China imekuwa mfano
wa kuigwa kwa kuenzi
maisha ya wazee.
Serikali ya Tanzania
kwa muda mrefu
imeshindwa kuwa na
sera zinazotekelezeka za
kuwahudumia wazee.
Serikali wala haionekani
kushughulishwa na suala
zima za kuwahudumia
wazee wetu, licha ya
kutumia nguvu zao
nyingi kuzaa na kulea
kizazi cha sasa cha
watanzania. Kutumia
nguvu zao kutumikia
Taifa letu katika nyanja
mbalimbali za kihuduma
na kimaendeleo. Leo
wanaachwa na wastani
wa umri wao wa kuishi
umeshuka kutokana na
kukosa huduma nzuri za
malezi.
Hata zile kambi chache
za kuwatunza kama ile
ya Nunge Kigamboni na
ile Funga Funga iliyopo
mkoani Morogoro, badala
ya kuwa mfano mzuri wa
kuwaenzi wazee wetu kwa
kuwapa huduma nzuri na
bora za malezi, zenyewe
zimegeuka kuwa mfano
kambi za kuwadhalilisha
babu na bibi zetu. Wanaishi
kwa kutegemea majaaliwa
ya wale wanaojisikia kutoa
misaada na sadaka. Kwa
kutizamama mifano ya
kambi hizi mbili za serikali,
hakuna mtanzania ambaye
anatamani mzee wake
akaishi huko kwa udhalili.
Serikali imeshindwa
kutambua ukweli kwamba
kila mtoto au kijana wa
leo ni mzee wa kesho.
Kwa msingi huo ni wajibu
serikali kuandaa sera ya
kulea wazee pamoja na
kuweka mazingira safi na
salama ya kuwawezesha
wazee kuishi maisha ya
stara na salama hata baada
ya nguvu zao za uzalishaji
kwisha.
Licha ya kwamba
desturi na utamaduni
wa kitanzania haujazoea
kuwatunza wazee
katika vituo vya
serikali, lakini ni ukweli
usipopingika kwamba
kama kungekuwepo na
huduma za kuridhisha
za wazee katika vituo
vichache vilivyopo, wezee
wengi wangehifadhiwa
huko. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba si kila
familia inaweza kuishi na
kuwatunza wazee wao.
Kuna haja ya serikali
yetu, kwa makusudi kabisa
kujifunza kwa swahiba

ANNUUR NEW.indd 5

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Maisha ni marefu China
Yaongoza kwa idadi ya wazee
Lakini serikali imemudu kuwalea

WAZEE nchini China.
wake mkubwa China,
namna ilivyoweza kutoa
huduma na kusimamia
maslahi ya kimaisha ya
wazee wake.
Katika miaka ya hivi
karibuni, China imejizatiti
kikamilifu kukabiliana na
ongezeko kubwa la watu
wenye umri mkubwa,
hali iliy olazimu nchi
hiyo kufikiri namna ya
kuwatunza wazee hao.
Imeelezwa kuwa
ongezeko la wazee China
limetokana na mabadiliko
katika muundo wa idadi
ya watu, kutokana na
utekelezaji wa sera ya
mtoto mmoja.
Aidha kuongezeka kwa
kiwango cha maisha na
kuboreka kwa huduma
za afya, wachina kwa
sasa wanaishi kwa muda
mrefu, hali ambayo
imefanya idadi ya wazee
kuongezeka.
Hata hivyo ongezeko
hilo la idadi ya wazee
limeleta changamoto
nyingine nchini humo,
ambayo ni namna ya
kuwatunze wazee hao.
China ni nchi yenye
watu bilioni 1.3, na ni moja
kati ya nchi ambazo idadi
ya wazee inaongezeka kwa
kasi. Hivi sasa wananchi
wa China wenye umri
wa zaidi ya miaka 60
wamefikia watu milioni
144, idadi ambayo ni nusu
ya idadi ya wazee wa bara
zima la Asia.
Inakadiriwa kuwa
hadi kufikia mwaka 2020,
idadi hiyo inatarajiwa
kuongezeka na kufikia

watu milioni 100. Wakati
idadi ya wazee ikiongezeka,
namna ya kuhakikisha
wa z e e wa n a i s h i k wa
raha mustarehe ni suala
linalofuatiliwa na jamii ya
China.
Maisha ya raha
mustarehe kwa wazee si
kama tu yanahusu chakula,
bali pia yanahusu afya
ya kisaikolojia. Pamoja
na matatizo mbalimbali
yanayosababishwa na
uzee, wazee pia wamekuwa
wakikabiliwa na tatizo
la kisaikolojia, hususan
wazee ambao waume au
wake zao walishafariki
dunia, wanasumbuliwa na
upweke na hofu ya kifo.
Wazee wanaonekana
kuwa na huzuni na ni
rahisi kukosa matumaini
ya k u e n d e l e a k u i s h i .
Kwa hiyo katika miaka
ya hivi karibuni suala
l a k u wa t u n z a wa z e e
k isa ik olojia lime a n z a
kuzingatiwa katika jamii
ya China, lengo likiwa ni
kuwasaidia waondokane
na upweke unaotokana
na kukosa mawasiliano na
jamaa na marafiki zao.
Katika eneo la
kuendeleza uchumi na
teknolojia la Taifa huko
Tianjin, mji uliopo pwani
ya Kaskazini mwa China,
kutokana na ushauri wa
serikali ya lilianzishwa
shirika la wazee, ambalo
linafanya shughuli
mbalimbali za maonesho
ya sanaa na michezo katika
makazi.
Hivi sasa shirika hilo
lina wanachama zaidi ya

elfu moja, na asilimia 95
ya wazee wanaoishi katika
e n e o h i l o wa m e wa h i
kushiriki kwenye shughuli
mbalimbali zilizoandaliwa
na shirika hilo. Wazee
wa huko walieleza kuwa,
kila ifikapo siku ya wazee
ambayo ni siku ya jadi
katika jamii ya China,
sherehe kubwa inafanyika
katika eneo hilo na kila
mwanachama wa shirika
la wazee anapewa zawadi
ya maua.
Shirika hilo la
wazee pia lilianzisha
vikundi mbalimbali
vinavyoshirikisha wazee,
vikiwemo vikundi vya
baiskeli, mpira wa meza,
dansi, wanamitindo
wazee, upigaji picha na
kwaya.
S h i r i k a
linawahamasisha wazee
kufanya shughuli
mbalimbali kama vile
kusafiri kwa baiskeli
k u z u n g u k a k a n d o ya
bahari nk.
Kutokana na shughuli
za namna hiyo, wazee
wamekuwa na matumaini
makubwa zaidi ya maisha.
Pamoja na maendeleo
yaliyopatikana katika
shughuli za kuwahudumia
wazee, serikali ya
China imeweka bayana
changamoto zinazoikabili
katika kutimiza lengo
la kuhakikisha wazee
wanaishi kwa raha
mustarehe.
Kuongezeka kwa idadi
ya wazee kumeongeza
mzigo kwa mfumo wa
kuwahudumia wazee.

Kwa mujibu wa takwimu,
kwa kila wazee elfu moja
wa China wana vitanda
10 tu katika vituo vya
kuwatunza wazee, huku
idadi hiyo ya vitanda ni
kati ya 50 na 70 katika nchi
zilizoendelea. Asilimia
60 ya wazee wa China
wanaishi katika maeneo
ya vijiji, ambapo mifumo
ya kuwahudumia wazee,
matibabu na hifadhi ya
jamii bado haijakamilika.
Serikali ya China imetoa
ahadi kwamba, itaendelea
kutenga fedha zaidi katika
hifadhi ya jamii, hatua kwa
hatua kukamilisha mfumo
wa kuwahudumia wazee
unaowanufaisha wananchi
wote na unaolingana na
maendeleo ya uchumi na
jamii ya China, ili wazee
ama wanaoishi mijini au
vijijini waishi kwa raha
mustarehe.
Naibu Mkurugenzi
wa ofisi ya kamati
inayoshughulikia mambo
ya wazee ya taifa ya China
Bw. Li Bengong, alifafanua
mpango wa China katika
miaka kadhaa ijayo.
Katika kipindi kati ya
mwaka 2006 na 2010,
vilitimizwa vigezo
kadhaa halisi. Kwa
mfano kuongeza vitanda
milioni 2.2 katika vituo
vya kuwatunza wazee
wanaoishi vijijini, ambao
hawana kipato wala uwezo
wa kufanya kazi.
Aidha serikali katika
ngazi mbalimbali ilipanga
hatua kwa hatua kuongeza
fedha zinazotumika
katika ujenzi wa vifaa
vinavyowahudumia
wazee, elimu ya wazee,
utafiti wa sayansi
u n a o h u s u wa z e e , n a
shughuli mbalimbali
zinazowashirikisha wazee,
lengo likiwa ni kuhakikisha
wazee wanaishi kwa raha
mustarehe. CRI
Awali serikali ilitoa
waraka kuhusu maendeleo
ya s e k t a ya h u d u m a
ya wazee nchini China
ulitolewa tarehe 12 mwezi
Desemba 2006 Beijing.
Waraka huo uliainisha
kwamba katika miaka ya
karibuni idadi ya wazee
nchini China inaongezeka
kwa kasi.
Ili kukabiliwa na
changamoto hiyo, serikali
ya China ilichukua hatua
za kiuchumi, kisheria na
kiutawala kuhakikisha
maslahi na haki ya wazee
na kuhimiza maendeleo ya
shughuli za utoaji huduma
kwa wazee.
Waraka huo wa serikali
unaeleza mambo saba
yanayohusu kuongezeka
kwa kasi idadi ya wazee
nchini China, ujenzi wa
mfumo wa dhamana kwa
wazee na kuimarisha
dhamana kwa stahili na
maslahi ya wazee.
Hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka 2005, idadi
Inaendelea Uk. 15

11/26/2015 6:13:28 PM

6

Hoja ya Juma Kilaghai

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Unataka kuiba fedha kihalali? Anzisha Benki!
Kiasi cha miaka 20 au 25
iliyopita, niliwahi kusoma
kitabu cha hadithi cha
m wa n d i s h i m m o j a wa
Kimarekani anayeitwa Mario
Puzo. Huyu ni mwandishi
wa hadithi moja maarufu
sana duniani inayoitwa
'THE GOD FATHER'. Na
kama ilivyokuwa katika
h a d i t h i ya ' T H E G O D
FAT H E R ' , m a u d h u i ya
hadithi ninayoizungumzia
pia yalikuwa yanahusisha
harakati za genge la uhalifu
la MAFIA.
Katika hadithi hiyo
niliyosoma, ambayo
nadhani kichwa chake cha
habari kilikuwa kinaitwa
'FOOLS DIE' au 'ORMETA',
sikumbuki vizuri kipi ni
kipi, kuna kauli ya mmoja wa
wahusika ambayo ilininasa
sana. Kauli hii ilitolewa katika
mkutano wa viongozi wakuu
wa MAFIA na mmoja wa
viongozi hao, akiwa na nia
ya kuwashawishi wenzake
kubadili mbinu za uhalifu.
"KUNA HAJA GANI YA
KUENDELEA NA WIZI
WA KUTUMIA SILAHA,
WAKATI NJIA BORA ZA
KUIBA, TENA AMBAZO
NI HALALI ZIPO? Alihoji
kiongozi huyo.
"NI MBINU GANI HIZO?"
Wenzake walitaka kujua.
"BENKI. TUANZISHENI
BENKI! UKIWA NA BENKI
U TA I B A U P E N D AV Y O
NA RAHA YENYEWE NI
KWAMBA WIZI WENYEWE
K W E N Y E M A C H O YA
SHERIA UTAKUWA NI
HALALI!"
Wakati huo sikuipa hii
kauli uzito wowote, pamoja
na kwamba ilinasa kwenye
ubongo wangu na kubakia.
Nadhani sababu ya kutoipa
uzito wa kutosha wakati huo
ni uzoefu mdogo niliokuwa
nao wakati huo kuhusu
masuala ya fedha, na utendaji
wa mabenki. Uzoefu wangu
uliishia katika kujua kuwa
benki ilikuwa ni mahala
salama pa kuweka fedha
zako, na unapokuwa na shida
unakwenda kuzichukua.
Hata hivyo kadri miaka
i l i v y o k u wa i n a k we n d a ,
ndivyo jinsi ambavyo
nimezidi kumuelewa yule
kiongozi wa genge la MAFIA
na kuukiri ukweli uliosheheni
kwenye kauli yake.
Uchunguzi wangu umebaini
kuwa njia zinazotumiwa na
mabenki kuibia wateja wao ni
nyingi na baadhi yao ni hizi
zifuatazo:
Kwanza ni kuwarubuni
watu kufungua akaunti za
akiba na amana kwa ahadi
ya kuwapa riba mwisho wa
mwaka ya (3% au 4% kama ni
akaunti za akiba na 7% kama
ni akaunti za amana). Haraka
haraka unaweza usione kuwa
kuna tatizo hapa, lakini lipo.

ANNUUR NEW.indd 6

Benki zinachukua fedha zako
hizo na kuwakopesha watu
wenye kuhitaji kwa tozo
la riba kubwa (wastani wa
18% hadi 60%! kwa mabenki
mengi yaliyoko nchini).
Katika 18% iliyotozwa,
benki inachukua 4% au 7%,
inakupa; inabaki na 14% au
11% , na kisha inatangaza
ni jinsi gani benki hiyo ni
madhubuti, kiasi cha kuweza
kutengeneza faida kubwa!
A i d h a , wa k a t i b e n k i
zinapokuhitaji uhifadhi fedha
zako kwao kwa muda mrefu
hawakuambii kuwa kitendo
hicho kinaweza kukutia
hasara kwa njia ya fedha
zako kupoteza thamani. Kwa
nchi kama Tanzania ambayo
mfumuko wa bei ni zaidi ya
5% kwa mwaka, na shilingi
yake inapoteza thamani mara
kwa mara dhidi fedha za
kigeni, fedha zinazowekwa
tu bila kuingizwa kwenye
mzunguko zikazalisha
fedha nyingine, aghalabu
zinapoteza thamani kwa
zaidi ya 5% kila mwaka
kutokana na mfumuko wa bei
pekee, achilia mbali thamani
inayopotea kutokana na
kushuka kwa thamani ya
shilingi. Hata kama benki
itakupa hiyo riba ya 3% au
4% au 7%, bado utakuwa
umekula hasara kutokana na
thamani iliyopotea kwenye
fedha zako.
Njia ya pili ni kujenga
mazingira ya kumlazimisha
mteja kulipia baadhi ya
huduma bila sababu za
msingi. Kwa mfano, siku hizi
kila benki inatumia mashine
nyingi za ATM ikiwa ni njia
ya kurahisisha uchukuaji
wa fedha katika akaunti
za akiba za wateja. Katika
kila muamala unaofanya
katika hizi mashine, iwe ni
kutoa pesa, kuomba salio au
kuomba risiti ya muamala,
akaunti yako inakatwa kiasi
fulani cha pesa! Ukisema

uache kutumia ATM uende
dirishani, huko unaambiwa
utapewa pesa lakini ukubali
kuadhibiwa (aghalabu
adhabu husika ni makato
makubwa kuliko hata hayo ya
ATM) kwa kuacha kutumia
ATM zilizoko.
Tatu ni kutumia ujuzi
mdogo wa wateja wa
mambo ya fedha kuwaibia
kupitia riba isiyopungua
(FLAT INTEREST), pale
wanapoomba mikopo. Kwa
kawaida unapokopa, kwa
mfano shilingi milioni 20,
kwa mkataba wa kuulipa
mkopo huo ndani ya miezi
12 kwa mfano, unaambiwa
pia na kiwango cha riba
inayohusika. Kwa mfano,
kama utaambiwa kuwa riba
husika ni 18%, maana yake ni
kwamba iwapo utalipa fedha
hiyo kwa mkupuo mmoja
baada ya miezi 12 utalipa

na riba ya 18% ambayo ni
Tshs 3,600,000.00. Kwa bahati
mbaya baadhi ya mabenki
hukupangia marejesho ya
kila mwezi lakini inapokuja
kwenye suala la riba,
wanakutoza kana kwamba
fedha yote ya mkopo unailipa
kwa mkupuo mmoja!
Tofauti iliyopo ni kwamba,
kama unaulipa mkopo
huo kwa mafungu ya kila
mwezi, riba unayotozwa
inatakiwa iendelee kupungua
kila mwezi (REDUCING
INTEREST) kwa sababu
m k o p o u n a o d a i wa n a o
unapungua kila mwezi,
kutokana na marejesho
unayofanya. Kwa kutumia
mfano wetu huu hapa wa
mkopo wa milioni 20, riba
katika mwezi wa kwanza
wa marejesho itakuwa Tshs
300,000.00 na katika mwezi
wa mwisho wa marejesho,

itakuwa Tshs 27,097.00. Kwa
utaratibu huu jumla ya riba
yote utakayokuwa umelipa
kwa mwaka mzima itakuwa
Tshs 2,003,198.00. Tofauti
kati ya mtu aliyetozwa riba
kwa mfumo huu, na yule
aliyetozwa kwa mfumo wa
riba isiyopungua ni Ths
1,596,000.00! Kiasi hiki,
ambacho kimsingi unaibiwa,
ni karibia 80% ya riba halisi
uliyokuwa unatakiwa kulipa.
Njia ya nne, ni kutumia
m u d a wa m k a t a b a wa
kulipa deni kama kigezo cha
kukulazimisha kulipa riba ya
kipindi chote cha mkataba,
hata kama utaamua kuachana
na deni lako kabla ya muda
uliomo kwenye mkataba
kufikia ukomo. Kuna wakati
baada ya kuhudumia mkopo
wako kwa muda, mfano
miezi mitatu, unapata fungu
kubwa la fedha kutoka
vyanzo vingine (kwa mfano
unalipwa fedha ulizokuwa
unadai mahala) na unaamua
kutumia fedha hizi kulipa
mkopo unaodaiwa katika
fungu moja na kuachana
nao. Haikusaidii kitu!
Haikusaidii kwa sababu benki
itang'ang'ania ulipe riba yote
iliyobaki. Kwa mfano, kama
mkopo ulikuwa wa miezi 12,
basi benki itakutaka ulipe
riba ya miezi 9 iliyokuwa
imebakia katika kipindi cha
mkataba wako!
Kuibiwa kwa namna hii
ndiko kulikodhamiriwa
kwenye kauli ya yule kinara
wa MAFIA. Wizi hadharani,
na hakuna mtu anakuuliza!
Hii ina maana kuwa, kama
ni lazima ukope, basi kabla
hujaamua kutafuta mkopo
huo, ni bora kuingia kazini na
kutembelea mabenki mengi
k a d r i i n a v y o we z e k a n a ,
kutafuta benki ambayo
iko tayari kukupa mkopo
unaohitaji kwa masharti
ambayo hayatakuumiza sana!
Benki ambayo haitatumia
shida yako kukuibia.

Nafasi za Masomo Sotele Sekondari 2016

Uongozi wa Shule ya SOTELE SEKONDARI (iliyo chini ya TAMPO) iliyopo kata
ya Dondo Tarafa ya Kisiju wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani inawatangazia
Waislamu wote nafasi za masomo kwa mwaka mpya wa masomo 2016 kwa kidato
cha I,II,III,IV fomu zinapatikana katika mikoa ifuatayo: Mkoa wa DSM Imamu Mwinyikai, Sheikhat Hisa Magomeni Kichangani,Juma Nchia
Ununio College Boko, Tampro Magomeni Usalama, Imamu Shaabani Masjid Tungi
Temeke. Imamu Mkadam Masjid Haqa Buguruni, Imamu Yusufu kwa mwalimu Daudi
Masjid Mtambani Kinondoni mkoa wa Pwani Rufiji Mwl Sodungu 0719 402695 sotele
shuleni mkuranga. Mkoani Tanga Sheikh Koja mtihani wa Usajili utafanyika tarehe
29/11/2015 katika vituo vifuatavyo: Ridhwaa Seminary Kinondoni Mkwajuni DSM na
Sotele Sekondari Mkuranga- Pwani Saa 2:30 Asubuhi kwa maelezo zaidi wasiliana
na MWL Saiboko 0784 299 945, Mwl Pilly 0784 657216, Pazi Mwinyimvua 0655
654900 Yusufu Shaabani 0715 818187, Mwl Ally 0784 879197 Omar Tampro makao
makuu 0714 151532, Mkoa wa Tanga Sheikh Koja 0717 247297, Mkoani Mtwara
Mwl. Jazari 0717 235011, Masasi Imamu Mcholo 0715 181485, Newala Idd Abdul
0785 722988, Mkoani Lindi Imam Maarufu 0716 260035, Kilwa Masoko Abdallah
Kaundunde 0784 610444, Mkoani Singida Mwl. Mang’ola 0787 105182 na
Zanzibar Ofisi za UKUEM Makao Makuu 0777 125074.

11/26/2015 6:13:28 PM

7
Mhe. Ban Ki Moon –
Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa
Mhe. Magniz Lyketoft –
M/kiti wa Mkutano Mkuu
wa Umoja wa Mataifa
Mhe. Mathayo Rekroft
– M/kiti wa Baraza la
Usalama
Mhe. Ford Sik – M/
kiti wa Kamati husika ya
haki za Wapalestina zisizo
hamishika.
Napenda kuchukua
nafasi hii kufikisha
salamu za Palestina
na za wananchi wake,
waliohudhuria na kwa
marafiki kote duniani,
walioshiriki nao katika
maadhimisho ya siku hii
ya kimataifa ya kuungana
na Wapalestina.
Hii ni baada ya
miezi miwili tu tokea
kupeperushwa kwa
shangwe na nderemo,
bendera ya Palestina mjini
New York Marekani,
jambo linalotufurahisha
wote.
Rais pia amechukua
nafasi kuzishukuru nchi
zote zilizokubali uwepo
wa dola ya Palestina, pia
zile zote zilizochangia
ufanisi wa suala hilo
kupitia kura zao katika
Umoja wa Mataifa na
sekta zake zote.
Mchango huo ni
katika ufanisi wa sekta
na maazimio mbalimbali
ya h u s u y o Pa l e s t i n a ,
kikiwemo kituo chake
ndani ya umoja wa
Mataifa kitachosaidia
kuleta amani ya kweli
Mashariki ya Kati na
duniani kwa ujumla.
Aidha amerejea
shukrani zake kwa taasisii
zisizokuwa za kiserikali,
asasi za kiraia, marafiki
na wadau wote wa
uhuru na amani duniani,
wanaosimama kidete na
ndugu zao Wapalestina
katika kufikia uhuru
wao, ili kuleta amani ya
kudumu.
A m e o n g e z a k u wa ,
Umoja wa Mataifa
umeshughulikia suala la
Palestina tokea mwanzo na
kuliweka katika agenda za
vikao vingi vya kimataifa,
huku ikilijengea mikakati
na maazimio mbalimbali
ya s i y o e p u k i k a k wa
lengo la kufikia suluhisho
lifaalo.
Hivyo tunathibitisha
uwepo wa suala hilo kwake
hadi hapo patapofikia
ufumbuzi unaoridhiwa na
pande husika kwa mujibu
wa kanuni za kimataifa.
Hivyo, tunapongeza
juhudi zinazofanywa na
Katibu Mkuu wa Umoja
wa mataifa Mhe. Ban Ki
Moon, pia kamati husika
ya haki za Wapalestina
zisizo hamishika, iliyo
chini ya M/kiti wake
balozi wa Senegal Mhe.

ANNUUR NEW.indd 7

MAKALA

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Hotuba ya Rais Mahmuud Abbas wa Palestina
M/KITI WA KAMATI TENDAJI YA JUMUIYA YA UKOMBOZI WA PALESTINA (PLO)
MNASABA WA SIKU YA KIMATAIFA YA MSHIKAMANO NA WAPALESTINA
23 NOVEMBER 2015

Rais Mahmuud Abbas wa Palestina
Ford Sik.
Vilevile wajumbe, nchi
waangalizi, sekta zote
za Umoja wa mataifa,
hasa inayojihusisha na
wakimbizi wa Kipalestina
(UNNRWA), Mashirika
yote yanayosaidia
Pa l e s t i n a i l i k u f i k i a
mpango wa amani.
Umoja wa Mataifa na
sekta zake pia Mahakama
ya kimataifa ya uadilifu
na usawa, tayari
vimesaini maazimio
n afuu k wa Pa le s tin a .
Hivyo tunasikitika kuona
hayajapitishwa maazimio
hayo, jambo lililosababisha
kuzidi mivutano kwa
muda mrefu, huku
Palestina ikiathirika kwa
kiasi kikubwa.
Kufeli kwa utekelezaji
wa kanuni na maazimio
hayo, daima kunainyima
Palestina haki zake za
kimsingi, huku ikieleweka
u we p o wa b a a d h i ya
vigezo katika Umoja wa
Mataifa vihusuvyo Israeli
havijapitishwa, jambo
linaloipa jeuri na kujiona
ni dola iliyo juu ya sheria
haiwezi kuadhibiwa.
Rais Abbas ameongeza
kusema kwamba,
kuendelea kuwepo kwa
uvamizi wa Israeli katika
ardhi yetu, ujenzi endelevu
wa makazi ya kilowezi,
kuzidi kwa utekaji nyara,
kuwanyonga vijana na
watoto wetu, uwepo wa
vikwazo katika ukanda wa
Gaza na mengine mengi
ya kinyama yafanywayo
na waisraeli.
Ni uthibitisho tosha
kuwa nchi hiyo inavunja
kanuni za kimataifa,

inapuuza mpango wa
amani na kuendeleza
uvamizi wake wa
kimabavu.
M i a k a
m i n g i
imetahadharisha matokeo
ya yanayoendelea mjini
Jerusalem iliyovamiwa
kimabavu na maeneo
yake ya jirani, yakiwemo
mambo kadhaa mabaya
dhidi ya Wapalestina,
huku walowezi wakiwa
chini ya kivuli cha majeshi
ya kizayuni ya Israeli ili
kubadili historia ya Msikiti
Mtukufu wa Agswa
iliyopo tokea mwaka 1967.
Hii inalenga kugeuza
migogro ya kisiasa na
kisheria iwe ya kidini
zaidi, jambo ambalo
litaleta matokeo mabaya
mno kwa wote na ambalo
halikubaliki kamwe.
Hivyo ni lazima kusitisha
juhudi za kuendeleza
m a k a z i ya wa l o w e z i
na zile zote za Israeli
zinazolenga kuharibu
bali kufuta kabisa historia
ya Wapalestina na mji
mtukufu ili Israeli ichukue
Msikiti Mtukufu na eneo
zima.
K wa k u f e l i j u h u d i
za jamii ya kimataifa
k u i e p u s h a Pa l e s t i n a
na dhuluma za Israeli,
imepelekea wananchi
wa Pa l e s t i n a k u k o s a
mustakabali mwema, hasa
vijana. Tunatilia mkazo wa
kufanyika juhudi zaidi za
kimataifa ili kuleta amani
Mashariki ya kati, kwa
msingi wa kuwepo dola
mbili iliyopo tokea mwaka
1967.
Kwa mujibu wa
maazimio ya Umoja wa

M a t a i f a ya l i y o f i k i wa
mjini Madrid-Hispania
kuhusu amani na usalama
wa Kiarabu yanataja pia
kumaliza uvamizi huo wa
Israeli, kwani hakuna haja
tena ya kupoteza muda
bali ni lazima ifanyike kazi
ya ziada ili kufanikisha
mpango wa amani.
Rais ameendelea zaidi
kusema kuwa, ninyi nyote
mnajua kwamba lengo
letu ni kuleta amani, ndio
maana bado tunaendelea
kutoa fursa ya hilo. Mara
kadhaa Israeli imeharibu
juhudi hizo, ili iendelee
kujenga makazi ya
kilowezi na ukuta wa
kibaguzi katika ardhi ya
Palestina.
Tunajiuliza nini lengo
la Israeli katika kuweka
kiasi cha makazi laki sita
(600,000) ndani ya ardhi
ya Palestina, huku ikielewa
kuwa kufanya hivyo ni
miongoni mwa uhalifu
wa kivita kwa mujibu
wa maazimio ya Geneva
ya m wa k a 1 9 4 9 , p i a
inapingana na ufumbuzi
wa kuwepo dola mbili.
Hatua ya Israeli
kubomoa misingi
iliyowekwa kisiasa,
kiuchumi na kiusalama,
inatufanya tushindwe
kuendelea na utekelezaji
wa maazimio hayo upande
mmoja bila ya Israeli.
Isipokuwa tunaendelea
kutekeleza sheria na ahadi
za kimataifa kwa nia njema
ili kufikia mpango wa
amani.
Hivyo, tutaendelea
kujiunga na jamii za
kimataifa na mikataba
yake ili kulinda haki
zetu, huku tukihakikisha
usalama wa taifa letu
kwa njia mbalimbali za
kisheria na kiusalama
tulizo nazo. Hakika
kuliondolea dhuluma
taifa letu ni jukumu la
kitabia na kibinaadamu,
tunazidi kuiomba jamii
ya kimataifa kuilazimisha
Israeli kuachana na
kuikandamiza Palestina,
bali ifanyie kazi maazimio
ya kimataifa ili kumaliza
hali hiyo.
Kwa upande mwingine,
Rais Abbas amehoji kuwa,
hadi lini itaachwa Israeli
ikikiuka maazimio ya
kimataifa kana kwamba
ni dola iliyo juu ya sheria?
Huku wananchi wa
Palestina wakiendelea
kukaliwa kimabavu na
kudhulumiwa haki zao
kwa maslahi ya walowezi
wa c h a c h e wa k i g a i d i
wa n a o f u m b i a m a c h o
maovu yao na adhabu
yao?

Hakika jamii ya
kimataifa inatakiwa zaidi
leo kuilinda Palestina
muda wote wa uvamizi,
huku ikiisaidia kupata
haki yake na kupanga
mustakabali wake,
ikiwemo haki ya kupata
uhuru wake na kuwa dola
yenye mji mkuu wake
Jerusalem ya Mashariki
kama ilivyo katika mipaka
ya mwaka 1967.
Hii itatuwezesha
kuishi kwa amani na
jirani yetu Israeli huku
tukiheshimiana kwa
mujibu wa makubaliano
ya Umoja wa Mataifa na
kimataifa, pia kuwepo
suluhisho la wakimbizi wa
Palestina kwa mujibu wa
agizo la Mkutano Mkuu
waUmoja huo namba 194,
inayotaja pia kuwatoa
wafungwa na waliotekwa
nyara wote wa Kipalestina
waliopo katika jela za
Israeli.
Rais ametilia mkazo
kwamba, lengo ni
kumaliza kabisa uvamizi
wa Israeli katika ardhi
ya Palestina, pia kupata
uhuru wake na uongozi
wake na sio kumdhulumu
yeyote kama wanavyodai
baadhi ya watu. Ni dola
itayosifika na yote mazuri
bila ya ubaguzi wa aina
yoyote, hivyo tutaendelea
na harakati kwa msaada
wa m a r a f i k i n a w o t e
wengine ili kufikia lengo
hilo.
Vile vile mikono yetu
bado imenyooshwa kutaka
amani ya kweli kwa misingi
ya sheria za kimataifa na
maazimio ya Umoja wa
Mataifa, kinyume na hivyo
ni kurefusha muda wa
mgogoro, kukata matarajio
mema na kuzidisha
kinyongo na chuki kwa
walengwa.
Wananchi wa Palestina
ni haki yao kupata neema
ya uhuru na yote mazuri
chini ya dola yao huru
yenye mji mkuu wake
Jerusalem ya Mashariki,
hili ni jambo la lazima ili
kuleta amani, usalama na
utulivu katika Mashariki
ya kati. Amani ndio lengo
letu kuu na ndio maslahi
hasa ya Palestina, nchi
za Kiarabu na dunia kwa
ujumla.
Rais Mahmuud Abbas
amemalizia hotuba yake
kwa kusema kwamba;
Hilo linawezekana endapo
tu kukiwepo uongozi
thabiti na uthubutu wa
k isiasa unaoong ozwa
na nia njema, kwa lengo
la kujenga mustakabali
mwema kwa wote.
Contact us: P.O Box
20307, 612 UN Road –
Upanga West, Dar es
Salaam Tel: 2152813,
2150643 Fax: 2153257
Email: pict@pal-tz.
orgWebsite: www.pal-tz.
Org.

11/26/2015 6:13:29 PM

8

Makala

K

Tathmini ya uchaguzi na
‘Viburi Mauti’ Zanzibar

WA N Z A n i a n z e
kwa kuwataka
radhi waungwana
wote hapa barzani
kwa kuadimika kwangu
au kukaa kimya kirefu
japokuwa niliutolea
u f a f a n u z i u k i m ya h u u
kabla, lakini kwa kuwa
nimezidisha muda, basi
wajibu kuanza kwa
kutakana radhi. Lakini pia
kabla ya yote au awalani
ya hayo, ni lazima sana
kuanza kwa kumshukuru
Mola wetu kwani bila yeye
hapa leo tusingekutana
kuongea, kunon’gonezana
au kuambizana neno.
Uchaguzi umekwisha
kama tunavyojua na
mshindi anajulikana, ingawa
hakutangazwa bado na
wahusika na tunavyoambiwa
kuwa ametenda dhambi
mbaya sana iliyo juu
ya uhaini kwa kuwa
amejitangaza mwenyewe na
hilo ni kosa kwa sheria za
Zanzibar kama nchi, ZEC,
polisi au CCM kwa ujumla.
Binafsi silioni kosa hapa kwa
sababu halipo. Mgombea
wa urais Maalim Seif Sharrif
Hammad wa chama cha CUF
hakuvunja sheria yoyote
na wala hajatamka kuwa
yeye ndie RAIS wa Zanzibar.
Alichokisema na kudai ni
kutaka chombo husika yaani
Z E C wa m t a n g a z e ye ye
mshindi baada ya kuweka
wazi au kuonyesha kura zake
HALALI zilizothibitishwa na
kuwekwa sahihi na mihuri
na wahusika wote na vituo
vyao wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar na zile za mpinzani
wake.
Kuhusu Zanzibar kama
nchi, nafikiri tumeshawahi
kupata jawabu ya kitendawili
hicho wakati wa ile kesi
iliyowakabili watuhumiwa
waliotaka kupindua visiwa
hivi na kesi kufika mahakama
ya kuu/rufaa ya Tanzania na
ndipo tulipo pata jawabu
ya kuwa hapa hakuna nchi,
kuna nini... hilo mtanisaidia.
Kilichotendeka Oktoba
25 siku ya uchaguzi ndio
kile kile nilisema sana hapa
kuwa chama changu, yaani
CCM kitashindwa vibaya.
Nimeandika sana kuhusu
hatma hii hapa na wengi
mtakuwa mashahidi wangu
kwa kuwa haya sio mageni
k w e t u s o t e h a s a wa l e
tunaotumia muda mrefu
na kuumiza vichwa vyetu
kwa kuitakia kheri nchi hii
isiyotakiwa na ‘Tanganyika’.
Nilifika kuweka wazi kuwa
nitakuwa tayari kuja mbele
yenu tena hapa kuwataka
radhi ikiwa CCM itashinda
uchaguzi huu, tutashinda
pia niliyajua zamani kuwa
hapa hapana uchaguzi, bali
tujitayarishe na uchafuzi na
ndio huu unaoendelea sasa
baada ya mwenyekiti wa
ZEC bwana Jecha kuamua
kuufuta uchaguzi na kuanza
machafuzi ya makusudi ili
kukinusuru chama chetu
baada ya kuona matokeo
halali na halisi ya uchaguzi

ANNUUR NEW.indd 8

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

DKT. Ali Mohamed Shein

MAALIM Seif Sharif Hamad

JECHA Salum Jecha

wenyewe.
Ni vema tukayadhukuru
yote ya nyuma ili tuweze
kujua wapi tulikosea au wapi
hakuhitaji marekebisho na
nini la kufanya tuepukane na
maafa tunayotengenezewa
na viongozi wetu wa CCM
Zanzibar na Tanganyika
waliopo madarakani na
wale waliostaafu, lakini bado
wanafanya kazi za chama
Cha Mapinduzi kwa malipo
wanayoyajua wao wenyewe.
Kwa sababu hakuna karatasi
au vocha hata moja utakayo
iona inayoidhinisha malipo
ya viongozi hao akiwemo
Bwana Ali Hassan Mwinyi.
Sasa la kujiuliza safari zote
hizi za Zanzibar/Dar za kila
kukicha, zinafanywa kwa
mapenzi ya nchi peke yake?
Au chama peke yake? Au
kuna tija gani ndani yake?
Sababu kubwa ya
mwenyekiti wa ZEC kufuta
uchaguzi inayopewa
kipaumbele hapa visiwani na
watetezi wengi kama si wote
wa chama changu cha CCM
isipokuwa mimi, au baadhi
yetu tusiopenda au kufarijika
kwa kujidanganya makusudi
kwa sababu kuna uwezekano
mtu ukajidanganya kwa
b a h a t i m b a ya , n i k u l e
kusema kuwa Pemba ndio
kumetokea uchafuzi wa hali
ya juu na huko ni sawa na
kusema kuwa hakukuwa na
wasimamizi wala ukaguzi
wa kura hata uhesabuji wa
kura pia ulifanyika chini
ya miti kwa kuwa ofisi
zilikuwa zinavuja maji na viti
vinawasha kama upupu. Pia
nambari za uhakiki wa kura
na vitambulisho zilifutwa
na kuandikwa kwa wino
baada ya kukarabatiwa. Huu
ni uongo uliojaa uzandiki.
Pemba hawana bahati siku
zote kwa sababu wameamua
kwa kujua tena kwa ridhaa
ya o n a k wa m a k u s u d i
matupu kuikataa CCM
miaka yote na kuinyima kura
hata ya balozi wa nyumba

kumi kumi kwa sababu
wametumia haki yao ya
kidemokrasia ya kukichagua
chama wanachokitaka hata
kama hakitowafaa huko
usoni, lakini huo ni uamuzi
wao na ni lazima hatuna hiari
tuuheshimu na kuulinda
uamuzi wao huo.
Sio rahisi kwa chama
changu kupata usingizi
na kuukubali ukweli huu.
Tutawasingizia Pemba miaka
yote tukipenda kwa raha zetu,
lakini kamwe hautokuwa
ukweli wa hali halisi. Hali
halisi CCM hatutakiwi tena
hapa visiwani na wengi ya
wananchi wetu. Hii sio siri
tena. Kwa nini tumekuwa
wakaidi na vipofu?
Shemeji yangu alikuwa
mmoja ya wasimamizi wa
uchaguzi pale Kibanda Maiti
alichokuja kunihadithia
yeye kilimshitua, mimi
kilinichekesha. Chumba
alichopangiwa kukisimamia
ilikuwa ni cha waajiriwa wa
vikosi vya SMZ peke yao
au niseme wengi nitakuwa
niko sahihi wakati ulipofika
wa kuhesabu kura ulipofika
waligundua yeye na wenziwe
waajiriwa hao wapya na
wakongwe wa vikosi vya
SMZ nusu yao wamempigia
kura mgombea wa CUF
yaani Maalim Seif juu ya
kutishwa kufukuzwa kazi
kulikofanywa na viongozi
wa CCM na makamanda
wao. Sasa bado tutazituma
lawama zetu Pemba wakati
kura za urais zilizo mpa
ushindi Maalim karibu zote
zimetoka Zanzibar (Unguja).
Nirudi kwenye katiba
iliyotuletea balaa sisi
CCM tulipojikusanya pale
Dodoma na kumtukana Mzee
Warioba na rasimu zake mbili
alizoziandika akishirikiana
na mwana diplomasia
Mohamad Yussuf Mshamba
pamoja na wasomi wengine
waliobobea katika sheria
na lugha. Tulijiona tuko
juu ya ulimwengu wa siasa

na Tanzania, ni shamba la
shemeji yetu na hati miliki ya
eka hizi anazo dada yetu chini
ya mto kwa amani kabisa
hatukuwa na budi kulala
usingizi mnono kwa sababu
shemeji hawezi kuipata hati
miliki ya shamba hili bila
kumuamsha dada yetu. Kitu
ambacho hatukujua, hati
miliki haikuwepo uchagoni
kama tulivyodhani. Wenye
nchi walikuwa nayo
mikononi siku nyingi wala
hawakulala usingizi. Siku
imefika wanataka nchi yao
siku za kucheza na kuimba
mguu mbele mguu nyuma
zimekwisha, sisi ndio
tunataka uchaguzi urudiwe
ili tuendelee kuburudika
n a m u z e k a wa p i h a ya
tumeyakaanga wenyewe kwa
miaka yote hii tuliyoifanya
dhulma kwa viumbe hawa
wa kila rangi wanaopumua
h a p a v i s i wa n i n a wa l e
waliotangulia. Tumehutubia
ubaguzi wakati wote wa
kampeni tukiongozwa na
‘borafya’ huku viongozi
wa juu wakiwa nyuma ya
majukwaa wakitoa baraka
zao! Leo tunavuna matunda
ya ubaguzi tuliyo yapigia
debe kama wendawazimu
k wa
k u wa h o f i a
Waislamu wenzetu sijui
w a n g e l i k u wa m a k a f i r i
tungeliwasherekekea vipi?
Zanzibar kwa sasa
tunaenda kama MV
Jamhuri. Kwa wale wanao
ikumbuka yaani bega moja,
viburi vilivyojaa mauti
ndio vinavyoongoza visiwa
hivi. Kwa sasa tumechoka
na amani ya miaka mingi.
Hatuna budi kuitafuta shari
kwa bei yoyote. Hayo ndio
yaliyomo ndani ya mioyo
ya watawala wetu ambao
kwa sasa neno watawala
ndio neno sahihi kabisa kwa
kuwa hawana ridhaa yetu
kutuongoza na hatutaki
kuongozwa kwa nguvu au

mabavu. Niliwahi kusema
nchi itajiinamia. Nililitumia
hilo neno kwa kuwa ndilo
nililoliona linafaa. Kwa hali
hii leo hii Zanzibar imegeuka
ya maaskari na bunduki,
vifaru na zana zote za kijeshi,
zimeletwa hapa kutulinda
tusilaumiane? Kwa kweli
inasikitisha sana kuona visiwa
vya marashi ya karafuu kwa
sasa vinakaribia kunukia
baruti. Kinachosubiriwa
ni ama askari mmoja aliye
taahira afyatue risasi ovyo
au wenye haki wadai haki
yao kwa amani au fujo tena
itakuwa tumeshapata sababu
ya kuhalalisha “UCHAGUZI
URUDIWE” kwa sababu
tunachohitaji kwa bahati
mbaya sana ni tone la damu
limwagike ili watawala
waendelee kula nchi au
kututawala tukitaka tusitake.
Kumuapisha Maalim
seif kuwa rais ndio mtihani
mkubwa wa CCM. Kwa sasa
matokeo wameshayakubali
siku nyingi, tatizo ni
kiongozi mwenyewe sijui
a n a o g o p wa n i n i b wa n a
huyu na utu uzima huu alio
nao sasa. Kuna wakati hata
mimi nikimuogopa huyu
muungwana, ukweli niseme,
lakini sio leo hekima tupu
imejaa kichwani mwake
mengi yamemkuta katika
uhai wake hasa wa siasa.
Mandela alitegemewa na
wengi aje na kuna waliomtaka
na kumlazimisha alipize
kisasi kwa yote aliyofanyiwa
binafsi na watu wake Weusi
kwa Weupe, lakini alikataa na
alikuja na busara za kiongozi
mpevu mpaka leo Afrika ya
Kusini iko shwari.
Uholanzi wanakotoka
Wadachi kiasili, walijenga
miji maalum kwa kuwapokea
Wazungu wa Afrika ya Kusini
baada ya kupata uhuru
na kufukuzwa huko. Hivi
sasa wanajaza wakimbizi
t o k a d u n i a n i k o t e k wa
kuwa wale Wazungu walio
watarajia hawakupatikana.
Tuondoe viburi mauti kwa
kuogopana kusiko kuwa na
tija. Tunajitia vijiti vya macho
kwa kudhania tunajipura
kwa wanja. Tusisubiri upofu
ndio tujifunze kuona.
Naona kwa leo niishie
hapa. Naomba radhi kwa
makosa yatakayojitokeza.
Nina mengi sikuwahi au
k u j a a l i wa k u n e n a l e o ,
Inshaallah nitapata muda
nitajaribu tena kuelezea
kilichojiri, kinachojiri na
kitakachojiri hapa kwetu.
Tusisite kuomba salama.
Visiwa hivi vinafukuta moshi
mtupu kwa sasa. Wapulizaji
wako wengi. Magari ya zima
moto tunayo mawili tu, na
moja bovu. Kwa maana
hiyo, limebaki moja nalo
kongwe. Kwa ufupi, moto
una kila sababu ya kuwaka
na utushinde kuuzima. Sasa
wakati umefika wa kuachana
na “viburi mauti.”
Asanteni
Mzeekondo, comrade.

11/26/2015 6:14:10 PM

9
Inatoka Uk. 4

N a k wa m a a n a h i y o ,
kinachotakiwa ni kuimarisha
Somo la Uraia (Civics), ili
liweze kuwaweka pamoja
watoto wa dini zote na
kuwapatia mafunzo yote
yanayohusu kuwa raia wema.
Pengine la kutaja hapa
kwa muktadha wa nukta hii
ya IEP ni kuwa mauwaji ya
mwaka 2001 mara baada ya
uchaguzi mkuu, haikuwa
k wa s a b a b u z a wa t o t o
wa Pemba wanafundiswa
sana kuswali na kusimama
Qiyamul layl.
Lakini hata ukitizama
zogo lililotokea Arusha hadi
kuuliwa watu baada tena ya
uchaguzi mkuu 2010 huku
wengine wakitamba kuwa
wataifanya nchi isitawalike,
haikuwa kwa sababu watoto
wa Kikatoliki na Kiislamu
walisomeshwa na kuhimizwa
kunyenyekea katika Sala zao.
Hivi sasa kuna mgogoro
unaofukuta Geita unaotishia
hali ya amani kutokana
n a k u u l i wa a l i y e k u wa
Mwenyekiti wa CHADEMA
mkoani humo, Bwana
Alphonce Mawazo.
Wanaotuhumiwa
kumuuwa Mawazo,
hawajafanya jinai hiyo kwa
sababu Tanzania imechelewa
kufuata nyayo za Liberia
kufundisha Somo la Dini
kama taaluma.
Hivi sasa Charles
McArthur Ghankay Taylor
anatumikia kifungo cha

Na A. S. M Chachika
NIMESOMA kwa
m s h i t u k o t a a r i f a ya
Polisi Zanzibar juu
ya kushitakiwa watu
wanaodaiwa kuchafua
uchaguzi mkuu Zanzibar.
Na ikatajwa katika jumla
ya madai kwamba kuna
watu walikutwa na visu
na mapanga katika vituo
vya kupigia kura.
“Akifafanua miongoni
mwa makosa hayo
ni pamoja na kukutwa
watuhumiwa na silaha
katika vituo vya uchaguzi
kama vile visu na mapanga,
kuvamiwa au kupigwa
mawakala na kutolewa
mawakala katika vituo vya
kupigia kura.”
Limeandika gazeti la
Zanzibar Leo katika toleo
lake la jana Novemba 26,
2015, likinukuu taaifa ya
Naibu Mkurugenzi wa
Upelelezi Mashitaka ya
Jinai, Salum Msangi.
Ta a r i f a y a A f a n d e
Salum Msangi kama
alivyonukuliwa na gazeti
hilo ikasema kuwa mengi
ya matukio hayo ya kihalifu
na kuchafua uchaguzi
yalifanyika Pemba, japo
na Unguja yalikuwepo.
N i m e s e m a
nimeshtushwa kwa sababu
kubwa mbili. Moja ni
kuwa siku mbili kabla

ANNUUR NEW.indd 9

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Mtihani wa kwanza kwa Rais Magufuli

WA Z I R I M k u u , M h e .
Majaliwa Kassim Majaliwa.
miaka 50 katika moja ya
magereza ya Uingereza baada
ya kupatikana na hatia ya
uhaini wa kivita na mauwaji
yaliyofanyika wakati wa vita
ya wenyewe kwa wenyewe
S i e r r a L e o n e . A l i p e wa
hukumu hiyo na Mahakama
Maalum ya Umoja wa Mataifa
juu ya Sierra Leone (UNbacked Special Court for Sierra
Leone-SCSL).
S i e r r a
L e o n e
haikutumbukia katika
m a c h a f u k o n a m a u wa j i
yaliyokuja kumtupa Charles
Taylor katika ‘gereza’ la The
Hague kwa sababu ilikuwa

haina “Mwongozo wa
Ufundishaji na Ujifunzaji wa
Somo la Dini” uliotayarishwa
na serikali isiyo na dini.
Lakini ilikuwa ni
mambo ya siasa na ugomvi
wa wakubwa kugombea
dhahabu.
Juzi hapa kuamkia
uchaguzi mkuu, Rais Mstaafu
Jakaya Mrisho kikwete,
alitangaza kuimarishwa kwa
jeshi na polisi wakimiminiwa
vifaa.
S e r i k a l i h a i k u wa n a
wa s i wa s i k wa m b a k wa
vile watoto wa Kikristo na
Kiislamu katika shule za
msingi, hawasomi dini kama
taaluma, basi watatengana na
kugombana katika masiku ya
uchaguzi mkuu.
Na hivi sasa moshi unafuka
Zanzibar, wala likitokea
la kutokea haitakuwa kwa
sababu Zanzibar wao hawapo
katika mpango huu wa TET
kusomesha Somo la Dini
kama taaluma ‘Tanganyika’.
Juu ya hoja ya serikali
kuwa somo la dini
limeshindwa kutoa raia
wema wenye maadili na
ndio maana matukio ya uovu
yamekithiri, IEP imesema
kuwa wa kulaumiwa ni
serikali yenyewe.
Katika kulifafanua hilo
wakasema kuwa wakati
viongozi wa serikali
wakihimiza watu wa dini
k u f u n d i s h a wa t u t a b i a
njema na kukemea vitendo
vya uasherati na mavazi

yasiyo ya staha makanisani
na misikitini, wakati huo
huo “serikali inaruhusu
uingizaji wa kanda za ngono
zinazooneshwa hovyo
mitaani na kisha inaanzisha
programu za kuwaelekeza
na kuwahimiza watoto wa
shule za msingi kutumia
kondomu.”
Aidha, inaruhusu
mashindano ya kupita nusu
uchi hadharani kwa kisingizio
cha kuibua vipaji vya urembo,
na mambo mengine machafu
kama hayo.
Katika kuhitimisha hoja
zao IEP, walikumbusha
kuwa mpango kama huu
wa kufundisha dini moja
ulitangazwa bungeni mwaka
2004 na Waziri wa Elimu na
Utamaduni wa wakati huo
Mh. Joseph Mungai.
Hata hivyo, ulipingwa
na wadau wa dini zote. Na
kwamba katika mkutano
wa wadau wa dini wa Mei
2007 uliofanyika TET chini
ya Kamishna wa Elimuwa
wakati huo Rick Mpama,
wadau wa dini walipinga
hoja ya serikali kutaka
kubeba dhamana ya kuandaa
maudhui ya somo la dini.
Serikali ikakumbushwa
kuwa baada ya mashauriano
ya kina iliamuliwa kwamba
kila asasi ya dini iandae
mihutasari ya ngazi zote
kwa kufuata maudhui ya dini
yake huku ushirikiwa TET
ukiwa ni katika kushauri na
kuhakikisha kuwa utaalamu

Zanzibar inaelekea kubaya

RAIS Mstaafu Amani
Abeid Karume.

MAALIM Seif Sharif
Hamad.

ya taarifa hii ya Polisi
Zanzibar, kulikuwa na
taarifa katika mitandao
ya kijamii kwamba kuna
mashitaka yanaandaliwa
kuwabambikiza kesi feki
za kuchafua uchaguzi
Makamishna wa
Uchaguzi ili kushadidia
na kuipa nguvu hoja ya
kuharibika uchaguzi
ili kujenga ‘uhalali’ na
kukubalika kwa wananchi

kurejewa kwa uchaguzi
huo. Na ikatajwa kuwa
wanaokwenda mbio na
jambo hili ni Polisi.
Kushangaa kwangu
hakutokani na misingi
na sababu za Polisi
kuandaa mashitaka kama
haya ikizingatiwa ukweli
wa taarifa zilizokwisha
kutolewa na waangalizi wa
ndani na nje juu ya namna
uchaguzi ulivyokwenda

na ukizingatia pia
kwamba Polisi hao hao
ndio walikuwa wakilinda
usalama katika vituo vya
kupigia na kuhesabia kura,
lakini hakuna tukio lolote
ambapo walikamata watu
wakiwa na silaha ambao
walidhuru watu na silaha
hizo kiasi cha kuvuruga
uchaguzi. Kushtuka
kwangu kunatokana
na jinsi taarifa katika
mtandao zilivyofuatana
na hili analosema Afande
Msangi.
N a s h t u k a m a r a ya
pili kwa kuona taarifa
nyingine katika mitandao
ya kijamii ikitoa tahadhari
kwamba kuna mpango
umeandaliwa ambapo
watatumika ‘wahuni’ wa
ndani au watu wa nje ya
nchi kulipua mabomu.
“Mpango wa kuutatua
mzozo wa Uchaguzi kwa
kutega mabomu”, ndivyo
taarifa hizo zinavyosema
na kufafanua kuwa lengo
ni kuleta mkanganyiko na
kuzuiya juhudi zozote za
kuleta utatuzi wa amani
ili yale yanayotakiwa na
waliohusika na kufuta
uchaguzi yatimie.
Sasa hapa lazima
nishtuke kwa sababu kama

unazingatiwa katika kuandaa
mihutasari na vitabu husika.
Kwa mujibu wa
mafundisho ya Uislamu, dini
iliyovuliwa ibada ni ukafiri.
Ukisema unafundisha
dini kama taaluma, maana
ya k e n i k u wa n i k a m a
unavyofundisha kemia au
jiografia, sio lazima msomaji
atumie taaluma hiyo katika
maisha yake ya kila siku.
Kwa hiyo, unamfundisha
mtu ‘Uislamu’, usio na
kuswali, kutoa zaka, kufunga
na ibada nyingine.
U n a m f u n d i s h a
m t u Ta w h e e d , l a k i n i
unamwambia hapana mbaya
akiwa mshirikana.
Tawheed kama taaluma,
inaishia kumwambia mtoto
kuwa Waislamu wanasema
Mungu ni mmoja, lakini
Wakristo wao wana ‘Utatu’.
Haelekezwi wala halelewi
na kuhimizwa namna
Tawheed hiyo inavyotakiwa
kuathiri maisha yake ya kila
siku.
Katika Uislamu, hili ni
chukizo kubwa mbele ya
Mwenyezi Mungu.
Qur’an inasema: “Enyi
mlioamini! Mbona mnasema
msiyoyatenda? Ni chukizo
kubwa mbele ya Mwenyezi
Mungu kusema msiyotenda.”
(61:2-3)
Na dini yoyote haiwezi
kuwa na maana kama sio
Imani, Ibada Maalum na
vitendo vya kila siku vya
muumini katika maisha
kwa kuzingati imani ya Dini
husika.

hili la mashitaka lilitangulia
kwanza kurushwa katika
m i t a n d a o ya k i j a m i i ,
halafu Polisi wanaibuka
na majalada ya kesi, lazima
hapa wananchi wawe na
wasiwasi zinaposambazwa
taarifa kwamba kuna watu
wanapandikizwa kufanya
mashambulizi ya ‘kigaidi’
ya kupanga. Na mambo
kama haya kama yapo,
lililo la uhakika ni kuwa
hayawezi kuiacha nchi
salama. Itakuwa ni nuksi
na balaa juu ya balaa. Allah
atunusuru kwa Rehma
zake, maana inavoonekana
miongoni mwetu wapo
walio dhamiria shari.
‘Liwalo na liwe ilimradi
yetu tunayotaka yatimie.’
I t a k u m b u k wa
k uwa m a r a b a a d a ya
maridhiano yaliyofikiwa
na waheshimiwa Amani
Abeid Karume na Maalim
Seifu Shariff Hamad
ya kuacha tofauti zao
za kisiasa na kuundwa
Serikali ya Umoja wa
Kitaifa, gazeti hili Na.
874 la tarehe 22/01/2010,
liliandika makala iliyobeba
kichwa cha: “Zanzibar
yampata “Jalali Mfalme na
Mtaabadi Karama”.
Makala hiyo ilijikita
k a t i k a k u wa p o n g e z a
waungwana Karume
na Seifu kwa hatua yao
Inaendelea Uk. 10

11/26/2015 6:14:11 PM

10
Na Omar Msangi
TA A S I S I y a E l i m u
Ta n z a n i a ( T E T )
imetoa Mwongozo
wa Ufundishaji na
Ujifunzaji wa Somo la
Dini katika Elimu ya
Msingi Tanzania Bara.
Mwongozo huu unapiga
marufuku kusomesha
Somo la Dini kama Ibada,
bali sasa lisomeshwe
kama taaluma. Hoja
ya TET ni kuwa Somo
la Dini likisomeshwa
kwa mwelekeo wa
kumfanya mtoto kufanya
ibada na kuwa mchaMungu, itavunja umoja
n a m s i h i k a m a n o wa
Wa t a n z a n i a n a h a t a
kuvuruga amani iliyopo.
Kwamba somo likitoa
wahitimu ‘Waswaliji’ na
‘wafungaji’ wazuri wa
Kiislamu, watajiona bora
kuliko watu wengine,
kujenga chuki, mfarakano
na mwishowe kuhatarisha
amani.
Ni maoni ya TET
(Serikali) kuwa Somo
la Dini likisomeshwa
kama taaluma, litakuwa
chombo madhubuti
cha kuwaunganisha
Inatoka Uk. 9
ya kusahau tofauti zao,
kuweka kando ukubwa
wao katika taasisi zao
na kuangalia umuhimu
wa kuwaondolea
Wa z a n z i b a r i m a d h i l a
yaliyokuwa yakiwasibu.
Tu l i f i k i a u a m u z i wa
kuwanasibisha na Mfalme
Jalali na Mtaabadi Karama
kama walivyosimuliwa
na Marehemu Shaaban
Robert katika riwaya
ya k e ya K u s a d i k i k a ,
walivyoafikiana kuwaacha
hu ru vi jan a wao s ita
waliotiwa Jela bila kuwa na
kosa la kisheria. Vijana hao
walileta uongozi ulioweza
kuwakomboa Wasadikika
kutokana na madhila ya
ujahili.
Pamoja na kuwapongeza
waungwana Karume na
Seif, tulitumia pia makala
ile kuwatahadharisha
k u wa : “ Wa j i e p u s h e
na kulaumiana,
wajitahadharishe na wale
miongoni mwao ambao
ni mfano wa Saluli katika
kisa cha Muhajirina na
Answar”.
Katika gazeti hilo hilo
Na. 874, Mhariri aliweka
Tahariri iliyochambua
kwa undani na waledi
na ushahidi mzito mengi
yanayoisibu Zanzibar.
Nitakumbushia machache
tu lakini msomaji zingatia
kuwa haya yote hayakuwa
mawazo wala maoni ya
Mhariri, bali marejeo
yaliyohifadhiwa katika

ANNUUR NEW.indd 10

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Dr. Leonard, agenda hii ya nani?
Msemayo hayana ukweli wala maslahi na nchi

Cote d'Ivoire.) Mgogoro
uliosababisha mamia

KAIMU Mkurugenzi wa TET, Dkt. Leonard D. Akwilapo

Watanzania wenye imani
tofauti na kuwafanya
wapendane, kuvumiliana
na kuthamini utu. Na
kwamba katika usomeshaji
huo, yazingatiwe
mambo ya msingi
yanayotuunganisha sote

kama binadamu, ndio
maana mambo ya ibada
yanawekwa pembeni.
Tafiti zimefanyika,
ya k a c h a m b u l i wa n a
kuandikwa mengi sana
juu ya mgogoro wa Ivory
Coast (Cote d'Ivoire

kwa maelfu ya watu kufa.
Tunaambiwa kuwa nchi
hiyo ikiongozwa na Félix
Houphouët-Boigny baada ya
kupata uhuru wake kutoka
kwa Wafaransa mwaka 1960
ilipata maendeleo makubwa
katika miaka ya mwanzo ya
uhuru. Na alijitahidi sana
katika hiyo miaka ya mwanzo
kuwaweka watu wake, wa
kabila na dini tofauti kama
taifa moja.
Hata hivyo, kidogo kidogo
na chini kwa chini yakaanza
kuibuka malalamiko
kwamba, baadhi ya watu
walikuwa wakipendelewa
huku wengine wakibaguliwa
na kutupwa nyuma
katika maendeleo. Katika
waliokuwa wakiona kuwa
hawatendewi haki, ni watu
kutoka Kaskazini mwa nchi
hiyo ambao wengi wao
walikuwa Waislamu.
Alipofariki Rais Boigny
mwaka 1993, na nchi
kushikwa na Henri Konan
Bédié, huyu anatajwa
kuimarisha upendeleo kwa
watu wa kabila lake na watu

Zanzibar inaelekea kubaya
vitabu na nyaraka tofauti
za Kilimwengu.
Yote aliyoyachambua
Mhariri yanatokana na
Kitabu cha Don Peterson;
“ Revolution in Zanzibar,
An American’s cold War
Tale”. Moja linasema;
“Baada ya Mapinduzi
ya Z a n z i b a r h u e n d a
Zanzibar inakuwa kama
Malaysia au Singapore
kimaendeleo.” Marekani
ilihofia kwa maendeleo
hayo na kuhofia kuwa
itakuwa kama Cuba.
La pili ni kuwa, “Hofu
ya Mwalimu Nyerere
ilikuwa kubwa, kama
Zanzibar itapiga hatua
hiyo kimaendeleo huku
Dar es Salaam ikibaki
masikini. Jingine ni
hofu ya Nyerere na Jobu
Lusinde kuwa, Zanzibar
ikiachwa iende kivyake,
itaipiku Tanganyika katika
maendelo. Ni mengi
sana yalichimbuliwa na
kuchambuliwa. Na kwa
hakika ni vyema msomaji
ukapata gazeti hilo upate
kufaidi yaliyonukuliwa
humo.
A l l a h
( S W )
Ametuelekeza ndani ya
Q u r’a n Tu k u f u k u wa
turejee katika historia ili
tujifunze kutoka wale
waliotutangulia. Ndio
maana aya kadhaa za

Qur’an Tukufu zinaanza
na wito wa: “Hal ataaka hadith…….,
Alantara kaifafa ala…..,
Wadhikur fiikitab….”.
Haya na mengine mengi
ndani ya Qur’an Tukufu
ya n a m u a g i z a M t u m e
(SAW) na Uma wake kuwa
wajifunze mengi kutoka
kwa watu waliotangulia.
Kwa muktadha huo,
haya yanayojiri Zanzibar
hivi sasa tutayanasibisha
na kisa cha Nabii Musa
na Harun, na Bani Israil.
Kwa mujibu wa Qur’an,
nabii Musa na Harun (AS)
waliwatoa wana wa Israil
katika utumwa wa Farao
wa Misri na kuwavusha
b a h a r i ya S h a m k wa
idhini ya Allah (SW).
Wakiwa pale jangwani,
Nabii Musa (AS) akaitwa
mlimani na Allah (SW)
kupokea wahay. Wakati
akiwa mlimani alijitokeza
mtu akiitwa Samiriy na
k uwalag h ai wan a wa
Israil na kuwatengenezea
ndama wa dhahabu ili
wamuabudu badala ya
Allah (SW). (Qur’an 20:85
na 95 – 97)
Waheshimiwa Amani
Karume na Maalim Seif
walifanya juhudi kubwa
k u wa t o a Wa z a n z i b a r
katika madhila ya
kuhasimiana, kufarakana

kiasi cha kufikia hata
kutokuzikana baina ya
wana CCM na wana CUF.
Hatua ya kufikia
m u a f a k a wa k u we k a
kando tofauti zao na
kufikia maamuzi ya
kuundwa kwa Serikali ya
Umoja wa Kitaifa ilikuwa
ya kuenziwa. Hata hivyo,
wengine mingoni mwao
hawakufurahia hali hiyo
kwani ni miongoni mwa
wale walikuwa hawataki
Zanzibar istawi. Sasa
huyo ambaye amejivika
uhasimu kama ule wa yule
Samiriy aliyewaghilibu
Ban – Israil ni nani?
K w a
h a k i k a
tusipomtambua
atatufikisha hatua kama ile
ya Waisrail kumwambia
Musa (AS), hatuingii
sisi huko. Hali hiyo
iliwasababishia kuzuiwa
kuingia huko na kupewa
adhabu ya kutangatanga
j a n g wa n i k wa m i a k a
arubaini. (Qur’an 5:23 – 29)
Hebu sisi Wazanzibari
tutafakari na kujihadhari.
Tumtambue huyo Samiriy
wa Kizanzibari tumuepuke.
Kauli kama: “Hatutoi
N c h i k wa K a r a t a s i ” .
“Wakitaka wapindue”,
zitutume kutafuta
suluhu. Tujiulize, kama
wapiga kura wa Zanzibar
ndio waliomchagua

wa Kusini kwa ujumla ambao
wengi wao ni Wakristo. Kilio
na malalamiko kutoka kwa
watu wa Kaskazini yakawa
yanaongezeka kila uchao na
hasa Rais Bédié alipomzuiya
Alassane Ouattara kutoka
Kaskazini kugombea urais
mwaka 1995.
Ubaguzi wa Bédié uliingia
mpaka serikalini na jeshini
ambapo watu kutoka
Kaskazini walijiona kama
wanatengwa na kunyimwa
fursa za vyeo na marupurupu
mbalimbali tofauti na
wenzao wa Kusini. Hali hiyo
ilipelekea jeshi kupindua
serikali na ulipofanyikwa
u c h a g u z i m wa k a 2 0 0 0 ,
Alassane Ouattara, kutoka
Kaskazini, alizuiwa tena
kugombea. Katika uchaguzi
ule Gbagbo alitangazwa
mshindi.
“After becoming president,
Gbagbo began to consolidate
power for his own ethnic group
and continued the exclusion of
northerners in the government
and military.”
Ndivyo taarifa mbalimbali
z i n a v y o s e m a k wa m b a ,
alichofanya Gbagbo baada
ya kushika serikalini, ni
kuimarsiha ubaguzi ndani
ya serikali na jeshini kwa
kuzidi kuwatenga watu wa
Kaskazini (Waislamu), hali

Inaendelea Uk. 11

Rais wa Muungano na
Wabunge wa Muungano
ambao uchaguzi huo ni
halali. Inakuwaje kura
walizopiga kuchagua Rais
wa Zanzibar na Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi
ziwe haramu? Hiki ni
kiroja cha watoto pacha,
mmoja wa halali mwingine
wa haram (bastard).
Tujiulize, hivi mama
mjamzito akajifungua
mapacha, kuna uwezekano
watoto hao mmoja ni
mtoto halali ndani ya ndoa
na pacha wake yeye ni wa
nje ya ndoa?
Mzanzibar gani
mwenye akili timamu
asiyehuzunishwa na
uamuzi wa Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi
(ZEC) kuhalalisha pacha
mmoja na kuharamisha
pacha wa pili.
Tutafakari na tumuombe
Allah atuepushe na
fitina inayotunyemelea.
Bila uamuzi wa busara
na kurejea kwenye haki,
uadilifu na ukweli,
tutaonja ‘joto ya jiwe’ la
Bani Israil kuhangaika
miaka arubaini tukitafuta
‘nchi’, Amani na
Maendeleo, hatutaipata.
Tutazama katika Idhilali na
hatutapata wa kutunusuru
wala kuona mlango wa
kutokea.

