You are on page 1of 4

KARAGOSI

Dkt. Muhammed Seif Khatib

KARAGOSI

ni

kinyago

kinachoninginizwa

kuchezeshwa kwa kuvutwa uzi.


mnyama au binadamu.

uzi

na

Karagosi huchukua sura ya

Kawaida yule mwenye kumwendesha

huyo karagosi huwa haonekani.


mwenye uzi

kwenye

Akitaka kucheka au kununa

aliyenyuma ya pazia ndiye anayeamua.

Akitaka

karagosi ainame au atembee siyo karagosi mwenye kuamua bali


aliyeshika uzi ndiye anayeamua.

Hata maneno anayosema

karagosi huwa siyo maneno yake bali ni maneno ya kutumwa.


Akiamua

kuimba ingawa karagosi ndiye atafunua

kinywa na

kujidai kuimba kwa mbwembwe na pozi lakini maneno si yake ni


ya mwenye kushika uzi wa kuchezesha karagosi. Katika uwanja
wa siasa karagosi hatafautiani na kibaraka. Huyu ni mwanasiasa
anayetumiwa na mwingine kwa manufaa ya anayefanya shughuli
hiyo bila kujali madhara anayopata wenzake katika jamii. Wapo
viongozi vibaraka katika

vyama vya siasa.

Hawa huwa

wanatumwa na mabeberu kwa masilahi yao bila kujali madhara


wanayopata wananchi au taifa. Hawa hujivika sura ya uanasiasa
usoni ili waonekane wazalendo, watetezi na wapenda nchi na
wananchi.

Hupewa fedha,

ughaibuni.

Huitwa Ulaya, Arabuni au Marekani kufadhiliwa.

Karagosi

maelekezo na

misaada huko

wakirudi nchini hutumiwa kuharibu shughuli nchini

mwake kwa kutumia kuviza maendeleo, kuitisha migomo, hujuma


hata kuendesha ugaidi. Mara zote karagosi ndiye anawaambia
hao wenye kushika uzi wa kumchezesha azuiye
1

misaada na

mikopo isiletwe nchini mwake. Ukaragosi wake unamfanya asijali


madhara yanayowafika watu wa nchi yake.

Afrika imekuwa na

vibaraka aina ya karagosi tokea wakati wa harakati za kudai


uhuru hadi sasa. Kule Angola, alikuwepo Savimbi na chama chake
cha UNITA.

Huyo alifadhiliwa na kusaidiwa na mabeberu ili

wazalendo na chama
hatia

MPLA kisishike serekali.

Watu waso na

kwa maelfu waliuwawa wakiwemo watoto na wanawake.

Karagosi Savimbi alikuwa akipewa msaada wa fedha, silaha na


mbinu za mikakati na mabeberu.
Angola ilichelewa kupata uhuru wake kwa usaliti wa Savimbi.
Hata hivyo, wengi wape, Angola ikapata uhuru wake. Nini
matokeo ya kibaraka huyu?

Mabeberu

wakamchoka na kufanya mbinu ili

kama

kawaida yao

auwawe. Wamemsahau.

Kibaraka karagosi mwingine wa Afrika ni Mabutu wa Congo. Ni


yeye alitumwa kumua Lumumba, mwanampinduzi na mzalendo
kwa manufaa ya mabeberu.

Mabutu akawa dikteta, ameua,

ametesa na amenyonya uchumi wa Congo.

Mabeberu kama

kawaida yao, baada ya kumtumia Mabutu kwa masilahi yao,


mwisho wakamuacha afe

kwa saratani

bila msaada wowote.

Viongozi hawa vikaragosi katika Afrika wametumika sana

kwa

maelekezo ya mataifa ya magharibi.


Ni hawa ambao ni

makasuku ambao wanasema ambayo

wakubwa wanayoyataka.

Ni hawa ambao ni mawakala wao


2

hutenda

wanachotaka.

Ni

hawa

ndiyo

makuwadi

wao,

wanaowasemea.
Zanzibar imefanya uchaguzi mwaka wa jana uchaguzi uligubikwa
na ghiliba za kuiba kura, vitisho na hujuma kadha.

Nilidhani

wakubwa huko nje ambao ndiyo miamba ya demokrasia, wao


wangekuwa wa kwanza kuunga mkono marejeo hayo kinyume
chake wamekuwa vikwazo. Sasa Wametafuta Savimbi na Mabutu
wao huko Zanizbar ili wafanye kazi ya ukaragosi. Wamemfunga
uzi na kuanza kumchezesha. Wakamua wao acheke, huvuta uzi
wa uso, ili ukunjuke, naye acheke. Wakiamua atembea, huvuta
uzi wa miguu, ili atembee. Wakipenda azungumze, atazungumza
lakini anayoyasema yanapitia tu kinywani mwaka lakini maagizo
ya wenye karagosi. Huitwa Dubai, London, New York ili kupewa
maelekezo na maagizo nini la kufanya. Huko huwekwa kitako na
kupewa mikakati namna ya kuikwamisha nchi katika maendeleo
yake.

Wakati huo hao,

mabeberu kwa kutumia vyombo

walivyoviunda wao wenyewe


kutoshiriki

hutoa sauti ya kutishia ya

uchaguzi wa marejeo wakiwa waangalizi wao.

Baadaye, watasusa kutoa misaada na mikopo kwa nchi. Tabia ya


undumakuwili kwa wakubwa hao imezoeleka sana.
uchaguzi kurejewa hawataki.
sauti.

Zanzibar

Karagosi wao hutumika kupaza

Zipo nchi kadhaa ambazo hata hakuna vyama siasi na

hakuna chaguzi lakini wameufyata.


mafuta na rasmali zao.

Kisa?

Wanabembeleza

Saudia, Omani au EAU wana vyama

siasa? Kuna uchaguzi wa Rais?

Tunamsubiri akirudi atwambiye


3

aliyoambiwa huko alipokwenda kufundwa. Utakuwa ukaragosi na


ubarakala tu!