JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MATUMIZI MABAYA YA MAWASILIANO NA UDANGANYIFU KATIKA USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI NCHINI NIKOSA LA JINAI 1. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi cha miaka kumi iliyopita zimekuwa sana na kuwafikia watu wengi zaidi. Ni ukweli usiopingika kuwa watanzania wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, hususani katika mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji, intaneti na huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika. 2. Aidha kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi hususani matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali. Matumizi haya yamewanufaisha watanzaia kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania. 3. Pamoja na maendeleo haya chanya kwa nchi yetu, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo ugomvi, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla. 4. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inawatahadharisha wananchi kwamba ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010. Wananchi wanashauriwa kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri na kuhakikisha tunadumisha amani na upendo miongoni mwa watanzania.

5. Aidha mamlaka inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa kusajili laini yako ya simu, kwa kutumia utambulisho wa udanganyifu pia ni kosa la jinai. Mtumiaji wa huduma za mawasiliano unatakiwa kwenda kwa mtoa huduma au wakala wake ukiwa na kitambulisho sahihi chenye picha yako na kutoa taarifa sahihi. Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, kifungu cha 131, kimeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika namba ya simu isiyosajiliwa. Adhabu ya faini ya shilingi laki tano (Tshs 500,000.00) au kifungo cha miezi mitatu itatolewa kwa yeyote atakayekiuka sheria hii.

6. Kuanzia tarehe 1 Juni 2013 saa sita usiku, laini zote za simu ambazo hazijaanza kutumika zilifungwa (locked) na haziruhusiwi kutumika hadi mtumiaji atakapoisajili laini yake mpya kwa watoa huduma. Kama kuna mwananchi atakaenunua laini, na kuweza kuitumia bila ya kuisajili, anaombwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

7. Watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawakuwa wamesajili namba zao za simu wafanye hivyo mara moja. Ifahamike kwamba ilipofika tarehe 10 Julai 2013 saa sita usiku, laini za simu ambazo zilikuwa zinatumika na zilikuwa bado hazijasajiliwa hadi wakati huo, zilifungwa. Kufungua laini iliyofungwa, mtumiaji atapaswa kwenda kwenye ofisi ya mtoa huduma wake au wakala wake kusajili upya na kuthibitishwa ili laini yake ifunguliwe. 8. Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta na ya Taifa kwa ujumla. 9. Faida za kusajili laini ya simu ni nyingi zikiwemo usalama katika huduma za kutuma na kupokea pesa kwa mitandao ya simu. Kununua na kulipia gharama mbalimbali zikiwemo za bili za umeme, maji, na ushuru na pia kusaidia upelelezi iwapo kuna matumizi mabaya ya simu. 10. jinai: Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la

a) Kuuza laini za simu kama wewe si wakala wa mtoa huduma: Iwapo mtu atakamatwa na kutiwa hatiani akiuza laini za simu ikiwa yeye si wakala wa kampuni ya simu atahukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kufungwa jela miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja. b) Kutumia simu isiyosajiliwa: Mtu yeyote anayetumia simu isiyosajiliwa anatenda kosa la jinai na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi laki tano, au kifungo cha miezi mitatu jela. c) Kutoa taarifa za uongo wakati wa kusajili namba ya simu: Mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo akijua kuwa taarifa hizo si za kweli anatenda kosa la jinai na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu au kifungo cha miezi kumi na miwili au adhabu zote kwa pamoja. d) Kumsaidia mtu mwingine atende kosa kwa mujibu wa sheria za mawasiliano naye anatenda kosa na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi milioni tatu au kufungwa jela miezi kumi na miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja. e) Kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani, kugombanisha watu, kufanya uchochezi wa kidini au kisiasa, kueneza chuki, kusambaza uongo na kuleta vurugu katika jamii ni kosa la jinai na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobanika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria. f) Mwananchi ukipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kasha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu. Imetolewa na:

MSEMAJI MAMLAKA YA MAWASILIANO MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA 26 July 2013

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY

PRESS RELEASE MISUSE OF COMMUNICATION SERVICES AND SIMCARD REGISTRATION USING FALSE IDENTITY IS A CRIMINAL OFFENSE
1. The Communication services uses in the country has grown in past ten years and reach a larger number of people. It is a fact that more Tanzanians benefits in the use of communications value added services, especially mobile telephony, broadcasting, internet use, as well as mobile money banking. More people use their mobile phones for a range of services, from voice, SMS, and many more.

2. There has been an increase of internet use for Tanzanians. More are using social networks such as Facebook, Twitter, BBM and read from different blogs. The use of internet and especially the use of social networks has helped many Tanzanians to learn, get informed and educated for their daily issues in life including creating harmony among citizens. 3. Much as many have benefitted with the development of ICT’s in the country, there has been misuse of communications services by a few, especially in the mobile telephony use, social networks, radio broadcasting as well as Television broadcasting. Some of these have been used to create disharmony, creates misunderstanding in the

society, telling untruth stories and destabilizes a section of the society and its development. 4. Tanzania Communications Regulatory Authority wishes to remind all consumers and the general public that, it is a criminal offence to misuse communication services in Tanzania as stipulated in the Electronic and Postal Communications Act of 2003. The Authority would like to inform the general public that if used as intended, the communications services are an integral part of the country’s development and can create harmony and benefits each and every one of us.

5. The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) also cautions the public that it is a criminal office to register your SIM card using false or untrue identity. As a user of mobile phone service, you are advised to visit the office of your service provider or their agents for registration with your photo identity for verification. You are required to provide correct information. The Electronic and Postal Communications Act (EPOCA) of 2010, under section 131, stipulates that it is a criminal offence for any person who knowingly uses or causes to be used an unregistered SIM and shall be liable on conviction to a fine of five hundred thousand Tanzanian shillings (Tshs. 500,000.00) or imprisonment for a term three months.

6. Effective midnight of 1st June 2013, all new unused SIM cards were locked; it is prohibited to use the SIM card and will only be activated upon registration and verification. TCRA appeals to the general public to report to the Authority, if there is anybody who is able to buys a SIM card and makes a call without first registering it.

7. The general public is hereby informed that, as from midnight of 10th July 2013, all unregistered SIM cards which were in use were disconnected. To activate disconnected SIM card, one has to go through registration and verification process to be re-activated.

8. Consumers and the public are hereby urged to support the ongoing efforts to enforce SIM card registration. The success of SIM card registration will lead to enhancement of security, welfare of Tanzanians and the development of the communications sector. 9. SIM Card registration exercise is of multiple benefits like electronic money transfer services (sending and receiving money through mobile phones). Settlement of bills like buying of electric charges, payment of water bills and other revenues.

THE Authority wishes to remind the general public that it is a criminal offence to;

a) Selling SIM cards without authority of Network Service Licensee:
Any dealer or person who sells or distributes any SIM– cards without authorization of the appropriate Network Service Licensee shall be guilty of an offence and be liable on conviction to a fine of seven million Tanzanian shillings or to imprisonment for a term of two years or to both. Section 125 of the Act.

b) Failure to give satisfactory account of mobile telephone or SIM card:
Any person who is found in possession of any mobile telephone or SIM - card in regard to which there is reasonable suspicion that it has been stolen and is unable to give a satisfactory account of such possession, commits an offence and is liable on conviction to a fine not exceeding five hundred thousand Tanzanian shillings or to imprisonment for a term not exceeding three months. Section 126 and 127.

c)Tempering with mobile Telephone or Sim Card
Section 129 of the Act provides that; Any person who, intentionally and unlawfully in any manner-tempers, modifies, alters, reconfigures or interferes with mobile telephone or SIM card or any part. Also, any person who) reverse e ngineers, decompiles, disassembles or interferes with mobile telephone or SIM card, or any part thereof,commits an offence and shall be liable on conviction to a fine of thirty million Tanzanian shillings or to imprisonment for a term not exceeding ten years or both.

d)Failure to record sale of mobile telephone and SIM card:
Section 130 of the Act maintains that, any person who sells or in any other manner provides, any mobile telephone or SIM card to any other person, natural or legal, without recording the particulars of that person as required by section 102 of this Act, commits an offence and on conviction shall be liable to a fine of three million Tanzanian shillings or to imprisonment for a term of twelve months or to both. • Where the offender is a network service licensee or operator

it shall be liable to a fine of fifteen million Tanzanian shillings. • Where the offender is an employee of the Network Service licensee or a legal person, he shall be liable to the same penalty as provided under sub-section (1).

e) Use of unregistered SIM Card
Any person who knowingly uses or causes to be used an unregistered SIM card commits an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding five hundred thousand Tanzanian shillings or imprisonment for a term not exceeding three months. Section 131

f) Provision of False information or statement
Any person who furnishes information or makes a statement knowing that such information or statement is false, incorrect or misleading or not believing it to be true, commits an offence and shall be liable on conviction to a fine of three million Tanzanian shillings or to imprisonment for a term of twelve months or to both. Section 132

g) Obstruction to perform duties
Any person who obstructs, hinders or interferes with an authorised person to execute any direction issued under this Act or assists with the execution thereof, commits an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding three million Tanzanian shillings or to imprisonment for a term of twelve months or to both. Section 133 h) Uses of any communication services to crate dishamony, creating rift in the society, inciting, spreading lies and untruth claims, is a criminal offence. If you receive a message likely to cause disharmony, false or one that may incite others, report to relevant authority and delete the message. Do not forward such messages as you will be part of the criminal offence.

Issued by:
SPOKESPERSON

TANZANIA COMMINICATIONS REGULATORY AUTHORITY 26th July 2013

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful