www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

(2) HIJJI, UFE MUISLAMU!(2) HIJJI, UFE

Padri Mushi katolewa kafara kama Askofu Oscar Romero?
ISSN 0856 - 3861 Na. 1059 RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22 - 28, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Ewe MUISLAMU, Unajua kuwa anayekufa bila kuhiji hali ya kuwa aliwahi kupata uwezo anakufa Yahudi au Nasara, na Uislamu hautomtambua? Hijja ni haki ya Mola wako iliyopo juu yako! Basi mpe Mola wako haki yake kwanza kabla kuridhisha nafsi yako kwa kufanya mengine. Gharama zote ni Dola 4,300 tu. Karibu Ahlu Sunna wal Jamaa. Tafadhaliwasiliana nasi ifuatavyo: Tanzania Bara: 0717224437; 0777462022;Unguja: 0777458075;Pemba: 0776357117.7.

Haraka ya kuwaita ‘FBI’ na ‘CIA’ ya nini? Hakuna tulilojifunza kwa Mauricio Funes? Waislam, Wakristo wawe makini wasipotoshwe

Ni kweli Waziri Mkuu: La Waislamu gumu ila… Maalim Seif akerwa na kauli ya Nchimbi
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Dkt. Emmanuel Nchimbi (katikati) akiwa na Kamanda wa Polisi Zanzibar, Mussa Juma. AMESEMA kweli Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda. Waislamu walijisahau wakadhani kuwa wanaweza kutoa malalamiko, madai na mashariti, serikali ikasikiliza na kutekeleza. Hilo liliwezekana kwa Wakristo ambao tunaambiwa kuwa walimpa mashariti

Hayati PADRI Evarest Mushi

HAYATI Askofu Oscar Romero?

Ya Wakristo yametekelezwa papo hapo Waliochafua karatasi za mitihani si wajinga Ni namna ya kupinga ya “Timu ya Wanga”
m a g u m u Wa z i r i w a Mambo ya Ndani Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi na akayatekeleza mara moja ila akaomba muda wa kutekeleza jambo moja tu katika mashariti matano aliyopewa. Pengine kwa kuona kuwa Wakristo wao wametoa mashariti na kukubaliwa papo hapo na serikali, Inaendelea Uk. 2

Asema Zanzibar hakuna ugaidi Wananchi wasijekamatwa ovyo JUMAZA yaonya vyombo vya habari

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

Tahariri/Tangazo
AN-NUUR
Ukiacha yale malalamiko ya Wakuu wa Shule za Kiislamu mwaka jana, zipo tuhuma nyingi ambazo zinawafanya wanafunzi kutokuwa na imani na kuamini kuwa F, E na D wanazopewa zinatokana kweli na makisi walizopewa na wasahihishaji mitihani au wametunukiwa na ‘Timu ya Wanga’. Katika hali kama hii, zaweza kuwepo namna nyingi za kuonyesha kutoridhika (ku-protest) na utaratibu unaotumika kutahini. Lakini jingine ni hali iliyopo mashuleni. Zipo shule ambapo zaidi ya nusu ya wanafunzi huhama au kuacha shule kwa sababu hakuna walimu, madawati, hakuna vyoo au matatizo mengine. Unafikiri hao wachache watakaobaki hadi kufanya mtihani wa kidato cha nne au cha sita, wataandika nini kama si kuonyesha kuwa hawaridhiki na mfumo uliopo ambao umewatupa na haujali kuwa nao wanastahiki kupata eilimu bora? Kama litakuwepo kosa, basi itakuwa kwa hao walioandika matusi, lakini vinginevyo kama tunataka kutatua tatizo, basi tuwaone wanafunzi walioandika mashairi na kuwalaumu wabunge badala ya kuandika majibu, ni mashujaa. Wanaonyesha kutokuridhika kwao na hali ilivyo nchini. Shuleni hakuna walimu wala vitabu na wachache waliopo hawafundishi. Hii ndio hali halisi katika nchi hii na wala isidhaniwe kuwa ni tatizo la Wizara ya Elimu pekee. Wapi kuna nafuu? Bomba linapita mtaani, lakini hakuna maji. Umeme kila leo ni wa kukatika ovyo. Kilimo imekuwa wimbo, hakuna maendeleo yoyote. Acha mpira, hata tukiambiwa kuingia mashindano ya kucheza ngoma, hakuna tutakachoambulia. Angalia vichekesho (komedi) vya nchi jirani ulinganishe na wa hapa kwetu. Almuhimu tunasema

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013 kuwa mambo yanakwenda ovyo katika nchi hii. Nchi ndogo kama Rwanda ambayo imetoka katika machafuko hivi karibuni tu, inatuwashia taa ya kutupita kwa kasi katika kila kitu. Sisi tumo tu tunapiga porojo. Kwa mtaalamu yoyote wa elimu na utahini, hawezi kukubaliana na maelezo ya Ndalichako kuwa kuchora Mess na kuandika mashairi ndio kuliko sababisha wanafunzi kufeli zaidi ya asilimia 60. Atuambie katika hao waliopata sifuri (F), wangapi ni katika hao waliomchora Mess na kuandika ‘single’ za muziki? Atuambie, katika kutoa matokeo hayo, CA zimepewa uzito gani? Na je, Kamati yake ya Kutunuku mwaka huu kwa kila somo, A, B, C na D, zimeanzia na alama ngapi na kwa nini? Lakini Swali muhimu ambalo linahitaji kujibiwa kwa uhakika ni hili: Je, matokeo haya yaliyotangazwa na Waziri Kawambwa, ni matokeo halisi yanayowakilisha ufaulu (alama) zilizotolewa na wasahihishaji? Kujua ukweli huu ni jambo jepesi sana. Karatasi za mitihani zipo, hazijachomwa moto. Zipitiwe kuhakikisha kuwa makisi zilizotolewa ndio zilizotangazwa na Baraza la Mitihani. Hizi hoja za walimu hawasomeshi, hakuna walimu, hakuna vifaa, watoto hawasomi, shule za Kata hivi na vile, ni hoja za kupotosha. Huko kunaweza kuwa na matatizo kweli, lakini sio kuzaa matokeo haya. Tatizo lipo Baraza la Mitihani na Kamati yake ya Kutunuku. Kama serikali itaona kuwa hakuna haja ya kujua ukweli juu ya matokeo haya, kwa maana ya kujua iwapo F walizopata watahiniwa zaidi ya asilimia 60 ni zao au ni zakuchakachuliwa, itabidi tuwe na wasiwasi kuwa serikali yenyewe inahusika katika mchezo huu. Ni kuku anayekunywa mayai yake au paka anayekula watoto wake. Sasa swali litabaki kwa lengo gani? Kwa masilahi gani? Ili iwe nini? Kwa sasa tusingependa kuingia katika uvumi na nadharia zinazosambaa za vurugu za mikopo kwa wanafunzi na uchaguzi mkuu 2015.

AN-NUUR

MAONI YETU

Ni kweli Waziri Mkuu: La Waislamu gumu ila…
Inatoka Uk. 1 Waislamu nao waliomba wenzao waliokamatwa waachiwe waje katika kikao na Waziri Mkuu, hata hivyo wakaambiwa kuwa mashariti yao ni magumu. Linalowashangaza Waislamu ni kuwa vurugu zimetokea baina ya pande mbili na kuleta maafa, lakini wanaokamatwa na kuzuiliwa ni watu wa upande mmoja tu. Aidha kinachoshangaza zaidi ni kuwa kabla ya tukio hilo, walionekana wachungaji wakihamasisha waumini wao kuchinja na kupeleka nyama sokoni, kitendo ambacho ndicho kilichozua balaa hadi kuleta maafa ya kifo, majeuhi na kuharibiwa mali, lakini walioshiriki kufanya uchochezi huo hakuna aliyekamatwa. Wote wapo huru. swali, waliandika nyimbo za muziki na wengine kutumia karatasi za majibu kuandika barua kulalamikia wapenzi wao. Akasema, wengine badala ya kujibu mtihani wanalaumu wabunge. “Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge…mtu anaandika nawashangaa wabunge wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala ya kujadili kero za wananchi waliowachagua wanapokea timu zilizoshinda makombe…” Anayeeleza habari hizi akishangaa na kuwalaumu wanafunzi walioandika maneno haya ni kiongozi mtendaji mkuu wa taasisi inayolalamikiwa kuwa “Baraza lake limekuwa kama Timu ya Wanga”. Utaratibu wa CA haujulikani wala hicho kinachoitwa Kamati ya Kutunuku madaraja haijulikani inatumia vigezo gani kwani imekuwa siri yao isiyofuata kanuni za kitaalamu kama taarifa za watafiti na wachunguzi zilivo washangaza na kuwashtua wengi. Tunasema ni kama ‘Timu ya Wanga’ kwa sababu hakuna sababu yoyote ya kuingia akilini inayoweza kutolewa, ni kwa nini inachukua muda mrefu sana majibu kutolewa baada ya wasahihishaji kufanya kazi yao na kurekodi alama za mitihani yote kwa kila mtahiniwa, hasa ikizingatiwa kuwa hizi ni zama za tekinolojia ya komputa na IT!

Kufeli wanafunzi Ya p o m e n g i yamesemwa juu ya kufeli sana wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu. Na zaidi juu ya baadhi ya wanafunzi kuandika vitu visivyo husika kama vile kuchora picha za wanamichezo maarufu na hata kuandika matusi. Sisi tuseme kuwa zipo njia nyingi za watu kuonyesha hisia zao kuwa hawaridhiki au wanapinga jambo fulani. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dr. Joyce Ndalichako anasema kuwa wapo baadhi ya wanafunzi badala kuandika majibu ya

P.O. Box 55105, Tel: 2450069, 0712 974428 Fax: 2450822 D’ Salaam E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL

Maandalizi kwa wanaorudia Kidato cha IV, 2013
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza kozi maalum ya maandalizi kwa wanaorudia kufanya mtihani wa Kidato cha IV, 2013. Programu hii itaanza tarehe 28/02/2013 hadi tarehe 28/08/2013 Jumatatu hadi Jumamosi saa 2:00 kamili Asubuhi hadi saa 9:10 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya Dini ya Kiislamu, English Language. Lugha ya Kiarabu. Basic Mathematics, History, Geography, Civics, Physics, Chemistry, Biology, Book Keeping, Commerce. Kiswahili Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni kwa Tshs 10,000/=

Mlete mwanao apate Elimu bora itakayomwezesha kujiunga na Kidato cha Tano.
Kwa mawasiliano zaidi piga namba: 0714 888557/0659 204013 Wabillah Tawfiiq MKUU WA SHULE

Waislam wataka haki Waziri Mkuu akwepa
Abariki kuachiwa Wakristo waliofanya vurugu Waislamu waliokamatwa hawajulikani walipo
pamoja tukio hili, kinyume na hivyo hatutoshiriki katika mazungumzo yoyote na hatuko tayari kuzungumza na wewe.” Kilisema chanzo chetu cha habari kikimnukuu msemaji wa Waislamu katika kikako hicho. Chanzo hicho cha habari kimesema kuwa katika majumsho ya majibu yake kwa Waislamu, Waziri Pinda, alisema watu hao (Waislamu) wana kesi ya mauaji lakini Wachungaji wao wana kesi ya kuchinja, kwa hiyo alidai kwamba kesi ya kuchinja ina dhamana na kesi ya mauaji ina taratibu zake. Baada ya majibu hayo ya Waziri Mkuu, An nuur limeelezwa kuwa msemaji wa Waislamu katika kikao hicho, alionyesha ishara ya kuomba kutoa hoja (taarifa), zaidi ya mara nne lakini Waziri Mkuu, alipuuza na ndipo alipotoa Takbira, na Waislamu kuitikia kisha walitoka nje wakimuacha (Pinda) na Maaskofu. Awali katika hoja za msingi, mbele ya Waziri Mkuu Pinda, aliyekuwa ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kufuatia hoja na madai ya Maaskofu kwa Serikali, Waislamu walimtaka Waziri huyo, kusema kama Serikali itakuwa tayari kuhudumia f a m i l i a z a Wa i s l a m u waliouwawa na Serikali kwa mashinikizo ya Maaskofu. Hoja hiyo ya Waislamu ilikuja kufuatia Maaskofu katika kikao hicho kuitaka Serikali kumuhudumia mjane wa Mchungaji aliyeuwawa katika vurugu za Buseresere. “Kama Serikari itakuwa tayari kumuhudumia huyo mjane wa Mchungaji, Waislamu pia tunakutaka ututhibitishie kama Serikali itakuwa tayari kuhudumia f a m i l i a z a Wa i s l a m u waliouwawa katika nchi hii kama wanavyodai hivi sasa Wakristo kwa huyo Mchungaji.” Kilisema chanzo chetu cha habari
Na Bakari Mwakangwale

3

Habari

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

WA Z I R I M k u u , Mheshimiwa Mizengo Pinda, amejikuta akibaki ukumbini yeye pamoja na Maaskofu, katika kikao cha kutafuta muafaka wa vurugu za Wakristo kuchinja, Mkoani Geita k u f u a t i a Wa i s l a m u kutoka nje ya ukumbi. Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimedai kuwa, Waislamu waliamua kuachana na kikao hicho, baada ya Waziri Mkuu kuwajibu kuwa hatoweza k u w a t o w a Wa i s l a m u wanaoshikiliwa na Polisi, kwa kuwa wana kesi ya mauaji na Maaskofu walioachiwa wana kesi ya kuchinja. Majibu hayo ya Waziri Mkuu, yanafuatia mashariti sita ya Waislamu waliyoyatoa ili kuweza kushiriki katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Februari 17, 2013, ili kuweza kupata suluhu kati ya Waislamu na Wakristo katika sakata la kuchinja. Imedaiwa kuwa kumekuwa na manug’uniko kutoka kwa Waislamu Mkoani Geita, wakidai kutotendewa haki tokea kuibuka kwa vurugu hizo, mapema hivi karibuni. Zaidi wamedai ni pale ambapo watuhumiwa Maaskofu na Wakristo, waliokamatwa katika vurugu hizo, kuachiwa kwa inayodaiwa amri ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emannuel Nchimbi, baada ya kutekeleza msimamo wa Maaskofu kuwa hawapo tayari kuzungumza naye hadi pale wenzao waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi waachiwe, jambo ambalo lilitekelezwa. “Sasa sisi kama Waislamu tunakutaka wewe kama Waziri Mkuu, kwamba wale wenzetu waliko ndani nao waachiwe na waletwe katika kikao hiki kama walivyotolewa wale Maaskofu ili tujadili kwa

kikimnukuu msemaji wa Waislamu katika kikao hicho. Msemaji huyo wa Waislamu aliyetajwa kwa majina ya Bw. Hamza Omari, alifafanua kwamba Waislamu katika nchi hii wameshauwawa wengi, kwa kutekeleza maagizo ya Maaskofu, yakiwemo m a u a j i y a Wa i s l a m u Mwembechai, Kijana wa Kiislamu Kakola, Shinyanga na hata Zanzibar. Bw. Omari, alisema katika mauaji yote hayo haijapata kutokea kiongozi yoyote wa Serikali kuhudhuria mazishi ya Waislamu hao, wala kiongozi wa Serikali kuomba msamaha wa aina yoyote au kutoa rambirambi kama inavyofanya kwa Wakristo. Waislamu hao wakamtaka Wa z i r i M k u u P i n d a , akubali Serikali kutoa ahadi yakulipa fidia ya uharibifu uliotokea katika Msikiti wa Buseresere, kama ilivyoahidi kulipa fidia Makanisa yaliyoungua moto katika vurugu za kidini zilizotokea Mbagala Jijini Dar es Salaam. B w. O m a r i a l i s e m a kwamba, Serikali imekuwa inaegemea upande mmoja wa Wakristo, kila inapotokea mgongano baina ya dini hizo mbili, na kuwapuuza Waislamu jambo ambalo ni hatari. Alitolea mfano matukio ya Mbagala na Zanzibar kwamba baada ya kuungua moto, walionekana viongozi wa Serikali wakubwa wakiomba radhi na kuahidi kuwashughulikia wale waliofanya uharibifu huo na ahadi ya kulipa fidia, jambo ambalo ni kinyume kabisa inapotokea uharibifu Msikitini. “Kwa maana hiyo kule Buseresere Msikitini, katika vurugu hizi, Wakristo wamevunja vibanda vya Msikiti na mali zingine kuteketezwa kwa moto, tunakutaka wewe Waziri Mkuu, uweze kuthibitishia, kama Serikali iliweza kuahidi na kulipa fidia Makanisa, je Serikali ipo

WAZIRI Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda tayari kuahidi na kulipa fidia mali za Msikiti wa Buseresere”?, Chanzo chetu kilimnukuu Bw. Omari, akitoa hoja za Waislamu. Wa i s l a m u hao w a l i m w a m b i a Wa z i r i Mkuu Pinda, wakimtaja ofisa mmoja wa Polisi Buseresere, na askari mmoja akiwa katika sare za kazini na bunduki mkononi, kwamba walioneka katika tukio la uchinjaji Kanisani, kabla ya vurugu kuibuka. Lakini pia alidai kuna aliyempiga Muislamu risasi ya mguuni katika vurugu hizo pamoja na kiongozi mmoja wa siasa aliyekuwa kinara wa uhamasishaji Wakristo kuchinja, mpaka sasa alidai haijafahamika watu hao wote, Serikali imewachukulia hatua gani. Wa i s l a m u hao walionyesha kushangazwa na hatua zilizochukuliwa za kuwahamisha watuhumiwa wa Kiislamu kutoka Mkoa wa Geita, lilipotokea tukio na kudaiwa kupelekwa Biharamulo, ambako hakuhusiki na vurugu hizo. Wa i s l a m u pia walilalamika kitendo cha Wachungaji waliosababisha kadhia hiyo kuachiwa, kwa tamko la Waziri wa Mambo ya Ndani, (Nchimbi), baada ya Wakristo kutoa sharti la kwamba hawawezi kuzungumza naye mpaka Wachungaji walio ndani waachiwe na washiriki katika kikao hicho na Waziri alitekeleza hilo. Aw a l i m s e m a j i w a Maaskofu katika kikao hicho, alimtaka Waziri Mkuu Pinda, kutoa msimamo wa Serikali kama wachije au wala, sambamba na Serikali kumlea mjane wa Mchungaji aliyekufa. “Tunachotaka kutoka kwako wewe muheshimiwa Waziri Mkuu ni kauli moja tu, tuchinje au tusichinje, lakini pia Serikali imlee mjanae wa Mchungaji aliyekufa.” Kilinukuu chanzo chetu cha habari, kutoka kwa Askofu, huyo. Askofu Mussa Masanja, alieleza kuwa kwa mujibu wa vitabu vitakatifu yaani Qur an na Biblia, ni kwamba Qur’ an inaruhusu kula nyama iliyochinjwa na mtu wa kitabu, huku akinukuu maelezo ya Sheikh Alhad Mussa, aliyeongea mapema hivi karibuni, kupitia chombo kimoja cha Televisheni. Lakini, Askofu huyo
Inaendelea Uk. 4

4

Maoni

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Maalim Seif akerwa na kauli ya Nchimbi
Na Alghaithiyyah, Zanzibar kuwa kisiwa cha amani. Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF ametoa kauli hiyo kisiwani Pemba wakati akifungua semina ya madiwani wa CUF inayofanyika ukumbi wa kiwanda cha mafuta ya makonyo Wawi. Amesema kwa niaba yake binafsi, chama chake na Serikali analaani vikali kitendo hicho cha kinyama ambacho kimeitia doa kubwa Zanzibar. Amesema kitendo hicho ambacho hakikubaliki ni cha kusikitisha kwa vile Wazanzibari wamekuwa wakiishi kwa kuvuliana kwa kipindi kirefu bila ya kutoa vitendo hivyo. Amesema ni wajibu wa Wazanzibari kuendeleza sifa njema ya Zanzibar kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kuishi kwa kuvuliana na kuwapa matumaini wageni wanaokuja kuitembelea Zanzibar kwa shughuli mbali mbali ikiwemo ya utalii. Ameviomba vyombo vya dola kufanya kazi ya ziada kuwatafuta waliohusika na tukio hilo na kuchukuliwa hatua za kisheria. Hata hivyo amesema wakati uchunguzi huo ukiendelea kufanyika, ni vyema kwa vyombo vya dola kufanya kazi kwa umakini mkubwa ili kuepuka kuwahusisha watu wasiohusika na tukio hilo. Wa k a t i h u o h u o , Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) imekemea vikali kauli za baadhi ya vyombo vya habari vinavyonasibisha Waislamu na tukio hili na kuvitahadharisha vyombo hivyo kutoanza kutoa taarifa ambazo kwa makusudi zinaweza kupandikiza chuki na uhasama katika jamii na hatimae kuotesha mizizi ya fitna na kupelekea Taifa kuingia kwenye machafuko. Aidha JUMAZA imeziomba Serikali zote mbili kuwa makini katika kipindi hiki kwa kujizuia kutoa maneno yanayoashiria kuhusisha tukio hili na upande fulani wakati bado uchunguzi unaendelea. Taarifa ya JUMAZA kwa waandishi wa habari iliyosainiwa na Katibu wake Sheikh Muhiddin Zuberi Muhiddin, imeliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa uadilifu usioambatana na shinikizo la mtu au kikundi chochote ili hatimae ukweli halisi ujulikane na bila ya kuwadhuru wasiohusika.

MAALIM Seif ameelezea kusikitishwa kwake na kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi ya kupandikiza ugaidi Zanzibar. Maalim Seif amesema hayo kufuatia kauli ya Waziri Nchimbi kwamba mauwaji ya Padri Evarist Mushi ni ugaidi. Licha ya kukiri kuwa mauwaji hayo ni uhalifu, lakini haijafikia hatua ya kuitangaza Zanzibar kuwa nchi ya kigaidi, na kwamba kufanya hivyo ni kuijengea sifa mbaya Zanzibar. “Kauli kama hizi ukweli hazisaidii zaidi ya kutuvuruga, ni kweli ni kitendo kibaya na kikubwa, lakini ugaidi ni mkubwa zaidi na sisi hatujafikia na wala hatutofikia hatua hiyo”, alionya Maalim Seif. Amesema ni vyema kwa viongozi wanaotokea upande wa pili wa Muungano kufanya mashauriano na viongozi wa Zanzibar kabla ya kutoa kauli ambazo zinaijengea sifa mbaya na kuitia doa Zanzibar. Awali Maalim Seif Sharif Hamad amelaani vikali kitendo kwa kupigwa risasi na kuuliwa kwa Padri Evarist

MAKAMU wa kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad Mushi wa kanisa katoliki Zanzibar na kusema kuwa kitendo hicho kimevuruga sifa njema ya Zanzibar ya

Inatoka Uk. 3 alidaiwa kusema, Biblia hairuhusu Wakristo kula nyama iliyochinjwa kwa Mungu mwingine na kwamba kwa Muislamu kuchinja ni ibada iliyokamili, akahoji iweje wao (Wakristo) walazimishwe kuabudu kupitia imani ya Kiislamu? Alisema, kwamba wao Wakristo hawapo tayari kuendelea kula nyama zinazochinjwa na Waislamu kwa sababu ya mazoea tu, kwani alidai mazoea huwa yanabadilika, hivyo alidai mazoea huwa inafika wakati yanabadilika. Askofu, huyo imedaiwa kuwa alimtaka Waziri Mkuu Pinda, kupiga marufuku

Waislam wataka haki Waziri Mkuu akwepa
CD, DVD, machapisho ya Waislamu yenye uchochezi sambamba na vyombo vya habari vyenye mlengo huo. “Ni vyema sasa Serikali ikasikiliza matamko yao, mfano CD, DVD na machapisho ya Kiislamu yenye uchochezi pamoja na vyombo vya habari vyenye mlengo huo vinatakiwa vipigwe marufuku mara moja.” Alinukuliwa akisema Askofu huyo. Taarifa zaidi zimesema, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amedai kuwa bado ana nia ya kukutana tena na wadau hao wa dini hizo mbili, Mkoani Geita, baada ya kuandaa mazingira mazuri ya kufikia muafaka. Kwa upande wa Waislamu wamedai kuwa wao msimamo wao utabaki palepale kwanza wapate majibu juu ya hoja zao walizozitoa kwa Waziri Mkuu na wenzao kuachiwa kama walivyoachiwa Maaskofu, kinyume na hapo hawapo tayari kukutana na kiongozi yoyote wa Serikali. Wa m e d i a k u w a n i dhahiri haki inapindishwa na kudhihiri ni jinsi gani Serikali inavyowakandamiza Waislamu na kuwapendelea Wa k r i s t o h a t a p a l e yanapokuja masuala ya kisheria. Waislamu hao wamedai kuwa, kama vurugu zimetokea pande mbili na mauaji yametokea, basi wale wote wanakamatwa wanakuwa ni watuhumiwa kama ni wa vurugu au mauaji, mpaka pale Mahakama itakapo amua. “Lakini katika vurugu zile, Waziri Pinda na Nchimbi, wameshaainisha makosa, kuwa hawa Waislamu ndio wanahusika na mauaji na Wakristo hawahusiki, kabla hata ya kwenda Mahakamani sasa utaona jinsi gani viongozi wa nchi hii wanavyowatazama vibaya Waislamu.” Alisema Mama Sauda, kwa njia ya simu kutoka Geita. Wa t u h u m i w a h a o Wa i s l a m u , i n a d a i w a waliondoshwa Mkoani Geita, na kupelekwa, Biharamulo hata hivyo viongozi wa Waislamu wanajipanga kwenda, huko kujua zaidi hatma ya

Waislamu hao. “Baada ya kutolewa Buseresere, walipelekwa Chato kisha walihamishiwa Biharamulo, wakati huko ni mkoa mwingine sasa hatuelewi inafanywa hivyo kwa mujibu wa sheria gani, na hadi sasa hatuelewi kama wapo salama au la kwani miongoni mwao ni wale majeruhi walikatwa mapanga.” Alisema Ust. Saleh Haruna. Ta a r i f a z a a w a l i zilifahamisha kuwa watuhumiwa watatu wameshafikishwa Mahakamini na kusomewa kosa la mauwaji na wengine makosa ya jinai ambao wa tuhuma za mauwaji wamepelekwa mahabusu Biharamulo na wengine Chato.

5
PARIS AFISA anayeshughulikia masuala ya dini katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, amesema kuwa idadi ya watu wanaoingia katika dini ya Uislamu imeongezeka mara dufu nchini humo katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Bernard Godard, amebainisha suala hilo katika ripoti iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa na kuongeza kuwa, suala la watu kuingia katika dini ya Uislamu nchini Ufaransa, limekuwa jambo muhimu na kwamba ongezeko la idadi ya watu wanaoingia katika dini hiyo nchini humo hususan mwaka 2000 ni jambo linalohitaji kupewa mazingatio. Imeelezwa kuwa mwenendo mzuri wa Waislamu wa Ufaransa katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiutamaduni, ndio unaowavutia Wafaransa wengi katika dini ya Uislamu licha ya propaganda chafu

Habari za Kimataifa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Wafaransa wanaosilimu waongezeka mara dufu

Ufisadi tishio kwa maendeleo Afrika
RAIS wa Ufaransa, Francois Hollande
zinazofanywa na vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na Waislamu. Wafaransa milioni sita ni waumini wa dini ya Kiislamu na Wafaransa

kati ya laki moja hadi mbili wameingia katika dini hiyo. Ta k w i m u h i z o zinaonesha kuwa idadi ya Wafaransa wanaoingia katika dini ya Uislamu tangu mwaka 2000, imeongezeka mara dufu ikilinganishwa na ile ya mwaka 1986 ya watu laki tano pekee kwa mwaka.

Semina ya Maimamu Mahakama ya Misri na Makhatibu yakataa sheria ya uchaguzi
CAIRO MAHAKAMa ya Katiba ya Misri imekataa vipengele vitano katika sheria ya uchaguzi na kuirejesha katika Baraza la Ushauri la nchi hiyo, jambo ambalo huenda likachelewesha uchaguzi wa Bunge nchini humo. Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo imesema, korti imerejesha sheria hiyo iliyotungwa kuhusiana na uchaguzi wa Bunge kwa Baraza la Ushauri, baada ya kuvichunguza vipengele vitano vya sheria hiyo na kugundua kuwa ni kinyume na katiba.

Semina ya Maimamu na Makhatibu chini ya Masheikh: Amrani Kilemile Abdallah Bawaziri Ahmed Twalib Itakayofanyika: Uwanja wa Sababa (Ukumnbi wa Wizara ya Fedha) Muda: Saa 2L30 asubuhi - 6:30 mchana. Siku: Jumamosi na Jumapili Tarehe: 23/2/2012 - 24/2/2013 Wote Mnakaribishwa

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu, na Rais Muhammad Mursi, alitakiwa kuipitisha sheria hiyo Februari 25 na kutangaza tarehe ya uchaguzi. Mahakama ya Katiba ya Misri inaundwa na majaji wa wakati wa utawala uliopinduliwa wa Hosni Mubarak na baada ya mapinduzi ya wananchi wa Misri, Mahakama imekuwa ikiingilia mara kwa mara maamuzi ya serikali ya mpito na hata kulivunja Bunge.

Benki ya Dunia imetangaza kuwa, ubadhirifu wa mali na ufisadi ni kikwazo kikubwa cha ustawi wa nchi zinazoendelea hasa za barani Afrika. Ripoti ya Benki ya Dunia imebainisha kuwa, nchi zinazoendelea, hususan za bara la Afrika hupata hasara ya dola bilioni 4 kila mwaka kutokana na ubadhirifu na ufisadi wa kiidara. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonesha kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya kubakia nyuma kimaendeleo kwa nchi nyingi na suala la kuenea ufisadi katika nchi hizo. Aidha tathmini ya Benki hiyo inaonesha kwamba, mipango mingi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea hasa barani Afrika, imekuwa ikikwama kutokana na ulaji rushwa, ufisadi na ubabaishaji uliokithiri na kwamba, masuala hayo ndio chanzo halisi cha kukwama juhudi za maendeleo katika nchi nyingi hasa za barani Afrika. Ukosefu wa utawala bora umeelezwa kuwa, ni kikwazo kingine cha maendeleo na ustawi katika nchi zinazoendelea.

6
Na Shaaban Rajab
MIUJIZA ya Sheikh Said John, ilianza kujitokeza tangu wakati anazaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha mwaka 1989. Mzee John Edward, alimwambia mwanaye Joseph, “Ulipozaliwa tu, hukutoa sauti wala kuonyesha kutapatapa (movement), ili kuthihirisha dalili ya kuwepo uhai, vipimo vya madaktari havikugundua kuwepo uhai, wakasema, haikuwa riziki, mtoto amepoteza” . Mzee Hassan (John) Edward, alimwambia mwanaye Said (Joseph) John. Shariff Said John, ambaye anapenda zaidi kuitwa Sherikh Said John, akidai kuwa cheo cha Shariff ni daraja kubwa sana kumzidi, alizaliwa katika familia ya Kikristo, wazazi wake wakiwa ni waumini wa dhehebu la Pentekoste Assemblies of God. Sheikh Said anasema kuwa, mara baada ya madaktari kuthibitisha kwa vipimo kuwa amefariki, baba yake, Mzee John akashauriwa arudi nyumbani kufanya maandalizi ya kuzika kichanga. Baadae alirejea Hospitalini na wazee wawili kuchukua mwili wa mwanaye mchanga. Walimchukua kichanga na kuanza hatua za kurejea nyumbani. Lakini walipokuwa njiani, mtoto alipiga chafya na kuanza kulia, hapo hapo iliwalazimu kurudi tena hospitalini ili upata maelekezo zaidi kwa madaktari. Madaktari kwa mara nyingine wakachukua vipimo na kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na kuthibitishwa kuwa kafa, alikuwa hai. Baada ya matibabu na kinga kwa mtoto, Mzee John na wenzake walirejea nyumbani. Baada ya siku chache kupita, mtoto alibatizwa na kupewa jina la Joseph. Hivyo jina lake rasmi likawa ni Joseph John Edward. Kwa kuwa wazazi wake Joseph walikuwa ni waumini wa Kikristo, walikuwa na kawaida ya kwenda Kanisani kila Jumapili kwa ajili ya ibada. Kwa kuwa Joseph alikuwa mchanga, waliandamana naye. Alipokuwa kanisani, aidha alilala fofofo wanapoingia kanisani au alilia sana, kiasi cha wazazi kulazimishwa kutoka nje kwani kilio cha mtoto kilivuruga ibada

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013
Sheikh Saidi John, alipata udhamini wa kwenda kusoma nchini Afrika Kusini katika chuo cha Kiislamu cha Darul Ulum- Pretoria. Hapo alisoma masomo ya dini na sekula kwa miaka sita. Kabla ya hapo hakuwahi kusoma shule yeyote wala Madrasa yeyote. Hata hivyo katika hali ya kushtua kidogo, alipoanza shule, Mwenyezi Mungu alimjaalia uwezo wa ajabu na kumudu kusoma shule ya msingi mpaka High School na kuhitimu. Alifanya vizuri katika dini na kutakiwa kuendelea kuhadhiri chuoni hapo, ambapo aliajiriwa kama Junior Lecturer chuoni hapo. 2012 alipewa mwaliko kwenda India katika jimbo la Kerala kwa ajili ya Da’awa. Kwa sasa Sheikh Saidi John (Sheriff) anaishi Mtoni jijini Dar es Salaam na wazazi wake ambao awali aliwaacha Arusha. Mwaka 1998 wazazi wake nao walisilimu. Baba yake, mzee John Edward alisilimu na anaitwa Hassan Edward na mama yake aliyekuwa akiitwa Rose, sasa anaitwa Zainab. Tangu kurejea kutoka Afrika Kusini, Sheikh Saidi John, ameanzisha taasisi ya Da’awa inayoitwa Said John Da’awa Trust Fund, ambayo kazi yake ni kueneza Da’awah na kufanya mihadhara ndani na nje ya nchi. Mbali na kazi huyo, Sheikh Saidi kuanzia tarehe 2 Machi, 20013, ameanzisha utaratibu wa kusoma dua kila siku za Jumamosi na Jumapili, kuanzia saa 1:00 asubuhi huko Tandika mtaa wa Sambwisi. Dua hiyo itakuwa ikisomwa kwa ajili ya kuwaombea wenye shida mbalimbali na kwamba, Wale wanaotaka kushiriki katika dua hiyo na Sheikh, hawahitajiki kulipa chohote. Baadhi ya Masharif waliowahi kutokea nchini ni Sheikh Sharif Mikidad Matongo, aliyezaliwa mkoani Tabora mwaka 1986. Naye alizaliwa katika familia ya Kikristo na alitabiri kutokea nchini watoto wenye miujiza ya Qur’an na Sunna za Mtume (s.a.w) wapatao watano. Mwaka 1,989 akazaliwa Sheikh Saidi John mkoani Arusha. Baadae akazaliwa Sheikh Iddi Khalifa, maarufu kwa jina la Shariff Kichwa. Yeye hivi sasa yupo nchini Gambia akiendelea na kazi ya Da’awa na kusoma kwa udhamini wa Rais Yahya Jammeh wa Gambia.

AN-NUUR

Sheikh Said John (Shariff)

Madaktari walithitisha kafa Sasa anaendesha mihadhara kimataifa

Shariff Said John (katikati) akiwa nchini India katika moja ya mihadhara yake.
iliyokuwa ikiendelea. Wa z a z i w a J o s e p h hawakujua tatizo ni nini kwa kuwa mtoto haumwi na alikuwa kashiba. Wakaona ni hali hiyo inaweza kumpata mtoto mchanga. Mtoto Joseph alipotimiza umri wa miaka mitatu, akalikana jina lake la Kikristo na kujiita Saidi, na kusema yeye ni Muislamu. Akaanza kusikika akisema maneno ambayo kwa wazazi w a l i o k u w a Wa k r i s t o , hawakujua maana yake. Kwa mtazamo wao, walidhani mtoto wao amekubwa na mapepo machafu. Kufuatia hali hiyo Mzee Joseph na mkewe Rose walianza kuombea kwa jina la Yesu ili mapepo yanayomwandama mtoto wao yatoke. K a t i k a h a l i iliyowashangaza zaidi, kila wachungaji walipomfanyia maombi, mtoto Joseph alikuwa akisema hana mapepo, bali yeye ni Muislamu na aliangusha kilio kikali hadi wakati fulani kupoteza fahamu. Baada ya hali kuwa hivyo, Mzee John alipendekeza kusitishwa maombi kwa mwanaye. Lakini mama mtoto, yaani Bi. Rose, hakukubali ushauri huo na kusisitiza kuendelea kuombewa mtoto ili mashetani yamtoke. Uliibuka mzozo kati ya wazazi wawili. Mama yake Joseph yeye alihofu hali itakuwaje iwapo kanisa na majirani zake wakisikia mtoto wake kwa umri alio nao anasoma Kiarabu na anasema yeye ni Muislamu. Ukafika wakati akatishia maisha ya mtoto. Baba, yaani mzee John kuona hali hiyo, kwa kuwa wote hawawezi kuishi na mtoto wao na kumuua lisingekuwa jambo zuri, wakaona bora wamtenge. Joseph alipelekwa kwa binamu yake Maryam, ambaye ni Muislamu aliyeishi Dar es Salaam. Maryam alimpokea mtoto Joseph licha ya kuwa katika mazingira magumu. Baada ya kusikia yale maneno aliyokuwa akiyasema Joseph, alibaini mara moja kuwa ni Qur’an na Hadithi za Mtume (s.a.w). Hata hivyo naye alishangazwa kwa umri mdogo wa mtoto Joseph wa miaka mitatu kusoma Qur’an na Hadithi, huku akiwa hajafunzwa na yeyote na anatoka katika familia ya Kikristo. Bi. Maryam alimfuata Marhum Sheikh Hilal Shaweji Kipozeo na Alhad Musa, kuwaelezea jambo hilo. Nao walilipeleka kwa Waislamu. Mwaka 1995 Sheikh Said (Joseph) alianza kuhubiri mihadhara katika misikiti mbalimbali jijini Dar. Alifanya ziara mbalimba za mihadhara mikoani nchini kwa mialiko ya Masheikh. Mwanza, Dodoma, Kagera, Musoma, Tanga, Mtwara, Lind ink. Mwaka 1999 alianza ziara za mihadhara nje ya nchi hususan Malawi, ambako walifanya mihadhara nchi nzima, wilaya na vijiji isipokuwa wilaya ya Nkata Bay. Mihadhara hiyo ilimvuta hadi Rais wa nchi hiyo wakati huo Bw. Bakil Muluzi. Wakazuru Ikulu na kufanya mazungumzo naye na kuomba dua. Mwaka 2000 akafanya ziara ya mwaka mzima nchini Msumbiji. Huko nako walifanya mihadhara mikoa yote. Kama ilivyokuwa Malawi, Rais wa wakati huo wa Msumbiji, Bw. Joachim Chisano, naye alivutiwa na mihadhara ya Sheikh Saidi na kumwalika Ikulu ya Maputo na kufanya naye mazungumzo na kufanya dua. Katika ziara za mihadhara ya Sheikh Saidi John aliyofanya, watu takriban 28,000 waliweza kusilimu. Mwaka 2002 mwishoni

7
ubora wa watu katika kuwahudumia ni wazazi wawili ambao ndio sababu ya kuwepo kwetu baada ya Mwenyezi Mungu basi wao ndio wenye haki sana juu ya huduma hizi muhimu amesema mwenyezi Mungu (na wazazi wawili muwafanyie wema) na neno wema hapa na ukomo na mwisho wa neno na mwisho wa neno katika lugha ya kiaarabu inaleta faidia ya kudumu na kuthibiti na kuendelea. Na vile vile jamaa na watoto umeamrisha Uislamu kuwahudumia kwa wema na kwa ukarimu ulio nzuri amesema Mtume (S.A.W) mbora wenu mbora wenu kwa watu wake na mimi ni mbora wenu kwa watu wangu) na baada ya watu wangu ni watoto jirani umeamrisha Uislamu kuishi nao vizuri na kuacha kuwaudhi na tuwahifadhi na kuwasaidia. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (na Muabuduni Mwenyezi Mungu na msimshirikishe na kitu chochote na wazazi wawili muwafanyie wema na wale jamaa wa karibu na mayatima na masikini

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Msamaha katika kuhudumiana ni amri ya Uislamu
na jirani wa Dini moja na jirani wa Dini tofauti na rafiki wakando yaimani na wasafiri) na amesema Mtume (S.A.W) (hakuacha kuniusia mimi jibrili hadi nikadhani jirani yangu atanirithi au nitamrithi kwa hakika alipewa habari Mtume juu ya mwanamke ambaye anasimama usiku kwa ibada na kufunga mchana lakini anamuudhi jirani yake kwa ulimi wake na kuishi nae vibaya akasema mtume (S.A.W) huyo ni motoni) Basi huu ndio msamaha katika kuhudumiana kwa namna mbalimbali za watu na msamaha huu unafikia watu wambali ya Dini kwa kuhusisha na kukusanya walio waislamu na wasio waislamu amesema Mwenyezi Mungu (hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha uadilifu na wema na kuwapa ndugu wakaribu na anazuia maovu na mabaya na Jeuri anawaonyeni huwenda mkakumbuka) na amesema tena (na semeni kwa watu yaliyo mazuri basi neno watu inakusanya mataifa yote na jamii zote. Kisha ukazingatia Uislamu juu ya namna miongoni mwa kuhudumiana inawezekana ikawa na kanuniani au Dhulma na udanganyifu. Amebainisha kwamba Mwenyezi Mungu anawahurumia waja wake ambao wanasamehe katika huduma zao na wengine

SHEIKH WAHEED MANSOOR MOHAMED SHUKRANI zote anastahiki Mwenyezi Mungu mola wa viumbe wote na Rehema na Amani zimfikie mbora wa mitume. Ama baada ya utangulizi huu. Kwa hakika Dini ya Kiislamu ndini ya kukamilisha katika mashina yake na matawi imetia nguvu dini juu ya kufafanua kwamba kuhudumiana vizuri ni msingi Mkuu wa Dini hii. Bali imekuja katika Hadithi ya Mtume (S.A.W) (Dini ni kuhudumiana) na kuhudumiana huku lazima kuwe na misingi iliyofafanuliwa nguzo zake ambazo ni:Msamaha uadilifu na upendo. Na kuhudumiana vizuri ni miongoni mwa amri za Dini yetu hii tukufu. Kwa hakika imefahamisha na kubainisha kuwa

katika kuuza na kununua na kukopesha na kudai. Amesema mtume (S.A.W) amemrehemu mola wetu mtu ambaye anapouza husamehe na anaponunua husamehe na anapodai husamehe) na katika mapokezi mengine na anapolipa neno kusamehe lina maana ya kuwa mpole laini na huruma katika kuuza kwake na kununua kwake na kulipa kwake na kudai kwake Deni na mengineyo ni wajibu awe Muislamu mpole kwa watu na usamehevu wa kulipa maana yake ulipe hali ya kuwa roho yako iwe radhi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aturuzuku moyo wa kuhudumia ulio mwema.

UMRAH 2013 / 1434 SAFARI YA UMRAH YA SIKU 1O KWA DOLA 1450
KUONDOKA TAREHE 27 MARCHI NA KURUDI TAREHE 7 APRIL 2013 GHARAMA INAJUMUISHA: TIKETI YA NDEGE YA KWENDA NA KURUDI DAR-MADINA, JEDDAH- DAR MALAZI SIKU 4 MADINA HOTELI YA NYOTA TATU YA AL ANSAAR NEW PALACE MALAZI SIKU 6 MAKKA HOTELI YA NYOTA TATU YA NAWRAT SHAMS ZIYARAH SEHEMU ZA KIHISTORIA MADINA SIKU YA MWISHO YA KUJISAJILI NI TAREHE 15 MARCHI 2013 KWA MAWASILIANO ZAIDI NA USAJILI WASILIANA: PEACE TRAVEL, MTAA WA MAFIA INATAZAMANA NA MASJID MANYEMA. NAMBA YA SIMU 0655/0784 411 788, 0777 411 020, 0713 530 036 Barua pepe: peacetraveltz@gmail.com • HUDUMA YA UMRAH KWA MTU BINAFSI, FAMILIA NA KIKUNDI INAPATIKANA WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA HADI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI • USAJILI WA HIJJA 2013 / 1434 UMESHAANZA GHARAMA NI DOLA 4450 KWA KILA KITU. PIA TUNATOA MSAADAWA HUDUMA YA KUOMBA VIZA ZA SAUDI ARABIA (UMRAH), UAE (DUBAI), MAREKANI, UINGEREZA,CANADA, THAILAND, UCHINA, UTURIKI, MISRI, YEMEN, NIGERIA, JAPAN, INDONESIA, INDIA, NA NCHI ZINGINEZO. Nyote mnakaribishwa Khidmat Islamiyah kwa huduma Bora

TANGAZO
VITABU VIPYA VYA MIHADHARA, MASWALI NA MAJIBU BAINA YA WAHADHIRI WA KIISLAMU NA WACHUNGAJI, PAMOJA NA MAWAIDHA YA SHEIKH NURDIN KISHKI. VINAPATIKANA MSIKITI WA MTORO (DUKANI KWA SAIMU) KARIAKOO. PIA VINAPATIKA KATIKA MADUKA YOTE YA VITABU VYA DINI JIJINI DAR ES SALAAM, KWA JUMLA NA REJAREJA. PATA NAKALA YAKO SASA. 0713 47 10 90, 0685 47 10 90, 0773 19 46 6.

8

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

9
Na Omar Msangi YA P O mambo yanachefua japo inakuwa ni uhuru wa kila mtu kufikiri, kusema, kutoa maoni na kutenda aonavyo inafaa. Lakini kabla ya kusema zaidi niungane na Watanzania pamoja na wapenda amani wote, kwanza kulani mauaji ya Padri Evarist Mushi na pia kutoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa karibu wa marehemu Padri Mushi. Pili niseme pia kuwa ni matarajio yangu kwamba vyombo vya dola vitatekeleza wajibu wao kwa umakini, uadilifu na kwa kufuata sheria kuhakikisha kuwa wahusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria. Nasema kwa umakini kwa sababu zipo kauli zimetolewa na zinazoendelea kutolea ambazo zinatia wasiwasi. Moja ni pale Rais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliposema kuwa ameviagiza vyombo vya dola kushirikiana na mashirika ya upelelezi ya nchi za nje katika kuchunguza mauwaji haya. Kauli hiyo ya Mheshimiwa Rais ikakolezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi pale aliposema kuwa Kuuliwa Padri Mushi ni tukio la kigaidi na kusisitiza kwamba tayari keshapewa kibali na Rais Kikwete kutumia mashirika ya nchi za nje. Japo si Rais Kikwete wala Waziri Nchimbi aliyefafanua ni nchi gani itaalikwa kufanya uchunguzi, lakini mara tu baada ya kauli ya Rais na Waziri, Ubalozi wa Marekani ukatoa kauli ya kwamba ipo tayari kutoa msaada. Lakini pia ukifuatailia mijadala inayoendelea katika vyombo vya habari, kilicho katika midomo ya watu ni ‘FBI’ na ‘CIA’. Gazeti moja likifurahia ujio wa ‘FBI’ katika toleo lake la Jumatano Februari 20, 2013 likachekelea likisema: “FBI wadaiwa kutua kisiri siri na kuwashikisha adabu wahusika wote. Wana vifaa vya kisasa vya kubaini mtuhumiwa popote.”

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Padri Mushi katolewa kafara kama Askofu Oscar Romero?

Rais Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Kisha gazeti hilo huku likiwa limeweka picha ya askari wa Marekani ukurasa wa mbele, likadai

TAARIFA za awali tulizo nazo zinafahamisha kuwa Al-Jazira Islamic Center, ni Kituo cha Kiislamu kilichopo Ukerewe na kilichosajiliwa na Serikali mwaka 2000 kwa Sheria ya Usajili iliyo chini ya Kabidhi Wazii kikitoa masomo ya Dini ya Kiislamu pamoja na huduma za Kijamii. Baadhi ya huduma za kijamii zilizokwisha kutolewa na taasisi hiyo imeelezwa kuwa ni pamoja na kuchimba visima vya maji safi-Visima 38 wilaya ya Ukerewe na Msoma. Pili, kutoa misaada ya vyakula na nguo na misaada mbali mbali kwa wenyeji bila kujali dini zao. Pia taasisi hiyo imejenga nyumba ya mwalimu na darasa la wanafunzi katika shule ya msingi ya Neduye na kuwachimbia kisima cha maji kwa ajili ya wanafunzi na maeneo jirani. Al Jazeera pia imechimbia kisima katika Shule ya Sekondari ya Nansio na ina mpango wa kujenga Secondari kwa ajili ya wananchi wa Ukerewe. Hiki ndio chuo ambacho hivi sasa baadhi ya magazeti yanadai kuwa ni chuo cha magaidi na kwamba kinaingiza silaha nchini bila ya serikali kujua. Likitoa shutuma hizo gazeti la Mtanzania linasema

Kituo cha Kiislamu Al-Jazeera
kuwa licha ya kuwa wahitimu wa Chuo hicho wanakuwa magaidi wa Al Qaida na Al Shabab, lakini pia huingiza silaha (za kijeshi na kufanyia ugaidi bila ya vyombo vya dola kujua). Yametajwa pia masuala ya kufundisha kareti na kun- Fu pamoja na kupokea wageni kutoka Kenya, Somalia na ufadhili kutoka Oman na nchi nyingine za Kiarabu. Dhana inayojengwa hapa ni kana kwamba ni haramu na marufuku katika nchi hii kujifunza kareti na imekuwa chuo na kituo hicho pekee cha Al Jazeera kinachotoa mafunzo/ mazoezi hayo. Dhana nyingine potofu inayopandikizwa ni hili la kupokea wageni na kupata misaada kutoka nchi za nje. Hoja hapa sio kwamba Chuo hicho kinapokea wageni au la na wala sio kama kinapokea misaada au la. Sio kazi yetu kuwasemea au kuwatetea Al Jazeera Islamic Centre. Swali la kuuliza hapa ni je, tangu lini ikawa haramu katika nchi hii kwa taasisi za kidini, kijamii na serikali kupokea misaada kutoka nje? Au haramu hii ni zinapopokea taasisi za Kiislamu misaada kutoka Qatar na Oman? Tangu lini ikawa haramu katika nchi hii kuingia wageni kutoka Kenya, Uganda, Arabuni na hata Somalia?

Rais wa El Salvador, Mauricio Funes kunukuu kauli ya muumini mmoja wa Parokia ya Minara Miwili akisema: “Kwa kweli tumefurahi

kusikia kuna uwezekano wa wapelelezi kutoka nje ya nchi kufika Zanzibar na kufuatilia chanzo cha mauwaji haya…”. Lakini zaidi ya hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikikoleza ‘agenda’ ya ugaidi na vingine vikija na kauli kana kwamba imethibiti ugaidi upo nchini na magaidi hao ndio waliomuuwa Padri na magaidi wenyewe ni Uamsho na akina Ponda na wanachosubiri ni kuona ‘FBI’ na ‘CIA’ wakiwatia adabu. Nianze kwa kusema kuwa inavoonekana ni kuwa lililokuwa likitakiwa huenda limetimia. Ni aibu na msiba mkubwa. Tusubiri, balaa kubwa

Ama katika jambo la kipuuzi na la kuitukana Idara ya Uhamiaji, Polisi, Usalama wa Taifa, Vyombo vya Dola/ Sheria na Serikali kwa ujumla; ni hili la kuleta hoja kuwa kinaweza kujengwa kituo cha kufunza ugaidi kikafanya kazi kwa zaidi ya miaka 10 huku kikiingiza silaha za kivita nchini, serikali ikiwa haina habari mpaka izinduliwe katika usingizi na aliyejiita Ratifa Baranyikwa wa Mtanzania! Na ili kudramatize, inawekwa ramani kuonyesha ilivyo vigumu kufika Al Jazeera Islamic Centre. Kama vile kusema kuwa ‘magaidi’ hawa wa Kiislamu wamechagua kuweka chuo chao cha kigaidi kisiwani katika ziwa Victoria mahali ambapo si rahisi Polisi, Uhamiaji na Usalama wa Taifa kufika! Hata hivyo, maadhali wanaotukanwa na kutafutiwa sababu ni Waislamu, wala hutasikia serikali ikisema kitu. Lakini maadhali jambo hili na agenda hii sio jambo la kuihusu Al Jazeera Islamic Center pekee bali Waislamu wote, itakuwa ni jukumu la Waislamu (ikiwemo An nuur), kufuatilia tuhuma na yale yote yaliyosemwa na Ratifa (Latifa?) Baranyikwa ili kujua ukweli. Mhariri

linakuja. Ila wasichojua washenga wa ajali hii ni kuwa balaa linalokuja halitachagua, mwandishi, Muislamu wala Mkristo. Nimesema kuwa ni aibu na msiba mkubwa kwa sababu tukio limetokea kabla hata polisi hawajaanza uchunguzi, serikali inatangaza kuwa haiwezi kufanya kazi hiyo bila ya msaada wa watu wa nje. Inachosema na kukiri serikali hapa ni kuwa waliohusika na mauwaji hayo si wananchi wake. Sina uhakika kwamba kuna serikali yoyote duniani ambayo ina polisi na vyombo vya dola ambavyo havina uwezo wa kuchunguza uhalifu ndani ya nchi yake. Labda Tanzania itakuwa ya kwanza. Kwa hiyo inachotuambia serikali yetu hapa ni kuwa haya si mauwaji ya kihalifu, ni mauwaji ya kupanga. Na kama ni ‘ugaidi’ kama alivyosema Waziri wetu Nchimbi, basi utakuwa ni ugadi wa kupanga (False Flag Terror Attacks) na ndio maana haraka haraka serikali inatuambia kuwa itawaalika wenye agenda yao ya ugaidi wafanye uchunguzi. Kama ndio hivyo, basi tumemwelewa M h es h imiw a R ais n a Waziri wetu wa Mambo ya Ndani. Na kwa bahati nzuri wenyewe haraka haraka wakatoa kauli za kuleta watu wao utadhani walikuwa wamejiandaa wanasubiri fursa hiyo. Pengine swali linalokuja hapa ni hili, hii haraka ya kualika ‘Watu wa nje inatoka wapi?’ Huyu anayealikwa, upi wasifu wake? Katika taarifa ya BBC Alhamisi Machi 25, 2010 (na vyombo vingine vya habari vya kimataifa) iliripotiwa kuwa Rais wa El Salvador, Mauricio Funes, ameomba radhi kutokana na mauaji ya Askofu Oscar Romero. Archbishop Romero aliuliwa kwa kupigwa risasi akiongoza misa Machi 24, 1980. “I am seeking pardon in the name of the state. The archbishop was a victim of right-wing death squads who unfortunately acted with the protection, collaboration or Inaendelea Uk. 10

10
Inatoka Uk. 9

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013 Waziri Nchimbi wanatarajia kuwa watatua nchini muda si mrefu kutupa msaada wa kipolisi na kikachero! Na baadhi ya magazeti yanangoja kwa hamu ujio huo hata wakaona fahari kuweka picha ya askari wa Marekani katika kurasa za mbele za magazeti yao! Kwa muda mrefu katika nchi hii kumekuwa na jitihada za makusudi za kupandikiza ugaidi ili kutoa nafasi kwa wenye agenda zao wapate fursa ya kusambaza makucha yao ya kikachero na kijeshi. Ukiacha zile porojo za ‘Al Qaida’ wa Kiburushi waliodaiwa kuingia nchini wakawinda Mikumi na Serengeti na kuondoka na kitoweo kuwapelekea Al Qaida wenzao kule Kandahar bila kuonekana na vyombo vyetu vya usalama (!?), hekaya za Fazul hadi usanii wa mtoto wa shule ya msingi aliyepenya ngome ya ulinzi Ubalozi wa Marekani akiwa na ‘mabomu’, sasa tunaletewa ugoro mwingine wa chuo cha Kiislamu Ukerewe kinachodaiwa kuingiza wakufunzi wa ugaidi nchini na silaha za kijeshi bila ya vyombo vya dola kujua. Na sasa ndio wanastuliwa na gazeti moja! Japo haya ni matusi makubwa na kuvidhalilisha vyombo vya dola na serikali yenyewe, lakini maadhali habari hizi zinasaidia kupalilia agenda ya kupandikiza ‘ugaidi wa kupanga nchini’ kama ilivyopepewa Al Shabab Kenya, wala hutasikia kauli ya serikali kama ambavyo mpaka sasa ipo kimya kuhusu wale Wazungu wanaodaiwa kuwepo katika mhadhara wa kuhamasisha Wakristo kuchinja na kupeleka nyama sokoni kule Buselesele, Geita. Pengine ingekuwa vyema kama kuna watu washaingia mkataba wa kutoa sadaka nchi hii, wawaruhusu tu ‘Wazungu’ wao waje wachukue madini watakayo, mafuta, gesi, ardhi, TANESCO na kuweka kambi zao za kijeshi. Njia wanayotaka kuchukua italeta maafa makubwa. Na hili si jambo la kufikirika. Hii imedhihirika katika nchi mbalimbali zilizokubali kulazimishwa kuwatafuna Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

participation of state agents”. Ilisema taarifa ya BBC ikimnukuu Rais Funes akizindua sanamu ya Askofu Osca Romero katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa El Salvador kama namna ya kumuenzi na kumkumbuka askofu huyo. Alichosema Rais Mauricio Funes ni kuwa anaomba radhi kwa niaba ya serikali kutokana na kuuliwa askofu Oscar Romero kwa sababu askofu huyo aliuliwa na kikosi cha wauaji (death squads) ambao walikuwa wakilindwa na kushirikiana na vikosi vya serikali. Ufupi wa maneno ni kuwa waliomuuwa Askofu Mkuu Oscar Romero walitumwa na serikali. Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi ya Tume iliyoteuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1993 ili kutafuta ukweli, mauwaji ya Askofu Mkuu Osca Romero yalitekelezwa na “Rightwing death squads?” kwa maelekezo na amri ya Roberto D’Aubuisson, ambaye alikuwa afisa wa jeshi la El Salvador. Pengine swali ni je, nani Askofu Romero? Kwa nini aliuliwa? Na ni nani hawa “Right-wing death squads?” Taarifa ya The New York Times, March 31, 1980, inasema kuwa Archbishop Romero, alikuwa mstari wa mbele kupinga mauwaji na mateso waliyokuwa wakifanyiwa wananchi wa El Salvador, na kutetea haki za binadamu kwa ujumla katika Latin America. Kwa hiyo ukiacha kazi zake za kidini za ki-uaskofu, Askofu Mkuu Oscar Romero alikuwa miongoni mwa wanaharakati wa El Salvador waliopinga ubeberu wa Marekani katika nchi hiyo. Alikuwa mtetezi wa masikini katika nchi hiyo na akiendesha harakati za kupinga uwepo wa makachero na wanajeshi wa Marekani katika El Salvador akisema kuwa wanasaidia askari wa nchi hiyo kuuwa wananchi wasio na hatia. Kwamba kwa msaada wao, Polisi, Jeshi na serikali ya El Salvador, ilikuwa ikiuwa watu wake wasio na hatia. Na kama ni hatia, basi ilikuwa kupinga ubeberu

Padri Mushi katolewa kafara kama Askofu Oscar Romero?

Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh

General David Petraeus mwaka 2005 akinukuliwa na mwandishi Jonathan D. Tepperman (Senior Editor of the main establishment journal, Foreign Affairs of the Council on Foreign Relations) akikiri kuwa katika kulinda maslahi ya Marekani walikuwa wakiwasaidia walioitwa ‘bad guys’ kuwaangamiza ‘bad guys’. ‘Bad guys’ kwa maana ya watu waovu wa kwanza, ni vikundi vya kigaidi, wauwaji na watesaji. ‘Bad guys’ wa pili aliowataja ni wale wote waliokuwa wakiendesha harakati za kiraia kupinga unyonyaji na ubeberu wa Marekani: Kwa maneno yake alisema: “We did back the guys who went after the bad guys. And [we] defined ‘bad guys’ pretty broadly.” (Angalia: Salvador in Iraq: Flash Back” Council on Foreign Relations, by Jonathan D. Tepperman, Senior Editor of Foreign Affairs, 5 April 2005.) Askofu Mkuu Oscar Romero alikuwa ‘bad guy’ katika kundi la pili. Sasa hao ndio wanaotarajiwa kuwa katika lile kundi la watu walioombwa na serikali yetu watusaidie kumsaka muuwaji wa Padri Evarist Mushi. Hao ndio ambao baadhi ya waandishi na wananchi katika kusherehesha kwao kauli ya Rais Kikwete na

wa Marekani katika nchi hiyo. Ta a r i f a y a B B C niliyonukuu inasema kuwa mnamo Februari 1980, Askofu Mkuu Romero alimtaka Rais wa Marekani wakati huo Jimmy Carter, kuacha kuipa serikali ya El Salvador msaada kwa sababu misaada hiyo inatumiwa na wanajeshi na polisi kuuwa raia. Lakini Carter hakusikiliza kilio hicho na ndipo Machi 24, 1980 akauliwa Askofu Mkuu Romero. Gazeti la The New York Times, la October 22, 1987, Ukurasa wa 11 lina makala iliyoandikwa na Lindsey Gruson, pamoja na mambo mengine, makala hiyo inaarifu kuwa msaada wa Serikali ya Marekani wa kikachero na kipolisi kwa serikali ya El Salvador, umekuwa ukitumika kufundisha polisi watesaji wa raia, vikosi vya wauwaji (death squads) waliokuwa wakiuwa raia na vikosi vya kigaidi vilivyokuwa vikifanya ugaidi wa kupangwa na dola (statesponsored terrorism), ambao yote hayo kwa ujumla yaliisambaratisha El Salvador ikawa kama Jahannamu kwa wananchi wa nchi hiyo katika miaka ya 1980’s. Ikiwa na kichwa cha habari “Salvador Divided over Aid to Police”, makala

hiyo ilisema kuwa “The aid package… is destructive b e c a u s e i t re w a rd s unrepentent torturers and members of the right-wing death squads.” Na kwamba hawa “death squads” ndio waliohusika kuuwa maelfu ya raia katika miaka ya 1970s na 1980s. Sasa hao ndio “rightwing death squads” waliomuuwa Askofu Mkuu Oscar Romero kwa vile alikuwa mtetezi wa wanyonge na akipinga ubeberu wa Marekani katika El Salvador. Na kama alivyojisema Holly Burkhalter, wanapoingia watoa misaada ya kipolisi na kikachero, lengo lao kubwa ni kulinda masilahi yao na hufanya hivyo hata kama itabidi kuuwa watu kupitia serikali zao wenyewe. “We’re getting back in the business of helping governments crack down on their own people.” Anasema Holly Burkhalter, ambaye ni mwakilishi wa Americas Wa t c h Wa s h i n g t o n . Burkhalter alikuwa akizungumzia misaada mipya kwa nchi za Latin Amerika akisema kuwa itakachosaidia misaada hiyo ni kuongeza vurugu, mauaji na mateso kwa raia. Naye Lawrence Korb, (Assistant Secretary of Defense from 1981 to 1985)

11

Makala/Tangazo

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk. 10

Padri Mushi katolewa kafara kama Askofu Oscar Romero?
la kuuliwa Padri Mushi, ikifuatiwa na kauli za wanasiasa na ushereheshaji wa baadhi ya waandishi wa habari, utaona kuwa kuna jitihada za makusudi za kupandikiza kitisho. Inapotokea kauliwa Padri, hapana shaka kishindo chake ni kikubwa. Na pengine kilichotarajiwa ni kupatikana kianzio cha kupandikiza kitisho cha kweli. Kisasi juu ya kisasi. Kama nadharia hii itakuwa kweli, basi Padri Evarist Mushi atakuwa ametolewa kafara. Kutokana na kafara hii, huenda watu wengi zaidi wakatolewa kafara pia ili kuleta mzizimo wa kitisho cha kweli. Lakini jingine ambalo ni la uhakika ni kuwa wale washirika wetu tunaodhani kuwa watatusaidia kuwapata wauaji na kutuliza hali nchi itulie na idumu katika amani, umoja, mshikamano na udugu; hawatotusaidia kumjua muuwaji wa kweli japo wao wenyewe wanaweza kumjua. Na maadhali tumewaita wenyewe, itabidi pia tu w e t a y a r i k u k u b a l i k ila w a n a c h o t u a m b i a na kutuagiza kufanya. Kama ni kujua ukweli, pengine tutakuja kuujua miaka mingi ijayo kupitia Wikileaks. Aliyekuwa Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh aliambiwa awaruhusu askari wa Marekani wauwe raia wake lakini taarifa ya serikali iseme kuwa ni vikosi vya serikali ya Ye m e n v i n a p a m b a n a na magaidi. Akakubali. Wikileaks ndiyo iliyokuja kumuumbua. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP Novemba 28, 2010 likinukuu nyaraka za siri zilizotolewa la WikiLeaks, Ali Abdullah Salehe alinukuliwa akisema kuwa serikali yake itaendelea kusema kuwa mabomu ya Marekani yanayouwa raia wa Yemen ni ya Polisi na Askari wa Yemen. “We will continue saying

ASKOFO Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycarp Kadinali Pengo

raia wake wenyewe kwa kuwapachika ugaidi. Mauwaji ya Padri Mushi yaliyofuatiwa na hizi kauli za haraka haraka za kutaka msaada wa ‘FBI’ na ‘CIA’, yanaleta wasiwasi mkubwa kwamba huenda kuna jambo limepikwa kuitumbukiza nchi hii katika janga. Na kama wananchi, Waislamu na Wakristo hawatakuwa makini, wakadandia na kubebwa na hizi kauli za wanasiasa na baadhi ya waandishi wa habari, itakuja kuwa balaa. Ukiangalia mgogoro wa kuchinja kule Geita, lile la Uamsho na kutekwa Sheikh Farid na sasa hili

Je umemaliza darasa la saba au kidato cha nne na hujui la kufanya? Kituo cha mafunzo na stadi za kazi Dar es Salaam kinawatangazia OFA MAALUM ya nafasi za MAFUNZO katika kozi zifuatazo:1. Uwalimu wa Chekechea (miezi 9 ada 450,000 tu (F IV)) 2. Matumizi na ufundi wa kompyuta (miezi 4 ada 100,000 (F IV)) 3. Ushonaji na kudarizi (miezi 6 ada 100,000 (STD VII)). Ni muhimu kuwa:  watakaosoma ualimu wa chekechea watasomeshwa kiingereza bure na watapelekwa masomo kwa vitendo chini ya usimamizi wa kituo.  Wanafunzi watasaidiwa mbinu za kutafuta ajira watakapomaliza.  wanafunzi wa Kompyuta kozi watakazosoma ni pamoja na website development, graphic designing, computer maintenance na database management. Kituo kipo Tabata karibu na Chuo cha St. Meries nyuma ya Alfaruk Sekondari School (Africa Muslim Agency) palipokuwa na chuo cha uwalimu SAFINA na Temeke Masjid Tungi. Kujiunga fika ofisi za TAMPRO magomeni au mahali chuo kilipo kuchukua fomu au piga simu 0714151532, 0767151532 au 0718807228 kwa maelezo zaidi. DAR ES SALAAM SDC TUNAKUONGOZA KATIKA MAISHA YAKO

ya Serikali yetu kuita ‘makachero wa nchi rafiki’, Je, tumenogewa na kutamani nasi kushiriki mchezo huu wa Ali Saleh? Alichozawadiwa Abadullah ni kuwa pamoja na kuwa aliuwa sana wananchi wake walioandamana wakitaka demokrasia, hakushutumiwa na Marekani wala kuwekewa mkakati wa kung’olewa kama anavyoandamwa hivi sasa Bashar El Assad wa Syria. Je, nasi tuna wasiwasi kuwa huenda huko mbele ya safari tukakabiliwa na nguvu ya umma kama ilivyotokea kwa Ali Saleh? Je, ukaribisho huu wa haraka haraka ndio kujiandalia na kujiwekea akiba ya kulindwa na kukaribishwa White House kama Ali Saleh alivyokaribishwa Washington katika kilele cha umwagaji damu nchini mwake? Kila ambako walitiwa ujinga wakaona kuwa baadhi ya raia na watu wao ni magaidi, hakuna salama. Na balaa la mchezo huu likiingia nchini, hakuna atakaye kuwa salama. Na likiingia, ndio limeingia. Haliondoki kwa urahisi maana wenye agenda yao watataka kitisho kidumu ili kuhalalisha na kujenga hoja ya kuendelea kuwepo. Kwa hiyo itabidi matukio ya kigaidi ya kuuwana yadumishwe. Ndio yanayowakuta Pakistan, Ye m e n , I r a q , S o m a l i a , Afghanistan na Kenya. Kwa hiyo kwa wananchi, kwa Watanzania nasema kuwa kama ni watu wa kujifunza tujifunze kutokana na yale yanayokuwata waliotutangulia katika boti hii inayozama huku waliomo wakitushangaa

the bombs are ours, not yours,” alinukuliwa Saleh katika mazungumzo yake na General David Petraeus, ambaye wakati huo alikuwa Kamanda wa Majeshi ya Marekani katika Mashariki ya kati. Katika haraka hii

WAHI SASA NAFASI NI CHACHE MNO

tunavyojitahidi kuikimbilia kuingia wakati wao wapo katika taharuki wakitaka kujiokoa lakini hawaoni pa kutokea.

12
Kalamu leo nashika, ya kwangu kuyaandika, Moyoni yalofichika, na huzuni kuiweka, Leo nataka pasuka, na uwazi kuuweka, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari.

Mashairi NDALICHAKO TAHADHARI

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Kweli mmekithirisha, kwa yale mnayofanya, Waislamu kufelisha, matokeo kudanganya, Shule zenu kupandisha, kwa njia zenu za panya, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Vijana wajitahidi, kitabu kukomalia, Tena wafanya juhudi, na uzembe kwao doa, Ilikuwa yao budi, tokea kufurahia, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. One zao mwangaza, na four mkazijaza, Ziro mkaziongeza, na two kuzipoteza, Shule zenu zikajaza, kwa one za kuingiza, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Kichwani yatuzunguka, yale ya mwaka wa jana, Ndugu zetu kuanguka, na vyuo kutoviona, Ziro kwao kuziweka, na one mkazibana, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Kumi na moja yafika, tarehe iliyopangwa, Ya vijana kujiweka, kwa namba walizopangwa, Darasani kujazika, mtihani kuupiga, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Vijana wamejipika, vyema wamejiandaa, Peni zao kuzishika, kwa vyuo kuendeleza, Dhuluma msijeweka, one zao kuzitoa, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Kwa hiyo haina budi, A zao kuziweka, Kwa hii yao juhudi, kwao hazina mashaka, Msijefanya hurudi, kwa f kuzibandika, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Kalamu nchini naweka, ya kufelishwa, Hakuwa patashika, waislamu kufelishwa, Haki sasa twaitaka, usawa kusimamisha, Kumi na moja yafika, Ndalichako tahadhari. Hussein J.B Gombeye Mwanafunzi Nyasaka Islamic Sec School.

Kesi ya Sheikh Ponda na udanganyifu wa D.P.P
NAOMBA unipatie nafasi ya kufikisha huu ujumbe kwa wahusika wote wa Mfumo kandamizi Kristo. Kilichonisukuma kuja na ujumbe huu ni habari ilioandikwa na gazeti la Mtanzania Uk. wa mbele toleo Na 7228 la tarehe 14/02/2013, yaani Alhamis wiki iliyopita. Habari hiyo yenye kichwa cha habari iliyoandikwa kwa maandishi makubwa “D.P.P amtwisha zigo zito Sheikh Ponda”, chini ikifuatiwa na maneno madogo ya wastani yaliyosema ANADAIWA KUHUSIKA NA ALSHABAAB, vurugu za Zanzibar, Polisi yawaonya Wa i s l a m u w a n a o t a k a kuandamana kesho”. Ndugu zangu Watanzania, bila kubagua dini wala chama cha siasa, bila kubagua sekta binafsi au s e r i k a l i, i ta k u mb u k w a kama miaka miwili na zaidi iliyopita kumekuwa na hoja na mvutano kati ya taasisi mbalimbali za Kiislamu. Na kuhusu kuzuwia kuuzwa kiwanja cha Waislamu kilichokuwa kijengwe Chuo Kikuu cha Waislamu Tanzania. Taasisi za Kiislamu zikiwataka viongozi wa Bakwata, kuacha kuuza kiwanja hicho kwa kuwa ni mali ya ummah wa Waislamu Tanzania, iliyotokana na na Taasisi ya Kusimamia Maslah ya Waislamu Afrika ya Mashariki. Hoja muhimu ni kuwa, wakati kiwanja hicho kilipomilikiwa na Jumuia ya EAMWS, Bakwata haikuwepo na hazikuwepo taasisi tofauti za Kiislamu za kuwatenganisha kama ilivyo leo, isipokuwa taasisi ya EAMWS, ambayo ilisimamia mambo na m a s l a h i y a Wa i s l a m u . Kilikuwa ni chombo cha kutegemewa na Waislamu wote na kilikubalika na Waislamu wote, Kenya, Uganda na Tanzania. Kuundwa kwa taasisi iliyobatizwa jina la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) hayakuwa maamuzi ya Waislamu wenyewe wa Tanzania, bali mipango ya Mwalimu Julius Nyerere na Maaskofu wake wa Kanisa Katoliki kuivunja EAMWS. Na halikuundwa kwa manufaa wala maslahi ya Waislamu wa Tanzania ila ni mipango ya kujilinda na mfumo kandamizi aliouasisi kwa kushauriwa na viongozi wa Kanisa. Hivi ninavyoandika ujumbe huu kwa Waislamu wenye ufahamu aliowajaalia Mwenyezi Mungu, wanachoelewa kuhusu B A K WATA n i c h o m b o cha kuhujumu umoja wa Wa i s l a m u , m a e n d e l e o ya Waislamu, na jitihada zozote zinazoashiria kutaka kuwaunganisha na kuwakomboa Waislamu Tanzania. Na Bakwata wenyewe hili wanalijua vyema. Kwa kujua kuwa hawakubaliki, ndio maana mara kwa mara wamekuwa wakiungana na Maaskofu katika kauli zao za kuvichochea vyombo vya dola kukiuka hata taratibu za kisheria ili kuwashughulikia Masheikh wote wanaoonekana kuwa ni kikwazo kwao katika jitihada zao za kuwakandamiza na kuhujumu maendeleo ya Waislamu. Lengo ni ili wawe huru kuendeleza hujuma na udhalimu wao. Hoja bado ipo, kuundwa kwa Bakwata sio makubaliano kutoka kwa Waislamu wa Tanzania, ambao wakati huo walikuwa wamoja, wenye kuongozwa na taasisi iliyokubaliwa na makundi yote ya Kiislamu. Kimsingi ilipaswa kuanzishwa Bakwata iwajumuishe Waislamu wa makundi yote ya Kiislamu nchini na ndipo liwe Baraza Kuu la Waislamu Tanzania. Kwa hivyo basi, kwa kuwa haikuwajumuisha katika kuanzishwa kwake na muundo wake wa kiuongozi, haina haki ya kuuza chochote walichokirithi bila ridhaa za Waislamu wote, kile kilichotokana na jumuiya ya EAMWS iliyokuwa ikisimamia mambo na maslahi ya Waislam Afrika Mashariki. Sheikh Ponda Issa Ponda, k u w a o n g o z a Wa i s l a m u kuzuwia kuuzwa mali za Waislamu wote, inayouzwa kwa manufaa ya watu wachache, kosa lake liko wapi? Mkurugezi wa Mashtaka, DPP Dr. Eliazer Feleshi, dhamana uliyopewa ya

VIWANJA VILIVYOPIMWA KONGOWE – KIBAHA TOWNSHIP REGISTERED PLAN No. 70995 BLOCK H
PLOT HATUA ENEO – MRABA GHARAMA TSH

H1 H2 H3 H4 H5 H6 H7 H8 H9 H10 H11 H12

50 x 29 32 x 32 50 x 30 37 x 30 50 X 45 33 x 37 60 x 45 50 x 40 67 x 50 70 x 45 90 x 50 59 x 40

1341 Sqm 1136 Sqm 1470 Sqm 1115 Sqm 2259 Sqm 1566 Sqm 2423 Sqm 1984 Sqm 3564 Sqm 2842 Sqm 3780 Sqm 2292 Sqm

4,023,000/= 3408000/= 4410000/= 3345000/= 6750000/= 4695000/= 7269000/= 5952000/= 10692000/= 8526000/= 11340000/= 6876000/=

Vipo Barabara ya Kongowe-Soga Kilomita moja toka barabara ya Morogoro. Simu No.0755 090 754/0715 090 754.

kusimamia serikali ni kubwa. Lakini unaonekana kuingilia uhuru wa mahakama. Umeeleza kwa mujibu wa taarifa zako zilizoandikwa ndani ya gazeti lililotajwa hapo juu, Ponda alihusika na vurugu za Zanzibar, na amehusika kumuua Sheikh katika vurugu za Mombasa nchini Kenya. Na anahusika na kundi la Al- Ashabaab kule nchini Somalia na kwamba, Ponda Issa Ponda si raia halali wa Tanzania. Ni Vema ukaujulisha Ummah wa Watanzania kwani Serikali ina Idara za kiusalama na uhamiaji nchini, zenye majukumu ya kubainisha mambo ya mtu mapema kabla ya mtu kutuhumiwa na mashitaka mengine. Ama suala la vurugu za Mombasa limepita zaidi ya miezi miwili sasa, kwa nini polisi na DPP msubiri kumkamata Ponda kwa mambo ya kiwanja cha Markaz Changombe halafu baada ya miezi mitatu, ndio mnatuletea hoja za mashitaka kama haya? Ponda kahusika vipi kumuua Sheikh wa Mombasa? Ndugu DPP, una taarifa zozote zilizokufikia zinazoonyesha kuwa Sheikh Ponda aliwahi kuwa na uhasama na Sheikh mwenzake wa Mombasa? Idara ya Uhamiaji ndio inayotambuwa watu wote wanaoingia ndani ya nchi na kutoka nchini, Bw. Eliazer Feleshi, unazo taarifa ni mara ngapi kasafiri Ponda kutoka Tanzania kwenda Somalia na kurudi? Ili upatikane uhakika unaothibiti kuueleza umma kuwa ni al-Shabaab? Au uhamiaji wana taarifa juu ya Al Shabab walioingia nchini na kukutana na Ponda? Kama ndio, mbona hawakukamatwa? Au wakati huo Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na serikali kwa ujumla ilikwenda likizo? Kuhusu vurugu Zanzibar, kwa jinsi hali ilivyo na maneno aliyonukuliwa kuyatoa, DPP anaashiria kuwa ni mtu wa Kanisa na anatumia vitengo walivyo navyo kuwachongea Waislamu. Tafuteni waliohusika na vurugu Zanzibar. Acheni kuwasingizia Waislamu na viongozi wao ili kuwakamata, kuwatesa na Inaendelea Uk. 13

13

MAKALA

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Matokeo haya yanatuzalia matabaka hatari
Na Shaban Rajab

KWELI wanafunzi wengi wanaposhindwa kufaulu m t i h a n i w a Ta i f a , i n a t i a uchungu. Bila shaka uchungu unaopatikana sasa, ni funzo tosha kwa wale wanaopuuza malalamiko yanayotolewa na wenye uchungu wa kufelishwa watoto wao, lakini malalamiko yao yasimguse yeyote. Na hata inapotokea jamii fulani ya watu kudhulumiwa, wanapolalamikia dhulma, huishia kupuuzwa na kukejeliwa. Wakorofi, walalamishi. Hata baada ya shinikizo, ukweli unapobainika, kudaiwa ni makosa ya komputa! Safari hii inaonekana ladha ya uchungu wa kushindwa imewagusa wengi na kilio kimekuwa cha wengi pia. Sote tunafahamu kuwa maisha bila elimu katika ulimwengu wa sasa, ni maisha yasiyokuwa na uhakika. Elimu ndio dira sahihi ya maisha ya kila mtu. Elimu inaweza kulikomboa taifa au kuliangusha taifa. Elimu ndio matumaini si kwa taifa tu, bali hata kwa familia na mtu mmoja mmoja. Elimu ndio urithi pekee wa uhakika ambao mtu anaweza kumwachia mwanaye au ndugu yake, ili iweze kumfaa katika maisha yake ya kila siku. Taifa la watu wasio na elimu, ni taifa linalovutia hatari na lisilokuwa na matumaini wala matarajio mema kwa watu wake. Ni taifa linalosubiri watu wake kugawana umaskini, udhalili na aibu. Wakati wazazi wengi na watoto wao wakigugumia uchungu wa matokeo mabovu ya kidato cha nne, lipo tabaka la wazazi ambao wanachekelea na kufurahia kufaulu vizuri watoto wao. Huwezi kumkuta mtoto wa vigogo wa serikali, Mkurugenzi, Katibu Mkuu wa Wizara, Waziri, Mkuu wa Mkoa, Wilaya, Mbunge au mfanyabiashara tajiri, mwanaye anasoma katika shule za Kata. Shule ambazo hazina walimu, na kama wapo hawana sifa. Shule ambazo hakuna vifaa vya kufundishia, hakuna vitabu, madawati ya kugombania, hakuna maabara. Shule ambazo walimu wanadai mafao serikalini miaka nenda. Wanafundisha wakiwa wamekata tamaa na ajira zao. Wanaingia darasani kutimiza wajibu na kujiondokea kusaka maisha kwenye biashara ndogondogo au kufundisha tuition. Katika mazingira haya, watoto wa wakubwa tangu chekechea hadi kidato cha sita wanasoma shule za binafsi za gharama kubwa. Mtoto anapelekwa na kurudi shule kwa gari. Shule ambazo zina walimu bora wanaolipwa sawia. Zina kila vifaa va kutosha vya kufundishia, mwalimu anafundisha kwa matumaini.

Kabwela hadhubutu kumpeleka mtoto wake huko, kwa kuwa hana ubavu wa kulipa ada ya milioni tano kwa mwaka. Matokeo yake ni kwamba, watoto hao wanaosoma wa St. kwa mamilioni, ndio wanaopata elimu nzuri na kufaulu. Hawa ndio watakaohitimu hadi vyuo vikuu na kuja kuchukua nafasi za wazazi wao. Wale wa Kata ndio wale wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika. Kwa kuwa nafasi za shule za sekondari za kata ni kwa ajili yao, husombwa vivyo hivyo kwenda kidato cha kwanza hadi cha nne na kumaliza na daraja sifuri. Matokeo ya kidato cha nne 2012, yanadhibitisha mazingira haya. Kwa mfano, katika shule ishirini bora zilizotajwa na Waziri wa Elimu Dk. Shukuru Kawambwa, ni shule mbili tu za serikali zilizoingia katika orodha hiyo. Ni Mzumbe sekondari ya Morogoro na Kibaha sekondari ya Pwani. Tena shule zenyewe ni zile ambazo zinafahamika kuwa ni zile za vipaji maalum. Kama si kwa sababu ya kuchukua wanafunzi wenye vipaji maalum, bila shaka shule hizi za serikali nazo zingeangukia pua. Hakuna shule hata moja ya Kata iliyopenya hapa. Zaidi ni kwamba, matokeo haya yameonyesha shule za Kata, wanakosoma makabwela zikitamba kwa kushindwa vibaya. Wanafunzi 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata daraja 0. Tunatarajia hawa watakwenda wapi. Wanafunzi 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne. Katika hawa ni wachache sana watakuwa

na alama 27 zinazoweza kuwafanya kwenda vyuo vya ualimu. Waliosalia watakwenda wapi? Baada ya hapo huzagaa mitaani kusaka kazi za vibarua, umachinga, kupiga debe, kuokota chupa za maji nk. Na

baadhi wakiamini kuwa nafasi pekee ya kumudu maisha yao ni kujaribu kuingia kwenye usanii. Baadhi watapotea kabisa kwa kujihusisha na matumizi ya mihadarati na uhalifu. Kwa ujumla watabakia kuwa

tabaka la watawaliwa dhidi ya tabaka la watawala, ambalo wazazi wao ambao ni watawala, walimudu kuwasomesha katika shule hizo bora za gharama kubwa za binafsi na kuhitimu. Wanafunzi waliofaulu ni 23,520 sawa na asilimia 5.16. Bila shaka wengi katika hawa ndio wale wa shule za seminari na nyingine za binafsi za gharama kubwa. Huku kabwela hafiki. Hili ni daraja la watoto wa vigogo, matajiri. Hali ikiendela hivi, tabaka la hawa litashika hatamu za mamlaka na kuendelea kuneemeka. Wa n a f u n z i w a l i o f a n y a mtihani walikuwa ni 456,137, lakini waliokuwa shuleni ni 397,136 na wa kujitegemea walikuwa 68,806. Labda katika mazingira haya, inawezekana kuwa sababu ya wenye dhamana ya elimu serikalini, ambao ndio wasimamizi wa sekta nzima ya elimu nchini, wamekuwa sio wasikivu na wasiojali wala kuguswa, pale wananchi wanapolalamikia elimu mbovu katika shule za Kata na zile za serikali pamoja na utendaji unaotia mashaka wa Baraza la Mitihani Nchini (NECTA). Tumeona namna ambavyo Mh. Mbatia alivyozodolewa Bungeni. Pamoja na nia yake safi, bado wasioguswa na athari wanazopata makabwela katika elimu wakaizima hoja. Kile walichokitetea dhidi ya hoja za Mh. Mbatia, ni sehemu ya matokeo tuliyoyapata sasa.

Kesi ya Sheikh Ponda na udanganyifu wa D.P.P
Inatoka Uk. 12 kuwadhalilisha. Tunajua fika kwamba hoja ya Zanzibar kutaka kuwa Dola huru na kuwepo Muungano wa Mkataba, ndio sababu kubwa ya harakati zenu za kupindisha ukweli na kutesa watu. Ni rahisi kuwadaganya watu fulani kwa muda fulani, lakini sio rahisi kuwadanganya watu wote kwa muda wote. Vipi msubiri kumkamata Ponda kwa sababu nyingine kabisa, na kisha kumtwisha mizigo ambayo hata akili zenu zinashuhudia kuwa mnasema uongo? Ni aibu kusingizia watu mashitaka ya uongo. Kama Biblia inavyofundisha kuwa usimshudie jirani yako uongo. Au kwa vile ni Muislamu, mwiko huo wa Biblia unaondoka? Maandiko mengine yanasema, na maaskari nao walikuja kwa Yesu na wakamuuliza wakisema, Mwalimu na sisi tufanye nini ili tupate kuingia Ufalme wa Mbinguni. Akawaambia, msishitaki mtu kwa uongo! Ni aibu kwa taifa, vyombo vyenye mamlaka ya kulinda na kusimamia haki za raia wake, kuona vinawalinda wachache wanaohujumu haki za wengine badala ya kuwasaidia wengi wanaohujumiwa. Hoja ya Sheikh Ponda, sio raia wa nchi hii, tayari Idara ya Uhamiaji ilishabainisha wazi kuwa ni raia halali wa nchi hii. Hata hivyo hakuna Mtanzania ambaye ataweza kuonyesha au kuthibisha kwamba babu yake wa kwanza kabisa katika ukoo, au kabila lake kuwa ni Mtanzania. Tukianza kutafuta raia halali kabisa tokea kuumbwa Adam na Hawa hadi sisi, hata DPP atakuwa sio raia halali wa Tanzania. Na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamini Mkapa pia sio Raia wa asili wa Tanzania, kwani Wamakuwa wote Asili yao ni Msumbiji (Mozambiki) mikoa mitatu yote ya kusini mwa Tanzania itakuwa si mali wala ardhi ya Tanzania. Mimi ni Mmakuwa, babu zangu walitokea Msumbiji, baba au niseme wazazi wangu wote wamezaliwa mkoa wa Mtwara, tokea kuzaliwa wazazi wangu hadi watoto wao wote hawajawahi kwenda Msumbiji na hawana hakika kama kuna ndugu yao huko Msumbiji. Au ndio kusema wa Lindi, Mtwara na Ruvuma sio Watanzania? Hoja anazobebeshwa Sheikh Ponda zote ni batili. Chanzo cha kukamatwa kwake ni kutetea kutouzwa kiwanja cha Markaz ya Kiislamu Chang’ombe. Kisheria ni shauri hili lililopaswa kushughulikiwa na Mahakama ya Ardhi. Tangu lini kesi ya ardhi ikawa haina dhamana? Ni vema wahusika waone aibu kuendelea kumshikilia Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake, kwa tuhuma za Zanzibar au al Shabaab. Hizo ni agenda za siri za kuwatia hatiani. Leo tuko duniani, lakini tuelewe sote tutarudi kwa Allah (S.W.T) aliye Hakimu mwaadilifu, Asiyeonea, kudhulumu, wala kusingizia watu makosa wasiyoyatenda. Ni mimi Msomaji wa

14

Makala

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Tatizo ni Dr. Kawambwa au Mfumo wa Ufisadi?
Na Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)
haitoshi kukidhi mahitaji ya chini ya maisha, na serikali imekuwa ikiwapiga dana dana na kuwaambia haina pesa! Walimu wameendelea kuwapo makazini lakini hawana furaha kwa vile wanaamini kwamba nchi hii ni tajiri sana, sasa inakuwaje serikali ishindwe kuwapa mishahara mizuri! Madaktari nao wameshagoma mara nyingi wakidai mishahara ni midogo. Lakini pamoja na kazi ngumu za madaktari na umuhimu wa kazi zao bado serikali inasema haina pesa! Serikali yetu siku zote haina pesa lakini kila ukifungua magazeti asilimia themanini ya habari za mazeti yetu ni kashfa mbali mbali kuhusu ufisadi wa aidha pesa za umma au rasimali zetu, na ufisadi huu unaofanywa na viongozi mbali mbali wa umma! Sasa kama serikali ni masikini, huo utajiri wa kutisha unaofisadiwa na baadhi ya viongozi unatoka wapi! Tanzania ina dhahabu nyingi sana, pamoja na kwamba murahaba wa dhahabu ni asilimia thelathini (30%), lakini cha kushangaza tunapata murahaba wa asilimia tatu (3%) tu! Ni kwa nini hiyo asilimia ishirini na saba (27%) isitumike kuwalipa walimu mishahara mizuri ili watoe elimu bora kwa wanafunzi wetu! Au ni kwa nini asilimia hiyo ishirini na saba isitumike kunua vifaa vya maabara kwenye shule zetu za kata ili wanafunzi wapate elimu bora kama wenzao wanaosoma shule za akademi! Tumeshuhudia wajumbe wa Bodi za Wakurugenzi wa mashirika mbalimbali nchini wakilipana mamilioni ya shilingi kama posho za vikao! Je, hawa waheshimiwa wanakutana mara ngapi kwa mwezi kama siyo kwa wiki!? Je, wajumbe hawa wangelipana hata shilingi laki moja kila mtu na pesa nyingine inayobaki wakalipwa walimu kungekuwa na ubaya gani!? Je, kwenye wajumbe hawa wa bodi hizi kuna hata mmoja ambaye mtoto wake anasoma shule ya kata? Nimesoma taarifa moja hivi karibuni inayosema Tanzania inapoteza kila mwaka tani 15 za dhahabu inayochimbwa hapa nchini! Sasa hebu tuangalie tani moja ya dhahabu ni gramu 1,000,000 na kila gramu moja ni shilling laki moja (Tsh. 100,000), hivyo tani 15 za dhahabu ni sawa na shilingi tirilioni moja na nusu! Je, pesa hizi hazingetosha kuwalipa walimu mishahara minono wakajituma kufa na kupona? Utajiri wote huu wa nchi wanafaidi watu wachache sana! Haya hao twiga walipelekwa Qatar zimepatikana billion ngapi na pesa hizo zipo wapi?

M AT O K E O y a k i d a t o cha nne yametangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo vya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa, matokeo hayo yapokelewa kwa hoja na sababu mbali mbali kwa vile idadi ya wanafunzi waliopata divisheni zero ni asilimia sitini ambayo ni kubwa ukilinganisha na miaka yote ya nyuma! Wa s h i k a d a u w e n g i wamechangia mawazo yao na kila aliyechangia amekuwa na mtizamo wake: wengine wamesema Wizara ya Elimu ihamishiwe Ofisi ya Rais; wengine wamesema walimu ni watoro kwa vile hawalipwi vizuri; wengine wamesema walimu hawahusishwi na utaratibu wa kupangwa mitaala; wengine wamesema mitaala ni mibovu; na wengine wamesema Waziri na uongozi wake wote wa juu wajiuzulu! Na mimi kama mdau wa elimu nitakuwa sijawatendea Watanzania wenzangu haki kama mjadala huu utapita bila ya kuchangia maoni yangu. Mimi nina mtizamo tofauti kidogo na wadau wenzangu ambao wamechangia katika tatizo hili la kufeli mitihani kwa wanafunzi wa kidato cha nne: Napenda nianzie mbali na nichambue kila sababu ili tuweze kujua kwa nini tumepata matokeo mabaya; nawaombeni muangalie suala zima la maisha ya kila siku jinsi tunavyoishi hapa nchini, tunaishi katika matabaka: tabaka la watawala na watawaliwa; tabaka la matajiri na masikini; na katika matabaka haya mawili makubwa ni kwamba kila tabaka lina mfumo wake wa elimu kuanzia ngazi ya chekechea hadi kidato cha nne; watawala na matajiri wapo katika tabaka moja; na tabaka lingine ni lile la watawaliwa na masikini nao hawa wapo kwenye tabaka lao, lakini pamoja na kwamba matabaka haya yana mifumo tofauti kuanzia chekechea hadi kidato cha nne, lakini wanafanya mtihani mmoja bila ya kujali kwamba umesomea kwenye mfumo gani! Watoto wa watawala na matajiri wanasoma kwenye shule maalumu ambazo hujulikana kama akademi kuanzia chekechea hadi kidato cha nne, ni shule ambazo zina walimu wazuri wanaojituma kwa vile wanalipwa vizuri na pia wanajitahidi sana kuwafundisha vizuri watoto wa watawala na matajiri ili waendelee kulipwa vizuri. Watoto wa watawaliwa na masikini wanasoma shule za serikali na shule za kata ambazo

Dr. Shukuru Kawambwa.
kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne kuna walimu wawili wote ni wa masomo ya Arts lakini shule hiyo ya kata ina masomo ya Arts na sayansi! Na kutokana na hali halisi walimu hawa wawili muda mwingi huwa hawaingii darasani kwa vile wao ni walimu wa Arts wakati kuna madarasa ya sayansi, hivyo wanachokifanya ni kuwaagiza wanafunzi wajisomee wenyewe, na wakifika kidato cha nne wanafanya mtihani mmoja na wanafunzi wa tabaka la watawala na matajiri ambao shule zao zina walimu wazuri sana, pia wanasoma masomo ya ziada (tuition), wanakula vizuri hivyo hata akili inafanya kazi vizuri, majumbani kwao wanajisomea pia kwa kutumia umeme; mwanafunzi wa shule ya kata pamoja na kwamba akiwa shuleni hafundishwi bali anaambiwa ajisomee na ana njaa, lakini pia akirudi nyumbani hawezi hata kujisomea kwa vile hata umeme hakuna, na wakati mwingine hata kibatari kinakosa mafuta ya taa! Sasa tukirudi kwenye matokeo tunakuta kwamba wanafunzi wengi waliofeli ni wale wa shule za kata na zile shule za serikali ambazo wanasoma watoto wa watawaliwa na masikini. Wajibu wa kutoa elimu kwa raia ni wajibu wa kila serikali, sasa inapofikia mahali serikali inatoa elimu kwa upendeleo wa matabaka, serikali hiyo inajenga taifa la namna gani? Serikali inajenga taifa la wajinga na werevu! Mwanafunzi aliyesoma shule ya kata na kufeli ana makosa gani? Kwa vile amesoma shule ya kata lakini amefanya mtihani wa shule za akademia? Sasa hapo ni nani alaumiwe, alaumiwe mwanafunzi au serikali iliyomnyima walimu wa kumfunsha? Kuanzishwa kwa shule za kata hapa nchini ni utaratibu

Dr. Joyce Ndalichako.
mzuri wa kumuwezesha kila Mtanzania kupata elimu ya sekondari, lakini serikali imeshindwa kuzipatia shule hizi walimu wa kutosha na wenye sifa za kufundisha, na kwa mtizamo wangu, hili tatizo limesababishwa na mfumo mbaya wa utawala hapa nchini. Kwa miaka mingi tumekuwa hatuna utaratibu mzuri wa kugawana pato la taifa (poor distribution of national wealth). Ninaposema mgawanyo mbovu wa pato la taifa, sina maana kwamba serikali ichukuwe pesa hazina imgawie kila Mtanzania, hapana, bali nina maana kwamba mapato ya taifa hayaelekezwi kwenye shughuli mbali mbali zenye maslahi kwa taifa (kwa mfano mishahara ya wafanyikazi mbali mbali wa umma, vifaa vya mashuleni na mahospitalini), bali pato hili limekuwa likitumiwa katika mambo ambayo hayana tija kwa taifa, na hata wakati mwingine kutumiwa kwa manufaa binafsi ya watu wachache sana. Nchi yetu ni tajiri tena tajiri sana, lakini utajiri wa nchi yetu wanafaidi watu wachache sana, na hawa ndio wanaotusababishia matokeo yote haya ya wanafunzi kufeli na mengine mengi tu! Ta n g u s h u l e z a k a t a zimeanzishwa zimekuwa katika tatizo la kutokuwa na walimu wa kutosha na hata wasiokuwa na sifa, kutokuwa na vyumba vya maabara na vifaa vya maabara, na vitabu vya kufundishia, lakini ukiangalia siyo kwamba hapa nchini hakuna walimu wa kutosha na wenye sifa, hapana, tatizo ni pesa, pesa za kuwalipa walimu mishahara mizuri inayofanana na ile ya wabunge, pesa ya kununua vifaa vya maabara, pesa ya kununua vitabu vya kufundishia! Tatizo hili la pesa ni tatizo sugu kwani umoja wa walimu Tanzania wamekuwa wakifanya migomo kila mwaka ya kudai kwamba mishahara ni midogo

Je, pesa hizo zisingeweza kuwalipa walimu mishahara minono wakajituma kikamilifu kama wanavyojituma wenzao wa shule za akademi!? Wa c h a n g i a j i w e n g i wanaangalia tu matokeo ya mitihani lakini hawaangalii chanzo cha kusababisha matokeo hayo; tukianza kumsakama Dr. Kawambwa na uongozi wake wote wa juu kwamba wajiuzulu kwa vile ni chanzo cha tatizo la kufeli kwa wanafunzi tutakuwa hatujatatua tatizo, kwa vile hata wakija akina Profesa Kawambwa wengine hawabadilisha matokeo ya kufeli kwa wanafunzi kwa vile tatizo halipo wizarani! Kama nchi imeshindwa kudhibiti rasimali zake kwa manufaa ya raia wake, kwa kuhakikisha kwamba walimu wanalipwa mishara minono na pia kuhakikisha kwamba shule zote za serikali na zile za akademi zinakuwa na viwango sawa na mfumo mmoja wa elimu ili wanafunzi wapimwe kiuwezo katika mazingira sawa, lakini wanafunzi wamegawanywa katika matabaka mawili: tabaka la wanaopendelewa na kufaidi rasimali za taifa; na tabaka lingine ni lile la wanafunzi wa masikini waliotelekezwa kama vile siyo raia wa nchi hii! Sasa mwanafunzi wa shule ya kata ambaye ametelekezwa na serikali akipata divisheni zero unamlaumu waziri!? Ulitaka waziri atoe pesa yake mfukoni awalipe walimu mishahara minono? Au ulitaka waziri atoe mshahara wake azinunulie shule za kata zote Tanzania nzima vifaa vya maabara? Au ulitaka waziri na uongozi wake wote wa juu waende wakafundishe huko shule za kata ili watoto wafaulu mitihani? Tatizo letu hapa ni mfumo mbovu wa ugawanyaji wa pato la taifa, mfumo ambao umekumbatia hulka za kifisadi, hivyo kumlaumu aliyetangaza matokeo ya mtihani tutakuwa hatupo sahihi kabisa! Tatizo ni mfumo wa ufisadi! Mfumo unaojali wachache na kugandamiza waliowengi. Waziri ni mtu mdogo sana kutatua au kubadilisha mfumo wa nchi, mfumo wa nchi haubadilishwi na waziri, labda kama tunafanya siasa tu ambazo hazina tija kwa taifa. Tunachotakiwa hapa ni kumfanya kila mmoja wetu aelewa kwamba rasimali zote zilizopo hapa nchini ni mali ya Watanzania wote, na kila Mtanzania ana haki sawa na mwingine kuhusu mgawanyo wa rasimali hizo. Tukifanikiwa kulitekeleza hilo, tutakuwa tumetatua tatizo la kuzorota kwa elimu na matatizo mengine mengi yanayozikabili wizara zetu zote na yanayoikabili nchi hii kwa ujumla.

15

TANGAZO

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO – 2013/2014
Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

• • •
1.

KIRINJIKO ISLAMIC SECONDARY SCHOOL NYASAKA ISLAMIC SECONDARY SCHOOL UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOO L

– – –

SAME – KILIMANJARO MWANZA DAR ES SALAAM

Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu kwa gharama nafuu. Shule hizi ni za mchanganyiko wa wavulana na wasichana na zinapokea wanafunzi wa bweni tu. 2. Masomo yanayofundishwa ni Islamic knowledge, ‘Combinations’ za SAYANSI, ARTS, BIASHARA pamoja na COMPYUTA. 3. Muombaji awe na ‘Crediti’ 3 au zaidi na angalau ‘D’ ya Elimu ya Dini ya Kiislamu katika matokeo ya kidato cha nne. Ikiwa ana ‘F’ au hakufanya Elimu ya Dini ya Kiislamu, basi awe tayari kusoma programu maalum ya Maarifa ya Uislamu atakapokuwa kidato cha tano. 4. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 18 /05 /2013 5. Fomu za Maombi zinapatikana kwa gharama ya shilingi 10,000/= katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini. • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • • 6. Arusha Kilimanjaro Tanga Mwanza Musoma Kagera Shinyanga Ofisi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610 Moshi: Msikiti wa Riadha – 0654 723 418 Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075 Uongofu Bookshop: - 0784 982525/ Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685 Ofisi ya Islamic Education Panel - Mwanza - Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Duka la Kansolele -Stendi ya zamani sokoni - 0714587193 Bukoba: Alhuda Café Kwa mzee Kinobe karibu na ofisi za TRA. - 0688 479 667 Msiikiti wa Majengo-0718866869 Kahama ofisi ya AN –NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930 Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin – 0655144474 Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380 Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086 Ofisis ya Islamic Ed. Panel – karibu Nuru snack Hotel – 0714285465 Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 Msikiti wa mwanga Kigoma: 0753 355224 Kibondo – Islamic Nursery School: 0784 442860 Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Amana Islamic S.S 0786 729 973 Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU – 0715 681701/0716791113 Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole – 0713 200209 Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Madrastun – Najah: 0714 522 122 Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Madrasatul – Fallah: 0777125074Ofisi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu – 0653705627

Dar es Salaam Morogoro Dodoma Singida Manyara Kigoma Lindi Mtwara Songea Mbeya Rukwa Tabora Iringa Pemba Unguja Mafia -

-

Pia Fomu zinapatikana kwenye Tovuti: www.ipctz.org. Ikumbukwe kuwa watakaopata fomu kupitia tovuti (download) watatakiwa kuzilipia wakati wa kuzirejesha. USIKOSE NAFASI HII ADHIMU – WAHI KUCHUKUA FOMU SASA! Wabillah Tawfiiq MKURUGENZI

16

AN-NUUR
16

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

RABBIUL THAN 1434, IJUMAA FEBRUARI 22-28, 2013

AN-NUUR

Na Bakari Mwakangwale

MASHAHIDI upande wa Mashitaka, katika kesi inayomkabili Sheikh Ponda Issa Ponda, na wenzake wamejikuta wakijichanganya katika kutoa ushahidi wa watuhumiwa hao. Kesi hiyo ambayo wiki hii imesikilizwa kwa siku tatu mfululizo, mbele ya Hakim Mkazi Kisutu, Bi. Victoria Nongwa, Jijini Dar es Salaam, ilishuhudia mashahidi ambao ni maafisa wa Polisi wapelelezi wakibabaika kujibu maswali ya jopo la Mawakili wa washitakiwa. Akitoa ushahidi wake kwa upande wa mashitaka Mahakamani hapo, shahidi namba nane, Sajenti Mkombozi (46), wa kituo cha Polisi, Mbagala, alidai kuwa watuhumiwa walikiri kosa la kuchukua vitu vilivyopo katika eneo la kiwanja cha Markazi. Hata hivyo alipoulizwa n a Wa k i l i N a s s o r o , walivipeleka wapi vitu hivyo, Afande Mkombozi alisema kwamba walivitumia kujengea Msikiti katika kiwanja hicho palepale. Sajenti Mkombozi alifafanua kuwa kufanya hivyo ni wizi, kwa maana wizi ni kuhamisha kitu kutoka sehemu kilipokuwa na kukipeleka sehemu nyingine kwa matumizi binafsi. Wa k i l i N a s s o r o akimuhoji shahidi huyo kwa kutumia maelezo ya Ustadh Mukadamu aliyoyatoa akiwa kituo cha Polisi Kikuu cha Polisi (Central Police Station) baada ya kukamatwa, kwamba nini haswa kosa la Mukadam, afande alisema, anatuhumiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai (katika kiwanja hicho). Alipoulizwa kama anamfahamu mmiliki wa eneo la kiwanja hicho, afande huyo alijibu kuwa katika upelelezi wake alibaini kuwa mmiliki wa eneo hilo anaitwa Hafidhi.

Polisi wajichanganya kesi ya Sheikh Ponda

SHEIKH Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na Ustadh Swaleh Mukadam katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake, Sajenti yake kufuatia maswali ya ardhi nyingine iliyopo Juma, kutoka kituo cha Wakili Nassoro, alidai Kisarawe. Lakini pia shahidi Polisi Chang’ombe, akitoa kuwa mmiliki wa eneo la ushahidi wake Mahakamani kiwanja cha Markazi ni mtu huyo alifafanua kuwa h a p o , a k i o n g o z w a n a anayejulikana kwa jina la alibaini kwamba wapo Wakili wa Serikali, Tumaini Bw. Suleimani, na kusisitiza wanaodai kuwa kiwanja Kweka, alisema kuwa kesi kuwa Hafidhi, alikuwa ni hicho ni cha Waislamu na inayowakabili Ponda na mtoa taarifa aliyekuwa Bakwata hawana uwezo wenzake, ilifunguliwa a k i t u m w a n a m w e n y e wa kukigawa, kukiuza au na mlalamikaji Hafidhi, kiwanja (Suleiman). kukifanyia mabadiliko N a a l i p o t a k i w a yoyote. ambaye alilalamika kuwa Kwa maelezo hayo, ameingiliwa kwa jinai kuthibitisha na Wakili wa upande wa utetezi kwamba Wakili Nassoro, alimuuliza katika kiwanja chake. Sajenti Juma, alisema, ni karatasi au nyaraka zipi kuwa kwa maana hiyo w a l i m t a k a H a f i d h i , a m b a y o i n a y o o n y e s h a hapo kuna hoja mbiIi awasilishe nyaraka za uhalali wa Suleimani, kuwa zinazokinzana, baina ya kuthibitisha kuwa kiwanja mmiliki wa eneo hilo, alidai pande mbili kuhusu ardhi kile ni mali yake, jambo kuwa hakumbuki. hiyo, Afande, Juma alikiri Akijibu swali la wakili kuwa pande hizo zipo. ambalo alifanya hivyo “Unafikiri Polisi na n a k u j i r i d h i s h a k u w a Nassoro, Sajent Juma, kiwanja ni mali yake alisema kwamba aligundua Mahakama ya Hakimu (Hafidhi), sambamba na katika upelezi wake wa kadhia Mkazi Kisutu wanamamlaka kuthibitishiwa na Afisa ya kiwanja hicho, kuwa kwa mujibu wa sheria Ardhi wa Halmashauri ya Bakwata, hawakuliuza eneo ya kutatua mgogoro wa hilo, bali wamebadilishana ardhi”? Alihoji Wakili Manispaa ya Temeke. Hata hivyo katika majibu k w a k u p e w a e n e o l a Nassoro, ambapo Sajenti

Juma, alijibu ‘Hapana’ Na hata alipoulizwa ni vyombo gani vinavyoshughulikia migogoro ya ardhi, Sajenti Juma, alijibu kuwa ni Mahakama ya Ardhi. “Je katika Mahakama hii (Kisutu), inaweza kusema kuwa ni nani mmiliki halali wa eneo lenye mgogoro? Shahidi huyo, alipiga kimya! Wa k i l i N a s s o r o alimuuliza Sajent Juma baada ya kusoma maelezo (waraka) ya Sheikh Ponda, kwamba maelezo hayo yanahusika vipi na kesi inayo wakabili wateja wake, ambapo Afisa huyo wa Polisi mpelelezi, alijibu kuwa ni kushawishi watu kuingia sehemu kwa jinai, hiyo alidai ni kwa mujibu wa taarifa za kiitelejensia. “Je, katika maelezo ya Sheikh Ponda, uliyoyasoma mbele ya Mahakama, aliyoyatoa Polisi, kuna sehemu inayoonyesha alieleza alihamasisha watu kuvamia eneo hilo?” Alihoji wakili Nassoro, na Mpelelezi huyo wa Jeshi la Polisi, alijibu “Hapo, hamana”. Katika hatua nyingine Mahakamani hapo, Wakili wa upande wa utetezi Nassoro, alidai kuwa karatasi ya maelezo ya mahojiano kati ya Sheikh Mukadam na Polisi, ambayo, ilizua mabishano ya kisheria, katika muda wa kumhoji mtuhumiwa, kisheria, ilighushiwa. Wakili Juma alisema katika karatasi hiyo, awali (asubuhi ya Jumatatu na Jumanne) ilikuwa imeandikwa muda tu yaani 11:15, lakini haikuainisha ni jioni au asubuhi, lakini muda huu (saa saba, mchana, Jumanne) imeongezewa hrs. “Mheshiwa Hakimu, kuna kosa limefanywa na wenzetu, kulikuwa na maelezo ya muda iliandikiwa 11:15, haikuwa haifahamiki ni jioni au asubuhi, lakini sasa tumerudi kuna nyongeza ya hrs, mwanzo hayakuwepo sasa hivi yapo, wenzetu wamefoji.” Alisema wakili Juma.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful