Sauti ya Waislamu

Taasisi za Kiislamu zisaidie wasiopata mkopo wa Bodi
Wahitimu MUM watakiwa kuwa mfano kwa jamii Hajat Malale awataka Uk. 12 kushikamana na Uislamu

Waliotoka rumande wafichua makubwa
Washukuru kwa Da’wah waliyopiga gerezani Wadai Polisi walipora mali za watuhumiwa Unyama wa Israel Gaza - Uk. 3

ISSN 0856 - 3861 Na. 1046 MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23-29, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Baniani mbaya, ...

Karume atakiwa kusamehe wahafidhina wasiojitambua
‘Skolashipu’ za Qaboos wanapokea, lakini… Kudai haki ya Zanzibar wanatishiwa Sultan! Mbona Bara hatusikii kitisho cha Malkia (UK)?
Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu wa Zanzibar Mheshimiwa Amani Abeid Aman Karume ametakiwa kuwasamehe wanaomkejeli na kumtukana kwa sababu hawajitambui wala kujua wanalolifanya. Inaendelea Uk.5

Sultan Qaboos wa Oman.

Mh. Shamhuna. Uk. 4

Waislamu wataka kujua hatma ya TV yao Imaan Sheikh Farid asema

Unguja itakomboka
Ataka ‘Tanganyika’ iungane na Kenya Apaza sauti Mahakamani “mnautaka?”

Ni baada ya kukosa kibali kwa muda mrefu Wasema kama tatizo ni fedha waambiwe TCRA wasema malalamiko yapelekwe kwa DG

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Islamic Foundation na TV Imaan, Sheikh Aref M. Nahdi, amesema kuwa wametimiza mashariti yote yanayohitaka kupata

kibali cha kujenga Studio ya TV ila hawajui ni kwa nini mamlaka husika inachelewa kuwapa kibali hicho-yaani Construction Permit (CP). Nahd amesema kama ni
Inaendelea Uk. 11

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Habari
AN-NUUR

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

Sheikh Farid asema Unguja itakomboka
Alghaithiyyah, Zanzibar “MANAUTAKA?” Alihoji kwa sauti Sheikh Farid na kurudia mara tatu nje ya mahakama juzi ambapo wananchi waliokuwepo walijibu “hatutaki” huku wakimshangilia. Hali hiyo ilionekana kuwafurahisha wananchi waliokuja kusikiliza kesi hiyo nje ya Mahakama Kuu huku Sheikh Farid mwenyewe akionyesha kutokuyumba katika kile anachokisimamia na kupigania. Hii ni mara ya pili kwa Sheikh Farid kusema maneno kama hayo wakati akipanda gari kurejeshwa rumande ambapo wiki iliyopita alisema “Haki haifichwi lazima itakuja juu siku moja” wakati Sheikh Azzan akisema “Zanzibar Kwanza”. Kesi ya watuhumiwa hao imekuwa ikisikilizwa katika mahakama kimya kimya bila ya kuruhusiwa kuingia ndugu na jamaa za watuhumiwa hao lakini wamekuwa wakisubiri nje na ndipo juzi wakashangiriwa walipowaona wakitolewa ndani na kuanza kuwapigia takbira wakimaanisha Mungu Mkubwa mahakamani hapo. Kesi hiyo imekuwa ikisikilizwa ndani na wenye kuruhusiwa kuingia ndani ni maafisa wa polisi wa usalama, jeshi la polisi na baadhi ya waandishi wa habari wachache hata hivyo ulinzi katika maeneo yote ukiimarishwa huku badhi ya maafisa usalama wakiwa wametanda katika kila kona ya mahakama hiyo iliyopo Mji Mkongwe wa Unguja. Wa k a t i h u o h u o , Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake 7 wataendelea kusota rumande baada ya pingamizi lao la dhamana kushindwa kufunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP). Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar George Joseph Kazi alitoa uamuzi wake huo baada ya kusikiliza hoja zilizotolewa na pande zote mbili wiki iliyopita na kuutaka upande wa utetezi kuwasilisha malalamiko yao Mahakama Kuu juu ya madai ya ukiukwaji Katiba na sheria yanayodaiwa kufanyiwa watuhumiwa hao huko rumande. Mrajis alisema kuwa, Mahakama Kuu ndicho chombo pekee chenye kutoa tafsiri na ufafanuzi wowote wa Katiba, na kwa mujibu wa sheria mahakama yake haina uwezo kisheria kusikiliza madai hayo yaliowasilishwa. Uamuzi huo wa Mrajis umekuja kufuatia malalamiko ya ukiukwaji wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na ukiukwaji wa haki za binadamu wanaofanyiwa viongozi hao wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) baada ya kuwasilishwa mahakamani hapo na mawakili wao watatu wakiongozwa na Salim Tawfik, Abdallah Juma na Suleiman Salum wiki iliyopita. Mawakili hao waliiambia mahakama kuwa wateja wao huko katika magereza ya Kilimani wananyimwa haki zao za msingi za kuonana na ndugu na jamaa zao, wanafungiwa ndani saa 24 bila ya kuonana na mtu yeyote wakati watuhumiwa wengine wanapewa fursa hiyo, wananyimwa haki ya kufanya ibada hasa sala ya Ijumaa, kunyimwa fursa ya kubadilisha nguo na kusababisha kuvaa nguo hizo hizo zaidi ya wiki tatu sasa, na pia kutenganishwa kila mtu chumba chake na kukataliwa kukutana na wenzao wakati wao bado ni watuhumiwa na hawajatiwa hatiani. Madai mengine yaliowasilisha na mawakili hao ni kule kunyimwa fursa ya kuletewa vyakula kutoka nyumbani wakati watuhumiwa wenzao wanaletewa na kukatazwa kwenda kusali msikitini wakati katika magereza kuna msikiti na wenzao wote wanapata fursa hiyo ya kujumuika na wenzao kusali na pia kunyolewa ndevu wakati maafisa wa magareza wanafahamu kuwanyoa ndevu ni kuwadhalilisha. Aw a l i M a h a k a m a n i hapo upande wa Mashitaka ulioongozwa na Mwanasheria kutoka ofisi ya Mkurgenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), Ramadhan Nassib, alitetea hoja hizo na kuiambia mahakama hiyo kuwa suala hilo sio pahala pake na kuutaka upande wa utetezi kuwasilisha madai hayo Mahakama Kuu ambayo ndiyo yenye uwezo wa kutoa tafsri na maelekezo ya ukiukwaji wa Katiba.

MAONI YETU

Dawa za uzazi wa mpango ni hatari. Wananchi tuwe makini
HABARI iliyoripotwa na gazeti la Mwananchi la Jumatano Novemba 21, 2012, imewashtua wengi baada ya kubainisha kuwa sindano za uzazi wa mpango, zimethibitika kuwa ni hatari kwa maisha ya watu. Kwamba kutokana na utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Marekani, tena Tanzania ikiwa ni moja ya nchi ambazo utafiti huo umefanyika, imebainika kuwa sindano hizo zinaharakisha kasi ya maambukizi ya ukimwi, kwa kuwa zina vichocheo vingi ambavyo huhuisha virusi vya ukimwi. Si hivyo tu, bali pia sindano hizo zina vichocheo ambavyo huongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake. Hiyo ni mbali na madhara mengine ambayo tayari yanajulikana ambayo yamekuwa yakiwaathiri wanawake yakiwemo kukithiri kwa matatizo wakati wa kujifungua, kuharibika mimba au kutokupata kabisa na kuharibika mfumo wa kawaida wa mahusiano ya mume na mke. Swadakta, labda sasa wanaharakati wa uzazi wa mpango, watakuwa wakitafakari juu ya hatma ya maisha na afya za wanawake wa Kitanzania. Kwa kuwa mstari wa mbele wa kuhamasisha na kusisitiza juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango, hususan sindano, vidonge, vijiti na kitanzi. Mara kwa mara tumeshuhudia baadhi ya wanawake wakilalamika kuwa wanapotumia njia hizi, hunenepa sana, wengine wamedai kukosa siku zao za ada na wapo waliosema kuwa matumizi ya njia hizi kuna uwezekano wa kupata saratani. Hata hivyo, iliendelezwa kampeni kali na wataalam wa uzazi wa mpango na wanaharakati wa haki za wanawake, kwamba madai hayo sio sahihi na kwamba, wanawake wasipotoshwe na waondoe wasiwasi juu ya matumizi ya njia hizo. Mara nyingi wakielezwa kwamba wanapotokewa na hali hizo zinazotajwa kama ndio madhara, wasiwe na wasiwasi kwani njia hizo zimedhibitishwa kiafya na hazina madhara kwa mwanamke. Wapo waliokataa katakata matumizi ya njia hizi. Bila shaka hawa walionekana majuha na waoga kwa waume zao katika kuchukua maamuzi. Lakini kwa matokeo ya utafiti huu, bila shaka wanawake hawa ndio waliookoka na wenye kujihakikishia usalama zaidi wa maisha na uzazi wao. Walioshikilia ushawishi wa wanaharakati na kuonekana ni watu ndio wa kileo, bila kuzingatia kwa kina athari za kutumia njia hizi za uzazi, bila shaka taarifa za ugunduzi wa utafiti huu zitakuwa zinawaogofya na kuwachanganya. Angalizo letu ni kwamba, tusifike mahali tukatekeleza mikakati ya watu kwasababu ya pato au biashara hasa katika masuala yanayogusa afya za watu. Tusifanye biashara katika maisha ya watu. Tatizo lililopo ni kuwa hakuna ‘forum’ inayowakutanisha wote waliotumia madawa hayo wakapata madhara wakajieleza na kutoa uzoefu wao. Kila mmoja anajiugulia pweke binafsi. Ni muhimu tuwe makini kufuatilia kwa kina malalamiko ya watu wanaohisi kuathirika na kampeni hizi za kushawishi uzazi wa mpango au chanjo za kinga au maradhi. Bila shaka njia hizi artificial za uzazi wa mpango zina madhara makubwa japo hatutaki kukiri kwa kuwa hatujafikiri na kutambua kiwango cha athari kilichopo na kinachokuja. Tatizo kubwa ni kuwa mambo haya yamekuwa yakipokewa na kubarikiwa kupitia mikono ya kisiasa. Wenye makampuni yao ya kimataifa ya kutengeneza madawa washajua bei ya wanasiasa na namna ya kuwafikia. Dakitari mmoja bingwa wa magonjwa ya wanawake aliwahi kumwonya rafiki yake kwamba asithubutu kumpa mkewe madawa ya kuzuiya mimba (uzazi wa mpango). Sasa mtu unajiuliza, kwa nini liwe ni suala la mtaalamu kuwaonya ndugu na rafiki zake? Kwa nini isiwe ni kauli ya serikali na ya kitaalamu kwa watu wote. Jibu lake ni kuwa wenye biashara yao washamalizana na wanasiasa (na hata wataaalmu ili wasipige kelee). Mwananchi unaumia. Tuchukue tahadhari. Tuwe makini.

Wa n a s h e r i a w e n g i n e wa upande wa waendesha mashitaka waliosikiliza kesi hiyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Mashitaka ni Rashid Fadhil na Raya Issa Mselem ambaye aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa hapo sio mahali pale na kama wanataka wafungue madai katika mahakama husika. Raya aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika. Katika uamuzi wake, George Kazi ambaye pia ni hakimu wa mahakama ya mkoa Vuga, alisema mahakama yake haiwezi kutoa tamko la ukiukwaji katiba, na kufahamisha kuwa Mahakama Kuu ndiyo pekee yenye Mamlaka ya kusikiliza na kutoa maamuzi yanayohusiana na ukiukwaji wa Katiba. Mrajis huyo wa Mahakama Kuu ameutaka upande huo wa utetezi kufungua madai yao hayo Mahakama Kuu, kwani ndicho chombo pekee chenye Mamlaka ya kusikiliza masuala ya Katiba na sio katika mahakama hiyo ambayo inasikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa hao wanane. Mrajis wa Mahakama Kuu alikubaliana na ombi lililowasilishwa kutoka upande wa waendesha mashitaka kuiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 29 mwaka huu kwa kutajwa. Washitakiwa katika kesi hiyo ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) wa Kwamtipura, Mussa Juma Issa (37) mkaazi Makadara na Azzan Khalid Hamdan (48) mkaazi wa Mfenesini. Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Suleiman Juma Suleiman (66) mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakari Suleiman (39) wa Tomondo pamoja na Ghalib Ahmada Omar (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe wote ni wakaazi wa Zanzibar. Wote hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka ya uvunjifu wa amani, ushawishi wa kuchochea na kurubuni watu, kula njama pamoja na Inaendelea Uk. 5

3

Israel yaangamiza raia, watoto Gaza
Na Mwandishi Wetu msongamano wa watu, kwa maana ya watu wengi kuishi katika sehemu ndogo kuliko sehemu yoyote duniani, kwa hiyo kombora likipiga nyumba, ni dhahiri nyumba nyingi jirani zitaathirika pia. Usiku wa Jumatatu nyumba mbili zililipuliwa ambapo watu wane (4) waliuliwa wawili wakiwa watoto na wengine 42 kujeruhiwa vibaya. Baada ya shambulio katika nyumba hizo, yalifuatia mashambulizi mengine mawili ambapo mtoto mmoja aliuliwa na watu watano wakiwa shambani mwao. Kabla ya hapo, nyumba ya ghorofa mbili ilishambuliwa na kuangamizwa kabisa ambapo watu 11, wengi wao wakiwa akina mama na watoto waliuliwa. Katika uvamizi wa Januari 2009 uliopewa jina Cast Lead, Profesa Jeremy Salt aliandika ujumbe kwa aliowaita makanda hodari wa Israel akiwahoji, wanajisikia vipi wakiwafyatulia wanawake na watoto makombora? Je, wanaona raha gani wakichinja wanawake, watoto wachanga na raia wa Palestina wasio na hatia! Hawaoni hata chembe ya huruma wakati wakivurumisha makombora kuangamiza nyumba ambazo wana uhakika kuwa ndani yake kuna watu ama wanakula, wanapika au watoto wanafanya kazi zao za shule? Hawajisikii vibaya kuangamiza nyumba za watu, shule zao na hospitali walizojenga kwa tabu kutokana na vikwazo walivyowekewa na Israel? ‘Nyie makanda hodari’ wa Israel, je mnalala usingizi na kukoroma wala hayawajii maruweruwe juu ya unyama mliofanya kwa kuuwa familia, baba, mama na watoto wao wakiwa jikoni, wengine ukumbini (living rooms), watoto wakiwa wamelala, wakiwa shuleni, na wale mnaowauwa wakiwa Msikitini, s h a m b a n i n a ofisini? Je, wakulima wa Kipalestina wakiwa shambani, akina mama na watoto, walimu darasani na Imam msikitini, wanahatarisha vipi amani ya Israel? Hamuoni aibu wala kujisikia vibaya? Nyie watu gani msioona vibaya kuwafanyia wenzenu ukatili wa aina hii?

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

Israel imeangamzia raia 162 wasio na hatia Gaza kabla ya kutangazwa kusitishwa mashambulizi hiyo juzi. Kwa upande wa Israel imedaiwa kuwa wameuliwa watu watano kutokana na maroketi yanayorushwa na wapiganaji wa Hamas. Habari za mashambulizi kwa Wapalestina yamekuwa yakipotoshwa pale ilipodaiwa kuwa kuna vita kati ya Israel na Gaza. Hakuwezi kuwa na vita baina ya Wapalestina wa Gaza na Israel. Gaza ni sehemu iliyozingirwa na Israel hakiingii kitu wala mtu mpaka ruhusa ya Israel. Nyumba zilizoangamizwa na Israel mwaka 2009 mpaka leo hazijajengwa au kufanyiwa ukarabati kwa sababu toka mwaka huo mpaka leo, Israel haijaruhusu kupita hata mfuko mmoja wa saruji! Sasa watu kama hao wanapigana vipi? Katika shambulio moja wiki iliyopita, Israel iliangamiza nyumba ya familia moja ambapo watu 11 waliuliwa wakiwemo wanawake watano akiwemo bi kizee wa miaka 80 na watoto wanne. Shambulio hilo la kombora, liliangamiza kabisa nyumba ya familia ya Dalou katika wilya ya Sheikh Radwan. Ilikuwa kazi kubwa kufukua maiti za vichanga katika kifusi cha nyumba hiyo na kisha kupelekwa ‘moshwari’ katika hospitali ya Shifa. Katika shambulio moja, nyumba ya familia moja iliangamizwa wakiuliwa watoto wawili, watu wazima wawili na wengine 42 kujeruhiwa. Hali ya kutisha ilielezwa kuwepo katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Shifaa ambapo zinaonekana maiti za watoto wachanga wakiwa wamewekwa pamoja wakiwa wamejaa damu na vumbi kutokana na kufukiwa na kifusi. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la Associated Press (AP), watu wengi wameuliwa kutokana na nyumba zao kuangamizwa kwa makombora na hivyo kufukiwa katika vifusi. Katika waliokumbwa na balaa hilo wiki hii ni pamoja na familia ya Abdel Aal ambayo nyumba yao iliangamziwa kabisa. Kama inavyofahamika kuwa Gaza ni mji ambao una

Mashambulizi yasitishwa
Mateso mikononi mwa ‘wakoloni’ na ‘makaburu’ wa Kiyahudi, yamekuwa ndio maisha ya Wapalestina kwa miaka mingi sasa. Yamekuwa ndio hali yao ya kila siku. Hebu fikiria kuishi katika mazingira ambayo hujui kama itafika jioni ukiwa hai au maiti! Mfikirie mtoto anayezaliwa na kukulia katika mazingira haya ya kukaliwa kimabavu na Israel!

Waliotoka rumande wafichua makubwa
Na Bakari Mwakangwale Ustadh Abubakar aliwatanabaisha Waislamu akisema, kwamba siku zote dhalimu anapodhulumu pindi akibaini yule aliyedhulumiwa anataka kuchukua haki yake, huonekana mwenye haki ndiyo anataka kudhulumu. Ama akizungumzia kadhia ya Markazi Chang’ombe, kabla na baada ya kukamatwa alisema ilianza Oktoba 12, mwaka huu, baada ya swala ya Ijumaa, pale ambapo umma wa Kiislamu ulipoamua kwenda kuinusuri ardhi ya Waislamu ambayo imeuzwa na Bakwata kwa mfanyabiashara. Alisema, Waislamu wakiwa pale waliinua jengo la Msikiti na kuupa jina la Hassan Bin Ameir, ambaye Waislamu wanapaswa kumkumbuka, na eneo lile ndio ilikuwa mahala pake kulingana na historia yake kwa Waislamu hapa nchini. “ H a s s a n B i n A m e i r, alikuwa ni kiongozi mpigania haki za Waislamu, kiongozi aliyewatendea haki Waislamu wa nchi hii ambaye ndiye anastahili kupewa kumbukumbu katika kiwanja kile cha Markazi Chang’ombe, maana bila yeye na Tewa Said Tewa, huwezi kuelezea kiwanja kile bila kuwataja wapambanaji hao.” Alisema Ust. Juma. Alisema, wakiwa pale kwa muda mchache walisimamisha kuta, waliweka sakafu na kupiga bati, lakini alidai katika hatua za awali walifika askari kisha kukutana na Ustadhi Ismaili, ambaye aliongea kwa niaba ya Waislamu, akawatembeza eneo hilo na kuwapa histori ya eneo hilo kwa kirefu. Maafande wale, waliondoka huku wakimtaka Ustadh Isamili, afike kituo cha Polisi Chang’ombe, Temeke,

protection” iliyotolewa ili kuwalinda raia. Umoja wa Mataifa na Katika Operation Cast Lead, ilikuwa msiba mkubwa Baraza lake la Usalama, lilikaa kwa Wapalestina. Kwanza kimya likitizama zaidi ya Israel, ukiacha silaha nzito Wapalestina 1,400 wakiuliwa kama ‘Missiles, bombs, shells’ na makazi yao kuharibiwa ambazo Wapalestina hawana, kabisa. Katika operesheni hiyo, Israel ilitumia mpaka silaha haramu (illegal weapons) hakuna kilichosalimika. kama ‘White phosphorus) Shule, Vyuo Vikuu, Misikiti, ambayo ni silaha ya kemikali hopitali, viwanda, mpaka ofisi za taasisi za Umoja wa inayounguza vibaya. Lakini pamoja na uhalifu Mataifa, ziliangamizwa kwa wote huo, hakuna “Security mabomu na makombora. UN C o u n c i l n o - f l y z o n e kimyaa!

BAADHI ya watuhumiwa wa kesi ya kiwanja cha Markazi Chang’ombe, Jijini Dar es Salaam, waliotoka kwa dhamana mapema wiki iliyopita, wamesema wamejifunza na kubaini mambo mengi wakiwa gerezani. Akiongea na Waislamu katika Msikiti wa Mtambani, katika maadhimisho ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislamu 1434, Ijumaa ya wiki iliyopita, mmoja wa watuhumiwa hao, Ustadh Abubakar Juma, amesema kikubwa kilichotawala huko ni udhalilishaji. Akifafanua Ustadh Juma, alisema kuna namna nyingi za kudhalilisha Uislamu na mbaya zaidi ni pale Muislamu anapowekwa uchi, kwani alidai baada ya kufikishwa gerezani waliamuliwa Waislamu wote kuvuliwa nguo. Alisema, walimueleza kiongozi wa gereza kuwa haiwezekani wakavuliwa nguo katika mazingira hayo, hata hivyo kiongozi huyo, alidai atakachoweza kuwasaidi ni kuwatenganisha wale wenye umri mdogo na wenye umri mkubwa. “ Yu l e b w a n a a l i s e m a wenye umri chini ya miaka 35, watavuliwa kivyao na wale wazee kwa wazee watavuliwa kivyao. Hii ni hali iliyokuwepo huko.” Alisema. Lakini kwa upande mwingine alisema, wamefurahiya maisha ya gerezani kwani kwa mwenye kujitambua hupata muda mwingi wa kufanya ibada, na kwa muda huo waliowekwa mahabusu wameweza kusilimisha Wakristo zaidi ya 11.

lakini Waislamu waliafikiana aongozane na Waislamu wengine watatu kituoni hapo, akiwemo Ustadhi Mukadam (anayeshikiliwa na Polisi hadi sasa). Alisema, lengo kuu la kuitwa Polisi, walielezwa ni kukutanishwa na yule aliyeuziwa eneo lile, alidai kinyume na matarajio hayo walikuta ramani ya eneo hilo ambayo haionyeshi mwanzo wa kiwanja wala mwisho wa kiwanja. Wakiwa huko wajumbe hao, walitakiwa waandike maelezo, jambo ambalo hawakulifanya kwa maelezo kuwa wao si viongozi bali wapo viongozi wanaopaswa kutoa maelezo hayo kwa maandishi wanayoyataka. Alisema, wakiwa Markazi Chang’ombe majira ya saa tano usiku, walipata taarifa kuwa Sheikh Ponda, kakamatwa akiwa Masjidi Tungi, Temeke, na usiku huo huo wa saa tisa zilivamia gari za Polisi zisizopungua kumi na mbili, kikiwemo kikosi cha mbwa, walivunja geti na kuanza kamata kamata. Alisema, baada ya kuingia hapakuwa na mtu katika jengo la Markaz zaidi ya kinamama wasiopungua 12, ndani ya Msikiti wa Markaz, na Waislamu wengine walikuwa katika Msikiti walioujenga wakiwa pale. “Ilisikika sauti ya afande ikisema, ‘piga risasi wale’ kwa kweli tulijua kuwa ndiyo yametimia, tuliwaambia msipige risasi sisi hatuna silaha yoyote, sauti ile iliamrisha tena ‘toka mbele hatua tano’ tukatekeleza amri hiyo, ikatoka amri nyingine, ‘inua mikono juu, tukainua’…… ‘piga magoti tukapiga’…….
Inaendelea Uk. 5

Skolashipu za Qabusi- Lengo litafikiwa?
Na Mwandishi Maalum KWA muda mrefu sasa Zanzibar imekuwa nyuma sana kimaendeleo ya Elimu. Na hali ya unyuma wenyewe huu unazidi kuwa mkubwa pale linapokuja suala la ushiriki wetu na nafasi ya Wazanzibari kujipatia Elimu ya juu iliyo jambo la muungano. Zanzibar tuko nyuma sana kielimu ya juu na hili limechangiwa na mambo mengi ukiwemo Muungano wetu, tusioruhusiwa kuuhoji. Tangu kianzishwe Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam ambacho ndicho Chuo Kikuu cha kwanza hapa Tanzania, sasa ni mwaka usiopungua wa 45. Nakumbuka chuo kile ndio chachu ya maendeleo unayoyaona leo Bara kwani vijana kadhaa wenye sifa na wasio sifa waliwezeshwa na kujipatia Elimu yao na wengine magamba yao matupu akina ‘kihio’ na ‘juzi hapa tumeyasikia ya muungao wa Pemba na Zimbabwe’, lakini ndio wanazo digirii zao japo karatasini na sio kichwani. Sisi huku tumeachwa na maneno mengi. Nakumbuka Wazanzibari waliowakipata nafasi ya kujiunga pale kwa mwaka ilikuwa ni watu kumi kama sikosei. Sasa wewe fikiria Chuo Kikuu kizima kinachukuwa Wazanzibari kumi tu hadi mwishoni mwa miaka ya 1990. Na hata baada ya hapo idadi ya Wazanzibari katika chuo hicho kikuu na vyengine vya bara hairidhishi. Na hii haikutokana na kuwa kulikuwa hakuna wenye sifa huku Zanzibar. La hasha! Ndio muundo wetu wa Muungano. ‘Wanyime Elimu, tuwatawale.’ Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Taifa- SUZA, C h u k w a n i n a Tu n g u u , kumemkombowa na kumfunguwa macho Mzanzibari kwa kiasi kikubwa. Naamini kitendo hiki hakikuwaridhisha wengine wanaotaka mfumo huu wa muungano uendelee maana tukisoma tutajuwa kudai haki zetu na usawa. Na hili haliepukiki. Tumesoma, japo hivyo hivyo kwa taabu, na sasa tunahoji Muungano na hata usawa katika nyadhifa mbali mbali ndani ya Muungano. Hili pia haliwapendezi wenzetu. Hata hivyo, moja kati ya vikwazo vikubwa ambavyo kwa sasa vinawakabili wanafunzi wa Zanzibar kusonga mbele Elimu ya juu hasa kiwango cha Masters na PhD ni ukosefu wa Udhamini. Naamini kuna ‘scholarship’ lukuki zinazokuja Tanzania, lakini zote hazitufikii sisi huku Zanzibar. Na hata hizo chache zinazoletwa wakubwa zetu huzifungia mabweta kwani huwa hawana mtoto wao, mjomba wala shangazi yao mwenye sifa, kwa hiyo hata wenye sifa wakiwepo, wote nao wakose. Hivi ndivyo tulivyo. Kule Bara mwaka jana Chevening Scholarship, hakuna Mzanzibar aliepata. Ndio tunajuwa kuna udini katika Scholarship na hili halina shaka hata Chembe. Kuna Common wealth Scholarship kule, sisi hatupati dumu dawamu. Kuna usiasa huko dhidi ya Wazanzibari. Kuna Scholarship zikiletwa hapa na kumfikia Bwana mkubwa mmoja. Ukiritimba mtupu na majibu yasiyo ridhisha na hata akizitangaza bado siku mbili ‘deadline’, hatupati. Ndio sisi kwa sisi hao! Scholarship pekee ambazo Mzanzibari hupata nadra sana ni za Ubalozi wa Marekani, nazo basi zisipitie Zanzibar na pia ni kwa juhudi na heshima ya wawakilishi wa ubalozi wa Marekani waliopo Zanzibar. Hizi kuna vijana wetu wanaozipata lakini ni ‘haba nasi’ kusema kweli. Na kwa mantiki na sababu kama hizi, utakuta bado Wazanzibari hatuendi usoni katika Elimu ya juu. Kuna Wazanzibari lukuki hivi sasa hapa Nyumbani wenye ‘Admission’ za vyuo mbalimbali lakini wameshindwa na udhamini. Hawana msaada. Muungu haachi mjawe. Muda mfupi uliopita tumeenda Tunguu kushuhudia uzinduzi wa ‘Scholarship’ za Sultan Qabus wa Oman kwa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). Scholarship hizi ni neema na mafanikio tele kwa Wazanzibar iwapo lengo lilokusudiwa litasimamiwa kwa misingi ya haki, ukweli na uwazi. Udhamini huu wa Elimu ya juu kutoka Oman utawadhamini Wazanzibar 50 kila mwaka kwenda kusoma katika ngazi tafauti katika vyuo tafauti tafauti duniani. Kheri iliyoje hii kutoka kwa muumba. Kwa sasa akina sisi wenye watoto wa kusoma, tumeingia tamaa kupita mpaka kwani kama watakwenda vijana 50 kila mwaka baada ya miaka kumi tutakuwa na wangapi? Haya ni mafanikio makubwa. Hongera sana mfalme Qabus, sadakatu jaariya yako hii baba! Mungu akuzidishie kheri na sie tuneemeke zaidi wakitaka watawala wetu. Lakini wakati tukijipongeza na kufurahia neema hii najihisi macho yana machozi na moyo unanipiga kwa kasi kwa woga. Hii ni ishara ya kuwa nina wasiwasi. Khofu yangu kubwa ni kuwa jee, Udhamini huu utamnufaisha Mzanzibar kweli? Siamini na sitaki kuamini kama msaada huu utamnufaisha Mzanzibari, isipokuwa tutarajie moja kati ya matatu yafuatayo kwa udhamini huu. Kwanza, iwapo Udhamini huu utasimamiwa kwa haki wakapatiwa kweli Wazanzibari watupu 50 kila mwaka, udhamini huu hautafika miaka mine utakufa. Wenzetu wa bara watauchochachocha mpaka ukatike uondolewe. Na hili si geni kwao kutufanyia. Tulikuwa na maonyesho ya Biashara hapa wakati wa Komando Salmin. Waliyapiga vita mpaka yakasimama na kufa kabisa. Wao hadi leo wana sabasaba wala hatuwahoji. Na hili hawataliacha lifanikiwe. Tuombe uhai. Pili, ikiwa watashindwa kulifanya hili la kwanza, kuanzia sasa watapandikizwa vijana wa bara wenye digirii za akina ‘Vihio’, wakishakuja watapewa vitambulisho na vyeti vya kuzaliwa vya Zanzibar. Wasiofanyiwa tohara watafanyiwa hapa usiku usiku. Wasiovaa buibui na hijabu watajifunza hapa hapa mpaka wafanane na sisi. Hawa ndio watakaopata nafasi hizi za mfalme Kabusi na sisi tutabaki kusema ‘nami nilipeleka maombi’, au tutaambiwa hatujui ‘kimombo’ ila wao ndio wanaojua kusema hicho kiluga cha Wazungu zaidi kuliko sisi. Tatu, nafasi hizi zitatolewa kwa wanasiasa. Haya sasa niambie kuna Mzanzibari atakaepata nafasi ya masomo hapo? Unamjuwa nani atakwenda kusoma hapo? Subiri na chunguza. Kwa sasa nabakisha shaka zangu hizo tatu tu, lakini naamini kwa nguvu yote hivi ndivyo ‘Scholarship’ za Qabus zitakavyotolewa na zitakavyosimamiwa. Wazanzibari wachache mno watakaonufaika na hizi na kama hatuamini tukae mkao wa kula. Kila la heri na ‘Scholarship’ za Qabus. Zanzibar ni njema, atakae aje!

4

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

Press Release Sultan Qaboos Academic Fellowship (SQAF) Program for the State University of Zanzibar (SUZA)
16th Novemba, 2012 Kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mkuu wa SUZA, Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, nina furaha kubwa kupata heshima ya kuitangaza Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA kwa ajili ya Wazanzibari kwa mintarafu ya kujenga uwezo katika rasilimali watu utakaokuwa na wataalamu watakaomudu kuleta maendeleo, utangamano na ustawi bora wa uchumi wa Zanzibar. Bila shaka yoyote Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA itachangia kwa ujumla katika maendeleo ya Zanzibar na kwa ajili hiyo kuyatimiza matarajio mema ya Sultan Qaboos bin Said, Sultan wa Oman na ya Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kujenga amani na mustakbal mwema wa Zanzibar. SUZA ndiyo taasisi pekee ya kizalendo ya umma iliyokuwa na mtaala wa kuandaa rasilimali watu na maendeleo endelevu katika muktadha wa kuangalia kwa mapana maendeleo ya muda mrefu ya Zanzibar kama kisiwa katika Bahari ya Hindi kilicho na mazingira ya kipekee ilhali kipo karibu sana na Bara la Afrika. Kuna aina tatu za wanafunzi wenye sifa ambao wataweza kuomba nafasi katika Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA: 1. Waombaji ambao ni waajiriwa wa SUZA. 2. Waombaji ambao si waajiriwa wa SUZA lakini watapatiwa Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA lakini watafanya kazi SUZA baada ya kumaliza masomo yao. 3 . Wa o m b a j i m a k i n i kutoka taasisi nyingine wenye kuonyesha uwezo na utayari wa hali ya juu. Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA itakuwa na utaratibu wa kuwafunza wasomeshaji katika fani ya elimu, afya, mazingira, miundo mbinu, ujasiriamali katika ngazi ya Cheti, Shahada ya Kwanza, Uzamili na Uzamivu kutegemea mahitajio ya kistratijia ya muda mfupi, wa kati na mrefu wa Zanzibar. Aina tatu ya waombaji watanufaika katika nyanja za usomi, ufundi na utawala katika vyuo vya Ulaya, Marekani na Asia na msisitizo maalum utakuwa katika elimu na uhifadhi wa rasilimali watu ndani ya Zanzibar kupitia Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA. Wizara ya Elimu ya Juu ya Oman itashirikiana na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA katika kuutekeleza mpango huu na SUZA itashirikiana moja kwa moja na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali pamoja na taasisi stahili zilizopo kwa lengo la kuwapata wanafunzi bora kutoka sehemu zote za kijamii na za kielimu za Zanzibar watakaoomba nafasi kutoka Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA. Maombi yatakuwa bure kupitia mtandao ambao utaonyesha taarifa zote kuhusu sifa za kuchaguliwa, usajili na ukomo wake na taarifa hizi zitatolewa kwa njia ya matangazo kupitia vyombo vya habari ikionyeshwa pia kuanza rasmi kwa mwaka wa masomo wa 2013-2014. Natoa shukurani zangu za dhati na kumuomba Mola amlipe kheri nyingi Sultan Qaboos bin Said kwa juhudi zake katika kutia nguvu maendeleo ya kujenga raslimali watu kwa ajili ya amani na utengamano wa Zanzibar – Amin. Imetayarishwa na Kamati ya Muda ya SQAF ya baina ya Zanzibar na Oman. Kupata taarifa zaidi kuhusu Sultan Qaboos Academic Fellowship Program for SUZA tafadhali wasiliana na: Prof. Idris A. Rai Makamu Mkuu wa Chuo Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) Tel: 0772 195 965 Email: vc@suza.ac.tz

5
Inatoka Uk. 1 Aidha, ametakiwa kufahamu kuwa anachofanya ni kwa ajili ya nchi yake na watu wake, kwa hiyo asitizame madhara anayopata kama mtu binafsi, bali atizame vile ambavyo wapigania nchi kama ilivyokuwa katika mapinduzi, watu walikuwa tayari kupoteza maisha kwa ajili ya nchi yao. “Katika kupigania masilahi ya nchi, mara nyingi gharama huwa kubwa ambapo watu huwa tayari hata kufa, ninachomuomba Rais Mstaafu Karume ajue kuwa katika ‘struggle’ (mapambano) yoyote hapakosekani watu wagumu kuelewa na hata wasaliti, sasa hawa ni wa kuwahurumia maana hawajitambui, ile kukaliwa muda mrefu kumewadumaza hata ule uwezo wao wa kufikiri na kuyaona mambo na kuyapima, mimi namwomba asamehe na asikasirike maana akikasirika atakata tamaa kukimbia ‘struggle’”, amesema Mzee mmoja kada wa CCM ambaye hata hivyo hakutaka kutaja jina lake akisema hali ya hewa hairuhusu. Maoni hayo yanakuja kufuatia hali inayoendelea

Habari za Kimataifa

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012
kuwepo serikali ya maridhiano na umoja wa kitaifa. Watu ambao inaonekana wangependa kuona zikiendelea zile siasa za chuki, uhasama na faraka. Hata hivyo haijulikani kama watu hao wananufaika vipi na siasa hizo au basi tu wanatumiwa na watu wasioitakia mema Zanzibar bila wao kujijua. “Unajua katika ulimwengu huu wa kisiasa, unaweza kupenyezewa jambo ambalo ninakupa masilahi kidogo binafsi ya muda mfupi, we ukajiona ndio umepata ukaharibu masilahi ya taifa na nchi kwa karne zijazo bila kujua au ukajua lakini ukawa msaliti au kwa ujinga tu.” “Hebu niambie kama si ujinga au usaliti ulio wazi, kupinga hali hii ya maridhiano na kupinga Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili yaliyoepukana na mazonge haya ya kero za muungano; kunamsaidia nini mwananchi wa Zanzibar na Zanzibar yenyewe kama nchi?” Alisema na kuhitimisha Mzee huyo akitoa maoni yake kwa mwandishi mjini Zanzibar mapema wiki hii.

AN-NUUR

hivi sasa Zanzibar ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakimfanyia dhihaka Rais Mstaafu Mheshimiwa Amani Abeid Karume kwa msimamo wake kuwa kila mtu ni lazima asikilizwe hata anayetaka muungano wa mkataba maana hiyo ndiyo demokrasia. “Ukitaka kujua kuwa watu hawa hawajitambui au wamelemaa, wewe angalia misaada kupitia serikalini kutoka kwa Sultan wa Oman wanapokea, hutawasikia wakisema serikali imetekwa na Sultan, lakini Wazanzibari wanaposema wanataka Kiti chao Umoja wa Mataifa, mara propaganda za kurudi Sultani zinaibuka, mbona Bara wakipigania mambo yao hatusikii wakitishiana kurudi Malikia wa Uingereza au Kansela wa Ujerumani? Mbona ujinga huu tunakuwa nao sisi tu wa Visiwani tunaolalamikia kero za muungano?” Aliongeza na kuhoji Mzee huyo wa makamo ambaye amesema kuwa yeye msimamo wake ni kuwa na

Karume atakiwa kusamehe

RAIS Mstaafu Amani Abeid Karume serikali ya Zanzibar yenye mamlaka kamili kuliko ilivyo hivi sasa na kwamba maoni hayo atayasema wazi mbele ya Tume ya Jaji Warioba. Alitaja mfano wa misaada kutoka kwa Sultan kuwa ni pamoja na msaada wa kielimu unaojulikana kama Sultan Qaboos Academic Fellowship (SQAF), maalum kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Serikali Zanzibar (State University of Zanzibar-SUZA). “Mbona watu hawa

wanaowatishia watu kurudi Sultan, hatuwasikii wakimshambuliwa Waziri wa Elimu Mheshimiwa Shamhuna kwa kupokea Skolashipu hizo? Mbona watoto wao wanaomba kupata msaada huo wa kielimu, tena wanataka wapewe upendeleo; huku ni kupumbazwa na kupumbaa mpaka inafikia mtu hajui hata lipi la kukusaidia”, alisema Mzee huyo akionyesha kukerwa na watu wanaopiga propaganda ya kurudi Sultan. Toka Rais Mstaafu Amani Abeid Karume atoe hotuba Dodoma inayopinga hali ya kutishana Zanzibar na kutaka watu wapewe fursa ya kutoa maoni yao hata wale wanaotaka muungano wa mkataba, kumekuwa na makundi ya watu ambao wamekuwa wakipita kung’oa picha zake na wakati huo huo wakitoa kauli za kejeli dhidi yake. Watu hao wanadhaniwa kuwa ni wale wahafidhina ambao hawakutaka hata

Inatoka Uk. 3 waambieni wenzenu wasogee, walikuwa msikitini wakatoka pia, kisha tukaambiwa tulale chini.” Alisema, akihadithia tukio hilo. Alisema, utii wa amri zile za maafande kwa Waislamu, ambao alidai walitii kwa ajili ya kuepusha shari, uliwatia mashaka na kuhisi kuwa ulikuwa mtego wakidhani kuwa walikuwepo wengine wenye silaha katika eneo lile. Alisema, baada ya hapo kilichofuata, walianza kuwasachi mifukoni na kuchukua simu zao na pesa na walipojiridhisha kuwa Waislamu wale hawakuwa na silaha, pamoja na kutii amri, askari hao walianza kuwashushia vipigo mfululizo. Alisema, baada ya kutoka pale, walisogea katika jengo la Markazi, waliingia na kufanya upekuzi huku wakitoka na vifaa walivyoweza kuvibeba na kuingiza katika magari yao. Alisema, katika hali ya kushangaza askari wale walikuwa wamegawanyika kwani alidai kuna waliokuwa wakiwapiga na wengine

Waliotoka rumande wafichua makubwa

wakiwatetea na zaidi miongoni mwao walikuwa wakitokwa na machozi baada ya kuona wenzao walivyo washushia vipigo akina mama wa Kiislamu waliokuwa wakiwatoa ndani ya Msikiti wa Markazi. “Kina mama wale wa Kiislamu pamoja na vipigo vikali kutoka kwa maafande wale, walikuwa wakitoka wakitamka Shahada, kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na Mtume wake, huku wakiitwa Malaya, na matusi mengine mazito mazito, inasikitisha kuona jeshi la Polisi wanakuwa makatili kiasi kile bila kujali wale ni wanawake.” Alisema Ust. Abubakar. Alisema, majira ya saa kumi na moja na nusu, walimaliza uvamizi wao na kujiridhisha na kuondoka nao, na katika tukio jingine ni pale ambapo wanawake wa Kiislamu walipogoma na kuonyesha msimamo wa kutokukubali kuvuliwa Hijab zao na kupigwa picha na maafande wa kiume, mpaka pale walipopewa afande wa kike kwa ajili ya shughuli hiyo.

Sheikh Farid asema Unguja itakomboka
Msumbiji, Fuoni meli sita na Mbuyuni, ambayo kwa nyakati tofauti walishawishi na kuchochea watu kutenda makosa. Makosa waliyodaiwa kufanywa ni kuweka vizuizi barabarani kwa kutumia mawe, makontena ya kuhifadhia taka, matawi ya miti, mapipa ya mafuta, kuchoma maringi ya magari, kuharibu majengo tofauti, magari na kusababisha huduma muhimu za jamii za serikali kuweza kuharibwa na kusababisha hasara kuwa kwa watu binafsi na serikali. Shitaka la mwisho kwa washitakiwa wote hao ni la kula njama, ambapo sehemu tofauti zisizojulikana pamoja na muda wake ndani ya wilaya ya Mjini Unguja, kwa pamoja walidaiwa kula njama ya kusababisha Farid Hadi Ahmed kujificha katika sehemu ambazo hazijulikani na kupelekea uvunjifu wa amani katika jamii na kuzusha taharuki maeneo mbali mbali ya Zanzibar. Katika shitaka la nne la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, linamuhusu kiongozi mmoja wa Uamsho ni Azzan

Inatoka Uk. 2 shitaka la kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, ambalo linamkabili Azzan Khalid Hamdan pekee yake. Katika shitaka la uvunjifu wa amani chini ya kifungu cha 3 (d) cha sheria za Usalama wa Taifa sura ya 47 sheria ya mwaka 2002, washitakiwa wote hao walishitakiwa kwa kuhusishwa na matukio yaliyotokea Oktoba 17 na 18 mwaka huu kuanzia saa 12:00 za asubuhi hadi usiku wa manane. Katika shitaka hilo, kupitia barabara tofauti zilizomo ndani ya mkoa wa Mjini Magharibi Unguja walidaiwa kuharibu barabara, majengo, vyombo vya moto na pikipiki, na walifanya hivyo bila ya kuwepo sababu za msingi za kuharibu na kuteketeza kinyume cha maslahi ya umma na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi 5,000,000. Shitaka la pili linalowakabili ni la ushawishi na uchochezi, ambapo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa baina ya Mei 26 hadi Oktoba 19, 2010 watuhumiwa hao walifanya mikutano katika maeneo tofauti yakiwemo Lumumba,

Khalid Hamdan, ambalo katika shitaka hilo alidaiwa kumtolea maneno ya kashfa na matusi Kamishna wa Polisi wa Zanzibar Mussa Ali Mussa. Mbali na kudaiwa kumshambulia kwa matusi Kamishna huyo lakini pia kiongozi huyo alidaiwa kumwambia Kamishna huyo kuwa mjinga, jambo ambalo mahakama ilidaiwa kuwa lingeliweza kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii. Washitakiwa hao pia walitarajiwa kupandishwa tena katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe, mbele ya hakimu Ame Msaraka Pinja, kwa ajili ya kuendelea na kesi ya uchochezi wa kufanya fujo inayowakabili ambapo wiki iliyopita walipewa sharti gumu la dhamana ya kila mmoja kutakiwa kuwasilisha shilingi million moja taslimi na wadhamini watatu na kila mmoja aje na kiwango hicho cha fedha na awe na barua ya sheha na awe na kitambulisho vya Mzanzibari mkaazi na lazima wadhamini hao wawe ni wafanyakazi wa Serikali ya Mapnduzi Zanzibar.

6
Na Omar Msangi, Ramallah IJUMAA iliyopita Novemba 16, ilikuwa ngumu kwa Wa p a l e s t i n a . Wa k a t i mabomu na makombora yakivurumishwa Gaza, Yerusalem askari wa Israel walitanda kila mahali na hakuna mwanamume aliyeruhusiwa kuswali Ijumaa ila wazee tu. Kila aliye na umri chini ya miaka 50 hakuruhusiwa kupita vikwazo vya askari kwenda msikitini. Hayo yakijiri Yerusalem, Ramallah ilikuwa ni mapambano ya askari wa Israil wenye silaha kali na vijana wa Kipalestina waliokuwa wakivurumisha mawe. Ilikuwa mara tu baada ya mshuko wa Ijumaa watu walimwagika barabarani kuandamana, kwanza ikiwa ni kawaida yao kila wiki kuonyesha kupinga kwao uvamizi na ukaliaji wa kinguvu wa Israil katika ardhi yao. Na pili, kuwaunga mkono ndugu zao Gaza ambao kwa muda huo walikuwa wakishambuliwa na Israil. Tunafika katika makutano ya barabara mahali penye kizuizi cha polisi, tunakuta askari wengi wakifyatua risasi na mabomu ya machozi. Kwa mbele tunaona wanaolengwa ni vijana wa Kipalestina waliokuwa wakirusha mawe. Tunapita harakaharaka eneo hilo, mbele tunakuta askari wengine wakifyatua mabomu kuwatimua vijana waliokuwa wakiandamana huku wakiwarushia mawe askari wa Israil wakiwaambia watoke katika nchi yao. Tu n a p o f i k a h o t e l i n i tulipofikia tunakutana na wenzetu kutoka Canada ambao waliondoka asubuhi kuelekea Yerusalem kisha Tel Aviv kwa ajili ya kupanda ndege kurudi makwao. Wanasema wamekwama njiani kwa sababu ya mapambano ya vijana na askari wa Israil. Barabara zimefungwa. Wakati wa Isha unapoingia, kishindo cha risasi na mabomu kinasikika jirani na hoteli na tunaambiwa kuwa mitaani hakupitiki kwa sababu askari wa Israil wametanda mitaani ikitarajiwa kuwa kutakuwa na maandamano usiku kupiga mashambulizi Gaza. Kwa hiyo tunalazimika kubaki ndani japo tulitamani tungetembea kidogo kutizama mji ikiwa ni kuuaga kwa vile asubuhi yake ilikuwa tunaondoka kuelekea Amman, Jordan ambapo napo kupitia televisheni tunaona ghasia za kupinga serikali zinapamba moto.

Makala

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012
Labda niyaache hayo nigusie jambo moja lililojiri siku mbili kabla ambalo linahitaji maelezo. Ni saa saba adhuhuri adhana inasikika katika mitaa mbalimbali ya Bethlehem. Kama hukuambiwa utadhani kuwa upo Istanbul, Khartoum, Zanzibar au mji wowote wa Kiislamu. Kumbe upo mahali alipozaliwa Yesu (Nabii Isa a.s.) ambaye Wakristo wanadai kuwa ni mwana wa Mungu aliyekuja ili afe msalabani iwe ni kikomboleo cha dhambi zao. Wakati wito wa adhana, k u i t a Wa i s l a m u k a t i k a swala ukivuma, nilikuwa ndani ya Kanisa la Netivity lililojengwa mahali ambapo ndipo inapodhaniwa kuwa alizaliwa Yesu. Ni kanisa kongwe lenye vitu vingi vilivyohifadhiwa vya kale ikiwa ni pamoja na vifaa vilivyokuwa vikitumika katika ibada ndani ya kanisa hilo kwa mamia ya miaka yaliyopita. Zipo pia picha za makasisi walioongoza kanisa hilo kwa nyakati tofauti. Wakati huo kulikuwa na mamia ya watu ndani ya kanisa hilo. Sio kwa kufanya ibada lakini kama watalii toka sehemu mbalimbali duniani. Kwa nje kanisa hilo kubwa limezungukwa na misikiti iliyo hai kwa maana ya kuswaliwa swala za jamaa za kila siku. Jambo la kwanza ambalo huenda watu wengi hawalifahamu ni kuwa Yesu kazaliwa katika ardhi inayoitwa Palestina. Pili, watu wengi waliokuwa wakiishi alipozaliwa Yesu, walifuata Uislamu baada ya kuja Mtume Muhammad (s.a.w) ndio maana leo unakuta kuwa Waislamu ndio wengi Bethlehem na Yerusalem anapodaiwa kuteswa na kuzikwa Yesu. Kwa mujibu wa maelezo ya wenyeji nilioongea nao nikiwauliza ni kwa nini Wakristo ni wachache sana Bethlehem mahali ambapo ndipo alipozaliwa Yesu walisema kuwa zipo sababu kubwa mbili. Kwanza ni kuwa, Palestina ni ardhi ya Mitume toka Ibrahim, Is’haq, Yakoub ambao wote w a l i f u n d i s h a Ta w h e e d (Qur’an) na kwa hivyo suala la Mungu mmoja Muumba, ni kongwe kama ulivyo mji wenyewe. Kwa hiyo ukiwaambia kuna Mungu mmoja katika nafsi tatu (Utatu Matakatifu-Trinity), inakuwana dhana tata kwao. Kwa hiyo haikuwa rahisi kwao kukubali imani ya utatu na ndio maana hata Paulo alikimbilia kuanzisha Dini hiyo kule Antiokia (Ulaya) na Inaendelea Uk. 7

AN-NUUR

Unahitaji kuona kuamini

ASKARI wa Israel akiwafungulia geti watoto wa Qalqliah wakienda shule.

Hakuna kuswali Ijumaa ila wazee tu Bethlehem mji uliomkataa mwokozi Qalqilyah, mji gereza, kutoka kwa kibali

JUU bango likionesha muda wa kutoka na kuingia getini. Chini mtoto wa Shule kachelewa, Yahudi keshafunga lango hajui la kufanya.

7
Inatoka Uk. 6 alipokuja Mtume Muhammad (s.a.w) ilikuwa rahisi kwa Wapalestina kumkubali. Pili walisema kuwa hata wale Wakristo wachache waliokuwepo, mji huo ulipovamiwa na Israil, Wakristo wengi walikimbia wakiwaacha Waislamu ambao uzalendo wao ni mkubwa na wanaamini katika Jihad na kumtegemea Mwenyezi Mungu kutetea nchi yao, ardhi yao na haki zao na ndio mpaka leo wanapambana na Israil japo Israil ina maguvu ya kijeshi na ikiungwa mkono na mataifa makubwa. Pengine jambo jingine muhimu kusema hapa ni kuwa ardhi hii takatifu kwa Waislamu na Wakristo, hivi sasa ipo mikononi mwa Israil (Mayahudi) ambao hawamuamini Yesu wala kumfuata Mtume (s.a.w). Lakini kwa sasa wanaingiza pesa nyingi sana kupitia utalii kwa sababu watu wengi sana huja kuona alipozaliwa Yesu na anapodaiwa kuteswa na kuzikwa. Japo Bethlehem na ‘Tomb Garden’ zipo Palestina, lakini hivi sasa zinakaliwa kimabavu na Israil na kuingia hapo unaingia kwa kibali cha Mayahudi. Mpalestina ni marufuku kukanyaga hapo ila yule aliyezaliwa Yerusalem na amepewa kitambulisho rasmi. Nimeipa makala haya kichwa cha habari “Unahitaji kuona kuamini” kwa sababu yapo mambo huwezi kufikiria kuwa yanafanyika katika dunia hii ambapo Umoja wa Kimataifa (UN) na inayoitwa jumuiya ya kimataifa inapiga kelele kila siku juu ya haki za binadamu, uhuru, demokrasia na kuna na Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ambapo watu kadhaa washapelekewa huko. Sasa sikiliza: Qalqilyah ni mji mdogo katika PalestinaWest Bank, wenye idadi ya watu wasio pungua 50,000. Katika sensa ya 2007 walikuwa 47,730. Wavamizi Israil wameuzungushia mji huu mdogo ukuta mkubwa wenye urefu wa kilometa 700 kuzunguka mji mzima na urefu wa kwenda juu mita 8 hali inayoufanya mji huo kuwa kama gereza na kuacha lango moja tu la kutokea. Lango hilo hulindwa na askari na Wapalestina hawaruhusiwi kutoka hapo ila kwa muda maalum. Kwa upande mwingine Mpalestina asiye mkazi wa hapo, kwa maana ya kuwa hajapewa kipande maalum kutoka serikali ya Israil kuwa ni mkazi wa Qalqilyah, haruhusiwi kuingia hata kama ana ndugu zake humo. Kwa hiyo kama unakwenda shamba, kazini,

Unahitaji kuona kuamini
hospitali, watoto kwenda na kurudi shule; inabidi kuja kupiga foleni kusubiri lolote unalotaka kufanya nje ya Sinza/Kariakoo, lazima upitie lango linalolindwa na geti. Hayo ndiyo maisha ya kila siku ya Wapalestina wa

Makala

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012
Baraka Obama, Hillary Clinton, David Cameron, Umoja wa Mataifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa; ulishawasikia kuwasikia wote hawa wakizungumzia uvunjaji huu wa haki za binadamu?

AN-NUUR

WATOTO wa shule wakijaribu kupanda ukuta baada ya kufungiwa lango na askari wa Israel wakati wakirudi nyumbani kutoka shule. muda wa kufunguliwa lango. Ukichelewa, lango likifungwa hata kama ni mama mjamzito kashikwa na uchungu, atajifungulia au kufia hapo langoni maana Yahudi hatafungua lango mpaka muda ufike. Unafika asubuhi unakuta watoto wa skuli wamewahi wamepiga foleni wanasubiri askari wa Israil aje awafungulie. Wakitoka jioni ni hivyo hivyo. Kama kwa bahati mbaya mtoto atachelewa lango likafungwa, itabidi akatafute mahali pa kulala. Yahudi hatamfungulia mlango hata akilia vipi na akimghasi anaweza kumpiga risasi. Hebu jaaliya eneo lote la Sinza, Kijitonyama mpaka Mwenge au Kariakoo na Ilala yote linazungushwa ukuta mkubwa ambao mtu huwezi kuruka halafu kunawekwa lango moja tu la kutokea na kuingia. Halafu inawekwa ratiba ya kutoka na kuingia. Asubuhi saa 1 mpaka saa 3. Lango linafungwa, linafunguliwa tena saa 6 mpaka saa 9. Kisha linafungwa na kufunguliwa saa 11 mpaka saa 1 jioni. Kama unakwenda kazini, hospitali, shule na jambo askari wenye silaha kali. Utatoka kwa ratiba. We hata mkeo akishikwa na uchungu au mtu kapata kiharusi au ugonjwa wowote akawa mahututi, huwezi kuomba kupita kumpeleka mgonjwa hospitali ya Muhimbili au Mwananyamala/Amana nje ya ratiba ya kufunguliwa mji mdogo wa Qalqilyah kwa muda wa miaka 9 sasa. Ukuta huo ulijengwa mwaka 2003. Labda jiulize, kuna uvunjaji wa haki za binadamu uliozidi huu? Unageuza mji mzima kuwa gereza!! Jiulize tena, ulishawahi kumsikia Ban Ki-moon, Bila shaka hujasikia wala hujui kama kuna watu duniani wanafanyiwa unyama huo kwa sababu hiyo sio habari kwa BBC, CNN, Aljazeera, Sky News, Sauti ya Ujerumani (tunazoziona za maana sana)! Ndio maana nikasema, unahitaka kuona kuamini.

VIJANA wa Kipalestina wakimsaidia mwenzao aliyejeruhiwa katika maandamano mjini Ramallah Ijumaa iliyopita.

8
Na Ibn Rajab
KITABU cha Jan P. van Bergen, ‘Development and Religion in Tanzania,’ kimemnukuu Mwalimu Nyerere akisema kwamba maslahi ya dini yake (Ukatoliki) yanakuja mwanzo na kwamba kamwe hatokwenda kinyume na kanisa lake. Huu ni ushahidi wa wazi kwamba Nyerere alitawala nchi hii kwa maslahi ya kanisa lake. Ikumbukwe kwamba Waislamu wa Tanzania ndiyo waliokuwa wa kwanza duniani kuchangia fedha kwa ajili ya Wakatoliki waliotaka kujitenga nchini Nigeria katika jimbo la Biafra. Nyerere aliwachangisha fedha Waislamu wa Tanzania, ili zisaidie kupigana na Waislamu wenzao wa Nigeria. Harakati za Ukatoliki Nigeria, nchi yenye Waislamu wengi barani Afrika, zilitaka kulitenga jimbo la Biafra linalokaliwa na Wakristo wengi, ili kuepukana na kile walichoita “a calamitous slavery in an ocean of Muslims” (balaa la utumwa katika bahari ya Waislamu). Isitoshe, Nyerere alipoivamia Uganda mwaka 1979 na kumpindua Idd Amin Dada, inasemekana kuna askari walipewa maelekezo maalumu ya kuangamiza miji ya Waislamu nchini humo. Dk. Sengendo, msomi mashuhuri kutoka

Makala/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012
(World Council of Churches) au Shirikisho la Walutheri la Dunia (Lutheran World Federation). Kinyume chake, Waislamu wa Tanzania wamebanwa mno na hawana ruhusa ya kufungamana na taasisi yoyote ya Kiislamu katika ngazi ya dunia, iwe OIC au IOA (Jumuiya ya Kiislamu Afrika), kwa hoja kwamba Tanzania ni nchi ya Kisekula. Lakini Usekula ni Itikadi ya Kikristo (Mathayo 22:21) na inatoka mataifa ya Magharibi kama Marekani. Isitoshe, Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth), ambayo mkuu wake lazima awe Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana. Nimalizie tu kwa kutanabahisha kwamba mataifa ya Magharibi yana hamu kubwa na rasilimali za Tanzania na wanatamani kuitia nchi hii katika ukoloni mpya. Wanafanikisha ajenda yao hiyo kupitia makanisa. Kama wanalenga kuvuruga amani na utulivu wa nchi hii, ili wapate upenyo wa kuingia na kutukalia kimabavu, basi watasaidiwa na makanisa kukamilisha ajenda hiyo. Maaskofu na viongozi wa Serikali wasijifanye hawajui hilo. Makanisa ndiyo
yanayotumiwa na watu wa nje.

AN-NUUR

Uganda, alimwaga machozi pale Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, wakati alipogusia nukta hiyo katika mazungumzo yake na Waislamu mwanzoni mwa miaka ya tisini. Nyerere alimrejesha madarakani ndugu yake katika Msalaba, Milton Apollo Obote, Mkristo aliyemsaidia sana kuunda taifa la Tanzania kwa msaada wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), ambalo Mkurugenzi wake wakati ule alikuwa George Bush, ambaye baadaye akaja kuwa Rais wa Marekani. Ujenzi wa makanisa makubwa nchini Tanzania, wingi wa Seminari za Kikristo, utitiri wa mashirika ya Kikristo, idadi kubwa ya mapadri wa kigeni na masista wao makanisani, ni ushahidi mzito kwamba Taasisi za Kikristo hapa nchini, zina mafungamano na zinatumiwa na mataifa ya kigeni. Kwa sababu si rahisi, kwa michango ya waumini wao peke yake kuendesha shughuli hizo, ikiwa ni pamoja na kugharimia staili ya maisha ya juu ya viongozi wa makanisa. Makanisa yote ya

Makanisa ndiyo yanayotumiwa na mataifa ya nje sio Uamsho
Tanzania ni mali ya mataifa ya Magharibi, na huko ndiko yanakopewa maagizo na bajeti za kueneza Injili. Lakini ajabu, utawasikia viongozi wa Serikali wakiishambulia Jumuiya ya Uamsho, eti inatumiwa na maadui kutoka nje! Huku kutumika kwa makanisa hawaoni! Nadhani wanahitaji miwani. Kwa mfano, Kanisa Katoliki Tanzania ni mali ya Waitaliano, Wareno, Wahispania,Wabelgiji na Wafaransa. Kanisa la Kilutheri ni mali ya Wajerumani na Wadachi, waasisi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Kanisa la Anglikana ni mali ya Waingereza, Kanisa la Moravian ni mali ya nchi za Nordic(Sweden, Denmark, Norway), Kanisa la Pentekoste, Sabato, African Inland Mission na mengine kama hayo ni mali ya Marekani. Ushahidi mwingine wa mafungamano ya makanisa hayo na mataifa ya Magharibi ni ukweli kwamba makanisa yote katika nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwemo, yanachukuliwa kama “provinces” (majimbo), ikiimanisha kwamba yenyewe ni kama matawi tu, lakini uongozi wa juu kabisa wa makanisa hayo unatoka nchi za Magharibi badala ya nchi husika. Kuzagaa kwa makanisa mengi ya Kimagharibi nchini Tanzania, kumesababisha kuundwa kwa taasisi nyingi za Kikristo kama vile Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), chombo kinachowakilisha Wakatoliki, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (ELCT), chombo kinachowakilisha makanisa yasiyo ya Kikatoliki, Baraza la Wakristo Tanzania (CCT), chombo kinachojumuisha makanisa ya Kiprotestanti, Ofisi ya Askofu Mkuu wa Anglikana, Ofisi ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox la Ugiriki na Jumuiya ya taifa ya Kanisa la Bahai na mengineyo. Makanisa yote ya Tanzania, ama yamefungamana na Baraza la Makanisa Duniani

KINGDOM OF SAUDI ARABIA COMMITTEE OF DA-AWAH IN AFRICA

TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION
P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900, +255 754 208585, +255 752 245446. Email: info@tampro.org, Web: www.tampro.org

ZAWADI ZA MASHINDANO
Kamati ya Da-awah ya Afrika inawatangazia Waislamu wote kwamba zile zawadi za washindi wa mashindano kuhusu Familia ya Mtume (s.a.w.) na maswahaba (r.a.) yaliyofanyika mwaka huu 1433/ 2012, zitatolewa siku ya Ijumaa tarehe 23/ 11 / 2012 katika Msikiti wa Morogoro, Ilala Dar es Salaam maratu baada ya swala ya Ijumaa. Nyote mnakaribishwa. Wabillahi tawfiq

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA 2012
Jumuiya ya Wataalaam wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) inatoa taarifa ya kuwepo kwa Mkutano Mkuu wa Kumi na Tatu (13) wa wanachama wake. Mkutano huo utafanyika siku ya Jumanne na Jumatano, Tarehe 25-26 Desemba, 2012, kuanzia saa 2:00 asubuhi katika ukumbi wa Lamada Hotel Jijini Dar es Salaam. Siku ya Jumanne kutakuwa na semina juu ya “Cultural Transformation” na Uendeshaji wa NGOs, ripoti za matawi, kupitia Mpango Mkakati wa TAMPRO na kupokea salaam za wageni waalikwa. Siku ya Jumatano, Mkutano Mkuu utahusika na ajenda zifuatazo: Ufunguzi, Kuthibitisha akidi na Uanachama, Kupokea ajenda, Kuthibitisha wanachama wapya, Kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopita, Yatokanayo, Kupokea na Kujadili Taarifa ya Utendaji na Fedha 2012, Kuthibitisha wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini, Kupokea na Kujadili Mpango Kazi na Bajeti ya Mwaka 2013, Mengineyo, Kufunga. Wanachama wote mnaombwa kuhudhuria. TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA KATIBU MKUU BW. PAZI MWINYIMVUA

Kuwalenga raia: Mkakati maalum wa Israel
Na Steve Lendman
Novemba 27, 2012 - Mtandao wa kupashana habari WA B A B E h u c h a g u a washindani dhaifu kubamiza mangumi. Ushindani sawa hukwepwa. Ndivyo ilivyo katika viwanja vya shule au medani ya vita. Marekani na Israel hulka yao ni hiyo. Wanakwepa washindani ambao watawapa kiwango ambacho wao wametoa. Serikali za kihuni hazisemi kamwe ‘samahani.’ Katika Operesheni Funika Risasi mwezi Januari 2009, Profesa Jeremy Salt aliandika “Ujumbe kwa wapiganaji jasiri wa jeshi la anga la Israel.’ Aliyosema yanaonekana kwa kile kinachotokea sasa. Hivi unajisikiaje unapotupa makombora kwa watu usiowaona, aliuliza. Inasaidia kidogo (kisaikolojia) kutokuona unamwua nani? Dhamira yako inalainika kiasi kwa kufanya uharibifu mkubwa kwa watu wasioweza kujibu mapigo na kuvurugika kwa miundombinu ya kiraia? Unajisikia vyema kuua raia wanaume, wanawake, watoto na vichanga? Hii inakusumbua katika hisia zako, au unakuwa umetulia tu? Unalala vyema au unapata majinamizi kuhusu wanaume, wanawake na watoto ulioua nyumbani, vitandani, jikoni, sebuleni, shuleni, misikitini, kazini, au wakicheza? Hivi wakulima katika mashamba yao, kina mama na watoto, waalimu madarasani, maimamu misikitini, watoto wakicheza, wazee, wadhaifu au walemavu wanahatarisha usalama wako? Hivi kamwe unahoji ulichokifanya na kwa nini? Hivi huna haya, huna dhana ya ustaarabu, hujui kabisa tofauti kati ya jema na baya? Unaifahamu sheria? Kama ndivyo, kwanini unaivunja? Kufanya hivyo kunakuingiza katika wahalifu wa vita dhidi ya binadamu? Unafahamu hilo? Unafuata tu amri au una akili yako mwenyewe? Umewahi kuua raia kabla ya hapa? Utafanya hivyo tena kama ukiamriwa? Utaendelea kufuata amri kama kipofu au utafanya linalostahili? Wanaanga ‘jasiri’ wa Israel, askari, wanamaji na wapiganaji wengine ni vihoro. Wamekuwa wakifanya hivyo kwa miongo kadhaa. Kuteseka kwa Wapalestina ni mfumo wa maisha. Hebu fikiria kuishi kila siku na hujui utaishi au utakufa. Fikiria watoto wadogo wanaokua katika hali hiyo. Hivi watoto wa Israel wanajua kinachowapata watoto wa Palestina? Wanaambiwa? Wanajali? Wazazi wao je? Israel inapeleka maelfu ya askari na silaha nzito katika mpaka wa Gaza. Blogu ya DEBKAfile yenye uhusiano na Mossad, shirika la ujasusi la Israel, inasema: “Mkuu wa Majeshi Luteni Jenerali Benny Gantz na wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) wanaweka msukumo wa kuingiza majeshi Gaza, hatua ya pili ya Operesheni Mhimili wa Wingu, kuanza bila kuchelewa.” Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi wanapendelea kungoja. Mauaji mengine ya halaiki yanahofiwa. Raia huwa ndiyo wanaoteseka zaidi. Israel na Marekani wanadhamiria kuwalenga. Ni sehemu ya mkakati wa ukandamizaji wa nchi hizo mbili. Hawasumbuliwi na maisha ya watu, ni kupiga, kukandamiza na kunyonya. Funika Risasi ilikuwa na madhara ya kutisha, Makombora, mabomu, mizinga na silaha zisirohusiwa zilitumika dhidi ya watu wasioweza kujilinda, Mauaji ya watu wengi na uharibifu vilifuata. Vitendo vingi vya uhalifu mkubwa wa kivita vilifanywa. Maofisa wanaohusika bado hawajawajibika. Hapakuwa na azimio la Baraza la Usalama la kuzuia ndege zisiruke katika eneo la Gaza. Zaidi ya watu 1,400 wa Gaza waliteketea. Zaidi ya asilimia 80 walikuwa raia. Zaidi ya 300 walikuwa watoto. Takriban 5,300 walijeruhiwa. Zaidi ya 1,600 walikuwa watoto au vichanga. Israel iliwalenga kwa makusudi. Maeneo ya makazi, mashule, vyuo, misikiti, mahospitali, asasi za Umoja wa Mataifa, mitumbwi ya kuvulia, viwanda vya kiraia na karakana, majengo ya manispaa, mashirika ya misaada, miundombinu ya kiraia, na maeneo mengine yasiyo ya wapiganaji yalilengwa na kuvurumishiwa mabomu. Mashamba yalisambaratishwa na magreda. Njia za umeme na mifumo ya umwagiliaji viliteketezwa. Viongozi wa kimataifa hawakujali mauaji hayo ya watu na mateso. Ni askari watatu tu wa Israel wa ngazi za chini waliohukumiwa adhabu ndogo zisizo na maana. Familia ya al-Samouni ilipoteza watu 27. Salah alSamouni aliona mama yake akilipuliwa. Moto wa maroketi na mizinga ilimwua binti yake mwenye umri wa miaka miwili; baba, shangazi, binamu na familia yote. Majinuni wa vyombo vya habari hawakusema kitu. Wanaunga mkono uhalifu mkubwa wa Israel. Chini ya mzingiro, watu wa Gaza hawajapona madhara ya Funika Risasi. Sasa wanachelea uwezekano wa vita ambayo si ajabu ni mbaya zaidi ya ile ya 2008-09. Viongozi wa kimataifa wana sehemu yao katika dhulma hii kwa ukimya, kutojali, na/au kushiriki. Washington inahusika katika vita vyote vya Israel. Silaha, risasi na fedha zinatolewa. Kuungwa mkono kisiasa kunatolewa. Obama alimwambia Netanyahu, nenda kapige mabomu na mizinga utakavyo. Iite ‘kujihami’ na ujifanye kuwa hakuna anayejua kuwa sivyo. Hapo Novemba 15, Baraza la Senate lilipitisha azimio kwa kauli moja lisilo la kisheria la kuunga mkono. Hapakuwa na sauti iliyoinuliwa kupinga azimio hilo. AIPAC (kundi la kuhamasisha kuungwa mkono Israel katika Bunge la Marekani) liliwashukuru Obama na wajumbe wa Senate kwa kuiunga mkono Israel. Raia wa Gaza na wapiganaji wa kujihami wanatungiwa jina la magaidi. Ni mashujaa, si wahalifu. Novemba 14, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Mtandao wa Kupinga Kashfa (Anti-Defamation League, ADL) Abe Foxman alieleza kuunga mkono upigaji mabomu wa Israel na mizinga, akisema “Israel imeonyesha uvumilivu mkubwa mbele ya utupwaji wa maroketi na makombora kutokea Gaza. Operesheni hii inalenga moja wa moja uongozi unaohusika na mashambulio haya, pamoja na maghala na hifadhi nyingine za silaha zao.” “Hakuna nchi duniani ingekaa kimya na kuachia mashambulio kama hayo dhidi ya raia zaidi ya milioni moja.” “Jumuia ya Kimataifa ina jukumu la wazi la kulaani mashambulio haya na kuunga mkono hatua zilizochukuliwa na Israel dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi yanayofanyia shughuli zake Gaza wakati Israel ikitekeleza wajibu wake wa kwanza kulinda raia wake.” Kwa karibu karne moja, ADL ilikuwa jukwaa la kunadi ubabe wa Kiyahudi. Inaunga mkono hulka za kutumia mabavu kwa ukali katika kuikalia Palestina. Haijali mateso ya Wapalestina. Inaanzisha kampeni za kuwachafua wakinzani wake. Historia yake yote inachefua. Uhalifu wa Israel unaitwa kujilinda. Inacheza mchezo ule ule wa mlaumu mwathirika, kama Israel, Washington, AIPAC na asasi nyingine za Kizayuni. Ni haki za Wayahudi tu zenye umuhimu. Wapalestina wanageuzwa magaidi kwa kujilinda. Israel ilikubali kusimamisha operesheni za kijeshi wakati Waziri Mkuu wa Misri Hersham Kandil akiwa anatembelea Gaza. Yeye na mawaziri wengine wa Misri walifika Gaza siku ya Alhamisi. Alirudi Ijumaa. Mashambulio ya Israel

9

Makala/Tangazo

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

yaliendelea. Katika hospitali ya Al Shifa, Kandili aliwatembelea waathirika. Alilaani mashambulizi ya Israel, akisema: “Mkasa huu hauwezi kupita kimya kimya, na dunia lazima iwajibike kuzuia ushambuliaji huu.” Cairo itajitahidi kutafuta njia ya kurudisha amani, aliongeza. Kuanzia Jumamosi, zaidi ya Wapalestina 40 waliuawa. Mamia wengine walijeruhiwa. Wengi wako mahututi. Dazeni za mashambulizi ya ndege zinaendelea. Vifo na majeruhi vinaweza kuongezeka kwa kasi kubwa. Matarakimu ya hivi sasa yanadumaza athari halisi kwa sababu baadhi ya waathirika wamelala chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa. Kituo cha Kimataifa cha Habari za Mashariki ya Kati (IMEMC) kilisema Israel ilifanya mashambulizi 30 katika muda usiozidi dakika 30 siku ya Ijumaa. Kunako saa nne usiku Alhamisi, jeshi la Israel lilisema lilipiga maeneo lengwa 70 katika saa nzima iliyopita. Maeneo ya raia na majengo ya serikali yalipigwa mabomu na mizinga. Shule mbili za Umoja wa Mataifa zilipigwa. Uharibifu

Inaendelea Uk. 11

UBUNGO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGE
P.O. Box 55105, Dar Es Salaam Tel: 2450069 Fax: 2450822, Mob: 0712557099, TANZANIA

NAFASI ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO UALIMU WA MAARIFA YA UISLAMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI - 2013
Tunachukua fursa hii kuwatangazia Waislamu wanaume na wanawake nafasi za mafunzo ya Ualimu wa Maarifa ya Uislamu kwa shule za Msingi na Sekondari yatakayoanza Februari 2013. SIFA NA MASHARTI YA KUJIUNGA Muombaji atimize sifa na masharti yafuatazo:(i) Awe amemaliza juzuu ya 1 na 2 ya Maarifa ya Uislamu Darasa la Watu wazima kabla ya kujiunga. (ii) Awe amehitimu darasa la saba au kidato cha nne na awe anafundisha Madrasa au Maarifa ya Uislamu katika kipindi cha dini shule za Msingi au Sekondari kwa muda usiopungua mwaka mmoja. (iii) Awe anajua kusoma Qur’an kwa ufasaha. FOMU ZINAPATIKANA CHUONI UBUNGO KWA GHARAMA YA SHILINGI ELFU TANO TU. MUHIMU • Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 30/11/2012. • Usaili utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 01/12/2012 saa 2 asubuhi. Wabillah Tawfiiq MKUU WA CHUO

10

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

Huu si wakati wa maneno, tunahitaji vitendo Gaza!
Na Mwandishi Maalum majeshi ya uvamizi, kama w a l i v y o Wa i s l a m u w a Palestina. Nchi za Kiarabu zinazoizunguka Palestina, zina uwezo wa kutosha kijeshi, kuikomboa ardhi iliyoporwa ya Palestina na kumaliza kabisa ukandamizaji unaofanywa na Israeli dhidi ya Wapalestina. Lakini nani afanye hivyo! Kuna zaidi ya askari milioni 2, katika eneo la Mashariki ya Kati, wenye matumizi ya zaidi ya Dola Bilioni 100 kwa mwaka kwa ajili ya silaha tu. Misri peke yake, ina ndege za kivita 220 za F-16, ambazo ni za kisasa kabisa na jeshi bora lenye askari 450,000. Hivi hawa Mayahudi wana nguvu kiasi gani kushinda jeshi hili? 3-Tatizo ni watawala vibaraka katika nchi za Waislamu. Hawa ndiyo walinzi halisi wa Israeli. Wa t a w a l a h a w a n d i y o wanaozuia majeshi ya Waislamu katika nchi zao kutimiza jukumu lao. Kutoa tu matamko ya kuilaani Israeli na kuitisha vikao vya dharura hakuna maana yoyote, wakati bado wanaendeleza uhusiano wa kidiplomasia, kibiashara na ushirikiano wa kijeshi na Israeli. Kila Israeli inapofanya vitendo vya kihalifu dhidi ya Wapalestina wasio na hatia, watawala hawa katika nchi za Waislamu wataishia tu kutoa matamko matupu ya kulaani, ikiwa ni pamoja na kuitisha vikao vya dharura vya Jumuiya ya nchi za Kiarabu (Arab League). Watapiga domo na mwisho wake ni hapo hapo. Wanasubiri shambulio lingine la Israeli! 4-Serikali mpya ya Misri, inayoongozwa na Dk.Mohammed Mursi, sasa ndiyo inatakiwa ionyeshe kwa vitendo kama kweli iko pamoja na Waislamu duniani, ambao wanatarajia jeshi la Waislamu kuwalinda ndugu zao wanaoangamizwa kwa mabomu Gaza, ikiwa ni pamoja na kufanya harakati za kuikomboa Palestina. Waislamu duniani kote hawatarajii Misri kuwasaliti Waislamu wenzao wa Gaza katika kipindi hiki ambacho wanahitaji mno msaada wao. Hatudhani kwamba Utawala wa Misri ni sura mpya tu zinazotekeleza sera zile zile za mabeberu za kudumisha ‘amani’ na serikali ya Kizayuni ya Israeli. 5-Nchi za Waislamu katika eneo la Mashariki ya Kati na kwengineko zinahitaji kutawaliwa Kiislamu - ziwe na watawala kama walivyokuwa

SIKU ya Jumatano, Novemba 14 mwaka 2012, majeshi ya Israeli yamemuua Ahmed Al-Jabari, kamanda wa kijeshi wa Hamas, mtoto wake wa kiume na Wapalestina wengine kadhaa. Mashambulizi dhidi ya Gaza bado yanaendelea na idadi ya Wapalestina waliouawa na kujeruhiwa kupitia mashambulizi hayo inazidi kuongezeka kila uchao. Watu wengi duniani, kwa usahihi kabisa, wamelaani kitendo hiki cha kihalifu. Kufuatia matukio hayo, ni vizuri kuweka bayana nukta chache zifuatazo, ili kuwafanya wasomaji watafsiri matukio hayo kwa kutumia akili zao wenyewe, badala ya kulazimishwa na vyombo vya habari. Ajabu ya Rahman, vyombo vya habari vya Magharibi vinajenga picha ulimwenguni kana kwamba Wayahudi ndiyo wanaokandamizwa na Wapalestina, kwa hiyo wana haki ya kujihami kwa kuwaangamiza kwa makombora! 1-Mashambulizi ya kinyama ya Israeli dhidi ya Wapalestina wa Gaza, yanathibitisha wazi kwamba taifa hili la kiyazuni halina heshima hata kidogo na uhai wa binadamu. Hawajali kitu kwa sababu walishalaaniwa pia katika mauaji waliyofanya mjini Jenin, Lebanon na Gaza siku za nyuma. Miito ya ‘mchakato wa amani’ (peace process) katika eneo la Mashariki ya Kati, inazidi tu kuiimarisha Israeli dhidi ya Wapalestina. Ufumbuzi wa kuunda dola mbili zilizo sambamba (A two-state solution), yaani dola ya Israeli na Palestina, kama unavyopendekezwa na mataifa ya Magharibi, utazidi tu kuwatia utumwani Waislamu wa Palestina. Kwa sababu dola ya Wapalestina itakuwa dhaifu mno na uzoefu unaonyesha kwamba haitaundwa na Wapalestina wenyewe. Matukio ya mara kwa mara ya utumiaji nguvu, vitendo vya mauaji, vitisho na kibri, ndiyo majibu ya madhalimu wote katika historia, katika kuhalalisha mauaji na ukandamizaji wao ili waweze kuwepo. Bila ya hivyo hawawezi kuwepo ng’o! 2-Ni majeshi tu ndiyo yanayoweza kuwalinda watu wanaokaliwa kimabavu na

akina Salahuddin Ayubi au Muhammad al Fatih. Watawala hawa walihamasisha majeshi yao, walikomboa ardhi zilizokaliwa kimabavu na kutawala nchi za Waislamu kwa haki, amani na utulivu. Ukisoma historia ya Mashariki ya Kati, utaona kwamba hakuna kipindi ambacho eneo hili lilikuwa tulivu zaidi na lenye amani kuliko kipindi kile lilipotawaliwa Kiislamu. Huu ni ukweli ambao mabeberu wa Magharibi hawawezi kuusema ingawa wanaufahamu. 6-Kuungwa mkono kwa Israeli na Mataifa ya Magharibi, kama Marekani na Uingereza, kusiwashangaze sana watu. Wazo la kuundwa Israeli ni la Serikali ya Uingereza kupitia azimio la Balfour. Taifa hili la Kizayuni katikati ya mataifa

ya Waislamu, limekuwa likilelewa na kuimarishwa na mataifa ya Magharibi kwa miaka mingi, ili kulinda maslahi yao katika eneo la Mashariki ya Kati. Bila shaka watajaribu kufufua mazungumzo yaliyokwama ya mpango wao wa ‘Road Map’ kuelekea ‘two - state solution’ kwa maslahi ya mataifa yao. Lakini kwa Waislamu wa Palestina, mpango huo ni maangamizi kwa sababu unahalalisha kukaliwa kimabavu. Palestina inahitaji kukombolewa kabisa kutoka kwenye makucha ya Israeli. Huu si wakati wa mikutano, vikao vya wakuu wa nchi za Kiarabu, wala mazungumzo ya kuleta amani. Israeli kwa mara nyingine tena imemwaga d a m u y a Wa i s l a m u w a Gaza, na Mwenyezi Mungu

ameamrisha Jihad kama suluhisho kwa vitendo hivyo vya woga vinavyofanywa na Israeli. Majeshi ya Waislamu duniani kote yaitikie wito wa Mwenyezi Mungu pale aliposema: “Hawawi sawa Waislamu wanaokaa wasende vitani, isipokuwa wenye dharura. (Hawawi sawa) na wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewafadhilisha katika cheo wale wapiganao katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa nafsi zao na mali zao kuliko wakaao (wasende kupigana). Ingawa Mwenyezi Mungu amewaahidi wote (kupata) wema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhilisha - wale wapiganao kuliko wakaao - kwa ujira mkuu” Qur(4:95).

KONGOWE- MJI WA KIBAHA VINAUZWA (SURVEYED PLOTS AT KONGOWE- KIBAHA TOWNSHIP) Plan Na E`373/109 Reg. No. 70995 Plots No. Eneo / Sqm Bei 5 2,259 13,554,000 6 1,566 9,396,000 8 1,984 11,904,000 9 3,564 21,384,000 10 2,842 17,052,000 11 3,732 22,392,000 15 2,292 13,752,000 16 2,367 14,202,000 17 2,423 14,538,000 NB: Kila Sqm ni shilingi Elfu 6000/tu. Kilo Mita Moja kutoka Barabara ya Morogoro, Kuna Umeme, Maji na Barabara. Kwa mawasiliano zaidi piga simu zifuatazo. 0755 090754 au 0715 090 754

VIWANJA VILIVYOPIMWA

Kuwalenga raia: Mkakati maalum wa Israel
Inatoka Uk. 9
mkubwa uliripotiwa. Kituo cha kutafiti hali za wafungwa cha Ahrar kilisema kanisa lililokuwa linajengwa lililengwa. IMEMC ilisema “Watoto, vichanga, wanawame na vikongwe ni kati ya waliouawa, ikiwa ni pamoja na watoto ambao miili yao iliharibiwa vibaya na kuungua kutokana na makombora ya Israel. Mama mjamzito na kichanga chake tumboni ni kati ya waliouawa.” Wapiganaji wa kujihami wa Gaza walisema hawataheshimu masharti ya kuacha mapigano mradi Israel inaendelea kuua wanaume, wanawake, watoto, vichanga na vikongwe Palestina. Alhamisi jioni, nyumba moja ya Beit Hanoun ilipigwa bomu. Watoto watatu walikufa. Mmoja alikuwa na miaka tisa. Kichanga cha miezi kumi kiliuawa wakati nyumba nyingine ilipopigwa. Kipindi chote cha Ijumaa asubuhi, takriban watoto wanane, mama mjamzito na vikongwe wawili wanaume walikufa. Askari wa akiba 30,000 waliitwa. Livu za kijeshi zilifutwa. Vifaru, magari ya deraya na askari walikusanywa katika mpaka wa Gaza. Uvamizi unahofiwa kufuatia. Hapo Novemba 16. Mathaba alisema Tume ya Uhalifu wa Kivita ya Kuala Lumpur (KLWCC) nchini Malaysia “ilipokea malalamishi mengi kuhusiana na vitendo vya kinyama na uwezekano wa uhalifu wa kivita uliofanywa dhidi ya watu wa Palestina.” Novemba 20 na 21, siku mbili za kutoa ushahidi zimewekwa. Wajumbe wa tume ni pamoja na hakimu wa zamani Musa Ismail, mkuu wa zamani wa kitivo katika Chuo Kikuu cha Tekinolojia (MARA) Zulaiha Ismail, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kimataifa Michel Chossudovsky na wasimamizi wawili wa zamani wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya kibinadamu nchini Irak, Hans von Sponeck na Denis Halliday. Hapo Novemba 16, mtandao w a A l t e r n a t i v e N e w s . o rg uliandika “Hakuna pa kujificha: Raia wako chini ya mashambilizi eneo la Gaza.” Shuhuda mmoja alifika hospitali ya Al Shifa. Raia wengi wa Gaza waliojeruhiwa wako katika hali mbaya. Salem Waqef, mwenye unri wa miaka 40 alipata jeraha la ubongo. Yuko mahututi akisaidiwa na mashine ya kupumua. Hakuna uhakika kama ataishi. Haneen Tafesh mwenye umri wa miezi kumi alilazwa akiwa hana fahamui. Alipaja jeraha la fuvu la kichwa na kutokwa damu katika ubongo. Naye pia ni mahututi akipumua kwa mashine. Madaktari walisema hali yake iliharibika kuanzia alipolazwa, Saa chache baadaye akafa. Ahmed Durghmush alipata mshtuko wa ubongo. Chembe za risasi zilipenya fuvu lake. Ubungo ukatokeza katika jeraha lake. Hali yake pia iliharibika baada ya kufanyiwa upasuaji. Muda wote Alhamisi, wauguzi wa chumba cha dharura walikuwa wakiwahangaikia wagonjwa wapya. Majeruhi ni kuanzia wanaotibiwa kwa urahisi hadi waliojeruhiwa vibaya na hadi walio hatarini kufa. Mkurugenzi wa habari wa Wizara ya Sheria, Khalid Hamad, alikuwa nyumbani kombora lilipopenya nyumba ya jirani yake. Israel “ililenga raia kwa makusudi,” alisema. “Majeshi ya Israel hayafanyi makosa.” Duaa Hejazi mwenye umri wa miaka 13 aliletwa “akivuja damu ana.”Alipata majeraha ya risasi sehemu za juu za mwili. Chembe bado ziko kifuani mwake. Alipeleka ujumbe kwa watoto wengine wa Gaza, akisema: “Nasema, sisi ni watoto. Hakuna kilicho makosa yetu ili kuhitaji kupata mikasa hii, Wanakalia nchi yetu na nitasema, kama Abuu Omar alivyosema. Kama wewe ni mlima, upepo hautakutikisa. Hatuna woga. Tutabaki na nguvu.” Mkurugenzi Mkuu wa Al Shifa Dk. Mithad Abbas alieleza mazingira magumu ambako wahudumu wa hospitali inabidi wakabiliane, akisema: “Pale majeruhi wanapowasilishwa hospitalini mwetu, siyo katika mazingira ya kawaida. Wanakuja kama nyongeza ya uzingirwaji, uzuiwaji wa kuagiza vitu nje, ambako kumesababisha kukosekana kwa dawa muhimu na mahitaji mengine ya tiba.” Al Shifa ina upungufu wa dawa muhimu, vifaa muhimu na mahitaji ya akiba. Hizi ni pamoja na tembe za kumeza kuua wadudu mwilini (antibiotics), maji ya dripu, vileta ganzi, glovu, visafishaji, vitendea kazi kadhaa na vifaa vingine muhimu vya kitiba. Kukatwa umeme kunazidi masaa 12 kwa siku. Akiba kidogo ya mafuta inawezesha operesheni katika nyakati hizo. Dk. Abbas alisema akiba yake itaisha katika siku chache kama hali iliyo hivi sasa inaendelea. Hajui ni wapi kombora jingine litaangukia au bomu litalipua. Labda Al Shifa italengwa. Israel inaona asasi yoyote ya kiraia ni mawindo halali. Hapo Novemba 15, Harakati ya Kimataifa ya BDS (ya kuitenga, kuondoa uwekezaji na kuiwekea vikwazo Israel) ilitoa taarifa iliyosema, kwa uchache: “Zuia Mauaji Mapya ya Israel katika Gaza: Itenge Israel Sasa!” Licha ya taarifa zinazoelemea upande mmoja za vyombo vya habari vya Magharibi, Israel “ilianza na kuendeleza mashambulio haya mapya katika kipindi cha kujiandaa kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa, kuyakinisha busara kongwe nchini Israel ya miili ya Wapalestina kupata kura.” “Israel itaendelea kufanya mashambilizi, kutesa na uharamia wa dola kama haitahitajiwa kulipa gharama kubwa kwa maovu yake dhidi ya watu wa Palestina, Lebanon na wengine katika nchi za Kiarabu.” Ni muda muafaka wa BDS dhidi ya Israel. Hii ndiyo njia iliyo wazi zaidi kufikia uhuru, haki na usawa kwa Wapalestina na eneo lote.” Kinacholeta wasiwasi pia ni kura itakayopigwa Novemba 29 kuhusu uanachama muangalizi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa. Israel na Marekani zimefanya kila juhudi kuvuruga, Nchi wanachama wana kila sababu ya kuiunga mkono Palestina. Tutajua, chini ya wiki mbili. Kiongozi wa Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah aliwataka wakuu wa nchi za Kiarabu kutumia njia zote wanazoziweza kusimamisha mashambulio ya Israel katika Gaza. “Hakuna anayeziambia nchi za Kiarabu leo, ‘Tafadhali nenda fungua mipaka yako na anza operesheni kuikomboa Palestina.’ Tunachotaka ni kumaliza mashambulio Gaza.” Haya ni mapambano ya kila mtu.... Hatukuhitaji utoe jawabu. Tunataka jitihada.” “ We n g i n e w a n a s e m a Waarabu hawana ujasiri wa kuzuia uzalishaji mafuta. Punguza uuzaji nje wa mafuta au pandisha bei kidogo na utaitikisa Marekani,. Utaitikisa Ulaya.” “Ndugu zangu, kama hamwezi kukatisha mafuta, punguza uzalishaji au pandisha bei. Weka msukumo kidogo. Hakuna anayehimiza majeshi au vifaru au ndege za kivita.” Nasrallah aliyataja mashambuliizi ya Israel

11

Habari

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23 - 29, 2012

AN-NUUR

“mashambulizi ya kiharamia.”Uhalifu mwingi wa kivita na dhidi ya binadamu unafanyika. Mengi yako hatarini Palestina, eneo la Mashariki ya Kati na nje ya hapo. Mashambulizi ya kivita ya Washington yanaendelea. Vita nyingine zinapangwa. Israel ni mshirika muhimu. Nchi hizo mbili zina ajenda za kibabe juu ya nchi nyingine. Vita ni njia muhimu ya kuzifikia. Michel Chossudovsky anaita kushambuliza na kuvamia Gaza”sehemu ya ajenda pana ya kijeshi ya Marekani-NATO na Israel.” Kwa msingi wa kile kilichotokea baada ya 9/11, tarajia mabaya zaidi baadaye. (Makala hii Targeting Civilians: Israel’s Specialty iliyoandikwa na Steve Lendman, imefasiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija)

Waislamu wataka kujua atma ya TV yao Imaan
Inatoka Uk. 1

ada inayohitajika wamelipa ikiwa ni pamoja na kutoa maelezo ya sera na ratiba ya vipindi. Hata hivyo akasema, kwa muda mrefu wamekuwa wakizungushwa kupata CP na bado wanafuatilia kibali hicho. Mwenyekiti huyo wa TV Imaan ametoa maelezo hayo kufuatia malalamiko kutoka kwa Waislamu wengi waliotaka kujua ni kwa nini mpaka sasa TV hiyo haijakuwa na Studio na kuanza kurusha vipindi. Kwa muda mrefu sasa, TV Imaan imekuwa katika majaribio ambapo ilitarajiwa kwamba mpaka sasa wangekwisha kamilisha taratibu zote zilizowekwa na Mamlaka husika, yaani Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), na hivyo kuanza kurusha matangazo rasmi. Kwa muda sasa baadhi ya Waislamu wamekuwa wakihoji, ni kwa nini TV Imaan haianzi kurusha matangazo na imebaki tu katika kufanya majaribio katika satelaiti. Kufuatia malalamiko ya Waislamu waliofika katika ofisi za An nuur, Mwenyekiti wa TV Imaan ameongea na mwandishi akisema kuwa kwa upande

wao wametimiza mashariti yote na kwamba hata wao wanajiona wapo katika wakati mgumu kwa sababu wanajua hamu waliyo nayo Waislamu kuona TV yao ikiwa hewani. Akasema, bado wanafanya subra wakiamini kuwa TCRA itawapa kibali kinachohitajika, lakini kama muda utazidi kuwa mkubwa watalazimika kuwaita Waislamu waliokusanyika pale Uwanja wa Taifa Dar es Salaam na Arusha ili kuwaeleza vikwazo wanavyokumbana navyo katika kuanzisha TV hiyo. Akifafanua Aref amesema kuwa hawataweza kuepuka kuwaita Waislamu kama watakwama kwa sababu kama Waislamu walivyochangia fedha zao, wana haki pia ya kujua nini kinakwamisha TV hiyo kuanza. Akieleza hatua w aliy o f i k i a a m e s e m a kuwa walipewa mambo ya kutekeleza yakiwa ni kupata mkataba na “MUX Operators” ambapo wameshaingia mkataba na Star Media (T) Limited. Jambo la pili lilikuwa kuwasilisha sera ya TV (Editorial Policy) ambayo washapeleka na tatu kulipa ada ya dola 1,500 ambayo nayo washalipa. Aref amesema, ni imani yao kuwa TCRA watawapa kibali hicho, CP, kabla ya shinikizo kutoka kwa

Waislamu kuwazidia nguvu na kuamua kwenda tena Uwanja wa Taifa kujieleza kama walivyojieleza wakiomba michango ya Waislamu. Kwa upande wa TCRA, An nuur iliwasiliana na F. N. Ntobi na Chacha ambao ni katika maofisa waandamizi wa taasisi hiyo ambao walisema kuwa kama TV Imaan wana malalamiko, hawana sababu ya kusemea pembeni, bali wafike waonane na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka. Hata hivyo, kwa upande wa TV Imaan, wanadai kuwa walishawasilisha malalamiko yao kwa Mkurugenzi huyo baada ya kuona wanazungushwa sana katika ngazi za chini. Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mkuu (TCRA DG) Kumb. Namba TVI/ T C R A / V. 0 4 / 2 0 1 2 y a tarehe 6 Novemba, 2012, Mwenyekiti wa TV Imaan Aref Nahdi baada ya kutoa vielelezo vya kukamilisha mashariti waliyopewa, alimwomba DG huyo kuingilia kati suala hilo kwa vile kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakipewa ahadi hewa. Akamalizia kwa kasema kuwa kuchelewa kwao kutoa kibali, kunasababisha sintofahamu baina ya viongozi wa TV Imaan na Waislamu waliotoa sadaka zao kwa ajili ya TV.

AN-NUUR
12
Na Bakari Mwakangwale
TAASISI za Kiislamu nchini zimetakiwa kuwasaidia vijana wa Kiislamu wasiokuwa na uwezo wa kujilipia ada ya masomo ya Vyuo Vikuu ili kuendeleza Uislamu na wataalamu kwa ujumla. Wito huo umetolewa na Mweyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro, Dr. Mussa Assad, mbele ya Mkuu wa Chuo hicho katika mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo, mwishoni mwa wiki iliyopita. Akisoma nasaha hizo kwa niaba ya Dr. Assad, Bw. Ahmad Sagafu, aliye mjumbe wa Baraza la Chuo hicho alisema, kutokana na idadi kubwa iliyopatikana mwaka huu kwa vijana wengi wa Kiislamu kukosa mkopo toka Serikalini kupitia Bodi ya Mikopo, ni vyema Taasisi za Kiislamu zikajipanga ili kuwanusuru vijana hao siku za mbele. “ili kusaidia wanachuo wasiokuwa na uwezo wa kujilipia kwa ajili ya masomo yao, na haswa wanapokosa mkopo wa serikali, Taasisi za Kiislamu nchini zingejipanga katika kusaidia kuwalipia wale wanachuo wasio na uwezo ili kuuendeleza Uislamu na wataalamu nchini.” Alisema Bw. Sagafu. Wito huo kwa Taasisi za Kiislamu umekuja kufuatia wanafunzi wapatao 1600, ambao walitegemea kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo, kukosa mikopo hiyo, hivyo kushindwa kujiunga na Chuo. Alisema, hali hiyo imesababisha na kuchangia upungu wa wanafunzi waliotarajiwa kujiunga Chuoni hapo, baada ya kukosa Mikopo na kutokuwepo njia mbadala ya kuweza kuwanusuru na kuwasaidia vijana hao kujiunga na Chuo. “Upungufu huo unatokana

MUHARRAM 1434, IJUMAA NOVEMBA 23-29, 2012

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa na Jumanne
program tano za masomo, akizitaja kuwa ni Shahada ya Sanaa na Ualimu, Shahada ya Maarifa ya Uislamu na Ualimu, Shahada ya Mawasiliano ya Umma, Shahada ya sayansi na Ualimu pamoja na Shahada ya Lugha na Ukalimani. Alisema, kwa muda huo mfupi toka kuanzishwa kwa Chuo hicho, jina la Chuo limestawi na kuchanua vilivyo, kutokana na kuaminiwa na Watanzania wengi kutokana na ubora wa taaluma na malezi yatolewayo. Alisema, hali hiyo inajidhihirisha kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaoomba kudahiliwa katika Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro. Alisema, kwa mwaka huu wa masomo 2012/2013, jumla ya wanafunzi 1800, wenye sifa zinazostahili waliomba na kupewa fursa ya kusoma katika Chuo hicho, hata hivyo alisema baadhi yao wameshindwa kujiunga na masomo kutokana na kukosa Mikopo. Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Hajjat Mwantumu Malale, amewataka wahitimu kufungamana na Uislamu kwani Uislamu ndiyo njia sahihi ya maisha ya mwanaadam. Alisema, baada ya kutoka chuoni hapo, ni vyema waka wa mabalozi wazuri wa Chuo hicho na Uislamu kwa ujumla, kwani msomi Muislamu ni lazima awe tofauti na yule ambaye si Muislamu. Ama kwa upande wa wazazi, Hajjat Malale, aliwataka kuwa karibu na watoto wao toka ngazi ya chini ya kimasomo, kwani wao ndio msaada mkubwa katika hatua ya kijana anapohitaji kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu. Aliwataka wazazi kujiandaa mapema kwa ajili ya kuwalipia watoto wao ada ya elimu ya juu kutokana na hali ilivyo sasa, kwani hakuna uhakika wa moja kwa moja wa kupata Mikopo. Alisema, katika awamu hii ya mwaka 2012/2013, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kukosa Mikopo, toka Serikalini na miongoni mwao wamekwama kujiunga na vyuo. Alisema, ni vyema wazazi wakawa msaada kwa kuangalia njia mbadala ya kupata fedha ili wawawezesha watoto wao kujiunga na elimu ya juu, kwani anaamini wanaweza. Alisema, badala ya ndugu na wazazi kuchangisha pesa kwa ajili ya ngoma, Kitchen part, sendoff na hata harusi ambavyo hutumia pesa nyingi, ni vyema mwenendo huo ukabadilika na michango hiyo ielekezwe katika maswala ya elimu.

Taasisi za Kiislamu zisaidie wasiopata mkopo wa Bodi
Wahitimu MUM watakiwa kuwa mfano kwa jamii Hajat Malale awataka kushikamana na Uislamu

Masheikh waende vijijini
Na Abuu Khadija
Masheikh na wanazuoni wengi wa Kiislamu wamejisahau kuwafikia Waislamu wa vijijini na zaidi wameamua kijikita mijini, hususani Jijini Dar es Salaam. “Masheikh wengi wenye elimu wapo Jijini tu wakifanya mihadhara ya kiimani lakini wamejisahau kufika na huku vijijini kwani huduma yao ya kiimani inahitajika sana. Huku vijijini wengi wetu ni Waislamu lakini wanakosa elimu ya dini kwa kuwa walimu hakuna.” Alisema imam Kongoro. Alisema, pamoja na kuwa wana msikiti lakini wanakabiliwa na tatizo la kupata waendeshaji wa Madrasa za watu wazima na watoto. Hajjat, Gama, alifanya ziara hiyo baada ya kutoka kuhiji Makka mapema hivi karibuni, ambapo alifika kuwatembelea wajane na watoto yatima wapatao 20, waliopo katika Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani. Katika ziara hiyo, Hajjat Gama, alitoa sadaka kwa watoto na wajane hao huku akikabidhiwa ardhi ya ukubwa wa heka moja kwa ajili ya kuwajengea kituo maalum kwa ajili yao chini yake.

MKUU wa Chuo cha Waislamu Morogoro (MUM) Hajat Mwantum Malale (katikati) akiwa na baadhi ya wahitimu mara baada ya kutunukiwa shahada zao wiki iliyopita chuoani hapo. “Waliofanikiwa kumaliza na ukweli kwamba wanachuo kuanzishwa kwake mwaka masomo yao salama na ambao waliopata mikopo ni 251 tu, 2005, alisema jumla ya wahitimu leo (Jumamosi iliyopita) kutoka kwenye orodha ya 509, wamefanikiwa kumaliza wanatunukiwa shahada zao ni wanachuo 1800 waliopatiwa masomo yao salama na kustahiki 509. Nawaombea kwa Allah nafasi ya kujiunga na masomo kutunukiwa shahada zao. (s.w) ajaalie elimu yao iwe ni mwaka huu wa masomo.” Prof. Njozi, alitumia fursa yenye manufaa katika jamii Alisema Bw. Sagafu, hiyo kuwaombea dua kwa yetu.” Alisema Prof. Njozi. Naye Makamu Mkuu wa Mwenyezi Mungu wahitimu Awali Prof. Njozi, alisema Chuo hicho, Profesa Hamza hao awajaalie elimu waliyoipata wahitimu hao ambao awali Musafa Njozi, akiongea katika iwe ni yenye manufaa katika walikuwa 622, wamesomea mahafali hayo ya Tano toka jamii kwa ujumla.

MASHEIKH na Wanazuoni wa Kiislamu wa Jijini Dar es Salaam, wametakiwa kuwafikia Waislamu waliopo vijijini ili kutoa elimu kwa Waislamu walioko huko badala ya kuishia Jijini. Wito huo umetolewa na Imam wa Msikiti wa Nur, Masaganya, Wilayani Kisarawe, Sheikh Salum Omari Kongoro, katika hafla fupi iliyofanyika Msikitini hapo baada ya kutembelewa na Hajjat Rehema Amir Gama. Imamu Kongoro alisema

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Alisema, baada ya kukabidhiwa ardhi hiyo, Hajjat Gama, alisema atatafuta wadhamini pamoja washirikiane katika harakati za kujenga kituo hicho. “Nitakuwa bega kwa bega na watoto pamoja na wajane hawa, nimekabidhiwa shamba la heka moja kwa ajili ya kujenga kituo cha yatima iwapo nitapata kuungwa mkono nitashukuru Mungu.” Alisema Hajjat Gama, ambaye anaendesha Madrasatu Jannatil Islaamiyah, iliyopo Ilala, Mtaa wa Nzasa, namba 17..

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful