www.annuurpapers.co.

tz

Umoja wa Makanisa wamsukia kitanzi Kikwete
Kweli Mkapa ana haki ...Uk. 8
‘Wamshitaki’ kwa Waziri Emmanuel Nchimbi Wasema anaendesha ugaidi wa Kiislamu Atakiwa ajiuzulu na Timu yake yote ya Jihad

Katika Alama na Vitakatifu vya Allah ambavyo Ameonya visivunjiwe heshima, bali vitukuzwe, vingi sana vinapatikana Makka na Madina (Qur’ani, 5:2, 22:30). Kwa nini basi waislamu tusiitukuze sana Hijja! Bila shaka Allah Atafurahi na kuridhika sana na sisi, na makafiri watachukiwasana. Jiandikishe leo Ahlu Sunna wal Jamaa. Gharama zote ni Dola 4,300. Tafadhaliwasiliana n a s i i f u a t a v y o : Ta n z a n i a B a r a : 0717224437; 0777462022;Unguja: ISSN 0856 - 3861 Na. 1066 JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA -APRILI 12-18, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= 0777458075;Pemba: 0776357117.

Sauti ya Waislamu

(11) WAISLAMU TUITUKUZE HIJJA!

Zanzibar tusikubali kufanywa makuchi
T U S I P O K U WA makini, punde tu Zanzibar itakuwa maarufu kama ilivyo Afghanstan, Iraq na Syria! Hapo ‘wabaya’ wetu watapata sababu za kutosha za kuifanya

Wanataka tuwe maarufu kama Afghanistan Walete majeshi, misaada, kutufanya koloni Asili, utamaduni wa Mzanzibari utoweke

Kesi ya Masheikh Uamsho Ni sarakasi, danadana tupu
Na Alghaithiyyah Zanzibar

Zanzibar kuwa Mkoa au hata Wilaya. Utamaduni na asili ya Zanzibar ndo itapotea kabisa. Tusikubali kufanywa makuchi tukapiganishwa sie kwa sie. (Soma Uk. 6)

bado hawajafikishwa mahakamani. Habari kutoka katika mji WA L I O C H O M A huo mdogo katika Mkoa wa M s i k i t i Tu n d u m a ,

Waliochoma Msikiti Tunduma hawajafikishwa mahakamani
Na Bakari Mwakangwale

RAIS Mstaafu Benjamin William Mkapa.

Mahakama Kuu Vuga yasita kusikiliza Yasubiri kauli ya Mahakama ya Rufaa Kanuni ya haki iliyocheleweshwa…. Haifanyi kazi, au haiwahusu Masheikh?

VIONGOZI wa Kiislamu Zanzibar walio rumande, watazidi kukaa humo huku danadana na sarakasi za kisheria mahakamani zikiendelea. Mbeya zinafahamisha kuwa Wataendelea kuwepo humo Jeshi la Polisi, linaendelea baada ya haki yao ya dhamana kuwashikilia watuhumiwa 45 Inaendelea Uk. 10 Inaendelea Uk. 4

SHEIKH Farid Had.

2
www.annuurpapers.co.tz

Tahariri/Habari
Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013
Wanafanya yale yaliyo na masilahi na Kanisa badala ya Uislamu. Na kwa Serikali ni hivyo hivyo. Wanawasifia na kuwakumbatia walio tayari kuwatoa muhanga Waislamu na masilahi yao, ilimuradi wao wapendeze mbele ya Serikali. Sasa Mufti wa Bakwata Simba anaposema leo kuwa anaunda Tume ya Masheikh itakayokutana na Maaskofu ili kuondoa tofauti zilizopo, tofauti zipi. Askofu gani katika nchi hii anaweza kupokea maelekezo kutoka kwa Sheikh! Maaskofu walisema hawataki kuiona East Africa Muslim Welfare Society (EAMWS), ikapigwa marufuku na Nyerere. Wakasema hawataki kuona OIC wala Mahakama ya Kadhi. Imekuwa kama walivyotaka. Kwa upande mwingine, mwaka jana Mufti Simba alitoa kauli juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi pamoja na NECTA. Na kuhusu Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) akasema kuwa Baraza hilo halionyeshi sura ya kitaifa kwa sababu toka limeundwa limesheheni Wakristo watupu katika nafasi zote muhimu. Akataka liundwe upya. Labda Mufti Simba atuambie, toka ametoa kauli hizo, lipi limetekelezwa kama yanavyotekelezwa yale ya Maaskofu? Kama hakuna, ni kuwa wao Masheikh wakisema wanajisemea tu. Hakuna anayejali kuwa kuna mtu anasema na anasema nini! Sasa katika hali kama hiyo unatuma Tume Serikalini au kwa Maaskofu ukitarajia kupata nini? Sisi tunadhani kama ni kukutana na Maaskofu, labda hiyo Tume ya Mufti Simba wa Bakwata wakawaulize wenzao wa Kikristo, inakuwaje wao Maaskofu wakitaka jambo wanasikilizwa na Serikali, lakini wao Masheikh hawasikilizwi wala madai yao kutekelezwa? Kwa upande mwingine, h a t u o n i h i y o Ti m u y a Masheikh wa Mufti wa Bakwata itapata wapi uso na ujasiri wa kukutana na Waislamu kuwaelimisha hicho kinachoitwa dhamira nzuri ya Mufti Simba maana kama ni dhamira nzuri angeionyesha kwa kusimama na Waislamu wenzake katika kupigania Mahkama ya Kadhi.

AN-NUUR

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786
MAONI YETU

AKIONGEA na waandishi wa habari mapema wiki hii, Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi, amesema haoni sababu ya kuwepo mazungumzo baina ya viongozi wa Kiislamu na Kikristo kuzungumzia suala la kuchinja. Mengi amesema, kuliko kupoteza muda kuzungumzia jambo hilo, ni vema muda huo ukatumika kufanya mambo ya maana na ya maendeleo. Reginald Mengi ameyasema hayo baada ya kuonyesha kuwa haoni kuwa kuna sababu ya kuwepo mgogoro baina ya Waislamu na Wakristo kutokana na suala la kuchinja. Akisisitiza kuwa hakuna tatizo la msingi akasema kuwa kwa hakika itakuwa ni jambo la aibu kama Waislamu na Wakristo watajeruhiana na kutoana roho, kisa nini, kugombea nani achinje. “Mimi ni Mkristo, hoja yangu haiingilii undani wa imani za watu, lakini kwa utaratibu tuliorithishwa na wazee wetu kwa kuwa hadi leo haujatuathiri, tunaishi kwa amani na umoja, sioni sababu ya kuufuta, Waislamu waendelee kuchinja.” Alisema Mengi. Kwa upande mwingine imeripotiwa kuwa Mufti wa Bakwata anaunda Tume ya kukutana na viongozi wa Kikristo ili kuzungumza na kuondoa tofauti zinazoendelea, moja ikiwa ni hilo la kuchinja. Mufti Simba akasema kuwa anawaomba Maaskofu wawapokee Masheikh wake na kuwapa ushirikiano. Ni ukweli kuwa kama suala la kuchinja lingekuwa na mushkeli kwa upande w a Wa k r i s t o k i i m a n i , lisingesubiri mpaka wakati huu ndio lilipuke. Na msingi wenyewe ni kuwa kiimani, kimafundisho ya Kikristo na kwa mafundisho ya Biblia, Wakristo hawaharibu imani zao wala Ukristo wao kwa kula nyama iliyochinjwa na Waislamu. Ndio maana Reginald Mengi anasema kuwa “kwa utaratibu

Mengi kapatia

tuliorithishwa na wazee wetu …hadi leo haujatuathiri, tunaishi kwa amani na umoja”, na kwa hiyo akasema, haoni “sababu ya kuufuta, Waislamu waendelee kuchinja.” Sisi tunasema swadakta. Amesema kweli Reginald Mengi. Pamoja na elimu kidogo ya Biblia tuliyo nayo, lakini tuna uzoefu wa kutosha juu ya Wakristo wa nchi hii walivyo wakali na madhubuti katika kupigania haki zao za kidini pamoja na masilahi y a o k a m a Wa k r i s t o n a wananchi. Japo haliwadhuru kiimani, lakini tunaona jinsi walivyosimama imara kuzuiya serikali isijiunge na OIC. Tunaona pia jinsi Wakristo walivyokuja juu kuzuiya kurejeshwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini mpaka serikali inajikuta haiwezi kuwa na maamuzi yake yenyewe ila ipime kwanza joto la Wakristo. Hawa ndio Wakristo wa nchi hii. Kama jambo hili lingekuwa na mushkeli katika imani ya Kikristo, ni wazi kuwa tusingefika hapa tulipo na utaratibu huu ambapo ni Waislamu wanaochinja na kitoweo kuuzwa katika maduka ya nyama. Wala isingewezekana kwa Wakristo wanaojali ujirani, kumwita Muislamu awachinjie kuku! Sasa ukizingatia hayo unaweza kusema kuwa wanaofanya jambo hili liwe suala la kuleta mgogoro, wana agenda yao ambayo inapaswa waulizwe. Kama alivyosema tena Mengi, hili si suala la kuwakutanisha Masheikh na Mapadiri kwa sababu hakuna msigano wala utata wa kiimani na mafundisho. Kinachoweza kufanyika ni namna mbili. Moja ni kwa viongozi wa kanisa kuwaelimisha waumini wao juu ya suala hilo. Lakini pili, kama wapo baadhi ya viongozi wa makanisa wanaolichochea na kuwachochea waumini wao kuleta fujo, basi serikali ishughulike nao. Iwaite, kama kuna vifungu vipya vya Biblia vimekuja juu ya uchinjaji, waonyeshe. La sivyo serikali iwe na ujasiri wa kuwaambia waache fujo. Kwa watu walioamua kuleta fujo, watu walioamua

Kundecha apangua kauli ya Mzee Mkapa
Na Bakari Mwakangwale AMIR wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), Alhaj Mussa Yusuph Kundecha, amesema udini nchini Tanzania ni suala kongwe kabla na baada ya Uhuru. Amir Kundecha ameyasema hayo mapema wiki hii akiongea na An nuur, kufuatia kauli ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa, aliyejitapa kwamba, katika utawala wake aliongoza Taifa bila ya ubaguzi wa kidini. Alhaj Kundecha, alisema unapozungumzia suala la udini humu nchini muhanga mkubwa wa suala hilo ni Muislamu, kwani kihistoria udini uliletwa na Wakoloni na baada ya hapo umekuwa ukiendelezwa na marais wote katika Tanganyika/Tanzania huru. “Suala la udini hapa Tanzania ni kongwe, limeanza toka mkoloni kwani wakati anakuja upande mmoja alikuwa mueneza dini ya Kikristo na upande mwingine akiwa na mkataba wa kimataifa wa kupewa eneo hili kulitawala, kupitia mkataba wa Berlin.” Alifafanua Amiri Kundecha. Amir Kundecha alisema kuwa alichoongea Mzee Mkapa ni maneno ya kisiasa, yenye lengo la kuuhadaa umma, lakini akamtaka Rais huyo Mstaafu (Mkapa) kutambua kuwa uongo wowote ule bila kujali nani amesema, sio msingi wa kuondoa tatizo au shida iliyopo, bali unaikawiza tu, lakini kinyume chake ni kulikuza jambo na kuwa kubwa zaidi. Alibainisha kwamba, katika kumbukumbu zake, hakumbuki kama kuna utawala ambao Waislamu hawajalalamikia dhulma za udini dhidi yao na kwa bahati mbaya sana alidai, tawala zote zimekuwa zikiwapuuza, badala ya kufanyia kazi madai hayo. Alisema, tofauti ya awamu hizo ni uzito na madhila ya udini wenyewe kwa Waislamu katika kila awamu kuwa yanatofautiana na kwamba alidai hakuna Rais, aliyeonyesha dhamira ya dhati ya kuondosha udini uliopo nchini. Alisema, Mkapa (Benjamin), anayesema leo utawala wake haukuwa na udini yeye ni shahidi namba moja wa malalamiko ya Waislamu, pale Diamond Jubilee, aliposomewa risala kutoka Umoja wa Waislamu wote nchini. “Tunasema uongo hauondoi shida bwana, bali uongo hukuza shida tu, jambo hili analijua. Tunasema endapo tukiwa wakweli, itasaidia sana kushughulikia matatizo kwa

