You are on page 1of 9

HOTUBA

YA
MGENI RASMI
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO
MHESHIMIWA DKT. ASHATU KIJAJI (Mb)
WAKATI WA UFUNGUZI
WA
MKUTANO WA 25
WA MWAKA WA WANACHAMA NA WADAU WA
MFUKO WA PENSHENI WA PPF
KWENYE
UKUMBI WA KIMATAIFA WA MWL. JULIUS NYERERE- DAR ES
SALAAM
FEBRUARI 11, 2016

1

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa
PPF, Ndugu Ramadhani Khijjah;
Ndugu Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni
wa PPF;
Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) ;
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya
Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi Irene Isaka;
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ndugu
William Erio;
Viongozi wote wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Vyama vya
Wafanyakazi mliopo hapa;
Ndugu Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF;
Watoa Mada na Wajadili Mada;
Washiriki wa Mkutano huu;
Wanahabari;
Wafanyakazi wa PPF;
Mabibi na Mabwana.
2

3

Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe
binafsi Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni
wa PPF, Wajumbe wa Bodi yako na Menejimenti ya Mfuko wa
Pensheni wa PPF kwa heshima mliyonipa ya kunialika kuja
kufungua mkutano wenu huu wa 25 wa mwaka wa Wanachama
na Wadau wa PPF.

Nichukue pia fursa hii kwa niaba ya Serikali ya awamu ya tano
kuwashukuru wanachama na wadau wote kwa kufika na kushiriki
kwenye mkutano huu wa 25 wa mwaka wa wanachama na wadau
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.

Aidha ningependa kuupongeza Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa
kuandaa mkutano huu wa kila mwaka kwa mara ya 25 mfulululizo.
Sote tunafahamu kuwa, mikutano ya namna hii ni muhimu kwa
ajili ya ushirikishwaji, ubadilishanaji mawazo na kupokea maoni
kwa

nia

ya

kuboresha

utendaji

wananchama na jamii kwa ujumla.

na

utoaji

huduma

kwa

Utaratibu huu unaimarisha

uwazi na uwajibikaji na kuongeza imani ya wananchi na
wanachama kwa Mifuko yao.
4

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi, wakati unanikaribisha pamoja na
mambo mengine umeelezea ushiriki wa PPF katika kutekeleza
mada kuu na kwa kifupi umeweza kuelezea mafanikio ambayo
Mfuko umeyapata tangu Mkutano uliopita. Umeeleza jinsi Mfuko
wenu ulivyoweza kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hii ili
kuendana na mabadiliko yanayotokea kwenye jamii pamoja na
mafanikio ya Mfuko wa Pensheni wa PPF tangu mkutano uliopita
ambayo ni kuongezeka kwa mapato yanayotokana na michango
na uwekezaji, kukua kwa thamani ya Mfuko wa PPF na kufikia zaidi
ya

shilingi

trillioni

Nawapongeza

sana

mbili
kwa

hadi

mwishoni

mafanikio

hayo

mwa

Juni

hususani

2015.
kwenye

uwekezaji wenye tija eneo ambalo lina matatizo kwenye Taasisi
nyingi.

Vilevile umeelezea jinsi Mfuko wenu ulivyojikita katika matumizi
ya TEHAMA kwenye utoaji wa huduma; kutanua wigo wa
kuwasomesha watoto wa wanachama wenu wanaofariki wakiwa
kwenye ajira; kuendelea kutoa mikopo ya SACCOS ambapo mpaka
sasa mmetoa jumla ya shilingi bilioni 91.34 kwa wanachama
wenu, kuanzishwa kwa mfumo mpya wa “Wote Scheme “ kwa
5

sekta isiyokuwa rasmi, na mafao mapya ya Uzazi. Huu ni ubunifu
wa hali ya juu unavyoonesha jinsi mnavyowajali wanachama
wenu.Kwa niaba ya Serikali napenda kuwapongeza sana kwa
mafanikio hayo.

Mambo hayo niliyoyataja pamoja na Taarifa yako kuwa Mfuko
wenu umeshapata tuzo tatu za kimataifa kutoka Shirikisho la
Hifadhi ya Jamii duniani (ISSA) na tuzo mbili za hesabu bora kwa
miaka miwili mfululizo kutoka Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa
ndani (NBAA), na kuwa sasa huduma zenu ni za kiwango cha
kimataifa kama inavyodhihirishwa na cheti utoaji huduma bora
cha kimataifa ( ISO 9001: 2008 Certified) yamenifurahisha sana.

Kwa niaba ya Wizara ya Fedha napenda kuwaarifu kuwa Serikali
ina imani na utendaji mzuri wa Mfuko wenu na naipongeza sana
Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa PPF kwa hilo
Ni wazi kuwa wadau mlioko hapa na wengine watakaopata Taarifa
hizi kupitia kwenye vyombo vya habari watachangamkia fursa ya
kujiunga na Mfuko wa PPF ili waweze kunufaika na huduma za
kisasa na mafao bora yanayotolewa na Mfuko wenu.

6

Ndugu Mwenyekiti wa Bodi, nimalizie kwa kuzungumzia
baadhi ya changamoto ulizozitaja kama ifuatavyo:
(i)

Kuhusu

waaajiri

wasioleta

michango

kwa

wakati

ninaagiza kwamba waajiri wa namna hiyo waache tabia
hiyo mara moja kwani ni uvunjaji wa sheria na unaleta
usumbufu usio wa lazima kwa wastaafu na Mifuko.
Serikali imeshatoa agizo la kuwataka waajiri wote
kuhahakisha wana mikataba na wafanyakazi wao na
wanawaandikisha katika Mifuko ya hifadhi ya jamii na
kuwachangia

kama

sheria

inavyotaka.

Ninaagiza

kwamba hatua za kisheria zichukuliwe kwa kuwashtaki
waajiri wote wanaochelewesha michango na kuziomba
mahakama kesi hizo ziamuliwe kwa haraka ili kuondoa
kero kwa wananchi na Mifuko.Waajiri wakichangia kwa
mujibu wa sheria watawawezesha wanachama kupata
mafao yao kikamilifu na kwa wakati; wakati huo huo
kuifanya mifuko kubuni mafao zaidi kwa wanachama
badala ya kutumia muda mrefu kufuatilia kesi za
michango mahakamani.

7

(ii)

Kuhusu madeni ya

Serikali kwa PPF,tayari suala hili

linashughulikiwa ambapo tayari Wizara imeshaiagiza
Benki Kuu kuandaa non-cash bond

ambayo itatolewa

kwa Mfuko ikiwa ni mkakati wa kulipa madeni hayo.Pia
Serikali

imeshaanza

na

itaendelea

kuhakikisha

michango ya pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi
zinazopata

ruzuku

kutoka

Serikalini

inalipwa

kwa

wakati.

(iii) Kuhusu suala la mafao ya kujitoa, Wizara yangu
itawasiliana na

Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana,

Ajira na Walemavu ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa
suala hili kwani ni dhahiri kuwa linakwenda kinyume
cha kanuni za hifadhi ya jamii duniani na halina tija kwa
wafanyakazi na Mifuko.

Naomba

kabla

sijamaliza

zifuatazo:

8

nami

niwape

changamoto

i)

Mfuko uendelee kuboresha huduma kwa wanachama
wake kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ili kuwavuta watu
wengi zaidi kujiunga na PPF

ii)

Kwa kuzingatia mada kuu ya mkutano, Mfuko uangalie
uwekezaji katika maeneo ambayo bado haujaingia kwa
kuzingatia kanuni za uwekezaji zilizotolewa na Benki
Kuu ya Tanzania kwa kushirikiana na SSRA baada ya
kujidhihirisha kuwa uwekezaji huo utakuwa na tija ili
kujiongezea mapato na hivyo kuwa na uwezo mzuri
zaidi wa kuboresha mafao kwa wanachama wake.

Baada ya kusema maneno hayo, naomba sasa kutamka kwamba
mkutano huu wa 25 wa mwaka wa wanachama na wadau wa PPF
umefunguliwa rasmi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

9