11/26/2015 6:14:12 PM

11
Inatoka Uk. 10

iliyosababisha wanajeshi
kutoka Kaskazini kufanya
jaribio la mapinduzi
Septemba 2002 wakiongozwa
na Guillaume Soro. Baadae
wanajeshi hao waliunda
kikosi chao cha uasi
wakikiita New Forces (FN)
na wakafanikiwa kukamata
na kuiweka chini ya udhibiti
wao sehemu kuibwa ya
Kaskazini ya Ivory Coast
na hapo ndio machafuko na
vita kamili ya wenyewe kwa
wenyewe ikaanza rasmi.
Ilikuwa ni vita kati ya serikali
ya Kikristo Kusini (Christian
southern government) dhidi
ya waasi wa Kiislamu wa
Kaskazini (Muslim northern
rebels.)
Vi t a h i y o i l i m a l i z wa
mwaka 2007 kwa kusainiwa
makubaliano ya Ougadougou
(Ouagadougou Agreement)
ambapo pamoja na mambo
mengine ilikubaliwa kuwa
Gbagbo abaki kuwa Rais na
Soro awe Waziri Mkuu.
Katika uchaguzi mkuu
wa Desemba 2010, matokeo
ya awali yalionyesha kuwa
Ouattara alikuwa mshindi
kwa asilimia 54%. Ghafla
ikatangazwa kuwa matokeo
hayo yamefutwa na badala
ya k e L a u r e n t G b a g b o
akatangazwa kuendelea
kuwa Rais. Kilichofuatia
kinajulikana. Ni nchi
kutumbukia tena katika
machafuko na mauwaji
ambapo inakisiwa kuwa
zaidi ya watu 3000 waliuliwa.
“A decade ago, Ivory Coast
was seen as a haven of peace and
prosperity in West Africa. But
under the surface, the country
has long been deeply divided
along ethnic, religious and
economic lines.”
Ndivyo mchambuzi mmoja
anavyohitimisha utafiti wake
juu ya nini kiliisibu Ivory
Coast. Kwamba haitoshi
watu kusema kuwa nchi ni
kisiwa cha amani, lakini je,
katika hali halisi hakuna
malalamiko, japo ya chini
kwa chini, ya baadhi ya watu
kubaguliwa na kuonewa?
Panapofuka moshi,… dalili
ya mvua mawingu na cheche
huzaa moto.
Ukija kwa Anti-Balaka
n a S e l e k a , J a m h u r i ya
Afrika ya Kati, mchezo ni
huo huo. Inaelezwa kuwa
Waislamu ambao ni kama
asilimia 10 mpaka 15 ya
wananchi wa Afrika ya
Kati, wakiwa kama wapo
katika Bahari ya Ukatoliki,
wamekuwa wakibaguliwa
k i a s i u n a a m b i wa k u wa
maeneo yao yameachwa bila
ya miundo mbinu ya msingi
kiasi kwamba unaambiwa
nchi haipitiki kwa zaidi ya
nusu mwaka (wakati wa
mvua). Hakuna barabara,
shule wala hospitali za
kueleweka. Na kwa vile ni
vigumu kwao kufika miji
kama Bangui yenye huduma
nzuri za afya, Waislamu wa
Aftika ya Kati wamejikuta
wakikimbilia hospitali za miji

ANNUUR NEW.indd 11

Makala

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Dr. Leonard, agenda hii ya nani?
Mwalimu Nyerere alikuwa
M katoliki, na alipofika
D a r e s S a l a a m we n ye j i
wake walikuwa wazee wa
Kiislamu na Masheikh.
Mwalimu Nyerere aliwahi
kueleza mwenyewe kuwa
wakati mwingine alikuwa

LAURENT Gbagbo.

Catherine Samba-Panza,
Afrika ya Kati

ALASSANE Ouattara
ya mpakani ya Chad na hasa
mji wa Nyala, Sudan kupata
matibabu. Na ili kupata elimu
wanalazimika kuwapeleka
watoto wao Khartoum.
Ubaguzi, unyanyasaji,
upendeleo na hujuma za
namna hii zinazofanywa na
serikali dhidi ya makundi
tofauti ya raia, ndiyo iliyozaa
Anti-Balaka na Seleka.
Sasa turudi kwa Taasisi
yetu ya Elimu ambayo katika
kusisitiza nukta yake kwamba
suala la ibada lisihusishwe
katika Somo la Dini, inasema
kuwa, ibada na uchamungu
ukisomeshwa utaondoa
upendo na uvumilivu baina
ya waumini wa dini na
madhehebu tofauti. Kwamba
baadhi ya waumini wataona
kuwa dini yao na dhehebu
lao ni bora Zaidi kuliko
jingine hali itakayosababisha
dharau, chuki na kejeli
baina ya watu wa dini na
madhehebu tofauti.
Chuki iliyozaa machafuko

na mauwaji Cote d'Ivoire,
haikutokana na uchamungu
w a Wa k a t o l i k i w a l a
Waislamu. Ilitokana na
ubaguzi uliokuwa ukifanywa
na serikali dhidi ya kundi
moja katika jamii.
Katika Cote d'Ivoire,
tumeona jinsi ambavyo,
serikali ilifikia mpaka
mahali pa kuwazuiya raia
wake kutoka Kaskazini
kushiriki uchaguzi kama
wagombea na hata hatimaye
walipoingia wakashinda,
serikali ikaingilia kati na
kufuta matokeo. Yakazuka
machafuko na mauwaji.
Sasa leo pale Zanzibar
tukifuata nyayo zile zile
za akina Félix HouphouëtBoigny na Laurent Gbagbo
dhidi ya ‘Alassane Ouattara’
wa CUF na Wazanzibari wake,
likitokea la kutokea hatuwezi
kulaumu Ukristo au Uislamu
kuwa umeshindwa kujenga
mshikamano, uvumilivu na
amani Pemba na Unguja.

akiungana na Masheikh
na Wazee wa Kiislamu
katika funga za Sunna
na Dua. Leo Taasisi ya
Elimu inatuambia kuwa
kama dini haitafundishwa
kama ‘taaluma’, italeta
ubaguzi na chuki baina ya
Wakatoliki na Waislamu.
Sheikh Ramia na Mzee
Tambaza na akina Mshume
Kiate na Dossa Azizi
waliompokea na kumlea
Julius Nyerere Mkatoliki,
hawakuwa wanajua
Ukatoliki wa Mwalimu
unasema nini. Uislamu
wao waliusomea katika
Madrasa wakihimizwa
kuwa wacha-Mungu. Tena
wakati ule wakiwa na
Mahakama ya Kadhi. Sasa
leo kama serikali inaona
kuwa kunaanza kuibuka
chuki na mpasuko baina
ya Waislamu na Wakristo,
ijiulize kimetokea nini.
Lakini isisingizie dini.
Cote d'Ivoire na Afrika
ya K a t i wa m e u wa n a
Waislamu na Wakristo,
lakini sababu haikuwa
Dini. Sababu ilikuwa
serikali inayowabagua
na kuwakandamiza
Waislamu.
Sasa kama leo tunafikia
m a h a l i p a k u wa t o z a
Watanzania kodi, lakini
huku pembeni na kwa siri
serikali ikawa na MoU
na baadhi ya makundi
ya kidini, huku mitaani
napo kanzu, kilemba
na ndevu ikawa sababu
ya mtu kukamatwa na
k u i n g i z wa ‘ S h i m o n i ’
na ‘Guanatanamo’, hii
ni hali ile ile aliyosema
mwandishi mmoja juu
ya Ivory Coast kwamba
“Ivory Coast was seen as a
haven of peace and prosperity
in West Africa. But under
the surface, the country has
long been deeply divided
along ethnic, religious and
economic lines.”
Na hilo sio tatizo la
somo la dini. Sio tatizo
la jinsi Somo la Dini
linavyosomeshwa. Na ndio
maana machafuko ya Ivory
Coast hayakumalizwa kwa
“kufundisha Somo la Dini
kama taaluma.”
Bila shaka maofisa
wa TET watakuwa na
kumbukizi za kadhia ya
mabucha ya nguruwe.
Katika tukio lile Waislamu
waliwasilisha malalamiko
yao serikalini wakiomba
sheria za miji zizingatiwe
juu ya ufugaji wa
nguruwe na uwekaji wa
mabucha ya nyama ya
mnyama huyo. Maimamu

saba katika Wilaya ya
Kinondoni waliandika
barua serikalini baada ya
nguruwe wanaofugwa
ovyo kuranda na kuingia
katika misikiti kadhaa
eneo la Ubungo. Na katika
tukio jingine, mama wa
Kiislamu akauziwa nyama
ya nguruwe bila kujua.
Serikali ilipuuza barua
ile wala haikujibu. Vijana
wakachukua hatua.
Mtu mmoja aliwahi
kuniambia kwamba
India ikitokea nguruwe
kuingia msikitini, baada
ya dakika tano, tukio hilo
sio habari tena. Habari
itakuwa makumi kwa
mamia ya watu waliouliwa
na makanisa/misikiti
iliyochomwa moto. Ndio
sasa mtu utauliza kwa
nini watu wameuwana
na kuchoma makanisa
na misikiti, ndio utajuwa
kuwa kuna mtu alivunja
sheria ya mipango miji juu
ya ufugaji, nguruwe wake
akaingia Msikitini!
Labda tuwaulize TET,
vijana wale walichukua
hatua ya kuvunja mabucha
ya nguruwe kwa sababu
walisoma Somo la Dini
kama ibada badala ya
kulitizama kama taaluma?
Mbona wale Masheikh
waliompokea Julius
Nyerere Mkatoliki nao
hawakuwa wamesoma
kwa mtindo huu wanaoleta
sasa TET?
Ukija katika Kadhia ya
Mauwaji ya Mwembechai,
sura ni hiyo hiyo. Serikali
kusimama upande wa
dini moja dhidi ya watu
wa dini nyingine. Kauli ya
Paroko Lwambano ilikuwa
kama agizo kwa serikali.
Wa t u w a k a v a m i w a
misikitini na majumbani
mwao na kutupwa
rumande ikidaiwa kuwa
wanatukana na kukashifu
Ukristo.
Kwa vile hapakuwa na
kosa wala kesi, Serikali
ikaamua kuwatesa
Masheikh, Maimamu
na Waislamu wale kwa
kuwashikilia rumande
kwa zaidi ya miezi sita
bila ya dhamana, hatimaye
kesi zikafutwa.
Labda tuwaulize
tena TET, je, hali kama
hii inajenga umoja,
mshikamano na upendo
baina ya Waislamu na
Wakristo hata kama Somo
la Dini litasomeshwa kama
taaluma?
Ni kwa kuzingatia yote
haya, inabidi kumuuliza
Kaimu Mkurugenzi wa
TET, Dkt. Leonard D.
Akwilapo, hii agenda
ya kutaka Somo la Dini
lisomeshwe kama taaluma,
ya nani? Lengo lake nini?
Mbona hoja na sababu
z i n a z o t o l e wa h a z i n a
ukweli wala uhusiano
katika kujenga Tanzania
yenye umoja, upendo na
mshikamano?

11/26/2015 6:14:18 PM

12
Na Omar Msangi
“YULE nyoka akatupwa,
yule mkubwa, nyoka wa
zamani, aitwaye Ibilisi na
Shetani, audanganyaye
ulimwengu wote,
akatupwa hata nchi…
Ole wa nchi na bahari!
Kwa maana yule Ibilisi
ameshuka kwenu
mwenye ghadhabu
nyingi, akijua kuwa
ana wakati mc hac he
tu!” (Biblia, Ufunuo wa
Yohana 12: 9, 12)
Naomba wasomaji wa
makala hii kabla au baada
ya kumaliza kuisoma,
wafungue rejea zifuatayo
na naamini bado zitakuwa
zinapatikana katika
mtandao:
1. T w o T i m e r s Multiple Role Crisis Actors
Revealed.
2. 2. James Foley ISIS
Beheading Hoax Siblings
Kate and Michael Duping
Delight - Fake Tears Obama
Style!
Itizame mpaka mwisho
mpaka uungane kucheka
na mshereheshaji wa
Makala. Tazama pia:
“Same Actor playing in
two different crisis acting
roles”-(One as Michael
Foley-Brother of James Foley
in the 2014 ISIS beheading
HOAX and another as
Victim Jamie Rohrs in
the 2012 Batman theater
shooting hoax.)
Usichoke, tazama tena
video hii: “The Hacked
Jihad John Footage Smoking
Gun Evidence that Emwazi
is CIA. Au CIA Caught
Filming Fake ISIS Beheading.
W a l i m w e n g u
wamehamanika na hasa
katika ulimwengu wa
U l a ya n a M a r e k a n i .
Kila uchao, utasikia
limefanyika hili au lile
k a t i k a k u wa s a k a n a
k u wa t i a a d a b u wa t u
wanaodaiwa kufanya
shambulizi la kigaidi Paris
pamoja na washirika wao.
Waislamu katika Ufaransa
na Ubeligiji hawana raha.
U k i l a l a h u j u i i wa p o
itakuwa zamu yako ya
kuvamiwa na Polisi na
kubambikwa ‘ugaidi’
au itakuwa jirani yako.
Ilimuradi harakati za
kuwasaka wanaodaiwa
kuwa ‘magaidi’ wakitajwa
kuwa ni IS au Waislamu
wa siasa kali, linakwenda
kwa kasi. Na mpaka
sasa zoezi limefanikiwa
kwa kiwango kikubwa
kuhuisha kitisho cha
ugaidi lakini kubwa Zaidi
ambalo ndio lengo:
“ K u w a t i s h a
Wa l i m w e n g u k u w a

ANNUUR NEW.indd 12

MAKALA

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Jihadhari na ’Shetani’ huyu
Usiziamini televisheni, magazeti yake
Hoji kila anachokuambia. Tumia akili

Uislamu na Waislamu
ni mbegu hatari, kama
si kwa watu wote, lakini
angalau kwa ‘wastaarabu’
wa Ulaya na Marekani.”
Lakini hayo yakiendelea
n a k u s h i k i wa b a n g o
na vyombo vya habari,
maarufu, ‘main stream
media’, baada ya ule
mhemko wa mwanzo,
watu wenye akili zao
t i m a m u n a wa s i o n a
uvivu wa kufikiri,
wanaanza kuchambua
wakitenganisha pumba
na mchele. Na wengi
katika uchambuzi wao,
wanatumia taarifa na
picha zile zile rasmi za
serikali na ‘main stream
media’, kuhoji, nini hasa
kilitokea na nani kafanya
nini na kwa lengo gani?
Pengine na sisi tutumie
fursa hii kuangalia
machache katika
yaliyoibuka ili kupata
uelewa sahihi wa nini
kilitokea Paris katika
kilichoitwa shambulio la
kigaidi lililofanywa na IS.
Tuanze na taarifa kutoka
Israel.
Likiripoti juu ya
s h a m b u l i o l a Pa r i s ,
gazeti la Times of Israel
la Novemba 14, 2015
liliripoti kuwa, ukumbi
wa Disco ulioshambuliwa
ulikuwa unamilikiwa na
Mayahudi wawili ndugu,
na ukauzwa kwa mtu
mwingine siku chache
kabla ya tukio hilo.
“Jewish owners recently
sold Paris’s Bataclan theater,
where IS killed dozens.”

Ndivyo Times of Israel
lilivyoweka kichwa cha
habari na kueleza kuwa
wamiliki hao Mayahudi
ndugu walikuwa ni Pascal
Laloux na Joel.
Habari zaidi zikasema
kuwa, wamiliki hao wa
ukumbi wa starehe wa
Bataclan, walihamia Israel
baada ya kuuza ukumbi
huo ambao walikuwa
wakiuendesha kwa Zaidi
ya miaka 40.
Tuweke kituo hapa
tufafanue nukta moja:
Katika shambulio la
We s t g a t e S h o p p i n g
Mall, Nairobi jumba
lile linamilikiwa na raia
wa Israel. Ile hoteli ya
Pa r a d i s e K i k a m b a l a ,
Mombasa tuliyoambiwa
kwamba ilishambuliwa na
magaidi mwaka 2002 ni ya
raia wa Israel.
Kwa mujibu wa Times
of Israel, Joel akielezea
tukuo hilo anasema
kuwa walipata taarifa ya
kushambuliwa Bataclan
muda huo huo shambulio
likiendelea, magaidi
wakiuwa watu.
“I could hear the gunfire”,
anasema akimaanisha
kuwa alikuwa akisikia
milio ya risasi kupitia
simu ya mtu aliyempigia
ambaye alikuwa katika
eneo la tukio.
Tuweke kituo kingine
hapa tuhoji swali moja
tu la msingi. Magaidi
wameingia mahali,
wanapiga risasi ovyo na
kuuwa watu huku wengine

wakilipua mabomu ya
kujitoa muhanga kama
tulivyoambiwa kuwa
ndivyo ilivyokuwa katika
ukumbi wa Bataclan. Je,
katika hali hiyo, unakimbia
kusalimisha roho yako au
unahangaika kumpigia
simu mtu aliyeko mbali
mpaka unamsikizishia
milio ya risasi?
Akiendelea kusimulia
Joel anasema: “a member
of the Eagles of Death
Metal was hit by a bullet
and killed….There is blood
everywhere. It will take three
days just to clean that up.”
Joel yupo Israel wakati
shambulio likitokea, lakini
muda huo huo, kabla hata
polisi hawajatoa taarifa
anasema kuwa mmoja wa
wapiga muziki wa bendi
ya ‘Eagles of Death Metal’
iliyokuwa ikitumbuiza
alikuwa amepigwa risasi
na kufa.
Tujaaliye ni mtu alikuwa
amempigia simu, katika
hali ile ya mtafaruku,
magaidi wanapiga
na kuuwa watu ovyo,
huyo aliyempigia simu
ameweza kuwachambua
vipi waliokwisha kufa
na k u m t a m b u a h u y o
‘marehemu’ wa ‘Eagles of
Death Metal’ Band?
Lakini zaidi anasema
“There is blood everywhere.
It will take three days just to
clean that up”, akimanisha
kuwa damu imetapakaa
kila mahali na kwamba

itachukua siku tatu
kuweza kuisafisha damu
hiyo!
Tukio linatokea Paris,
we we u p o Te l Av i v ,
ushajua kuwa ukumbi
umetapakaa damu kila
mahali na ushakadiria
kuwa bila siku tatu za
kufanya usafi wa uhakika,
basi damu hiyo haiondoki!
“Blood Every where”,
ndivyo pia anavyoripoti
Julien Pearce (reporter &
Eyewitness) akinukuliwa
katika France 2/AFP na
Reuters, akidai kuwa
damu imetapaa kila
mahali kutokana na watu
kuraruliwa na risasi za
AK-47 za magaidi. Lakini
akiyasema hayo, picha
hazioneshi hata mtu
mmoja aliyepigwa risasi
na kuchuruzika damu.
Lakini ukiacha maswali
h a y o , m wa n d i s h i n a
mchambuzi mmoja
akichambua habari za
Mayahudi hao Pascal na
Joel katika gazeti la Times
of Israel, amekusanya
picha zote za CCTV na
zile zilizotolewa na polisi
na vyombo vya habari
zikielezea hali ilivyokuwa
wakati wa tukio, kisha
anauliza “iko wapi
damu?”
“Blood Bath in Paris”,
hizo ndio taarifa za
vyombo vya habari Ulaya
na Marekani. Ni kama
kusema Paris yalowa
damu kutokana na
shambulio la maghaidi
wa IS!
“Where is Blood?” Ipo
wapi damu? Wanahoji
wachambuzi wengi baada
ya kupitia picha zote
zilizokwisha kutolea na
polisi na vyombo vya
habari. Katika uchambuzi
huo, wanakuonyesha
‘clips’ za picha ndani ya
ukumbi kabla na baada
ya ‘shambulio’, hakuna
damu hata tone. Kuna
watu wamelala chini
wanaodaiwa kuwa ni
‘maiti’ wamefunikwa
shuka nyeupe safi, hazina
hata tone la wekundu wa
damu. Watu wanauliza,
watu hawa wameuliwa
kwa risasi za magidi,
mbona hawana majeraha
(open wounds)? Mbona
shuka walizofunikwa
hazina damu?
Lakini jingine
tunaambiwa alikuweko
mshambuliaji wa kujitoa
muhanga aliyelipua bomu.
Sasa unapelekwa ndani
ya huo ukumbi baada
ya shambulio, hakuna
hata kiyoo kimoja cha
madirisha kilichovunjika.
Katika baadhi ya meza
vikombe vya chai na gilazi
za vinjwaji zipo kama
zilivyokuwa juu ya meza
ila tu kuna viti viwili
vitatu vimepinduliwa.
Inaendelea Uk. 19

11/26/2015 6:14:19 PM

13

Safu ya Ben Rijal

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Misikiti katika Mji Mkongwe wa Zanzibar - 4

Mji Mkongwe wa Zanzibar
uliosimama pembezoni
mwa fukwe za kisiwa cha
Unguja ni eneo lilosheheni
tarekhe ya kila aina. Misikiti
iliyozunguka mji huu ni
mingi. Unapokuwa katika
mji huu huna sehemu ya
mtaa wake mmoja usiwe
umezungukwa na Misikiti
isiopungua 5.
Kama nilivyokwisha
kuelezea kabla katika
makala haya kuwa Misikiti
yote hiyo wajenzi wake
walikuwa ni wazalendo
waliokuwa wakiishi hapo
pasi kuangalia ufadhili
kutoka nje ikiwa ndio mtindo
wa siku hizi panapotaka
kujengwa Misikiti na
inapotaka kujengwa husubiri
ufadhili kutoka nje na kama
kutasubiriwa ujenzi utokane
na michango ya waumini,
utachukua muda mrefu sana

Sura ya Msikiti wa Ijumaa katika miaka ya 60
hadi kuweza kufanikishwa
lengo la kuusimamisha
Msikiti uliokusudiwa
kujengwa. Utakuta mara
nyengine Misikiti kuamua
kununua pampu ya maji ya
Shillingi laki na nusu hapo
utakiona kishindo mchango
utapochangishwa tena siku
ya sala ya Ijumaa, ukiuliza
kilichopatikana utaambiwa
zimepatikana shillingi alfu
kumi na tano au ishirini na
hao wachangiaji zile pesa
zilikuwa kwake hazina uzito
kama shillingi 100 au 200 au
500 ndizo huingizwa katika
kisanduku cha mchango.
Unapoisoma tarekhe ya
Misikiti iliojengwa katika Mji
Mkongwe wa Unguja utaona
jinsi waumini walioifahamu
namna ya kuitafuta Pepo

kwa walivyoitikia wito na
kujitolea kwa mali zao katika
ujenzi wa Misikiti.
Misikiti mbalimbali
Msikiti Baraza, katika
Msikiti huu kuna chuo
amabcho husomesha vijana
kujua kusoma Qu’ran na
kujifunza masomo ya dini
ikiwa pamoja na masomo ya
Fiqhi, hukumu za Qur’an,
hadithi za Mtume (SAW) n.k.
Chuo hichi cha namna yake
kikiana kuchukua wanafunzi
kuanzia umri wa miaka
mitano mtoto hupelekwa
kusoma hapo Msikiti Barza na
kulelewa kimaadili na kidini
na mtindo huo haujasita
hadi leo unaendelea. Msikiti
huu ni wa ghorofa mmoja,
chini kuna Msikiti na chuo
kikikuwepo juu.

Msikiti Baraza upo katika
eneo la Mkunazini, hajulikani
mjenzi wake khasa alikuwa
nani ila wengi wakiamini
kuwa Khamisi bin Uthman
mfanya biashara aliokuwa
akimiliki sehemu kubwa ya
majumba katika eneo hilo
kuwa labda ndio aliokuwa
mjenzi wa Msikiti huu, kwani
alikuwa akisali sala zake zote
hapo. Aidha akiuhudumia
Msikiti huu ulikuwa tayari
umeshasimama katika karne
ya 17 katika mwaka wa 1800
na kitu.
Wamesomesha watu wengi
katika Msikiti huu na darsa
zake zilikuwa Msikiti hujaa
na watu wengine hukosa
nafasi ndani wakabakia nje ya
Msikiti na kufwatilia darsa.
Sheikh Abdalla Saleh Farsy
kabla ya kuhama Zanzibar
na kuhamia Mombasa, Kenya
alikuwa akisomesha darsa
ya tafsiri ya Qur’an hapo na
ilikuwa huwezi kutia mguu
katika darsa hio iliyokuwa
ikifwatiliwa na wazee na
vijana wa makamo. Sheikh
Abdalla Saleh Farsy alikuwa
na upeo mkubwa wa tarekehe
kwa hio anapokizungumza
kitu hutoa na tarekhe yake.
Inasemekana kuwa fikra
ya Sheikh abdalla saleh
Farsy ya kutafsiri Qur’an
kwa Kiswahili ilimjia akiwa
anasomesha hapo Msikiti
Barza na kati ya wanafunzi
wake ambao akiwapa kazi

kila baada ya darsa kuandika
kile kilichosomeshwa alikuwa
Syd Abdulwahab Alawy na
wengineo, akitumia tafsiri
ya Jalaleyn ingawa katika
utangulizi wa tafsiri hio
alitumia Fitafahmul Quran ya
Sayid Abdul A’la Maududi.
Misikiti ya Ijumaa
Forodhani na Malindi
Misikiti hii ni maarufu
sana mmoja ukiitwa Msikiti
wa Ijumaa Forodhani na
kwa jina jengine ni Msikiti
wa Ijumaa mdogo na ule
mwengine ni Msikiti wa
Ijumaa wa Malindi au kwa
jina jengine Msikiti wa
Ijumaa mkubwa. Msikiti
wa Ijumaa wa Forodhani
unaunganishwa na kabila
la Kishatry ndio watu wa
m wa n z o k u u s i m a m i s h a
Msikiti huu. Ulikuja
ukabomoka Msikiti wote
kutokana na tetemeko la
ardhi lilotokea mwaka wa
1846. Ulipotaka kujengwa
tena alikuwa ni Sheikh Said
bin Seif al-Muharami ndio
aliokuja kuusimamisha tena
Msikiti huu. Sheikh Said bin
Seif al-Muharami alikuwa
ni mfuasi wa madhehebu
ya Ibadhi lakini alijenga
Msikiti ambao waliokuwa
wengi wao wakisali hapo na
hadi leo ni wale wanaofwata
madhehebu ya Sunni/
Shafii. Msikiti huu ulikuwa

Inaendelea Uk. 18

Sheikh Ali bin Khamis bin Salim Al-Barwany -6

K AT I K A k u e n d e l e a
kuwazungumzia wana
wazuoni wetu waliopita,
leo nitazungumzia gwiji
ambaye aliendeshana nyuga
na puta na watawala, huyo
sio mwengine ni Sheikh Ali
bin Khamis bin Salim AlBarwany.
Sheikh Ali bin Khamis bin
Salim Al-Barwany ni katika
Masheikhe ambao waliishi
katika umri mdogo sana
na kupitia misukosuko ya
kufungwa pale alipokuja
kukhitalifiana na mtawala
wa nyakati hizo kutokana
na madhebeu aliozaliwa
nayo nakuingia madhehebu
nyengine.
Sheikh Ali bin Khamis bin
Salim Al-Barwany alizaliwa
mwaka wa 1267 AH( 1852)
katika mtaa wa Baghani mtaa
ambao ukikaliwa na tajiri
mmoja mkubwa wa Zanzibar
aliokuwa akijulikana kwa
jina la Bwana Udi. Sheikh
Ali bin Khamis alikulia
katika mtaa huo wa Baghani.
Akiwa katika umri mdogo
alianza kujiunga na baraza
ya mfalme na kujadiliana
na wana baraza masuala ya
kila aina, kuanzia ya dini na
mambo ya kijamii. Akiwa
mwana baraza alikubalika

ANNUUR NEW.indd 13

SHEIKH Ali bin Khamis bin Salim Al-Barwany, huyu ni mwalimu wa Sayyid
Mansab na hawakupishana kwa namna ya mitizamo yao ilivyokuwa. Sheikh
Ali bin Khamis bin Salim Al-Barwany ni katika Masheikhe ambao waliishi
katika umri mdogo sana na kupitia misukosuko ya kufungwa pale alipokuja
kukhitalifiana na mtawala.
vilivyo kwani alitokana na
aila ambayo ilishikamana
vilivyo na majlisi ya mfalme,
kwa hiyo haikuwa tabu naye
kukubalika.
Sheikh Ali bin Khamis
bin Salim Al-Barwany
alibahatika kukutana na
wanavyuoni mbalimbali
ambao walikuwa wakimvutia
na kuanza kusoma kwao.
Kwa muda mfupi kabisa
aliweza kubadilika katika
macho ya watu kutokana na
uwezo aliokuja kuwa nao
wenye upeo mkubwa wa
elimu na hoja zilizokuwa na
uthabiti ndani yake.
Kati ya walimu wake
walioanza kumiminia elimu
walikuwa Makadhi wakubwa
wa madhehebu ya Ibadhi
a k i we m o S h e i k h Ya h ya
bin Khalfan Al-Kharusy
na Sheikh Muhammad bin
Suleiman Al-Mendhary.
Aidha, alisoma sana
kwa Sheikh Abdul Aziz

Abdulghany Al-Amawy,
ambaye akitajikana kati
ya maulamaa wakubwa
wa Kisuni wa wakati
huo. Akiwa anasoma kwa
mashekhe mbalimbali na
kupanua uwezo wake wa
kielimu na kushikamana nao
sawasawa, mara akaingia
nchini gwiji aliobobea katika
fani mbalimbali za dini ya
Kiislamu Sheikh Khamis bin
Slim Al-Khasby, Sheikh Ali
bin Khamis kusikia ujio wa
shekhe huyo akamvaa akawa
hatoki kwenye darasa zake
na aliweza kujifunza lugha ya
Kiarabu kwa upeo mkubwa
na fani mbalimbali za dini
ya Kiislamu na akawa ni
mmoja wa watu wanaoweza
kucheza na lugha ya Kiarabu
vilivyo na kuwa mwandishi
wa mashairi anayesifikana.
Syd Barghash alikuwa kati
ya wafalme ambao akipenda
maendeleo na kuona nchi
inasonga mbele katika nyanja

mbalimbali za kimaendeleo.
Kati ya mambo aliyoweza
kuyafanikisha kwa haraka
katika utawala wake, ni
kuweza kusambazwa kawa
maji katika maeneo ya mjini,
kuingiza karafuu ambazo
zikaja kuwa ndio uti wa
mgongo wa uchumi wa
Zanzibar pamoja na kuagizia
mtambo wa kuchapishia
vitabu ukiwa ndio mtambo
wa mwanzo kuonekana
katika nchi za Afrika ya
Mashariki.
Mtambo huo wa
kuchapishia vitabu katika
s i k u z a a wa l i u l i k u wa
kupiga chapa vitabu vya
Kiibadhi, ikawa kila kitabu
kinachochapishwa Sheikh
Ali bin Khamis bin Salim
Al-Barwany akikitungia
shairi ya kukisifu na kukipa
sura ambayo msomaji
atakikubali kitabu hicho
kilichochapishwa. Kutokana
na kazi nzuri aliokuwa

kiifanya ikawa kila siku
zikisonga mbele Sheikh Ali
bin Khamis bin Salim AlBarwany cheo chake kwa
mfalme kilikuwa kikipaa.
Kiu chake cha kujielimisha
kilikuwa kikubwa hasa akiwa
ni kijana mdogo sana kiumri
baada ya kuhitimu vizuri
masomo yake kwa Sheikh
Khamis bin Slim Al-Khasby
alikuja kushikamana naye
vilivyo. Sheikh Khamis bin
Slim Al-Khasby ni mzaliwa
wa Lamu na alikulia katika
mji mtukufu wa Makka.
Inasemekana kuwa ndio
aliokuja kumgeuza
madhehebu Sheikh Khamis
b i n S a l i m A l - B a r wa n y
kutoka Ibadhi na kuwa
S u n n i . K u b a d i l i k wa k e
madhehebu kulimkera sana
Sayyid Barghash na kumtaka
arudi katika madhehebu
ya k e ya a s i l i ya wa z e e
wake lakini Sheikh Khamis
bin bin Salim Al-Barwany
a l i s h i k a u z i u l e u l e wa
kutotaka kubadilika, baada
ya kushikilia msimamo wake
alifungwa jela na kuwekwa
korokoroni kwa matumaini
kuwa kuwekwa korokoroni
huwenda akabadili mawazo,
lakini ilikuwa kinyume
Inaendelea Uk. 18

11/26/2015 6:14:20 PM

14

MAKALA/MASHAIRI

'Medurusu kwa makini, diwani za manyakanga,
Ndanimwe ni'chobaini, ufarisi wa kutunga,
Sikushufu walakini, wa nudhumu kubananga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Nilibtadi diwani, ya 'Sheria za Kutunga',
AMRI wake ubini, KALUTA aloitunga,
Kwa uketo n'kabaini, kaifiya ya kutunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani

Nikafwatisha diwani, ya galacha wa kutunga,
Sautiye ya kizani, kwa lakabu ANDANENGA,
Nikaongeza uoni, kwa tungo zenye kianga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Kisha nikaja diwani, ya KANDORO kuienga,
'STAHARAKI' si geni, kwa mwendowe wa kugonga,
Ugunge nikabaini, anuwai wa kulonga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Thuma za kwake diwani, 'mwana'ufukwe wa Tanga,
Si mwingine SHAABANI, ROBATI ni la kupanga,
Babaye yu SELEMANI, kunga toka kwa wahenga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Si Bara si Visiwani, sijamshufu malenga,
Mithili ya za SHABANI, idadiye alotunga,
Si haba zake diwani, arubashara katunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Maudhui mwake ndani, nyanja tumbi yamegonga,
Siasa pamwe na dini, SHABANI hajavitenga,
Uchumi, utamaduni, vyote pamoja kakonga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Kadhalika na kwa fani, nudhumuze si mtonga,
Kwa vina na kwa mizani, kawimu kama mninga,
Si mavue wala guni, arudhi zenye kuchunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Mashairi si mizani, wala vina twajivunga,
Tungo tutumbi kudhani, ndizo tungo twajikenga,
Maudhui bila fani, muhali mioyo kukonga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Tofauti yetu nini, na nathari wanotunga,
Kwa utuvu andisini, na kwa makini kulunga,
Ukweli mtabaini, pamwe yele na ukenga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Tungo zetu wengi guni, wa zama hizi malenga,
Zimejaa walakini, hilo siwezi kukenga,
Si kama za wa zamani, maalimu wa kutunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Tujifunze kwa SHABANI, KALUTA na ANDANENGA,
Pamwe na kwa SAADANI, na wengine manyakanga,
Diwanizo tusomeni, zitatufunda kutunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Waaidha na uneni, wa kujuvya na kugunga,
Kwa balagha na bayani, na ujumi wa kulonga,
Lugha ina zake fani, Tuzitwalii malenga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
Washairi maizini, dhamira si kuwapinga,
Bali kukuchocheeni, nudhumu nyofu kutunga,
Mithili ya wa zamani, mafarisi wa kutunga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!
ABUU NYAMKOMOGI,
MWANZA.

ANNUUR NEW.indd 14

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Msamaha

JAPO NUDHUMU TWATUNGA.....!

Arudhi nilibaini, za namna ya kutunga,
Tena si utunzi guni, wa nudhumu kubananga,
Bali ule wa kanuni, wa tungo kuzifinyanga,
Japo nudhumu twatunga, si kama za wa zamani!

AN-NUUR

NA SHEIKH MUHSIN
ASAYID MOHAMED

S

H U K U R A N I
zote anatsahiki
Mwenyezi Mungu,
M o l a m l e z i wa
u l i m we n g u . M w i s h o
mwema ni kwa wacha
mungu na hakuna
uadui isipokuwa kwa
madhalimu.
Rehema na amani
zimfikie mbora wa mitume
na mwisho wa manabii,
aliye nrehema kwa
viumbe wote, mtume wetu
Muhammad na jamaa zake
za sahaba zake wote.
Kwa hakika Uislamu
ni dini inayozungumza
akili na kiwili wili na
humlazimisha Muislamu
k wa l i l e a n a l o l i we z a
kulitekeleza, na wala
hauja mlazimisha hata
mtu mmoja kufanya jambo
asiloliweza isipokuwa lile
analoliweza tu. Mwenyezi
Mungu ndiye ambaye
amemuuomba binadamu
na nafsi na anaijua uwezo
wake.
Amesema Mwenyezi
Mungu mtukufu:“Hailazimishi nafsi
isipokuwa inaloliweza”
(Baqara: 286).
Uma wetu wa Kiislamu
ameusifu Mwenyezi
Mungu katika kitabu chake
kitukufu kuwa ni uma
wa kati na kati. Amesema
Mwenyezi Mungu
mtukufu:“Na hivyo hivyo
tumekufanyeni uma
wakati na kati ili muwe
mashahidi kwa watu na
awe mtume kwenu ni
shahidi” (Baqara:143)
Mtume (saw) anasema,
“Nimetumilizwa katika
dini nyepesi”.
Laiti tutasimama
katika neno “nyepesi”
kwa kuangalia chochote
m i o n g o n i m wa s o m o
linalopatikana kwa upande
wa lugha na kisheria,
t u t a k u t a u we p e s i wa
kisheria ya Kiislamu tena
kwa uwazi kabisa kwa
yule anayeathirika na

uadilifu na kutoa haki
bila ya ujeuri au kupendela
mtu. Hebu tuanze hivi sasa
kwa maana ya kilugha
na tukimbilie neno
ambalo linalolitangaza
neno la Kiarabu ambalo
linaanzwa na herufi (sini)
na likamalizikia na herufi
(hai. Hakuna makosa
kuwa inahofisha kwamba
inazunguka upande wa
maana inayoshirkiana
baina yake. Inawakilisha
juu ya uwepesi na kuvaana
nako amesema Mwarabu,
mtu msamehevu kwa
watu mongoni mwa
watu wasamehevu na
mwanamke msamehevu
miongoni mwa wanawake
wenye kusamehe na
katika maneno juu ya
hilo hakika kwenye haki
msamehevu juu ya ubatili
na pia anasema Mwarabu
“msile mwepesi umeruka”
wala haukuasi. Kutokana
na hilo, wakasema “dini
n ye p e s i ” k wa m a a n a
iliyoepukana na ugumu na
uzito, maneno kutokana
na muelekeo huu,
linamaanisha uwepesi
na urahisi kwa namna
yoyote ya mpangilio wake
kwa sampuli yake kwa
kiasi cha hitilafu njia ya
mgawanyiko.
Katika hadithi:“uwepesi ni faida” na
kutokana na hilo, umekuja
wasifu Uislamu kuwa
ni dini nyepesi ambayo
haina dhiki wala ugumu
wala matatizo. Huenda
ikawa miongoni mwa
haki, tuashiria kwamba
matatizo ambayo
amekataa Mwenyezi
Mungu juu ya Uislamu na
imekataa mtazamo sahihi
juu ya sheria, haikua wazi
kidunia katika muono wa
Waarabu wa wazi nafsi
zao hadi akabainisha
kwao mfasiri wa wa Qurani, naye ni Ibnu Abbas
pale alivyosema: “Huo
ndio upana wa Uislamu
wa mtume katika watu
m i o n g o n i m wa wa t u
wake akamuuliza juu ya
matatizo akamwambia
na kuwaambia na wao
pamoja:
“Hivi nyinyi si
Waarabu?” Akamwita
m m o j a wa K i h u z a i l i
akamwambia, “hivi
matatizo kwenu ni nini?
Akasema matatizo ni mti,
ni jambo ambalo halina
matatizo. Amesema Ibnu
Abbasi (ra), “hilo ndilo
tatizo ambalo ameliondoa
Mwenyezi Mungu nalo

ni lile lisilo na matatizo.
Ama maana ya kisheria,
kwa maana ya neno la
msamaha ina maana ya
kuepukana na matatizo juu
ya Muislamu humuandaa
kukubali katika dini
ili ishikamane na ili
kusimamisha matendo
na ukweli wa rehema za
Mwenyezi Mungu kwa
waja wake. Na uwepesi
na msamaha sio alama
na nembo ya mpito
ambayo husemwa kwa
wakati maalum tu, bali ni
muongozo wa kimaisha na
katiba ya uma. Miongoni
mwa msamaha kwamba
sheria imekusanya mambo
mawili, faradhi (lazima)
na ruhusa na Mwenyezi
Mungu. Anapenda
kuchuliwa ruhusa zake
kama anavyopenda
kutekelezwa faradhi zake
kama ilivyokuja katika
hadithi sahihi-kwamba,
amesema Mtume (saw)
amesema Mwenyezi
Mungu “na hakufanya
kwenu ugumu katika dini”
(Al-Haj: 78)
Mambo ya uwepesi
kuwa ni muongozo
wa thabiti katika dini.
Amesema Mwenyezi
Mungu “wepesi na wala
hawatakii uzito” (Baqara:
185)
Laiti tukichukua
mifano mbalimbali,
tutakuta mwanzoni
m wa i b a d a a m b a z o
zimesimamia uwepesi
na kuondoa ugumu na
mashaka na wanasheria
wamechukuwa kanuni
za sheria hii kama vile
“jambo linapokuwa
gumu wepesi upokaribu
na mashaka huvuta
uwepesi” na “dharura
huruhusu vilivyo haramu”
na “dharura hakadiriwa
kwa kiasi chake.”
Pia tunakuta wepesi
katika kuhudumiana
kwa neno lake Mtume
(sa) kwamba, Mwenyezi
Mungu humrehemu
mtu ambaye anapouza
h u wa m s a m e h e v u n a
anaponunua na anapodai
deni.” Na katika
mapokezi mengine na
pale anapokopesha. Na
msamaha unakuwa hata
katika kauli. Amesema
Mwenyezi Mungu
mtukufu “Na waambie
watu maneno mazuri.” Na
neno lake “Ita watu katika
dini ya Mola wako mlezi
kwa hekima na mawaidha
mazuri na jadiliana nao
kwa yale yaliyo mazuri
Zaidi.”

11/26/2015 6:14:20 PM

15

MAKALA

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Mashambulizi ya Paris, nani alaumiwe?

I

Na Said Rajab

JUMAA ya Novemba
13 mwaka huu,
ilidaiwa kuwa jiji la
Paris, nchini Ufaransa,
lilishambuliwa kwa mabomu
ya kujitoa muhanga, hali
iliyosababisha vifo vya
watu 230 na wengine
kadhaa kujeruhiwa. Kwa
takriban wiki yote ya jana,
tulishuhudia vyombo vya
habari vya nchi za Magharibi
vikiripoti tukio lile kama
habari ya kwanza yenye
uzito mkubwa. Licha ya
hatari ya kuhukumu kabla
ya uchunguzi kufanyika,
hisia za watu wote duniani
zikaelekezwa na vyombo
hivyo kwamba waliolipua
mabomu yale ni Waislamu.
Ulimwengu umeshuhudia
maneno ya chuki dhidi
ya Uislamu yakihusishwa
na tukio hilo. Wanajaribu
kuhusisha uhalifu ule na
Uislamu.
Ningependa kuchambua
kidogo baadhi ya mambo
kuhusu shambulizi hili, ili
iwe changamoto ya fikra
kwa wasomaji wanaofuatilia
masuala ya ulimwengu.
Matukio kama hayo
yanapotokea, basi fursa pia
hupatikana ya kuwekana
s a wa k i m t a z a m o . K wa
masikitiko makubwa, kelele
hizi za vyombo vya habari,
zikiungwa mkono na maoni
ya wanasiasa wenye chuki
dhidi ya Uislamu, zinajenga
mtazamo kwamba, ingawa
Wa i s l a m u w o t e s i y o
"magaidi", lakini "magaidi"
wengi hakika ni Waislamu.
Hata hivyo, mtazamo kama
huo unakosa mashiko, pale
unapoulinganisha na idadi
halisi ya mashambulizi ya
kigaidi. Gazeti la Europol
lilichapisha takwimu
zinazoonyesha kwamba kati
ya mwaka 2006 mpaka 2008,
asilimia 99.6 ya shughuli
zote za kigaidi barani
Ulaya, zilifanywa na wasio
Waislamu.
Kinachokera zaidi ni
kwamba taarifa potofu za
vyombo vya habari ndizo
zinazoaminika na kujenga
mitazamo hasi dhidi ya
Waislamu, lakini zile halisi
hazipewi nafasi, kwa hiyo
h a z i j u l i k a n i k wa wa t u
wengi. Tatizo lingine kubwa
la vyombo vya habari ni
kutoa tuhuma za jumla
jumla. Yaani Muislamu
mmoja akituhumiwa kufanya
uhalifu, basi jamii nzima
ya Waislamu inalaumiwa
kwa hilo. Kimsingi, Uislamu
u n a k a t a z a v i t e n d o v ya
ukatili na kumwaga damu
za watu wasio na hatia, kama
tulivyoona katika mabomu
ya Paris. Kwanini Waislamu
wote wanaoishi Ufaransa
walaumiwe, wasumbuliwe
na watishiwe kwa sababu ya

ANNUUR NEW.indd 15

mabomu ya Paris?
Siyo Wakatoliki wote
wanaohusishwa na kashfa
ya kulawiti watoto, kwa
sababu tu baadhi ya mapadri
wamekuwa wakifanya
uchafu huo! Siyo Waingereza
wote ni waongo, kwa sababu
tu Serikali ya nchi hiyo,
iliudanganya ulimwengu
kuhusu Iraq kumiliki silaha
z a m a a n g a m i z i m wa k a
2003! Vilevile kuhusika
kwa Muislamu mmoja
katika uhalifu au tuhuma,
haiwafanyi Waislamu wote
katika jamii husika kuwa
wahalifu wa tuhuma hizo!
Vyombo vya habari vya
Magharibi vimewazoesha
watu wake kuwaangalia
Waislamu kama "Wao" na
wenyewe kujiona "Sisi"
ingawa wote ni raia wa nchi
moja. Mara nyingi utakuta
vyombo hivyo vinaripoti
matukio kama ya Paris katika
misingi ya "Wao", "Sisi", "Yao"
na "Yetu". Huwa wanasema
"Wao" hawapendi maadili
" Ye t u " . Wa m e s h a w e k a
kizingiti katika akili za
watu wao na Waislamu.
Wa m e j e n g a m a z i n g i r a
Waislamu waangaliwe kwa
mashaka kila uhalifu kama
wa Paris unapotokea.
Lakini mtu anahitaji
kuelewa msingi hasa wa
mashambulizi kama haya
ni nini? Kwa bahati mbaya
sana, mjadala kama huu
unapuuzwa kwa makusudi
kwa sababu utatoa taswira
Inatoka Uk. 5

ya wazee wenye umri wa
m iaka zaidi ya 60 nchini
China ilifikia kiasi cha milioni
140, ikichukua 11% ya jumla
ya idadi ya watu ya China.
Kwa kufuata kigezo cha
Umoja wa Mataifa, idadi ya
wazee wenye umri wa miaka
zaidi ya 60 ikizidi 10% ya
jumla ya idadi ya watu wake,
nchi hiyo inahesabiwa kuwa
ya jamii yenye idadi kubwa
ya wazee.
Tangu mwishoni mwa
miaka ya 90 ya karne iliyopita,
China iliingia kwenye jamii
yenye idadi kubwa ya wazee.
Ilipofika mwaka 2010, idadi
ya wazee wenye umri wa
miaka zaidi ya 60 nchini
China ilifikia 13% ya jumla
ya idadi ya watu wa China.
Naibu Mkurugenzi wa
ofisi ya Kamati ya shughuli
za wazee ya taifa Bw. Li
Bengong alisema, China ikiwa
ni nchi kubwa inayoendelea,
kutokana na hali ya idadi
kubwa ya wazee, ongezeko
la kasi la idadi ya wazee na
maendeleo yasiyo na uwiano
katika sehemu mbalimbali,
China imethibitisha lengo
la kuhimiza maendeleo ya
huduma ya wazee katika
mambo ya fedha, matibabu,
elimu na burudani.

sahihi na kuzikamata Serikali
za Magharibi kuwa ndizo
zinazojenga mazingira ya
chuki na hasira za kiasi hicho.
Serikali ya Ufaransa,
ikishirikiana na washirika
we n g i n e wa M a r e k a n i ,
imefanya uhalifu wa
kutisha dhidi ya Waislamu.
Ukiangalia mateso ya Libya,
Syria, vifo vya Iraq, Yemen,
Somalia, kuingilia kijeshi
Mali, kuunga mkono uhalifu
wa Israeli dhidi ya Palestina,
unaweza kuona sababu halisi
za huzuni, hasira na hisia
za wale wanaonyanyaswa.
Haya ndiyo masuala
mazito ambayo ulimwengu
wa M a g h a r i b i h a u t a k i
kuyaangalia kwa ukweli
wake. Uvamizi wa mataifa
ya Magharibi katika nchi
zingine na kudhibiti mambo,
umesababisha amani
kutoweka sehemu kubwa ya
dunia na uharibifu kutawala,
jambo ambalo linazalisha
chuki kwa viwango vikubwa
na vidogo. Ni jambo la upuuzi
sana kujaribu kukwepa hisia
zinazoendana na ukweli
huu na kuhamishia lawama
kwa Uislamu kama Itikadi.
Bila shaka, kujibu mapigo
kwa kuwashambulia wasio
na hatia inakatazwa katika
S h e r i a ya K i i s l a m u , n a
hakuna kisingizio chochote
cha kuhalalisha hilo, lakini
muktadha nyuma ya vurugu
za kisiasa, ambazo Waislamu
wanahusishwa, mara nyingi
hupuuzwa.

Tukienda mbali zaidi,
h e b u t u f a n ye t a t h m i n i
ndogo tu jinsi shambulizi
la Paris lilivyoripotiwa kwa
mapana na vyombo vya
habari vya Magharibi kama
unyama, halafu tulinganishe
na unyama unaofanywa
na mataifa ya Magharibi,
Ufaransa ikiwemo, dhidi ya
mataifa mengine. Vifo vya
maelfu ya watu katika nchi
za Syria, Iraq, Afghanistan,
Palestina, kwa vipimo vyote,
ni hali ngumu zaidi kuliko
vifo vya watu 230 vilivyotokea
Paris. Kwanini vyombo
vya habari na huruma ya
ulimwengu hailekezwi dhidi
ya unyama unaofanywa
kwenye nchi hizo, badala yake
tunalazimishwa kuamini
kwamba kilichofanyika Paris
ndiyo unyama zaidi? Hisia
hii ya huruma na huzuni
i l i y o o n y e s h wa k w e n y e
shambulizi la Paris huwa
inakwenda wapi wakati
Israeli inapoangusha
mabomu mahospitalini na
kuua raia kule Palestina?
Maneno makali ya kulaani
mashambulizi dhidi ya watu
wasio na hatia na upotevu
wa maisha ya binadamu
h u wa ya n a k u wa wa p i ,
wakati wananchi wa Libya,
Mali, Iraq, Afghanistan,
Pakistan na kwengineko
wanapoangamizwa? Hao
wanaoomboleza uhalifu
uliofanyika Paris wajitathmini
kama wanaweza kutaja hata
jina moja tu la muathirika wa

Maisha ni marefu China
Ili kutimiza vizuri lengo
h i l o , s e r i k a l i ya C h i n a
imechukua hatua mbalimbali
kulinda haki na maslahi
ya wazee, na kusawazisha
uhusiano kati ya huduma
za wazee na maendeleo ya
uchumi na jamii.
Katika miaka ya hivi
karibuni, serikali ya
China imejenga mfumo
wa dhamana kwa wazee
unaozingatia hali ya serikali,
jamii, familia na wazee, ili
kuhakikisha mahitaji ya
kimsingi ya wazee. Hivi sasa
utaratibu wa bima ya uzeeni
ya wafanyakazi wa viwanda
vya mijini umeundwa. Hadi
k u f i k i a m w i s h o n i m wa
mwaka 2005, idadi ya watu
waliojiunga na bima ya
uzeeni nchini China ilifikia
milioni 175, wakiwemo
wafanyakazi wastaafu zaidi
ya milioni 40. Mbali na hayo
serikali ya China imejenga
utaratibu wa dhamana kwa
kima cha chini na bima ya
uzeeni sehemu za vijijini,
ambao unaweka dhamana
kwa maisha ya kimsingi ya
wakazi maskini, wakiwemo
wazee maskini wa sehemu

ya vijijini.
Serikali pia imefanya kazi
kubwa kupunguza mzigo
wa gharama za matibabu
kwa wazee na kutoa msaada
maalumu wa tiba kwa wazee
na wagonjwa. Hadi kufikia
m w i s h o n i m wa m wa k a
2005 zahanati zaidi ya elfu
15 zilijengwa katika miji
mbalimbali nchini China,
ambazo zinatoa huduma za
afya na tiba kwa wazee hata
majumbani mwao.
China inazingatia sana
kulinda haki na maslahi ya
wazee, imebuni sheria na
kanuni za kisheria ikiwemo
sheria ya dhamana kwa
haki na maslahi ya wazee na
kujenga mfumo wa sheria
na sera kuhusu huduma
za jamii, utamaduni, elimu
dhamana kwa maslahi na
haki za wazee.
Idara husika ya huduma ya
kisheria imeanzisha mfuko
wa fedha wa kutoa msaada
wa kisheria kulinda haki na
maslahi ya wazee. Katika
miaka 5 iliyopita, idara ya
utoaji huduma ya kisheria
kwa wazee ilitoa wastani wa
misaada zaidi ya elfu 40 kwa

mabomu yanayoangushwa
na jeshi la nchi yao, dhidi
ya watu wasio na hatia
katika baadhi ya nchi hizo!
Wajiulize, wanathamini uhai
wa binadamu wenzao kwa
sababu ni binadamu, au kwa
sababu ni Wazungu wenzao
wanaotoka kwenye nchi
zao? Kama jibu ni binadamu
wenzao, kama mtu yeyote
mwenye akili atakavyojibu,
sasa kwanini tunafanya
upendeleo katika kutoa
huruma, mapenzi na simanzi
zetu? Lazima tuumizwe na
kukasirishwa na vitendo
vyote vya ukiukaji haki na
mauaji ya binadamu wasio
na hatia duniani kote.
Tu n a o n a u p e n d e l e o
waziwazi. Vifo vinavyotokea
ulimwengu wa Magharibi
vinaripotiwa kwa kina na
kugeuzwa ajenda ya dunia,
lakini vifo na madhila
yanayotokea katika
ulimwengu wa Waislamu
vinaripotiwa kidogo sana!
Mbaya zaidi madhila
hayo huletwa na Serikali
za Magharibi, hususan
Ufaransa.
Kwa kumalizia, hatua
zozote zitakazochukuliwa
na Ufaransa kupanga
m a s h a m b u l i z i d h i d i ya
Waislamu kwa kisingizio
cha kupambana na
ugaidi, ikitumia huruma
iliyopatikana kufuatia
uhalifu uliofanyika Paris,
lazima zipingwe kwa nguvu
zote.
mwaka kwa wazee.
Hadi kufikia mwishoni
mwa mwaka 2005, China
ilianzisha shule na vyuo
vya wazee zaidi ya elfu 26
pamoja na nyumba za

wazee karibu elfu 40. Ili
serikali na jamii ziweze
kushughulikia suala hilo,
hivi sasa haki na maslahi
ya wazee vyote vinalindwa
na sheria na wazee wa
China wanaishi maisha ya
furaha nay a uhakika. Hivi
sasa idadi ya wazee nchini
China inaongezeka kwa
zaidi ya 3% kila mwaka.
Ili kukabiliana na
changamoto ya ongezeko
kubwa la idadi ya wazee,
N a i b u M k u r u g e n z i wa

ofisi ya Kamati ya Shughuli
za Wazee ya Taifa Bw. Li
Bensong alisema, China
i t a c h u k u a h a t u a z e n ye
ufanisi zaidi ili kuwafanya
wazee waishi maisha mazuri.
Alisema fedha nyingi zaidi
zitatengwa kutoka kwenye

bajeti ili kuimarisha
dhamana ya jamii na
kuchangisha fedha za
dhamana ya jamii kwa
wazee kwa njia mbalimbali.
Makala hi imeandikwa
kwa msaada wa CRI.CN

11/26/2015 6:14:20 PM

16

MAKALA

K

Mume Bora wa Kiislamu

U WA m w e n z a
bora, ni muhimu
katika ndoa
yoyote. Ndoa
inatakiwa iwe uhusiano
kamilifu ambako watu
wawili wanaounganika
pamoja muda wote
watakuwa tayari kutoa,
n a s i y o k u t wa a - n a
kujitahidi muda wote
kujiboresha kwa ajili ya
upande wake mwingine.
Ndivyo inavyotakiwa
ili kuwa mume bora wa
Kiislamu, jambo ambalo
Uislamu unasisitiza, na
aliyeita watu kuingia
katika Uislamu,
Muhammad (swallahu
alei wasalaam) alielekeza
hivyo. Fuatilia haya ili
kuondoa kutokuelewa
kuhusu jinsi ya kuwa
mume nyota!
1. Anza na salaam nzuri:
unaporudi kutoka kazini,
au safarini, msalimie mkeo
kwa 'Asalaam aleykum,'
salamu ya kutakiana heri.
Kumbuka alichosema
Mtume Muhammad,
(SAW): "Nikuelelezeni
katika jambo, ambalo
mkilifanya, mtapendana?
Enezeni salaam miongoni
mwenu."
2 . M wa n g a l i e k wa
upendo. Mtume
M u h a m m a d ( S AW )
alisema: "Mume na
mke wakiangaliana
kwa upendo, Allah
huwaangalia wote
wawili kwa huruma."
Umwangalie machoni
unapozungumza na mkeo,
kama mwanamke ataona
thamani ya jambo hilo -na
kumwangalia kwa jicho la
upendo na siyo mradi tu
umemwangalia!
3. Muone na kutabasamu
kwake. Mtume (SAW)
aliona tabasamu kama
zawadi ya furaha - zawadi
ya hisia, si ya kubeba zawadi ambayo undani
wake unapokelewa na
moyo. Swahiba wa
Mtume, Jarir Abdallah,
alisema: "Tangu wakati
nimeukubali Uislamu,
Mtume hakuwahi hata
siku moja kutokuniona.
Wakati wowote aliponiona
alitabasamu kwangu," Na
usemi mwingine maarufu,
kuwa "Unapotabasamu
usoni kwa ndugu yako
(ikiwa na maana mtu
yeyote, si kanuni kwa
ndugu pekee) ni zaka."
Sasa, endapo umefanya
haya mawili katika
ndoa yako, uhusiano wa
msisitizo zaidi, fikiria jinsi
itakavyokuwa na heri
zaidi! Mwache mkeo aone
upendo wako kwake kwa
tabasamu yako ya wazi
unapomwona.
4 .
M w a m b i e
unampenda. Na
umwambie mara nyingi!
Na uwe na ubunifu mara
nyingine ongeza neno la
mahaba! Chukua mfano
kutoka kwa Mtume! Mke
wa Mtume, Hazrat Aisha,

ANNUUR NEW.indd 16

alikuwa anamwuliza:
"Nini upendo wako
kwangu?" Naye anajibn;
"Kama fundo la kamba,"
ikiwa na maana ina nguvu

na iko salama. Mara kadhaa
alikuwa anamwuliza: "Fundo
hilo likoje?" na angejibu
"katika hali ile ile!"
5. Mpe busu. Hiki ni
kitendo kidogo lakini chenye
athari kubwa! Mtume (SAW)
alikuwa akimbusu mkewe
kabla hajaenda kufanya sala,
Uelekeo chanya huleta ubora
katika mandhari hayo.
6. Fanya michezo naye:
mke wa Mtume, Hazrat Aisha
alisema alifuatana na Mtume
katika safari fulani. Wakati
huo alikuwa msichana tu na
hajawa mnene wala mzito.
Mtume akawambia watu
waendelee mbele. Halafu
Mtume akamwambia,
" S a s a , t u s h i n d a n e k wa
mbio!" Hazrat anasema
alikimbia akabakia mbele
yake. Mtume akabaki kimya
kwa muda. Baadaye Hazrat
A i s h a a k i wa a m e s a h a u
tukio hilo na kuongeza
uzito, akafuatana tena na
Mtume katika safari fulani.
Mtume kwa mara nyingine
t e n a a k a wa a m b i a wa t u
watangulie, wakapita mbele.
Halafu Mtume akamwambia
wafanye mashindano. Safari
hii Mtume akapita mbele
yake naye akabaki nyuma.
Hapo Mtume akacheka na
kusema, "Hii ni kutoa jibu la
kushindwa kwangu kabla."
7. Chukua muda wa kuwa
naye ukifanya anachokipenda
na wewe unachipenda! Hii
ndiyo njia nzuri zaidi ya
kulea ndoa na kuwa karibu

zaidi wote wawili. Mtume
(SAW), alikuwa akiendelea
kwa furaha na kungoja
akiwa na mkewe Hazrat
Aisha akiwa ameweka
shavu lake dhidi ya shavu
lake, akiangalia onyesho
la mikuki na majambia la
kikundi cha wa-Abyssinia
waliokuwa wakitembelea.
Ni pale tu alipochoshwa

na onyesho, alimwuliza
"umetosheka?" na alipokiri
hivyo, wakaondoka wote
pamoja.
8. Msaidie: Taarifa moja
inasema mke wa Mtume
alikuwa safarini pamoja
naye. Alichelewa hivyo
Mtume akampokea akiwa
analia. Mtume (SAW)
akafuta machozi yake kwa
mkono wake na kujaribu
awezavyo kumtuliza.
9. Mdsaidie shughuli
za nyumbani, au angalau
usafishe unapotumia.
Hazrat Aisha aliulizwa
kuhusu tabia za Mtume
nyumbani kwake. akajibu:
"Alikuwa akisaidia katika

kazi za familia na akisikia sauti
ya muadhini anaondoka."
Pia, Hazrat Aisha anaarifu
k wa m b a M t u m e ( S AW )
alikuwa akishona viatu
vyake mwenyewe, kushona
nguo zake na kufanya kazi
za nyumbani kama ambavyo
yeyote kati yenu anafanya
kazi za nyumbani kwake. Pia
aliarifu kuwa alikuwa mmoja
kati ya waume waliokuwa
wakifua nguo zao, kukamua
mbuzi zake na kufanya kazi."
Hasa akiwa mgonjwa au
amechoka, usingoje hadi
akuombe umsaidie.
10. Kula na kunywa
pamoja naye; nenda hatua
moja zaidi kimahaba na
kufanya kile Mtume (SAW)
angefanya! Wakati mkewe
akinywa kutoka chombo
fulani, alikuwa akitumia
chombo hicho pamoja naye,,
na kuweka mdomo wake
pale pale alipoweka mdomo
wake. Na wakati akila nyama
fulani, angetafuta mahali
hapo hapo kweka mdomo
wake na kula! Ukifanya
hivi, mkeo atajua unafanya
hivyo kumfurahisha na
atakuthamini kwa ishara hizo
ndogo ndogo za upendo!
11. Mwite kwa majina
matamu! Mtume (SAW)
alikuwa akimwita mkewe
"Aisha Humayra" akiwa
na maana ya 'ua' kwani

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

alikuwa mweupe na akiwa
na mashavu ya umbo la ua.
Buni majina matamu kwa
ajili ya mkeo, na utamkuta
ni msikivu zaidi na utaona
mawasiliano yenu yakistawi!
12. Zungumza naye. Ongea
naye kuhusu anavyojisikia
na kumbukumbu zako
nzuri. Tumia muda kuongea
pamoja. Ahirisha kueleza
habari mbaya hadi wakati
unaofaa. Tafuta njia iliyo
bora zaidi ya kupeleka habari
mbaya.
13. Uwe mchangamfu.
Uwe na furaha, mchangamfu,
rafiki na mpole unapokutana
na mkeo.
14. Uwe mkweli. Kwepa
kusema uwongo. Kama siyo
mkweli kwake, hatakuamini
hata siku moja. Wakati wote
sema ukweli.
15. Shauriana naye;
m p e n a f a s i a o n e k u wa
anachofikiri kina thamani
kwako. Badilisha maamuzi
yako kama ana wazo bora
zaidi. Mtume (SAW) wakati
mmoja aliondoka Madina na
maswahiba wake kwenda
kuhiji. Hata hivyo, alipofika
Makka, wasiokuwa Waislamu
waliwazuia wasiingie. Baada
ya h a p o M t u m e ( S AW )
alifanya mkataba nao ambao
haukuwa na maslahi kwa
Waislamu, ambayo bado
ilikuwa na maana kuwa
hawawezi kufanya hijja.
Maswahiba waliondoka
wamesikikika na kuchukizwa
na mkataba huo usio sawa.
na hawakuvunja hali
waliyokuwa nayo, ambayo
ni lazima uingie ili ufanye
hijja. Hali hiyo inavunjwa
kwa kunyoa au kupunguza
nywele, ikifuatwa na
mambo mengine. Mtume

(SAW), alipoona hali yao
imekuwa ya kuhuzunisha
akaomba ushauri kutoka
kwa mkewe. Alimshauri
kwenda kwao waziwazi
na kunyoa kichwa chake.
Alifuata ushauri wake.
n a m a s wa h i b a wa k e ,
wakiona akifanya hivyo,
wote wakaacha huzuni
yao na kumfuata mfano
wake. Ushauri wa mke
wa Mtume ulitwaliwa na
ukawa "umeokoa siku!"
Were na mkeo ni nusu
za nafsi zenu. Kupokea
ushauri wake ni kitu cha
msingi kitakacholea ndoa
yenu.
1 6 . M s h u k u r u k wa
mambo yote mazuri

anayofanya, hii itampa
kujiamini zaidi.
17. Mpelekee zawadi. Isiwe
zawadi ya gharama kubwa,
ila iwe kitu anachokipenda.
18. Sikiliza madai yake
halali. Mwache akuboreshe
kama mtu, Mhamasishe
awavute watu katika kufuata
njia njema na kuwaonya
watu wasizini. Mhamasishe
akutane na marafiki wake
wema na jamaa zake. Tokeni

pamoja katika burudani
halali. Mpe burudani
mwenyewe kwa njia zilizo
halali!
19. Uwe mtaratibu ukiwa
naye kitandani. Fuata
taratibu za Uislamu za ndoa
na kufanya mapenzi. Uwe na
maisha chanya ya mahusiano
kimapenzi pamoja naye na
kumsifu katika jambo hilo.
Ingiza njia halali za kuboresha
maisha yenu kimapenzi na
kuridhika kwake.
20. Fanya dua: Mwombe
Allah kukusaidia kufikia na
kuendeleza mahusianio safi
na mkeo.

Vidokezo: M s a i d i e
kumtumikia Allah.
Mwamshe katika sehemu
ya tatu ya usiku kusali
'Qiyam al-Layl,. Mfundishe
unachojua kuhusu Kurani,

Hadith, Tafsir na Dhikr. Uwe
mkarimu kwake. Uwe mpole
na mtaratibu kwa mwenza
wako. Mlee. Mwonyeshe
unajali na maneno mazuri
na shukrani. Elewa mahitaji
yake stahili na ya lazima na
jitahidi uwezavyo kuyafikia.
Mpeleke kutembelea
familia yake mara kwa mara
na hasa katika hafla tofauti.
Kamwe usimdharau. Kamwe
usiseme uwongo kwa mkeo.
Mwambie kuwa anapendeza.
Mwamini, mpende na
umwelewe. Mpeleke Hijja
na Umrah wakati wowote
unapoweza kufanya hivyo.

Wakati wote mshirikishe
(katika kufurahia
kichekesho fulani, mambo
maalum ya shughuli zako
za biashara, kazi, taaluma,
taarifa za dharura, mambo
ya familia, tabia zako).
Fanya mipango ya tafrija,
mikutano ya pamoja na
familia za marafiki zako
wa karibu ili kukuza
uhusiano wenu kifamilia,
panua upeo wake, na kwa
njia hiyo ataweza kukupa
msaada zaidi katika
masuala yako mengin e.
Mwangalie kama ambavyo
ungependa binti yako
aangaliwe na mumewe.
Tahadhari:
Katu

usimlaumu bila ushahidi
wa nguvu. Katu usivuruge
imani yake kwako hata
katika mzaha. Kwepa
ku mwaibisha kwa mfano

kwa kumtusi. Kwepa kurudi
katika muda usiotarajiwa
au wakati wa usiku, kwani
a n a we z a k u a n z a k u wa
na wasiwasi. Usiwaeleze
wanaume wengine jinsi
alivyo. Usiwalinganishe
wanawake wengine na yeye.
Kwepa kuzidisha Gheerah
(kung'ang'ania tabia njema).
Usimzuie kujibu simu. Mpe
nafasi asijisikie kubanwa
pumzi. Usimlaumu mkeo
kwa chakula kisichopikwa
vyema. Ukikipenda chakula,
kula na umshukuru.

Usipokipenda, usiseme
lolote. Usimvunjie
heshima. Kama umekwaza
hisia zake mahali fulani
sema "samahani," na
kujaribu kumpendeza.

11/26/2015 6:14:21 PM

17

Makala

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Viroja vya ‘Tanganyika’…
Na Rashid Al-Ghafri

C

HAMA cha
Mapinduzi
n d i c h o
kinachoendelea
kutawala nchini na sasa
kimefikia katika uongozi
wa awamu ya tano chini
rais Dr. John Pombe
Joseph Magufuli au
JPM. Uongozi wa awamu
zote huwa na kauli mbiu
zao na wa awamu hii
unajulikana kwa jina
la hapa kazi tu. Ni
matumaini ya Watanzania
wote kuona kauli mbiu
hiyo ya hapa kazi
inafikiwa na kutekelezwa,
isiwe ni wimbo kama ule
waliousikia na kuuimba
wa maisha bora kwa kila
Mtanzani.
Ndani ya siku hizi
chache zilizopita,
tumeshuhudia mfano wa
hapa kazi tu, lakini sijui
itakuwe kweli hapa kazi
tu au ni hapa mwanzo tu.
Kama ni msimu wa mvua,
tuseme hiyo imekuwa
rasha rasha kwa maeneo
hayo yalopitiwa na wengi
wetu. Tunasubiri mvua
kamili kwa maeneo
mengine.
B a a d a ya u t a n g u l i
huo,sasa niingie pale
nilipokusudia kwa leo ili
nami nichangie juu ya hili
la Mzee wa hapa kazi tu la
kuonyesha kuwa maneno
yake ya matumizi yasio ya
lazima yanaekwa kando
na ya muhimu yanapewa
kipaumbele. Kwa kuanzia
ameagiza na kutaka
sherehe za uhuru wa
Tanganyika kwa mwaka
huu zisiwepo na badala
yake pesa za sherehe
h i z o z i e l e k e z we k wa
jamii katika usafishaji na
uimarishaji wa mazingira,
kwa nia ya kupunguza au
kuondoa kabisa mripuko
wa ugonjwa wa kipindu
pindu ulioikumba nchi
kwa sasa. Kama hiyo
ndio dhamira, hata na
mimi naunga mkono
na wananchi nina
imani wataitikia wito
huo wakiamini kuwa
mazingira yetu ndio uhai
wetu.
Katika sherehe
kama hizi za uhuru wa
Tanganyika, ingependeza
zaidi kama zisingekuwepo
toka zamani na fedha
zake kuelekezwa katika
miradi ya maendeleo.
Ninasema hivi kwa sababu
mara kadhaa imekuwa
ikinadiwa na viongozi
h a o h a o wa s e r i k a l i

ANNUUR NEW.indd 17

Sherehe ya kuzaliwa mtoto
wakati mtoto kafa zamani

HAYATI Mwl. Julius K. Nyerere.
kwamba Tanganyika kama
Tanganyika haipo. Mimi
najiuliza, kama Tanganyika
haipo kwa nini sasa kila
mwaka tunafanya sherehe
na kupoteza fedha nyingi
sana kwa kitu ambacho
tayari hakipo.
Hili kwangu nimekuwa
nikizifananisha sherehe
hizi za uhuru wa
Ta n g a n y i k a a m b a y o
tunaambiwa imekufa sawa
na familia kuadhimisha
sherehe ya birthday ya
ndugu yao aliyefariki
miaka hamsini iliyopita.
Ni gharama za bure tu
kwani uzuri wa birthday ya
mtu ni mwenyewe awepo
kama ni kucheza na kupiga
makofi naye ashiriki huku
akishuhudia ndugu zake
waliohudhuria.
Uwamuzi huu wa
kuzipeleka fedha hizo
za sherehe za uhuru wa
Ta n g a n y i k a k wa v i l e
sio lazima kuwepo kwa
muono ya kupeleka fedha
kakita matumizi sahihi pia
lipo jambo jingine ambalo
nalo limekuwa likigharimu
fedha kibao huku faida
yake ikiwa ni chache au
haipo kabisa. Jambo hili
ni ule unaoitwa ‘Mwenge
wa Uhuru’ wa Tanganyika,
kama Tanganyika ilikufa

AN-NUUR

MAREHEMU Sheikh Abeid Aman Karume
mwaka 1964, Vipi Mwenge umasikini wakutupwa.
ulioasisiwa mwaka 1961
Ni vyumba vingapi
bado upo na unakimbizwa vya madarasa, zahanati
kwa gharama kibao za n g a p i , v i s i m a v i n g a p i
wavuja jasho wanyonge vinaweza kuchimbwa
wa Tanzania.
kwa fedha hizi ambazo
M w a l i m u N y e r e r e kila mwaka zimekuwa
a l i a s i s i M w e n g e n a zikipotea.
kusema ataupachika juu
Pia nako katika utunzaji
ya mlimaKilimanjaro, w a m a z i n g i r a k a m a
u m u l i k e h a t a n j e ya sababu hii iliyotolewa, ni
mipaka yetu ili nuru yake vyoo vingapi vinaweza
ilete amani na upendo kujengwa katika mashule
pale ilipokosekana. Azma a m b a y o m a t u n d u ya
hiyo licha ya kutembezwa vyoo ni machache au
kwake, bado haijatimia k w a s h u l e a m b a z o
k wa n a m n a m o j a a u wanajisaidia vichakani,
n y i n g i n e . Wa t a n z a n i sambamba na maeneo ya
hawako na amani kwani makazi nako ambako vyoo
amani hupatikana maisha vya umma vinahitajika
ya n a p o k u wa m a z u r i . i l i w a s i j i s a i d i e t e n a
Lakini Watanzania fedha vichochoroni, mazingira
za kuwaletea maendeleo yawesafi na magonjwa
zimekuwa zikitumika hayo ya mlipuko yasitokee
kukimbizia Mwenge nchi tena au udhibiti wake uwe
nzima yaani Tanganyika wakuridhisha.
na Zanzibar.
Naishauri serikali kwa
Serikali inaonaje katika hili na wengi wangefurahi
dhana hii ya uboreshaji kuona rasilimali zao zote
wa huduma za jamii, zinatumika vyema na sio
ikafuta mbio za Mwenge fedha tu kwani Mwenge
na mamilioni hayo mengi hugharimu hata wakati wa
ya k a e l e k e z wa k a t i k a wananchi vijijini kwenda
huduma za elimu, afya, katika kilimo kusubiria
kilimo na miundombini Mwenge na hii zamani
ya barabara kwa lengo ikishuhudiwa au mijini
la kukuza uchumi wa shughuli kusimama kwa
W a t a n z a n i a a m b a o muda.
hawana amali kwa
Wa p o wa t a k a o d a i

kwamba Mwenge ni
kichocheo cha maendeleo,
sasa inatupasa tujiulize
kama Mwenge huleta
maendeleo, nchi ambazo
hazina Mwenge hakuna
maendeleo, au tuangalie
hayo maendeleo ya
Mwenge yanayofanyika
ni miradi ya thamani
ngapi inayozungukiwa
na Mwenge wenyewe
unadharimu ngapi.
Tukirudi kwa lile la
usitishwaji wa sherehe
za uhuru wa Tanganyika
mwaka huu yaani
9/12/2015,isijekuwa ni
mwanzo na njia ya kufikia
m a l e n g o ya C C M ya
serikali mbili kuelekea
moja kama ilivodaiwa.
Kama hazitofanyika
tena sherehe hizo za
uhuru wa Tanganyika kwa
miaka inayofuata kwa
upande wa pili wa shilingi
ambao sio wa matumizi
ya s i y o ya l a z i m a , k wa
upande wa siasa itakuwa
ni kutoweka kabisa kwa
jina Tanganyika ambalo
bado wapo wazalendo wa
Tanganyika wanaoisubiri
Tanganyika irudi tena
kama ilivyokuwa kabla
ya 64.
Kwa muono huu
kutokuwepo kwa huo
uhuru wa Tanganyika
kunaweza pia kupelekea
wazalendo ambao
hufarijika japo mara moja
kwa mwaka kusikia neno
uhuru wa Tanganyika
neno hilo lisisikike tena
masikioni mwao.
Ikiwa hivo pia
itapelekea kutokuwepo
na kufutika kabisa sherehe
za muungano ya 26/4 na
badala yake siku hiyo
kujilikana kama siku ya
jamuhuri ya Tanzania.
Ikifikia
hapo
h a k u t a k u wa n a t e n a
sherehe za mapinduzi
wala serikali yake na hapo
ndoto za kila wazalendo
kupoteza ndoto zao yaani
Watanganyika kutorejea
t e n a Ta n g a n y i k a n a
Wa z a n z i b a r k u p o t e a
kabisa fikra na azma ya
kuwa na Zanzibar huru
yenye mamlaka kamili
kama wanavoililia ng'oa
kila uchao.
Na hapo ile safari
ya zamani ya CCM ya
serikali mbili kuelekea
moja itakuwa imetimia
kwa kupatikana Jamhuri
ya Tanzania na sio tena
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Asanteni na Allah
atupe mwisho mwema.

11/26/2015 6:14:24 PM

18

MAKALA

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Misikiti katika Mji Mkongwe wa Zanzibar - 4

Inatoka Uk. 13
ukisaliwa katika miaka ya
50 mwishowe na mwanzo
wa miaka 60 na mmoja wana
wa ukoo wa Kifalme Sayyid
Haroub ambaye alikuwa
peke yake katika ukoo wa
kifalme akifwata madhehebu
ya Sunni/Shafi. Msikiti
huu aidha ukisomeshwa
darsa zake na Syd Hamid
Mansab na akaja kupokewa
na mwanawe Syd Ahmed
Mansab ambao niliwaelezea
katika makala iliopita. Darsa
za Msikiti huu zilikuwa
zikisomeshwa baina ya
magharibi na isha.
Msikiti wa Ijumaa wa
Malindi huu ni Msikiti
mkubwa wa ghorofa moja
ukiwa upo karibu sana na
Bandari Kuu ya Unguja.
Unapoteremka bandarini
kwa boti itakuchukua chini
ya dakika tatu kuufikia
Msikiti huu.
Msikiti wa Ijumaa wa
Malindi umejengwa katika
mwaka wa 1831 na watu wa
ukoo wa Mafazi na mmoja
kati ya wanafamilia alitoa
kipande cha ardhi cha Miafuni
kiwe pesa zinazotokana na
hapo ziusimamie Msikiti
akijulikana kwa jina la
Mwinyi Sheikh bin Haji
Omar al-Mutafi. Msikiti
huu ulikuwa ukisaliwa na
wingi wa waumini katika Mji
Mkongwe. Sheikh Muhydin
al Shaikh bin Abdalla Qahtani
a m b a ye n i s h a m u e l e z e a
katika makala zangu kabla,
ni mmoja wa masheikhe

ambao aliotoa mchango
mkubwa wa dini visiwani
na kuwasomesha wengi kati
ya waliokuwa maulamaa
wakubwa na kutegemewa
Zanzibar wakiwa kina Sheikh
Ahmad bin Salmin, Sheikh
Shauri bin Haji Al-Shirazy wa
Donge, Sheikh Abdul Azi bin
Al-Amawy, Sheikh Suleymna
Hayatt akiwa Mhindi Khoja,
Sheikh Muhammad bin
Ahmad bin Mlomry, Sheikh
Hassan bin Yussuf Mngazija,
Sheikh Ahmad bin Salmin AsSabahy, Sheikh Fadhil bin Ali
Mngazija. Sheikh Muhydin
ndio aliokuja akaupanua
Msikiti wa Ijumaa wa Malindi
kwa msaada wa Mfalme
Sayyid bin Said na darsa
zake baadhi akizisomesha
hapo Msikiti wa Ijumaa wa
Malindi.
Msikiti wa Mwana Sitende
au kwa jina jengine Msikiti
Hamdani na Msikiti wa pili
ni Msikiti wa Bwana Sadiki
Misikiti hii miwili inaonekana
katika eneo la Mkunazini.
Wajenzi wa Msikiti huu asili
yao wanatokea katika mji wa
Kilwa, Tanzania bara wakati
huo ikiwa ni Tanganyika.
Misikiti hii ilijengwa katika
mwaka wa 1882 na mama
na mtoto wake, bibi Fatuma
Abubakar na mwanawe
Omar al-Hamdani. Bibi
Fatuma Abubakar alikuwa
na mali nyingi na alizielekeza
mali zake katika mambo ya
kheri yasiokuwa mambo
ya wanawake wa kimambo
leo waliojielekeza zaidi

kujiremba na kuvaa maguo
ya k i l a a i n a n a k u j i t i a
vikolimbo vya kila aina na
kupanda magari makubwa
makubwa na kukaa katika
makasri. Bibi Fatuma alikuwa
na uwezo wa kila aina,
lakini unaposoma tarekhe
huoni kuwa alijikita katika
anasa ila mambo yake yote
aliyaelekeza katika mambo
ya kheri yatayompelekea
kuipata Pepo.
Kisiwa cha Zanzibar ni
kisiwa kama visiwa yengine
vimekaliwa na watu wa
makabila mbalimbali kutoka
sehemu mbalimbali za
ulimwengu na hayo yanajiri
hadi leo. Katika mtaa wa
Mkunazini kuna Msikiti
unaojulikana kwa jina la
Msikiti Kinyozi ambao hauko
mbali na duka maarufu la
Abdulrahman Maperemende
na hivi sasa unakabiliana
na bekari ya Songa mbele,
Msikiti huu umejengwa
k a t i k a k a r n e ya 1 7 n a
Abdulrahman Ahmed Logan
Afghani mwenye asili ya
kutoka nchi ya Afghanistan
kazi yake ilikuwa ni kinyozi
n a m wa n a we a l i o k u wa
akijulikana kwa jina la
Muhammad Abdulrahman
Ahmed Logan Afghani.
Alikuja kuwa msomi wa
dini ya Kiislamu mkubwa
na alikuwa ni mcha
Mungu. Mtu na mwanawe
walijitolea nyumba zao 5 kodi
zinazotokana na nyumba
hizo ndizo ziendeshe Msikiti
huu.

Sura ya Msikiti wa Ijumaa wa Malindi hivi sasa
M s i k i t i m we n g i n e n i
Msikiti Rajab huu ulijengwa
na Rajab Abdulrazak Logan
kabla ya mwaka wa 1896.
Rajab Abdulrazak alikuwa
mfanya biashara aliweka
nyumba zake tatu kusimamia
Msikiti na kodi zitazopatikana
ndio ziendeshe Msikiti huo.
Misikiti mingi ilikuwa
ikiendeshwa na watu
a m b a o wa l i j i t o l e a m a l i
zao kusimamia Misikiti na
ilikuwa siku zote Misikiti
hiyo ikipata uangalzi na
inapofika mwezi wa Shaabani
kabla ya Ramadhani
hufanyiwa matengenezo
madogo madogo na kupakwa
rangi. Watu wengine ambao
hawakujenga Misikiti lakini
waliandika Wakfu mali zao
iwe inaiendesha hio Misikiti,
ikiwa majumba au mashamba

yao. Mali za watu zilipokuja
kutaifishwa ikiwa pamoja na
mashamba kugaiwa eka tatu
kwa wananchi ndio Misikiti
mingi ikakosa usimamizi
uliokuwa ukiiangalia na
kuitizama. Hivi sasa unakuta
ile taratibu ya kuiangalia
hio Misikiti imebaki katika
Misikiti michache kabisa
ukiwa mmoja wao ni Msikiti
Gofu.
Fwatana na mie katika
makala ya Misikiti katika
Mji Mkongwe wa Unguja.
(Rejea kubwa ya makala
haya ni kutokana na kitabu
cha Sheikh Abdalla Saleh
Farsy Baadhi ya Wanavyuoni
wa Kishafi wa Mashariki ya
Afrika na The History of
Conservation of Zanzibar
Stown Town kilichohaririwa
na Professor Abdul Sheriff).

Sheikh Ali bin Khamis bin Salim Al-Barwany -6

Inatoka Uk. 13
kwani vumbi lake huko

korokoroni ndio lilizidi na
kuwasha moto usiozimika.
Hapo tena ikawa kila
ikifika asubuhi Sayyid
Barghash akimtuma
Sheikh Muhammad bin
Sleiman al-Mandhry
kwenda kusema na
Sheikh Ali bin Khamis bin
Salim Al-Barwany arudi
kwenye madhehebu yake
ya asili, hayo aliyokuwa
a k i a m b i wa ya k i i n g i a
shikio la kulia na kutokea
shikio la kushoto na
kutomsikiliza mjumbe
n a u j u m b e a l i o p e wa .
Kutokana na kugonga
ukuta na kushikilia
msimamo wake Sayyid
Barghash akaona ni jambo
jema amwondoe machoni
m wa k e n a a m p e l e k e
Musqat, Oman ili aweze
kupoa na kuisemesha
nafsi yake. Kufika
huko ndio ikawa moto
u m e m wa g i wa p e t r o l .
Alizidisha vishindo akawa
hatoi utulivu kwa wenyeji
wake ikabidi arejeshwe

ANNUUR NEW.indd 18

Zanzibar. Aliporudishwa
Zanzibar alipelekwa jela
moja kwa moja kutokana
na msimamo wake
usiotetereka katika suala
la kujiunga na madehebu
ya Sunni.
Sayyid Barghash akijua
uwezo wa Sheikh Ali Bin
Khamis Al-Barwany na
athari atazoziwacha, kwa
hio hakusita kumtuma
Sheikh Sleiman kuendelea
kwenda kumnasihi Sheikh
Ali bin Khamis bin Salim
Al-Barwa n y k u wa ch a
misimamo yake na
kufahamisha kuwa kama
hatobadili msimamo wake
ajue atafia jela. Sheikh Ali
bin Khamis bin Salim AlBarwany akajibu jela ni
bora kwake na anastahabu
kubakia huko kwani yeye
sio wa mwanzo katika
tarekhe aliopambana
n a wa t a wa l a . S h e i k h
Suleiman akamnasihi
kuwa akubali mdomoni na
ndani ya nafsi yake abakie
alipo, akakubali hilo akiwa
lake khasa lipo moyoni,
mwishowe alikubali na
kula yamini kurudi katika

madhehebu ya asili ya
wazee wake kwa kufanya
hivyo akafunguliwa
jela, wengi waliokuwa
wanamfahamu walimuona
fika ni kuwa bado ni Sunni
kwa vishindo vyake.
Sayyid Barghash
a n a e l e z wa n a S h e i k h
Abdalla Saleh Farsy
kama ifwatavyo, “Sayyid
Barghash ni Harun Rashid
wa Ki-Busaidi wa Zanzibar
na ndio Maamun wao
pia. Ukubwa na fahari
na heshima na mengineo
aliotajikana nayo Harun
Rashid akiwa miongoni
wa wafalme wa Ki-Bani
Abass, ndio sifa aliosifika
nayo Sayyid Barghash.
Al-Maamun naye kati
ya wafalme wa BaniAbass alikuwa kipenda
elimu kwa kukusanya
chungu ya wanavyuoni
na ndivyo ilivyokuwa
kwa Sayyid Barghash
pia. Al-Maamuun
aliwataabisha vya
kutosha wale waliokuwa
hawafwati madhehebu
yake ndivyo hivyo
hivyo Sayyid Barghash

alivyowataabisha
waliokuwa hawafwati
madhehebu yake katika
wale aliokuwa karibu naye
kiukoo na karibu zake.
Imam Ahamd bin Hambal
alipata misukosuko
mikubwa yeye na wenziwe
kufungwa na Al-Maamun,
n a ye S a y y i d B a r g h a s
alimfunga Sheikh Ali bin
Khamis bin Salim AlBarwany na Sheikh Sheikh
Ali bin Abdalla Mazrui
pamoja na Sheikh Abdul
Aziz. Hapana aliokamilika
asiokuwa na dowa,
aliokamilika ni Allah.
Mola awarehemu wote,”
alimalizia Sheikh Abdalla
Saleh Farsy kumfasili
Sayyid Barghash.
Sheikh Ali bin Khamis
bin Salim Al-Barwany
baada ya kutolewa jela
hakuchukua muda
mrefu na kufariki akiwa
na umri wa miaka 36.
Aliyoyafanya yote na
kishindo alichokiweka
kupambana na mtawala
aliyafanya hayo akiwa na

umri mdogo. Sheikh Ali
bin Khamis bin Salim AlBarwany alifariki mfungo
p i l i m wa k a 1 3 3 0 A H
(August 1885).
M i s i m a m o ya k i n a
Sheikh Sheikh Ali bin
Khamis bin Salim AlBarwany ipo hadi leo
kwa baadhi ya masheikhe
walio na misimamo
na kutojipendekeza.
Mtindo
huu ndio
utakuwa ni mtiririko
hadi dunia itapomalizika.
Wa t a k u w e p o w e n y e
kujipendekeza kwa
watawala na watakuwepo
wenye misimamo thabiti
pasi na kutetereka.
Allah tujalie na
Masheikhe wetu tulionao
wazifwate nyayo za
watangulizi kama hawa
kina Sheikh Ali bin Khamis
bin Salim Al-Barwany
na Sheikh Sheikh Ali bin
Abdalla Mazrui pamojana
Sheikh Abdul Aziz na
wengineo, Ameen.
Fwatana na mie kumjua
Sheikh Hassan Bin Ameir
Al-Shirazy.

11/26/2015 6:14:25 PM

19
Inatoka Uk. 12

Mchambuzi anakuletea
picha ya mahali ambapo
limepigwa bomu la kweli
au mashambulizi ya
risasi za kweli, ukumbi
umefumuliwa paa
sikwambii madirisha
ya viyoo kwamba kuna
kilichosalimika.
“Parisians no longer feel
safe after what happened
here. The terrorists have
no rules. We have to take
the bull by the horns in the
battle against terror, and
France and the government
never do.”
Anasema Pascal
akihitimisha taarifa
yake katika Times of
Israel, akiwaaambia
Wafaransa wajue kuwa
hawapo salama tena
kutokana na ukatili
huu uliooneashwa na
magadi. Kwa hiyo ni
l a z i m a s e r i k a l i ya o
ichukue hatua kali
dhidi ya magaidi hao IS
(Waislamu)!
Na katika kukoleza
madai kuwa wahusika
ni Waislamu taarifa hiyo
ya Mayahudi ikasema
kuwa kuna kundi linajiita
‘Army of Islam’ ambalo
limekuwa likiwatishia
na kwamba lilipanga
kuipiga Bataclan toka
mwaka 2011 kwa
vile linamilikiwa na
Mayahudi.
Na unaweza kuona
harakati zinazofanywa
Ufarsana hivi sasa na
Ulaya yote kuwahujumu
Waislamu, huku harakati
za kuipiga Syria nazo
zikipamba moto.
Viroja vya Paris
Katika jumla ya vituko
vilivyoibuliwa katika
shambulio hili la Paris ni
kuwa vichwa vya habari
vya baadhi ya ‘habari
za sasa hivi’ (Breaking
News”, viliandikwa siku
mbili kabla ya tukio.
Tazama hii:
“Breaking: Death toll
From Paris Terror Attack
Rises to at least 120 with
270 others Injured.”
Wataalamu wa IT,
‘digitali’ wamechimbua
na kugundua kuwa
taarifa hii iliandikwa
Jumatano Novemba 11,
2015 saa 1 na dakika
44 jioni (19:44) wakati
shambulio lilifanyika
Ijumaa Novemba 13.
(Tazama: Tweeted two
days before it actually
happened.)
Chini ya taarifa hiyo,
utakuta pia habari ya
Giraldo Rivera wa Fox
News ambaye anamuhoji
Binti yake aliyekuwa
Paris na marafiki zake

ANNUUR NEW.indd 19

TANGAZO

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Jihadhari na ’Shetani’ huyu

KATIKA Picha hii imeelezwa kuwa watu wanasubiri kuokolewa baada ya kupigwa mabomu katika
uwanja wa mpira wa Paris, Ufaransa.
wawili katika mechi
ya kirafiki ya timu ya
Ufaransa na Ujerumani.
Baadae anahojiwa
Simona Rivera, dada
yake na huyo aliyeko
Paris kuangalia mechi.
Katika mahojiano hayo
anasema awali mdogo
wake alionyesha
wasiwasi wa kwenda
akihofia kuwa jambo
baya linaweza kutokea.
Mchambuzi anahoji
na kuwaambia watu
wa Ufaransa na Ulaya
wa j i u l i z e , ‘ i n a i n g i a
akilini kweli kwamba
wasichana kutoka
Marekani wanaweza
kuja Paris kwa lengo
la kuangalia mechi ya
kirafiki kati ya nchi hiyo
na Ujerumani?’ Au ni
wale wale “Crisis Actor”
ambao wapo kila mahali
iwe ‘Westgate, Nairobi,
Boston Bombing,
Kikambala, Batman
theater shooting?
Katika maelezo hayo
ya Binti wa Giraldo
wa Fox News anaeleza
ilivyokuwa mtafaruku
lilipolipuka bomu katika
uwanja wa mpira, habari
ambayo pia ilibebwa na
ABC News (ya Marekani
pia) kwa kichwa cha
habari: “Paris Attacks:

Terrifying Scenes From
French Stadium.”
Ufupi wa maneno
ikisema kuwa kulikuwa
n a h a l i ya k u t i s h a
na kiwewe baada ya
shambulio la bomu.
“Hamkani ipo wapi
hapa? Watu walio na
kiwewe cha hatari ya
magaidi wapo wapi?”
Anahoji mchambuzi
akionyesha hali
iliyokuwepo uwanjani
akitumia picha za
video zilizopigwa
wakati uliodaiwa
ni wa shambulio.
Wa n a o o n e k a n a n i
watizamaji mpira, wengi
wakihangaika kuchati
n a s i m u z a o , wa l a
hakuna anayeonyesha
dalili ya woga.
Mchambuzi huyo
anayepatikana katika
‘ l i n k ’ - P a r i s At t a c k
November 13, 2015:
False Flag Event, Hybrid
Authentic & Fraud,
akirudi katika ukumbi
wa astarehe wa Bataclan
anakuonyesha gari za
polisi zikifika eneo la
ukumbi huku muziki
ukirindima ndani.
Askari hao wanashuka,
inasikika milio katika
gari hilo mithili ya fataki,
askari wanakaa kama

wanakimbia kulikimbia
gari lao, kisha wanarudi.
Anakuonyesha watu
baada ya tukio, hakuna
mwenye damu, hakuna
damu katika sakafu na
hakuna hata mtu mmoja
anayeonyeshwa akiwa
na jeraha la kweli (open
wound).
Katika hali hiyo
mchambuzi anasema
‘ v i r o j a ’ v ya n a m n a
hii, Paris sio mwanzo.
Anaturejesha katika lile
shmabulio la Olympic
Pa r k , k u l e At l a n t a
mwaka 1996. Katika
shambulio lile CNN
katika hali ya kuvuta
hisia za watazamaji
wake katika moja ya
‘Breaking News’ zake
likanadi juu ya mabomu
mawili yaliyolipuka kwa
wakati mmoja kama
tulivyoambiwa katika
lile la Dar es Salaam na
Nairobi (simultaneous).
Katika kusherehesha
ikalezwa kuwa mabomu
yalikuwa mazito,
yameuwa, yamejeruhi,
watu wanakimbia ovyo
kusalimisha roho zao.
Ha ta hi v yo, wa tu
walipopitia picha kwa
makini, kilichosikika ni

sauti nzito, na ambayo
haikujeruhi mtu, bali
kulikuwa na harakati
kubwa za askari na
‘wasanii’ waliokuwa
wanajifanya wameumia
na bahati mbaya kwa
walioandaa ‘igizo’ hilo,
picha zikawa zinaonesha
wazi polisi wakiwapaka
damu/rangi nyekundu
‘waigizaji’ hao huku
wakiwafukuza watu
wakiwemo wapiga picha
(waandishi wa habari)
wa s i s o g e l e e m a h a l i
walipokuwa wakifanyia
igizo lao kando ya eneo
lilidaiwa kulipuliwa
kwa bomu. (Tazama: The
Atlanta Bombing in 1996
is 100% HOAX, PURE
and simple.”
Ndio haya ya Paris
ambapo Fox News
wanasema kuwa
u k u m b i wa s t a r e h e
ulishambuliwa
kwa ‘maguruneti’
yaliyosababisha
m a d i r i s h a
kusambaratuika, lakini
picha zinakuonyesha
kuwa hakuna hata kiyoo
kilichofanya ufa.
Ndio mmoja wa
wachambuzi wa habari
hizi za ugaidi Paris

11/26/2015 6:14:26 PM

AN-NUUR

20

MAKALA

20

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

WAT U w a l i j i k u t a
wakibubujikwa
na machozi. Ni
wale waliokuwa
wamemzunguka kijana.
Kijana aliyetoa ujumbe
mzito kwa watu wa Paris.
“Mimi ni Muislamu.
Ila nashangaa kuna watu
wananiita gaidi.”
“Mimi nakuamini
wewe. Je, wewe
unaniamini?”
“Kama unaniamini,
njoo unikumbatie.”
Alikuwa akisema na
kupaza sauti kijana huyo
wa Kiislamu akitembea
katika jiji la Paris jirani
na kunakodaiwa kutokea
shambulio la kigaidi
huku akiwa kaziba
macho na kilemba, haoni
anakokwenda.
Kama ilivyo kawaida
ya watu, na hasa mijini,
kufumba na kufumbua,
kundi kubwa la watu
lilikuwa limemzunguka.
Sasa badala ya

Soma gazeti la
AN-NUUR
KWA TSH 800/=
kila Ijumaa

AN-NUUR

SAFAR 1437, IJUMAA NOV. 27- DES. 3, 2015

Mimi ni Muislamu!
Kuwa na amani. Tusalimiane
Tupeane mikono kwa upendo

kutembea, ilibidi asimame
na kukariri maneno yale
yale mbele ya mamia ya
watizamaji.
Kwa namna alivyokuwa
a k i t a m k a k wa h i s i a :
“Mimi Muislamu, lakini
watu wananiambia
gaidi”, waliomzunguka
walikuwa wa kitokwa

na machozi na mmoja
mmoja wakijitokeza
kwenda kumkumbatia.
“Nakushukuruni
sana nyote. Tambueni
kuwa gaidi ni gaidi.
Hana nembo ya Uislamu

wala Ukristo. Nimefanya
haya kutuma ujumbe
kwenu nyote kwamba:
Gaidi ni muuwaji.
Uislamu, Ukristo, Dini,
zinakataza kuuwa.
(Muislamu hawezi kuwa
gaidi. Mkristo hawezi
kuwa gaidi)”
Alisema kijana huyo
akiondoa kilemba
alichokuwa amejifunika
macho.

Imarisheni taasisi za elimu
Na Bakari Mwakangwale

WAISLAMU wametakiwa
kutoa nguvu zao za hali
na mali, katika kujenga na
kuendeleza taasisi za elimu.
Wito huo umetolewa na
Ustadhi Zaharan Baraka,
akizungumza katika hafla
ya uchangiaji wa maendeleo
ya Shule ya Sekondari ya
Kiislamu ya Jioni (MESS)
iliyofanyika Jumamosi
ya wiki iliyopita, katika
viwanja vya Islamic Club,
Mwananyamala Jijini Dar
es Salaam.
Ust. Baraka alisema
uwepo wa vituo vya elimu
ni ukombozi kwa jamii ya
Kiislamu ambayo kwa muda
mrefu imekuwa ikipaza
sauti ya kubaguliwa katika
elimu.
Alisema, kutokana na
historia fupi ya kituo hicho
cha masomo ya Sekondari
yanayotolewa katika mfumo
wa elimu usio rasmi (Jioni
tu), inaonyesha kimekuwa
na msaada mkubwa kwa
Waislamu waliokosa fursa ya
kusoma elimu ya Sekondari
kupitia mfumo rasmi.
“Unapotambuwa
kwamba umekwama na njia
ya kujikwamua ipo, usipo

iendea njia hiyo unakuwa
umejiingiza katika mkwamo
zaidi.” Alisema Ust. Baraka.
“Vituo kama hivi (MESS)
vina umuhimu wake na
ni muhimu kuviendeleza
k wa m a n u f a a ya j a m i i
hususani kwa jamii ya
Waislamu, iliyokwamishwa
kielimu kutokana na
sababu mbalimbali
ambazo zimeandikwa na
kusimuliwa.” Alisema Ust.
Baraka.
Aidha, alisema wanafunzi
wanaotoka katika vituo
kama hivo huwa wanakuwa
viongozi wazuri katika jamii
kutokana na kupata elimu ya
kimazingira na kiroho kwani
huwezi kuwa na viongozi
wazuri wasiokuwa na elimu
katika maeneo hayo mawili.
Alisema, kiongozi yoyote
anayetambua haki ni yule
ambae ameelimika na
anamuogopa Allah (s.w) na
huyo ni lazima awe amepitia
katika vituo mfano wa
MESS, vyenye kuelimisha
imani ya kumjua Muumba
na elimu ya mazingira
yanayomzunguuka.
Kwa upande wake,
Ust. Jamada Shehe,
akizungumzia historia na
sababu ya kuanzishwa kwa
kituo hicho cha Sekondari

ya jioni (MESS), alisema ni
baada ya kuona uwepo wa
Waislamu wenye ufahamu
wa kusoma na kufika mbali
kielimu lakini wapo mitaani
au katika shughuli zao ndipo
ikaja fikra ya kuwainua
kitaaluma kwa muda mfupi
huku wakiendelea na
shughuli zao.
A l i s e m a , i l i k u we z a
kufikia lengo, kituo
kiliafikiana masomo hayo
yatolewe muda wa jioni
baada ya walengwa kumaliza
shughuli zao sambamba na
kuweza kuwapata walimu
wa kufundisha ambao wengi
wao ni wa kujitolea baada
ya kumaliza majukumu yao
katika shule walizo ajiriwa.
Ust. Shehe, alisema
utaratibu huu umeleta
tija kubwa kwa jamii ya
Waislamu waliokosa fursa
h i y o i l i h a l i u we z o wa
k u s o m a wa l i k u wa n a o
kwani akasema, mpaka sasa
kuna wanafunzi waliofika
na kuhitimu Vyuo Vikuu
na Vyuo vya kati na kozi
mbalimbali kutoka MESS.
“Ukiambiwa kuna
Waislamu wapo Vyuo Vikuu
wamepitia hapa na wana
uwezo mzuri tu unaweza

kujiuliza, Waislamu hawa
walishindwaje kuchaguliwa
kwenda Sekondari. Alisema
Ust. Shehe.
Mwenge Evening
Sekondary School (MESS)
ni Shule ya Sekondari ya jioni
iliyoasisiwa mwaka 2004,
katika kituo cha Kiislamu
cha Msikiti wa Mwenge
(MIC).
Lengo kuu la kuasisiwa
kwa kituo hicho ni
kuwasaidia au kuwainua
Waislamu wa rika na jinsia
zote ambao walikosa elimu
ya Sekondari katika mfumo
rasmi wa Serikali ambao ni
kusoma miaka minne.
Badala yake, MESS hutoa
elimu hiyo ya miaka minne
kwa muda wa miaka mitatu
tu, kwa muda wa nyakati
za jioni ili Waislamu ambao
hawakupata fursa ya elimu
kupitia mfumo ulio rasmi,
waweze kupata elimu hiyo
kwa mfumo usio rasmi na
kuweza kufikia malengo yao.
Tokea kuanzishwa kwake
miaka 11, iliyopita MESS
ambayo hutoa elimu hiyo
kwa ngazi ya O’ Level na A’
Level, imeweza kutawanya

wanafunzi wake katika vyuo
Vikuu vya Dar Es salaam
(UDSM), Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Chuo
Kikuu cha St. Augastino,
Mwanza (SAUT), Chuo
K i k u u C h a Wa i s l a m u
Morogoro (MUM), Chuo
Kikuu Huria (OUT).
Pia MESS, imefanikiwa
kupeleka wanafunzi katika
vyuo vya Ualimu, kama
vile Mpwapwa, Tukuyu,
Kirinjiko, Mpuguso pamoja
na Safina. Lakini pia wapo
wanafunzi katika vyuo vya
Bandari, St. Glory, Magogoni,
Sanfelis na vingine vingi.
Kwa mujibu wa uongozi
wa kituo hicho cha MESS,
ni kwamba Waislamu na
vijana hao waliotapakaa
katika vyuo mbalimbali
walikuwa wamekata tamaa
na elimu baada ya kukosa
fursa ya kuendelea na elimu
ya Sekondari katika mfumo
rasmi, lakini kituo hicho
kimeweza kufufua ndoto
zao, hata hivyo imeelezwa
kuwa miongoni mwa
wanafunzi wengine tayari
wapo katika ajira Serikalini
na katika sekta binafsi.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

ANNUUR NEW.indd 20

11/26/2015 6:14:27 PM