Sauti ya Waislamu

Amesema kweli Khatib Masjid TIC, Magomeni Mayahudi, Wakristo waielewa zaidi Qur’an 5:51 Wanaifanyia kazi. Makkah, Madinah kulipuliwa (?)

Waislamu wapo kama hawapo Uk. 9

Kashfa kwa Palisi, Usalama wa Taifa
Mwenzako akinyolewa…Serikali iepushe balaa Kenya imejitia kimbelembele, wanakiona cha moto Wabunge watuhumu “False Flag Terror Attacks”

ISSN 0856 - 3861 Na. 1012 JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Asilaumiwe Pengo wala Wilbrod Waislamu Slaa Kikwete anawajua vizuri
Kama ambavyo anawajua Wakristo

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema.

Maajabu! Mtoto azaliwa akiwa kashikilia Qur’an
Lagos,

MTOTO aliyezaliwa kashikilia Msahafu mdogo, Nigeria.

Kweli akina Jecha mnapanda viscudo
Lakini Viscudo vimekutieni upofu wa akili
aliekuwa Rais wa Tanzania akimueleza Jonathan Power akisema: “Viongozi wa Zanzibar wako tayari kuuwa lakini sio kuachia madaraka.” Sasa ikiwa viongozi akili zao zipo kwenye kupewa madaraka, hicho ndio wanachokitaka kama alivyosema Mheshimiwa Mkapa na wengine, maendeleo kwao ni kumiliki “Viscudo”, hiyo si hatari? (Soma Uk. 10)

Uk. 2

Apewa jina Abdulwahab Olarewaju Babatunde Familia nzima yasilimu. Qur’an yawekwa maktaba
Umati mkubwa wa watu walikusanyika mtaa wa Sonde, Ijeshatedo huko Lagos, ambapo ndipo nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo

MTOTO amezaliwa huko Nigeria akiwa kashikilia Qur’an ndogo mkononi.

KWELI Zanzibar ni nchi ya Kiafrika hilo halina ubishi. Lakini sio Wakfu wa kila Muafrika akiteremka Visiwani basi ndio mwenyewe. Mbona Msumbiji au Afrika ya Kusini hamuendi mkaleta upuuzi huo. Thubutu! Hayo fanyeni Zanzibar mchanga mara tu habari za kwa vile wenyewe shida yao kuzaliwa mtoto huyo kuenea kubwa ni madaraka na viscudo kwa kasi. “Wakati mtoto wangu tu. Tulimsikia Mheshimiwa Inaendelea Uk. 4 Benjamin William Mkapa

2

AN-NUUR

Tahariri/Tangazo
kusimamisha Uislamu? Hoja hapa ni je, Waislamu wanafanya nini katika kuufikisha Uislamu, kuusimamisha, kuupigania na kuuhami. Makala moja katika gazeti hili inaeleza jinsi makamanda katika jeshi la Marekani wanavyoichambua Al Maida: 51 na kuweka mikakati ya kuifanyia kazi. Katika moja ya mada zake aliyoipa jina “So What Can We Do? A CounterJihad Op Design Model, Luteni Kanali Matthew A. Dooley (Julai 2011) ananukuu kifungu cha 6 cha Katiba ya Marekani ambacho kinasema: “This Constitution and the Laws of the United States which shall be made in Pursuance thereof… shall be Supreme Law of the Land.” Akishanukuu akarejea katika mafundisho ya Uislamu ambayo yanawataka Waislamu waikamate Qur’an na Sunnah kwamba ndio “Supreme Law” kwao. Katiba na sharia zinazotungwa na binadamu zinakuja baadae. Katika somo lake anawataka wanafunzi wake wasiruhusu kwa namna yoyote Qur’an na Sunnah kuwa ndiyo juu ya Katiba ya Marekani. Lakini kwa upande mwingine anawaambia kuwa muda wa kuwa Muislamu anaifuata Qur’an na Sunnah, hatakuwa “Mmarekani halisi”. Atakuwa Muislamu kwanza. Ataikamata kwanza Qur’an. Hapa pia litakalowasaidia Waislamu sio kumlaumu Dooley na kumshambulia kama adui wa Uislamu. Yeye anatekeleza wajibu wake wa kuihami Marekani ‘Taifa la Kikristo’. Hoja kwa Muislamu, iwe wa Marekani au Tanzania, ni yeye anafanya nini kuhakikisha kuwa Uislamu unakuwa juu ya Katiba ya Marekani na Katiba ya Tanzania? Wapo pia Waislamu ambao imekuwa ni kama kiburudisho na ‘hobby’kwao kusimama katika majukwaa kuwashutumu baadhi ya viongozi wa Kikristo kama maadui wanaoupiga vita Uislamu. Labda swali ni je, tulimtarajia Muadhama Askofu Mkuu wa Jimbo

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012 Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kadinali Pengo afanye Jihad kuusimamisha Uislamu? Katika uwanja wa kisiasa, kumekuwa na shutuma pia kuwa baadhi ya vyama vya kisiasa na baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitumia vyama vyao vya siasa kupitishia agenda zao za kuimarisha Ukristo na kuupiga vita Uislamu. Ipo ile nadharia ya Charles Darwin ya “Sirvival of the fittest”. Kama Waislamu w ame k u w a w a n y o n g e wa kufikiri, kupanga na kutekeleza mipango yao ya maendeleo na kuusimamisha Uislamu, wakaruhusu wengine kuwakalia vichwani; itakuwa ni wao wenyewe wa kujilaumu. Mbona maswahaba hawakuwa hivyo? Kama alivyosema Khatib katika Masjid TIC, Magomeni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita; hivi sasa Waislamu wamekuwa dhaifu kiasi kwamba hata mmoja wao akikanyagwa ile kusema unanikanyaga anaona tabu. Na kwa kulijua hilo k w a m b a Wa i s l a m u wameukubali udhalili, wamekubali kuonewa na wameridhia na kuzoea kuishi na udhalili, ndio maana hata Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameona hata akiwapa ma-DC 40 katika jumla ya 133 hakuna tabu. Atasafiri kwenda Addis Ababa akirejea apande tena ndege kwenda Washington na kufanya shughuli zake za Urais bila kusikia kero yoyote kutoka kwa Waislamu. Na anajua kwa uhakika kabisa, kwamba jambo hilo hawezi kuwafanyia Wa k r i s t o . A k i f a n y a kinyume chake, Waislamu wakawa 133 na Wakristo 40 au japo akafanya nusu kwa nusu; Ikulu haitakalika. Litatimia lile neno “nchi haitatawalika.” Sasa kama mwanasiasa afanyeje? “Anawabamiza ambao wamekubali na kuzoea kuonewa.”

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110148, 0755 260 087, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

MAONI YETU

Asilaumiwe Pengo wala Wilbrod Slaa
TONNY Cartalucci ameandika makala akieleza jinsi aliowaita “ S u n n i E x t re m i s t s ” wanavyotumiwa na Marekani na Israel, kuiangamiza Syria. Akinukuu makala iliyoandikwa na mwandishi Seymour Hersh anasema kuwa toka mwaka 2007 kumekuwa na mpango wa pamoja kati ya Israel na Marekani kuandaa jeshi la “Sunni terrorists” ambao watatumiwa kila inapohitajika kusambaratisha moja ya nchi za Mashariki ya Kati. Ili kuificha Washington na Tel Aviv, akasema kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu zimekuwa ikitumiwa kama ndiyo mtekelezaji wa mpango huo. Anasema sio jambo la siri tena kuwa wanaoleta ghasia na kufanya mashambulizi ya kigaidi Syria hivi sasa ni katika wale wanaojiita wapiganaji wa Kiislamu wanaomshutumu Rais Bashar Assad kwamba si Muislamu safi na ni dikiteta. Wakidhani wanapigania demokrasia, makundi ya watu hao ndio wanaofanya mauwaji kila uchao likiwemo lile shambulio la kigaidi katika mji wa Damascus hivi karibuni ambalo lilisababisha kuuliwa makumi ya watu na mamia kujeruhiwa. Ametajwa mwana mfalme mmoja ambaye alikuwa Balozi Washington kwa miaka 22 hadi mwaka 2005 kwamba amekuwa mtu muhimu katika kuunda na kuvituma kazi vikundi hivi ambavyo hujulikana kwa majina tofauti. Kwa kiwango kikubwa vikundi hivi ndio vilivyotumika kumwangusha Muammar Gadhafi. Wakipata usaidizi, fedha na vifaa kutoka Marekani na NATO. Gadhafi ameondoka sasa ni wakati wa kushughulikiwa wao kama walivyoshughulikiwa Taliban waliosaidiwa na Marekani kupambana na Mrusi. Anachosema Tonny Cartalucci ni kuwa “Sunni Extremists” hao iwe kwa jina la ‘Slafi’, Al Qaidah au Muslim Brothehood, ndio hao hao hivi leo wanatumiwa kumpiga vita Bashar El Assad. Wanachoamini “Sunni Extremists” hao ni kuwa wanapigana Jihad kumwondoa Assad muuwaji, fisad, dikiteta ili waweke utawala wa Kiislamu. Hata hivyo wanasahau kuwa kama asivyotakiwa Assad, ndivyo hivyo, Marekani, Ulaya na Israel wasivyowataka Salafi na Ikhwanu Mulimeen. Tena wao ndio wabaya zaidi na wasiotakiwa kwa sababu wanataka kusimamisha U i s l a m u . Wa n a p e w a msaada na kutumiwa tu kwa sasa kisha wakishamaliza kazi ya kumtoa Assad wanageukiwa. Labda swali la kutafakari hapa ni je, nani wa kulaumiwa? Waislamu wachukue mwelekeo gani? Kama Mayahudi na Makafiri wana mpango wa kuangamiza Waislamu, kuangamiza nchi za Waislamu kama Iran, Syria na Libya; na wakafanikiwa kuwatumia baadhi ya Waislamu na nchi za Waislamu kufanikisha mpango wao; kubaki kuwalaumu Mayahudi, Marekani na makafiri wala haisaidii kitu. Wao walichofanya ni kutekeleza wajibu wao katika kupambana na Waislamu. Je, tulitarajia Yahudi asaidie

TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION (TAMPRO) TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO MAALUM YA KOMPUTA, USHONAJI NA KUDARIZI - TAMPRO SKILLS DEVELOPMENT CENTRE (TAMPRO-SDC) AWAMU YA KWANZA MEI 2012 TAMPRO inatangaza nafasi za mafunzo maalum katika fani za komputa, Ushonaji na Kudarizi katika chuo chake kipya kinachoitwa TAMPRO SKILLS DEVELOPMENT CENTRE (TAMPRO-SDC) kilichopo jirani na Msikiti wa Tungi, Temeke, Dar es Salaam. SIFA ZA MUOMBAJI: Kozi za komputa waombaji wawe wamemaliza kidato cha nne au zaidi. Kozi za ushonaji na kudarizi waombaji wawe wamemaliza darasa la saba au kidato cha nne au zaidi. MUDA WA MAFUNZO: Mafunzo yatakuwa ya miezi sita kwa ushonaji na kudarizi na miezi mitano kwa mafunzo ya komputa. Pia kutakuwa na muda wa mafunzo kwa vitendo. Masomo yataanza Juni 4, 2012. SIKU ZA MASOMO: Jumatatu hadi Ijumaa saa 2:30 hadi 5:00 asubuhi, saa 6:00 hadi 8:30 mchana na saa 9:00 hadi 12:00 jioni. GHARAMA ZA MAFUNZO: Tshs.60, 000/= kwa kipindi cha mafunzo. Barua za maombi na nakala za vyeti na namba za simu za muombaji au mzazi/mlezi vitumwe kwa anuani: MKURUGENZI MTENDAJI Jumuia ya Wataalam wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) S.L.P. 72045, Dar es Salaam Au ofisi ya TAMPRO Magomeni Usalama, Dar es Salaam Au kwa barua pepe: info@tampro.org, kopi kwa, tampro 1997@yahoo.co.uk, suke75@yahoo.com. Mwisho wa maombi ni tarehe 23/05/2012 NAFASI NI CHACHE WAHI SASA. Kwa maelezo zaidi piga simu: 0714 000 016 au 0716 574 266 au 0716 776 226 au 0714 878 407 Wote mnakaribishwa Imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji-TAMPRO

3

Kashfa kwa Palisi, Usalama wa Taifa
Na Mwandishi Wetu WA B U N G E w a K e n y a wametoa tuhuma nzito kwa polisi na Idara ya Usalama ya nchi hiyo ambayo lau ukweli utafichuka, itakuwa kashfa kubwa. Wabunge hao wanatuhumu kuwa kinachofanyika Kenya na kudaiwa kuwa ni mashambulizi ya kigaidi, huenda ikawa ni mchezo wa polisi na Idara ya Usalama wa Taifa. Kwa mujibu wa taarifa zilizorushwa hewani na kunukuliwa na kituo cha Chanel Ten katika taarifa zake za habari jana, baadhi ya wabunge wa nchi hiyo walionekana kuchachamaa wakizungumza kwa hasira na jazba wakidai kuwa mashambulizi ya kigaidi yanayodaiwa kufanywa na Al Shabab hufanywa na vyombo vya usalama. Wasiwasi huo unakuja huku baadhi ya wananchi wakidai kuwa kinachofanyika ni kufanya mashambulizi na kusingizia Al Shabab ili kupata kisingizio cha jeshi la Kenya kuendelea kuwepo Somalia katika ile kampeni iliyopewa jina la Operesheni Linda Nchi. Wabunge hao wanadai kuwa toka Kenya iingie Somalia kijeshi katika ile Operesheni Linda Nchi, ndio vinavyoitwa vitendo vya kigaidi vinaongezeka na kwamba ile kwamba vyombo vya usalama vinashindwa kukamata watu na kuwaonyesha hadharani kwamba hawa ndio Al Shabab wanaofanya mashambulizi ya kigaidi, inajenga wasiwasi mkubwa kwamba mashambulizi hayo ni jambo la kupanga. Aw a l i k a b l a K e n y a haijaingia Kenya, kulifanyika vitendo kadhaa vya kigaidi vikiwemo vya kutekwa nyara watalii, lakini wachunguzi wa mambo wakaonyesha wasiwasi kuwa yaweza matukio hayo yametumiwa kama kisingizio na wakatahadharisha kuwa hatua ya Kenya itazua balaa kubwa. Baadhi ya watu walitafsiri kuwa balaa litatokana na Al Shabab kulipiza kisasi kwa kupiga Kenya. Hata hivyo, watambuzi wa mambo wakasema kuwa tatizo halipo kwa Al Shabab kulipiza kisasi ila kwa Kenya kutafuta kisingizo cha kubaki Somalia. Kwamba ni lazima pawe na sababu za kuwashawishi Wakenya kwamba imekuwa lazima kwa vijana wao kufa Somalia na uchumi wa nchi kuangamia kwa kupigana vita. Ushawishi huo hauna njia nyingine ya uhakika zaidi ya kuhakikisha kuwa usalama wa Wakenya upo hatarini kila uchao Wakenya ni kupigwa maguruneti na kuuliwa na kutiwa vilema huku ikidaiwa kuwa wanaohusika ni Al Shabaab. Huo ndio mchezo Marekani, London, Australia na kwingineko walipoingia katika vita hii ya Bush dhidi ya ugaidi. Ndio mchezo uliofanyika katika ile “Anthrax Terror Attacks” kule Marekani wakafa watu kwa kimeta ikadaiwa kuwa ni kazi ya Saddam Hussein na Al Qaida. Kwa hiyo Kenya nao wanaonja joto ya jiwe kwa kujiingiza katika vita hii wakidai kuwa jirani zao Wasomali ni magaidi. Wanavuna walichochuma kwa mikono yao baada ya kushinikizwa na kutoswa Somalia kupambana na Wasomali wanaopigania kujitawala wenyewe badala ya mambo yao kuamuliwa Washington na Nairobi. Mchezo kama huu ulikuwa ukifanyika pia Zanzibar wakati wa kilele cha siasa za uhasama, chuki na visasi. Aliwahi kusimulia mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwamba siku moja polisi walifika saa nne katika mgahawa mmoja ambao huuza pia ulevi wakawaambia wateja waliokuwepo waondoke. Walipoondoka tu ikasikika milipuko na ikadaiwa kuwa ni shambulizo la bomu ambalo hata hivyo halikuwa limeleta madhara makubwa. Mashambulizi kama haya ndiyo huitwa “False Flag Operation” ambayo hutumika kama propaganda ya kupumbaza watu waridhie jambo fulani, washughulishwe na hali ya hatari huku wanasiasa wakifanya mambo yao au kufanywa makusudi ili ipatikane sababu ya kuwahujumu watu waliofanywa shabaha ya hujuma. Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saidi Mwema amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa pamoja na kuwa Tanzania ni salama, lakini bado inakabiliwa na kitisho cha ugaidi kutoka kwa Al Qaida na Al Shabab. IGP Mwema aliyasema hayo akiongea na waandishi wa habari juu ya ujio wa Kamishna wa Polisi Afrika ya Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Southern African Regional Police Chief Council Organisation (SARPCCO), Bwana Nhlanhla Mkhwanazi. Likipamba habari hiyo ya Mwema gazeti moja la kila siku la Kiingereza likakariri zile habari zilizodaiwa za “Al Shabaab Tanzania” waliodaiwa kutaka kushambulia kanisa la Efatha Life Ministry.

