You are on page 1of 2

CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA

SHAABAN ROBERT STREET
S. L.P 3918, D ar-es-salaam. 12/05/2011 Kwa msajili wa chuo, Chuo cha usimamizi wa fedha, S.L.P 3819, Dar-es-salaam. YAH:KUKATAA MADAI YALIYOTAJWA JUU YANGU Mheshimiwa,kichwa cha habari hapo juu cha husika,kwanza nasikitishwa sana na shutuma zilizotamkwa juu yangu kwani pamoja na kunisononesha zimenizoofisha kisaikolojia na kuharibu maandalizi yangu ya majaribio ya kwanza ya muhula wa pili wa mwaka.Nakataa na kukanusha madai hayo kama yalivyo kwa maelezo yafuatayo; Dai la kwanza: Nasikitishwa sana kutuhumiwa ya kuwa nimeshawishi wanafunzi wenzangu kufanya fujo na kukataa kuingia darasani kwa sababu ya pombe mnamo tarehe 28/02/2011 na tarehe 01/03/2011. Kwanza kabisa mimi si mtumiaji wa kilevi cha aina yoyote ile(pombe) na sijawahi kunywa pombe na sitegemei kunywa hata siku moja katika maisha yangu.Hivyo nimesikitishwa sana na shutuma hizo,nahitaji ushahidi wa kudhibitisha ya kuwa siku hiyo ya tarehe tajwa hapo juu nilikuwa nimekunywa pombe.Nadhani kwa shutuma hizo ni kunidhalilisha na kunichafua. Dai la pili: Nasikitishwa sana na shutuma ya kuwa nimezuia utendaji kazi wa wafanyakazi wa chuo kwa ushawishi wa pombe na kusababisha mitihani ya mwisho wa muhula wa kwanza kuahirishwa. Kama nilivyotangulia kueleza kwenye dai la kwanza ya kuwa mimi si mtumiaji wa kilevi cha aina yoyote ile nasikitishwa kwa madai hayo na vilevile nitahitaji ushahidi wa kudhibitisha ya kuwa mnamo tarehe 28/02/2011 nilikuwa nimekunywa pombe na kufanya madai tajwa juu yangu kwa ushawishi wa pombe,wakati mimi binafsi

…………………………….wanafunzi wote kufanya mitihani pasipo ulazima wa kufikisha asilimia sabini ya ada pamoja na kupewa vitambulisho vya kufanyia mitihani na yalitekelezwa.nilitegemea kama ni maelezo bunge la wanafunzi pamoja na serikali ya wanafunzi ndio wangetoa maelezo na si mwanafunzi mmojammoja kwani kwa kufanya hivyo ni uonevu na si haki Wako mtiifu.sihusiki na tatizo la wanafunzi kutoingia darasani na kufanya mitihani kama ilivyokuwa taratibu za chuo Dai la tatu: Kuhusu kukataa kuingia darasani mnamo tarehe 28/02/2011 na kukiuka sheria za chuo. Maamuzi ya wanafunzi kutoingia darasani na kufanya mitihani yalipitishwa na bunge la wanafunzi ifm(isrc) pamoja na serikali ya wanafunzi wa ifm(ifmso)wakishinikiza chuo kutoa ufumbuzi wa madai ya wanafinzi kama nilivyoyataja awali yakiwa ni kuahirishwa kwa mitihani.wanafunzi wote kuruhusiwa kufanya mitihani hata kama walikuwa hawajafikisha asilimia sabini ya ada na wanafunzi wote kupewa vitambulisho vya mitihani. Dai la nne: Kuhusu dai la nne nashangaa kutuhumiwa ya kuwa nimeandamana na kukusanya wanafunzi na kuwafanya wagome kuingia darasani. Nashindwa kuelewa ni kigezo gani kilichotumika mpaka mimi binafsi kupewa barua ya kutoa maelezo. Ninachofahamu wanafunzi wote wa chuo kwa tarehe tajwa hapo juu hawakuingia darasani je?wao wamepewa shutuma gani?Vilevile nisingeweza kuingia darasani kwa ajili ya usalama wangu kwani kwa siku tajwa hapo juu wanafunzi walikusanyika kwenye viwanja vya chuo wakiwa na madai yao na mliyatekeleza yakiwa ni kuahirishwa kwa mitihani. Ninachafahamu mnamo tarehe 28/02/2011 kulikuwa hakuna maandamano yoyote bali mkusanyiko wa wanafunzi kwenye viwanja vya ndani ya chuo. GEORGE FABIAN .