You are on page 1of 4

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA UMMA


1.0

UTARATIBU WA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA


WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
UTANGULIZI
Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wadau wakiwemo
wanafunzi wa elimu ya juu kuhusu kuchelewa au kutokushughulikiwa kwa
malalamiko yao yanayohusu mikopo ipasavyo katika ngazi za vyuo na
katika ofisi za Bodi. Kufuatia malalamiko hayo, Bodi imeboresha utaratibu
wa kushughulikia maswali au malalamiko katika ngazi zote ili kuongeza
ufanisi.
Hata hivyo, kabla ya kueleza kuhusu utaratibu huu ulioboreshwa,
tungependa kueleza sifa na vigezo vinavyotoa ustahili kwa Wanafunzi
kupata mkopo.

2.0

SIFA ZA MWOMBAJI
Utoaji mikopo unaongozwa na Sheria Na. 9 ya 2004 ya Bodi ya Mikopo
kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (kama ilivyorekebishwa) Na. 9 ya 2004
hususani vifungu vyake vya 16 na 17. Pamoja na mambo mengine, sheria
hii inaitaka Bodi kutoa msaada wa kifedha kwa njia ya mkopo kwa
mwanafunzi mwenye sifa ambaye ameomba kupewa mkopo huo
umwezeshe kugharamia mahitaji yake yote au baadhi katika masomo
yake ya elimu ya juu. Hivyo basi, kila mwaka Serikali kupitia Bodi,
huandaa vigezo na sifa zitakazotumika katika kutoa mikopo kwa mwaka
husika kwa kuzingatia matakwa ya sheria. Kimsingi vigezo ambavyo
vimebainishwa na sheria ni:
a)
Awe mtanzania;
b)
Awe ameomba mkopo kupitia mtandao wa Bodi (Online Loan
and Management System (OLAMS));
c)
Awe amechaguliwa kujiunga na masomo katika chuo chenye
ithibati kinachotambuliwa na kusajiliwa na TCU au NACTE kama
mwanafunzi full time;
d)
Awe ni mwanafunzi anayeendelea na masomo ambaye
amefaulu mitihani inayomwezesha kuendelea na mwaka
unaofuata wa masomo;
e)
Asiwe ni mnufaika wa mkopo au ruzuku kutoka taasisi nyingine
au watu wengine;
f)
Aliyemaliza kidato cha sita, mafunzo ya ufundi au ualimu .....
g)
Kwa kuzingatia idadi ya waombaji na uwezo wa Bodi ya kibajeti,
mikopo hutolewa kwanza kwa:
Sheria iliyoiunda Bodi imeipa mamlaka ya kutengeneza vigezo vya
nyongeza vinavyoboresha zoezi la utoaji wa mikopo ambapo kila
mwaka Bodi huandaa na kutangaza Mwongozo wa Ukopeshaji wa
1

mwaka unaofuatia ambao hutangazwa kabla ya msimu wa wanafunzi


kuomba mikopo kuanza. Mwongozo uliotangazwa kuongeza
uchambuaji maombi ya mikopo kwa ajili ya mwaka wa masomo
2015/16, ulitoa sifa zinazowapa waombaji ustahili kama ifuatavyo:

3.0

Wanafunzi wanaosoma programu za kipaumbele kwa taifa


ambao hupata asilimia 100. Programu hizo ni Sayansi za
Tiba, Ualimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati, Uhandisi
wa Umwagiliaji na Uhandisi wa Gesi na mafuta;
Yatima;
Wenye ulemavu
Wanafunzi wanaosoma programu nyingine hupangiwa
mikopo kwa kuzingatia uchambuzi unafanywa kwa
kutumia kingamuzi uwezo (Means Testing).