AN-NUUR

Habari

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

MKURUGENZI wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba Aidha, shambulio hilo “Last week police said kupanga kupiga propaganda ili they would launch immediate kuwapa kisingizio wanasaisa lilitanguliwa na onyo la investigations into threats by kufanya mambo yao katika kitisho cha ugaidi lililotolewa a suspected terrorist group hii wanayopita vita dhidi ya na Ubalozi wa Marekani jijini to blow up a Dar es Salaam ugaidi. Mahali pengine Cook Nairobi. church.” Katika taarifa yake ya onyo alisema kuwa “Al-Qaida, Gazeti hilo lilidai Ubalozi huo ulisema kuwa kumnukuu Mkurugenzi wa literally “the database”, was Upelelezi Makosa ya Jinai originally the computer file of ilikuwa na taarifa kwamba nchini, Robert Manumba the thousands of Mujahideen kungekuwa na shambulio la akisema kuwa wanafuatilia na who were recruited and trained kigaidi. Hata hiyo haikutajwa muda kuchunguza habari za magaidi with help from the CIA to hao wanaodaiwa kuwa na defeat the Russians.” na mahali pa shambulio ila Alichosema Robin Cook, ikaelezwa tu kuwa mipango ngome yao Tanga. Aliyewahi kuwa Waziri wa ambaye alijiuzulu Uwaziri, ya shambulizi ipo katika hatua Mambo ya Nje wa Uingereza, kupinga hatua ya Marekani za mwisho. Robin Cook, aliwahi kusema na Uingereza kuvamia Iraq “The embassy said Monday kuwa kinachoitwa Al Qaida mwaka 2003; kinathibitisha that the timing of the attack tu yaliyokwisha kusemwa na magaidi wanaodaiwa kutishia usalama wa Marekani na wanataaluma, wanajeshi is not known but they believe na Uingereza, ni mambo na makachero wengine hapo it to be at a final planning ya kupanga kwa faida ya awali toka ilipotangazwa vita stage.” Lilifahamisha Shirika la wanasiasa na baadhi ya nchi. dhidi ya Al Qaida. Gazeti la Los Angeles Times Habari la Associated Press “The truth is, there is no Islamic army or terrorist liliwahi kuandika makala – AP (Sun, Apr 29, 2012) group called Al Qaeda. And likichambua taarifa moja ya likinukuu habari za ubalozi any informed intelligence BBC (BBC documentary), huo. officer knows this. But there iliyopewa jina “The Power Wachambuzi wa mambo is a propaganda campaign to of Nightmares”, ambapo wanasema kuwa maadhali make the public believe in the inaonyeshwa jinsi suala la presence of an identified entity Al Qaida lilivyotumiwa kwa Kenya wamekubali kukokotwa representing the devil only in propaganda na jinsi ambavyo na kuingizwa katika vita hii, order to drive the TV watcher Marekani ilikuwa ikitoa wajiandae kulipa gharama to accept a unified international vitisho vya mashambulizi kubwa. leadership for a war against ya kigaidi na “false terror Kila uchao watasikia terrorism. The country behind attacks” na kusingizia Al m a s h a m b u l i z i i w e n i Qaida. this propaganda is the US.” maguruneti au bomu na Katika tukio la hivi karibuni wataambiwa ni Al Shabaab Alichosema Cook ni kuwa hakuna kitu kinachoitwa Al nchini Kenya, mtu mmoja w e n y e u h u s i a n o n a A l Qaida, Jeshi la Kiislamu (au aliuliwa na wengine kadhaa Qaida. Al Shabaab) ambao hutishia kujeruhiwa kutokana na Kingine watakachokuwa usalama wa Marekani na shambulio la guruneti. wakisikia mara kwa mara Shambuli hilo lililofanyika ni kauli za tahadhari kutoka dunia, bali ni jambo la kubuniwa kupiga propaganda katika kanisa moja jijini ubalozi wa Marekani kwamba na kwamba kachero yeyote Nairobi (Gods House of kuna tishio la shambulizi na makini (informed intelligence Miracle Church), Jumapili watapigwa kweli wauliwe. officer-wakiwemo IGP wetu iliyopita ni katika mfululizo Wa k i u l i w a k i s i n g i z i o Mwema, Kamishna Manumba wa mashambuli ambayo na Maofisa wa Idara ya yameacha watu wasio na hatia kinapatikana vijana wao Usalama) wanalijua jambo wakiuliwa na wengine kutiwa w a n a e n d e l e a k u u w a n a vilema toka Kenya ilipovamia kuuliwa Somalia. Kwa faida hili. Kwamba ni mambo ya Somalia. ya nani?

4

AN-NUUR

Habari/Tangazo

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012
ni ujumbe kutoka Toyibat International School, Gbagada, Lagos. Shule hiyo ya Kiislamu imetoa udhamini wa kumsomesha mtoto huyo kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu. Katika ujumbe wao kwa mtoto huyo, Abdulramon Sulaimon Adangba na Abdulahi Akinbode kutoka Nasru-lifathi Society of Nigeria kadhalika na Alifathiuquareeb Islamic Society of Nigeria, waliwataka wazazi wa mtoto huyo kutoruhusu mtu yeyote kumwita mtoto huyo Mtume au mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa sababu mtoto ni ishara tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Walimtahadharisha na watu watakotaka kumpa utukufu mtoto huyo na kuingia katika shirki. Baba mzazi wa mtoto huyo, Moshood Ogunsi, ambaye naye amesilimu, alikana kuitelekeza familia baada ya kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyanzo vya habari. Badala yake, Ogunsi alijawa na furaha na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kile alichokidhihirisha kwake na kwa familia yake. Baada ya hafla hiyo ya kusilimu na kumpa mtoto jina, eneo hilo liligeuka kuwa soko la kuuzia picha za mtoto huyo, ‘T’ shirts, mabango na kalenda zilizokuwa na picha ya mtoto huyo. Qur’an ambayo mtoto huyo alizaliwa nayo, ilifunguliwa katika makazi ya Imam Mkuu wa Lagos ili kushuhudiwa na wajumbe wengine wa Jumuia ya Maimam katika jimbo la Lagos.

Inatoka Uk. 1
alipozaliwa akiwa ameshikilia Qur’an katika mkono wake, muuguzi alisema: Qur’an hii inatakiwa kutupwa mbali. Lakini binafsi nilimsisitiza kuwa ni lazima kuiona kwanza Qur’an hiyo mama yangu kabla ya hatua yoyote ile inayoweza kuchukuliwa”; alielezea Kikolemo, mama wa mtoto ambaye ni Mkristo. Mkurugenzi wa hospitali ya Bodet Medical Hospital, Ikeja, Lagos, Dk. Bode Tawak, akijibu na kutoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo la ajabu alisema: “Kisayansi (kimatibabu), haikuwa jambo rahisi kwa mtoto kuzaliwa akiwa ameshikilia Qur’an mkononi.” “Ni tukio kubwa lilioje mkono wa mtoto kushikilia Qur ’an? Ni ukubwa na utukufu ulioje wa Qur’an hiyo? Ni jinsi gani Qur’an hiyo imeingia katika tumbo la mama yake? Sijui ni jinsi gani Qur’an inaweza kuingia ndani ya tumbo. Lakini kuna mambo mengi huwezi kueleza”, alisema Dk. Tawak. Kwa upande mwingine, vivumo vya “Allahu Akbar! Allahu Akbar!” vilitawala katika ukumbi uliofanyika sherehe ya kumpa jina mtoto huyo aliyezaliwa akiwa kashikilia Mas’haf ndogo kwa mkono wake wa kulia, katika mji wa Mushin, katika jimbo la Lagos nchini Nigeria mapema wiki hii. Kabla ya kujifungua, mumewe alidaiwa kumshawishi kuitoa mimba hiyo, lakini Bi. Kikelomo alikataa kufanya hivyo. “Baada ya kukataa kutoa mimba, mume wangu alinitelekeza akidai kuwa hilo ni tatizo langu, muuguzi aliyenizalisha, Bi. Victoria Moses, alishangazwa na tukio hilo, akataka Qur’an aliyokuwa kashika mtoto huyo itupwe lakini nilikataa. “Nikasema mama yangu l azima aio n e k w an za”, alisema Kikelomo. Habari zinaeleza kuwa Mchungaji wa kanisa analoabudia mwanamke huyo, Victoria Yetunde Dada, alisema wakati wa uja uzito, Kikelomo alikuwa akifika kanisani mara kwa mara kuomba na akamshauri asiitoe mimba hiyo baada ya aliyempa mimba kuikataa na kumtekeleza. Mkurugenzi wa madaktari katika Hospitali ya Ikeja, jijini Lagos, Dr. Bode Tawak, amesema kisayansi tukio hilo haliwezekani kabisa. “Unajiuliza maswali mengi. Kurani iliingiaje kwenye mfuko wa uzazi?

Maajabu! Mtoto azaliwa akiwa kashikilia Qur’an

Kuna mambo ambayo huwezi kuelezea lakini Nigeria mambo mengi ya ajabu hutokea na huwezi kuyafafanua kisayansi,” alisema Dk. Bode. Baadae ulikuwa kama uvamizi nyumbani kwa Kikelomo, baada ya watu kufurika asubuhi hadi usiku kuja kushuhudia muujiza wa Kikemo na mwanaye. Ilibidi polisi wa kutoka kituo cha Ijesha kuja kudhibiti hali. Ilibidi familia ya Bi. Kikelomo kuuahidi umati huo kuwa watampeleka mtoto na Qur’an katika Msikiti Mkuu wa Ijesha, ambako kila mmoja ataangalia hadi kuridhika. Baadae kitabu kiliwekwa kwenye boksi lisilozuia kuonekana kitu (transparent box) kwa jili ya kukitunza. Akizungumza baada ya tukio hilo, Kenny Ogunlana (31) rafiki wa Kikelomo alisema: “Nilimpeleka kituo cha afya kanisani baada ya kunieleza kuwa amezidiwa. Nilimhakikishia kuwa kila kitu kinawezekana kwa maombi. Alikuwa tayari amefikisha miezi 11 ya ujauzito.” “Wakunga walinieleza kuwa mtoto ni mkubwa sana, lakini sikumweleza Kikelomo, kwa sababu hakuwa katika hali ya kawaida. Alilazwa na baada ya muda nikaambiwa amejifungua mtoto akiwa kashika Qur’an”. Kikelomo alikuwa Mkristo, hivyo hakuweza mara moja kutambua kitu walichokikuta katika mkono wa kulia wa mtoto. Muuguzi naye hakujua.

Ni mama yake Kikelomo aliyeitambua haswa kuwa ni Qur’an Tukufu na kuwaita Maimamu wa eneo analoishi la Ijesha, ili kuelezea maana ya tukio hilo la mtoto kuzaliwa na Qur’an mkononi. Alhaj Ashimuyu Omotosho, Imam wa msikiti wa Ramatu Ishamiya, Ijesha, alisema aliitwa na aliwahi na kukuta tayari muuguzi ameshakitupa kitabu. “Ni kwa vipi utupe kitu bila kumsubiri mama wa mgonjwa ambaye alikuja kuniita? Hii ni alama ya Mungu. Kitu kinachoshangaza ni kwamba familia ni ya Kikristo. Inaonyesha tu wamoja kwa Mungu, lakini tumekuja duniani kuchagua na kwenda njia tofauti.” alisema Imam Omotosho. Kufuatia tukio hili, Bi. Kikelomo na mama yake, nao waliwaeleza Masheikh waliohudhuria sherehe hiyo kuwa nao wanataka kubadili dini na kuwa Waislamu. Nao wakasilimu na kuungana na mtoto wao. Mtoto alipewa jina la Abdulwahab Olarewaju Babatunde, na hapo kila aliyekuwepo alitoa kivumo cha “Allahu Akbar!” Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanaharakati wa National Missioner of Ansaru-deen, Alhaji Ahmaad Olarewaju, ambaye alinukuu aya ya Qur’an (Q41;53), ambapo Mwenyezi Mungu anasema atadhihirisha alama zake kwa watu mpaka kweli idhihiri. H a t a h i v y o alimtahadharisha mama wa mtoto kuwa asije

akamfananisha mtoto huyo na Mtume yeyote wa Mwenyezi Mungu. Alisema mtoto huyo amekuja duniani kama watoto wengine. Na kwamba katika Uislamu hakuna mahali ambako unaeleza kuwa mtoto anaweza kuwa na cheo kuliko watoto wengine. Olarewaju alisema kuwa kunakuwepo miujiza miongoni mwa watoto lakini Allah (SWT) anachagua ni wapi adhihirishe alama zake. Yeye pekee ndiye anayechagua kudhirisha kwa viumbe vyake. Miongoni mwa watu waliohudhuria hafla hiyo

Kupotea vyeti

Bwana Khamis Khatib Hassan (pichani) wa Kwale Micheweni Pemba anatangaza kupotelewa na vyeti vyake vifuatavyo: Form IV 2010. S1254/0128 pamoja na Result Slip, Micheweni Secondary School. Atakayeviokota apige simu Namba 0776 225818, 0652 410783 Au avipeleke kituo chochote cha polisi kilicho karibu naye.

5

AN-NUUR

Kimataifa

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

KHARTOUM MSHAURI wa Rais wa Sudan, Bw Mustafa Osman Ismail, amesema Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni adui mkubwa wa Waislamu, Wasudan na Waarabu. Aidha utawala wa rais Museveni umetuhumiwa kuwa unachochea hitilafu miongoni mwa nchi za Afrika. Akizungumza siku ya Ijumaa, Mshauri huyo aliongeza kuwa moja ya sababu ya kujitenga eneo la Sudan Kusini na Sudan Kaskazini, ni matokeo ya uchochezi wa Rais Museveni. B w. M u s t a f a O s m a n Ismail, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, amesema hivi sasa Rais Museveni ndie mchochezi mkuu wa hitilafu zinazoendelea kati ya Sudan na Sudan Kusini. Mshauri wa Rais wa Sudan amemtuhumu zaidi Museveni

“Museveni adui mkubwa wa Waislamu, Wasudan na Waarabu”
na kudai kuwa anatekeleza sera za kibeberu za Marekani na Utawala wa Kizayuni wa Israel. “Museveni ni moja kati ya mamluki muhimu zaidi wa Marekani na Utawala wa Kizayuni barani Afrika.” Alinukuliwa Bw. Ismail. Ikumbukwe kuwa Sudan Kusini ilitangaza kujitenga rasmi na Sudan Julai 9 mwaka 2011, lakini nchi hizo bado zinaendeleza vurugu kila moja ikitoa sababu zake. Wa k a t i h u o h u o imefichuliwa kuwa Sudan Kusini inatumia mamluki wa Marekani wa Shirika la Blackwater katika vurugu za kugombea mipaka katika ardhi ya Sudan. Imedaiwa kuwa shirika hilo la mamluki limebadilisha jina na sasa linajulikana kama Academy. Hayo yamefichuliwa na Profesa David Dishan, kiongozi wa chama cha upinzani cha Sudan Kusini kiitwacho South Sudan Democratic Front.

Na Wang Daiyu “TAFUTA elimu hata kama ni mbali kama uchina.” – Msemo wa Mtume Muhammad (saw) WATAFITI katika jimbo la Kaskazini Magharibi nchini China la Gansu wamegundua nakala ya Qur’an iliyoandikwa kwa mkono na kukamilishwa mwaka 1912, ambayo inasemekana kuwa ndiyo nakala ya zamani zaidi ya kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu kilichotafsiriwa kwa lugha ya kichina. Kitabu hicho cha tafsiri ya kichina kilichopatikana miongoni mwa mkusanyiko wa vitu vya kale na watafiti waliokuwa pamoja na Muslim Culture Institute of Lanzhou University, inaaminiwa kuwa kilitafsiriwa katika lugha ya Kichina na Sha Zhong pamoja na Ma Fulu. Wa w i l i h a o a m b a o wanaelezwa kuwa walikuwa ni Maimam na wajuzi wa lugha ya Kiarabu katika miji ya Lanzhou, Ding Shiren, alisema mkuu wa chuo hicho. Sha na Ma walianza kutafsiri Quran mwaka 1909 na kuhitimisha kazi yao mwaka 1912, alisema Ding. Baadae Sha alinakili kwa

Nakala ya zamani ya tafsiri ya Kimya cha mashirika ya haki za binadamu Qur’an kwa Kichina yagunduliwa dhidi ya mateso mateka wa Kipalestina
maandishi ya Kichina na kutengeneza nakala tatu za vitabu vilivyoandikwa kwa mkono, ambavyo vilitumika sana Lanzhou, Xinhua limeripoti. China ina kiasi cha Waislamu milioni 20 wengi wakiwa katika majimbo ya Xinjiang na Ningxia. Wakati Waislamu wa Xinjiang kwa kiasi kikubwa wakiwa ni Uygurs wenye asili ya Uturuki, Waislamu wa Ningixa wengi wao ni wa asili ya jamii ya Hui. Bw. Ding alisema matoleo mengine mawili ya tafsiri ya Qur ’an kwa kichina yalikamilika huko Gansu katika karne ya 20. Ding na wenzake bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa kuainisha matoleo hayo matatu. Alisema tafsiri ya Sha na Ma inaaminiwa na toleo la Kiarabu, ingawa sehemu ya maandishi ya Kichina yalitumia lahaja za Lanzhou. Wa t a a l a m w a n a s e m a Uislamu uliingia China kipindi cha Tang Dynasty (618-907). Lakini wanazuoni wa Kichina wa kale hawakutafsiri Qur’an, wakihofia kuwa wasingeweza kutafsiri kwa usahihi maandishi yake, alisema Bw. Ding. Source: Asian Age
GAZA MASHIRIKA ya kutetea haki za binadamu yamelaumiwa kwa kuendelea kupiga kimya dhidi ya jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala huo. Muhsin Saleh, ambaye ni mwalimu katika chuo kikuu cha Lebanon, amefichua kuwa mateka na wafungwa wengi walioko katika jela za kutisha za utawala wa Israel wanapata mateso makali. Alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya Press TV na kusema kuwa, mateso wanayoyapata mateka wa Kipalestina katika jela za mateso za utawala wa Kizayuni, yanapingana kabisa na sheria za kimataifa za haki za binaadamu. Amesisitiza kuwa, kwa mujibu wa vielelezo vya takwimu, asilimia 90 ya mateka na wafungwa wa Kipalestina waliomo katika jela hizo za Israel wanapata mateso makali kutoka kwa vikosi vya utawala huo. Katika upande mwingine, Naibu Waziri wa Masuala ya Mateka na Wapalestina Wa l i o a c h i l i w a H u r u w a serikali ya Palestina, amezitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwaunga mkono zaidi mateka wa Kipalestina na kuhakikisha wanatolewa katika jela hizo za utawala wa Kizayuni. Muhammad al Katri, amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Alam, mjini Ghaza na kuongeza kuwa, mateka wa Kipalestina wanakabiliwa na hali mbaya sana katika jela za Israel. Amesema mateka wa Kipalestina wanakabiliwa na hali mbaya mno hivi sasa wakiwa katika wiki ya nne ya kususia chakula na kadiri siku zinavyopita, ndivyo hali ya Wapalestina hao inavyozidi kuwa mbaya. Hata hivyo amesema, msimamo wa mateka hao ni imara na wanakabiliana vilivyo na ukandamizaji wanaofanyiwa na askari magereza wa Israel. Naibu Waziri huyo wa serikali ya Palestina ameongeza kuwa, ana matumaini harakati zinazofanyika huko Palestina na katika nchi za Kiarabu na Kiislamu za kuwaunga mkono mateka hao, zitaongezeka kwani mateka hao wanapigania haki zao za kimsingi ikiwa ni pamoja na kuikomboa Palestina kutoka katika makucha ya Wazayuni. Sehemu kubwa ya wafungwa na mateka wa Palestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel, hawajafikishwa mahakani wala kufunguliwa kesi dhidi ya tuhuma zinazowakabili,

RAIS Yoweri Kaguta Museven wa Uganda (kushoto) na Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

hali ambayo imewalazimu kusuasia kula, ikiwa ni sehemu ya shinikizo la kuutaka utawala wa Israel na mashirikika ya Kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuchukua hatua ili haki iweze kutendeka. Hivi karibunki mateka wanane wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Israel, walikimbizwa hospitalini kutokana na hali yao ya kiafya kuwa mbaya baada ya kushiriki katika mgomo wa kususia chakula kwa muda wa wiki kadhaa. Karibu mateka elfu mbili wa Kipalestina wamekuwa wakisusia chakula tangu tarehe 17 mwezi uliopita, wakilalamikia siasa za ukandamizaji dhidi yao na wafungwa wa Kipalestina katika jela za utawala wa Israel. Mateka hao wa Kipaletina wametangaza kuwa, wataendelea na mgomo wao huo hadi pale matakwa yao halali yatakapofikiwa. Mamia ya mateka wengine wa Kipalestina wametangaza kuungana na wenzao katika mgomo huo wa chakula. Katika hatua ya kufungamana na mateka hao, vijana wa Kipalestina wamefanya maandamano mbele ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Ramallah.

6

AN-NUUR

Makala

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012

Imethibitishwa: George W. Bush ni mhalifu wa kivita
Na Yvonne Ridley
May 11, 2012, “Mtandao wa kupashana habari” – Kuala Lumpur, Malaysia IMETHIBITISHWA: George W. Bush ni mhalifu wa kivita. Katika hukumu ambayo ni ya kwanza ya aina yake popote duniani, rais wa zamani wa Marekani na maofisa saba wa ngazi za juu wa utawala wake walipatikana Ijumaa iliyopita na makosa na jinai ya kivita. Bush, Dick Cheney (aliyekuwa Makamu wa Rais), Donald Rumsfeld (aliyekuwa Waziri wa Ulinzi), na washauri wao wa kisiasa Alberto Gonzales, David Addington, William Haynes, Jay Bybee na John Hoo walishtakiwa bila wao kuwepo mahakamani nchini Malaysia. Kesi hiyo iliyosikilizwa Kuala Lumpur ilisikia maelezo ya kuumiza moyo kutoka kwa waathirika wa mateso mikononi mwa askari wa Marekani na makampuni maalum ya ulinzi nchini Iraq na Afghanistan. Mashuhuda hao walikuwa ni pamoja na raia wa Uingereza Moazzam Begg, mfungwa wa zamani wa Guatanamo, na mwanamke wa Iraq Jameelah Abbas Hameedi ambaye aliteswa katika jela iliyopata sifa kwa maovu yake, Abu Ghraib. Katika hitimisho la kutoa ushahidi kwa wiki moja nzima, jopo la majaji watano lilifikia uamuzi wa pamoja ya hatia dhidi ya Bush, Cheney, Rumsfeld na washauri wao muhimu wa kisheria ambao wote walipatikana na hatia ya makosa ya jinai ya kivita kutokana na utesaji na vitendo vingine vya kikatili, visivyo vya klbinadamu na vya kuwadhalilisha waathirika. Maelezo ya kina ya mashitaka, taarifa za mashahidi na nyaraka nyinginezo, sasa yatapelekwa kwa Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, pamoja na Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama. Tume ya Jinai ya Kivita ya Kuala Lumpur pia imetoa rai kuwa majina ya Bush, Cheney, Rumsfeld, Gonzales, Yoo, Bybee, Addington na Haynes yaingizwe na kuongezwa katika Orodha ya Tume ya Wahalifu wa Kivita kwa kumbukumbu ya jamii. Jopo hilo la majaji liliundwa kwa ushauri wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Malaysia, Mahathir Mohammad, ambaye alipinga kwa dhati uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003. Aliketi mahakamani muda wote wa kusikilizwa kesi hiyo wakati jopo likichukua taarifa na ushuhuda wa mashahidi watatu, yaani Abbas Abid, Moazzam Begg na Jameelah Hameedi. Jopo pia lilisikiliza Taarifa ya Kisheria kutoka kwa mwananchi wa Iraq Ali Shalal na Rahul kwanza ambako majaji kadhaa wa Ulaya walitumia kanuni ya uwezo wa kushitakiwa mtu yeyote na popote, wakajitangaza kuwa wana sifa za kuweza kuhukumu makosa ya jinai yaliyofanywa na wakuu wa zamani wa nchi, licha ya sheria za kuwasamehe katika nchi zao. Wakati wote wa wiki nzima jopo lilifurika wataalamu wa kisheria na wanafunzi wa sheria wakati mashahidi wakitoa ushuhuda wao halafu kuongozwa katika maswali na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Jason Kay Kit Leon. Mahakama ilisikia jinsi: *Abbas Abid, injinia mwenye umri wa miaka 48 kutoka Fallujah nchini Iraq alivyoondolewa vidole vyake na koleo. *Ali Shalal alishambuliwa na nyaya za umeme zisizo na gamba na kupitishwa umeme na kutundikwa katika ukuta. *Moazzam Begg alipigwa, akavikwa nguo kufunika uso na kuwekwa katika selo maalum asikutane na watu. *Jameelah alivuliwa nguo na kudhalilishwa, na kutumika kama ngao-mtu wakati akisafirishwa kwa helikopta. Mashuhuda hao walieleza jinsi walivyobaki na vidonda vinavyotokana na mateso hayo hadi sasa. Moazzam Begg, ambaye sasa anafanya kazi kama mkurugenzi wa kituo cha kutetea haki za binadamu jijini London kiitwacho Cage prisoners alisema amefurahishwa sana na hukumu hiyo, lakini akaongeza: “Watu wanapozungumza habari za Nuremberg lazima ukumbuke kuwa wale walioshitakiwa walifunguliwa kesi baada ya vita.” “Hivi sasa Guantanamo bado imefunguliwa, watu bado wanashikiliwa pale na bado wanaendelea kuteswa pale.” Akijibu swali kuhusu tofauti kati ya tawala za Bush na Obama, aliongeza: “Kama Rais Bush alikuwa Rais wa mateso nje ya sheria, basi Rais Barak Obama ni Rais wa mauaji nje ya sheria kwa kutumia madege ya drone. Kazi yetu ndiyo kwanza imeanza.” Juhudi za waendesha mashitaka zililenga kuthibitisha kuwa wafanya maamuzi katika ngazi za juu kuanzia Rais Bush, Makamu wa Rais Cheney, Waziri wa Ulinzi Rumsfeld, wakisaidiwa na kupewa mori na wanasheria pamoja na makamanda na maofisa wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) – wote walifanya kazi kwa pamoja. Utesaji ulitumika kila mahali na ukawa kanuni iliyokubalika. Kwa mujibu wa waendesha mashitaka, ushuhuda wa mashahidi wote ulionyesha mwenendo wa kutumika dhidi yao kwa mbinu za kikatili, za kishenzi, zisizo na huruma na zinazodhalilisha utu wa

George W. Bush, Rais wa zamani wa Marekani.
Ahmed, ambaye pia ni raia wa Uingereza. Baada ya hukumu ya hatia kutolewa na majaji watano, Mahathir Mohammad alisema: “Mataifa yenye nguvu hayawajibiki hata kwa mauaji.” Mtaalamu wa masuala ya uhalifu wa kivita na mwanasheria Francis Boyle, Profesa wa sheria ya kimataifa katika Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Illinois nchini Marekani, alikuwa mmoja kati ya jopo la waendesha mashitaka. Baada ya hukumu alisema “hii ni mara ya kwanza watu hawa wamepatikana na hatia kokote duniani.” Wakati kesi hiyo inaonekana na wengi kuwa ni kama maonyesho tu, mpigania haki za binadamu Boyle alisema anatumaini Bush na washirika wake watajikuta wakifikishwa katika mahakama kama hizo kwingineko duniani. “ Tu l i j a r i b u m a r a t a t u kumpata Bush nchini Canada lakini tukazuiliwa na Serikali ya Canada, halafu tukamtisha Bush asifanye safari ya Uswisi. Jaribio la Hispania lilishindwa kutokana na serikali ya pale, na hiyo ilitokea pia Ujerumani.” Halafu Boyle akarejea Mkataba wa Nuremberg (uliowafikisha mahakamani viongozi wa Nazi walioanzisha Vita Vikuu vya Pili na kufanya mauaji ya halaiki maeneo mengi) ambao ulitumiwa na jopo hilo, alipoulizwa kuhusu uthabiti wa kisheria wa kesi hiyo nchini Malaysia. Alinukuu: “ Vi o n g o z i , w a a n d a a j i , wachocheaji na wahusika wengine walioshiriki katika kuandaa au kutekeleza mpango wa pamoja au njama za kufanya uhalifu wa kivita wanawajibika kwa vitendo vyote vilivyofanywa na mtu yeyote katika kutekeleza mpango huo.” Marekani inawajibika chini ya sheria za pamoja za kimataifa na Kanuni za Mkataba wa Nuremberg, alisema Boyle ambaye pia anaamini kesi hiyo ya wiki moja kwa hali yoyote ile ilikuwa ikifuatiliwa na maofisa wa Wizara ya Ulinzi na Ikulu ya Marekani. Profesa Gurdial Singh Nijar, ambaye aliongoza jopo la waendesha mashitaka alisema: “Jopo lilifanya kazi kwa uangalifu mkubwa kuhakikisha linasimama katika kanuni zilizoainishwa na mahakama za Nuremberg na mahakama za jinai za kimataifa” (yaani ile ya Yugoslavia, Rwanda na The Hague). Aliongeza kuwa anatumaini kuwa jopo hilo litafuatiliwa na kesi kama hiyo kwingineko duniani ambako “nchi zina wajibu wa kuwafikisha mahakamani wahalifu wa kivita” akichukua mfano wa dikteta wa zamani wa Chile, Augusto Pinochet ambaye alikamatwa nchini Uingereza na kupelekwa Hispania kwa mashitaka ya uhalifu wa kivita. “Pinochet alikuwa ameachia madaraka miaka minane tu iliyopita wakati hilo linatokea.” Kesi ya Pinochet ilikuwa ya

binadamu. Vi t e n d o h i v i v y a j i n a i vilitumika na kuongezeka kufikisha maumivu makali ilivyowezekana na taabu, walisema wanasheria. Rais wa jopo hilo Tan Sri Dato Lamin bin Haji Mohamed Yunus Lamin, alifikia tamati kuwa waendesha mashitaka walikuwa wamethibitisha “bila shaka yoyote kuwa washitakiwa, Rais wa zamani George Bush na wapanga njama wenzake walihusika katika utando wa amri, vidokezo, maelekezo, ushauri wa kisheria na vitendo ambavyo viliweka nia ya pamoja na lengo, shughuli ya pamoja na/au njama za kutenda jinai ya Utesaji na Makosa ya Vita, ikiwa ni pamoja na bila kuishia katika mpango wa pamoja na lengo la kufanya makosa yafuatayo kuhusiana na ‘Vita dhidi ya Ugaidi’ na vita vilivyoanzishwa na Marekani na wengine nchini Afghanistan na Iraq.” Rais Lamin aliimbia mahakama iliyokuwa imefurika: “Kama jopo la hisia ya haki, Jopo linafahamu fika kuwa hukumu yake ni ainisho tu katika undani wake. Jopo halina mamlaka ya kutekeleza hukumu, halina mamlaka ya kutamka adhabu ya kifungo kwa yeyote kati ya mmoja au zaidi kati ya watu wanane waliopatikana na hatia. Tunachoweza kufanya, chini ya Ibara ya 31 ya Sura ya VI sehemu ya pili ya Mkataba (wa Nuremberg) ni kupendekeza kwa Tume ya Makosa ya Jinai ya Kivita ya Kuala Lumpur (iliyounda jopo hilo) kufikisha tamati hii ya Jopo ya kupatikana na hatia, pamoja na nakala ya mwenendo wa kesi, kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, pamoja na Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama (la Umoja wa Mataifa). “Jopo pia linapendekeza kwa Tume ya Kuala Lumpur ya Jinai ya Vita kuwa majina yote ya watu wanane waliopatikana na hatia yaingizwe na kuongezwa katika Orodha ya Tume ya Wahalifu wa Kivita na ienezwe kama inavyopasa. “Jopo linapendekeza kwa Tume ya Jinai ya Vita kutoa uenezi mpana inavyowezekana kwa hukumu hii ya kupatikana na hatua na kutolewa kwa fidia, kwani huu ni uhalifu wa kivita unaotambulika kote ambako kuna wajibu kwa mataifa kuibua mashitaka kama mmojawapo kati ya washtakiwa hawa akiingia kwenye milki zao kisheria.” (Makala hii imefasiriwa na Anil Kija kutoka makala Bush Found Guilty Of War Crimes iliyoandikwa na Yvonne Ridley. Mwandishi wa habari wa Uingereza Yvonne Ridley pia ni mdhamini wa Cage prisoners)

7

AN-NUUR

Makala

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012 katika nyumba moja bila ya kuwepo mipaka ya kijinsia wala pazia la heshima kati ya watu wazima na watoto. Katika majumba haya wanaume na wanawake wasio maharimu, hukabiliana chumba kwa chumba, hupigana vikumbo sebuleni, hukaribiana kwa siri bafuni na vyooni n.k. Muda wa kuwa mazingira hayawakingi watu na jinsia tofauti, basi ile hatari iliyoepushwa na Uislamu kwa kutaka zinaa isikurubiwe, wanaume washushe macho yao na wanawake wachunge stara zao na kubaki majumbani, itakuwa zaidi. Kwa hali hii maisha haya ya upangaji yanapingana kabisa na maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Aidha watoto hulala na wazazi wao katika chumba kimoja kwa sababu ya kuwa ndicho wanachomiki wazazi, matokeo yake ni kuharibika kwa maadili ya watoto. Nyumba ya Muislamu ni mahali ambapo huweza kufanya mambo yake ya faragha kwa uhakika na utulivu bila kuingiliwa na mtu. Hivyo kujisitiri na aibu, kupata usalama na stara ya mambo mbalimbali. Nyumba ya Muislamu ambayo inakosa kuwa na sifa hii na ikawa ni huria kwa kila mtu kujingilia, inakosa sifa ya kuwa ni nyumba ya Kiislamu. Nyumba ya Muislamu haitakikani kisheria kuwa kila mtu anakaribishwa na kuingia kama vile sokoni, bali inatakikana kuingia watu maalumu wenye sifa maalumu. Kwani kinyume cha hivyo kusipokuwepo na udhibiti na tahadhari kubwa mno kutatokea hatari na madhara makubwa yatakayosababishwa na watu ambao ni makhabithi kuwakaribirisha nyumbani kwani wataingiza familia ya Muislamu kwenye mambo ya “Munkarati”. Kwa mukhutasari hizi ni baadhi ya sifa ambazo zinastahiki kuwa kwenye nyumba ya Muislamu. Lakini nyumba nyingi mno za Waislamu zimekosa sifa za kuwa ni nyumba za Kiislamu. (Kwa maoni, mawasiliano tumia namba ya simu 0714 720 965)

Na Abu Saumu Kombo Hassani, Tanga

IMEPOKEWA kutoka kwa Osama bin Zaid (R.A.). (Hakika) Mtume ( S . A . W. ) a l i p a n d a katika kuta za mji wa Madina na akasema:“Je, mnaona ninayoyaona? Wakajibu: “Hapana”. Mtume (S.A.W) akasema: “Hakika mimi ninaona FITINA katika majumba yenu inamiminika kama inavyomiminika mvua.” (Imepokewa na Bukhari na Muslim) Fitina mahali inapomiminika ni katika majumba, hivyo inapaswa jamii kufahamu nafasi na umuhimu wa nyumba katika kulinda imani, utulivu wa nafsi, akili, kiwiliwili na kupata stara ya kibinadamu. Maskani au nyumba ni mahali ambapo mtu hupata kujikinga na kujistiri na ghasia za ulimwengu na kukhisi kuwa faragha na uhuru wa kufanya yake mbali na matatizo ya kijamii, akaweza kupumzisha kiwiwili chake na kutuliza nafsi yake. Na kwa sababu ya haya, Mwenyezi Mungu katika kuielezea neema zake juu ya waja wake na viumbe vyake kwa ujumla akasema: “Na Mwenyezi Mungu amekujalieni majumba yenu yawe makazi (Maskani) yenu” (Suratul An-Nahl 16:80). Kwa sababu hii Mtume (S.A.W.) alikuwa akipenda nyumba yenye nafasi na wasaa na kuchukulia hilo kuwa ni katika mambo ya starehe na furaha za kidunia, alisema: “Mambo manne ni katika mambo ya furaha: mwanamke mwema, nyumba yenye nafasi, jirani mwema, na kipando kizuri” (Ibn Hibban) Vile vile Mtume (S.A.W.) alikuwa akiomba sana dua hizi: “Ewe Mola nisamehe madhambi yangu, na unipe wasaa katika nyumba yangu na unitilie baraka katika riziki yangu”. (Nisai) Muislamu kwa Mwenyezi Mungu kumpatia neema ya kuwa na nyumba; ni neema kubwa ambayo watu wengi wameikosa. Hivyo inampasa mwenye kupata neema hiyo kuitumia kama nyenzo ya kujikurubisha

Nyumba ya Muislamu

kwa Allah (S.W) na isiwe ni katika “nakama” ya kuangamiza dini na dunia yake. Mwenyezi Mungu kwenye Qur’an anatufahamisha jinsi ambavyo mdudu chungu alivyo watahadharisha wadudu wenzie juu ya majeshi ya Suleman yalipokuwa kwenye msafara ili yasiweze kuwadhuru na kuwatangazia wenzie kwamba wajifiche kwenye majumba yao ili kuepukana na zahama ya majeshi hayo. Na pia Mtume (S.A.W) alipokutana na Jibril kwa mara ya kwanza kwenye jabal Hira alitishika sana na kukimbilia nyumbani kwake ili kupata utulivu na kuondokana na hofu iliyokuwa ikimkabili. Amesema Allah (S.W): “Na alipokusanyiwa Suleman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu. Mpaka walipofika kwenye bonde la wadudu chungu alisema mdudu chungu mmoja; Enyi waduduchungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Suleman na majeshi yake bila ya wao kutambua”. (Naml 27:17-18) na Rejea sababu za kuteremshwa “Sababu nuzul” ya Suratul Muzzammil na

Muddathir. Na pia mtu kukosa kumiliki nyumba nayo ni Fitina ya adhabu ambayo Mwenyezi Mungu ameikadiria kumfikia mja ili apate kumkumbuka na kumshukuru ambako kutapelekea kujirekebisha mienendo yake na kurejea kwa Allah (S.W), yaani kutubia. Ban-Israel walitiwa katika Fitina ya adhabu ya kukosa kuwa na makazi na kutangatanga kwa muda wa miaka arobaini (40) wakiwa jangwani. Amesema Allah (S.W.): “Akasema (Musa): Mola wangu mlezi! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu. Basi tutenge na hawa watu wapotovu. (Mwenyezi Mungu) akasema: basi nchi hiyo wameharamishiwa muda wa miaka arobaini, watakuwa wakitanga tanga katika ardhi. Basi wewe usiwasikitikie watu wapotovu”. (Suratul Maidah 5:25-26). Katika zama za Mtume ( S . A . W. ) a l i p o k u w a akiendesha dola ya Kiislamu pale Madina, Mwenyezi Mungu aliwaadhibu Mayahud kwa kosa la kumfayia hiyana Mtume (S.A.W.) na Waislamu kwa kuvunja mikataba waliyokubaliana. Hivyo wakabomoa nyumba zao kwa mikono yao na

mikono ya Waislamu. Amesema Allah (S.W.): “Na yeye ndiye aliyewatoa waliokufuru miongoni mwa watu wa kitabu katika nyumba zao wakati wa uhamisho wa kwanza. Hamkudhani kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawalinda na Mwenyenzi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu aliwafikia kwa mahali wasipo tazamia, na kuwatia woga katika nyoyo zao. Wakawa wanazibomoa nyumba zao kwa mikono yao na mikono ya waumini. Basi zingatieni enyi wenye macho”. (Suratul Hashri 59:2) Ninaposema maskani au makazi ninakusudia mtu kumiliki makazi yake. Lakini mtu kuwa anaishi katika makazi ya kupangisha aina ya “Changanyikeni” ambayo mwenye nyumba ndio mwenye mamlaka na maamuzi ya mwisho na mpangaji ni mtu kufuata tu masharti. Ni kuwa Muislamu itakuwa bado hajapata utulivu na wasaa wa kutekeleza ibada mbalimbali. Hivyo bado atakuwa yupo kwenye fitina kubwa mno, kutokana na kuwa upangaji wa changanyikeni una nafuu ya kodi lakini una athari mbaya kimaadili kutokana na ukweli kuwa familia nyingi zenye “akhalaki” tofauti husongamana

8

Mtii mume wako upate kuridhiwa na Allah (sw)
Na Pendo Masasa K AT I K A d a r a s a l a wanawake wiki hii tutakumbushana jambo muhimu sana kwa mwanamke wa Kiislamu, kama ilivyo kwa waumumi wa Kiislamu kwamba kukumbushana ni jambo muhimu ili kuweza kufikia malengo ya kumbwa kwetu. Kwanza nianze na kisa kimoja ambapo mwanamke mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w) na kumuuliza, “Mimi ni mwanamke niliyekuja kwako, jihad ni faradhi waliyoandikiwa wanaume, wakijeruhiwa hupata thawabu na wakifa huwa hai kwa Mola wao wakiruzukiwa, ama sisi wanawake ndiyo wasaidizi wao je, hatuna ujira kama wanavyo pata wao?” Mtume alimjibu mwanamke huyo kwa kusema, “waambie wanawake wenzako utakaokutana nao kuwa utiifu kwa mume na kujua haki zake ni sawa na jihaad, ni wachache miongoni mwenu mfanyao hayo”. Wanawake wa zama hizi kutokana na fikra tulizo jazwa na wanaharakati wa haki za wanawake bila kufahamu, wengi wameacha mfundisho ya dini, kiasi ambacho ule utii unaotakikana katika kumtii mume umepungua sana. Tumesahau kuwa ni moja ya jihad na kuna malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Mwanamke wa Kiislamu kufanya kibri cha kutotii maamrisho ya Allah (sw) na Mtume wake kwa kutozingatia maelezo yaliyotolewa, huwa tayari umejitengenezea njia ya motoni . Amesema Mtume (s.a.w) akiswali mwanamke swala zake tano na kufunga miezi ya Ramadhani na akihifadhi tupu yake na akatii mumewe, ataambiwa (siku ya kiyama) ingia peponi kwa mlango wowote unaotaka . Fahamu mwanamke wa Kiislamu kuwa mume wako ndiyo pepo yako pindi unapomtii kwa yale yanayoridhiwa na Allah (sw), ukiacha kumtii ni kuandaa mazingira ya motoni . Kinachotakiwa kuzingatia katika kumtii mume, ni kama jambo analotaka umtii kwalo linakubalika kwa mujibu wa dini ya Kiislamu. Jambo lisilokubalika kwa mujibu wa dini, mfano suala la kumshirikisha Mwenyezi

AN-NUUR

Darasa la wanawake/Tangazo

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012

Mungu huna haja ya kumtii. Tu k i t i z a m a m a t a t i z o mengi yanayozikabili familia nyingi, utaona sababu kubwa ni mke kumuasi mume wake na kutokuwa na utii kwa mumewe na kumukhalifu kwa lile lenye kuchukiza. Yote haya ni matokeo ya mwanamke kutokujua haki za mumewe juu yake au inawezekana kutokana na kiburi alichokuwa nacho, wasiwasi wa shaytwani na kushawishiwa vibaya ili wagombane mume na mke . Ya p a s a m w a n a k e w a Kiislamu ujue haki ya mume kwako, fadhila zake juu yako ni kubwa sana kama hadithi ya Mtume inavyosema: “Lau ingefaa kwa mwanadamu kumsujudia mwanadamu mwenzake, basi ningeliamrisha kwa mwanamke kumsujudia mumewe kwa ukubwa wa haki yake kwake “’ Vile vile yapasa kutambua kuwa wanaume ni viongozi kwa wanawake, hatuwezi kulikwepa hilo kwa mujibu wa maandiko na mafundisho y a d i n i y e t u . Tu k i z i d i kung’ang’ania dhana za kibinadamu za usawa zinazopigiwa chapuo na wanaharakati wa haki za wanawake wa kimagharibi, hakika watatupoteza na lazima mwisho wetu utakuwa mbaya kwa kuwa tutakuwa nje ya misingi ya Mungu aliyotuwekea kati ya mume na mke. Angalia mwanamke wa Kiislamu, Mwenyezi Mungu heshima aliyokupa ukimtii mumeo kama Mtume anavyosema: “Wanamtakia msamaha ndege mwanamke mwenye kumtii mumewe, ndege

angani samaki baharini [majini] malaika mbinguni [wote wanamtakia msamaha mwanamke huyo ] muda wote anapodumu katika radhi ya mumewe’’. Si moja Mtume [S.a.w] alikuwa akimuusia mwanaye Fatuma [R.a], Ewe Fatuma hakika ya mwanamke akitwanga kwa ajili ya mumewe na watoto Mwenyezi Mungu humuandikia kila punje moja ya ngano (au nafaka yoyote thawabu moja, humfutia dhambi moja na humnyanyua daraja moja) ya pepo , Ewe Fatuma hakika ya mwanamke akitabasamu wakati wa kumtazama mumewe Mwenyezi Mungu

humtizama na yeye kwa jicho la rehema . Mtume [s.a.w] akaendelea kumuusia mwanae, “Ewe Fatuma hakika ya mwanamke akiumia wakati wa kumtwangia mumewe, Mwenyezi Mungu atamtenganisha baina yake na moto kwa mipaka saba, Ewe Fatuma hakika mwanamke atakaye muhudumia mumewe kwa ukweli kabisa atatoka katika madhambi yake yote kama siku alivyozaliwa kwa mama yake”. Hakuishia hapo, alizidi kumuusia, Ewe Fatuma hakika ya mwanamke akibeba mimba tumboni Bismillah Rahman Rahim

mwake, malaika wanamtakia msamaha na Mwenyezi Mungu kumwandikia kila siku thawabu elfu moja na kumfutia madhambi elfu moja na akifa hutolewa katika madhambi kama siku alipozaliwa kwa mama yake. Ewe Fatuma, bora katika hayo yote ni radhi ya mume kwa mkewe, Ewe Fatuma hakika radhi ya mume ndiyo radhi ya Mwenyezi Mungu na kumuudhi mume ndiyo kumuudhi Mwenyezi Mungu . Kutokana na faida hizi anazopata mwanamke wa Kiislamu kupitia wanaume, ndipo Bi. Aisha (R.a ) mke wa Mtume [s.a.w ] aliponadi kuwaambia wanawake, “enyi makundi ya wanawake lau mngelijua haki za wanaume zenu juu yenu, angalifuta mwanamke vumbi katika nyayo za mumewe kwa paji la uso wake’’. Kwa hivyo wanawake wa Kiislamu tuishi kwa kuwasoma na kuwaiga wanawake wema waliotangulia, kuwaiga kwa vitendo vyao tutakuwa wenye kufanikiwa katika ndoa. Malengo ya Wanaharakati wa Haki za Wanawake sio mazuri. Zaidi wanakusudia wanawake waende kinyume na mafundisho ya dini kwa sababu tu ya matamanio ya kibinafsi hapa duniani. Kumtii mume kuna faida kwetu vile vile ni Jihaad, na kumuasi kuna hasara kubwa kwetu .

DAR ES SALAAM No. Usajili CU-112 UDAHILI (INTERVIEW) MAFUNZO YA UALIMU 2012-2013 CHUO KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO NA UDAHILI 1 June 2012 saa 2:00 Asubuhi. GRADE III A NA DIPLOMA KWA VIGEZO VYA WIZARA YA ELIMU NA BARAZA LA MITIHANI.
Waliosoma Elimu ya dini ya Kiislami EDK na madrasa watapata kipaumbele. UDAHILI UTAFANYIKA KWENYE VITUO VYOTE VYA KUCHUKULIA FOMU VILIVYOPO MIKOANI KWA DAR ES SALAAM UTAFANYIKA CHUONI UNUNIO. KWA MAWASILIANO ZAIDI: MKUU WA CHUO: 0713 022178 MSAJILI 0715 822332 0784 822332 0756 822332 Wabillah Tawfiq

CHUO CHA UALIMU UNUNIO

9

AN-NUUR

Makala

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

Waislamu wapo kama hawapo
Amesema kweli Khatib Masjid TIC, Magomeni Mayahudi, Wakristo waielewa zaidi Qur’an 5:51 Wanaifanyia kazi. Makkah, Madinah kulipuliwa (?)
Na Omar Msangi IJUMAA ya wiki iliyopita Khatib katika msikiti wa Ijumaa, Magomeni TIC, maarufu Kichangani, alitoa khutba ambayo inapasa kutiliwa mkazo kwa faida ya Waislamu wote nchini. Akirejea aya ya 2 katika suratul Jumua (62) alisisitiza umuhimu wa kosoma akisema kuwa hakuna Muislamu anayetakiwa kuwa ‘maamuma’ kwa maana ya mtu asiyejua. Ile kwamba Allah katika Qur’an anauliza “Je, wanalingana wanaojua na wasiojua”, ni kielelezo na msisitizo kuwa Muislamu anatakiwa awe msomi, awe mjanja na ayajue vyema mazingira anamoishi. Watu wanaweza kupishana katika kujua. Huyu akawa bingwa wa fani fulani na yule akabobea katika fani nyingine, lakini almuhimu watu wote wanatakiwa wawe wajuzi. Katika ufafanuzi wake Khatib alisema kuwa muhimu na la mwanzo ni kila Muislamu kuijua Qur’an. Watu wajue Kitabu cha Allah na wakisome kwa mazingatio kwa sababu ndio Mwongozo wa maisha yao. Lakini zaidi ya hapo, Waislamu wanatakiwa wayajue mazingira yao. Wajue mambo yanayotokea katika ulimwengu wanamoishi na waweze kuyapa tafsiri sahihi. Alisema, ile hekma iliyotajwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) kawafundisha Waislamu HIKMA, maana yake pana ni kukiweka kila kitu mahali pake. Jambo ulielewe vile lilivyo na linavyokuathiri iwe ni kwa faida au hasara. Hata hivyo akionyesha masikitiko yake Khatib alisema kuwa ilivyo hivi sasa ni kana kwamba Waislamu hawapo. Wapo kama hawapo. Akasema, ni kwa kutoyajua mambo na kutojitambua, baadhi ya Waislamu wamekuwa wakitumiwa ovyo (bila kujijua kwamba wanatumiwa kuudhuru Uislamu na kuwadhuru Waislamu.) Au wakawa wanafanya mambo serikalini na hiyo huwafanya ‘kuvimba vichwa’. Wakajifakhari kujiita Mufti, Sheikh Mkuu, Sheikh wa Mkoa, Naibu Mufti, Sheikh w a Wi l a y a , K a t i b u w a Bakwata Mkoa na vyeo vingine kama hivyo katika Bakwata. Na kwa bahati mbaya kabisa, baadhi yao wamekuwa wakitumia vyeo hivyo kupiga hodi katika ofisi za serikali kuwafitini Waislamu au kukwamisha baadhi ya miradi ya maendeleo ya Waislamu. Lakini labda tujiulize, Mtei alipodai kuwa Tume ya Warioba imejaa Waislamu, alitizama wangapi wanaswali swala tano na wangapi hawaswali? Alitizama wangapi Bakwata na wangapi wafuasi wa Bakwata au alitizama tu majina ya Waislamu? “FBI Teaches Agents: ‘Mainstream’ Muslims Are ‘Violent, Radical’”, ni makala iliyoandikwa na Bwana Spencer Ackerman (Septemba 14, 2011). Katika makala hiyo anasema kuwa kwa wale wenye agenda ya kupambana na Uislamu duniani, hawabagui huyu Muislamu ni “moderates” au siasa kali. Huyu Bakwata, Salafi, Answaru sunnah au Msoma Maulidi. Akinukuu kauli za makamanda wa FBI na wa jeshi la Marekani anasema kuwa katika mafunzo yao wapiganaji hao wa kile kinachodaiwa kuwa ni ugaidi, wanafundishwa kuwa Muislamu yeyote, maadhali anaisoma na kuiamini Qur’an ni hatari. Ni adui wa kupigwa vita. “The FBI is teaching its counterterrorism agents that “main stream”… Muslims are likely to be terrorist sympathizers;…(because) …Any war against nonbelievers is justified” under Muslim law; a “moderating process cannot happen if the Koran continues to be regarded as the unalterable word of Allah.” H a y o n d i y o wanayofundishwa makamanda, askari wa miguu na mgambo wa vita dhidi ya ugaidi. Kwamba muda wa kuwa Muislamu anaamini kuwa Qur’an ni kitabu cha Allah, huyo si mtu wa kuamini. Ni wa kupigwa vita. Kama ni kumtumia, mtumie kwa tahadhari huku naye ukimuwekea mkakati wa kumuangamiza. Labda tujiulize, kuna Bakwata Inaendelea Uk. 14

ambayo hayana tija na wao wenyewe au na Uislamu. Katika ufafanuzi wake alizungumzia tukio la hivi karibuni ambapo mwanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei alitoa kauli akisema kuwa katika uteuzi wake Rais Kikwete kajaza Waislamu wengi katika Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba nchini. Alisema, ukitizama Tume ile kwa upande wa wajumbe wa Tanzania Bara, Wakristo ndio wengi, lakini Mtei kaja juu. Jambo hili Waislamu wameliweka wapi, wamelipa tafsiri gani? Alihoji. Alieleza kuwa ukichambua jambo hilo kwa undani utaona kuwa ‘jamaa hawa’ wana agenda za ziada zaidi ya hizi za kuangalia masuala ya kitaifa na kinchi. Kwa nini watake wawe wengi kila mahali, katika kila mabaraza, kila tume na kila sehemu ya serikali? Haya ndiyo maswali inatakiwa Waislamu wajiulize. Hata hivyo akasema, inavyoonekana Waislamu hawapo. Hawapo ndio maana wanaweza wakaibuka akina Mzee Mtei na kusema waliyosema. Hoja ya msingi ni kuwa n i Wa i s l a m u w a n g a p i wanajishughulisha na kuhoji

ni kwa nini “hawa jamaa” wapo wengi kila mahali na huja juu wakiona kuna mahali angalau Waislamu nao wapo wapo? Je, Waislamu nao inawashugulisha kuona wapo wangapi katika ma-DC, maRC, Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakurugenzi n.k? Kwa kutozingatia na kujua mambo yanavyokwenda katika jamii, Khatib akasema ndio unakuta baadhi ya Waislamu na hasa vijana huparamia tu mambo iwe ni kuingia katika vyama vya kisiasa au kushabikia agenda za baadhi ya makundi katika jamii kumbe wenzao wana agenda zilizojificha. Kiasi wiki mbili zilizopita niliandika makala nikigusia hali ya kushambuliana katika majukwaa inayofanywa na baadhi ya wahadhiri na masheikh. Huyu akishutumu kundi hili na yule akijibu mapigo. Jumanne wiki hii nilisikia mawaidha kama hayo yaliyorekodiwa katika CD ambapo Masheikh wa Mombasa, Kenya walikuwa wakirushiana madongo katika mdahalo wakilumbana juu ya “Maulid”. Tukiacha malumbano kama hayo, nchini hapa kumekuwa na mgawanyiko wa Waislamu katika makundi makubwa mawili. Moja ni

wale wanaoitwa wa Bakwata na wale wanaoipinga Bakwata. Ufupi wa maneno Bakwata na Masheikh wake wanashutumiwa kuwa wanatumiwa kudumaza maendeleo ya Waislamu. Na hii ni kutokana na historia ya kuundwa kwake. Kwamba iliundwa baada ya kuvunjwa East Africa Muslim Welfare Society, jumuiya iliyowaweka p a m o j a Wa i s l a m u w a Afrika Mashariki na kuanza kutekeleza mipango ya kuwaletea maendeleo katika elimu, afya na huduma za kijamii. Kwamba baada ya kupigwa marufuku EAMWS, Bakwata ilitwaa mali za jumuiya hiyo, lakini haikuweza kufanya lolote zaidi ya kutumia mali hizo kifisadi. Inadaiwa pia kuwa mara nyingi viongozi wa Bakwata wamekuwa wakikaa mbali na shida na madai ya Waislamu. Kama taasisi ya kitaifa na inayotambulika na kukubalika rasmi na serikali, haijitokezi kupigania haki za Waislamu. Kwa hiyo unaweza kusema kuwa ni haki kabisa kwa Waislamu kuwashutumu Bakwata na kujitenga nao. Kwa upande mwingine, masheikh wa Bakwata nao hujisikia sana wakijiona kuwa wao ndio wasemaji wa Waislamu wanaotambulika

10

AN-NUUR

Makala

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012

Kweli mnapanda viscudo akina Jecha
Lakini Viscudo vimekutieni upofu wa akili
hawa tokea zamani ni huu:“Tunataka kuwahakikishia wale wote wanaojiita kama ni Wazanzibari kwamba, chochote isiyokua dola ya Kiafrika hakitakubaliwa itakapopatikana Serikali huru. Vile vile tunapinga Serikali yenye mchanganyiko na makabila katika Visiwa hivi, kwani ni kinyume na msimamo wa Chama hichi. Nimeeleza hapo awali tofauti za kimtazamo, fikra na kauli za Viongozi ndio husababisha faida na hasara. Haya mapambano ya fikra hizi ndio yanayoendelezwa hadi hivi sasa. Hebu fikiria ikiwa Nyerere ni Muafrika lakini analitambua kabila lake kwamba ni Mzanaki hebu wewe Muafrika wa hapa Zanzibar iwe ndio kweli hujielewi ni wa kabila gani? Sio lengo langu kuzungumzia Ukabila lakini hawa Viongozi wababaishaji wanaojiita ni Waafrika huku wakiyasahau Makabila yao huu ni utumwa wa fikra. Kama Uafrika ndio nguzo, basi aende Kenya, Mali, Rwanda watampokea na kuishi bila hati, viza au kibali chochote. Si Muafrika? Hivyo mtu wa Kilimanjaro hajielewi kwamba yeye ni Mchaga? Au mtu wa Mbeya hajielewi kwamba yeye ni Mnyakyusa au mtu wa Iringa hajielewi kama yeye ni Mhehe? Hao wote si Waafrika ikwa Nyerere anasema hivi kwamba yeye ni Mzanaki hali ni Muafrika safi. Je! wewe Muafrika wa Zanzibar utakua huna kabila?. Halafu unataka kuwaambia wenzako kwamba wewe ndio mwenye Visiwa hivi mwengine yoyote hana maana. Eti umepinduwa, masikini roho yako “wewe umepinduliwa” na bado Mapinduzi daima, Mapinduzi yataendelea hivi hivi mbele ya macho yenu. Si mumeona au mnajitia upofu? Siku zote mkituambia hawa kina Seif ni wapinga Mapinduzi leo wao ndio wamekuwa wanamapinduzi na kuvikalia viti vya Baraza la Mapinduzi, si Mapinduzi daima itikieni basi “daima”. Hivi sasa kwenye mikutano yenu mkisema Mapinduzi basi watu wa Visiwa hivi wanaitikia kweli kweli kwamba sasa kweli Mapinduzi daima, maana mnapinduliwa kwa vile mnapanda viscudo akina Jecha na Pandu. Viscudo vimekutieni upofu wa akili. Ni dhahiri wengi wenu mnaona gari ndio kitu kikubwa sana katika maisha yenu hivyo kiongozi yupo radhi kuuza nchi kwa sababu anamilikishwa “kiscudo”, aibu tupu. Aibu kama mtu hajui hata kabila yake eti “Mwafrika” basi waafrika si wana makabila yao jamani, sasa nyinyi mnaojiita waafrika wa Zanzibar ndio hamna makabila sio uwongo huo. Msibabaishe watu hapa Visiwani kila mtu ana asili na kabila lake msitupe uwenyeji wa kijumlajumla.

Na Ibrahim Mohamed Hussein NIMEHAMASIKA kuandika makala hii baada ya kusoma gazeti la An-nuur la April 20-26,2012 makala isemayo:“Mashekh sasa waanza kuparurana hadharani.” Mkutano wa CCM katika viwanja vya Magogoni, Jumapili April 14, 2012 mimi sikwenda lakini nimesoma ndani ya gazeti la AN-NUUR. Moja ya neno ambalo limefanya na lina uzito wake lililotamkwa hapo mkutanoni ni hii kauli ya :- “Shekh, sema kweli japo inauma hii tutaisema wacha iwaumize.” Tunachosema ni kwamba sisi ni Wazanzibari kama walivyo Watanganyika, kama walivyo Wakenya, wa Uganda, Wazambia au Waingereza. Ujumla wetu ndio unafanya Utaifa wetu hatuwezi kuitwa Waafrika kwa sababu ya kikundi kichache kutaka kutimiza lengo la siasa la kuifanya Zanzibar ni Visiwa vya Tanganyika. Historia ya Zanzibar na kuwepo kwa Washirazi hakukuanza wakati wa kuundwa kwa jumuia hizi. Watu walijitambua kuwa ni Waafrika kutoka Tanganyika walikuwepo kabla ya jumuia hizi kuundwa. Nimeeleza kwamba Washirazi wanajuulikana kuwepo kwake hapa Zanzibar tangu Karne ya tisa na kabla hapo kwa ushahidi wa vitu na majengo. Mfano mzuri ni ule wa Msikiti wa Kizimkazi na kupatikana kumbukumbu za vitu baada ya kuchimbwa magofu ya Tumbatu na Pemba. Nyerere alijua kwamba kama hakupata wenyeji wa Zanzibar yaani Washirazi asingeweza kupata matakwa yake ya miaka ya nyuma. Mtazamo, fikra na kauli ya Nyerere ni kuviburuta Visiwa vya Zanzibar na kuvitupa katikati ya Bahari ya Hindi ili visionekane kabisa. Huu ni mtazamo na fikra za Nyerere ambao amezitamka na tukazielewa. Watanganyika kupitia kwa Nyerere wakiunda Tawi la Africa Association ambalo kutokana na Tawi hilo ndio Nyerere atakapolitumia ili kufikisha malengo yake. Tawi hili liliwakilisha Waafrika waliozaliwa sehemu mbali mbali za Afrika Mashariki na kati hasa Bara la Nyika Mrima mtazamo, fikra na kauli ya ndugu zetu

MHE. Benjamin William Mkapa
Nyinyi Waafrika na wengine wote hapa Zanzibar ni haki sawa, kweli Zanzibar ni nchi ya Kiafrika hilo halina ubishi. Lakini sio Wakfu wa kila Muafrika akiteremka Visiwani basi ndio mwenyewe. Mbona Msumbiji au Afrika ya Kusini hamuendi mkaleta upuuzi huo mtachinjwa. Tumeshuhudia vitimbi vinavyofanywa na nchi hizo kwa Waafrika wenzao, nani asiyejua hayo. Thubutu! Upuuzi huo ufanyeni Zanzibar kwa vile wenyewe shida yao kubwa ni madaraka na viscudo tu. Tumeshuhudia Mh. Benjamin Wi l l i a m M k a p a a l i e k u w a Rais wa Tanzania akimueleza Jonathan Power na kumwambia:“Viongozi wa Zanzibar wako tayari kuuwa lakini sio kuachia madaraka.” Sasa ikiwa viongozi akili zao zipo kwenye kupewa madaraka hicho ndio wanachokitaka kama alivyosema Mheshimiwa Mkapa na wengine, maendeleo kwao ni kumiliki “Viscudo” hiyo si hatari? Vi o n g o z i w e n z e n u w a Kiafrika kibao wameuwawa nyie kimyaa!!, Nchi haina uwezo wa kujiamulia mambo yake yaliyo muhimu nyinyi kimyaa!! Mh. Aboud Jumbe katolewa madarakani na hao hao Waafrika wenzake nyie kimyaa!!, almuradi mnayo madaraka na mnamiliki Viscudo, basi ndio mshafika, zaidi ya hapo ni kujitilia vitumbua vyenu mchanga. Ni nyinyi mlioifikisha Zanzibar na kuikosesha kutambulika na kuheshimika kama Dola kutokana na udhaifu wa baadhi ya Viongozi wanaotaka madaraka kwa kupita mlago wa “Muafrika”. Sasa tumkamate nani na kila Muafrika hapa Visiwani ndio mwenye kauli na haki wengineo wowote hawana haki? “Sheikh, sema kweli japo inauma hii tutaisema wacha

iwaumize. Hiyo ndio kweli ipokeeni na mbadilike. Mh. Aboud Jumbe amewaambieni wapi hamna mazingatio hata kidogo, Jumbe amesema ndani ya kitabu chake The Partner Ship uk. 87 “Mbinu na ushawishi wa hila umekuwa ndio MSINGI wa makusudio na malengo katika utekelezaj wa Chama cha Mapinduzi”. Sasa Jumbe ni Muafrika mwenzenu na kiongozi wenu. Mheshimiwa Mkapa ndio Muafrika na kiongozi mkubwa ambae mlikua mkimtetemekea sana anapokohowa, wote hawa wamesema maneno mazito masikioni mwenu. Mkapa amekwambieni ila mbaya ya Viongozi wa Zanzibar kuwa wao wanachodai zaidi ni madaraka kwa hilo wako tayari kuuwa. Jumbe amewaambieni kwamba CCM inatumia hila katika kuyafikia malengo yao. Kauli hizo sio zangu enyi Waafrika wa Zanzibar, hizo ni kauli za watu wanaoyajua ya ndani na ya mbali sana. Na Nyerere alikuja kumalizia pale alipokwenda Dodoma kuuzima moto wa G55 wa kutaka Serikali 3. Alisema “Nyinyi mnawachukia Wazanzibari kwa sababu ya Uislamu wao, hizo ndio chuki zilizokusukumeni na mkataka kudai Tanganyika ndani ya Muungano”. Najua kweli inauma, kweli haimheshimu mkubwa wala mdogo kweli ni kweli tu. Hebu zipimeni kauli za Viongozi hao watatu wa Kitaifa, Nyerere, Mkapa na Jumbe, je! ni waongo Viongozi hawa katika kauli zao hizo? Kama viongozi wetu ndio hawa hawatambui kabisa, hawa hawawezi kupigania Zanzibar kisawasawa kwa vile hawana dhima na nchi hii, wao walipata madaraka kwa vile walikuwa ni Waafrika ikiwa Mganda au Mkenya au Mtanganyika basi imani zao za kinchi zitasimama katika nchi zao walikotokea wao au wazazi wao Zanzibar ina wenyewe toka hapo asili na wenyewe ndio hao Washirazi, ukipinga hili hebu nipe tafsiri ya A.S.P Tafrisi yake ni Chama Cha Waafrika na Washirazi na ukitaka zaidi soma maelezo haya: Nyerere alikua Unguja siku ya tarehe 1-2-1959 kama mgeni wa Tawi lake aliloliasisi la African Association na hutuba yake ilikua ni hivi:“Sisi ni watu wawili (yaani Mshirazai na Muafrika) tunataka kufyeka pori na pori hilo sharti tuwe na panga na bei ya panga ni shilingi 3. Na sisi ni watu wawili, kila mmoja ana shilingi moja. Je! ile shilingi ya tatu tutaipata wapi? Kama sisi tunataka kufyeka msitu huo tuwe sote mkono mmoja tuungane, tuchange tununue panga, ndipo tutapoweza kuweka safi huu mwitu”. Baada ya jitihada kubwa

Inaendelea Uk. 11

11

AN-NUUR

Ijue Sheria

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012
wanawake watatu, ni sawa na katika baraza la ardhi la Kata kwamba katika watu hao wane na wasiozid watu nane wanawake ni lazima wawe watatu ambao ni lazima wachaguliwe na kamati ya Kata (Ward Committee) kama inavyoonyeshwa katika sheria ya kata, Ward Tribunals, Act 1985. Kwa mujibu wa sheria ya kata, ili mtu aweze kuchaguliwa kufanya kazi katika Baraza la Ardhi la Kata, ni lazima vigezo vyote nilivyokwisha vitaja katika Baraza la Ardhi la Kijiji vizingatiwe. Na atakuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya hapo ataweza kuchaguliwa tena. Majukumu makuu ya Baraza la Ardhi la Kata ni mengi, ikiwemo kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo katika kata kwa kusuluhisha na kusaidia pande zote mbili kufikia katika maamuzi ya busara na muafaka. Vivile Baraza litakuwa na uwezo wa kushuhulikia migogoro inayohusu sheria ya ardhi ya mijini, Land act, No. 4,1999 na sheria ya Ardhi ya Vijijiniyaani village Land Act. No.5,1999. Katika utekelezaji wa haki baraza litazingatia kanuni zote za kimila katika usuluhishi, mbinu zote asilia katika kutenda haki. (Natural justice) pamoja na mbinu nyingine zote kama alivyowahi kufundishwa au kupewa katika mafunzo yoyote yale yanayohusu usuluhishi wa Ardhi. Katika matatizo yote yanayohusu usuluhishi, Baraza litahitajika kuwa na watu watatu akiwemo mwanamke mmoja. Endapo kutakuwa na mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya baraza la kata, basi mtu huyo anaweza kukata rufaa kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (District Land and Housing Tribunal). Na ikumbukwe kwamba rufani hiyo isiwe zaidi ya siku 45 tangu siku ya maamuzi ya baraza la Kata yalipotolewa. Wakati mwingine tutaona muundo wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (District Land and Housing Tribunal), Mahakama kuu kitengo cha Ardhi, High Court (Land Division, hapa kuna mabadiliko kidogo kwani siku hizi mahakama zote kuu zimepewa mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ardhi, na mwisho tutaangalia Mahakama ya Rufani Tanzania katika kusikiliza migogoro ya Ardhi.

Sheria ya Ardhi

Utatuzi wa migogoro ya ardhi
mwaka 1998 Tanzania iliunda Sera ya Ardhi (National Land Policy, 1998). Sera hii inazungumzia mambo mengi ikiwemo haki ya mwanamke katika kumiliki ardhi, haki sawa ya kumiliki ardhi, kuhusiana na haki ya mwekezaji Tanzania pamoja na usuluhishi katika migogoro ya ardhi. Hata hivyo sera hii ilipelekea kupitishwa kwa sheria kuu mbili za ardhi yaani Sheria ya Ardhi ya Mjini, Land Act No. 4 na sheria ya ardhi ya Vijijini yaani Village Land Act, No. 5, zote kwa pamoja zilipitishwa mwaka 1999. Ukilinganisha na hapo nyuma kabla ya sheria hizi, utaona kupitishwa kwa sheria hizi kumeweza kurahisisha utatuzi wa migogoro ya ardhi. Sheria hizi zinafanya kazi kwa pamoja na sheria nyingine kama vile sheria ya usajili wa ardhi, (Land Registration

Na- Kissima Adolf 0713 401812 Email: adolfkissima@yahoo.com

Kweli mnapanda viscudo akina Jecha
Inatoka Uk. 10
Nyerere aliweza kuunganisha makundi mawili ya kikabila lile la Shirazi na Waafrika na hapo ndio ikazaliwa AfroShirazi Part. Karume alikuwa Afroshirazi Bara na Viongozi wengine wenye asili za Bara na Viongozi wengine walikuwa Afro-Shirazi Zanzibar. Baada tu ya Mapinduzi Karume alipiga marufuku na kuwataka wale wote wanaojiita Washirazi wakafute yaani (wakane) kujiita Washirazi na wajiandikishe kama kabila ni” Mwafrika” . Ndio hili zogo la kundi hili ambalo hujinasibisha na Uafrika ili kuwazima wale wenyeji ambao Nyerere alikuja Unguja kwamba waungane, kumbe walikuwa na siri juu ya jambo hilo. Ndio kusema Viongozi hasa wenye asili mchanganyiko hawana haki zaidi ya hawa wanaojitia Uafrika lakini hawazijuwi kabila zao. Hawa ndio wanaojiona ni wao tu waliopindua. Mzee Hassan Nassor Moyo anasema: “ Wa k a t i t u n a t a y a r i s h a mambo yetu (Mapinduzi) tulikuwa na Uhusiano kati yetu A.S.P na Umma Party na hili huwezi kulikataa, sasa baada ya Mapinduzi tukawachukua

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya juhudi kubwa katika kuhakikisha usimamizi na umiliki wa ardhi ni wa haki kwa kila Mtanzania. Utakumbuka

baadhi ya wanachama wa Umma Party kama Babu na Khamis Abdalla Amri wakawa ndani ya Baraza la Mapinduzi la mwanzo ili kudumisha ule uhusiano”. Kauli za viongozi, mfano Mzee Moyo anasema tuache siasa chafu, kama kuna Watanzania wameanza kuingiza element za Uarabu na Ukabila wapumbavu, wapuuzi kabisa, tena wanaosema hivyo ni watu wasokua na hoja wanatafuta kuchimba upuuzi ili wazushe. Tunaelewa Tanzania ina mchanganyiko wa makabila mengi na rangi mbali mbali kwa hivyo huwezi ukataka wewe utumie turufu ya Uafrika kati ya raia wengine mchanganyiko tena ni Waafrika vile vile isipokuwa asili zao ni tofauti. Sasa ni wakati muwafaka wa kutetea nchi yetu ijipatie mafanikio ya kiuchumi na kisiasa tuwache siasa za Uafrika na Uarabu au lugha ya “sisi Muungano tunaujua sana kuliko wao” haitusaidii kitu. Jaribu kuijua sana Zanzibar na kukielewa nini ilichokipoteza nchi yetu, vipi tuisaidie ili vitoto na vijukuu vyetu vipate kurithi hatma ya nchi yenye kila maendeleo.

Act, Cap 334), sheria ya usuluhishi migogoro ya Ardhi, The courts (Land Dispute Settlements) Act ,2002, sheria ya mipango mji, na nyinginezo. Sheria hizi kwa pamoja zimeweza kusimamia Ardhi pamoja na usuluhishi wa migogoro ya Ardhi. Hata hivyo pamoja na uwepo wa sheria zote hizi, bado kumekuwepo na ongezeko la migogoro ya ardhi siku kwa siku. Utakubaliana nami tu endapo utakuwa na utaratibu wa kutembelea mabaraza ya ardhi au mahakama kitengo cha ardhi. Leo tutaangalia katika sheria hizi ni vyombo vipi vimeundwa kwa mujibu wa sheria katika kutatua migogoro ya ardhi. Vyombo hivi vimeainishwa katika shera ya ardhi, Land Act No.4 pamoja na Sheria ya usuluhisho wa migogoro ya ardhi, The Courts (Land Disputes Settlements)Act, 2002. Vyombo hivyo ni kama, Baraza la Ardhi la Kijiji, (The Village Land Council) Baraza la Ardhi la Kata, (The Ward Tribunal) Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (The District Land and Housing Tribunal), Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, The High Court( Land Division) na Mahakama ya Rufani Tanzania. Baraza la Ardhi la Kijiji: Baraza hili linakuwepo kila katika kijiji. Ili maamuzi ya Baraza hili yatambulike kisheria, ni lazima muundo wa baraza hili likidhi matakwa ya sheria. Sheria inasema baraza hili muundo wake ni lazima liwe na watu saba, na katika watu saba hao ni lazima wanawake wawe watatu. Endapo idadi ya watu katika baraza hilo hawajafika idadi niliyoitaja hapo au wanawake watatu hawajajumlishwa katika idadi hiyo, basi kisheria baraza hilo ni batili pamoja na maamuzi yake. Watu wote hao ni lazima wapitishwe na Halimashauri ya kijji na kufanyiwa uhakiki na kikao cha kijiji. Tuangalie ni vigezo gani mtu atastahili kuwa navyo

ili aweze kupitishwa na Halimashauri ya Kijiji na baadaye apitishwe kwenye kikao cha kijiji. Ni lazima mtu huyo awe mkazi kijiji husika, mtu huyo awe mwanachama katika kikao kikuu (National Asembly), mtu huyu asiwe ni Hakimu mwenye mamlaka katika wilaya ambayo baraza la kijiji linafanya kazi. Vilevile mtu huyo ni lazima awe mtu mzima, mtu mzima katika sheria hizi ni mtu yoyote Yule mwenye miaka zaidi ya kumi nane., awe na akili timamu, ikumbukwe kuna wale watu ambao huwa na matatizo ya akili ya muda (temporary insane) watu wa aina hii vivile hawatakuwa na nafasi katika Baraza la Ardhi la Kijiji. Mtu huyo ni lazima awe raia wa Tanzania, utakumbuka awali nilizungumzia kuwa ni lazima msuluhuhishi huyo awe mkazi wa kijiji, bado sheria inasema mtu huyo awe raia wa Tanzania. Mwisho kama kawaida mtu huyo asiwe ametenda au kuhukumiwa katika makosa ya jinai. Kwa mujibu wa sheria Baraza la Ardhi la Kijiji, litakuwa na majukumu mbalimbali kama vile, kupokea malalamiko mbalimbali yanayohusiana na ardhi. Kuandaa mikutano kwa ajili ya kusikiliza migoro ya ardhi toka pande zote mbili, yaani mlalamikaji na mlalamikiwa. Vilevile Baraza litakuwa na wajibu wa kusuluhisha pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha pande zote kwa pamoja wanafikia makubaliano kwa pamoja bila kinyongo. (mutual agreement). Baraza la Ardhi la Kata ( T h e Wa rd Tr i b u n a l ) : Ndugu msomaji, sheria ipo wazi, endapo mtu yoyote aliyepeleka shauri lake katika Baraza la Ardhi la Kijiji lakini bado hajakubaliana au bado hajaridhika na maamuzi yaliyoyolewa na baraza hilo, basi mtu huyo anaweza kupeleka malalamiko yake katika ngazi ya kata, yaani kwenye Baraza la Ardhi la Kata (The Ward Tribunal). Mabaraza ya kata yameanzishwa kwa mujibu na taratibu zilizomo kwenye sheria za kata yaani (Ward Tribunals Act, 1985). Kila baraza la Kata litakuwa na watu wasiopungua wane na wasiozidi watu nane. Kama tulivyokwisha ona katika baraza la ardhi la kijiji kwamba ni lazima kuwepo na

12

AN-NUUR

Barua/Mashairi

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

Naanza kumhimidi, Mola wangu Subhana Yu pweke tena wahidi, aso mke wala mwana Mwenye aali weledi, kwa ghaibu na bayana UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Insani hatuna budi, kutafakari kwa kina Kwa kila letu kusudi, la siri na la bayana La kinywa na la fuadi, si kunga kwa SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Uongozi njema sudi, kwa anolenga ‘ubwana’ Hukazana kwa juhudi, kukwepa nongo utwana Lengole ni kufaidi, si dhima kwa SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Jambole kulisanidi, vyovyote atang’ang’ana Kwa uvumba au udi, ili liweze kufana Hata kama kwa kutadi, mipaka ya SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Ahadi ataahidi,lukuki tena mwanana Keshoye huzikaidi, na nyingine huzikana Kuulizwa hana budi, na Allahu SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Kitini hanayo budi, hugeuka kuwa ‘bwana’ Husimika yake jadi, ya asili huikana Kwa kujitenga baidi, na mila ya SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Hujali wake mradi, wa juzi, leo na jana Japo ni wa kifisadi, huhisi wa kiungwana Kwa ya kwake itikadi, u mwema kwa SUBHANA UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Nane si lengo kuzidi, zatosha kukumbushana Si tunu ya ufisadi, uongozi ni dhamana Kaditamati idadi, INSHALLAH tutaonana UONGOZI ni DHAMANA, si TUNU ya UFISADI. Abuu Nyamkmogi Mwanza

UONGOZI NI DHAMANA

Ndugu Mhariri,

Kujua idadi yetu ni muhimu. Tutajuaje?
kuchukua sensa, ama taasisi ambazo zimejipanga. Inaweza saidia kupata takwimu sahihi kwa kila msikiti na Taifa kwa ujumla. Wasiwasi wangu ni mwitikio wa hilo pia. Je, mpango huo utasimamiwa na nani katika wilaya, mkoa na taifa? Hii ni changamoto nyingine inayotukabili. Tatizo jingine lipo. Msikiti ninaoswali mimi, uko mjini na waumini unatarajia kuwa watakuwa ni waelewa. Tulianzisha na kufanya zoezi hili la sensa kutaka kujua idadi ya waumini wa msikiti

Assalaam alaikum Nina hakika, wito wa kuisusia sensa, hautapata mwitikio mkubwa kwa kuwa ujumbe huu hauwezi kumfikia kila Muislamu wa nchi hii. Watakaopata taarifa hizi ni wale wa mijini na wenye kupata na kutumia huduma ya internet kama sisi. Pia elimu ya kinachokusudiwa, bado haijafika kwa walengwa. Ni sahihi kuitumia misikiti

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie: Mhariri AN-NUUR, S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk

wetu na kupata picha halisi ya hali zao kiujumla. Wa Allaah, baadhi ya waumini hawakutoa taarifa zinazotakiwa na hawakuonesha hata chembe ya ushirikiano katika zoezi hili. Ni watu ambao tunaswali nao jamaa mara kwa mara, lakini inakuwa kana kwamba hawatuamini. Hii ni changamoto nyingine inayoweza kujitokeza. Ni muhimu kujitokeza katika zoezi hili la kitaifa, ila pana haja ya sisi pia kujipanga kujua idadi yetu wenyewe. In any case, hata kama watasema tuko 51%, sawa tutaridhika kuwa tuko wengi, lakini ni kweli ndio takwimu halisi? What if tuko 62%... Abu Aasim T. Ally Dar es Salaam

TAKWIMU YA SENSA (JIBU)
Nimesikia sauti, yenye swali la malenga, Mwororo na madhubuti, lengole kitaka mwanga, Si kuleta varangati, au mambo kubananga, Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Swalilo kaka ni nyeti, linohoji ile kunga, Iungayo katikati, viwili vile viunga, Cha ule mji wa kati, na wa’baba’ wakupanga Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Tangu kale hata kati, mamboyo wote hupanga, La baba huwa ni nyeti, hata kama la kijinga, Kwa kukiuka shuruti, la sensa wameboronga Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Takwimu za hatihati, za urongo na kutunga, Zilorushwa kwa umati, kwa TBC kutinga, Kwa ukosa ithibati, hata mimi nazipinga, Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Jambo kama hili nyeti, mwathubutu kulilonga, Pasi hata ithibati, iwe kwenu kesho kinga, Chombo cha taifa eti, sendelee kutuvunga, Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Vinginevyo ithibati, kitoe kwa kilolonga, Kwa kupotosha umati, kwa wa babaye ushenga, Kama la mkakati, kwa pamoja walipanga, Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Mshana ni chako kiti, ukimya utakufunga, ‘Tawajibishwakwa korti, wa timuyo ushenga, Twaingoja yako hati, ya radhi au kupinga, Ni TAKWIMU za KUPANGA, zisizo na ITHIBATI. Dhimayo si usaliti, ya taifa kuyaunga, Si kuuawa umati, kwa takwimu za kutunga, Sensa ‘dataze’ ni nyeti,

Akaa! Mbona Nikabu mwaitia aibu?
Ndugu Mhariri DUNIA mtego wa panya, ukiichezea itakunasa. Usemi wa hekma, tuliourithi kwa wahenga. Unatuasa, unatuonya dhidi ya maovu. Juu ya yote wazee kwa vijana wa leo wamelewa chakari anasa wanasema huo ndio usasa. Mimi najiruzuku kutumia kalamu kuwapiga msasa. Tu n a p o s e m a d u n i a inaghururi maana yake nini? Swadakta. Neno limepata mnenaye. Ghururi kwa maoni yangu ni kudanganyiika na maisha haya mafupi. Maisha ya kitendawili lakini bado watu hawatumii akili wala kufikiri. Wako hukufuru lakini mwisho wao hauwi mwema. Hutangatanga na njia, hujililia na kujijutia. Waswahili wanasema, kabla hujafa hujaumbika. Echo! Funika kombe wee mwana… apite. Inasikitisha, inakihirisha, baadhi ya wasichana wa Kizanzibari waungwana kuwaona kwenye kumbi za starehe au sehemu za mapumziko mfano Jamhuri garden, Victoria na Forodhani na nikabu zao wamepakatana na mabwana. Heee! Poo! Hawaachi, hiyo ni laana inayomuudhi Subhanna. Utafiti unaonyesha wengine huitumia nikabu kujifichia maovu. Mfano kwa lugha ya sasa kule tunachokiita kupiga virungu Kiswahili sanifu ombaomba, wengine hutumia kwa wizi, uzinzi hata ujambazi. Juzi juzi hapa kwetu Zanzibar alikamatwa melini mwanamke aliyemuiba mtoto hospitali ya Mnazi Mmoja. Tena alivaa nikabu. Nikabu si vazi baya, lakini wale wanaolitum ia vibaya wanalipaka matope. Matokeo yake wanawake wema na wacha Mungu hupewa jina la kebehi la Ninja kwa kule tu kuvaa nikabu kwao na hawajaufanya uninja wanapita tu na zao. Wengi husingizia mabalaa kemekem. Zanzibar kuanza

kuibwa watoto ni jambo la kuhuzunisha, kusikitisha tena la kutisha mwenye machozi ya karibu haki yake kulia. Janga hilo ni letu sote tutalitatuwaje? Qur’an tukufu suratul Luqman 31 aya ya 16 inatufunza jambo muhimu sana pale Luqman alipomuusia mwanawe: “Ewe mwanangu kwa hakika jambo lolote utakalolifanya japokuwa na uzito wa chembe ya hardali (ikiwa imejificha ndani ya mwamba) mbinguni au ardhini Mwenyezi Mungu (atalifichua atalidhihirisha) bila shaka Mungu ni mjuzi na mwenye habari”. Binadamu tunaweza tusimjue mfanya maovu wa kujificha lakini kwa mujibu wa Qur ’an Mwenyezi Mungu ni mweledi wa yote tuyatendayo ya siri au dhahiri na tutalipwa. Ndugu zangu katika imani, tutubie makosa yetu na tusiyarejee tena. Tuzirejeshe nafsi zetu kwake katika hali ya wenye kuridhika ili tupate yale tuliyoahidiwa peponi. Mzee Hassan Mkwende Hassan

13

AN-NUUR

Makala/Shairi/Barua

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

Vigogo CCM msiwakasirikie wakosoaji
Zifanyieni kazi changamoto mkinusuru chama
Na Shaaban Rajab WA K AT I C h a m a c h a Mapinduzi kikiendelea kuporomoka na kupoteza mvuto kwa umma, baadhi ya watendaji wake wa ngazi za juu wanazidi kupinga na kuendelea kuwapa watu moyo kwamba chama bado ni imara na hakijaathirika kama inavyofikiriwa. Kutokana na hali kutokuwa shwari ndani ya chama, imefikia hata baadhi ya makada wakongwe na wazoefu wa chama hicho kukosoa hadharani na kutoa tahadhari kuhusu muelekeo na mustakabi wa chama siku zijazo. Lakini kutoa kwao tahadhari na kubainisha udhaifu na hitilafu za kimaadili na kiuongozi unaokimaliza chama, wanaonekana kama waasi na wasiokitakia mema chama. Mzee Joseph Butiku, Dkt. Hassy Kitine, Edward Lowassa, Peter Kisumo, Mzee Yusuf Makamba ni baadhi ya makada wakongwe ambao wamekuwa wakitoa tahadhari za mara kwa mara juu ya mwelekeo wa chama. Hata hivyo kauli zao zimekuwa zikifanyiwa mzaha na kebehi na baadhi ya viongozi wa CCM walioko madarakani kwa sasa. Mara nyingi wamekuwa wakibezwa na changamoto zao kupuuzwa pale wanapozitoa. Badala ya kauli za ukosoaji zinazotolewa na wakongwe hao katika chama kuchukuliwa kama changamoto na kufanyiwa kazi, watendaji, hasa wa ngazi za juu wa chama wamekuwa wakiona ukosoaji huo kama ‘mapigo’ dhidi yao. Kutokana na kuwepo dhana hiyo, wakati mwingine wenye dhamana hulazimika kutoa kauli za kupuuzia hoja za wakosoaji hao na kuwapa matumaini wana CCM kwamba, bado chama kipo imara na hakuna haja ya kuwa na hofu. Ukiacha hoja za ukosoaji zinazotolewa na kina Butiku na Kitine, ambazo zinalenga zaidi matatizo ya kimaadili katika chama, Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, amekuwa miongoni mwa wana CCM nguli ambao hawaridhishwi na mwenendo wa chama na serikali kwa ujumla. Hasa ikizingatiwa kwamba Arusha, ambako akisema “Adui akiendelea kukutukana maana yake unaendelea vizuri, maana akikusifia ujue unaelekea kufa, watu wote wenye akili hawajatulaumu”. “Ukiona fisi anachekelea wakati simba anawinda ni kwa sababu tu anasubiri mzoga”. (Bila shaka akiwananga wapinzani) “Ukijichoma mwiba mwili unakuwa na shida lakini hauwezi kusikia akili ikipiga kelele isipokuwa inakuelekeza tu jinsi ya kuondoa mwiba na katika kuuondoa, huwezi kukata mkono au mguu unachofanya ni kuondoa mwiba tu mwili unabaki salama”. Huwezi kuona Simba amelala amejipumzisha Fisi wakachelekea, mafisi wanachekelea tu pale wanapoona Simba anawinda, maana wanasubiri mzoga. “Hao mafisi walipiga kelele fukuza, sijui fanya nini… chama makini hakiendeshi shughuli zake hivyo, kuna njia, lazima ubuni na kutengeneza njia na mfumo wa kushughulikia mambo kwa utaratibu na kuondoa matatizo kwa mfumo husika. “Sasa mambo mengine mnayaweka katika system (mfumo) wenye taratibu za kumaliza matatizo kama hayo, ukijichoma mwiba mwili unakuwa na shida lakini hauwezi kusikia akili ikipiga kelele isipokuwa inakuelekeza tu jinsi ya kuondoa mwiba na katika kuuondoa, huwezi kukata mkono au mguu unachofanya ni kuondoa mwiba tu mwili unabaki salama. Nina maana kwamba chama chetu bado kiko imara licha ya mawingu yaliyopita na watu kufikiri tu kwamba tutafukuzana hovyo. (Kipindi cha shinikizo la kuvuana magamba). Mukama anadhihirisha kwamba chama bado imara na anasema ushahidi upo. Amesema kuwa yeyote aliyeona mkutano wa maadhimisho ya miaka 35 ya CCM kule Mwanza atakuwa mtu wa ajabu kutokiri kuwa chama chake bado ni imara. Anadai watu waliokuwa nje walioshindwa kuingia ndani walikuwa wengi kupita kiasi. “Yeyote anayedai kuwa chama hiki hakina mvuto unamjibu tu kama Mwalimu

Mh. Edward Lowassa. ndiko anakotoka Lowassa, ndiko kunakoadhirika zaidi na mmomonyoko wa chama. Hivi karibuni Bw. Lowassa akihutubia mkutano wa hadhara huko Mto wa Mbu, Arusha alisema kuwa CCM kinakabiliwa na tatizo la kiutendaji na uongozi. Kauli ambayo mara moja ilijibiwa na Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama, ambaye alionyesha kukerwa na changamoto aliyoitoa Lowassa. Mukama alijibu mapigo akisema kuwa haikuwa sahihi kwa Bw. Lowassa kutoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara, akimaanisha kwamba anajua utaratibu wa chama wa kutoa kauli kama hiyo. Katibu huyo aliongeza kuwa Bw. Lowassa alipaswa kuzungumzia shida zilizopo jimboni mwake zikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya wawekezaji na wananchi, wakulima na wafugaji kuliko kukishambulia chama chake. Hata hivyo, Mukama naye hakuonekana kusubiri utaratibu wa chama kujibu mapigo kwa Lowassa. Siku chache baadae, katika mkutano wa Halmashauri ya CCM (NEC) uliofanyika D odoma, K atibu M kuu mstaafu wa CCM, Yusuf Rajab Makamba, alinukuliwa kutoa changamoto zake dhidi ya watendaji wa CCM. Makamba aliegemea zaidi kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akidaiwa kusema kwamba amekifanya chama kama mali yake binafsi huku akitizamwa tu. Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la chama hicho, Peter Kisumo, naye alitoa kali zaidi pale aliponukuliwa akisema kuwa Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, ameonyesha utendaji mbovu tangu alipoteuliwa na Mweyekiti Jakaya Kikwete kushika wadhifa huo. Mukama ametuhumiwa kutumia muda mwingi kutoa misamiati isiyokuwa na tija kwa CCM. Bila shaka baadhi ya misamiati ya Mukama ni kama ifuatayo: Alinukuliwa

(Nyerere) alivyomjibu mwandishi wa habari aliyemuuliza swali kwamba; “Wewe umevunja sheria ya kimataifa kwa kumwondoa Head of the State Iddi Amin aliyetushambulia kule Kagera.” Alimnukuu Mwalimu Nyerere akimjibu mwandishi huyo wa habari, “Watu wenye akili hawajatulaumu.” Kumng’oa Idd Amin”. Mukama anasema yeyote ambaye anauliza swali la kijinga kwamba CCM… eti CCM imekosa mvuto…, akimsikia kiongozi wa chama fulani akisema hivyo yeye anasema kuwa CCM ikikosa mvuto, basi huyo atakuwa alishavunda na kutupwa kabisa. Chama bado kina mvuto. (Nukuu na Raia Mwema). Misamiati ya namna hii ndio iliyomkera Kisumo, kwa kuwa ni ya kinadharia zaidi kuliko vitendo. Inakumbukwa kwamba siku chache zilizopita, baada ya ripoti ya ukaguzi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujadiliwa Bungeni na kufuatiwa na mapendekezo ya Kamati tatu za kudumu za Bunge, ile ya Hesabu za Serikali, ya Mashirika ya Umma na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilson Mkama, alikosoa utaratibu uliotumika wa kuwatuhumu watuhumiwa na kutoa mapendekezo yake. Aprili 4, Mukama alionyesha kutokukubaliana juu ya kile alichokiona kuwa ni tabia za viongozi wa Kamati za Bunge kudharau kanuni za Bunge kwa kuhukumu masuala bila kufuata utaratibu. Alisema baadhi wanajulikana kwa kujichukulia madaraka na kuweka wazi mambo hadharani kwa kudokeza masuala waliyoyajadili na watu na taasisi badala ya kuwasilisha ofisini kwa spika kwanza kwa ajili kuchukuliwa hatua zinazostahili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mukama alishauri kwamba kamati hizo wanalikwamisha bunge kwa kumwaga ripoti walizozijadili katika mikutano yao kwa vyombo vya habari, hivyo kuuacha umma ukiwa umechanganyikiwa. Alisema utaratibu unataka kamati hizo kwanza kuwasilisha ripoti kwa spika Inaendelea Uk. 14

14

AN-NUUR

Makala

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012
lakini haaminiki kwa Yahudi au Mkristo. Swali ni je, Waislamu wameielewa Al Maida: 51 kama walivyoielewa Makamanda hawa wa jeshi la Marekani? Pamoja na yote wanayofanya, yakiwemo haya ya vita na mauwaji Iraq, Afghanistan, Libya, Yemen, Somalia, Pakistan, Palestina, Lebanon na hii vita dhidi ya ugaidi; lakini makamanda

Inatoka Uk. 9 ambaye haamini kuwa Qur’an ni kitabu cha Allah? Kuna Msoma Maulid ambaye ana Kitabu chake zaidi ya hii Qur’an yenye Juzuu 30? La kujitambua hapa kama alivyohimiza Khatib pale Masjid Magomeni Kichangani ni kuwa, sisi sote mbele ya Kafiri, ni hali moja. Tunatizamwa kama maadui. Hata kama kuna mmoja wetu iwe Bakwata, Sheikh binafsi au taasisi yoyote, ataona anapendwa (na serikali au adui wa Uislamu), ajue anatumiwa tu kwa muda kuwaangamiza wenzake, kisha itafuata zamu yake. Katika makala yao “U.S. Military Taught Officers: Use ‘Hiroshima’ Tactics for ‘Total War’ on Islam” (May 10, 2012), waandishi na wachambuzi Noah Shachtman na mwenzake Spencer Ackerman, wanafichua kuwa katika kukamilisha inayoitwa vita dhidi ya ugaidi (Waislamu), maofisa wa kijeshi wa Marekani wametakiwa kuangalia uwezekano wa kuwaangamiza Waislamu wapatao bilioni 1.4 kwa kuipiga bomu la nyukilia Makkah na Madinah kama ilivyokuwa Hiroshima na Nagasaki. “The U.S. military taught its future leaders that a “total war” against the world’s 1.4 billion Muslims would be necessary to protect America from Islamic terrorists”.

Waislamu wapo kama hawapo
Hivyo ndivyo wanavyosema mabawana hao wakinukuu baadhi ya makala na vitini vilivyokuwa vikitumika katika mafunzo ya maofisa wa kijeshi Chuo cha Maofisa wa Jeshi, Defense Department’s Joint Forces S t a ff C o l l e g e , N o r f o l k , Virginia. Akitoa mafunzo hayo kwa maofisa wa ngazi za juu wa jeshi (Makapteni, maLuteni Kanali na Makanali n.k), mtoa mada Luteni Kanali (Army Lt. Col.) Matthew A. Dooley, amesema kuwa, adui hasa wa Marekani na Ulaya sio Al’Qaida bali Uislamu wenyewe. “We have now come to understand that there is no such thing as ‘moderate Islam. It is therefore time for the United States to make our true intentions clear. This barbaric ideology will no longer be tolerated. Islam must change or we will facilitate its selfdestruction.” Anasema Luteni Kanali Dooley akiwapiga msasa makamanda hao akimaanisha kuwa hakuna kitu kinaitwa “Uislamu Poa”, kwa hiyo kilichopo ni kuuangamiza Uislamu wote (au Waislamu waubadili kwa kutupa aya nyingine). Ni baada ya kuyasema hayo, Dooley akahitimisha kwa kusema kuwa, uangaliwe uwezekano wa kuipiga Makkah na Madinah kwa mabomu ya nyukilia mithili ya yale yaliyovurumishwa Hiroshima na Nagasaki. Mhadhiri mwingine John Guandolo (FBI) katika mada yake ,“Usual Responses from the Enemy When Presented With the Truth” alieleza kuwa ni katika mafundisho ya Qur’an na Sunnah, Waislamu kuwafanya Mayahudi na Wakristo maadui. Katika kufafanua nukta hiyo ilisomwa na kufafanuliwa Aya ya 51 ya Sura ya 5 (Surat Almaida). Sura hiyo inasema, “Enyi Mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa marafiki (wa kuwapa siri zenu); wao kwa wao ni marafiki. Na miongoni mwenu atakayefanya urafiki huo nao, basi huyo atakuwa pamoja nao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi (njia ya kheri) watu madhalimu.” (Al Maida: 51) Ni baada ya kuichambua aya hii, maofisa hao wa kijeshi wa Marekani wanasema kuwa hoja hapa sio Al Qaidah, Osama (au Al Shabab, Siasa Kali, Bakwata au Salafi), bali tatizo ni Uislamu wenyewe. Makamanda hao wa jeshi walipitia pia na kuchambua Hadithi mbili katika Bukhar. Hadithi hizo zinasema: Wamepokea Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) kutoka kwa Abuhurairah (r.a) amesema: kwamba Mtume ( s.a.w) amesema: “Hakitasimama Kiama mpaka wapigane Waislamu na Mayahudi, mpaka litasema jiwe nyuma yake kuna Yahudi ‘Ewe Muislamu huyu Myahudi yupo nyuma yangu njoo umuue.” “Na katika mapokezi ya Muslim, ”Hakitasimama Kiama mpaka Waislamu wawapige Mayahudi, mpaka atajificha Myahudi nyuma ya jiwe au mti: (na mti au jiwe hilo litasema), ewe Muislamu, ewe mja wa Mwenyezi Mungu, huyu hapa Yahudi nyuma yangu njoo umuue, isipokuwa mti wa Gharqad, kwani ni mti wa Mayahudi.” Kwa kuzipitia Aya na Hadithi kama hizi, wasio Waislamu kwa maana ya M a y a h u d i n a Wa k r i s t o muda wote huwachukulia Waislamu kuwa ni maadui. Hawawaamini na muda wote hupanga mipango ya kujihami nao hata kama hawaonekani kufanya lolote. Maadhali hajaritadi, Muislamu, hata awe asi na wa hovyo atakavyokuwa,

Vigogo CCM msiwakasirikie wakosoaji
hizo ni kufanya mabadiliko ya Mawaziri kufuatia tuhuma za rushwa na uwajibikaji zilizokuwa zikiwakabili kufuatia uthibitisho wa ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, ambapo wengi waliopendekezwa na kamati hizo kuondolewa waliondolewa. Kwa jinsi CCM inavyomong’onyoka kwa kukosekana uadilifu miongoni mwa watu waliopewa dhamana ndani ya chama na serikali, haidhaniwi kwamba ulikuwa muda mwafaka kwa Kwa katibu Mkuu wa Chama kuja na hoja za kuwahurumia wasiokuwa waadilifu kipindi hiki, hususan wakati huu ambapo kumekithiri wizi, ubadhirifu, ufisadi na ulevi wa madaraka, hali ambayo inampa taabu Rais Kikwete kutimiza azma zake kama alivyokusudia. Pamoja na jitihada zinazofanyika za kuwapa moyo wana CCM juu ya hali ya chama, mwenendo halisi wa ustawi wa chama si mzuri kama inavyodaiwa. Karibu kila chaguzi ndogo iliyofanyika, CCM kimekuwa kikizidi kupukutisha viti ilivyokuwa ikivishikilia. Si vya ubunge au Udiwani. Kuanzia kule Songea, Mwanza, Msambweni Tanga, Arumeru Mashariki na kwingineko, ni ushahidi wa kimantiki kwamba hali si nzuri. Achilia mbali kushindwa kutetea viti hivyo ilivyokuwa navyo awali, siku za hivi karibuni makanda, viongozi na wanachama wengi wa CCM wamejitoa kwenye chama, hususan vijana. Kasi imeongezeka baada ya kuondoka Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, James Ole Millya. Pamoja na kuwepo shida hizo, bado mdudu wa makundi angali anapekenya ndani ya boma la chama, tatizo ambalo bado uongozi haujalipatia

Ukichukua walivyo Waislamu hivi leo, nani mbuni katika katuni hii?

wa kupambana na Uislamu wanaona hawajafanya kitu. Tizama katuni ambayo hutumiwa katika mafunzo yao. Wanasema kuwa wakati Uislamu unahimiza kuangamiza ukafiri ili Waislamu watawale dunia, Wakristo na Mayahudi walio wengi wanakuwa kama mbuni. Wanaficha vichwa vyao mchangani wakidhani kuwa adui ( Wa i s l a m u ) h a w a o n i . Kumbe adui anapanga kuwavamia na kukata shingo na miguu yao. Labda tujiulize tena, hivi wanaojifanya na kujidanganya kuwa hakuna adui na hawafanyi lolote kujihami, ni Waislamu au Mayahudi na Wakristo ?

Inatoka Uk. 13 wa Bunge, ambaye baadae ataamua kuziweka mbele ya Bunge kwa ajili ya kujadiliwa au kuchukuliwa hatua, jambo ambalo alidai kuwa mara nyingi hazifanyiki. Alisema Kamati hizo zimekuwa zikitoa ripoti zake kwa vyombo vya habari, jambo ambalo sio haki kabisa. Alizitaka kamati hizo kufuata misingi ya haki kwa kuwapa watu wanaowatuhumu nafasi ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa. Kwamba kamati hizo zimekuwa zikiweka wazi kila jambo hadharani kabla ya kuzipa mamlaka husika au watu wanaohusika muda wa kuelezea masuala wanayohusishwa nayo. Hata hivyo pamoja na ukosoaji huo wa Mukama, bado serikali iliona kuna haja na mantiki ya kuendelea kufanyia kazi sehemu kubwa ya mapendekezo ya Kamati na kuchukua hatua. Moja ya hatua

BW. Yusuf Makamba ufumbuzi wa uhakika na kukosoa waziwazi utendaji wa kudumu. Zimeonekana wa chama. Kwa jinsi hali ilivyo kwa lawama na kushutumiana baada ya mgombea wa chama sasa, si jambo la busara kuwapuuza au kuwakasirikia kuanguka huko Arusha. M a z i n g i r a h a y a wakosoaji. Jambo la n d a n i y a c h a m a n d i y o msingi ni kushauriana nao yanayowasukuma makada kuzishughulikia changamoto wakongwe na maveterani wanazozitoa ili kunusuru wa chama kupata ujasiri wa hali.

15

AN-NUUR

Habari

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18-24, 2012

Wazazi watoa onyo kwa mwalimu
Ni yule aliyetumia hijabu kufutia ubao
wa wanafunzi alipotoka darasani kufuatilia ufutio huo ofisini, huku nyuma mwalimu huyo aliwavua wanafunzi watatu hijabu zao na kuanza kufutia ubao huku akiwaamuru wengine kuzivua na kuzitundika katika madirisha ya darasa hilo. “Mwalimu aliwavua hijabu wenzetu watatu, akaanza kuzifutia ubaoni kwani ufutio wenyewe aliondoka nao jana yake. Baada ya hapo aliamuru wote tuvue hijabu zetu na tuzitundike madirishani.” Alisema mwanafunzi mmoja. Kwa upande wake, Amiri wa Kamati ya Kuendeleza Uislamu wilayani humo Na Bakari Mwakangwale WAZAZI wa Kiislamu katika Kijiji cha Matogoro, Wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, wametoa onyo kwa mwalimu Venant Chingwile, wa shule ya msingi Amani kufuatia kitendo chake cha kuwavua mabinti wa Kiislamu hijabu zao kisha kuzifutia ubao. Mwalimu huyo amefanya kitendo hicho kwa wanafunzi wapatao 28 wa Kiislamu wa darasa la sita shuleni hapo, baada ya kukosa ufutio wa ubao (duster) darasani humo. Baada ya taarifa hizo kuwafikia wazazi, waliamua kwenda shuleni hapo na kuonana na mwalimu Mkuu wa shule hiyo, wakitaka kujua sababu zilizosababisha mwalimu Chingwile, kuwadhalilisha mabinti wao na imani yao kwa ujumla. Taarifa zinaeleza kuwa katika kikao kisichokuwa rasmi, mwalimu huyo alikiri kufanya kitendo hicho na kuwataka radhi wazazi hao, huku Mkuu wa Shule hiyo naye akiwasihi wazazi hao kumsamehe mtumishi wake. Akiongea kwa njia ya simu kwa niaba ya wenzake, mmoja wa wazazi hao kutoka Tandahimba ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa wasingependa kuona tukio hilo linajirudia tena shuleni hapo. Mzazi huyo alisema kwamba kwa kuwa tukio hilo si mara ya kwanza kutokea shuleni hapo, alitoa onyo kwamba sasa hawatakuwa tayari kuvumilia au kutafuta uongozi kuzungumzia kadhia kama hiyo na kwamba, watakachofanya ni kushughulika na mwalimu atakayethubutu kurejea unyanyasaji huo kulingana na uzito wa tukio husika. Baadhi ya wanafunzi hao (majina tunayahifadhi) walidai kuwa mwalimu Chingwile, aliingia darasani kwa lengo la kufundisha na alipoingia aliulizia ufutio wa ubao ambapo wanafunzi walimjibu kuwa aliondoka nao baada ya kumaliza kufundisha kipindi kilichopita. Wamedai kuwa mmoja Ustadhi Ramadhani Mtoe, akielezea tukio hilo na hatua walizochukua alisema wameunda kamati ya watu watatu kufuatilia kadhia hiyo. Alisema kabla ya wazazi hao kwenda shuleni hapo, wao walishafika shuleni hapo kama kamati kutoka Masjidi Al-Aqswa, wakiwakilisha waumini wa Msikiti huo waliochukizwa na kitendo cha Mwalimu huyo kulidhalilisha vazi la Kiislamu na mabinti wa Kiislamu. “Tulifika pale kuonana na Mkuu wa shule tukiwa kamati ya watu watatu kutoka Masjid Al-Aqswa. Tulikuwa mimi (Amir Mtoe), Ust. Jamalidin Juma pamoja na Ust. Umar.” Alisema. Alisema baada ya kuonana na mkuu wa shule, aliwataka radhi Waislamu na kuahidi kukutana na walimu wote kulizungumzia suala hilo. Hata hivyo kamati hiyo ilimtaka mkuu huyo wa shule, kumuamuru mwalimu mkosaji kuomba radhi kwa maandishi, jambo ambalo kamati hiyo ilidai kuwa Mkuu huyo alisema kuwa ataandika na kuomba radhi kwa niaba ya mwalimu huyo baada ya majumuisho ya kikao cha kumjadili mwalimu Chingwile, kisha ataikabidhi kwa Waislamu na wazazi. “Baada ya kumtaka mwalimu Chingwile, aombe radhi kwa maandishi, Mkuu

Polisi Unguja wadaiwa kulinda wahalifu
Inatoka Uk. 16 alisema kwa uchungu na masikitiko Bi Salama. Inadaiwa kuwa thamani ya vitu vilivyopotea siku hiyo ya tukio ni pesa tasilim laki 2, simu za mkononi mbili moja ya shilingi elfu 50 na moja ya shilingi elfu 30, vyombo, nguo na nyumba ambayo gharama zake hazijajulikana. Mwandishi hakuweza kumpata mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Haji ili kujua kulikoni juu ya shutuma hizo lakini hakupatikana na kuamua kwenda kwa Sheha wa Shehia ya Fuoni Kibondeni Nasibu Kheri Nasibu. Sheha Nasibu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba hata yeye anashangaa kwa nini kesdi haijafikishwa mahakamani. “Aaah! Naumwa sana, kweli nyumba ilichomwa moto ila tatizo liko polisi ndo linasababisha kesi ichelewe kwenda mahakamani kwa sababu Polisi hawajenda eneo la tukio mpaka leo eti kwa sababu hawana gari, sasa hata mimi sijui wana maana gani kwani siwezi kufuatilia kutokana na hali yangu kama unavyoniona”, alisema Sheha huyo. Hata hivyo kwa upande wa jeshi la polisi Kamanda wa Mkoa wa Kusini (RPC) Augustine Ollomi akizungumza na mwandishi

wake alisema ataiandika yeye kisha ataikabidhi kwa Waislamu.” Alisema Amir Ramadhani, akimnukuu mkuu wa shule hiyo. Imeelezwa kuwa mwaka 2010, katika shule hiyo hiyo, lilitokea tukio la kuwavua mabinti hijabu zao na kudaiwa kufanywa na mwalimu aliyetajwa kwa jina la Danyaeri Mwankenja, ambaye alihamishiwa katika shule nyingine. Mpashaji habari anadai kuwa mwalimu Chingwile, ambaye niliye mpiga kinanda mashuhuri katika Kanisa lake hapo Tandahimba, ndiye aliyechukuwa nafasi ya mwalimu Mwankeja aliyehamishwa 2010.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Eammanuel Nchimbi (kushoto) akiwa pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye. wa habari hizi hivi karibuni huko ofisini kwake Mwera nje kidogo na mji wa Unguja amekiri kuwa nyumba ya Bi Salama imechomwa moto. Kamanda huyo amesema chanzo cha moto huo ni sintofahamu zilzotokea baina ya Bi Salama na mtuhumiwa Haji Amer Makame (29) Mshirazi wa Chunga Birikani, na kwamba upelelezi unaendelea ila wako mbioni kukamilisha ili ipelekwe mahakamani. “Muhusika wa hii kesi atuvumilie kwa sababu upelelezi haujakamilika ila tuko mbioni kukamilisha na itakwenda mahakamani”, alisema Augustine Ollomi Kamanda huyo wa polisi alitaja thamani ya paa la nyumba lililoteketezwa na moto kuwa ni laki mbili kwani ni paa la makuti. Nyumba hiyo kwa sasa inaendelea kubomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa kisiwani Unguja kwani ni nyumba ya udongo. Bi Salama Duweki ambaye ni Mjane anaomba msaada kwa wananchi, jumuiya na taasisi zimsaidie kwani hana uwezo wa kujenga nyumba nyingine. Kwa sasa anaishi kwa jirani zake. Tukio hilo la moto lilitokea huko Fuoni Kibondeni nje kidogo na mji wa Unguja tarehe 30th April, 2012 saa tisa za usiku yenye namba ya kesi RB No 1115/2012.

AN-NUUR
16

AN-NUUR

16

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012

USIKOSE KUSOMA AN-NUUR KILA IJUMAA

JAMADUL THAN 1433, IJUMAA MEI 18 - 24, 2012

Polisi Unguja wadaiwa kulinda wahalifu
Aliyechoma moto nyumba anatamba mitaani
ulikamilika”, alisema Bi Salama. Akifafanua zaidi akasema kuwa baada ya tukio akaw2a anapelekewa salamu za vitisho na mtuhumiwa. “Mtuhumiwa alimtuma mwanangu maneno mabaya mengi, nikamfata kwake nikiwa na jirani yangu tukamkuta mtuhumiwa na mkewe nikamwambia maneno uliyoyasema ni kesi ya kuhatarisha maisha yangu kwani sijui uhuni gani utakaotaka kunifanyia sasa nakwambia kama deni la nazi unazodaiwa kubwa kaombe upunguziwe deni ulipe mambo yaishe, mtuhumiwa akaomba radhi tukaondoka”, Bi Duweki alisema. Hata hivyo anasema, vitisho viliendelea Na Zainabu Mtima JESHI la Polisi Zanzibar limedaiwa kulinda wahalifu jambo ambalo hulivunjia heshma na kuondoa imani kwa wananchi. Katika tukio la hivi karibuni polisi wanadaiwa kumwachia mtuhumiwa anayedaiwa kuchoma moto nyumba lakini pia wakakalia jalada badala ya kufikisha kesi mahakamani. Tukio hilo linadaiwa kutokea Fuoni, Kibondeni mjini Zanzibar. Aliyekumbwa na janga la kuchomewa nyumba ni Bi Salama ambaye nyumba yake imechomwa hivi karibuni na mhalifu hajafikishwa mahakamani. “Mimi mama yangu kachomewa nyumba yake moto na imeteketea paa lote na kesi iko polisi mpaka leo haijapelekwa mahakamani, ukienda kusikiliza unaulizwa umeitwa? Na mtuhumiwa tunaemshuku yuko mtaani keshatoka polisi jambo ambalo hatujui Jeshi la Polisi wana maana gani kutufanyia ukatili huo” alisema Mwalimu Ramadhani ambaye ni mtoto wa Bi Salama. Kwa upande wake Bi Salama Duweki Salmini (55) Mshirazi pia ni mjumbe wa Sheha ya Shehia ya Fuoni Kibondeni anasema kabla ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya mwanae mmoja na mtuhumiwa. Akifafanua akasema kuwa yeye ana “mtoto anaitwa Shani Hassan Ashraki ambaye kazi yake ni kusimamia shamba la minazi la mzee Mzuka, kuna kijana ambaye namtuhumu kuchoma nyumba yangu moto anaitwa Haji. Aliiba nazi katika shamba la Shani zenye thamani ya laki moja, kesi hiyo ikafika kwa kamanda wa polisi jamii Dini Haji mtuhumiwa alikubali kulipa kwani ushahidi hadi lilipotokea tukio la kuchomewa nyumba. Anasema, baada ya kufika kesi Polisi mtuhumiwa alikamatwa na Sheha wa Shehia ya Fuoni Kibondeni alikataa kumchukulia dhamana. H a t a h i v y o , kinachomshangaza Bi Salama ni kuwa mtuhumiwa anamuona mtaani na kesi yake haijapelekwa mahakamani. “Tulipofika polisi Sheha wa Shehia ya Fuoni alikataa kumchukulia dhamana mara, namuona mtaani nikaenda kumuuliza polisi kulikoni, polisi akanijibu kwani unataka akae hapa maisha, mpaka leo kimya sijui kinachoendelea,”

Inaendelea Uk. 15

MKUU wa Jeshi la Polis nchini, IGP Said Mwema.

UKIPITA chungulia ndani ya ukuta inaonyesha Mkurugenzi hajapata fungu la kufyeka majani au haoni kuna tatizo. Hapa ni Raha Raha, Zanzibar.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.