You are on page 1of 1

Msanii wa filamu Vincent Kigosi Ray baada ya kuchanwa

kwenye wimbo wa Nay wa Mitego Shika Adabu Yako kuwa


bado anaishi kwao, amejibu tuhuma hizo kwa kudai anaishi kwao
mpaka sasa ili kuwa karibu na Mama yake.
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM
Ijumaa hii, Ray alisema yeye ni mtoto wa mwisho hivyo anahitaji
kuwa karibu zaidi na Mama yake.
Ni kweli naishi nyumbani na kuishi kwetu sio kama sina
nyumba, na kuishi nyumbani sio dhambi. Uwezo wa kupanga
ninao lakini mama yangu hapendi nihame nyumbani kwetu ,
alisema Ray.
Kujitegemea ni maamuzi yako binafsi, mimi naishi nyumbani na
mama yangu ni mtoto wa mwisho lakini huwa sipendi
kujionyesha nina utajiri gani?, Sipendi kupost mali zangu, sinina
nyumba, magari ni ishu zangu binafsi, kila msanii ana style yake
ya maisha, mwingine anapenda kujionyesha kwenye mitandao
ana mali gani, aliongeza Ray.
Pia Ray alisema yeye na mpenzi wake Chuchu Hans kila mtu
anaishi kwake.
Mpenzi wangu anaishi kwake na mimi naishi nyumbani kwetu.
Mama yangu alishaniambia hata nikihama atakuja kuishi na
mimi nyumbani kwangu. Chuchu Hans anajua kuhusu hili hata
nyumba anayoishi nimempangia mimi, alisema Ray.