UTANGAZAJI WA WAOMBAJI WALIOFANIKIWA KUPANGIWA


MIKOPO NA UANDAAJI WA MALIPO
3.1

UTANGAZAJI WA MAJINA YA WAOMBAJI WALIOPANGIWA


MIKOPO
Baada ya uchambuzi wa taarifa zote za waombaji kwa kuzingatia
mwongozo uliotolewa kufanyika taarifa za, waombaji waliofanikiwa.
Kupangiwa mikopo (loan allocation) hutumwa vyuoni, hupokelewa
na Menejimenti za vyuo na kufikishwa kwenye madawati ya mikopo
(Loan Officers) ya vyuo husika huitangaza orodha hiyo kwa
Wanafunzi halali wa vyuo husika kwa njia mbalimbali kama
kubandika kwenye ubao wa matangazo (notice board) na kupeleka
ofisi za Serikali za Wanafunzi.. Aidha, orodha hiyo huwekwa kwenye
mtandao wa Bodi (OLAMS) ili wanafunzi waweze kuiona.
3.2 UANDAAJI WA MALIPO
Malipo hufanywa kwa waombaji waliofanikiwa kupata Mikopo malipo yaoo
hupelekwa kwenye chuo ili chuo kiwalipe baada ya kuwatambua vizuri
kuwa ni Wanafunzi halali wa chuo hicho kwa kuangalia vitambulisho vyao.
ambapo Bodi ya Mikopo hufanya malipo kwa njia ya cheque kwa
kukilipa chuo husika ambacho huwajibika kuwalipa wanafunzi ndani ya
siku saba (07) tangu kipokee fedha kutoka Bodi ya Mikopo.
3.3 MAJUKUMU YA LOAN OFFICER
Mnamo mwaka 2011 serikali iliunda Tume ambayo ilitazama namna ya
kuboresha mfumo mzima wa Utoaji wa Mikopo. Pamoja na mambo
mengine, tume ilipendekeza kuanzishwa kwa madawati ya Mikopo kwenye
kila chuo. Watumishi katika madawati hayo walitakiwa kuitwa Maafisa
Mikopo.
Majukumu yao yanatakiwa kuwa ni:
a.
b.

Kutunza kumbukumbu ya wanafunzi wote wanaopata mikopo


kutoka Bodi ya Mikopo;
Kuhakiki uwepo wa wanafunzi waliopangiwa mikopo katika chuo
chake kabla wanafunzi hao hawajapokea malipo;
2

c.

d.

e.
f.
g.

4.0

Kuanzisha na kutunza kumbukumbu ya wanafunzi wanufaika wa


mikopo na wanaoacha masomo kwa sababu mbalimbali (Kifo,
uhamisho, kuahirisha n.k). Aidha, Loan Officer huyu, anapaswa
kuandaa taarifa hizi na kuziwasilisha Bodi ya Mikopo kila mwisho
wa robo mwaka wa masomo;
Kuratibu uandaaji wa matokeo ya mitihani ya wanafunzi na
kuyawasilisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 30 kabla ya kuanza
kwa mwaka mpya wa masomo na kwa matokeo ya marudio
9Supplimetary Examinations), angalau siku 30 baada ya chuo
kufunguliwa;
Kuratibu uandaaji na uwasilishaji wa Ankara na Madai (Invoices
and Claims) kwa wanafunzi wenye mikopo kwa ajili ya malipo;
Kuhakikisha wanufaika halali wanathibitisha upokeaji mikopo kwa
kutia saini kwenye karatasi za malipo na kuhakikisha kwa wale
ambao hawajasaini, fedha zao zinarudishwa Bodi ya Mikopo; na
Kupokea na kuyafanyia kazi maswali na malalamiko kutoka kwa
wanafunzi yanayohusu utoaji wa mikopo na kuyatolea ufafanuzi.
Ikiwa yanahitaji ufafanuzi wa ziada, kuwasilisha kwa Bodi ya
Mikopo kwa hatua zaidi

