You are on page 1of 8

9

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

WAISLAMU duniani kote wanasoma Aya za Qur’an kwa sauti nzuri na Qiraa za kupendeza. Karibu kila khutba, mhadhara au mada za Waislamu zinamrejea Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Qur’an yenyewe imekuwa halisi kwa wanadamu kupitia maisha ya Mtume huyu wa Mwenyezi Mungu. Kuna Aya katika Qur’an Tukufu zinazomrejea Muhammad (saw) moja kwa moja kama shujaa na kiigizo chema kwetu: “Bila shaka mnao mfano mwema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana” Qur(21:33). Kama mfano mwema wa tabia ya binadamu, Mtume ameziteka fikra na hisia za mabilioni ya Waislamu duniani kote, kwa zaidi ya karne 14 zilizopita. Mguso wa kihisia wa Waislamu kwa Muhammad (saw) kusema ukweli ni mkubwa sana na hauna shaka kabisa, lakini mshikamano wa kifikra na Mtume wa Mwenyezi Mungu, bado shida kubwa miongoni mwa Waislamu. Kusema ukweli, Waislamu wachache sana tumefanya jitihada zinazohitajika kumfahamu Mtume kama Mkuu wa nchi, Mlinzi wa Itikadi (Aqidah) na Jemedari wa Majeshi. Sisi tunapendelea zaidi kuwa na Mtume wa kiroho tu, au Mtume wa Kimaadili au Mtume wa “kidini”. Na hapa ndipo tulipomuangusha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Tunaweza kuelewa jinsi fikra za Kimagharibi zinavyotapatapa zikitafuta maainisho ya kisekula kuhusu uhai na uwepo wa Mwenyezi Mungu. Hatukubaliani nayo, lakini tunaelewa jinsi inavyokuja. Lakini tukijiangalia wenyewe kama Waislamu, vipi tunaweza kutoa ufafanuzi wa kumuweka Mtume wa Mwenyezi Mungu katika mazingira ya kisekula? Nini kinaweza kufafanua, katika karne zote hizi 14 tangu Hijra, kushusha Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu kuishia kwenye mapishi, mavazi, kupiga mswaki, afya na masuala meng ine bin af s i? Yuk o wapi Mtume aliyehangaika Makkah kwa miaka 13, akivumilia manyanyaso, kuvunjiwa heshima, mateso kwa wafuasi wake, kutengwa

Mtume amenyooka, harakati zetu zimepinda!
WAKATI Waislamu duniani kote wakijiandaa kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (saw), nadhani ni fursa nyingine adhimu ya kumueleza Mtume huyu wa Mwenyezi Mungu kwa usahihi na jinsi alivyoendesha harakati zake za kusimamisha dini ya Allah katika ardhi. Mbinu alizotumia, mipango aliyobuni na mikakati aliyoweka mpaka Uislamu ukasimama katika kiwango cha juu kabisa, ndiyo dira inayopaswa kufuatwa na wanaharakati wote duniani, wakiwemo wa Tanzania, kama harakati zao zinalenga kusimamisha Uislamu. Fuatana na Mchambuzi wako SAID RAJAB katika makala hii.

KUMRADHI katika picha wa kwanza kulia ni Sheikih Musa Juma na si Sheikh Mselem kama ilivyochapishwa katika toleo lililopita. kijamii, kuwekewa vikwazo vya kiuchumi, na hatimaye majaribio ya Washirikina wa Makkah kutaka kumuua? Fikra za Waislamu duniani leo bado hazijazama kiasi cha kutosha na kutoa mwelekeo wa suala hili muhimu. Matokeo yake ni kuongezeka kwa idadi ya Waislamu duniani ambao wametengwa kijamii, wameenguliwa kisiasa na kukandamizwa kiuchumi. Hii haiwezi kuendelea milele. Lazima tuanze kumfuata Mtume wetu, siyo tu kwenye mambo mepesi tunayoyapenda, bali hata yale mazito aliyoyafanya, ambayo yamewaletea Waislamu heshima na ushindi dhidi ya makafiri. Makala hii fupi inalenga zaidi kuangalia, japo kwa uchache, tabia njema za Mtume wa Mwenyezi Mungu na yale aliyoyafanya katika harakati zake za kusimamisha sheria ya Allah katika ardhi. Je? Mtume wa Mwenyezi Mungu alianza na taratibu za Ibada au Itikadi? Waislamu wote tunajua kwamba watu wa mwanzo kabisa kumkubali Muhammad (saw) kama Mtume wa Mwenyezi Mungu, walikuwa mke wake Khadijah, ndugu yake Ali, mtoto wake wa kumlea Zaid na rafiki yake Abubakar. Tuna maana gani tukisema watu hawa walikubali ujumbe wake? Ujumbe wenyewe ulikuwa nini wakati ule? Alikuwa akimuhimiza kila mtu kuswali? Au jinsi ya kuoga janaba? Au alikuwa akiwaletea mpangilio mpya wa majukumu? Nadhani ni wazi kabisa kwamba katika hatua hii ya awali kulikuwa hakuna haja ya taratibu za Swala, Zaka, Swaumu wala Hijja kama tunavyozielewa leo. Mtume wa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye kiigizo chetu, hakuwa akiwataka watu kuwa Waislamu wa taratibu za Ibada. Hizi taratibu za Ibada zilikuja muda mfupi kabla au baada ya Hijra ya kuelekea Madina. Kwa zaidi ya miaka kumi timilifu, Muhammad (saw) alikuwa akijaribu kuwasiliana na watu wa jamii yake kuhusu kitu fulani, ambacho walikuwa wakikipinga vikali. Bila shaka kitu hicho siyo taratibu za Ibada za Kiislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa akijaribu kukusanya dhamira za mtu mmoja mmoja, ili kuleta mabadiliko makubwa ya kijamii (Social Transformation). Alikuwa amelenga, hatimaye kutokomeza kabisa mpangilio wa kijamii na kiuchumi (socio - economic order) uliotawala Makka wakati ule, na kuleta mpangilio mpya unaotokana na ‘Wahyi’ aliokuwa akipokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mchakato huo umewekwa kwa muhtasari na Waislamu kwenye nguzo ya Imani au tangazo la Utii, ambalo linamfanya Mwenyezi Mungu kuwa mwenye Mamlaka pekee ya mwisho kwa binadamu, na Muhammad (saw) ni mjumbe wake, ambaye anawasilisha na kuafafanua ukweli huu. Wakati Muhammad (saw) alipoanza harakati zake hizo, ambazo zilimchukua maisha yake yote, kama walivyokuwa Mitume waliopita kabla yake, aligusa mahusiano ya kijamii na ya mtu mmoja mmoja. Aligusa mahusiano ya watu ambao kwa miaka arobaini alikuwa karibu nao, na wengine alizaliwa nao, na wengine walikua pamoja na wengine aliishi nao. Wa k a t i M t u m e w a Mwenyezi Mungu alipoanza harakati zake za kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu kwenye ardhi, tunajifunza kutoka kwenye historia kwamba watu wachache sana walijitolea mali na nafsi zao kuungana naye

katika kusambaza ujumbe wa Qur’an. Lakini wakazi wengi wa Makka walimkataa na kumpinga. Katika miaka hii ya awali, Waislamu madhubuti waliokuwa karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu walilazimika kuficha ukweli kwamba wameshaachana na jamii yao, hususani katika nyanja za uchumi, siasa na mwenendo wa kijamii. Hata Abubakar (ra), ambaye alikuwa kiongozi katika ukoo wake, na mtu aliyeheshimika sana miongoni mwa vigogo wa Makka alilazimika kuficha utii wake mpya. Kadri muda ilivyokwenda, watu wengine wa Makka wakawa Waislamu. Vigogo kama Talha bin Ubaidillah, S a a d b i n A b i - Wa q q a s , Abdulrahman bin Auf, Zubeir bin Awwam, Uthman bin Affan na wazito wengine. Zaidi ya watu mia mbili mjini Makkah wakahama kutoka ushirikina na kuingia kwenye Uislamu. Lakini kadri idadi ya Waislamu ilivyokuwa ikiongezeka, ndipo upinzani dhidi yao ulipozidi kuwa mkali. Pia imenukuliwa katika historia kwamba wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipoanza da’awah yake, alipita nyumba kwa nyumba, akijaribu kuwafafanulia watu kuhusu umuhimu wa kutii mamlaka ya Mwenyezi Mungu, badala ya kutii mamlaka za kidunia. Aliweza kufanya hivyo bila ya kuleta mgongano kwa sababu ya heshima kubwa aliyokuwa nayo katika jamii. Ujumbe wake ulikuwa kumfuata Mwenyezi Mungu na kumtii kikamilifu, badala ya “kumuabudu” tu. Watu waliposhawishika na ujumbe huu, walikubaliwa katika kundi la Waislamu wa awali. Muungano huu wa Kiitikadi wa Waislamu wa mwanzo haukuanzia msikitini. Kulikuwa hakuna Misikiti Makka wakati ule, na wala hakuna mtu aliyeujenga. Hata hivyo, palikuwa na mahali pa kukutania palipoitwa ‘Dar ul - Arqam’, ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwafundisha Waislamu maana za Aya za Qur’an zilizoshuka wakati ule. Pale Waislamu walisoma kwa kina maana za Aya za Qur’an na kuzifanyia kazi. ‘Dar ul- Arqam’ pia, wanatueleza wanazuoni wa historia, lilikuwa kimbilio la Waislamu hawa wa awali,
Inaendelea Uk. 11

10

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Tamko la Maaskofu wa TanzaniaChristian Forum lina ukweli wowote?

Na Khalid S Mtwangi

KUNDI la maaskofu na viongozi wengine wa madhhebi mengi ya Kikristo yametoa tamko kali sana kuhusu uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu h u m u n c h i n i . Ta m k o hilo limetolewa chini ya taasisi inayoitwa Tanzania Christian Forum. Kwanza hayo ni maajabu makubwa kwa vile baadhi ya madhhebi katika muungano huo huwa hawaelewani kabisa katika mambo ya imani, hasa kati ya wale wanmaojulikana k a m a Wa l o k o l e n a Kanisa Katoliki. Hawa Walokole, ama Pentecoste humwita Baba Mtakatifu Papa kuwa anaeneza ushirikina (purbveypor of superstition). Leo hii ni ajabu hapa petu Tanzania hawa wameungana kuwapiga vita Waislamu. Hakika itakuwa sahihi kabisa kulitafsiri lile tamko lao kama ni tangazo la vita kati ya Wakristo kwa upande mmoja na Waislamu upande wa pili, hata kama vita hivyo mpaka sasa ni vya kujibishana maneno tu. Serekali kuu ikiwa kati ama kuwasaidia wale walio tangaza vita hivyo ama kuhakikisha kuwa kila siku haki inapatikana kwa kila Mtanzania. Ni kutimiza jukumu la kutoa haki tu kwa Wananchi wote ndio kutaweza kuepusha madhara yanayoweza kutokana na vita hivyo angalau vya maneno. Ikubalike kuwa vita hivi havitokani na wao Maaskofu kuhubiri mafundisho ya dini yao kwa mfano kumkubali Yesu kuwa mkombozi na Mtoto wa Mungu na ni Mungu aliyekuja akiwa katika wajihi wa BinAdam. Wanaamini kuwa hayo ni mafundisho yake Yesu hata kama ushahidi hauwahakikishii hivyo. Na wanaotoa ushahidi huo mara nyingi sio Waislamu tu bali baadhi ya Wakristo hasa

RAIS Jakaya Kikwete. wale wasomi wachambuzi wa Biblia na waandishi vitabu wa huko Ulaya. Kinachogomba hapa ni kuwa huyu Yesu ambaye WaKristo wanambambika sifa zote hizo ni Rasu-ul-Llah Issa AS kwa Waislamu. Hawa Waislamu wanatakikana kumpa heshima maalum akiwa Mtume na Mjumbe wa Mwenye ezi Mungu, lakini ni MTUME na MJUMBE tu. Wanapohubiri hivyo ni lazima wajulishe waumini wao kuwa hakika wao hawana ushahidi kuwa Yesu ni Mungu ama Mtoto wa Mungu, sasa ni haya ndiyo yanawaudhi waumini wa dini ya Kikristo na viongozi wao yaani mapadri wachungaji na maaskofu. Lakini hawana haki ya kuchukia hivyo kwa sababu hiyo ndiyo imani ya Waislamu na wahubiri wao wanawafundisha hivyo. Ni baadhi ya hawa viongozi wa Kikristo ndio nao wanawahubiria waumini wao kuwa Uislamu ni dini ya giza, Mtume Muhammad SAW ni Mtume bandia. Haya ni ya kila siku Waislamu wanafahamu. Kwa hilo hawa Waislamu wanastahili sifa ya uvumilivu kwani wao hawajatoa kauli kali ya kuwalaani viongozi wa Kikristo kwa kuhubiri uwongo huo. Swali muhimu hapa ni kujiuliza mwananchi yeyote anayeipenda nchi yake kama ilikuwa lazima kwa hawa

PAPA Benedict XVI watumishi wa Mungu kutoa vitisho kama vilivyomo katika tamko lao. Hivi haikuwezekana kupitia njia nyingine kujaribu kutatua tatizo hawa watumishi wa Mungu wanaloliona linaathiri mstakbali wa Tanzania? Ubaya zaidi ni kuwa tamko lao lina misingi ya mambo ambayo si ya kweli, ni ya kuzusha yakiambatana na hoja zi sio kuwa na mantiki. Kwanza hebu wasomaji watafakari shutuma za ati Waislamu wanaukashifu Ukristo. Imeelezwa huko nyuma mahubiri ya hawa Watumishi wa Mungu kumuhusu wanayemwita Yesu Kristo. Hakuna haja ya kurudia tena kuwa huyu ni Maja na Mtume wa Mungu tu katika mafundisho ya Waislamu. Ni binadamu aliyezaliwa na mama akanyonyeshwa na kutahiriwa kama wanaume wengine. Sasa kimantiki tu, haiwezekani aliyemshika mtoto huyu Yesu akamtahiri aamini kuwa huyu ndiye Mungu wake Mkuu. Kwa hiyo wakimwita hivyo na kutokukubali kuwa ni Mtoto wa Mungiu ama ni Mungu Waislamu wanasema kama wanavyofundishwa na imani yao. Hakuna zaidi ya hayo. Jambo moja kubwa ambalo Waislamu wanalilalamikia sana ni kule kunyimwa haki yao. Hii kwa kiasi kikubwa inatokana na kile Waislamu wanakiita MFUMOKRISTO.

ASKOFU mkuu wa KKKT Neno hili linawaudhi sana hawa watumishi wa Mungu; lakini wangekuwa watu wanaopenda kutoa haki wangetambua na kukubali kuwa hakika uko huo M F U M O K R I S TO h a p a nchini ambao pia unawaathiri sana Waislamu. Wanaloweza kufanya na wafanye kwa ufanisi kabisa ni kuwahubiria waumini wa makanisa yao wakisisitiza kuwa watumishi Serekalini watoe haki bila upendeleo mkubwa kwa Wakristo wenzao, huku Waislamu wakinyimwa haki zao. Baba Askofu Mkuu Elineza Sandoro wa KKKT anahubiri mara nyingi sana kuwa pale ambao hapana haki hapawezi kuwa na amani. Huyu mzee anasoma Biblia gani kama sio ile anayosoma Askofu Mkuu Mokiwa; ile ya Askofu Bruno Ngonyani labda inaweza kuwa tofauti kidogo. Hata hivyo lazima inaagiza kutoa haki. Wasomi wengi wanasema kuwa Yesu alikuwa mwanamapinduzi akitetea sana haki za wanyonge. Ninyi mnaojiita wafuasi wake Je? Ilipotangazwa kuwa siku ya Jumamosi nayo itakuwa ni siku ya mapumziko uwongo mwingi ulitolewa kuficha kwa nini hasa siku hiyo nayo imeteuliwa kuwa siyo siku ya kazi. Ilitambuliwa kuwa idadi ya waumini wa makanisa ya Pentecost ilikuwa imeongezeka marudufu

nchini humu kiasi kwamba siku ya Jumamosi ofisi nyingi zilibaki tupu. Hawa waumini hawakufika kazini hata kama walikuwa hawakupata ruhusa ya kuhudhuria ibada siku hiyo ya SABATO. Hutokea kuwa Waislamu hawapati ruhusa ya kuhudhuria ibada siku ya Ijumaa. Ni kwa sababu MFUMOKRISTO una nguvu sana nchini humu ndio ilikuwa rahisi kabisa kutangaza kuwa Jumamosi itakuwa siku ya mapumziko. Mpaka leo hii inakuwa vigumu sana kwa wanafunzi wa Kiislamu kuhudhuria ibada siku ya Ijumaa. Kwa vile sio siku ya mapumziko waalim wa Kikristo mashuleni huwakosesha makusudi wanafunzi hao masomo yaliyomuhimu kabisa. MFUMOKRISTO unafanya kazi. Linakuwa ni jambo la ajabu kabisa hawa watumishi wa Mungu kuwakasirikia Waislamu wanaposema kuwa kuna MFUMO KRISTO nchini humu kwa vile mfumo huo umekuwemo tangu wakati wa ukoloni na haujabadilishwa. Ila tu hivi sasa unatumiwa sana kuwanyima Waislamu haki zao. Nitoe mifani miwili tu, ingawa ni rahisi kujaza kitabu kizima kikiwa na mifano ya kuhakikisha kuwa MFUMOKRISTO upo na unaishi na afya yake nzurin tu. Kuna ushahidi kuwa kuna Waislamu wa Lindi walihangaishwa sana kupata leseni ya kuendesha shule yao walioijenga kwa nguvu zao wenyewe. Walikuwa wakizunguushwa kwa takriban mwaka mzima kila mara wakiambiwa hawajakamilisha hiki ama kile. Waziri wa Elimu ya wakati ule ambaye ni Mkristo aliingilia kati alipotambua kwamba wakati hawa WaSwahili wa Lindi wanahangaishwa kulikuwa na Padiri Mzungu ambaye alipewa leseni ya kuendesha shule kwa urahisi kabisa wakati naye alikuwa hajakamilisha masharti fulani. Watoa leseni walikuwa wote ni Inaendelea Uk. 11

11

Tamko la Maaskofu wa Tanzania-Christian Forum lina ukweli wowote?
Inatoka Uk. 10 Rais wa nchi hadharani kama alivyofanya Muhasham Polycarp Cardinal Pengo alivyoweza kufanya hivyo kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Na Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Askofu Mkuu Dkt Valentono Mokiwa kumpa Rais saa arobaini na nane kujibu swali alilotaka lijibiwe huyu Mtumishi wa Mungu. MFUMOKRISTO kweli unatawala. Huko nyuma baada ya mkutano wao huko Bagamoyo, viongozi wa Makanisa waliwahi kutoa tamko kali wakiiamrisha Serekali kuwakamata Wa i s l a m u w a n a o t o a mihadhara eti kuukashifu Ukristo. Walitishia kuwa kama Serekali haikufanya hivyo kulikuwa na uwezekano wa kutokea fujo na damu ya binadamu kumwaika. Sheikh Mbukuzi akiwa kiongozi wa Shura ya Maimam alitoa tamko ambalo halikuwa kali kama hilo la Maaskofu lakini

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

waumini wa Kanisa Katoliki. MFUMOKRISTO ulkuwa ukifanya kazi yake. Pia ilitokea kwamba maofisa wa Wizara ya Elimu walikwenda kufanyia Kazi yao Morogoro kukimbia mazingira ya kazi nyingi ofisi Dar es Salaam. Sikuu ya IDD UDH-HA iliwakuta huko, lakini kiongozi wa msafara wao alikana kutoa ruhusa maofisa wa Kiislamu kuhudhiria hiyo ibada muhimu sana. Lakini alifunga kazi siku ya Jumapili kutoa nafasi ya maofisa wa Kikristo kuhudhiuria misa. MFUMOKRISTO unafanya kazi yake hapo. Mifano yote hii ni ya kweli kabisa; hakuna uzushi hata kidogo na wasoma magazeti bila shaka waliweza kusoma taarifa ya mkasa huu wa pili, wa Morogoro. Ni MFUMOKRISTO tu unaoweza kumpa kiongozi wa dini ujasiri wa kumkemea

litahdharisha kuvunjika kwa amani ikiwa dhulma dhidi ya Waislamu haitamalizwa. Masikini Sheikh Mbukuzi alikamatwa na kutiwa jela, akavunjiwa heshima yake kabisa. Pia kutokana na ugomvi ulioko katika Kanisa Katoliki kati ya viongozi wa Kanisa hilo na wanaoitwa Wanamaombi wakiwa wafuasi wa Father Mkwera Padri mmoja aliyempiga Mwana maombi ilibidi apelekwe mahakamani. Kwanza askari wa kituo cha Magomeni walipata kigugumizi kumpeleka mahakamani padre Yule. Hata alipofikishwa mahakamani kama muhalifu mtuhumiwa yeye alipiokelewa kwa hashima kabisa na kupewa kiti cha kuka akisubiro kupandishwa kizimbani. Haya yote ni kweli kabisa na yaliwezdekana

tu kwa nguvu ya MFUMOKRISTO. Hivi ni kwa nini hawa watumishi wa Mungu hawaoni vibaya kuvunja Amri za Mungu alizopewa Nabii Musa? Wanaweza kusema uwongo hadharani kiasi hicho? Hivi ni kweli uongozi wa Serekali nchi hii ni asilimia tisini ni Waislamu? Serekali ni zaidi ya Rais, Makamu wake, Mkuu wa Polisi nakadhalika. Kwa mfumo wa Serekali ulivyo hivi sasa ni Makatibu Wakuu ndio watendaji wakuu na ndio washika fedha zote na kusimamia matumizi yake. Sasa hebu watuambie ukweli hawa watumishi wa Mungu kuna Makatibu wakuu wangapi walio Waislamu katika Serekali hii ya leo na ya jana na hata ya juzi. Enyi watumishi wa Mungu (Mwenye Nafsi Tatu- ahsante Nacaea)

kwa jina la mnayemwita Muokozi acheni uchochezi. Ni uchochezi unaotokana na uwongo mkubwa kuwa Waislamu wanataka kuwauwa maaskofu. Inafahamika wazi kabisa kuwa Muhasham Polycarp Cardinal Pengo ni mmoja wa viongozi wa makanisa ambaye haipendi kabisa dini ya Kiislamu kama alivyo kiongozi wake Papa Benedict XVI. Lakini kusema kuwa kuna Waislamu ambao wanataka kumuuwa huyu Mukombe ni uwongo kabisa. Dhambi kubwa. Ni vizuri kutia mkazo kwamba Tanzania Christian Forum wasisitize kwa waumini wao kutoa haki kwa wote bila upendeleo kwa misingi ya dini. Vitisho vyote walivyovileta hawa watumishi wa Mungu havitakuwa lazima. SHIME WAHUBIRI HAKI NA SIO VITISHO!!!!!
hizo. Si kwamba alikuwa na nia ya kuwachochea, isipokuwa maneno yake ya ukweli, yaliyojaa haki, ndiyo yaliyotikisa tabaka tawala la Makka. Na mfano huu ndiyo msingi muhimu wa Sunna na Sira. Katika hatua ya pili, Mtume mwenyewe ndiye aliyebeba matokeo ya ghadhabu za vigogo wa Makka. Ustahimilivu huu na nguvu ya kibinadamu kukabili shinikizo kali, bila ya kuathiri au kuchakachua ukweli tunaopaswa kusema, ni sunna muhimu na sehemu ya mwenendo wa Mtume. (Itaendelea)

Inatoka Uk. 9 ambapo walihisi wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kila shinikizo dhidi yao kutoka kwa Washirikina wa Makka l i l i p o z i d i . Wa l i e n d e l e a kukutana pale kwa siri mpaka Mwenyezi Mungu alipotoa maelekezo, ambayo yalifungua ukurasa mpya wa mahusiano baina ya Waislamu na Washirikina wa Makka: “Basi yatangaze uliyoamrishwa (wala usijali upinzani wao) na ujitenge mbali na (vitendo vya) hao washirikina” Qur(15:94). Haikuwa siri Muhammad (saw) alikuwa katika Kazi Maalumu ya Kiungu (Divine Mission), kubadilisha jinsi watu walivyohusiana wenyewe kwa wenyewe na jinsi walivyohusiana na Mwenyezi Mungu. Hicho ndiyo kilikuwa kipengele muhimu sana cha harakati zake. Ameleta mfumo mpya wa maisha (Dini) ambao binadamu na Mwenyezi Mungu wanahusiana. Alijua hili lingehitaji mshikamano na Waislamu wote kufanyakazi ya kuleta mpangilio mpya wa kijamii. Washirikina wa Makka walitambua haraka sana hatari ya mfumo huu mpya kwa hadhi na maslahi yao. Hawakutaka mtu yeyote,

Mtume amenyooka, harakati zetu zimepinda!
hata Mtume wa Mwenyezi Mungu, avuruge biashara zao nono, masoko yao ya watumwa na imani zao za kishirikina zinazolinda unyonyaji huo. Ikumbukwe kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuwalingania makafiri Uislamu. Aliwalingania watu wa kawaida (wananchi). Hawa ndiyo watu ambao Mtume amekuja kuwazindua. Kabla hawajaletewa Uislamu, hawakuwa makafiri; ni pale tu walipomkana Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ndipo wakawa na hatia ya kufru na shirki. Lakini hata hivyo milango ya toba ilikuwa wazi kwao. Wakati fikra za Kiislamu zilipoanza kukubalika kwa watu wengi zaidi wa kawaida, vigogo wa Makka waliogopa kweli! Ilikuwa ni hofu ya uwepo wao, ambayo haina uhusiano wowote na jinsi Waislamu walivyotekeleza taratibu zao za Ibada. Katika hatua hii, kile ambacho kilianza kama ufafanuzi wa Uislamu, kikawa mgongano mkubwa wa imani na fikra. Kuanzia hapo na kuendelea, uhusiano kati ya Waislamu wanaoibuka Makkah na watawala wa Makka, ukawa ni mapambano ya kifikra, kimaslahi na kimaongozi kati ya Uislamu na Ukafiri. Shinikizo dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwa Washirikina wa Makka lilikuwa kubwa mno, lakini kamwe Mtume hakubadili msimamo wake. Subira hii na msimamo wa kuvumilia mateso, kero, manyanyaso na maumivu mbalimbali, imechukuliwa kuwa sunna muhimu sana, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu ameuachia umma huu. Tabia yake ya kijamii, mpango wake wa kazi na kampeni zake makini dhidi ya mifumo migumu ya kikafiri, hakutajwi kabisa na pengine hata kutambuliwa na wanaharakati wa Kiislamu leo! Mtume alifanyiwa dhihaka na watu wazito wa Makka waliodhibiti uchumi, siasa, majeshi na masuala ya kijamii. Maquraysh walijaribu kumpuuza, wakitarajia kwa kufanya hivyo watamkatisha tamaa aache harakati zake. Moja ya kejeli zao ni pale kila Mtume alipowapita kwenye mikutano au mijumuiko yao

walisema: “Huyo anakuja mjukuu wa Abdul Mutallib, ambaye anasema mbingu zinazungumza naye!” Hiyo ndiyo hali ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu alikabiliana nayo. Kila jibu alilotoa ni mafundisho ambayo Waislamu tunapaswa kuyaiga. Katika hatua ya kwanza, Mtume alisema kitu ambacho kiliwatikisa vigogo wa Makka kwa kiasi ambacho kiliwafanya watoe kejeli za kipumbavu kama

1118 sqm - 4 Milion, 1261 sqm 5 milion, 1348 sqm 5.5 milion, 674 sqm 3 milion, 848 sqm - 3.4 milion, 510sqm - 1.5 milion, 516sqm - 2 milion, 522sqm - 2 milion, 523sqm - 2 milion, 646sqm - 2.6 milion, 656sqm - 2.6 milion, 474sqm 1.8 milion, 456 sqm 1.8 milion, 538 sqm 1.8 milion, 469sqm 1.9 milion, 406 sqm 1.6 milion, 356sqm 1.5 milion, 399sqm 1.6 milion, 359sqm 1.5 milion, 612sqm 3 milion. Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

Viwanja vilivyopimwa vinauzwa Kongowe Kibaha

12

Barua/Shairi

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

MATHNA:
1.Mume wangu nakupenda, dunia naieleza Unanitia kidonda, ambacho kitanimaliza Kwanini unanitenda, mwengine kumuongeza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 2.Najua ni haki yako, mathna kutekeleza Ibada yenye mashiko, Rasuli ndiye wakwanza Kwetu yeye ni itiko, pekee wa kumgeza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 3.Usinione kituko, maswali kukuuliza Ulichokiona huko, kipi sijatekeleza? Nipatie lalamiko, hali ni taigeuza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 4.’’Shepu’’ zao za kichina, niwengi zimewaponza Mtoto alivyonona, kupita kakuchokoza Fahamu ukawa huna, ukaenda bembeleza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 5.Tazama wake uzuri, hapo ndipo pakuanza Amejitia uturi, na nguo za kupendeza Umbo lake kasitiri, haramu kulieneza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 6. Ukoo sijasahau, ni muhimu kuchunguza Kweli ni washika dau, au mkia buruza Usijefanya dharau, jambo hili kupuuza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 7. Zingatia zake mali, ni wapi amewekeza? Isije kuwa muhali, za kwangu kuzieneza Nimechuma jua kali, machungu sijamaliza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 8. Amezingatia Dini, ama wataka mfunza? Jambo hili ni makini, kipolo sito lilaza Watapoteza imani, wanangu wakenda cheza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 9. Si semi nimeruhusu, ukaanza jipongeza Bado ni ‘’pasu kwa pasu’’, sikubali jilegeza Kabisa lengo la kisu, napinga si kuumiza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza 10. Kadimati kaditama, hapa ndio namaliza Nenda kaowe salama, shika ya kukuongoza Usije enda mrama, dira ukaipoteza Najua ni haki yako, mathna kutekeleza Is-haq Hemed Mzuzuri S.L.P. 1031 MUM Morogoro hemedisihaka@yahoo.com

SMZ na ‘ubwabwa wa shingo’ usiokwisha
SERIKALI kimantiki ni chombo kikuu cha nchi, chenye nguvu na mamlaka ya kujifanyia na kujiamulia mambo yake mwenyewe. Isitoshe, Serikali ni chombo ambacho kina wajibu mkubwa wa kusimamia maslahi ya nchi, wananchi, na muruwa wa nchi kwa ujumla. Kwa kufanya haya Serikali huwa ni chombo chenye dhamana ya kusimamia shuhuli zote za maendeleo, kuzitathmini na kuzichukulia hatua inayofaa, ikibidi kuwa hivyo. Serikali ina wajibu wa kupambana na uchumi kwa nguvu zote kuhakisha kuwa nchi na wanachi hawarudi nyuma zaidi badala yake wanakwenda mbele. Pamoja na changa moto za mabadiliko ya kiuchumi, na hali zinazopelekea kudorora kwa uchumi wa nchi, Serikali bado ina wajibu wa kuandaa mikakati ya kupambana na hali hiyo isiathiri sana nchi na kuirudisha nyuma zaidi kimaendeleo. Hivi ndivyo Serikali inayojali dhamana zake inavyotakiwa kusimama. Cha kushangaza katika safu hii leo, ni kuona Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imefika hatua ya kuwa tukae na kuanza kuitathmini kwa kuiuliza maswali kadhaa ya kututhibitishia utendaji wake kama Serikali. Na hili hatutaki itubainsihie kwa kutuonesha kama ipo na ina nguvu kwa kutujazia vyombo vya dola na usalama kutukandamiza, kutudhulumu na kutuangamiza kama tulivyozoea. Tunataka ituthibishie kwa vitendo juu ya utendaji na utekelezaji wa kazi zake, mpaka tukafika hapa tulipo. Itueleze inakuwaje kuwa kila uchao tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Ni ajabu bin-aibu kuona Serikali yetu licha ya kutimiza nusu karne ya uhuru, bado yaendelea kujiita changa. H aikuw i, haitanuki w ala haisogei mbele pamoja na juhudi nyingi zinazofanywa kuikwamuwa na wananchi na mataifa wahisani. Imekuwa sasa kila uchao afadhali ya jana. Serikali yetu ni tegemezi kuliko Serikali nyingi duniani. Na bahati mbaya utegemezi wenyewe haumaliziki. Na bahati mbaya hata tukisaidiwa ni mwaka mmoja tu hakuna kinachobakia tena. Serikali imesaidiwa mambo mangapi na wafadhili na matokea yake hata kuyasimamia inashindwa. Leo hii Serikali inaweza ikapewa msaada wa magari ya ujenzi wa bara bara, mathalan. Magari yale yatajulikana kuedeshwa tu, kikiharibika kipuri hata cha shilingi mia tano, hicho hakitafutwi, na gari hilo hufa, ilhali bado lilikuwa linatengezeka. Na mtindo huu sio kwa magari tu, ni kila kitu tunachopewa au kusaidiwa huwa hivyo. Umefika pahala tunategemea hata kipuri cha mia tano tufadhiliwe. Serikali inashangaza sana kuona hata baadhi ya majengo yake muhimu kama vile ukumbi wa Chachani na hata majumba ya Mji Mkongwe, yanafikia kuanguka, na hakuna kiongozi mwenye habari. Serikali husubiri mpaka majengo yaanguke au yaangazwe kwenye vyombo vya habari, ndio ikimbilie kukaguwa kama vile wao hawaishi kamwe nchi hio au hawakuwepo. Na bila shaka hawapo kweli maana wameshuhulika na mambo yao binafsi na vikao vya kujaza askari na vikosi bila kujali hali za wananchi. Tumezoewea kuona Serikali ikijitokeza haraka haraka kila pale mwanchi au kikundi cha wananchi kinapochomoza kudai haki yao au jambo lao fulani la msingi. Hapo Serikali hupata silaha, na fedha hupatikana za kulisha vikosi na kupigisha kambi za kuwatesa wahusika. Na hili huendelea kwa miezi k a d h a a . Tu m e o n a k u l e Shengejuu mwaka 1995, Piki mwaka 2005, na hivi majuzi hapo Bububu. Katika hali kama hizo Serikali hukubali iingie cha tisa cha kumi kiwafukie lakini waoneshe nguvu na uwezo wao. Hupatikana makachero waliobobea na kila kitu alimradi nguvu yao hapo ionekane na wananchi waitambue Serikali yao kama ipo. Na huu ndio utamaduni inaoujenga Serikali kuwa ili ijulikane kama ipo, ni lazima ipige, ikamate watu na kuwaweka ndani bila ya dhamana na sio ilete maendeleo ambayo ndio chachu ya hio amani na utulivu wanayoihubiri kila siku. Lakini kwa mtazamo wao amani haiji ila kwa ncha ya upanga! Cha kushagaza zaidi, nguvu ya Serikali yetu ipo katika kuonea raia tu na sio kwa kuijenga nchi hii. Leo hii wakati Serikali ikijipatia mapato makubwa ya bandari na uwanja wa ndege, inashindwa kujega miundo mbinu ya Sehemu hizo. Badala yake inawauzia wafanyabiashara, tena kimya kimya. Serikali badala ya kukarabati majengo yake yanayobomoka, kuboresha huduma za afya maspitalini na elimu bora shuleni, inajinulia magari makubwa na kujipagia mishahara minono. Badala ya kutunza fukwe na ardhi zetu Serikali inauzia wageni ambao wanaturudisha kule kwenye ukoloni. Leo hii kuna maeneo Zanzibar raia hathubutu kupita na wala sio maeneo ya jeshi, ulinzi wala usalama. Kisa, kuna Wazungu. Leo hii kuna ardhi na visiwa vimeuzwa kwa miaka 100 ijayo na nyengine zimeuzwa kwa kudumu, tena kwa wageni. Faida ya mauzo hayo haionekani. Inakuwa nchi yetu ni fungu la kukosa tu. Huu ni ubwabwa wa

shingo kusema kweli. Ni ukweli usifiochika kwamba Serikali haina kipato kikubwa lakini hili linatokana na ubwabwa wao wa shingo vile vile. Ya kwamba hicho kinachopatikana kinawanufaisha wengine, na hicho kidogo kinachobakia kinaishia matumboni mwa watu. Kinachobaki ni kupita nchi hii na ile kuomba misaada. Wakishakupewa misaada hiyo, tunajikaza kuweka mawe ya msingi na kuizindua. Miaka miwili miradi ile imakufa na wala Seikali haina habari tena. Cha kusikitisha mno ni kuwa hata ukiangalia sababu ya kifo cha miradi hio, ni kukosekana usimamizi nzuri tu wa Serikali na watendaji wake. Tumefadhiliwa ujenzi wa mji mkongwe, umetushinda. Awali tulifadhiliwa na Japan katika Idara ya Habari na Maelezo pale TVZ, matokeo yake jengo linashindwa hata kupakwa rangi. Mitambo iliyomo imekufa. Kila kitu kimekufa. Jengo la Raha Leo tuliofadhiliwa na China linavunja kama muembe, hakuna usafi wa mazingira kulizunguka wala ukarabati. Nani anajali angalau kuchomelea makuti tu kule paani? Juzi tumeshafadhiliwa mitambo ya ‘digital’, baada ya mwaka imekufa na licha ya kuwa mwananchi asie ana ajira atalazimika kulipia kuona habari katika TV, huduma hio itakosekana kwa wanaolipia na wasiolipia baada ya mitambo hio kufa bila kukarabatiwa. Haya ndio mazoea yetu. Iwapi Redio Zanzibar iliyoikisikika mpaka Mombasa Kenya? Haisikiki hata Pemba. TVZ, kwa miaka haipatikani Pemba, kunani? Serikali ichanga! Kwa haya na mengine mengi, kuna kila sababu ya kusema kwamba Serikali yetu haiwajibiki ipasavyo. Na bahati mbaya imejenga utamaduni mbaya sana wa kutegemea wahisani katika kila jambo. Wakati kukiwa na mipango kadhaa ya kujipangia maendeleo na kujitegemea kama tulivyokuwa zamani. Serikali imeshuhulika na kijumba hodi kuomba misaada. Ukweli tumeshafadhiliwa mengi, na kuyauwa baada ya mwaka bila hata kuyakarabati hata ikiwa matengenezo hayo tunayamudu wenyewe. Na sasa kuna kila dalili kwamba wahisani wameanza kuchoka. Wanatuona mzigo usiobebeka. Hivyo kuna haja tubadilike. Japo hatuwezi kutambaa kwa uchanga wetu, basi hata kujishikilia vichwa hatujaweza? Tutatoka lini ubwabwa wa shingo? Nawasilisha. (Mwananchi mpenda maendeleo. Umenukuliwa kutoka mtandao)

13

Makala

Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba ya umma?-2
Na Dr. Noordin Jella

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

KWENYE nchi za Kijamaa Kitengo cha Usalama wa Taifa kinapofanya unyama wa kuteka raia, kuwatesa na hata kuwaua, au wanapowavamia raia majumbani mwao (vitendo vya ujambazi), huwa wanasingizia majambazi, lakini kiukweli wao wenyewe ndiyo majambazi kwani hata kwenye kitengo chao kuna Mkurugenzi wa Ujambazi na Idara ya Ujambazi pia, na Idara ya Polisi huwa siku zote ndiyo wanaobebeshwa mzigo wa kuwasafisha Usalama wa Taifa kwa kuchukua lawama zote na kujifanya kuwa wimbi la ujambazi limezidi na wao kama polisi wameshindwa kulidhibiti! Wanafanya hivyo ili kujipendekeza kwa Rais kwa vile Kitengo cha Usalama wa Taifa katika nchi za Kikomunisti kipo katika ofisi ya Rais hivyo wakiacha kitengo hicho kikalaumiwa ina maana Rais ndiye atakayekuwa analaumiwa, na kiutaratibu Rais katika nchi za Kijamaa ni Mungu Mtu hana dhambi wala lawama au wengine wanapendelea kumuita “Mwenyekheri”, yaani mtu mtakatifu asiyekuwa na dhambi! Hivyo ni kwamba Idara ya Polisi huwa ndiyo wanaotumiwa kubeba lawama zote na kujitolea kukubali kwamba wao ndiyo wahusika wa shutuma zote zile zinazoilenga Ofisi ya Rais, na hata wakati mwingine wanaweza kutafutwa watu wa kujitolea na kudai kwamba wao ndio wahusika wa shutuma hizo, hivyo wakapelekwa mahakamani wakashitakiwa na kuhukumiwa kifungo cha UONGO ili mradi tu wananchi waridhike wasiendelee kumlaumu Rais. Kwenye nchi za Kijamaa Madaktari na wauguzi hulipwa mishahara midogo sana kuliko idara zingine. Hii hufanyika makusudi ili wachukue rushwa toka kwa wateja (wagonjwa) wao kwa vile serikali inaelewa wazi kuwa wapo kwenye kitengo muhimu ambacho kwa vyovyote vile raia atatoa rushwa atake asitake. Serikali za Kijamaa zinaamini fika kwamba lazima Madaktari na Wauguzi wawe wanachukua rushwa ila tu waendelee

MWALIMU J.K. Nyerere. kufanya hivyo ili mradi wagonjwa wasilalamike. Rushwa na Ufisadi ni uti wa mgongo wa mfumo wa siasa za Ujamaa, ndiyo maana utakuta huduma au bidhaa mbali mbali hupatikana kwa vibali, na vibali maana yake ni kwamba lazima utoe rushwa kwa wale waliopewa mamlaka za kutoa vibali hivyo. Nchi zote zilizokuwa zinafuata siasa za Kijamaa zimeshindwa kufanya mabadiliko ya ukweli ya kutoka kwenye Ujamaa na kwenda kwenye Ubepari (free market economy), na matokeo yake nchi nyingi zimeishia kujenga serikali na mfumo wa Kijambazi “Banditry Government”. Kumekuwa na wimbi kubwa la Ufisadi wa kutisha kwenye zile nchi zote zilizokuwa zikifuata siasa za Kikomunist. Hii haitokei kwa bahati mbaya, hapana. Hutokea hivyo kwa makusudi kwa vile mfumo wa Kijamaa ni mfumo gandamizi, mfumo wa matabaka, tabaka la wanaoongoza na tabaka la wanaoongozwa, na kila tabaka lina kiwango chake cha maisha. Enzi za Soviet Union ilikuwa si rahisi kwa mtu wa kawaida anayetoka kwenye kundi la watawaliwa amtembelee mtu aliyeko kwenye kundi la watawala bila taarifa. Ilikuwa ni lazima utoe taarifa ili mtawala atengeneze mazingira duni yanayofanana na yale ya mtawaliwa ili asije akashtuka, kwa vile wanapokuwa wenyewe kwa wenyewe (watawala) wanaishi maisha ya kifahari sana, wakati watu wa kawaida (watawaliwa) wanatumia bidhaa zilizotengenezwa ndani ya nchi yao ambazo zina viwango duni wao (watawala) walikuwa wanakula bidhaa

ALHAJ Ali Hassan Mwinyi toka nchi za Magharibi (Bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa). Nguo zao pia zilikuwa zinatoka nchi za Magharibi lakini walikuwa hawazivai ndani ya nchi mpaka wakisafiri nchi za nje. Walikuwa wakifanya hivyo ili wananchi wasije wakashtuka kwamba wanaibiwa. Enzi za Soviet Union ukikutana na Mrusi mjini New York - Marekani ulikuwa huwezi kumtofautisha na Mmarekani labda aongee kwa vile walikuwa wanavaa vitu vizito vya bei mbaya ambavyo hata Wamarekani wenyewe hawawezi kuvinunua. Wakomunisti wa Kirusi walikuwa Mafisadi wa kutisha lakini walikuwa na Nidhamu ya hali ya juu na ya kutisha. Walijitahidi sana kuwaficha raia wa kawaida yale wanayoyafanya. Mwaka 1997 waandishi wa habari wa Urusi waliwahi kumuuliza kiongozi wa chama cha kikomunist cha Urusi kama anajua zilipotokomea US $ 400 billion za Wa k o m u n i s t i a m b a z o zilihifadhiwa bank za nje. Kati ya mwaka 2000 na 2005 waziri mmoja toka nchi ya Afrika Mashariki iliyokuwa inafuata siasa za Kikomunisti alienda Marekani kikazi, basi baada ya mazungumzo na maofisa mbali mbali wa serikali ya Marekani, waziri huyo alitoa ofa kwa wajumbe wote waliokuwapo kwenye mkutano huo akiwaambia wale na wanywe chochote wanachotaka atalipa! Wamarekani walishangaa waziri ambaye amekuja kuomba msaada wa pesa kwamba nchi yake ina kabiliwa na ukata anawezaje kutoa ofa kubwa kiasi hicho. Wengi wakawa na wasi wasi kwamba anaweza ashindwe

MHE. Benjamin W. Mkapa kulipa! Wageni wakaitikia wito wakala na kunywa kwa nguvu zao zote. Bili ikaja US $ 200,000, waziri akaingiza mkono mfukoni akatoa master card (visa) ikatolewa dola laki mbili na baada ya hapo waziri akarudisha card yake kwenye wallet kwa ushujaa na furaha tele! Mwaka 1998 wanasheria wawili wa Marekani waligundua kwamba katika bank account moja huko New Jersey Marekani kulikuwa na US $ 5 Billion zilizowekwa kwa jina na Kigogo mmoja wa serikali ya Angola. Ikumbukwe kwamba Vigogo wengi duniani huweka pesa zao kwenye bank za Switzerland ambapo ndipo wanapoamini ni pepo ya dunia ya wale waliojaliwa kutawala, hivyo kama New Jersey kuna UD $ 5 Billion! Je, huko Switzerland huyo muheshimiwa au Kigogo huyo atakuwa na Billion ngapi? Ukitumia methods za theory of probability utapata jibu sahihi, ili mradi tu ukumbuke kwamba probability haiwezi kuwa chini ya zero au kuwa zaidi ya moja . Kwenye nchi zote za Kikomunisti uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali wa umma unafanyika kama ushahidi tu, lakini kura za wananchi huwa hazihesabiwi. Wananchi wanapiga kura lakini viongozi walishachaguliwa siku nyingi. Wakati mwingine hata post wanakuwa wameshapangiwa wakati wananchi wanapiga kura! Ee huo ndiyo Ujamaa ndugu zangu, ujamaa ambao Nyerere aliupenda sana, na aliusimamia kwa kila hali kwa miaka 23! Ujamaa maana yake Endeleeni kutuvumilia!

RAIS Jakaya Kikwete. Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbali mbali ya ufisadi hapa nchini (EPA, MEREMETA, KAGODA, BUZIGWA, NYAMONGO, CONTAINER LAPEMBE ZA NDOVU NA FARU HUKO VIETNAM NA CHINA, TWIGA KUPANDA NDEGE n.k.). Kila palipokuwa na mkusanyiko wa watu (Vijiweni): kwenye Dala Dala, Sokoni, Magengeni, Ndani ya Mabasi yaendayo Mikoani, Mitaani na Vijijini kote nilikopita nimesikia watu wa rika mbali mbali wenye hasira wanajadili na kubishana bila ya kupata suluhu, na wengine wamekuwa wakisema “Kama Nyerere angekuwepo haya yote yasingetokea” Maneno haya akiyaongea mtu aliyezaliwa baada ya mwaka 1985 siwezi kumlaumu kwa vile hakuwahi kusikia harufu na wala hakuwahi kumuona Nyerere akiwa madarakani na wala hakuwahi kunywa UJI wa kibaba cha “KAYA” uliokuwa unagawiwa kila nyumba baada ya nchi kukumbwa na tetemeko la njaa lililosababishwa na vita vya Uganda na Ta n z a n i a . I s i p o k u w a maneno haya yananikera sana pale yanapoongelewa na Wakubwa wenzangu, na wengine kwa bahati mbaya zaidi wakati Nyerere akiwa madarakani w ao tayari walikuwa wanategemewa (yaani walikuwa na familia). Nasema ama kweli Watanzania hatuna kumbukumbu kabisa. Watanzania tumekuwa na kumbukumbu Duni kabisa. Tu m e k u w a k a m a w a t u tuliopumbazwa kwa vile vichwa vyetu havikumbuki jana wala havifikirii kesho. Vichwa vyetu vinajua leo ni Inaendelea Uk. 14

14

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Ugaidi wenye ‘sura ya kiutu’:
Na Profesa Michel Chossudovsky Januari 6, 2013, ‘Mtandao wa Kupashana Habari” Kusajiliwa kwa vikundi vya wauaji ni sehemu mahsusi ya ajenda ya kijeshi ya jeshi la Marekani. Kuna historia ndefu na ngumu ya Marekani kutoa fedha kwa siri kuwezesha brigedi za kigaidi na mauaji ya kulengwa ambayo yalianzia katika vita vya Vietnam. Wakati majeshi ya serikali yanaendelea kukabiliana na kile kinachojiita ‘Jeshi Huru la Syria’ (FSA), mizizi ya kihistoria ya vita vya kificho vya nchi za Magharibi dhidi ya Syria - ambavyo vimesababisha mauaji yasiyotajika - lazima sasa ifunuliwe wazi. Kuanzia ilivyoanza Machi 2011, Marekani na washirika wake wameunga mkono kuanzishwa kwa vikundi vya mauaji na kuingiza brigedi za kigaidi katika mpango ulioasisiwa kwa uangalifu. Kusajiliwa na kupewa mafunzo kwa brigedi za kigaidi katika Irak na Syria kuliendana na ‘mtindo wa Salvador,’ ambao ni mfano maalum wa operesheni za kigaidi kuua watu wengi zilizoasisiwa huko Marekani ya Kati. Ilitumika kwanza nchini El Salvador, wakati wananchi wa huko wakipambana na utawala dhalimu wa kijeshi wa maswahiba wa Marekani, ambako watu 75,000 walipoteza maisha. Kuundwa kwa vikundi vya mauaji nchini Syria kunajengwa katika historia na uzoefu wa Marekani katika kuunda brigedi za kigaidi nchini Irak, chini ya mkakati wa Pentagon (Makao Makuu ya Jeshi la Marekani) wa ‘kukabiliana na ugaidi.’ Kuundwa kwa Vikundi vya Mauaji nchini Irak Vi k u n d i v y a m a u a j i vinavyofadhiliwa na Marekani viliundwa nchini Irak mwaka 2004-2005 katika mtitiriko ulioanza chini ya Balozi wa Marekani John Negroponte ambaye alipelekwa Baghdad na Wizara ya Mambo ya Nje mwezi Juni 2004. Negroponte alikuwa ndiye ‘mtu wa kazi hiyo.’ Akiwa balozi wa Marekani nchini Honduras kuanzia 1981 nadi 1985, Negroponte alichukua nafasi muhimu ya kuunga mkono na kusimamia kundi la Contra la Nicaragua likiwa limejichimbia Honduras, na pia akisimamia vitendo vya vikundi vya kijeshi vya mauaji nchini Honduras. Chini ya utawala wa Jenerali Gustavo Alvarez Martinez, serikali ya kijeshi ya Honduras ilikuwa mshirika wa karibu wa utawala wa Reagan nchini Marekani, na walikuwa ‘wanapotea’ wapinzani wa kisiasa kwa makundi, kwa njia inayoshabihiana na mtindo wa kawaida wa makundi ya mauaji. Hapo Januari 2005 Pentagon ilithibitisha kuwa ilikuwa inaangalia: “kuundwa kwa vikundi vya mashambulio ya kushtukiza ya Wakurdi na Wa-Shia kulenga viongozi wa upinzani dhidi ya Marekani katika mwelekeo wa kimkakati unaofanana na mapambano ya Marekani dhidi ya magaidi wa kimapinduzi wa Marekani ya Kati miaka 20- iliyopita.” Chini ya k i l i c h o i t w a ‘mkakati wa Salvador,’ vikosi vya Irak na Marekani vingepelekwa kuua au kutekwa viongozi wa harakati dhidi ya Marekani, hata nchini Syria, ambako baadhi wanaaminika wametafuta hifadhi. Vikundi vya mauaji vingeleta zogo na ingebidi viwe siri. Uzoefu na vikundi ‘vya mauaji’ katika Amerika ya Kati bado ni mbichi kwa wengi hata sasa, na ilisaidia kuchafua sura ya Marekani katika ukanda huo. Halafu, utawala wa Reagan ukaanzisha na kufunza vikundi vya wakereketwa wa kupinga ukomunisti kuyeyusha harakati ya wazalendo nchini El Salvador, kuwaua viongozi wake na watu wanaowasaidia.

Historia ya vikundi vya mauaji Marekani
Vikundi vya mauaji Irak na Syria Mizizi ya kihistoria ya vita iliyojificha ya Marekani na NATO dhidi ya Syria
John Negroponte, balozi wa Marekani mjini Baghdad, alikuwa na kiti cha mstari wa mbele kama Balozi wa Marekani nchini Honduras kati ya 1981 na 1985. Vikundi vya mauaji vilikuwa sehemu mahsusi ya siasa za Amerika ya Kusini wakati huo...... Katika miaka ya 1980 mwanzoni, utawala wa Rais Reagan ulifadhili na kusaidia kutoa mafunzo kwa makundi ya Nicaragua yaitwayo Contras (dhidi ya....), yaani ya uasi, yakijichimbia Honduras kupambana kuuondoa utawala wa kiSandinista (wa kimapinduzi) nchini Nicaragua. Makundi ya Contras yalipata silaha kutokana na uuzaji haramu wa silaha kwa (serikali ya kimapinduzi ya) Iran, kashfa ambayo ilikuwa na kila chembe ya kuweza kumuondoa madarakani Bw. Reagan. Mwelekeo wa pendekezo la Pentagon nchini Irak ....ni kufuata mfano huo.... Hakuna uhakika kama azma kuu ya mkakati huo ni kuwaua wapinzani (wa utawala wa Irak) au kuwateka nyara na kuwapeleka kwa kuhojiwa. Mkakati wowote wa kuingilia Syria itabidi ufanywe na vikosi maalum vya jeshi la Marekani. Pia hakuna uhakika nani atawajibika kwa mpango kama huo - kama ni Makao Makuu ya Jeshi la Marekani (Pentagon) au Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), Operesheni kificho kama hizo kwa jadi zimekuwa zikiendeshwa na CIA, ‘ikicheza mbali’ na utawala ulioko madarakani wakati huo, kuwapa uwezo maofisa wa Marekani kudai kuwa hawafahamu jambo kama hilo. Hiyo ilikuwa wazi katika taarifa “Vikundi vya mauaji” kama vya El Salvador kutumiwa na Marekani dhidi ya wanaharakati Irakiliwekwa kurasa za mtandao za gazeti la New York Times, Januari 10, 2005. Wakati lengo la mkakati uliobainishwa wa ‘Mbinu ya Salvador Irak’ likiwa ni “kuitungua” harakati ya Irak, katika hali halisi brigedi

RAIS Barack Obama wa Marekani. za kigaidi zilizoundwa na Mshauri wa Masuala ya Marekani zilishiriki katika Siasa katika Ubalozi wa mauaji ya wananchi wa Marekani chini ya Balozi k a w a i d a k w a l e n g o l a John Negroponte. Hakuwa kupandikiza chuki za kikabila tu sehemu ya washiriki wa na madhehebu. Kwa upande ndani bali alikuwa mshirika mwingine, CIA na MI6 wa Negroponte katika kuunda (Idara ya Ujasusi ya Jeshi mkakati wa Salvador kwa Irak. la Uingereza) walikuwa Misingi kadhaa ya mkakati w a n a s i m a m i a v i k u n d i huo ilikuwa imeshawekwa vilivyoitwa ni Al Qaeda mjini Najaf kabla ya Ford nchini Irak vikihusika katika kuhamishiwa Baghdad. John Negroponte na Robert mauaji ya kulenga miongoni mwa watu wa madhehebu ya Stephen Ford walikuwa Shia. Kilichokuwa muhimu wakiratibu kusajiliwa askari z a i d i n i k u w a v i k u n d i wa vikundi vya mauaji hivyo vya mauaji vilikuwa Irak. Wakati Negroponte vinaunganishwa kimtandao akiendesha operesheni kutoka na kushauriwa na maofisa ofisini mwake katika ubalozi, wa vikosi maalum vya Jeshi Robert S. Ford, ambaye anaongea bila kigugumizi la Marekani. Robert Stephen Ford - Kiarabu na Kituruki, alipewa ambaye baadaye aliteuliwa d h a m a n a y a k u a n z i s h a kuwa Balozi wa Marekani mawasiliano na vikundi nchini Syria - alikuwa vya wapiganaji wa Shia na sehemu ya ‘timu Negroponte’ Kurdi nje ya eneo la usalama Baghdad kuanzia 2004 hadi ilipojichimbia serikali ya Irak 2005. Mwezi Januari 2004 inayofadhiliwa na Marekani. Maofisa wengine wawili alipelekwa kama mwakilishi wa Marekani katika mji wa wa ubalozi, yaani Henry madhehebu ya Shia wa Najaf Ensher (naibu wa Ford) na ambao ulikuwa ngome kuu ya ofisa kijana katika kitengo jeshi la Mahdi, ambao alianza cha siasa, Jeffrey Beals, walikuwa na nafasi muhimu mawasiliano nao. Mwezi Januari 2005, Robert ya “kuzungumza na Wairaki S. Ford aliteuliwa Mwambata Inaendelea Uk. 15

15
Inatoka Uk. 14 tofauti, ikiwa ni pamoja na wenye siasa kali,” (taarifa iliyotolewa katika gazeti la New Yorker, Machi 26, 2007). Ofisa mwingine muhimu katika ‘timu Negroponte’ alikuwa James Franklin Jeffrey, aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Albanmia (2002 hadi 2004). Mwaka 2010, Jeffrey aliteuliwa Balozi wa Marekani nchini Irak (2010 -2012). Negroponte pia alimwingiza katika timu hiyo mmoja wa washirika wake wa awali, Kanali James Steele (mstaafu) aliyekuwa mshirika katika mikakati akiwa Honduras. Chini ya ‘mkakati wa Salvador’ Negroponte alisaidiwa na mshirika wake kutoka enzi zake Amerika ya Kati miaka ya 1980, Kanali Mstaafu James Steele, ambaye wadhifa wake (ubalozini) Baghdad ulikuwa Mshauri wa Majeshi ya Usalama ya Irak. Alisimamia usajili na mafunzo ya maofisa wa Shirika la Badr na Jeshi la Mehdi, makundi mawili makubwa ya Washia nchini Irak, kuwalenga viongozi na mitandao ya misaada ya wanaharakati w a K i - S u n n i . Vi k i w a vimepangwa au vinginevyo, vikundi hivi haraka vilivuka mipaka na kuwa chanzo kikuu cha mauaji nchini Irak. Iwe imenuiwa au la, idadi ya walioteswa, miili iliyoharibiwa ikionekana kote mjini Baghdad inazalishwa na vikundi vya mauaji ambavyo msukumo wake ulitoka kwa John Negroponte. Na ni uhasama huu wa kidhehebu uliochochewa na Marekani ambao uliifikisha Irak

Makala

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

AN-NUUR

Historia ya vikundi vya mauaji Marekani
katika dimbwi la umwagaji damu ambako imetumbukia hivi sasa. (Dahr Jamail, “Kusimamia kupanuka kwa vita: Negroponte na timu mpya ya Bush nchini Irak,” Antiwar/com (mtandao wa wapinga vita) Januari 7, 2007) “Kanali Steele alihusika, kwa mujibu wa Dennis Kucinih (mjumbe wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani) kutekeleza mkakati nchini El Salvador ambako makumi ya maelfu ya Wa-Salvadore ‘walipotea,’ au waliuawa, akiwemo Askofu Mkuu Oscar Romero na watawa wanne wa Marekani.” Alipoteuliwa kwenda Baghdad, Kanali Steele alipewa jukumu la kusimamia kikosi maalum cha kupambana na harakati (uasi) kinachoitwa “Makomandoo Maalum wa Polisi” chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Irak (iliripotiwa na shirika la habari la Cuba, ACN, Havana, Juni 14, 2006). Taarifa zinathinitisha kuwa “Jeshi la Marekani liliwatoa wafungwa wake wengi kwa Brigedi ya Mbwamwitu (Wolf Brigade), batalioni ya pili iliyoogopeka ya makomandoo maalum wa Wizara ya Mambo ya Ndani,” ambao ilitokea kuwa chini ya maelekezo ya Kanali Steele. “Askari wa Marekani walisimama pembeni wasifanye lolote,” wakati washirika wa Brigedi ya Mbwamwitu wakipiga na kutesa wafungwa. Makomandoo wa Wizara ya Mambo ya Ndani waliikamata maktaba ya Samarra na kuigeuza kuwa kituo cha kuzuia watu, alisema mwakilishi huyo. Mahojiano yaliyofanywa na Maass (wa gazeti la New York Times) mwaka 2005 katika jela hiyo ya kutengenezwa, akifuatana na mshauri wa kijeshi wa Marekani katika brigedi hiyo, Kanali James Steele, ilikuwa ikikatishwa na vilio vya mfungwa mmoja nje, alisema. Steele anasemekana aliwahi kuajiriwa kama mshauri wa kusaidia kuvunja uasi nchini El Salvador,” taarifa hiyo iliongeza. (Makala hii imetafsiriwa na Anil Kija kutoka makala: Terrorism with a “Human Face”: The History of America’s Death Squads. *Death Squads in Iraq and Syria. The Historical Roots of US-NATO’s Covert War on Syria-Iliyoandikwa na Prof . Michel Chossudovsky Itaendelea)

Je, Nyerere ni kikwazo cha katiba ya umma?-2
Inatoka Uk. 13 leo basi. Kwa nini tuwalaumu baadhi ya Mawaziri na Maafisa wa serikali kwa vitendo vya rushwa na ufisadi! Kwani wamefanya nini cha ajabu! Huu ndiyo mfumo wetu wa utawala. Ukistaajabu ya Tanzania utaona ya Angola; na ukistaajabu ya Cuba utaona ya North Korea. Huu ndiyo mfumo wa Ujamaa, Ujamaa maana yake ni tuvumilieni “Sisi wenzenu tumejaliwa”. Haya yanayotokea hivi sasa hapa nchini hayakuanza leo, wala hakuyaanzisha Mzee Mwinyi, wala Mkapa, wala Kikwete, bali haya aliyaanzisha Nyerere mwenyewe na aliyalea yeye mwenyewe na alipotoka madarakani hakutaka yafike kikomo bali alitaka yaendelee, ila yaendelee kwa ustaarabu ule ule aliokuwa anaundeleza yeye mwenyewe. Isipokuwa warithi wake wameshindwa kuyaendeleza katika ukimya ule ule uliokuwepo kutokana na sababu nyingi tu za mabadiliko ya hali ya hewa duniani zikiwepo marekebisho ya utawala, wimbi la demokrasia, uhuru wa kuongea wa Raia na vyombo vya habari. Wa k a t i w a N y e r e r e kulikuwepo na Ufisadi mkubwa wa kutisha lakini wakati wake hapakuwa na uhuru wa kuongea, magazeti yote na radio Tanzania vilikuwa mali ya serikali na wote waliokuwa wanafanya kazi huko walikuwa watu w a U s a l a m a w a Ta i f a , hivyo kila kitu kilichujwa kwanza kabla ya kuchapisha na kile kilichoonekana kitaleta minong’ono hakikuchapishwa kabisa, na Watanzania walijengwa na Propaganda mbaya ya kwamba habari nzuri na sahihi ni zile zinazotolewa na magazeti na radio ya Taifa basi. Magazeti ya nchi za nje yalikuwa hayauzwi hapa nyumbani. Magazeti ya kutoka nje yaliyoruhusiwa ni yale ambayo yamesomwa na wanausalama na kuona hayana habari yoyote ya kuwaamsha Watanzania usingizini. Nyerere alipiga marufuku magari kutembea Jumamosi na Jumapili mpaka upate kibali, na pia tusisahau vibali hivi ndicho chanzo cha kuenea kwa rushwa nchini na leo hii eti tunamtafuta mchawi wa rushwa ni nani!? Pia Nyerere alipiga marufuku mtu yeyote kuwa na Video, au TV alisema ni starehe! Lakini yeye nyumbani kwake Msasani alikuwa na TV na alikuwa na antennae ya ungo mkubwa ambao alikuwa anakamata matangazo ya nchi mbalimbali duniani! Wakati wa Nyerere kulikuwa na magazeti ya Uhuru, Mzalendo ya lugha ya Kiswahili, na Daily News na Sunday News yote mali ya serikali. Ili uwe Mhariri Mkuu wa Magazeti haya lazima uwe ni mtu wa System, na pia kulikuwepo na Radio Tanzania ambayo ilikuwa mali ya serikali, na ili uwe Mkurugenzi wa Radio hiyo lazima uwe mtu wa System na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM. Habari zote zilizokuwa zikitangazwa lazima kwanza zichujwe. Hivyo ni kwamba habari zote za Ufisadi zilifichwa kulingana na ufisadi wenyewe na nani anashutumiwa kwa ufisadi huo. Mwalimu Nyerere alikuwa hafukuzi mtu kazi kwa kufanya ufisadi, bali alikuwa anawahamishia sehemu nyingine. Ukifanya ufisadi kwenye shirika la BET unahamishiwa Air Tanzania, aliyefanya ufisadi Air Tanzania anahamishiwa Bandarini, na aliyefanya ufisadi Bandarini anahamishiwa RTC na kadhalika. Mkuu wa Mkoa akifisadi mkoa huu anahamishiwa mkoa mwingine; na Mkuu wa Wilaya aliyefisadi wilaya hii huhamishiwa wilaya nyingine nakadhalika! Balozi akifisadi Ubalozi huu, anahamishiwa Ubalozi mwingine akajirekebishe! Watanzania hatuna kumbukumbu, tukumbukeni ufisadi uliotokea miaka ya sabini na themanini; Mashirika na Makampuni ya umma yalifisadiwa sana, lakini waliohusika walihamishwahamishwa tu, na wengine baada ya kufanya ufisadi wa kutisha walipelekwa ubalozini nchi za nje wakapumzike! Huyo ndiye aliyekuwa Mwalimu Nyerere ninayemfahamu mimi. Isipokuwa huyu Nyerere mnayemfagilia hivi sasa mimi simjui! Kwa nini tumlaumu Dr. Kikwete kwamba hataki kuwawajibisha Mafisadi wakati Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anatawala kwa kutumia System ile ile ya Nyerere na watu anaofanya nao kazi ni wale wale waliokuwa wanafanya kazi na Nyerere ambao hawakuzoea kujiuzulu wala kufukuzwa kazi? Wao walizoeshwa kulindwa kwa kubadilishiwa kazi au kupewa uhamisho! Serikali ya Mheshimiwa Benjamin William Mkapa imefanya ufisadi mkubwa sana katika wizara ya madini na ufisadi huu ukifanyika Nyerere alikuwa hai licha ya kwamba hakuwepo madarakani! Na Ufisadi huu bila kuficha utawatesa Watanzania kwa miaka mingi ijayo. Lakini pamoja na ufisadi wa kutisha uliofanyika ni kwamba ufisadi huu umefanywa na System ya Nyerere kwa vile wote hawa na marafiki zao ni wale wale vijana wa Mheshimiwa Nyerere ambaye alikuwa

hakuzoea kumfukuza mtu kazi bali kuwalinda kwa kuwahamishahamisha na kuwakemea tu kisha mambo yameisha. Tukistaajabu mikataba ya aibu ya Dhahabu ya wakati wa Mzee Mkapa, tunaweza tukahuzunika na kushika vichwa kwa mikataba ya Almasi. Tunalalamika kwamba Dhahabu zitaisha tutaachiwa mashimo, mbona hatulalamiki kwamba Alimasi imeisha tumeachiwa mashimo? Au na mikataba ya Alimasi pia aliisaini Mkapa? Pia lazima tujiulize ujasiri wa Mkapa kuwatangazia Watanzania kwamba amesaini mikataba ya 3% na wala siyo 33% na wala siyo 49% na wala siyo 60% au 70% ameutoa wapi? Lazima kuna vigezo ambavyo amevitumia kuwatangazia Watanzania kwamba ni 3% tu. Alimasi imeisha na hakuna tulichokipata toka kwenye Alimasi, bali tumebakia na uendelezo ule ule wa kumsifia “Baba wa Taifa!” (Makala hii imeandikwa na Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics) FormerLecturer of Mzumbe, O p e n & K I U – D a r, Universities. Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political Analyst Email: norjella@yahoo. com Mobile: +255 782 000 131)

16

AN-NUUR
16
Akifafanua namna ya uendeshaji utakavyokuwa katika mahakama hiyo, Chengulla alisema kuwa, kazi kubwa ya mahakama hiyo itakuwa ni kutoa hukumu. “Mahakama hii itafanya kazi ya kutoa hukumu tu kwani uchunguzi, ushahidi na mahojiano vilikwishafanywa kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya uchunguzi wa Maadili ya Viongozi wa Umma na ukapitishwa na Bunge ambalo linawakilisha mamlaka kamili ya wananchi, hivyo hakutahitajika kuendesha kesi”, alisema. Sanjari na hilo, SUMKI ikapendekeza Katiba ijayo itamke wazi kwamba, kiongozi yeyote wa umma atayetuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi, rushwa na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo, anyang’anywe haraka hati yake ya kusafiria pamoja na kusimamishwa kazi katika nafasi atakayokuwa anaishikilia. Kuhusu njia za utendaji serikalini, Shirika hilo limesema kuwa, Rais ama kiongozi yeyote asiwe

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

RABBIUL AWWAL 1434, IJUMAA JANUARI 18 - 24, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

AN-NUUR

Kuwe na Mahakama za Kidini
Na Bakari Mwakangwale SHIRIKA lisilo la kiserikali la Uboreshaji na Mahusiano Mema ya Kijamii Tanzania (SUMKI) limesema upo umuhimu wa Katiba ijayo ikaruhusu kutumika kwa sheria za kidini kwa wale watakao kuwa tayari kuhukumiwa kwa mujibu wa mafundisho ya dini zao. Hayo yamo katika maoni yao waliyoyawasilishwa juma lililopita mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiomba uhuru wa wanadini na Ibada upanuliwe zaidi. Kwa mujibu wa maoni hayo yaliyowasilishwa na viongozi wandamizi wa SUMKI chini ya Mkurugenzi wake Mussa Chengulla, watu wote watakaokuwa tayari kuhukumiwa kwa mujibu wa dini zao watalazimika kusaini hati maalum ya makubaliano. “Hukumu hii ya kidini itamuhusu mwanadini yeyote atakayefikisha umri wa kujua zuri na baya (baleghe). “Aidha ikitokea mwanadini kufanya kosa litakalolazimika kuhukumiwa kiserikali na kidini, kipengele hiki kinaelekeza kuwa sheria (hukumu) ya dini itatumika baada ya hukumu ya kiserikali kupita”, ilisema sehemu ya 10 ya maoni hayo. Mbali na Mahakama ya Kadhi, SUMKI imependekeza Katiba mpya ieleze wazi uwepo wa Mahakama Maalum ya Viongozi wa Umma. “Mahakama Maalum ya Viongozi wa Umma ni Mahakama mahsusi juu ya viongozi wa umma watakaohusika na makosa ya uvunjifu wa maadili ya uongozi wa umma, matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu pamoja na kuisababishia serikali hasara. “Maamuzi ya Mahakama hii yawe ya mwisho na yasiingiliwe na muhimili mwingine wowote wa dola ama chombo chochote kile”, limesema Shirika hilo.

JAJI Joseph Sinde Warioba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. na mamlaka ya kupanga mishahara, posho ama marupurupu ya viongozi wa umma, badala yake shughuli hiyo ifanywe na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uchunguzi wa Maadili ya Viongozi wa Umma. “Kiongozi yeyote wa Umma asipewe nafasi ya kuanzisha sekta yoyote ndani ya Serikali mpaka wazo hilo litakapofikishwa Bungeni ili lijadiliwe na wabunge kwa niaba ya wananchi. Wabunge ndio watakaokuwa na haki ya kukubali jambo hilo au kinyume chake bila kuingiliwa na muhimili wowote wa dola”, limesema Shirika hilo na kuongeza; “Kusiwepo kiongozi anayeshikilia nafasi mbili za uongozi ama zaidi ndani ya serikali”

Maalim Seif ahimiza elimu kwa wasichana
Mkoa wa Kaskazini Unguja MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amekemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwanyima fursa za kielimu watoto wa kike, hatua ambayo inadumaza maendeleo yao na taifa kwa ujumla. Amesema moja kati ya malengo makuu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ni kuondoa ubaguzi wa aina zote, sambamba na kuwapatia elimu watoto wote bila ya kuwepo ubaguzi wa kipato au jinsia. Maalim Seif ameeleza hayo hivi karibuni baada ya kufungua jengo la madarasa manne la skuli ya Mbuyutende jimbo la Matemwe, ikiwa ni katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema elimu ndio msingi wa maendeleo kwa watoto, hivyo wazazi wanapaswa kuwapatia elimu watoto wao, ili kuhakikisha kuwa wanawajengea mazingira bora ya maisha yao ya baadae. Sambamba na hilo Maalim Seif ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuangalia uwezekano wa kuifanyia marekebisho mitaala yake ya elimu, ili iendane na wakati na kukidhi mahitaji ya soko la ajira. “ Wa p o v i j a n a w e n g i wamemaliza hadi vyuo vikuu lakini hawana ajira, kwa hivyo mitaala yetu hii lazima iwaandae vijana waweze kujiari wanapohitimu masomo yao”, alifahamisha Maalim Seif. Kuhusu upungufu wa walimu katika skuli za vijijini Maalim Seif amesema tatizo hilo linachangiwa na ukosefu wa nyumba za walimu, na kutoa wito kwa Wizara ya Elimu kushirikiana na serikali ya Mkoa huo kutafuta nyumba za walimu ili kuondosha tatizo hilo. “Ukosefu wa nyumba za walimu ndio tatizo la msingi la upungufu wa walimu katika skuli za vijijini, kwa hivyo Wizara ya Elimu shirikianeni kwa karibu na Mkoa pamoja na Halmashauri kutafuta nyumba ijapo za kukodi, ili walimu wanaotoka mbali wapate mahali pazuri pa kuishi”, aliagiza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar. Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna ameahidi kukamilisha upatikanaji

wa madawati katika skuli hiyo, ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira bora. Katika risala ya wananchi wa kijiji cha Mbuyutende iliyosomwa na nd. Makame Juma, wananchi hao wamesema licha ya mafanikio waliyoyapata katika kijiji hicho, bado wanakabiliwa na matatizo kadhaa yakiwemo ukosefu wa maji safi na salama, umeme na barabara. Katika hafla hiyo jumla ya shilingi milioni 11 na laki nne zimechangwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo jipya la skuli hiyo ambapo Maalim Seif ameahidi kuchangia shilingi milioni tano. (Habari kwa hisani ya Hassan Hamad (OMKR)

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.