You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK
OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli


amemteua Mhe. Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya
Rufani.
Kabla ya uteuzi huo Mhe. Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi.
Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Mhe. Anne Semamba
Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF).
Uteuzi wa Mhe. Anne Semamba Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza tarehe 25 Mei,
2016.
Mhe. Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Balozi Ali Mchumo.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria
Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es
salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).
Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo
cha Sokoine (SUA) Morogoro.
Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick
Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

30 Mei, 2016