UTARATIBU
ULIOBORESHWA
MALAMAMIKO YA WANAFUNZI

WA

KUSHUGHULIKIA

Kama tulivyosema hapo awali, ili kuboresha ufanisi wa utoaji mikopo,


mwezi Agosti mwaka 2011, Serikali kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi ilivielekeza vyuo vyote za elimu ya juu kuanzisha
madawati yatakayoratibu na kusimamia masuala ya mikopo na ruzuku
kwa wanafunzi wa vyuo husika. Agizo hili limetekelezwa vizuri kiasi
na hivi sasa kila chuo cha elimu ya juu kina Afisa anayesimamia
masuala
ya
mikopo
na
ruzuku
kwa
wanafunzi
wao
wanaokopesheka.
Hivyo, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwakumbusha wadau wake wote, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu, kuhusu utaratibu wa kuwasilisha malalamiko au maswali
yanayohusu mikopo na ruzuku kwa wanafunzi wa elimu ya juu kama
ifuatavyo hapa chini.
i.

KWANZA, mwanafunzi yeyote anayefadhiliwa na Serikali kupitia


Bodi ya Mikopo mwenye swali au malalamiko anatakiwa kuwasilisha
suala lake kwa Afisa mhusika anayesimamia Dawati la
Mikopo/Ruzuku (Loan Officer) aliyepo chuoni kwake. Hao Loan
Officers hivi sasa wana uzoefu wa masuala ya mikopo na ruzuku
zitolewazo na Bodi;

ii.

PILI, baada ya swali au malalamiko kupokelewa, Loan Officer huyo


anapaswa kuyapokea na kuyatafutia suluhisho malalamiko hayo na
kumjibu mwanafunzi ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo
hiyo, tangu apokee swali au malalamiko hayo;

iii.

TATU, ikiwa siku mbili (02) zitapita bila mwanafunzi kupata jibu,
mwanafunzi awasilishe malalamiko yake kwa mamlaka ya juu ya
3

huyo Loan Officer ambaye naye anapaswa kutoa majibu au


kuchukua hatua ndani ya siku mbili (02), kama siyo siku hiyo hiyo;

3.0

iv.

NNE, ikiwa kiongozi wa chuo husika cha elimu ya juu atakuwa hana
jibu la swali au malalamiko yaliyowasilishwa kwake, anapaswa
kuwasilisha suala hilo Ofisi ya Bodi ya Mikopo ya Kanda iliyo karibu
na chuo chake. Ofisi ya Kanda itawajibika kutoa jibu siku hiyo hiyo ya
kupokea maswali au malalamiko hayo au kuwasilisha suala hilo
Makao Makuu ya Bodi ya Mikopo kama hana maelezo yake;

v.

TANO, kwa vyuo vya elimu ya juu ambavyo havipo karibu na ofisi za
Kanda za Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo husika unapaswa
kuwasiliana na makao Makuu ya Bodi ya Mikopo moja kwa moja kwa
njia ya barua pepe ifuatayo: malalamiko@heslb.go.tz ;

vi.

SITA, baada ya kupokea malalamiko hayo, Bodi ya Mikopo Makao


Makuu itatoa majibu kwa malalamiko/maswali yaliyowasilishwa siku
hiyo hiyo au ndani ya siku mbili (02) tangu kupokelewa kwa
malalamiko au maswali hayo; na

vii.

SABA, mara tu baada ya kupokea majibu ya swali au malalamiko


yaliyowasilishwa kutoka Bodi ya Mikopo, uongozi wa chuo cha elimu
ya juu utayafikisha majibu hayo kwa mwanafunzi husika siku hiyo
hiyo kupitia kwa Loan Officer wa chuo husika.

HITIMISHO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inasisitiza kuwa ni muhimu
kwa wanafunzi na wadau wote kuzingatia utaratibu huu ili kuongeza
ufanisi katika kushughulikia malalamiko ya wanafunzi.
IMETOLEWA NA:
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
FEBRUARI, 2016