kutumia suala la kuchinja kuwafarakanisha Waislamu na Wakristo katika nchi hii, si watu wa kutulizwa na Timu ya Masheikh wa Mufti Simba. Katika suala la Mahakama ya Kadhi, Waislamu waliunda Timu ya Masheikh (Bakwata ikiwemo) ambao wangekutana na Serikali kuzungumzia suala hilo mpaka kupata ufumbuzi. Wakati mchakato ukiendelea, ghafla Mufti akawaacha Waislamu akaungana na Serikali kwenda kutangaza ‘Kadhi Mkuu wa Bakwata’. Serikali ikapumua. Sasa kila anayehoji Mahakama ya Kadhi anaonekana kama analeta ukorofi kwa sababu Kadhi ashapatikana. Maaskofu nao wamefurahi kwa sababu hatua ya Mufti Simba kutangaza Kadhi Mkuu na Makadhi wa Mikoa, imevunja nguvu ya Waislamu katika kupigania kuwepo Mahakama ya Kadhi nchini. Kwa maneno mengine, alichofanya Mufti Simba ndicho walichotaka Maaskofu. Kwamba iwepo Mahakama ya Kadhi kiini macho. Ambayo haipo kisheria, haitambuliki na haina maana yoyote. Basi ukisikia Maaskofu wanawasifia baadhi ya Masheikh, hasa wa Bakwata, ni kwa sababu hii.

wakati na kwa namna nzuri tu, tukiwa waongo tutakawiza ukweli kupatikana.” “Lakini pia shida itakuwa kubwa kwa sababu kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele athari ya jambo hilo linazidi kutanuka kama inavyoonekana hivi sasa.” Alisema Alhaj Kundecha. Akiuzungumzia utawala wa Mzee Mkapa (1995-2005), Amir Kundecha, alisema Waislamu walikuwa wahanga katika sehemu mbalimbali, kuanzia katika ajira, elimu utawala wake pia umefelisha Waislamu, walikuwa wahanga katika uchumi, wahanga katika utawala. Amir Kundecha, alisema ikija kutokea ukapatikana utawala wa haki na sheria kutokana na kuwa dhulma huwa haidumu milele, sheria ikachukua mkondo wake, hata yeye (Mkapa) hatanusurika. Alhaj Kundecha, alitolea mfano ile ripoti ya Waislamu aliyoipokea, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, wakati wa utawala wake akidai kupatiwa ushahidi wa kisayansi madai ya Waislamu kisha alipelekewa ushahidi huo. Alisema, alipopelekewa ushahidi huo, badala ya kuchukua hatua, akarudi nyuma pasi ya kuchukua hatua zozote na kudai matatizo ya Waislamu ni ya kihistoria na hayatatuliki, jambo ambalo si sawa.

3

Umoja wa Makanisa wamsukia kitanzi Kikwete
Na Mwandishi Wetu
vikali na Mungu kwamba wasiivunje kamwe miiko hii yote, kwa sababu vyote hivyo vya Waislamu vinaswaliwa kwa mashetani yaani Allah na majini. Kiwango cha ugaidi kilichofikiwa dhidi ya Ukristo nchini kimelazimisha mipango madhubuti ya kuhakikisha kwamba huduma zote hizi zinatolewa na Wakristo kwa ajili ya Wakristo, ili wakiisha kutubia dhambi ya kukinywea kikombe cha mashetani kwa miaka mingi sasa wasiirudie tena, kwani Yesu yuaja.” Imesema katika kumalizia barua hiyo huku ikiwataka Wakristo wasinunue katika maduka ya Waislamu wala kula katika migahawa yao, kulala katika hoteli zao au kupanda daladala zao “kwa sababu vyote hivyo vya Waislamu vinaswaliwa kwa mashetani yaani Allah na majini.” Imekuwa vigumu kufahamu ni kwa nini Kamati hii Huru ya Umoja wa Makanisa imeamua ‘kumshitaki’ Mheshimiwa Rais Kikwete kwa Waziri wake. Hata hivyo, baadhi ya vifungu katika barua yao vinatoa dalili ni kwa nini wamefanya hivyo. Moja ya dalili hizo ni pale wanaposema kuwa Wizara yake “imetumika sana kwa ugaidi wa Kiislamu nchini, na zaidi Jeshi la Polisi, ingawa Idara ya Uhamiaji nayo imetumika kuwaingiza nchini magaidi wengi.” Wakionyesha zaidi ni kwa nini wameamua kumshitakia yeye Waziri wanasema kuwa Polisi walio chini yake wanatumika kuzima ‘Crusade’ hasa wanapoona Wa i s l a m u w a n a k i m b i a Uislamu na kujisalimisha k w a Ye s u n a h a s a “waonapo ‘Biblia ni Jibu’ wanauangamiza Uislamu kwa kutoboa siri za ushetani wa Allah na mtume wake, kutoka katika vitabu vya Kiislamu na Biblia Takatifu. (Na kwamba) Ugaidi huu wa Polisi umewatesa sana wahubiri wa Kikristo nchi nzima mpaka Zanzibar.” Kwa upande mwingine wameonyesha kuwa wamelazimika kumwandikia Waziri Nchimbi akiwa na dhamana ya usalama wa ndani ya nchi kwa sababu anaonekana kutowajibika ipasavyo kuzuiya magaidi wa Al Shabab na Al Qaida kuingia nchini. “Mheshimiwa Waziri, siyo siri kwamba wapiganaji wengi wa Kiislamu wameandaliwa nje na ndani ya nchi kwa ajili ya ugaidi dhidi ya Ukristo nchini. Hata wale waliokwenda Somalia kufunzwa na Al-Shabab na Al-Qaida jinsi ya kuangamiza makafir (Wakristo) mpaka kwa mabomu ambayo wamefundishwa hata kuyatengeneza, wamerejea nchini kwa ajili ya vita.” “Hivi sasa misikiti mingi nchini inatumika kwa mafunzo ya kivita. Ugaidi unafundishwa kwa nguvu katika vituo maalum vya Kiwalani (Jijini Dar es Salaam), Ukala katika Ziwa Victoria, Namtumbo, Ifakara, Uvinza, Morogoro, Tanga, Pemba na kwingine.” Hata hivyo, pamoja na maelezo hayo ambayo yanatoa ishara ni kwa nini mashitaka na malalamiko haya yameelekezwa k w a Wa z i r i N c h i m b i , inavyoonekana kuna sababu nyingine muhimu zaidi ambayo inajitokeza pale Kamati Huru ya Umoja wa Makanisa inapomwelekea Mheshimiwa Nchimbi ikisema: “Mheshimiwa Waziri, tunaheshimu sana uzalendo wako na umakini wako katika masuala nyeti, pamoja na hofu uliyo nayo kwa Mungu. Tunaamini kwamba…Rais akighafilika kama binadamu wengine upo wewe wa kumsaidia upesi kupunguza mizigo ili chombo kivuke maji ya hatari.” Hivi karibuni mara baada ya kutokea ile jinai mbaya ya kuuliwa Padiri Mushi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi alikuwa wa mwanzo katika viongozi wa serikali kudai kuwa lile lilikuwa tukio la kigaidi. Kwamba waliofanya mauwaji yale walikuwa magaidi. Hata hivyo, si rahisi kusema kwa uhakika iwapo ugaidi aliokuwa akizungumzia Mheshimiwa Wa z i r i D r. E m m a n u e l Nchimbi, unahusiana na huu unaozungumziwa na Kamati Huru ya Umoja wa Makanisa Tanzania.

Habari

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

WANAOJIITA Kamati Huru ya Umoja wa Makanisa nchini, wamemwandikia Waziri wa Mambo ya Ndani Mheshimiwa Dr. Emmanuel Nchimbi wakimtaka amsaidie Rais Kikwete kutanabahi kwamba anatakiwa “ajiuzulu pamoja na timu yake yote ya Jihad.” Umoja huo umetoa maelekezo hayo baada ya kumtuhumu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa anaendesha Jihad ya kuwauwa Wakristo na Ukristo. Katika barua yao kwa Mheshimiwa Waziri Nchimbi ya tarehe 31 Machi, 2013 wametahadharisha wakisema kuwa itakuwa ni maangamizi kwa wana-jihad kama wanadhani kuwa Wakristo watawageuzia shavu la kulia. “Ndugu Waziri, ni vyema ukamsaidia Rais Kikwete kusoma nyakati. Wakristo 28 milioni kuchokozwa na Waislamu 11 milioni, hatima yake inaeleweka hata kwa mjinga.” Katika barua hiyo iliyonakiliwa kwa taasisi zote za Kikristo nchini pamoja na Bakwata, Waziri Nchimbi anafahamishwa kuwa Wakristo wote kwa pamoja wanamtaka Rais Kikwete ajiuzulu. “Ndugu Waziri, unafahamu kwamba Wakristo milioni 28 wa Taifa hili kama Mwili mmoja wa Kikristo, na kama familia moja ya wana wa milki ya Mungu, wametoa Tamko kwamba Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu pamoja na timu yake yote ya jihad, kwa kuongoza nchi yetu kwa udini mahala pa utawala wa Sheria, na kuipuuza kabisa Katiba ya Nchi.” Wakifafanua waliouita udini na ujahidina wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete wamesema kuwa ni pamoja na kuwalazimisha kula nyama iliyochinjwa na Waislamu wakati “ni marufuku Wakristo kula chochote kilichoswaliwa kwa Allah na mashetani wengine. (Kwamba) Mungu anawapiga marufuku Wakristo kushirikiana na mashetani, kwamba ni marufuku kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani yaani Allah na majini.” Imesema na kufafanua barua hiyo ambayo pia

RAIS Jakaya Kikwete imenakiliwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Spika wa Bunge na taasisi za Kikristo nje ya nchi. Jambo jingine analoshutumiwa Rais Kikwete na hivyo kushitakiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Dr. Emmanuel Nchimbi, ni kuwa amepiga marufuku Redio ya Kikristo, Redio Neema, ambayo inaelezwa kuwa inafanya kazi ya kupambana na ugaidi wa Kiislamu. Umoja huo ukamtaka Waziri Nchimbi kuhakikisha kuwa Redio hiyo inafunguliwa mara moja na kwa upande mwingine kumtaka Rais Kikwete awaombe radhi Wakristo. “Mheshimiwa Waziri (Dr. Emmanuel Nchimbi), kilichoitwa “uchochezi wa kidini” ni uhanga wa Redio Neema na Askofu Mpemba, wa kuishindania Imani ya Kristo kama Mungu alivyowaagiza Wakristo katika Biblia Takatifu… Kama kweli Rais Jakaya Kikwete yuko kinyume na ugaidi huu unaoendeshwa dhidi ya Wakristo nchini, ni lazima afanye yafuatayo: Awaombe radhi Wakristo kwa kutumia dola kuukandamiza Ukristo nchini, na kutumia dola kuuimarisha ugaidi wa Kiislamu…(na pia) awaombe msamaha Wakristo kwa kufungiwa Redio Neema, eti isipinge ugaidi dhidi ya Ukristo.” Pamoja na kumshutumu Rais Kikwete, Umoja huo wa Makanisa umeushitaki pia Uislamu kwa Waziri Nchimbi kwamba unawaagiza Waislamu kuwakata shingo Wakristo na kwamba ugaidi huo ulianzishwa rasmi wakati wa Awamu ya Pili ikiongozwa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi. “Ndugu Waziri, Jihad ya kuchochea kuwakata shingo Wakristo nchini na kuteketeza makanisa, wakisimama katika maamrisho ya mungu wao Allah katika Qur’an sura 9:30, sura 47:4 (ziko aya 320 zinazochochea ugaidi), ilianza rasmi mwaka 1986 kwa udhamini wa Ali Hassan Mwinyi, kinyume cha Katiba ya Nchi na maadili ya Taifa letu.” Inasema sehemu barua hiyo. Japo Bakwata wanaonyesha kupewa nakala, bado hakuna dalili kwamba wameifanyia kazi barua hiyo na haijulikani ni kwa nini Umoja huo wa Makanisa ukaamua kuwapa nakala wakati humo ndani wamemuita Allah kuwa ni shetani. Aidha, bado hakuna ishara yoyote kwamba serikali imeifanyia kazi hasa ukizingatia uzito wa kufru na kashfa iliyofanywa dhidi ya Waislamu na Uislamu kwa Mola wao kuitwa shetani na Uislamu kuitwa kuwa ni ugaidi. “Wakristo wameonywa

Mchungaji Hadija apanda mbegu ya farka Mbezi Louis
Na Mwandishi Wetu

4

Habari

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

Familia ya Kiislamu yatiwa msukosuko Polisi waingilia kati wabaini chuki za kidini
kuwa mwezi Machi mwaka huu, mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mchungaji Hadija, mkazi wa eneo hilo la Louis Pub, naye alidai kuwa majira ya saa kumi usiku, watu wasiofahamika walifika nyumbani kwake na kumwagia maji kupitia dirishani. Ilielezwa kuwa kufuatia tukio hilo, watu walikusanyika kujua kulikoni. Mchungaji huyo alidai kuwa waliofanya kitendo hicho walikimbilia kwa mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Juma. Habari z a tu k i o h ilo zilifikishwa kituo cha polisi Mbezi Louis, ambapo Oss kituoni hapo aliongoza hadi eneo la tukio na kuwakuta wakazi wa eneo hilo wakiwa na mapanga tayari kwenda nyumbani kwa Bw. Juma Ngunda, ambako yapata umbali wa kilometa moja na nusu. Hata hivyo baada ya polisi kuingia kati, walifika

M AT U K I O m f u l u l i z o ya mauaji na uhalifu yaliyotokea katika mtaa wa Louis Pub, Mbezi Louis jijini Dar es Salaam, yamezua faraka miongoni mwa wakazi wa eneo hilo. Taarifa zinaeleza kuwa mwezi Februari mwaka huu, mtoto mmoja wa kike aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza, alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha. Wakati sababu za kifo cha binti huyo zikiwa bado hazijabainika huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo, yalifuatia matukio mengine mfululizo ambapo mtoto mwingine wa kike alipoteza maisha na kudaiwa kuwa alichomwa sindano kitovuni na kukatwa na wembe shingoni. Mtoto huyo alidaiwa kuwa alikuwa ni rafiki wa aliyefariki mara ya kwanza. Ta a r i f a z i n a b a i n i s h a

Inatoka Uk. 1

Waliochoma Msikiti Tunduma hawajafikishwa mahakamani
suala la kuchinja kwa sasa wanachinja Waislamu kama kawaida huku zoezi hilo likisimamiwa na Polisi, ili kuepusha watu wasioruhusiwa kuchinja kujiingiza katika zoezi hilo na kusababisha ghasia nyingine. Hata hivyo Waislamu katika mji huo wamelazimika kufungua bucha yao maalum chini ya Umoja wa Kiislamu Tunduma, ili kujiridhisha zaidi na uhalali wa nyama na kuepuka na hofu ya kulishwa vibudu. Kwa mujibu wa muumini mmoja wa Kiislamu aliye makazi wa Mji huo, Bw. Mwinshehe Rashidi, alisema bucha hiyo imepewa jina la ‘Sisi kwa Sisi’, iliyopo katika mtaa wa Majengo, CCM. Bw. Rashid alisema Waislamu wamelazimika kufungua bucha hiyo baada ya sakata la Wakristo kuzidi kushika kasi ya kulazimisha kuchinja, na kupeleka nyama hizo katika mabucha kiholela, kwa kuwa bucha nyingi zinamilikiwa na Wakristo. Naye Ustadhi AbdulAzizi Madenge, akiongea na Gazeti hili toka Tunduma, alisema kumekuwa na vikao baina ya viongozi wa dini na Serikali vimekuwa vikiendelea, ambapo tayari viongozi hao wa Serikali Mkoani Mbeya, wameshafanya vikao vitatu. Ust. Madenge, aliyemhadhiri wa dini ya Kiislamu, aliainisha vikao hivyo vilivyofanyika kuwa ni baina ya Maaskofu na Mkuu wa Wilaya, Masheikh na Mkuu wa Wilaya na cha mwisho kilijumisha makundi yote hayo chini ya Mkuu wa Mkoa. Ust. Madenge, aliyefika katika mji huo kushuhudia kadhia hiyo alisema, Mkuu wa Wilaya, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (RPC) Bw. Othman Diwani pamoja na Afisa Usalama w a Wi l a y a w a l i f i k a kushuhudia Msikiti ulioathiriwa na Wakristo. Kwa upande wake Amir Kundecha, wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) alisema, Waislamu wanashangaa watuhumiwa hao kucheleweshwa kufikishwa katika vyombo vya sheria, ili hali suala lipo wazi. Amir Kundecha, alisema moja ya dhulma wanayoilalamikia Wa i s l a m u n c h i n i n i sheria kuonekana kali kwa Waislamu na kukosa makali kwa Wakristo, hata kama makosa yanayofanywa yanawiana au yanayofanywa na Wakristo kuwa makubwa zaidi. Kiongozi huyo wa Baraza Kuu, alisema kosa huwa kosa linapofanywa na Muislamu lakini linapofanywa na Mkristo, huwezi kusikia vishindo, na hunyamaziwa hata linavyomalizwa huwezi

nyumbani kwa Bw. Ngunda na kuwakamata wadogo zake wanne, ambao ni Ally Ngunda, mwanafunzi wa kidato cha nne, Hamis Ngunda, Kassim Ngunda, Mohammed Ngunda, mwanafunzi wa kidato cha kwanza, wakituhumiwa kumwagia maji Mchungaji Hadija. Baada ya tukio hilo kufikishwa kituo cha polisi, mashitaka yalibadilishwa na vijana hao wakatuhumiwa kumchoma mtu sindano kitovuni. Baada ya siku tatu, kesi ya kumchoma binti huyo kwa sindano nayo ilibadilishwa na safari hii wakatuhumiwa kwa mauaji. Hata hivyo baadae kaka wa watuhumiwa hao Bw. Juma Ngunda, ambaye anadaiwa ndiye mlengwa mkuu anayetuhumiwa na baadhi ya wakazi hao, alifika kituoni hapo ili kujua kisa na sababu ya kukamatwa wadogo zake ambao ni wanafunzi. Baada ya kutoa maelezo

ya kina juu matukio yaliyowahi kutokea katika eneo hilo na jinsi matukio hayo yanavyohusishwa na familia yake, polisi waliamua kukubali kutoa dhamana kwa wadogo zake lakini wakatikiwa kuripoti kituoni hapo kila siku ya Jumatatu wakati upelelezi zaidi ukiendelea. Wakati hayo yakiendelea, Mchungaji Hadija alidaiwa kuendelea kuhamasisha baadhi ya wakazi wa eneo hilo, kushinikiza kuitishwa mkutano wa wakazi wote ili kupiga kura za kumpata mtu wanayemshuku kuhatarisha usalama wa wakazi hao. Kufuatia shinikizo hilo lililokusudiwa kumtia hatiani Bw. Juma, mkutano uliitishwa na OSS kituo cha Polisi Mbezi Louis kualikwa kuusimamia. Hata hivyo OSS alipofika katika mkutano huo, aliwaambia wakazi hao kuwa utaratibu huo sio suluhu na haukubaliki kipolisi kwa kuwa kuna dalili za kupigwa kura za chuki na si za kumtafuta mhalifu. Baadhi ya wakazi waliunga

mkono kauli ya OSS lakini wengine walipinga kiasi cha kutaka kuzua vurugu wakishinikiza kupigwa kura hizo. Kufuatia hali hiyo, OSS akaridhia kura hizo kupigwa. Hata hivyo baada ya kura kupigwa na polisi kufanya uchunguzi zaidi, na hata baada ya kumhoji Mchungaji Hadija na Bw. Juma Ngunda, ilielezwa kuwa walibaini kuwa kesi zilizopo ni matokeo ya chuki za kidini zaidi. Kwamba hazikupatikana dalili zozote zenye ushahidi wa kuihusisha familia ya Bw. Ngunda na matuko hayo. Hadi sasa kesi hiyo bado ipo kituo cha polisi Mbezi Louis, na haijapelekwa mahakamani kutokana na kugubikwa na uzushi uliombatana na chuki zinazodaiwa kuasisiwa na Mchungaji huyo. Wakati hali ikifikia hapo, kuna taarifa kwamba tayari Mchungaji Hadija, amehama eneo hilo na sasa anadaiwa anaishi Manzese.

wa vurugu za kuchinja na kuchoma moto Msikiti. Awali Jeshi la Polisi liliwatia mbaroni watuhumiwa wa vurugu na maandamano hayo wapatao 90 na baada ya mahojiano, wamechujwa na kubakia 45. Imearifiwa kuwa watuhumiwa hao, hadi sasa bado wapo rumande huku ikiarifiwa kuwa dhamana yao imefungwa, mpaka hapo kesi yao itakapo tajwa April 18, 2013. “ Mpaka sasa (jumatano ya wiki hii) bado watuhumiwa hao hawajafikishwa mahakamani, hivyo h a i j a f a h a m i k a watafunguliwa mashitaka gani, mpaka hapo April 18, inayodaiwa kuwa ndiyo siku watakayopelekwa Mahakamani”. Kilisema chanzo chetu cha habari kutoka Tunduma, kwa njia ya simu. Chanzo hicho kilisema,

kujua mpaka husaulika. Amir Kundecha alisema, kosa likifanywa na Wakristo, sio tatizo na hufanywa kuwa la mtu na mtu lakini likifanywa na Muislamu litahusishwa na Waislamu na dini yake itahusishwa pia, na hata viongozi wao (Masheikh) kutiwa misukosuko. Amiri Kundecha alisema, hata vyombo vya habari huwa kimya ikiwa muathirika ni Muislamu, mathalani alisema, Mjini Tunduma Msikiti umechomwa moto, kisha kung’olewa madirisha na milango, lakini hawaandiki Msikiti umechomwa. “Isipokuwa tu, ikitokea katika Kanisa hata kama ufito umeanguka kwa kishido cha Waislamu waliopita nje kwa shughuli zao utaambiwa Waislamu wamevunja Kanisa, na vyombo vya habari vyote vitashupalia ufito huo wa Kanisa.” Alisema.

5
Misikiti mipya 1,110 kujengwa Iran mwaka huu
SHIRIKA la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA), limetangaza mpango wa kujenga misikiti 1,110 mipya katika maeneo mbalimbali nchini Iran. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Naibu Mkuu wa Shirika la Kutoa Misaada la Imam Khomeini (MA) Saeed Sattari, amesema misikiti hiyo itajengwa katika kipindi cha mwaka moja ujao chini ya ‘Mpango Zakat’. Amesema mpango huo ulianzishwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwajengea misikiti wale wasio na uwezo. Bw. Sattari, amesema kuwa tangu mpango huo uanzishwe, karibu misikiti 6,000 imejengwa kote Iran kwa kutumia fedha za Zakat na misaada ya wafadhili na serikali. Ameongeza kuwa sehemu kubwa ya misikiti mipya itajengwa vijijini kwa kuzingatia mahitajio ya jamii husika. Hata hivyo Naibu Mkuu wa Shirika la MA, ametoa wito kwa wanaojiweza katika jamii kusaidia ujenzi wa misikiti nchini.

Habari za Kimataifa

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

Hamas yawatia nguvuni majasusi wa Ulaya
MOHAMMED Lafi, Mkuu wa Usalama wa Ndani wa Palestina Harakati ya Mapaambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesema kuwa vikosi vya usalama vya HAMAS vimewatia mbaroni watu kadhaa katika Ukanda nwa Ghaza wanaoshukiwa kuwa majasusi wa mashirika kadhaa ya ujasusi ya nchi za Magharibi na Kiarabu. To v u t i y a Wi z a r a y a Mambo ya Ndani wa serikali ya Palestina inayoongozwa na harakati ya Hamas, imemnukuu Mohammed Lafi, Mkuu wa Usalama wa ndani akisema kuwa, nusu ya majasusi hao wamekiri kuwa wamekuwa wakifanya vitendo vya kijasusi kwenye ukanda huo. Lafi amewaonya Wa p a l e s t i n a w e n g i n e wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya kuyapatia taarifa mashirika ya kijasusi ya nchi za Magharibi. Itakumbukwa kuwa, Wi z a r a y a M a m b o y a Ndani wa serikali ya Hamas katikati ya mwezi Machi mwaka huu, iliwaonya wale wote wanaoufanyia ujasusi utawala wa Kizayuni kwamba watasakwa bila ya huruma iwapo hawatajikabidhi kwa vyomo husika hadi kufikia Aprili 11.

CIA yatoa mafunzo kwa magaidi Syria
GAZETI la Guardian linalochapishwa nchini U i n g e re z a l i m e f i c h u a kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani CIA, linatoa mafunzo kwa kundi la waasi wa Syria kwa lengo la kulinda usalama wa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walioko katika eneo la miinuko ya Golan la Syria linalokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Toleo la jana la gazeti hilo limefichua kwamba Shirika la Ujasusi la Marekani linaendesha mafunzo hayo kwenye kambi zake zilizoko nchini Jordan, ili waasi hao wanaofungamana na kundi la al Qaeda wachunge usalama wa majeshi ya Israel yaliyoko katika eneo la milima ya Golan. Gazeti hilo limeandika kuwa, baadhi ya magaidi hao

NEWCASTLE, Mwaka jana, uongozi wa timu ya soka ya Newcastle United ya Uingereza ulitangaza wazi kuwa ilikuwa na mpango wa

Wachezaji Newcastle wapata chumba cha kusalia
kutaka kuwa na chuba maalum katika uwanja wake wa soka kwa ajili ya kuwawezesha wachezaji wake Waislamu kutekeleza ibada zao. Hivi sasa uongozi huo umetangaza kuwa tayari klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo, imewaandalia chumba maalumu cha kusalia wachezaji wake Waislamu katika uwanja wa mpira wa timu hiyo. Magazeti ya Uingereza yameandika habari hiyo na kubainisha kwamba, timu ya Newcastle ina wachezaji saba Waislamu na kabla ya kuandaliwa chumba hicho maalumu cha kusalia, wachezaji hao Waislamu walikuwa katika vyumba tofauti kabla au baada ya mechi katika uwanja maalumu wa mpira wa timu hiyo wa St James Park. Wachezaji Waislamu wa timu ya Newcastle ni Massadio Haidara, Hatem Ben Arfa, Moussa Sissoko, Mapou YangaMbiwa, Cheick Tiote, Papiss Cisse na Mehdi Abeid. Gazeti la Daily Mirror la Uingereza linaripoti kwamba, mchezaji Demba Ba, ambaye hivi karibuni alijiunga na timu ya Chelsea ndiye aliyekuwa akiwasalisha wachezaji Waislamu wa timu yake hiyo ya zamani. Demba Ba anasifika kuwa ni mcha Mungu na mtekelezaji mzuri wa ibada. Siku zote akifunga goli husujudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu. Ba anasema, anapenda kusali swala tano na katu hapendi

BAADHI ya wachezaji wa Newcastle United ya Uingereza.

starehe za pombe na sigara. Wachezaji Waislamu wa timu ya soka ya Newcastle ya Uingereza mbali na kutekeleza ipasavyo ibada ya swala tano kwa siku, wana kawaida ya kusali kwa ajili ya kuomba dua kabla ya mechi wakiiombea ushindi timu yao na wengi wao wanapofunga goli husujudu na kumshukuru Mwenyezi Mungu, ada ambayo bila shaka inapaswa kuigwa na wachezaji wengine Waislamu. Timu ya soka ya Newcastle ndio yenye wachezaji wengi zaidi Waislamu kati ya timu zinazoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

ITKAF Masjid Swabirina Maduka mawili Chang'ombe
Uongozi wa Masjid Swabirina au Mbuyuni uliopo Chang'ombe Keko Maduka Mawili Jijini Dar es Salaam unawaarifu Waislamu wote kutakuwa na Ibada maalum ya Itkaf itakayofanyika msikitini hapo siku ya Jumamosi (kesho) tarehe 13/4/2013 baada ya swala ya Isha. Wabillah Tawfiiq

RAIS wa Syria, Dkt. Bashar al-Assad

wa Syria, tayari wako katika eneo hilo baada ya kupata mafunzo kutoka kambi za CIA nchini Jordan. Guardian katika siku za hivi karibuni lilifichua baadhi ya nchi za Magharibi zinazotoa mafunzo ya kijeshi kwa makundi ya kigaidi ya Syria nchini Jordan.

6
Na Dk. Noordin Jella (Ph. D. in Economics) MATUKIO ya kusikitisha, kufedhehesha na yakushangaza yamekuwa yakitokea Zanzibar tangu mwaka jana baada ya Wazanzibar kuanzisha harakati za kurudisha Zanzibar yenye mamlaka kamili (Zanzibar huru), harakati zilizoanzia kwenye Baraza la Wawakilishi mwaka 2010, kwa kubadili katiba ya Zanzibar na kuitaja Zanzibar kuwa ni nchi kamili! Vugu vugu lililochagizwa zaidi na Jumuia ya Mihadhara na ya Kiislamu (UAMSHO). Vugu vugu hilo lilileta mvutano kati ya jeshi la polisi na wafuasi wa Masheikh wanaoongoza Jumuia ya UAMSHO. Jambo la kushangaza, mapambano yalikuwa ni kati ya polisi na wafuasi wa UAMSHO, lakini asubuhi ikasikika Makanisa kadhaa yamechomwa moto! Eti Wazanzibar hao (UAMSHO) ambao wamekuwa wakiishi kwa amani na upendo na Wakristo kwa karne tele zilizopita, leo hii wameacha nyumba zote za askari wanaopigana nao, wana CCM, viongozi wa SMZ, na Masheha, badala yake wameenda kuchoma moto makanisa! Hapa tukaambiwa uchunguzi utafanyika na wahusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria….watu wakakamatwa kwa nzo, wakatafutwa kila mwenye ndevu akanyolewa, wakahilikishwa kwa kutumia technologia (kama alivyosema Kamishna Mussa), wakaangalia kanda za video kubaini walokuwepo kwenye vurugu zile na kuwakamata! Tukasubri majibu, tuambiwe ni nani hasa alochoma Makanisa. Ikabaki kuwa “watu wasiojulikana” Jibu mpaka leo hakuna! Tukakaa tena kidogo, tukasikia Sheikh Farid H ad katekw a, jes hi la polisi likasema hajui alipo, itakuwa kajiteka! Vurugu zikazuka tena, Makanisa yakachomwa tena, lakini mara hii wakaongeza na kuchoma maskani za CCM, na polisi mmoja akauliwa kwa kukatwakatwa kwa mapanga! Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema, akasema ametuma makachero wenye ujuzi wa hali ya juu (walobobea) kutoka Makao Makuu Dar es Salaam, kwenda Zanzibar kuwatafuta wahusika wote waloua na kuchoma makanisa ili wafikishwe kwenye vyombo

MAKALA

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013
UAMSHO hao, kauliwa Padri “UAMSHO”, kamwagiwa tindi kali Sheikh Soraga “UAMSHO”, limechomwa Kanisa-“UAMSHO”!. Serikali imekuwa ikikawia kufanya kazi yake (Jeshi la Polisi) kama walivyoafanya kule Mwanza alipouliwa RCO , badala yake jamii imeachwa ihukumu kwa hisia. Hii ni hatari! Maana sasa viongozi wa UAMSHO wako ndani, UAMSHO hajulikani ni nani, lakini mauaji yanaendelea. Sasa akiuliwa Padri au kuchomwa Kanisa utasikia “ni Waislamu hao, naam hisia hisia, “Waislamu hao wa Zanzibar sasa washakuwa magaidi! Si ndo alivyosema Nchimbi?” Na sasa akiuliwa Sheikh au ikichomwa Misikiti, kwa hisia tu watasema “Wakristo hao” na Wakristo nao washakuwa magaidi! Tunako kwenda siko! Siamini na kamwe sitoamini kwamba, eti matukio haya yanafanywa na Mzanzibar wa kawaida, awe Mkiristo au Muislamu. Kamwe siamini kama Mzanzibar wa kawaida anamiliki silaha ya moto na amekuwa mjuzi wakuitumia kiasi kwamba anaweza kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa huku akiwa kwenye vespa na kumuua Padri. Siamini kuwa tuna wadunguaji mahiri Zanzibar wanaomiliki silaha. Siamini kabisa kama kweli Mzanzibar anaweza kumvamia Sheikh na kumkatakata mapanga. Nani basi anayefanya haya? Na anafanya haya kwa nini? Na Kwanini mpaka leo Kamishna Mussa hajatoa majibu ya walofanya matukio haya? Inasikitisha na kushangaza s a n a Wa z i r i m w e n y e dhamana na ulinzi wa taifa hili, anaibuka akiwa na hoja kwamba wanaofanya matukio hayo ni magaidi. Kwamba imeshindikana kuwadhibiti magaidi mpaka wameweza kuingia ndani ya nchi, wakaweza kumiliki silaha, wakaweza kupanga na kutekeleza mauaji na uharibifu wa nyumba za ibada wakati wenyewe wakiwa macho. Lakini pia tungeambiwa hawa magaidi wana madai (demand) gani. Japo hakuna maelezo yanayotosheleza kuhusu maana ya ugaidi, lakini Maana ya kufikirika ya neno gaidi (terrorist) ni mtu anayeleta madhara katika jamii au anayefanya mashambulizi au utekaji kwa lengo la kuogofya mamlaka au mtu husika ili atekelezewe madai yake. Kwa misingi hiyo gaidi huwa akishatenda huwa hutokeza Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

SHEIKH Farid Hadd akiongea na vyombo vya habari.

Tusipotumia akili zetu vizuri tutapiganishwa kama makuchi
vya sheria.…Tukasubiri na tunaendelea kusubiri, bila kupata majibu mpaka leo! Hatujakaa vizuri, tukasikia Sheikh Soraga, kamwagiwa tindi kali usoni, na “mtu asiyejulikana”! Kama kawaida tukaambiwa tena, jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuwatia nguvuni wahusika. Mpaka naandika makala hii hakuna jibu la nani alommwagia Sheikh Soraga tindi kali! Jeshi la Polisi bado lafanya uchunguzi! Tukiwa bado tunatafakari hayo, tunasikia tena Padri Ambrose kashambuliwa kwa risasi na “watu wasiojulikana”! Lengo ilikuwa ni kumuua, lakini bahati nzuri yupo hai! Hili likaendelea kutushangaza wengi, eti mara hii Wazanzibar wamekuwa wanamiliki silaha za moto na ni wajuzi wa kuzitumia! Wamekuwa wadunguaji (snipers). Hapa sasa tukasikia kauli kali zaidi, tena kutoka kwa viongozi wa juu zaidi kisiasa katika nchi yetu, akiwemo Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa serikali ya Zanzibar Dr. Ali Shein, wakilaani na kuvitaka vyombo vyote vya usalama, wakiwemo Usalama wa Taifa kufanya uchunguzi kwa weledi wa juu kabisa ili kubaini na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika! Tukasubiri na tunaendelea kusubiri kuwajua wahusika, lakini mpaka sasa hakuna jibu! Juzi tena tunasikia Padri Mushi, ameuliwa kwa risasi na “watu wasojulikana”! Mauaji hayo yanatokea tena ndani ya Zanzibar hiyo hiyo! Mara hii Tanzania zima ikatikisika, kauli nzito nzito kutoka kila kiongozi wa nchi hii, kuanzia Rais wa Tanzania, Rais wa SMZ, Waziri wa Mambo ya Ndani, n.k. Karibu kila mwenye mdomo (access ya vyombo vya habari) alisema na kulaani. Tukaambiwa FBI, CIA, wakishirikiana na TISS watakuja kuchunguza na kuwatia nguvuni walomuuwa na waloratibu mauaji hayo. Bado twasubiri! T u k i w a b a d o tumehamanika na matukio hayo, tukiwa bado tunanyoosheana vidole, na kutupiana lawama, tukiwa tunazidi kuandamwa na wingu zito, sasa tunasikia Imamu Sheikh Ali Khamis huko Kitope (Kaskazini Unguja) ameuliwa kwa kukatwa katwa mapanga na “watu wasiojulikana”! Nategemea kauli zitakuwa hizo hizo, “Uchunguzi utafanyika…” Na sisi ni kama vifaranga vya kuku, tutanyonya kesho, na bado twasubiri kunyonya! Kwa kweli ukiangalia ukubwa wa visiwa vya (Zanzibar) na idadi ya watu wake na ukilinganisha na matukio haya, utaona kwamba ni matukio mengi sana na yametokea katika kipindi kifupi sana. Ni matukio yakusikitisha na kulaaniwa na kila muungwana. Matukio yasiyopaswa kutokea katika jamii ya watu walostaarabika kama Zanzibar. Kinachosikitisha na kutisha ambacho ndicho kilichonisukuma kuandika haya, ni kuwa matukio yote haya yamekuwa yakiishia kuhukumiwa na jamii kwa hisia tu, huku serkali ikiwa na majibu ya “watu wasojulikana, upelelezi unaendelea”, Lakini jamii na hata viongozi wa serkali na dini wamekuwa wakitumia hisia zao, utashi na mihemko yao kushutumu na hata kuhukumu baadhi ya kikundi au kundi katika jamii. Mwanzaoni wapo walojaribu kuhusisha matukio hayo na CUF, lakini walipoona wazanzibar wa hivi sasa hawatopigana wala kuuana kwa sababu ya vyama vya siasa, wakakosa nguvu. Lakini mara zote kundi la UAMSHO, limekuwa ndio kitambaa (leso) cha kufutia mafua, jasho, mate, n.k., kila tukio likitokea, basi utasikia

7

TANGAZO

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

8
Na Omar Msangi
KAMA ilivyoripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari wiki hii, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa hakubaliani na mwenendo wa CCM na Serikali yake katika suala la kushughulikia udini. Pengine mtu angetaka kuuliza, hivi ni kipi Mheshimiwa Mkapa asichoridhika nacho? Je, ni kwa vile toka aondoke madarakani hatujashuhudia tena askari akiamriwa “Piga yule”, “Na yule” “Bado (hajafa) mwongeze”. Na kweli polisi anafyatua risasi kuwalenga shabaha na kuuwa Waislamu kama ilivyokuwa pale Mwembechai? Au ni kwa vile haijatokea tena kwa Serikali kuendesha kamatakamata ya Masheikh na kuwalundika ndani kwa shinikizo la Maaskofu kama ilivyotokea katika Serikali yake? Tunachokumbuka na rekodi zinavyoonyesha ni kuwa kwa agizo na kwa shinikizo la Paroko Lwambano, Serikali ya Mkapa iliwakamata Masheikh, wazee wa Kiislamu, Maimamu na wahadhiri na kuwaweka ndani. Tunachokumbuka na rekodi zinavyoonyesha ni kuwa kwa shinikizo hilo la Padiri Camillus Lwambano, Polisi walivamia Msikiti wa Mwembechai wakauvurumishia mabomu ya machozi ambapo wanawake waliokuwa ndani ya Msikiti huo waliumizwa vibaya na kisha kupigwa sana na kudhalilishwa na kisha kuwekwa rumande ambapo walidhalilishwa zaidi. Je, kwa vile toka atoke madarakani, Serikali haijarudia tena jinai hii, japo bado inatembea na RB shingoni, ndio kisichomridhisha Mheshimiwa Mkapa? Chanzo cha mauwaji ya Mwembechai na jinai yote iliyofanywa na Serikali ya Mkapa katika kadhia ile, ni Maaskofu kutokutaka Waislamu waseme kuwa Yesu Si Mungu kama Qur’an yao inavyosema. Ufupi wa maneno na katika lugha nyepesi ni kuwa Serikali ya Mkapa iliuwa Waislamu na kuwatesa wengine wengi kutokana na imani yao ya kidini. Ilifanya hayo kulinda na kuuhami Ukristo na kuwahami Maaskofu na Wachungaji ambao walikuwa wamekwama kutetea Imani ya Utatu wakataka Serikali ndio ifanye kazi hiyo. Sasa, Mheshimiwa Mkapa anaposema leo kuwa haridhiki na jinsi Serikali ya Rais Kikwete inavyoshughulikia suala la udini, je, anataka Serikali iendelee kusimama kutetea Utatu na Uungu wa Yesu badala ya kazi hiyo kufanywa na viongozi wa makanisa? Kama vyombo vya habari vilivyoarifu, Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa amesifia utawala wake kwa kuongoza taifa bila ya kubaguana na kwamba anasikitishwa na matukio ya udini, ambayo yanaashiria kuvuruga amani na utulivu wa Tanzania katika siku za karibuni.

Makala/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013
ambapo kule Korogwe kijana mmoja aliwekwa ndani kwa kuandika katika baisikeli yake kuwa Yesu Si Mungu na kile kilichotokea kule Morogoro ambapo Ofisa wa Polisi alitaka Mungu wa Waislamu afikishwe mahakamani kwa kuleta Qur’an inayokanusha uungu wa Yesu; ilikuwa ni katika jitihada za Serikali ya Mkapa kushikamana na misingi ya Mwalimu Nyerere ya kulitetea Kanisa na kulipa “A Better Chance” dhidi ya Uislamu. Je, hii ndiyo misingi anayoilalamikia Mzee Mkapa kuwa Rais Kikwete kaachana nayo? Pengine nimkumbushe Mzee Mkapa kuwa katika suala la “Yesu ni Mungu” Vs “Yesu si Mungu”, aliwasikiliza viongozi wa Makanisa na kupuuza malalamiko ya Waislamu kuwa hawatendewi haki Kikatiba, Kisheria (za nchi) na kidini. Hata hivyo, Waislamu walipokuja na madai ya Mahakama ya Kadhi na suala la OIC, akasema kuwa hawezi kupuuza maoni ya Wakristo. Na kwa vile Wakristo walikuwa hawataki mambo hayo, huo ukawa ndio msimamo wa Serikali. Hata hivyo, kwa Mzee Mkapa hayo yote yamefanyika kwa sababu hakuwa mdini na kwamba alijitahidi sana kuwatendea haki wananchi wote! Sasa pengine swali la kujiuliza ni hili: Kama baada ya kujitahidi sana kutokuwa mdini, ndio ameishia na kadhia ya Mwembechai, kukamatwa na kuwekwa ndani Profesa Jahazi bila kusahau kuuliwa Imam pale Mwembetanga kabla ya mauwaji ya Pemba 2001; je asingejitahidi kujizuiya kuwa mdini, hali ingekuwaje?

AN-NUUR

Kweli Mkapa ana haki kujisifia na kushangaa
Mkapa amenukuliwa akiyasema hayo hivi karibuni wakati akitoa salamu zake baada ya kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Desdelius Rwoma. Mkapa alisema anachojivunia ni kuheshimiwa na waumini wa madhehebu yote. “Wakati wa utawala wangu nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kuwahudumia wananchi bila kuwepo kwa malalamiko ya kubaguana katika jamii.” Alisema. Hapa inabidi kuweka nukta, kukaa kitako na kutafakati kidogo. Anachosema Mheshimiwa Mkapa ni kuwa pamoja na yale tuliyoshuhudia ya mauwaji ya Mwembechai, kukamatwa Masheikh na kuteswa kwa kusoma hadharani aya za Qur’an zinazokataa Utatu, kufa na kufufuka kwa Yesu, ni kwamba yote hayo aliyafanya baada ya kujitahidi sana kuzuiya hisia zake za ‘Ukatoliki’ na ‘udini’. Na mwenyewe anajisifia akisema kuwa amejitahidi sana kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi. Kwamba baada ya kujitahidi sana ndio akaishia na “Mauwaji ya Mwembechai”!!! Ambapo Polisi waliouwa Wa i s l a m u w a l i p o n g e z w a , tunasikia wengine wakapewa vyeo. Lakini zaidi ni kuwa hata Waislamu walipotaka mauwaji yale yafanyiwe ‘Inquest’ kama sheria inavyotaka akakataa. Katika mazingira kama haya, kweli Mheshimiwa Mkapa ana haki ya kushangaa na pengine tuseme, ana haki ya kuwashangaa Waislamu. Kwamba baada ya kufanya jinai ya Mwembechai, bado aliwapata Masheikh wa kukaa meza moja na Serikali yake kuwashutumu Marehemu na wafiwa. Lakini pia pamoja na mauwaji hayo na kukataa kufanya uchunguzi, bado hajafikishwa ICC. Yawezekana kile kitendo cha Sheikh wetu Hamid Jongo na baadhi ya Masheikh wengine, kukaa meza moja na Serikali ya Mkapa nje ya Msikiti wa Mwembechai, hata kabla wafiwa hawajatokana mazikoni, ndio kinampa nguvu leo Mheshimiwa Mkapa kusema na kutamba kwamba anaheshimiwa na watu wa dini na madhehebu zote! Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hatakubali kuona Kanisa Katoliki likijitia katika

Pamoja na mauwaji Mwembechai, Pemba… Hakuruhusu Inquest na hajafikishwa ICC Ushauri wake kwa Kikwete utatuangamiza Je, anataka aendeleze ya Paroko Lwambano?

tope kama ilivyotokea katika nchi nyingine za Ulaya. Na akaahidi kuwa atalipa fursa

Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa.

pekee, fursa ya upendeleo lipate kunawiri na kustawi. Hapana shaka ile heka heka tuliyokuwa tukiishuhudia

Ahlul Daawa Hajj And Travel Agency

Inawatangazia Waislamu wote Kuwa Imeandaa Safari ya Hijja Mwaka 2013 Sawa na Mwaka 1434 Hijria kwa Dola US$ 3550 tu. Umra kwa Mwezi wa Ramadhani itakuwa ni Dola US$ 1995 Fomu zinapatikana katika ofisi zifuatazo:1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba Namba 26 Mkabala na Showroom ya Magari Tel 0713 730 444, au 0773 804101 au 0785 930444 na 0773 930444. 2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel 0777 484982 au 0777 413 987. 3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es salaam 0784 453838 4. Abdallah Salehe Mazrui ( HOKO) Dar es salaam 0715 724 444 5. Salim Is-haq Dar es salaam 0754 286010 au 0774 786101 6. Dukani kwa Abdala Hafidh Mazrui wete pemba 0777 482 665 7. Dukani kwa Mohamed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456911 8. Sheikh Daudi khamis sheha 0777 679692 9. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Wahi kulipia. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930444. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo 0777 484982 au 0777 413 987. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar 0777 417736 Sheikh Salim Mohamed Salim 0774 412974 au Kupitia ACCOUNT NAMBA 048101000030 NBC Tanbih: Atakae maliza Taratibu zote kuanzia sasa Mpaka 15 July 2013 atapata Punguzo la asilimia 16% atalipia $ Dola 2982 tu. Atakae maliza Taratibu zote kuanzia Tarehe 16-july Hadi Tarehe 15 Augost 2013 atapata Punguzo la Asilimia sita 6% atalipia Dola $3337 tu. Kutakuwa na umra ya utangulizi kabla ya Umra ya Hijja kwa atakae maliza kufanya hivyo. Atakae maliza taratibu zote mwanzo ndie atakae shughulikiwa mwanzo. Ukilipia kwa njia ya Account kwanza piga simu 0774 412975. Kumbuka Kikundi cha Ahlul Daawa Kwa Bei nafuu kuliko wote na Huduma bora Kuliko wengi. Nyote mnakaribishwa

9
Na Ibrahim Noor “KWELI Zanzibar ilikuwa na watu wachache waliojiweza sana kimaisha na kulikuwa pia na idadi ya masikini, lakini wengi zaidi walikuwa na maisha ya wastani ambayo hayakuwa na tafauti kubwa baina yao, na si kweli kabisa kuwa utajiri ulikuwa ni wa watu wa kabila fulani tu na umasikini ulikuwa ni wa watu wa asili fulani tu. Nikukumbusheni mfano mmoja: wenye umri kama wangu mlioishi Unguja mjini nina hakika mtakumbuka kuwa Darajani (ukishavuka daraja kuelekea Ng’ambo) palikuwa wakisimama mbele ya ukuta Waarabu masikini, wengine vipofu, wakiomba.” Mtanisamehe kuwa katika risala yangu hii nitarejelea baadhi ya maneno niliyokwisha kukuelezeni kabla kwa mukhtasari. Lakini kwanza naanza kwa kumshukuru Sheikh Salim Msoma kwa makala yake yenye maana na kwa kuelewa vizuri yaliyopita. Mara nyingi huwa nazozana na watafiti wanaokuja kwangu kutaka kujua ninayoyaelewa na niliyoyashuhudia. Nazozana nao pale wanapoyapa maelezo ya kila waliyemhoji uzito sawasawa. Fulani kasema hivi na fulani kaelezea vile, kwa hivyo ni hivi na hivi. Lakini mtafiti huyo huyo ukimwuliza, jee unapokuwa mgonjwa na unahitajia upasuzi utakubali upasuliwe na yoyote anayejua kutumia visu? Kwa mfano, utakubali upasuliwe na muuzaji nyama au utamtafuta tabibu mjuzi wa kupasua na mwenye kuelewa ugonjwa ulionao? Utakubali upasuliwe na muuza nyama badala ya tabibu kwa sababu wote wawili ni wajuzi wa kutumia visu na ni mahodari wa kukata nyama? Iwapo hutakubali kupasuliwa na muuza nyama kwa sababu hana ujuzi wa kutibu, basi vipi utayaweka sawa maelezo ya asiyejuwa na yule anayejua? Haya ndiyo maradhi waliyonayo watafiti wengi. Wa z a n z i b a r i w e n g i wanaelezea wanayoyajua wao binafsi na wengi katika walioishi mjini hawayajui kabisa maisha ya shamba wala ya watu wa Ng’ambo na pia ni kweli kuwa walio mashambani wanaelewa machache ya walioko mjini. Na huku kutokuelewa ndiko kulikopelekea kuwa wengi kuwa na dhana nyingi na ukweli mchache. Halikadhalika, mambo yalikuwa hivyo hivyo kukhusu makabila,

Makala

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013
huku hajui kama atapata faida au khasara. Kazi bado haikwishia hapo. Baada ya janguo la nazi, Waarabu hao wakawa wanapita chini ya minazi na kuokota nazi wenyewe na kupakia katika gari lao la ng’ombe au katika makapu yaliyopakiwa juu ya punda wakapeleka kwenye kufuliwa na wakafua nazi wenyewe, wakazivunja na kuzianika wenyewe, wakizisukua na wengine wakizitia katika tanuri za mbata. Zikiwa tayari wakizitia katika magunia wenyewe na wakiyapakia magunia katika magari ya ng’ombe kwenda kuziuza. Kama kuna faida ni yao, kama kuna khasara ni yao pia. La kweli ni kuwa kazi ngumu wakizifanya Waarabu kwa khiyari zao bila ya kulalamika. Zaidi ya hayo, kukinyesha mvua kwa juma moja, basi Mwarabu amekula khasara ya kweli. Katika mashamba ya mikarafuu, hali ni hiyo hiyo. Baada ya kuchumisha karafuu na kuwalipa wachumi kazi yote ya kuanika na kuanua ilikuwa ikifanywa na Waarabu wenyewe. Kukinyesha mvua kwa juma moja, basi Mwarabu amekula khasara ya kweli. Mmanga huyo huyo, na wengi kama hao, waliotumia jasho lao na pesa zao, wao na aila zao zisizokuwa na dhambi yoyote ya biashara ya utumwa wakawa ndiwo wa mwanzo kuingiliwa nyumbani mwao na kupigwa mapanga kinyama kabisa. Kisa nini – eti sababu ni Mwarabu – Siku ya Qiyama tutakapokuwa mbele ya Mwenye-enzi Mungu Subhanah waTaala na kumtegemea Mtume wetu (SAW) atuombee maghfira, tutamwambia nini Mtume ( S AW ) : “ Tu n a k u o m b a Mtume wa Mwenye-enzi Mungu utuombee maghfira kwa sababu tumewauwa bure bila ya sababu, wafuasi wako Waislamu waliokuwa wakiswali na kukuswalia na wewe Mtume wao (SAW), lakini kwa chuki zetu tumewauwa kwa sababu tu walikuwa ni jamaa zako Waarabu wenziyo”! Hakuna maskhara wala mizaha huko twendako. Wahindi pia wamefanywa kisingizio cha kutupiwa taka za ubepari. Ingawa hapana shaka walikuweko mabepari wachache. Uliza nani waliokuwa madobi wa kufua nguo na kupiga pasi; wakienda nayo mirundo ya nguo mpaka Wireless au Saa Teni na kuzifua kwa mikono yao, kuzianika na kungojea zikauke. Wakisha kurudi nazo huzipiga pasi; yote haya ili wajipatie pesa teni, bila ya Inaendelea Uk. 11

AN-NUUR

Yaulizeni myajue, Zanzibar musiyazue

Mwarabu masikini muuza kahawa kabla ya 1964 hata ikapelekea watu wa asili fulani wote kuonekana ni matajiri na wengine kudhaniwa ni masikini. Maelezo haya ndiyo yaliyotanda katika vitabu na makala zilizoandikwa katika majarida na magazeti, na ubaya zaidi ni kuwa fikira hizi zilitapakazwa katika majukwaa ya siasa, tena kwa chuki kubwa sana na kupandisha mori katika hisia za wajinga na hili kusababisha k u u w a w a Wa z a n z i b a r i wengi, na pia wasiokuwa Wazanzibari, bure bila ya sababu. Sote tumesoma na kusikia mara kwa mara kuwa Waarabu walikuwa matajiri wenye mashamba mengi na majumba; Wahindi tunaelezwa kuwa walikuwa mabepari; Waafrika (pamoja na Washirazi) walikuwa mafakiri na kadhalika na kadhalika. Bila ya kufanya utafiti wa kina huwezi kuelewa ukweli na uwongo wa hizi khabari zinazotapakazwa. Inahitajia pia uishi na watu wa sehemu mbalimbali ili uweze kuelewa vipi wanaishi. Namshukuru Subhana waTaala kuwa katika maisha yangu nimeishi Mjini Unguja, nimeishi Pemba, nimeishi mashamba na nikitembea sana Ng’ambo. Pia, nimeishi bara Tanganyika, Kenya na Uganda. Kweli Zanzibar ilikuwa na watu wachache waliojiweza sana kimaisha na kulikuwa pia na idadi ya masikini, lakini wengi zaidi walikuwa na maisha ya wastani ambayo hayakuwa na tafauti kubwa baina yao, na si kweli kabisa kuwa utajiri ulikuwa ni wa watu wa kabila fulani tu na umasikini ulikuwa ni wa watu wa asili fulani tu. Nikukumbusheni mfano mmoja: wenye umri kama wangu mlioishi Unguja mjini nina hakika mtakumbuka kuwa Darajani (ukishavuka daraja kuelekea Ng’ambo) palikuwa wakisimama mbele ya ukuta Waarabu masikini, wengine vipofu, wakiomba. Narejelea tena, hapana shaka kuwa walikuwepo Wa a r a b u w a c h a c h e waliokuwa matajiri, lakini mengi yanayosemwa ni ya uzushi mtupu. Waarabu wamefanywa kama magodoro ya usumba. Kila mara hutandikwa bakora ili mabwana — wanasiasa za chuki – wapate kulala na kulalia magodoro vizuri. Uliza vizuri ni nani

waliokuwa wazegazega wa madebe mazito ya maji kupeleka majumbani ili wapate pesa mbili? Uliza nani waliokuwa wakikokota marikwama zamani kabla ya wengineo? Uliza nani walikuwa mahamali wa kubeba mizigo ya wasafiri bandarini – hata kule kuwakaribisha wageni kwa maneno ya Kiarabu “ahlan byk, ahlan byk” yaani “karibu, karibu” yakageuzwa badaye na kuwa “halambee” na Wakikuyu wakabirua “lam” na “ree” wakiimba “harambee”!? U liza nani w alikuw a wachanja kuni na wauzaji wa makaa. Uliza nani walikuwa wauza kahawa kwa midele barabarani!? Uliza nani walikuwa wakisuka makanda ya kupakilia mizigo!? Angalieni pia picha kwenye makala hii. Ukishamaliza hayo, bado kuna ya “wazamia lulu”; wala usidhani nazungumzia kuzamia lulu baharini, bali naelezea ya wale waliokuwa wakitapisha vyoo na kuingia wenyewe malindini na kuchota viliomo kwa ndoo na kumimina katika mapipa waliyoyaweka juu ya marikwama, na wakishajaza, huyakokota wenyewe marikwama na kwenda kumwaga “lulu” kulikorukhusiwa. Uliza nani waliokuwa wavuvi wa dagaa!? Uliza nani waliokuwa wakiuza papa na nguru wakavu!? Uliza nani waliokuwa wakikodi mashamba ya mikarafuu na minazi, wakiwakodi pia wakwezi na kuwalipa na baada ya kuangua nazi, wakiziokota wenyewe katika makanda ya punda au katika magari ya ng’ombe na kupeleka kwenye janguo!? Mwarabu aliyetoka kwao Omani ndani akakusanya pesa kwa jamaa zake masikini wenziwe na kuagana kuwa atakachochuma watagawana. Mmanga huyo akafunga safari ya miguu au ngamia kwa siku nyingi mpaka kufika kwenye mji ulioko pwani akangojea jahazi na kulipa ujira, akasafiri safari ya mawimbi na miuya ya “mswaliye Mtume” mwezi mzima au zaidi mpaka akafika Unguja, akaenda kwa Sheikh Abdullah bin Suleiman, akapokelewa na kuelezea haja yake. Akaazimwa gari la ng’ombe au akanunua na akatafutiwa shamba la kukodi minazi na mikarafuu kwa miezi au mwaka. Akaajiri wakwezi na watu wa kuchuma karafuu. Akawalipa ujira

10
Ni ala ala jirani, msemo wetu wa ada Lengo kuu kuthamini, ya ujirani ibada Katu si kwa kufurani, inotengua aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani.

Mashairi/Makala UJIRANI WA KUFRU !

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

Usia wa Adinani, kwetu kwao ni saada Si kwa kukhini imani, tena kwa yao irada Bali kwa dini kuwini, na kuilinda aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. Kushiriki Pasakani, ni kiuko la kaida Kisa eti ujirani, usijepata kudoda Twaiwekaje rehani, swahihi yetu aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. Twajitia usungoni, kushiriki ushuhuda Kesho tutajibu nini, kwa ALLAH si kwa buruda Kwalo tujitanibuni, tusikhalifu aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. Ya ala ala jirani, yaendane na aqida Yasiwe ya ujirani, dhidi ya yetu aqida Kushiriki Pasakani, ni hilaki kwa aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. Tuachane ikhiwani, na ya ujahili ada Kwa kuhuluti imani, utatu na tauhida Kulikoni na kwanini, tuikufuru aqida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. Haya shime waumini, kulinda yetu aqida Si kwa mtutu vitani, kwa kughairi fuada Tusije kesho narini, tukasalia halida Tusitengue aqida, kwa nembo ya ujirani. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

NIKAHI YA UWAWARU
Nikahi kuhadithia, ya panya wetu na paka Kila ni pofikiria, ni baki kuhuzunika Mwishowe likanijia, wazo kalamu kushika Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Tama nilijishikia, kwa nikahi kufungika Maajabu ya dunia, pamoja kujumuika Maadui asilia, kulikoni nina shaka Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Si jingine zao nia, zino shakani niweka Tofauti si sawia, ndoani kujumuika Nibashiricho udhia, kama si panya kulika Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Siri ninakuibia, panya upate zinduka Kadhalika na usia, nakupa wa uhakika Kesho utajajutia, kwavyo ‘kija’ kengeuka Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Ebu kipanya sikia, mwenza wako shume-paka Adaye ni kujilia, panya wa ‘homu’ na nyika Ni siri nakuibia, kabla yajakufika Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Ewe panya Malkia, kufuyo katu si paka Hadhiyo wajishushia, kwa kuolewa na paka Kwa hiyo nakuusia, muombe yako talaka Ndoa ya panya na paka, si ndoa bali udhia. Panya ulojifungia, Mwanza si ndoa na paka Umbuzo washadidia, rudi nyumbani haraka Wino umeniishia, bado mwisho sijafika Si ndoa bali udhia, ndoa ya panya na paka. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Inatoka Uk. 1 kuzuiwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) huku kwa upande mwingine Mahakama na wanasheria wakihoji hatua hiyo lakini pia Mahakama Kuu ikishindwa kutoa hukumu ambapo hivi sasa inasubiri kauli ya Mahakama ya Rufaa. Mahakama Kuu ya Zanzibar imesema haitasikiliza kesi inayowakabili viongozi hao wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) hadi pale Mahakama ya Rufani itakapotoa maamuzi juu ya rufani zilizokatwa huko. Upande wa mashitaka wa serikali umekata rufani Mahakama ya Rufani ukipinga maamuzi ya Jaji Fatma Himid Mahmoud anayesikiliza kesi hiyo aliyoutaka upeleke kwa maandishi sababu za kuzuia dhamana ya washitakiwa hao. Mwanasheria wa serikali, Raya Issa Mselem aliiambia Mahakama juzi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Ibrahim Mzee Ibrahim hakuridhishwa na maamuzi hayo ya Mahakama hasa ya kuwasilisha kwa maandishi sababu za kupinga dhamana kwa washitakiwa hao. Alidai kuwa kutokana na hali hiyo DPP ameamua kukata rufani Mahakama ya Rufani. Kwa mfumo wa Mahakama Ta n z a n i a , M a h a k a m a ya Rufani ni suala la Muungano. Hiyo itakuwa rufani ya pili kukatwa na upande wa mashitaka katika kesi hiyo baada ya awali kupinga maamizi ya Jaji Abraham Mwampashi wa Mahakama Kuu Zanzibar aliyefuta maagizo ya Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi likiwemo la kuwanyima dhamana washitakiwa hao. Wakili wa utetezi, Salum Toufiq ameiomba Mahakama kutokubaliana na uamuzi huo kwani upande wa mashitaka unahalifu amri ya Mahakama kwamba kama kulikuwa na sababu za msingi ilikuwa waeleze mapema . Jaji Fatma alisema

Kesi ya Masheikh Uamsho Ni sarakasi, danadana tupu
amesikia maombi ya pande zote mbili hivyo upande wa mashitaka unayo haki ya kukata rufani na atasikiliza kesi hiyo baada ya maamuzi ya Mahakama ya Rufani au zikipita siku 60 bila ya maamuzi. Suala la msingi hapa katika lugha nyepesi ni kuwa Mahakama ilihoji hatua ya DPP kuzuiya dhamana ya washitakiwa na kutakiwa kuwasilisha hoja zake ili mahakama izipime uzito wake. Kwa upande mwingine, DPP naye anakataa kuhojiwa na kutakiwa kuwasilisha mahakamani sababu zake za kuzuiya dhamana za washitakiwa ndio maana anakata rufaa katika Mahakama ya Rufaa. Kwa rufaa hii, washitakiwa wataendelea kukaa rumande hadi hapo rufaa ya DPP itakaposikilizwa katika Mahakama ya Rufaa na kutolewa maamuzi. Swali ambalo pengine linaulizwa ni iwapo ile kanuni kwamba haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokataliwa, inafaa kutumiwa katika suala hili la Masheikh na viongozi wa Waislamu.

Hoja yenyewe ni kuwa jaaliya iwapo mwisho wa yote itaonekana kuwa hapakuwa na haki wala sababu za msingi kwa mujibu wa Katiba ya Nchi; walionyimwa haki yao ya dhamana watalipwa vipi kwa dhulma waliyofanyiwa! Washitakiwa hao ambao wataendelea kusota rumande ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni, Mselem Ali Mselem (52) mkaazi wa Kwamtipura, Mussa Juma Mussa (47) mkaazi wa Makadara na Azan Khalid (48) mkaazi wa Mfenesini. Wengine ni Suleiman Juma Suleiman (66), mkaazi wa Makadara, Khamis Ali Suleiman (59) mkaazi wa Mwanakwerekwe, Hassan Bakar Suleiman (39) mkaazi w a To m o n d o , G h a l i b Ahmada Juma (39) mkaazi wa Mwanakwerekwe na Abdallah Said (48) mkaazi wa Misufini. Wa s h i t a k i w a hao wamefikishwa mahakamani kwa madai ya kuharibu mali, uchochezi, ushawishi na kuhamasisha fujo na kuhatarisha usalama.

VITABU VYA JUMBE THE PARTNERSHIP

Vitabu vya The Partnership kwa Kiswahili vya Alhaj Aboud Jumbe Mwinyi kwa bei ya jumla na rejareja vinapatikana Masomo Bookshop. Kwa mawasiliano piga 0777 464748 au 024 2231048 au fika Masomo Bookshop Zanzibar na kuonana na Nizar.

11
Inatoka Uk. 9 kulaumu wala kulalamika. Uliza pia nani walikuwa wakishona viatu; nani wapakia dongo za kujengea katika magari ya punda; nani walikuwa wakiuza bajia na mbatata njiani; nani walikuwa wakifinyanga vyungu; nani walikuwa wawashi na mafundi wa magari ya moto na ya kukokota!? Uliza, uliza, uliza usichoke kuutafuta ukweli. Ukweli ndiwo utakaokutoa katika utumwa wa kiakili na mawazo na kukuweka katika njia huru. Jee, na maisha ya “walio wengi” Zanzibar, yaani Washirazi yalikuwa vipi? Washirazi wengi waliokuwa wakiishi katika mashamba yao wenyewe na wakitegemea mazao ya mashamba yao na wakijitegemea kwa jasho lao. Wengi wakijituma wenyewe na mpaka leo, kwa jumla, hali ni hivyo hivyo, ila wale waliokubali kudanganywa kwa mamilioni ya pesa za Tanzania na kuyauza mashamba ya koo zao na kujikuta kumbe wameuza mbachao kwa mswala upitao na kujikuta katika hali za majuto mjukuu. Inasikitisha! Wengi ya Washirazi na pia

Makala/Tangazo

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

AN-NUUR

Yaulizeni myajue, Zanzibar musiyazue

MWARABU kinyozi akimnyoa Mswahili Waarabu walioishi shamba hawakuyataka maisha ya mjini ya “kupigana vikumbo.” Walifadhili ngongomwe, sauti za matawi yanapokwaruzana kwa ajili ya kusukumwa na upepo na za majani na ndege. Walifadhili pia na mazao yaliyokuwa mashambani mwao kuliko ghasia za mjini. Mimi hustaajabu sana ninapowaona watu waliosoma, kila pakiandikwa

makala juu ya Zanzibar, khasa kwa Kiingereza, huchukulia kuwa mwandishi anaelewa vizuri anayoyazungumza! Kwanza tutiye katika mizani na kujiuliza iwapo mwandishi kweli aliielewa hali ya maisha ya watu kwa mapana yake au kwa mahala na mazingira aliyoishi na kwa muda aliokuwepo Zanzibar anatuelezea ya utotoni na kwa mtizamo wa kindoto? Pia tunaposoma magazeti, tujiulize iwapo mwandishi kweli anawaelewa Wazanzibari na maisha yao yalivyokuwa kabla ya mavamizi au ndiyo anarejelea kikasuku yale yale ya utumbo wa siasa za ubaguzi na chuki? Na tuulize na masuala mengine muhimu na siyo kupotezewa na kuupoteza wakati wetu bure. Kuwa kila mara tunapiga khatua moja katika kuuelewa ukweli na kurudi nyuma khatua kumi katika kujitia katika mitego ya uzushi wenye khatari mbele, inachokesha sana na kuumiza vichwa. (Makala hii imenukuliwa kutoka katika mtandao wa kijamii wa Mzalendo)

Inatoka Uk.6

Tusipotumia akili zetu vizuri
Kupigana kwao makuchi hawa ndo furaha ya wapiganishaji. Pengine wapiganaishaji hucheza kamari na mwenye kuchi aliyeshinda akapata malipo. Historia ni mwalimu nzuri, tunasoma kwamba kule India wakati wa harakati za kudai uhuru zilizokuwa zikiongozwa na Mahtma Gandhi, wakati huo India ikiwa koloni la Muingereza, wakoloni hawa walikuwa wakiwapiganisha Waislamu na Wahindu ili kujenga hoja ya kutowapa uhuru. Wa l i k u w a w a k i c h i n j a nguruwe kisha wakiwatupa kwenye Misikiti ya Waislamu. K w a h i s i a Wa i s l a m u wakiwashutumu Wahindu kwa kuwatupia nyama haramu, najisi kwenye nyumba zao tukufu za ibada, kisha wakoloni hawa wakichinja ng’ombe na kuwatupa kwenye mahekalu ya Wahindu, Wahindu nao kwa hisia tu, wakawashutumu Waislamu kwamba ndio wanaowauwa m i u n g u y a o ( Wa h i n d u wanaabudu ng’ombe kama Mungu wao), kisha wanawatupa kwenye nyumba zao za ibada! Kwa hisia wakaishia kupigana na kuuwana….mkoloni akazidi kutawala. Hali hii ndio ninayoiona Zanzibar. Matukio ya kumwagia kinyesi visima vya maji, kuchomwa moto nyumba za Masheha, kulipuliwa mabomu ofisi za CCM, tuliyaona mageni yalipoanza miaka 90 kule kisiwani Pemba. Tukawa twaambiwa ni wapinzani, wafukuwa hadi barabara na kuvunja mabomba ya maji. Lakini kisha tukayazoea, na

UMOJA WA WAHADHIRI WA KIISLAMU TANZANIA
Email uwakita@yahoo.com P.O. Box 16106 Dar es salaam /Tel: 0713 276980 / 0715 589502

wazi wazi na kusema, mimi ndio niliofanya jambo kadhaa ili unipe kitu kadha, au utekeleze masharti kadhaa, usipotekeleza nitafanya tena jambo kadha. Sasa matukio yote haya hakuna kikundi, wala mtu alojitokeza kukiri kufanya na kusema amefanya ili apewe nini au anadai nini. Ingefaa sasa tuambiwe magaidi hawa wana madai gani? Tuambiwe, wanaua Mapadri ili wapewe nini na Kanisa Katoliki? Wanaua na kuwamwagia tindi kali Masheikh ili wapewe nini na Waislamu? Nakumbuka nilipokuwa na miaka 12, ilikuwa tukifunga skuli (nilikuwa skuli ya Jadida, Wete), nikienda kwa bibi yangu Pandani kwa Mwewe, kuna mengi niliyapenda huko Pandani, ikiwemo kuchota maji kwenye kisima cha ndoo kwa kutumia “roda”, lakini jambo jengine lililokuwa nikilifanya ni kuamka mapema sana kwa ajili ya mchezo wa kupiganisha kuku. Niliupenda sana mchezo huu! Walipiganishwa majogoo wa kila aina kuanzia makuchi, majogoo upanga n.k. Lakini ugomvi wa makuchi ulikuwa mtamu sana, hawachoki haraka, wajuzi wa kupigana, hawakubali kushindwa, si woga na wepesi wa kupiganishwa. Walipiganishwa makuchi wale bila wenyewe kuwa na sababu ya msingi ya kupigana. Walipiganishwa bila kujuwa kwa nini wanapigana. Walipigana sababu tu wametumwa kupigana.

jamiii ikamjua hasa anayefanya hayo ni nani. Sasa kumezuka jipya, lakini safari hii si Pemba, ni kwa dada yake, Unguja, kumezuka fasheni yake ya kuua viongozi wa dini, wanauliwa Mapadri leo, na kesho wanauliwa Masheikh. Ni lazima tutumie akili zetu vizuri katika kutafakari mambo haya. Tuweke hisia zetu na misukumo ya kiimani pembeni. Tumuombe Mungu wetu atupe hekima ya kuangalia matukio haya kwa jicho la tatu, atupe hekma ya kuwa waadilifu katika kuchambua matukio haya. La sivyo, basi, leo atauliwa Padri John, kwa hisia upande mmoja utasema “Waislamu hao”, kesho atauliwa Sheikh Abdalllah, kwa hisia upande mwengine utasema “Wakristo hao”. Kitakachofuata sihitaji kukieleza hapa, maana wote tunajua! Mungu atunusuru! Wapiganishaji watakuwa wamekaa pembeni wakitutazama tunavyouana kwa ujinga wetu. Watakuwa wanasubiri kuleta misaada ya kibinaadam (kama wanavyoita wenyewe), watasubiri kuleta majeshi yao kusimamia amani, watapata habari za kutangaza kwenye vyombo vyao vya habari. Zanzibar itakuwa maarufu kama ilivyo Afghanstan, Iraq, Syria, n.k! Watapata sababu za kutosha za kuifanya Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania. Utamaduni na asili ya Zanzibar ndo itapotea kabisa. Tusikubali kufanywa makuchi tukapiganishwa sie kwa sie.

Kutokana na matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea dhidi ya dini yetu, Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania pamoja na mambo mengine tumekusudia kufanya kongamano kubwa la kihistoria litakalo jibu waraka wa wakristo uliotolewa hivi karibuni, na kusomwa katika misa ya Pasaka Nchini, uliyotayarishwa na Baraza la Maaskofu, waraka huo wenye uchochezi dhidi ya Waislamu Nchini. Kongamano hilo litakalofanyika siku ya Jumapili tarehe 14/4/2013 kuanzia saa 6:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni katika Msikiti wa Kichangani (T.I.C) Magomeni, Masheikh Wahadhiri na waharakati mbali mbali watakuwepo. Waislamu wote mnaombwa kuhudhuria kwa wingi na kila mwenye kupata taarifa hii amuarifu na mwenzie ni muhimu kwa ajili ya kulinda na kutetea heshima ya Dini. Kurugenzi ya Habari na Mambo ya Dharura. Umoja wa Wahadhiri wa Kiislamu Tanzania

KONGAMANO

AN-NUUR
12
Kutanika saa sita mchana eneo la Lafayette, 1600 Barabara ya Pennsylvania, NW Zaidi ya watu 5,000 wameuawa nje ya sheria kwa mashambulio ya midege ya drone ya Marekani katika miaka michache iliyopita, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watoto kati ya raia wengi wa kawaida ambao wameuawa na mitambo hii ya kujiendesha yenyewe na kuua. Wakiwa wameketi katika ofisi zao maili elfu kadhaa kutoka walengwa wao, waendeshaji wa Marekani wanapanga kikawaida tu ‘kubonyeza kitufe’ na kuwaua walengwa hao ardhini ambao hawajui nini kinaendelea, kwa makombora ya ‘moto wa jehanamu’ yanayoangushwa kutoka ndege zisizoonekana za drone. Nchini Pakistan na Afghanistan, wanavijiji wamefanya maandamano dhidi ya midege ya drone baada ya watoto wao kuunguzwa kabisa na mabomu hayo wakiokota kuni au kulima katika mashamba ya jirani. Serikali ya Marekani inafanya kazi kama kundi la wauaji, ikiwaruhusu rais na viongozi wa jeshi kuandaa orodha za siri za watu ambao wamechaguliwa kwa kuuawa. Hakuna mkondo wa sheria, hakuna mashitaka, hakuna ushahidi – watu hao wanachaguliwa kuuawa na wanauawa, na raia wengine walioko

JAMADUL AWWAL 1434, IJUMAA APRILI 12-18, 2013

Usikose nakala yako ya AN-NUUR kila Ijumaa

Midege ya drone ya Marekani itoke Afrika
Itoke pia Arabuni, Asia na kote kwingine! Jumuika mbele ya Ikulu ya Marekani

karibu nao wanakufa. Midege ya drone ndiyo silaha inayopendelewa. Katika karne ya 19, ilikuwa ni mbinu ya kawaida kwa mabeberu kutumia boti zenye silaha nzito kuzunguka duniani na kupata wanachotaka, wakijibu upinzani kwa matakwa yao kwa risasi na mizinga ya boti hizo. Kutumia au tishio la kutumia nguvu za jeshi baharini kulitumiwa na Uingereza, Marekani na mataifa mengine ya kibeberu kulazimisha mikataba ya kinyonyaji ya biashara na makubaliano ya kisiasa yaliyolazimishwa mataifa mbalimbali duniani. Mipango ya serikali ya Marekani ya kutumia midege ya drone

MIDEGE ya drone ya Marekani inafuatilia malengo la Marekani); Akbar ambayo ni sawa na yale Muhammad, mwakilishi ya boti za bunduki nzito. wa kimataifa wa kundi la Inawezesha Marekani Taifa la Uislamu; Jukwaa kusogeza zaidi uwezo l a K u a m s h a U p y a wake wa kijeshi juu ya Uzalendo wa Kiafrika; nchi yoyote ambayo Wakazi Nje wa Afrika h a i n a u w e z o , a u wanaotaka Demokrasia uthubutu, wa kuiangusha na Maendeleo; CRI kwa risasi midege hiyo. PanAfricain; Jumuisho Jiunge na sisi katika la Wagambia wapendao Ikulu ya Marekani kwa Demokrasia wakaao matembezi na mkutano W a s h i n g t o n D C ; w a h a d h a r a h a p o Ramsey Clark, zamani Mkuu wa Jumamosi, Aprili 13 Mwanasheria Marekani; Wapiganaji kuwezesha dunia ielewe wa Zamani Watakao kuwa watu wa nchi hii Amani; Kanali Ann (Marekani) wanataka Wright; CODEPINK; “ M i d e g e y a d r o n e Baraza la Mahusiano ya itoke Afrika, Mashariki Marekani na Uislamu; ya Kati, Asia na kote M k u r u g e n z i M k u u wa Baraza hilo; Nisa kwingine !” Wa l i o t i a s a i n i n i Muhammad, mwandishi, gazeti la Mwito wa pamoja na: M f u n g a m a n o Mwisho; Jared Ball, w a J I B U ; C y n t h i a mwendesha kipindi McKinney, Mwakilishi cha maoni redioni; wa zamani (Bunge WPFW (Pacifica);

Mchungaji Graylan H a g l e r, m c h u n g a j i mwandamizi; Kanisa la Umoja wa Kristo la Plymouth; Imam Mahdi Bray, Jukwaa la Uhuru; Ve r h e y d e n - H i l i a r d , mkurugenzi mtendaji, Mfuko wa Ushirikiano wa Haki kwa Jamii; Zaki Baruti, shirika la Universal African People’s Organisation; Kamati ya Urafiki ya Irani na Marekani (AIFC), Peta Lindsay, Chama cha Ujamaa na Ukombozi; Uhuru Haiti; Kamati ya Elimu ya Siasa na Harakati – Chuo Kikuu cha Howard; Philly Dhidi ya Vita; Wanafunzi Wapenda Haki kwa Palestina – Chuo Kikuu cha Temple; Ainisho la Kusaka Amani, Chuo Kikuu cha Temple; na wengine wengi.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful