You are on page 1of 7

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

TANGAZO
Natafuta Mbia wa Biashara ya GAREJI awe Jijini Dar es salaam au Mikoani au Kuuza vifaa vya Gereji. Nina Vifaa vya Kunyooshea magari, Vifaa vya Makanika. Pia nina Spana aina zote za Ujerumani na Italia. Kwa mawasiliano zaidi piga simu no 0784 939445, 0655 919445.

Koti la Muungano linatubana-Maalim
Na Mwandishi Wetu

ISSN 0856 - 3861 Na. 1054 RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs

Mfumokristo nusura uwakoseshe swala Masheikh
Na Bakari Mwakangwale

MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema koti la Muungano kwa sasa linawabana Wazanzibari na kudai kuwa haoni

kuwepo kwa nia njema baada ya kipindi cha miaka 49 ya Muungano huo. Maalim Seif ambaye ni kiongozi wa kwanza wa juu wa Serikali kukutana na Tume Katiba (Tume y a Wa r i o b a ) k a t i k a Inaendelea Uk. 3

Tanganyika ‘ilifanya usanii’, ikatoweka Ikaibuka na joho la Tanzania inafaidi Kwa miaka 49 usanii huo unaiumiza Zanzibar

ILIKUWA almanusra, Maalim Ally Bassaleh na Masheikh wenzake wangekosa swala ya Aljumaa kutokana na mfumokristo ulioifanya Tu m e y a W a r i o b a isijali kwamba wao ni Waislamu na Masheikh wa Misikiti. Kwa kutokujali huko, anasema Bassaleh kuwa Tume iliwapangia kufika kutoa maoni muda ambao walitakiwa kuandaa hutuba za Ijumaa na kuchukua udhu kwa ajili ya swala.

Hicho ni kielezo tosha kwamba Uislamu na Waislamu hawathaminiwi na inachukuliwa kana kwamba hawapo kwa sababu hakukuwa na sababu yoyote ya msingi kuchagua siku ya Ijumaa badala ya siku nyingine sita za wiki. Akiongea na Waandishi wa habari, mara baada ya kuwasilisha maoni yao katika Tume ya maoni, Ijumaa ya wiki iliyopita, Maalim Ally Bassaleh, alisema, wamekutana na Tume hiyo kama wawakilishi wa makundi maalum ya kijamii. Mara kwa mara viongozi wa Tume ya kukusanya maoni,

Inaendelea Uk. 3

Kesi ya Ponda mashahidi wajichanganya mahakamani

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kulia) akiteta na wakili wake Juma Nassor katika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni washitakiwa wenzake katika kesi hiyo. Uk. 4

2
AN-NUUR

Tahariri/Habari/Tangazo RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA

S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Serikali ionyeshe imetatuaje kero za kidini kabla ya kuja na vitisho
RAIS Jakaya Kikwete ameeleza hivi karibuni kuwa serikali yake haitavumilia vurugu za kidini, ukabila na ukanda ambazo zilitaka kuliingiza taifa katika matatizo. Rais Kikwete alitoa kauli hiyo wakati alipojumuika na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya Ikulu jijini Dar. Hata hivyo hatuamini kwamba matatizo ya kidini ambayo yanayoifanya serikali ikose uvumilivu, yalishughulikiwa ipasavyo katika kuyatatua na watu wakaendelea kuishi kwa amani na kuaminiana kiimani. Hatuoni kama serikali ilikuwa na nia ya dhati katika kutatua hitilafu hizo za kidini, ambazo zimeachwa au kupuuzwa kwa muda mrefu bila kufanyika jitihada za dhati za kuzipatia suluhu. Ta n g u k a d h i a y a Mwembechai, malalamiko juu ya kujiunga OIC, kurejeshwa Mahakama ya Kadhi, mkataba wa MoU, kashfa ya NECTA, malalamiko ya kuwepo Mfumo Kristo serikalini nk. Hakuna hata suala moja lililopatiwa utatuzi na mambo yakatulia, zaidi ya kubainika dharau, ghiliba na kupuuzwa. Katika mazingira haya, tunaona kwamba ni vyema serikali ikaeleza kwanza ni kwa kiasi gani imefaulu kutatua matatizo ya kidini yaliyowahi kujitokeza nchini, kabla ya kuja na kauli za kukosa uvumilivu wa kile inachokiita vurugu za kidini. Tuelezwe ni kwa kiasi gani serikali imefanikiwa kutatua suala la kurejeshwa mahakama ya kadhi nchini, ili ipatikane sababu ya kukosa uvumilivu. Tufahamishwe kwanza ni jitihada gani zimefanyika kufuatilia ukweli na uthabiti wa malalamiko ya Waislamu kudai kuwa wanadhulumiwa kutokana na serikali kuendeshwa na mfumo kristo, unaolipendelea Kanisa. Serikalini imechukua hatua gani kuondoa kasoro hiyo. Labda ungepatikana ufafanuzi wa serikali, ilikuwaje iingie mkataba wa kutumia fedha za umma kulinufaisha kanisa (MoU), huku ikidai haina dini. Sote tunafahamu kuwa tangu yawepo malalamiko y a Wa i s l a m u j u u y a makataba huu wanaouita nio wakibaguzi kiimani, serikali hadi leo imeshindwa kutoa ufafanuzi juu ya hatua yake hiyo, na wala haipo tayari kufanya hivyo. Sisi tunaona kwamba serikali haitakuwa imetenda haki katika msimamo wake huo wa kukosa uvumilivu, kwakuwa kiini cha matatizo na hitilafu za kidini bado vingalipo na vimeachwa bila kuguswa. Dawa ya jipu ni kuondoa kiini chake. Hatudhani kwamba hata ukikosekana uvumilivu, basi kuendelea kupuuzia matatizo au kutumia nguvu za dola kwa wanaodai haki au wanaodhulumiwa ndio itakuwa suluhu ya kudumu ya matatizo ya kiimani kwa watanzania. Kuna haja ya serikali na viongozi wake kusikiliza shida za wananchi wake na kuzifanyika kazi bila kumuonea mtu. Wenye haki wapewe haki yao, wanaodhulumu walipe wale waliodhulumiwa. Serikali ni ya watu wote kwa imani zao. Hapo itapatikana suluhu ya kweli na si vinginevyo.

Tanganyika, Zanzibar waulizwe wanautaka?
Na Mwandishi Maalum, Zanzibar

JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

JUMUIYA ya Wanawake wa Kiislamu Zanzibar imesema kuwa utayarishaji wa katiba mpya hauwezi kuleta mafanikio iwapo suala la muungano halikujadiliwa kwanza. W a m e s e m a , kinachofanyika hivi sasa ni kama kulazimisha na kufanya udikiteta watu wakubali muungano uliopo jambo ambalo haliwezi kuleta amani ya kudumu inayotakiwa. Wa n a w a k e h a o w a JUWAKIZA wameyasema hayo mapema wiki hii katika ukumbi wa ofisi ya tume ya mabadiliko ya katiba Kikwajuni Gofu Zanzibar wakati wa kutoa maoni yao juu ya katiba mpya.

Mmoja wa wazungumzaji Ukht. Halima Kasim alionyesha kushangaa watu kujadili katiba ya muungano huku kukiwa hakuna katiba ya Tanganyika inayoungana na Zanzibar. Akitoa dukuduku lake mjumbe huyo alisema kuwa Wazanzibari wamechoshwa na muungano uliokuwepo na kwamba wanataka muungano wa mkataba, serikali tatu, la sivyo ujifilie kwa mbali. Amesema hali ya vurugu na kudhalilishwa kwa viongozi wa kijamii, kisiasa na kidini inayotokea Zanzibar, chanzo chake ni aina ya muungano uliopo ambao hauwapi uhuru Wazanzibari wa kujiamlia mambo yao wenyewe. Wachangiaji wengine walionyesha udanganyifu unaofanyika ambapo

“Serikali inasema haina dini lakini siku za ibada za Wakristo hakuna kazi, siku ya Ijumaa watu wanakwenda kazini kama kawaida.” Amesema Bi Aisha. Ni katika kuhoji hali hiyo ikadaiwa kuwa k a m a Ta n z a n y i k a wameona kuwa namna ya kuuenzi Ukristo ni kuifanya Jumapili kuwa siku ya mapumziko, basi Wazanzibari nao wana Ijumaa.
Kwa upande mwingine wakasema kuwa ni hitajio la kidini kwa Waislamu kuwa na Mahkama zao ili kuhukumu mambo yao Kiislamu.

hudaiwa kuwa nchi haina dini wakati Jumapili siku ya Wakristo ya kufanya ibada imefanywa ndio siku ya mapumziko.

TANZANIA MUSLIM PROFESSIONALS ASSOCIATION
P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900, +255 713 731300, +255 754261600. Email: info@tampro.org, Web: www.tampro.org

KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU
Kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari, Shule za Serikali zilizoshika nafasi 10 za mwisho katika matokeo ya mtihani wa kidato cha pili uliofanyika mwaka 2012, zote zinatoka mikoa ya Mtwara na Lindi. Zaidi ya hayo, Mkoa wa Dodoma umeendelea kushika mkia katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012, huku wilaya ya Kondoa ikiongoza kwa asilimia 43 kwa kuwa na idadi ya shule 37 ambazo hazikupata mwanafunzi hata mmoja aliyechaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari. Kama hatua ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuikabili changamoto ya hapo juu, Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) kwa kushirikiana na Chuo cha Ualimu Safina, Dar es Salaam, inawaalika wamiliki wa shule na vyuo vya ualimu, wakuu wa shule na vyuo vya ualimu, walimu wa shule na vyuo vya ualimu na wadau wengine wa elimu katika kongamano la kujadili changamoto ya shule za msingi na kata hasa katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Dodoma. Kongamano hilo litafanyika siku ya Jumamosi, Januari 26, 2013, kuanzia saa 3.00 asubuhi mpaka 9.00 alaasiri katika ukumbi wa Basihaya Camp, Boko, Dar es Salaam. Wadau wanaotaka kuhudhuria kongamano hilo wanaombwa wathibitishe kupitia simu japo kwa sms namba 0778 776226, 0653 326145, 0713 208585, 0655 654900. Baadhi ya waheshimiwa wabunge na madiwani wa mikoa iliyotajwa hapo juu pia, watahudhuria. SHARIFU MUHAMMED (MRATIBU WA KONGAMANO)

utaratibu wa kukusanya maoni, alisema hakuna nia njema katika kutatua kero za Muungano, hali inayopelekea usumbufu kwa wananchi hasa upande wa Zanzibar.

Inatoka Uk. 1

Koti la Muungano linatubana-Maalim
mfumo uliopo wa Muungano waliouzoea (pengine kwa sababu unawanufaisha wao) wanaweza kudai kwamba hatua hizi zinazopendekezwa haziashirii nia njema ya kuendeleza na kuimarisha Muungano. Mimi binafsi na wenzangu tunaoamini katika Muungano wa Mkataba hatuamini hivyo. Tunaamini katika kuwa wakweli na wawazi, kwamba hivyo ndivyo mahitaji ya wakati huu

3

Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Maalim Seif alikutana na Tume hiyo hivi karibuni nyumbani kwake Mbweni, Unguja ambapo alisema Muungano wa Serikali mbili uliopo sasa hauwezi kutatua kero zinazowakabili wananchi: “Koti la Muungano linatubana sana na tunahitaji kushona koti jipya kulingana na hali zetu za sasa,” alisema Maalim Seif mbele ya Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba. Alishauri kutokana na hali hiyo ni vyema muundo wa Muungano ukaangaliwa upya na kusisitiza msimamo wake wa kuwepo Muungano wa mkataba ambapo kila nchi itakuwa na mamlaka yake kamili: “ Tu n a m i a k a 4 9 y a Muungano bila kuonyesha mafanikio ya kuridhisha ya kutatua kero za wananchi… sasa tunahitaji kushona koti, ili kila nchi iwe na mamlaka yake ya ndani na nje,” alisema Maalim Seif. Alisema katika kipindi h i c h o Tu m e n a K a m a t i kadhaa zimeundwa katika kushughulikia kero za Muungano, lakini mafanikio yake ni madogo, hali inayotia wasiwasi, kuongezeka kwa kero hizo badala ya kutatuliwa. Maalim Seif alifahamisha, Zanzibar imekuwa muathirika mkubwa wa Muungano uliyopo, hasa katika nyanja za uchumi na siasa, baada mshirika wake ‘TANGANYIKA’ kutoweka, na kutumika jina la Tanzania kwa maslahi ya upande mmoja wa Muungano. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF), baada ya kutoa maoni hayo, alikutana na waandishi wa habari katika hoteli ya Bwawani, ambapo alifafanua maoni yake hayo na kuweka bayana kwa wananchi wote maelezo yake aliyoyatoa kwa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya. Akizungumzia mfumo wa muungano wa mkataba, Maalim Seif amesema kuwa kumekuwa na upotoshaji wa makusudi juu ya dhana hii wakidai kuwa huko ni kuvunja muungano. “ Wa s i o i t a k i a m e m a Zanzibar au wang’ang’anizi wa

Inatoka Uk. 1 wamekuwa wakiripotiwa wakidai kuwa wanaotoa maoni juu ya masuala yahusuyo Waislamu, wanashindwa kutoa ufafanuzi kama kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi, Tanzania kujiunga na OIC, katiba kutokutoa fursa ya ibada kwa Waislamu, kama ilivyo kwa Wakristo. Akieleza ni yepi waliyowasilisha katika Tume hiyo, Maalim Bassaleh, alisema wameeleza kwamba kuwepo kisheria kwa Mahakama ya Kadhi, ni sehemu ya Waislamu katika uhuru wao wa kuabudu. Alisema, waliieleza Tume kuwa pamoja na katiba ya nchi ina sheria zake za kisekula, lakini hizo sheria za kisekula zinakubali na kutambua katika masuala ya ndoa, talaka, mirathi na waqfu, kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu. Alisema, walibainishia tume hiyo kwamba, tatizo lililopo ni pale familia ya Kiislamu mfano, ikiwa na mgogoro wa mirathi huenda Mahakamani, na huko hujitambulisha kwamba wao ni Waislamu, na mgogoro wao wanataka uhukumiwe Kiislamu. Alisema, hakimu hukubali kwamba sheria inawarahusu kumaliza Kiislamu lakini hakimu mwenyewe haelewi sheria ya mirathi ya Kiislamu, hivyo inamlazimu kutoa barua waende katika taasisi fulani ya dini, huko wakagawiane kisha warejee Mahakamani hapo ili hakim aidhinishe, ili iwe na nguvu. “Anaidhinisha nini wakati sheria yenywewe huijui, anapiga muhuri kitu ambacho hakijui, yule atakayegawa akikosea au akifanya makusudi kupindisha haki.” Alisema Maalim Bassaleh. “Nikawapa mfano wa

Mfumokristo nusura umkoseshe swala Maalim Bassaleh
mgonjwa aliyekwenda hospitali ya Rufaa Muhimbili, amefika pale amechunguzwa ikaonekana kwamba ana saratani (Kansa), pale Muhimbili, ataambiwa ugonjwa huo una kitengo chake maalum, ambapo ni hospitali ya Ocean Road, mgonjwa huyo atapelekwa huko ili aweze kupata tiba sahihi.” Alisema. Alisema, huo ni mafano na pesa inatoka Serikalini, akatanabaisha kwamba, kwa Waislamu, kitengo chao cha ‘Kansa’ ni hiyo Mhakama ya Kadhi, linapokuja shauri mbele ya Mahakama ya kawaida wakashindwa kulitafutia dawa mgogoro ule wapelekwe kule katika Mahakama ya Kadhi. A l i s e m a , Wa i s l a m u wanaposema wanataka Mahakama ya kadhi wanataka haki yao ya Uhuru wa kuabudu, katika utaratibu unaokubalika na mamlaka ya nchi, katika masusla ya ndoa, mirathi, Talaka na waqfu kama ilivyo utatuzi wa masuala mengine, ya kitabibu au kisheria na si vinginevyo. Alisema, suala lingine ambalo wamelitolea maoni ni kuhusu katiba kutoa fursa ya ibada kwa Waislamu, pamoja na kwamba Katiba ya sasa inadai inatoa uhuru wa kuabudu, lakini kwa Waislamu uhuru huo haupo. “Nikawambia mfano uliohai, ni hivi sasa kwamba leo Waislamu tunatakiwa kujiandaa na Ibada ya swala ya Ijumaa, na nyinyi mmetuita viongozi wa dini bila kujali leo ni siku maalum ya kuabudu Wa i s l a m u n a m i o n g o n i mwetu ndio Mashekh katika Misikiti yao na wanangojewa kuongoza ibada.” “Hivyo hamkuona siku ya kutuita ikawa ni Ijumaa, tena asubuhi hii? Hali hii ndiyo inayo wasababisha Waislamu walalamike, kuwa hawana uhuru wa kuabudu, wanaona kwamba hawatendewi haki, hawathaminiwi kama wenzao Wakristo”. Alisema Maalim Bassaleh. Maalim Bassaleh, aliilalamikia hali hiyo akidai kwamba nusra yeye na wenzake waikosa ibada ya Swala ya Ijumaa, baada ya kupangiwa siku ya Ijumaa, kuonana na wajumbe wa Tume ya Maoni kutoa maoni yao kupitia Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T). “Wametuita leo (Ijumaa iliyopita), tena asubuhi muda wa kujiandaa na ibada, lakini ukiangalia jambo lenyewe nalo ni zito, la kuangalia mustakabali wetu kama Waislamu kama Watanzania kwa miaka ijayo, hata hivyo tumeweza kwenda tumeonana nao kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi maoni mengine na ufafanuzi tumekubaliana kuyapeleka kwa maandishi.” Alisema Maalim Bassaleh. Alisema, katika kuwasilisha maoni yao waliyagawa katika makundi mawili makuu, kwanza ni yale ambayo yanawagusa wao kama Waislamu, ambayo ndiyo hayo aliyoyaeleza na yale yanayowagusa kama Watanzania. Alisema, kwa upande wa pili wakiwa kama Watanzania, walipendekeza kuwepo na mfumo wa Serikali tatu, ambapo walipendekeza kuwepo na Serikali ya Zanzibar, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano. Alisema, mfumo huo utaodoa migogoro na kero zinazoitwa za Muungano, lakini pia wamependekeza kuwepo kwa Mahakama ya Katiba ya nchi, ili suala linalohusiana na mgogoro wa Muungano, lipelekwe katika Mahakama ya Katiba. Wakati huo huo, Maalim Ally Bassaleh, amesisistiza kwamba Mfumokristo katika nchi hii upo na kwamba Waislamu wanauleza kwa ushahidi.

na zama hizi yanavyodai.” Hata hivyo akasema kuwa yote hayo hufanyika kwa sababu kuna watu waliozoeya kufanya mambo kibabe na hawataki kubadilika. “Ulimwengu unabadilika kwa kasi. Zama za kuendesha mambo kwa ubabe na ukichwa ngumu zimepitwa na wakati. Tuache ile tabia ya kuyaona mapendekezo ya kubadili mfumo wa Muungano kuwa yana nia ya kuuvunja

Muungano huo. Muungano ili udumu unahitaji ridhaa ya walioungana. Muasisi wa Muungano huu, Mwalimu Nyerere mwenyewe, aliwahi kueleza umuhimu wa ridhaa katika masuala haya na kuonyesha kwamba ridhaa ya mshirika mmojawapo ikiondoka, Muungano hauwezi kusimama.” Maalim akasisitiza kuwa “Wazanzibari ni watu wenye historia ya maingiliano ya

jamii za watu mbali mbali na hivyo hawawezi kukataa umoja, alimradi tu umoja huo uwe na maslahi na faida kwao.” Bali akasema kuwa “Mfumo uliopo sasa hauinufaishi Zanzibar na hivyo haukubaliki kwa Wazanzibari.” Ndio pale akasema kuwa “Koti la Muungano kama lilivyo sasa linabana sana. (na kwamba) Wakati umefika tushone koti jipya kwa mujibu wa mahitaji ya zama hizi.”

Akiongea na Waislamu mara baada ya swala ya Ijumaa, ya wiki iliyopita, katika msikiti wa Idrisa, alisema Maaskofu wamekuwa wakijaribu kukanusha huku wakidai mfumo huo unaletwa na Waislamu. Alisema, Waislamu na Masheikh wanaozungumzia kuwepo kwa Mfumokristo nchini, wanazungumza kwa ushahidi, kupitia wao wenyewe waliyoandika katika vitabu mbalimbali. “Sisi tunawaeleza kwa ushahidi kwamba Mfumokristo katika nchi hii upo, na waliotulieleza kwamba kuna mfumo huo wa kuwapendelea na kuwabagua Waislamu ni wao wenyewe Wakristo kupitia vitabu vyao mbalimbali sisi tulikuwa hatujui.” Alisema Maalim Bassaleh. Maalim Bassaleh, aliwataka Maaskofu wasiishie kukanusha tu, au kudai kwamba wanaoleta mfumo huo ni Waislamu bali waje na hoja na ushahidi au wakanushe yale yaliyoandikwa katika vitabu juu ya ushahidi wa kuwepo mfumokristo Serikalini. “Tunawaambia Maaskofu, Wa i s l a m u k a m w e hawatanyamazia hili, kwamba wataendelea kuiambia Serikali kwa mtindo huo huo wa kuainisha yaliyomo ndani ya vitabu, kisha waseme kipi walichozua Waislamu kuhusiana na kuwepo kwa Mfumokristo.” Alisema Maalim. Maalim Bassaleh, aliwashangaa Maaskofu hao kuwaingiza Waislamu lawamani kwa kusoma na kunukuu vitabu ilihali vitabu hivyo vipo na waandishi wake wangali hai huku wakishindwa kuyatolea ufafanuzi yale yaliyomo katika vitabu hivyo. Alitoa mfano wa kitabu kingine kilichomnukuu Mwl. Julius Nyerere, akisema kwamba atalipa Kanisa fursa ya upendeleo ya kunawiri.

4

Habari

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Kesi ya Ponda
Na Mwanishi Wetu

ILE kesi inayomkabili Katibu wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, jana iliendelea kusikilizwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mbele ya hakimu Bi. Victoria Nongwa. Safari hii kesi ilikuja kwa ajili ya kuendelea kusikiliza mashahidi wa upande wa mlalamikaji, ambapo mashahidi wawili Mzee Masoud Kome, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Bakwata na Bw. Hafidh Seif Othman, aliyejitambulisha kuwa ni mdau katika kampuni ya Agritanza na mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi. Akitoa ushahidi wake mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Mzee Kome kutoka Dodoma, alipoulizwa na wakili wa utetezi Bw. Juma Nassoro, iwapo anajua uwiano wa thamani kati ya kiwanja cha ekari nne cha Chang’ombe kilichouzwa na Bakwata kwa Agritanza na lile eneo la ekari arobaini lilipo Kisarawe kupewa bakwata, alisema hajui uwiano wa thamani yake. Alipoulizwa iwapo anawafahamu washatakiwa na anayeshtaki, Mzee Kombe alisema hawafahamu. Aidha alipoulizwa iweje amekuja kutoa ushahidi katika kesi asiyoifahamu, hakutoa jibu. Wa k i l i w a u t e t e z i alipouliza iwapo shahidi huyo aliwahi kuliona eneo hilo la ekari arobaini huko Kisarawe zilizotoleewa na agritanza kwa Bakwata akiwa Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini Bakwata, Mzee Kome alisema mbele ya hakimu kuwa hajawahi kufika katika eneo hilo na wala hafahamu Kisarawe kwenyewe. Ilielezwa kuwa dhumuni la Bakwata kupewa eneo la Changomb’e, lilikuwa ni kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu kwa msaada wa serikali ya Misri. Hata hivyo, shahidi huyo alipoulizwa na wakili wa

utetezi Bw. Juma Nassoro juu ya ukubwa wa eneo hilo wakati wakikabidhiwa Bakwata lilikuwa je, alisema lilikuwa kubwa ila liliuzwa kidogo kidogo na viongozi wasiokuwa waaminifu, ambao kwa sasa hawapo Bwakata. Kwa upande wa Shahidi mwingine Bw. Hafidh Othaman, yeye alipoulizwa na wakili huyo juu ya thamani ya vifaa vilivyoibwa katika kiwanja hicho cha Chabg’ombe, alijibu kuwa vilikuwa na thamani ya shilingi milioni 56 ukiondoa saruji. Aliulizwa iwapo waliokuwa wamevamia kiwanja anawafahamu, alijibu kuwa hawafahamu. Lakini alipoulizwa iwapo aliwaona wavamizi, alijibu kuwa hakuwaona isipokuwa Sheikh Ponda. Aw a l i w a k i l i J u m a Nassoro alisema shahidi Hafidh Othmani, wakati alipoulizwa juu ya umiliki wa eneo la Kisarawe, alisema ni la kwake. Lakini kwenye mkataba wa kubadilishana na Bakwata, imeelezwa kuwa eneo hilo ni mali ya Agritanza. Kwa upande mwingine, Shahidi Hafidh alipokwenda kwa mara ya kwanza Polisi kulalamika, alieleza kuwa eneo la Kisarawe ni mali ya kampuni ya Al-Hilal. Awali ilielezwa kuwa Bw. Hafidh alisema eneo hilo aliuziwa na serikali ya kijiji. Lakini alipoulizwa na wakili wa utetezi Yahya Njama, Hilal huyo huyo alisema kuwa eneo hilo la Kisarawe aliuziwa na familia ya Bw. James Mabina. Kwa maana hiyo wakili Nassoro anaeleza kuwa, inaonyesha mkataba walioingia Bakwata na Agritanza ulikuwa hewa, na ungeweza kuleta utata mkubwa hapo baadae. Yule shahidi mwingine wa upande wa mlalamikaji aliyeamriwa na mahakama kukamatwa, bado hajakamatwa na kufikiwshwa mahakamani hapo kama ilivyoamriwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi itakapotajwa tena Januari 31 mwaka huu.

PICHA juu na chini baadhi ya wathumiwa Waislamu wakiwa pamoja na Sheikh Ponda (hayupo pichani) katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

BAADHI ya wanafunzi wa Answaar Islamic Model School ya jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye chumba cha kompyuta shuleni hapo.

5

Habari za Kimataifa

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Iran yazindua helikopta mpya ya kivita
TEHRAN Iran imezindua halikopta mpya ya kivita inayojulikana kama “Toufan 2.” Helikopta hiyo imezinduliwa katika hafla iliyohuduriwa na Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bw. Vahidi amesema helikopta hiyo ni ya kizazi kipya cha helikopta za kivita na imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kabisa, ikiwa na uwezo mkubwa wa kulenga shabaha. Amesema helikopta hiyo iliyotengenezwa nchini humo ni ishara ya ubunifu na kujitegemea Iran licha ya kuwepo vikwazo vya maadui. Wa k a t i h u o h u o , Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesema mazoezi yake yamemalizika kwa mafanikio. Mazoezi hayo ya siku sita yalianza 28 Desemba, na yamefanyika katika eneo pana la fukweni, baharini na angani kwenye lango la Hormuz, Bahari ya Oman, kaskazini mwa Bahari ya Hindi, Ghuba ya Aden na lango la Babul Mandab. Msemaji wa mazoezi hiyo, Admeli Amir Rastegari, amesema malengo ya mazoezi hayo yamefikiwa kikamilifu kama ilivyopangwa. Mazoezi hayo yalijumuisha nyambizi, manowari, makombora, ndege zisizo na rubani, ndege za upelelezi na vita vya kielektroniki. Wa k u u w a J e s h i Wa n a m a j i l a I r a n wamesisitiza kuwa mazoezi hayo ya kijeshi yana ujumbe wa urafiki na udugu kwa mataifa rafiki na onyo kali kwa maadui.

RAIS wa utawala Israel, Shimon Peres, kwa mara ya kwanza amekiri kuwa utawala huo ulihusika na mauaji ya Rais wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Yasir Arafat. Peres, amesema Arafat hakupasa kuuliwa kwa sababu ulikuwepo uwezekano wa kufikia maelewano na yeye. Ameongeza kuwa kukosekana kwa Yasir Arafat, hali ya mambo imekuwa ngumu na tata zaidi. Oktoba 12 mwaka 2004, Yasir Arafat, alipelekwa Ufaransa kwa matibabu na kulazwa katika hospitali moja ya kijeshi iliyoko kwenye viunga vya mji mkuu wa nchi hiyo Paris. Hata hivyo sio tu kwamba hakupata nafuu, bali hali yake ilibadilika ghafla na kuwa mbaya zaidi na ilipofika Novemba 11 mwaka huo huo, alifariki dunia hospitalini hapo kutokana na athari ya sumu. Kwa muda wa miaka miwili kabla ya kufariki kwake, kiongozi huyo wa kwanza wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, alikuwa kwenye kizuizi nyumbani, alichowekewa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Tangu wakati ilipotangazwa habari ya kifo cha Arafat,

Peres akiri Israel ilihusika na mauaji ya Arafat
wachambuzi wengi wa mambo na wanaharakati wa kisiasa na hata vyombo vya habari, viliamini kuwa kifo chake kilikuwa cha kutatanisha. Ripoti za vyombo vya habari zilieleza kwamba kifo cha Yasir Arafat, hakikuwa cha kawaida bali aliuawa kutokana na athari za mada za sumu ya Polonium, iliyotiwa kwenye nguo zake. Ta n g u w a k a t i h u o , mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kiongozi huyo ulikuwa ni utawala wa Kizayuni wa Israel ambao kwa muda wote huo haukuwahi kukana tuhuma hizo. Siku za hivi karibuni, viongozi wa Palestina pamoja na mke wa hayati Arafat, Bi. Suha, walitaka maiti yake ifukuliwe na kufanywa uchunguzi tena wa kujua sababu ya kifo chake. Hatimaye mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana maiti ya Yasir Arafat ilifukuliwa na kufanyiwa uchunguzi na wataalamu kutoka nje. Ingawa hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi rasmi wa utawala wa Israel kukiri kwamba utawala huo ulihusika na mauaji ya Arafat, lakini hata kabla ya kufukuliwa maiti ya kiongozi huyo wa Palestina kwa ajili ya uchunguzi, mkewe yaani Suha Arafat, alikuwa amefichua hapo kabla kwamba Israel ndiyo iliyohusika na

Rais wa utawala Israel, Shimon Peres (kushoto) akisalimiana na Rais wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Yasir Arafat wakati huo.

mauaji ya mumewe. Inaelezwa kuwa kilichomfanya Shimon Peres, akiri kuhusika utawala wa Kizayuni na kifo cha Yasir Arafat, si matamshi yaliyotolewa na mke wa Arafat bali ni hali mbaya zaidi ambayo imekuwa nayo Israel hivi sasa baada ya kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Kuungama kwa Perez kunazidi kudhihirisha sura halisi ya Israel mbele ya fikra za walio wengi duniani. Imeonekana kuwa hatua hiyo ya Rais Perez inadhihirisha ukweli wa mambo wa kiutambulisha Israel kuwa na uhusiano na mfungamano wa moja kwa moja na mauaji na ugaidi. Inaelezwa kuwa kitu pekee kinachoitofautisha Israel na makundi ya kigaidi kama al Qaeda, ni kwamba kundi hilo halina mfungamano wowote wa kiserikali wakati Israel ni dhihirisho halisi la ugaidi wa kiserikali duniani. Jambo jingine muhimu ni kwamba, kukiri kwa Shimon Peres kwamba utawala wa Kizayuni wa Israel ulihusika na mauaji ya Yasir Arafat, kunaweza kuwapa haki ya kisheria viongozi wa Palestina ya kuufungulia mashtaka utawala huo haramu katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. (IRIB)

DEHL K I TA B U C H A Qur’ani na vitabu vya fasihi ya Kiislamu vimekuwa ndivyo vitabu vinavyouzwa kwa wingi zaidi katika tamasha la vitabu nchini India, ambalo limefanyika katika mji wa Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh. Tovuti ya The Hindu, imeripoti kuwa kusoma na kuelewa Qur’ani na vitabu vya fasihi vya Kiislamu, ilikuwa kazi ngumu kwa wananchi wa India kutokana na vitabu hivyo kuandikwa kwa lugha za Kiarabu, Kifarsi na Urdu. Hata hivyo tamasha la vitabu la Vijaywada, limepunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hilo kwa kuuza nakala za Qur’ani na vitabu vya fasihi ya Kiislamu kwa lugha za Kiingereza na Telgu. Wa s i m a m i z i w a tamasha hilo wanasema kuwa tarjumi ya Qur’ani Tukufu kwa lugha za Kiingereza na Telgu zinauzwa kwa wingi zaidi kuliko vitabu vingine katika matamasha hayo. Baada ya Qur’ani, vitabu vingine vinavyouzwa zaidi ni vile vinavyozungumzia maisha ya Mtume Muhammad (saw), swala na Mwenyezi Mungu SW, wanawake katika Uislamu na Qur’ani ya Sayansi. Tamasha la vitabu la Vijaywada hufanyika kila mwaka kuanzia Januari Mosi hadi 11. (IQNA)

Qur’ani kitabu kinachouzwa kwa zaidi India

Mapinduzi ya Zanzibar, ilikuwa ni ‘Crusade’
Na Said Rajab

6

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

JANUARI 12, mwaka 2013 tumeadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama ilivyo historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika, imepotoshwa kwa kiasi kikubwa na watu wasioitakia mema Zanzibar. Wa t a n z a n i a w e n g i hawafahamu ukweli kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar. Hawajui jinsi Mfumo - Kristo ulivyosimamia Mapinduzi hayo na baadaye Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Fuatana na mchambuzi wako Said Rajab. Ni miaka ya hivi karibuni tu ndiyo utafiti kuhusu Uislamu katika eneo la Afrika Mashariki umeanza kuwavutia wanazuoni na watafiti wa kisasa. Lakini wengi wao, walipuuza vita vya Msalaba dhidi ya Uislamu Afrika Mashariki, hususan Zanzibar. Ilipuuzwa kwa sababu migogoro ya kidini kama hii ilionekana ni ya Mashariki ya Kati, ingawa ukweli ni kwamba vita vya msalaba (crusade) dhidi ya Uislamu inaweza kuwepo kwenye nchi yoyote ya Wa i s l a m u , Z a n z i b a r ikiwemo. Ama kuhusu ‘crusade’ ya Wakatoliki Zanzibar, Nyerere alifanyakazi kwa karibu sana na Oscar Kambona, mwandani wake na mwanafunzi mwenzake katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, ambapo mwaka 1910, mkutano wa pili wa WCC (World Conference of Churches) Kongamano la Dunia la Makanisa, ulijadili tishio la Uislamu Afrika Mashariki. Ilikubaliwa kwa kishindo kwamba Mwafrika Mkristo ni mzuri zaidi (kwa uongozi) kuliko Mwafrika Muislamu. Kwa hiyo Nyerere alipewa kila aina ya msaada ili

MWALIMU Julius Kambarage Nyerere (kushoto)

aupige vita Uislamu Afrika Mashariki, baada ya kuondoka kwa Ukoloni wa Uingereza. Wa k a t i Ta n g a n y i k a ilipopata Uhuru wake mwaka 1961, Jomo Kenyatta wa Kenya, Milton Obote wa Uganda na Julius Nyerere wa Tanganyika walifanya Mkutano mzito jijini Nairobi Juni 5, mwaka 1963. Katika njama hii ya viongozi Wakristo, Zanzibar haikuwakilishwa wala kutajwa kwenye mkutano huu. Viongozi hawa, kwa kauli moja, walitangaza kushirikiana kikanda, chini ya msukumo wa ‘Umajumui wa Kiafrika’ (Pan Africanism): “Sisi (Nyerere, Obote na Kenyatta), viongozi wa watu na Serikali za Afrika Mashariki (i.e.Tanganyika, Uganda na Kenya)...tumejifunga kuunda shirikisho la kisiasa la Afrika Mashariki na tunasukumwa zaidi na Uafrika na wala siyo maslahi ya Kikanda” (p.1) Wa k a t i Z a n z i b a r ilipopata uhuru wake, Desemba 10, mwaka 1963 kutoka Serikali ya Uingereza, ikawa ni mwanachama wa Jumuiya

ya madola. Ikajiunga na Umoja wa Mataifa, Desemba 16, mwaka 1963 na iliwakilishwa na balozi Hilal bin Muhammed bin Hilal. Lakini, wakati Serikali mpya ya Zanzibar ilipotangaza muundo unaofanana na Dola ya Kiislamu, Makruseda wa Kiafrika wa Kikristo, wakaanza kupiga kelele kwamba Serikali ile itapandikiza Uarabu na Uislamu Zanzibar. Wakaivamia Zanzibar usiku wa manane wa January 11, mwaka 1964, chini ya “Field Marshall” aliyejipachika mwenyewe cheo hicho, John Okello, ambaye ni mpiganaji wa Kikristo kutoka Uganda. Malengo hasa ya Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa ni ‘Vita dhidi ya Uislamu’ kama Okello mwenyewe alivyobainisha ndani ya kitabu chake, ‘Revolution in Zanzibar ‘ (Mapinduzi Zanzibar), kwamba Mungu alimteua kufanya Mapinduzi yale kwa ajili ya Ukristo. Na kisha akanukuu kifungu kifuatacho cha Biblia kuhalalisha alichofanya: “Na sasa sikilizeni

enyi matajiri! Lieni na kuomboleza kwa sababu ya taabu zitakazowajieni. Mali zenu zimeoza, na nguo zenu zimeliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha vimeota kutu, na kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nayo itakula miili yenu kama vile moto. Ninyi mmejilundikia mali katika siku hizi za mwisho! Hamkuwalipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu. Sikilizeni malalamiko yao! Kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni mwa Bwana, Mwenye Nguvu. Mmeishi duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mmejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa. Mmemhukumu na kumwua mtu asiye na hatia, naye hakuwapigeni” (James 5:1-6) Okello pia amebainisha k w a m b a “ Wa p i g a n i a Uhuru” wake wametoka Ta n g a n y i k a , K e n y a , Uganda, Rhodesia (Zimbabwe), Nyasaland (Malawi) na Msumbiji. Waliua Waislamu 13,635 na wengine 21,462 waliwekwa kizuizini. January 11, mwaka 1964,

Okello aliwaamrisha Makruseda kwamba Waarabu wote (Waislamu) walio na umri kati ya miaka 18 na 55 lazima wauawe. Siku iliyofuata, mauaji ya Waislamu yakaanza na Okello akasema haya kwenye Redio ya Zanzibar: “Mimi ni Field Marshall! Okello! Enyi Mabeberu, hakuna tena Serikali ya Mabeberu katika visiwa hivi. Hii sasa ni Serikali ya Wapigania Uhuru. Amkeni enyi watu weusi. Kila mmoja wenu achukue bunduki na risasi na kuanza kupigana na masalia yote ya ubeberu katika visiwa hivi” (p.143). Asubuhi ile ile, Okello akatoa agizo kwa Jamshid bin Abdullah bin Khalifah (1963-1964), Sultan wa Zanzibar: “Umepewa dakika ishirini tu za kuua watoto wako na wake zako na kisha ujimalize wewe mwenyewe”. Revolution in Zanzibar (p.145). Lakini hata hivyo, Sultan wa Zanzibar alifanikiwa kutoroka kupitia Mombasa, Kenya. Wa a f r i k a w a l i o k o Tanganyika walisaidia sana kuipindua Serikali ya Zanzibar ambapo Makruseda walikuwa na silaha bora za kisasa kutoka Kenya na Tanganyika. Zaidi ya Makruseda 600 waliivamia Zanzibar usiku wa kuamkia January 12, mwaka 1964. Keith Kyle, Mwandishi wa Habari wa Uingereza katika eneo la Afrika Mashariki, aliandika makala zake mbili kwenye g a z e t i l a S p e c t a t o r, “Gideon’s (Okello) Voices” iliyochapishwa February 7, mwaka 1964 na “How it happened” iliyochapishwa February 14, mwaka 1964 anasema “baadhi ya Wakristo katika Serikali ya Tanganyika walihusika katika Mapinduzi (Vita vya Msalaba) ya Zanzibar” Inafahamika vizuri kwamba mauaji yalikuwa
Inaendelea Uk. 7

Mapinduzi ya Zanzibar, ilikuwa ni ‘Crusade’
Inatoka Uk. 6 ya kutisha mno kiasi kwamba Waislamu 100 waliuawa kwa kuokwa kwenye tanuri kama mikate kule Bambi. Abeid Karume (1905-1972, akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Karume alifanya mazungumzo ya siri na Rais wa Tanganyika, Julius Nyerere kuhusu kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika. Hali kama hii iliyotokea Zanzibari, iliwahi kutokea visiwa vya Mindanao Ufilipino, Dola ya Kiislamu iliyoanzishwa na Sultan Sayyid bin Abu Bakr al - Hadhramy zaidi ya miaka 400 kabla ya Kanisa Katoliki halijaingia Ufilipino na Tanganyika. Siku moja baada ya ‘Crusade’ visiwani Z a n z i b a r, U m o j a w a Vijana wa KANU, chama kilichokuwa kinatawala Kenya wakati ule, ulifanya mkutano wa dharura jijini Nairobi. Katika Mkutano huu, “azimio la kupongeza kuangushwa kwa utawala wa Zanzibar” lilipitishwa bila kupingwa. Azimio hilo lilifuatiwa na kikao cha siku mbili cha Baraza la Mawaziri wa Kenya, kilichoitishwa na Ofisi ya Waziri Mkuu. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanganyika, Oscar Kambona, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Makanisa Duniani (WCC). Alikuwepo pia Waziri wa Nchi wa Uganda George Magezi, wakati Joseph Marumbi, Waziri wa Nchi na Mambo ya Nje wa Kenya alikuwa akiwasiliana na Zanzibar kwa simu wakati wote. Alikuwa akiwasiliana na Edington Kisasi, Mkatoliki kutoka Moshi nchini Tanganyika, ambaye alikuwa ‘Superintendent’ wa Polisi Zanzibar aliyewekwa na Waingereza, ambaye baadaye akawa Kamishna wa kwanza wa Polisi Zanzibar baada ya ‘Crusade’ ya Zanzibar

7

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

VICTOR Okello kufanikiwa. Mkutano ule wa Baraza la Mawaziri, uliolenga kujadili matokeo (aftermath) ya ‘Crusade’ pia ulihudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Kenya, vikosi vya Uingereza vilivyopo Kenya na Mkuu wa Jeshi la Polisi, R.C Cating. Ndani ya siku mia moja za kwanza baada ya ‘Crusade’ visiwani Zanzibar, Nyerere alikula njama na viongozi mashuhuri wa Kikristo Afrika Mashariki na mabeberu wa Magharibi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Njama hii ilikuwa muhimu mno kiasi kwamba Serikali ya Marekani iliyokuwa ikiongozwa na Rais Lyndon Johnson (1963 - 1969), ikaipa Zanzibar kipaumbele cha juu katika Sera ya Nje ya Marekani, ukiondoa Vietnam na Cuba wakati ule. William Attwood, aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Kenya alisema kwamba: “The Western powers prepared a contingency plan in case the Union would fail... and (after the union), the laws of Tanganyika would become supreme to round up (Muslim) radicals in Zanzibar.” Ta f s i r i : “ M a t a i f a makubwa ya Magharibi yalishaandaa mpango kabambe iwapo Muungano huo ungeshindikana...na (baada ya muungano) sheria za Tanganyika ndizo zingetumika kuwadhibiti wakorofi visiwani Zanzibar” Pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Dean Rusk alitoa wito kwa mataifa ya Magharibi: “It is essential for Nyerere to be given the maximum support from the West”( “Ni muhimu sana kwa Nyere r e k u p e w a k i l a msaada atakaohitaji kutoka mataifa ya Magharibi”). Kwa hiyo, wakati Nyerere alipoenda Zanzibar April 22, mwaka 1964 kumshinikiza Karume kuhusu kuungana na Tanganyika, tayari alishapeleka askari wake

Zanzibar, January 13 mwaka 1964 wakiwa na silaha nzito kwa kile kilichoelezwa kama sababu za kiusalama, baada ya kushauriana na Okello. Mwandishi Martin Bailey amemnukuu Nyerere wakati alipohutubia mkutano wa hadhara jijini Dar es Salaam, Novemba 15, mwaka 1964: “Tulituma Polisi wetu Zanzibar. Baada ya kuvuka matatizo mbalimbali tuliungana. Sisi wenyewe kwa hiyari yetu tulikubali kuungana. Karume na Mimi tulikutana. Sisi wawili tu tulikutana. Wakati nilipotaja suala la Muungano, Karume hata hakufikiria mara mbili. Alinitaka palepale kuitisha mkutano wa Waandishi wa Habari na kutangaza nia yetu. Nilimshauri kusubiri kidogo kwa sababu ilikuwa mapema mno kwa waandishi wa habari kufahamishwa” Ni ukweli usiofichika kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalisimamiwa na hayati Mwalimu Nyerere kwa maslahi ya Mfumo Kristo zaidi kuliko Wazanzibar. Kupitia Mapinduzi hayo, Zanzibar imepoteza haiba yake ya Kiislamu na mamlaka yake ya Dola kwa Tanganyika tangu April 26, mwaka 1964.

Jumuiya ya Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania (TAMPRO) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAIYA) Wataendesha semina fupi elekezi juu ya utoaji na ugawaji wa Zaka. Aidha, semina hiyo itakwenda sambamba na zoezi la ugawaji wa Zaka kwa baadhi ya kinamama wajane wa Kiislamu na wanafunzi waliochaguliwa kupitia Misikiti yao. MUDA: SAA 2:30 ASUBUHI - SAA 6:45 MCHANA SIKU: ALHAMISI TAREHE 24/01/2013 UKUMBI: Lamada Hotel Kwa mawasiliano piga namba: 0716 776226, 0754 654900