ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Toleo la Pili 1

Je, Kitanzi cha Dodoma chashindwa kumnyonga Mansoor?

2

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

3

YALIYOMO

5

Othman Masoud:Jemedari wa kupigania haki
Msimamo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman (tazama Ukurasa 8), ni msimamo wa kizalendo, wa kupigiwa mfano na unaofaa kuigwa na wakuu wengine wa Serikali wenye hisia na nchi yao. chembe ya woga kwa kuwakwaa wakubwa wenye sera zinazopingana na msimamo wake. Wale wenye kumbeza na waliojitokeza kimbele mbele kumshauri Rais Ali Mohamed Shein amfukuze kazi wamekosea. Kwa kuuchukua msimamo aliouchukua Othman Masoud ameonyesha kuwa hana ubinafsi. Hayuko tayari kuiuza nchi yake kwa vijipesa viwili vitatu au kwa ulwa wa aina yoyote ile. Alipokuwa analihutubia kongamano la Baraza la Katiba la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar, Othman hakutafuna maneno, hakujifanya kibogoyo alipoutamka ukweli na wala hakubabaika kwa namna yoyote ile. Sauti yake ilijaa hamasa ya uzalendo wake; aliyaeleza mambo kwa busara na hikma, tena kwa taratibu. Kwa ufupi aliililia na kuipigania nchi yake. Hamna shaka yoyote kwamba yeye ni jemedari mzuri wa kuipigania ardhi iliyozikiwa kitovu chake. Inafaa tumshukuru Mungu kwani kila uchao anachomoza jemedari mwingine wa kuipigania Zanzibar yetu. Kila mmojawao akili kichwani. Vipi tushindwe kwenye vita hivi? Othman Masoud anautetea muundo wa Muungano utaokuwa na Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Katiba iliyo chini ya Jaji (Mstaafu) Joseph Warioba. Pamoja na kuubainisha msimamo wake kuhusu suala la Muungano Mwanasheria huyo Mkuu zaidi aliutumia wadhifa wake na uweledi wake wa mas’ala ya kisheria kutuelimisha Wazanzibari wenzake kuhusu mambo ya Katiba na jinsi Zanzibar inavyopunjwa ikiwa ndani ya Muungano wa serikali mbili kama ulivyo sasa chini ya ule aliouelezea kuwa “ukoloni kasorobo”. Alieleza pia kwamba muundo uliopo wa Muungano ndio wenye hatari ya kuuvunja Muungano kinyume na wanavyofikiria wahafidhina wa CCM/ Zanzibar na wale walio Bara wanaotishwa na wahafidhina hao. Ninaamini kabisa kwamba itikadi halisi ya wahafidhina hao ni kuendelea kuwa na madaraka ili wayatumie madaraka yao kujichumia mali. Huo ndio mkakati wao na hiyo ndiyo hali halisi ilivyo. Aghalabu watu wenye kuipenda nchi yao na walio tayari kujitolea mhanga kwa sababu ya nchi yao huwa hawawajali hao wahafidhina. Huwa hawawatii maanani. Wanafanya hivyo kwa sababu katika nyakati kama hizi za uwazi na demokrasia watu wa sampuli ya wahafidhina wetu wenye kuonya kuhusu ‘maafa’ mara nyingi, kama si zote, huwa ndio wasioisoma vizuri historia. Matokeo yake ni kwamba huishia kutupwa katika debe la taka la historia. Kwa upande mwingine, watu wa sampuli ya Masoud Othman, hata kama awali watakumbwa na misukosuko, misukosuo hiyo huwa ya mpito tu kwani huishia kubebwa na umma na kushangiriwa kwa ushindi wao kwa sababu daima wanakuwa wanapigania haki. - Ahmed Rajab
Zanzibar Daima Online Collective MHARIRI MKUU Mhariri: Ahmed Rajab Email: ahmed@ahmedrajab.com MHARIRI MSAIDIZI Mhariri: Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com MSANIFU MKUU Graphic Designer: Hassan M Khamis Email: hassan@zanzibarimage.com

Kutoka kwa Mhariri

12

62

8 10

Ni nadra siku hizi, hasa nchini mwetu, kuwaona au kuwasikia viongozi wenye vyeo vikubwa kama hicho cha Mwanasheria Mkuu wakijitokeza wazi, tena bila ya woga, kuitetea misimamo inayopingana na ile ya wakubwa wa nchi. Hivyo, Mheshimiwa huyu yuko katika tabaka la wale waliojitolea kuipigania nchi yao. Huo ndio uzalendo. Tena ni uzalendo wa hali ya juu. Si tu kuwa mtu ana mapenzi na nchi yake lakini pia kuwa ana moyo wa kujitolea kuipigania nchi yake na kuwa tayari kuziondoa, kuziweka upande au kuzipuuza tafauti zozote zilizopo — ziwe za kidini, za kikabila za kichama au za kiitikadi za kisiasa — baina yake na wananchi wenzake. Daima anakuwa anaiweka mbele nchi yake, naliwe liwalo. Othman Masoud ameudhihirishia ulimwengu na muhimu zaidi amewadhihirishia Wazanzibari wenzake kwamba yeye ni mzalendo wa aina hiyo. Tena ni mtu mwenye kujiamini. Nafikiri sababu inayomfanya ajiamini ni kuwa anaamini kwa dhati kwamba anaitetea haki. Hataki kuona dhulma inatendeka baina ya nchi mbili zilizo katika Muungano. Hataki kuiona nchi moja inaidhalilisha nyingine. Huko kujiamini kwake ndiko kunakomfanya asiwe na hata

WAANDISHI
Mohammed Ghassani Email: kghassany@gmail.com Mauwa Mohammed Email: mauwa100@yahoo.com Jabir Idrissa Email: jabirgood@yahoo.com Othman Miraji Email: mwinjuu@hotmail.com Hamza Rijaal Email: mzeeshari@hotmail.com Said S Salim Email: sssalim47@yahoo.com WASAMBAZAJI mzalendo.net zanzibardaima.com zanzibardaima/facebook MATANGAZO Kwa matangazo tafadhali wasiliana nasi kuptia: Hassan M Khamis Phone: +44 7588550153 Email: hassan@zanzibarimage.com WASILIANA NASI Tafadhali tuandikie maoni yako kupitia Email Email@zanzibardaima.com JARIDA HILI HUCHAPISHWA NA Zanzibar Daima Collective 233 Convent Way - Southall - Middlesex UB2 5UH United Kingdom Nonnstr. 25 53119 Bonn Germany

14

ššMwenyewe aamua kukaa kimya, nyota yake kisiasa yazidi kung’ara ššWengi wamuweka kundi la Jumbe, Seif ššMoyo asema hakutendewa haki

Mansoor apelekwa machinjioni Dodoma
W
Na Jabir Iddrisa
akatiI Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ikikutana mjini Dodoma huku ikitarajiwa kulijadili suala la Mwakilishi wa Kiembe Samaki, Mansoor Yussuf Himidi, imefahamika kuwa mwenyewe mwanasiasa huyo anaijua vyema hatima yake kisiasa. wa jungu la kufukuzwa kutoka CCM kupitia kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (KM-NEC) ya Zanzibar, bado ameamua kutosema lolote kuhusu hatua hiyo na mustakbali wake kisiasa. Hadi kufikia jana (Ijumaa) usiku Mansoor alionekana kwenye mitaa ya mjini Zanzibar, jambo linalomaanisha kwamba hakuwa ameitwa au amekwenda Dodoma kujitetea. Hilo la kutokuwapo mwenyewe Dodoma kujitetea, huenda likazusha uhalali wa kisheria wa NEC kumuadhibu mwanachama wake bila ya kwanza kumsikiliza. “Kimsingi, hawawezi kumfukuza moja kwa moja bila ya kwanza kumuita wakamsikiliza. Wakifanya hivyo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa CCM kumuhukumu mwanachama wake bila mwenyewe kuwapo,” kimesema chanzo hicho. Hata hivyo, chanzo chengine ndani ya kikao cha NEC imeliambia jarida hili kwamba suala la kumwita Mansoor kujieleza halina mantiki kwani kuna taarifa ya kamati ya maadili ya Chama ambayo imeambatanishwa na barua ya Mansoor kwa Katibu Mkuu wa CCM ambayo chanzo hicho kinadai kwamba Mansoor amesema kuwa yupo tayari kufukuzwa au kunyongwa

4

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

5

‘‘Akifungua Baraza la Katiba la CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kwamba wenye mawazo mbadala katika CCM juu ya Rasimu ya Katiba wavumiliwe, maana wote wakiwa na mawazo mfanano, huo sio mjadala. Naye Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, anaripotiwa kumueleza wazi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, katika kikao cha CC kwamba anachokifanya Zanzibar kitakiuwa Chama.” - Chanzo cha ZDOnlineo.’’

lakini sio kubadili msimamo wake kuelekea Muungano wa Mkataba.”Mimi najua lazima jambo hilo lije. ila kukubaliwa au kukataliwa kutategemea kikao,” kimefafanua chanzo hicho. NEC inakutana leo Jumamosi na kesho Jumapili kwenye ukumbi wake wa White House Mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake , Rais Jakaya Kikwete. Na kwa mujibu wa Katibu wa Itkadi na Uwenezi wa CCM, Nape Nnauye, ajenda kuu ya kikao ni kijadili maoni ya CCM juu ya rasimu ya katiba mpya. Inasemekana hapo ndipo patakapopokelewa pendekezo lililotoka Kamati Maalum baada ya kushindikana kumfukuza Mansoor palepale kwa vile suala lake liliwagawa wajumbe. Katika mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, mjadala juu ya kufukuzwa uwanachama Mansoor lilikaribia kukigawa chama hicho mapande mawili mbele ya Makamo Mwenyekiti wake, Dk. Ali Mohamed Shein. Wapo waliomkingia kifua kuwa hajatenda kosa lolote kwa msimamo wake wa kutoa maoni anayoyahisi ndiyo, na kwa kweli si peke yake katika wanachama anayetoa msimamo waziwazi; huku kundi jingine likimsakizia kuwa amezidi kipimo na anakivuruga chama. Dk. Shein ndiye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ameunda Baraza la Mawaziri kwa kuzingatia mfumo wa serikali ya Umoja wa Kitaifa ulioidhinishwa na Baraza la Wawakilishi baada ya kuridhiwa na wananchi kupitia kura ya maoni iliyoukubali kwa asilimia 66.4. Mansoor aliyeomba apumzishwe majukumu ya uwaziri baada ya uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2010, amebaki kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, na kuwa mmoja wa wana-CCM wachache ndani ya Baraza wanaotoa maoni yao kwa uhuru mkubwa, ukimuuliza, husema: “Kwa kweli sina maoni.”

Hata mwandishi wa habari hizi alipomuuliza kwa njia ya simu kama anadhani umekuwepo mkakati tangu hapo kabla, wa kumfukuza chama, anasema, “Kwa hakika mimi sijui lolote ndugu yangu.” Amefunga kazi kabisa na haongezi neno. Mansoor alijadiliwa kinagaubaga katika kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (KM-NEC-CCM) kilichoketi wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Ofisi Kuu za chama Kisiwandui baada ya kuwasilishwa yale yalioitwa “mashtaka ya utovu wa nidhamu” dhidi yake. Duru za kisiasa ndani ya CCM zinasema mashtaka hayo yaliandaliwa kwa minajili ya kumtia adabu anaonekana kuwa mtovu wa adabu kwa chama kwa kutoa kauli na maelezo yanayokiuka sera na ilani ya CCM. Mansour amekuwa mstari wa mbele kupigania Zanzibar yenye “mamlaka kamili” kama dola inayojitegemea tangu alipoanza kujitokeza hadharani kwenye vikao vya Baraza la Wawakilishi, akisema, “Mimi siungi mkono Muamsho (Uamsho), lakini kwa hii kaulimbiu yao ya Tuachiwe Tupumue, nakubaliana nao moja kwa moja.” Akiwa mjumbe wa Baraza hilo anayewakilisha jimbo la Kiembesamaki, Wilaya ya Mjini, Unguja, Mansoor hana wadhifa mkubwa katika chama tangu pale alipoondolewa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti, Katibu wa Uchumi na Fedha wa Halmashauri Kuu, upande wa Zanzibar. Wakati huo alikuwa ameshapoteza wadhifa wa uwaziri na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi (BLM) kwa kuwa ilisemekana alimuomba Rais Shein, asimfikirie kuwa mmoja wa mawaziri wake atakapounda serikali mpya. Kutokana na nyendo zake nje ya chama akitumia mwamvuli wa Kamati ya Maridhiano inayoongozwa na Mzee Hassan Nassor Moyo, viongozi wenzake

Uchunguzi wa Zanzibar Daima Online umegundua kwamba hata kama haonekani kushughulika sana, hilo linatokana na kuvuta kwake subira ili kuyaingia mwilini maji kwa vile kwa kupima hali halisi ilivyo, ni kama alishayavulia nguo. Chanzo cha kuaminika ndani ya CCM kimeliambia jarida hili kwamba Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, yupo mjini Dodoma, na ingawa chanzo hicho hakikutaka kuthibitisha, wengi wanasema kwamba Karume amekusudia kutumia nguvu yake kumtetea Mansoor ikiwa NEC itaamua kumjadili. “Siwezi kusema kwamba Karume anakwenda kutetea, lakini najua kuwa suala la Mansoor halitakuwa rahisi kiasi hicho.” Kilisema chanzo hicho. Mansoor, mwanasiasa kijana na mwenye kujiamini ambaye katikati ya wiki iliyopita alipiki-

“Akiwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi anayewakilisha jimbo la Kiembesamaki, Wilaya ya Mjini Unguja, Mansoor hana wadhifa mkubwa katika chama tangu pale alipoondolewa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti, Katibu wa Uchumi na Fedha wa Halmashauri Kuu upande wa Zanzibar.”

Inaendelea Uk. 6

6

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Magazetini kwa Ufupi
ya Katiba mpya kumekuwa na uhuru wa wanachama wa CCM kutoa maoni yao na ndivyo Halmashauri ilivyosema,” alisema kiongozi mmoja ndani ya Sekretarieti ya CCM Makao Makuu, Dodoma. Ameongeza: “Wengi wetu hatuamini kama huu ni wakati mwafaka wa kufukuzana eti kwa sababu tu mtu anasimamia maoni au msimamo wake kuhusu masuala haya ya mabadiliko ya Katiba. “Hali ni tofauti sana na wengine wanavyofikiria. Wengine tutajitahidi kusaidiana kuondosha mitizamo hii ya kufukuzana hata pasipo na sababu ya msingi. Haiwezekani mtu akisema tu maoni yake afukuzwe chama. Huu ni wendawazimu.” Kauli ya kada huyo kutoka Zanzibar imeonesha kuwa haitakuwa rahisi kuishawishi NEC kukubali pendekezo la Kamati Maalum ya Zanzibar kumfukuza uanachama Mansoor. Ofisa mwandamizi ndani ya ofisi kuu za CCM Lumumba amesema chama kiko makini kipindi hichi katika namna ya kuendesha siasa hata ndani ya chama kwa sababu “kutoa maamuzi holela kutakidhoofisha kuliko kukijenga.” Mjumbe mmoja wa NEC kutoka Bara amesema “Angalia hali ya mtafaruku Bukoba Mjini tu. Chama kimewekwa katika mtihani mkubwa kwa kufukuzwa madiwani. Matokeo yake viongozi wa juu wamelazimika kutunishiana misuli, wa mkoani wakitetea uamuzi huo na wa makao makuu wakiupinga. Mambo hayako rahisi kama wengine wanavyofikiria,” alisema mjumbe huyo. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ofisi kuu za CCM Lumumba, waraka wenye mapendekezo ya Kamati Maalum ya NEC ya Zanzibar yanayohusu hatima ya Mansoor umetinga ngazi ya juu. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ya Zanzibar, Mzee Hassan Nassor Moyo, amenukuliwa akisema kwamba kama CCM itamfukuza uanachama Mansoor itakuwa haikumtendea haki, kwani kile kinachodaiwa kuwa ni kosa lake la kupingana na sera ya CCM ya Muungano wa Serikali Mbili, si jambo sahihi. “Kama wameamua kumfukuza, mimi nasema ni jambo ambalo si sawasawa kwa sababu alichokifanya Mansoor ni kile kilichomo kwenye sheria na katiba za nchi. Ametoa maoni yake kwa mujibu wa ruhusa iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar pia. Hii ni haki yake ya kiraia.” Aliliambia shirika la utangazaji la Ujerumani, Deutsche Welle kwenye mahojiano yaliyorushwa saa 12 jioni Alhamis.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

7

Inatoka Uk. 5
wengi wakimchukulia kama mwasi wa sera za chama zinazoendelea kutii mfumo wa serikali mbili ndani ya Muungano. Si ajabu basi, jina lake lilipotajwa katika mashtaka ya kukiuka maadili ya uongozi, majina makubwa makubwa yalikuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati Maalum waliomsema vibaya na kumshutumu kuwa amekisaliti chama kilichompandisha hadhi. Wa kwanza aliyeongoza kampeni ya kutaka Mansoor afukuzwe uanachama alikuwa Borafia Silima Juma, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini. Borafia alisema tangu awali Mansoor hakuwa mwanachama wa CCM isipokuwa aliingizwa na shemeji yake, Amani Abeid Karume, alipokuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar. “Alipewa madaraka makubwa huku akifahamika kuwa ni mfuasi wa chama pinzani (CUF),” Borafia alinukuliwa kusema katika kikao cha Kamati Maalum kilichomalizika usiku wa manane. Hoja hiyo iliungwa mkono na Makamu Mwenyekiti wa WAZAZI Zanzibar, Dogo Iddi Mabrouk aliyesema kuwa umaarufu wa Mansoor  kisiasa ulitokana na nguvu ya CCM siyo yake binafsi. “Hana ubavu wa kushinda uwakilishi jimbo la Kiembesamaki hata akifukuzwa uanachama leo… hakuna haja ya kuendelea kumbembeleza mwanachama ambaye si mtii wa Katiba ya CCM na misimamo yake. Kubaki na wanachama wa aina ya Mansour ni hatari kwa uhai wa CCM,” alisema Dogo. Miongoni mwa wajumbe waliomkingia kifua Mansoor alikuwa Machano Othman Said ambaye alisema kumfukuza uanachama Mansoor itakuwa ni kumuonea kwa sababu anatoa maoni yake binafsi kama wanavyotoa wanachama wengine kuhusu utaratibu wa kupatikana kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano. Uchunguzi wa Zanzibar Daima Online umebaini kuwa si viongozi wengi wa juu walio radhi Mansoor afukuzwe kutoka CCM. Tangu juzi mwandishi wa makala haya amejitahidi kukutana na viongozi wa juu wa CCM na baadhi yao akizungumza nao kwa simu, na wengi wao wamethibitisha kuwa si rahisi Halmashauri Kuu ya Taifa kuidhinisha kumtema Mansoor. “Angalau kwa sasa sioni uwezekano wa NEC kuidhinisha kumfukuza mwanachama mwenye hadhi kama yeye. Na ujue tangu kuzinduliwa kwa rasimu ya awali

Ujumbe wa viongozi na wataalamu 20 kutoka China unatarajiwa kuwasili Zanzibar hivi karibuni ili kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika sekta ya uvuvi. Hayo yalisemwa na Balozi mdogo wa China, Chen Qiiman, alipokwenda kuzungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ofisini mwake Vuga, Unguja.

China yaombwa kuwekeza kwenye sekta ya viwanda Zanzibar
Balozi Chen aliahidi kwamba China itaendelea kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo visiwani Zanzibar.

Dk. Shein azindua maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar
Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, liliripoti Zanzibar Leo Agosti 16. Dk.Shein aliyasema hayo wakati wa hotuba yake ya uzinduzi wa sherehe hizo huko mjini Unguja na aliwataka wananchi wadumishe umoja na mshikamano walionao. Alisema sherehe hizo ni kwa Wazanzibari wote, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kikamilifu ili kuonesha umoja na mshikamano uliopo nchini. “Leo tarehe Agost 15, nachukua fursa hii kutamka kwamba maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yamezinduliwa rasmi, nakutakieni ushiriki na maandalizi mema” alisema Dk. Shein. Kauli mbiu ya sherehe hizo ni “Tudumishe Amani na Maendeleo Mapinduzi Daima.”

Kwa upande wake, Balozi Iddi aliiomba Serikali ya China kujikita katika uwekezaji wa sekta ya viwanda Zanzibar. ,Alisema China ni miongoni mwa nchi zilizosimama mstari wa mbele kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar

baada ya Mapinduzi ya 1964, kwa kuwekeza katika viwanda mbali mbali, hatua ambayo iliwapatia vijana ajira pamoja na kuuinua uchumi wa Zanzibar. Aliusifu mchango huo wa China ambao, alisema, umesaidia kuleta maendeleo Zanzibar katika sekta za elimu na afya. [Chanzo Nipashe 19 Agosti.]

Ponda afutiwa kesi ya uchochezi
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amefutiwa kesi ya uchochezi wa vurugu iliyokuwa ikimkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, liliripoti gazeti la Habari Leo la 20 Agosti. Awali Ponda alisomewa shtaka la kuwahamasisha wafuasi wake wafanye fujo huku akiwa wodini katika kitengo cha Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MoI) wiki iliyopita. Ponda alifutiwa mashtaka hayo na Hakimu Mkazi, Hellen Riwa, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha hati ya kufuta mashtaka hayo kwa kuwa hana haja ya kuendelea kumshitaki. Licha ya kupata msamaha huo, Sheikh Ponda alisafirishwa kwa helikopta kuelekea mkoani Morogoro, ambako huko alisomewa mashtaka mengine matatu yanayomkabili. Mashtaka hayo ni pamoja na kuwashawishi watu wawapige wanakamati za ulinzi wa misikiti, kwa madai ya kuwa kamati hizo zimeundwa na BAKWATA ambao ni ‘vibaraka wa CCM’. Shtaka la pili ni kwamba Ponda anadaiwa kuwaambia Waislamu kwamba, Serikali ilipeleka Jeshi Mtwara kushughulikia vurugu iliyotokana na gesi kwa kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakaazi wake ni Waislamu. Shtaka la tatu ni kuwa Ponda anadaiwa kutoa kauli ambazo ziliwashawishi Waislamu kutenda makosa. Hata hivyo, Sheikh Ponda alikana mashtaka hayo lakini wakili Kigoda alidai uchunguzi umekamilika na kutaka kesi hiyo ipangiwe tarehe ya kusikilizwa. Upande wa mashitaka uliwasilisha ombi la dhamana kwa mshitakiwa lakini hakimu aliamuru Sheikh Ponda aendelee kuwekwa rumande hadi siku ya kusikilizwa tena kesi hiyo.

“Bila ya kauli sawa, si Muungano bali ni

MAKALA MAALUM
8
ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

9 SIASA

ukoloni kasorobo”

TANBIHI: Jumamosi ya tarehe 17 Agosti 2013, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, OTHMAN MASOUD OTHMAN, alitoa hotuba mbele ya Kongamano la Baraza la Katiba la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar, ambapo alizungumzia mapungufu kadhaa yaliyomo kwenye muundo wa sasa wa Muungano na alionesha kuwa anakubaliana na pendekezo la Muundo wa Serikali Tatu kama lilivyotolewa na Tume ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba. Hapa tunaichapisha sehemu ya hotuba hiyo kwa manufaa ya wasomaji wetu.

wao wenyewe kule bungeni na akawa ndiye kiongozi wa hiyo serikali ya Muugano? Maana huwezi kuwazuia Watanganyika wasiwachague wale kuja kuuongoza Muungano. Vyenginevyo, mtu atwambie kwamba “Tunao uwezo wa kuwazuia wasimchague mtu mwengine zaidi ya aliyepo sasa“. Lakini kinyume na hivyo, mtakuja kufanya nini? “Si tatizo kama sisi wa Zanzibar tunamchukia kiongozi anayeendesha serikali ya Muungano, lakini kama yeye anatuchukia sisi litakuwa tatizo kubwa. Na mtu ambaye ametangaza hadharani hakutambui, ni sawa na mwanamme kutukanwa matusi makubwa ya kuitwa vyengine. Si utapigana? “Ndiyo hayo wenzetu waliyofanya na wapo na huwezi kusema kwamba hawana uwezo wa kesho kushika serikali hiyo tunayotaka kuiamini kuikabidhi mambo ya Muungano. Tuwe wakweli. Tusitake kuichukua nyumba yetu tukaiweka rehani dukani kwa kupata kilo ya mchele. “Jambo jengine la msingi ni usawa katika masuala ya msingi ya Muungano. Haya ni mambo ambayo lazima muyaangalie vizuri ndani ya rasimu. La kwanza ni usimamizi wa hayo mambo ya Muungano. Kwanza msimamizi mkubwa wa Mambo ya Muungano ni Rais wa Muungano. Hivyo ni lazima tuwe na utaratibu wa kuwa na fursa na haki sawa ya kusema huyu tunamtaka, huyu hatumtaki. “Na hiyo ndiyo kasoro kubwa iliyopo sasa hivi. Anayegombea urais wa Muungano hana hata haja ya kuja Zanzibar kupiga kampeni. Kura 500,000 ni za nini kwake? Kwa hivyo, amekuwa akichaguliwa Rais wa Muungano, ama sisi tumtake au tusimtake, ingawa anakuja kusimamia mambo ya pamoja ya Muungano. “Kama wewe mshirika kwenye Muungano huo huna sauti katika

kumchagua huyo – ya kusema huyu ni sawa, na huyu si sawa – basi huo si Muungano. Tuutafutie jina jengine tuuite. That’s dominionship, kasoro kidogo ya ukoloni. “Hiyo ni kasoro kubwa iliyopo hivi sasa na lazima katika katiba inayokuja hilo liondoke. Yaani kwenye kile chombo kinachosimamia yale mambo ya Muungano, ni lazima Zanzibar iwe na sauti sawa katika kuichagua. Kama haipo hiyo, musijidanganye. Huo si Muungano. Huo ni ukoloni kasorobo. “Jengine ni katika kutunga sera za Muungano. Sisi ni washirika. Lazima tuwe na sauti katika kuamua sera za kimuungano. Hawezi mmoja katika washirika akatuamulia. Hilo lazima tuliangalie: mfumo wa Bunge, mfumo wa Baraza la Mawaziri na vyombo vya kutunga sera. “La tatu ni katika kutunga sheria. Kwa mujibu wa Katiba ya sasa, Ibara ya 98, Mambo yote ya Muungano yanatungiwa sheria na upande mmoja, kwa sababu kutunga sheria kwa mambo yaliyoko kwenye Jadweli la Kwanza, yote ni kwa wingi mdogo. Haya ndiyo mambo ya Muungano. “Na haya ni mambo ya ajabu kwelikweli. Mheshimiwa Hamza Hassan huwa anayaeleza vizuri kwa kusema kama tungekuwa tunayajua haya yaliyomo kwenye Katiba ya sasa hivi, tungezimia. Tungesema kwa kweli Mungu ametupenda, kwa kuwa tuko hai mpaka leo. “Kwa sababu Bunge limepewa uwezo wa kuyatungia sheria mambo hayo kwa wingi mdogo wa kura na daima wenzetu wamekuwa wengi kuliko sisi. Huo ni utaratibu wa ajabu kweli kweli. Kwa hivyo, mnapoipitia rasimu hii, lazima hilo mliangalie. Hapo ndipo mtakapomalizika. Hilo ni pamoja na namna ya kuyaongeza na kuyapunguza mambo ya Muungano. “Lakini jambo jengine muhimu ni

namna ya matumizi ya rasilimali za Muungano. Kwamba katika uwekezaji wa rasilimali, kama vile makao makuu, sote tufaidike nao kwa kuwa kuna mambo ambayo tumekubaliana kuwa ni ya Muungano. “Kwa mfano, licha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuwa na makao makuu yake mjini Arusha, Tanzania, taasisi za jumuiya hiyo ziko kwenye mataifa mbalimbali wanachama. Kwa sababu huo ndio uwekezaji. Ukiweka makao makuu mahala fulani, watu wa hapo watapata ajira. “Ni jambo la kufurahisha kuambiwa kuwa makao makuu ya Baraza la Kiswahili la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yatakuwa Zanzibar, lakini la kusikitisha kwamba kwenye huu Muungano wetu wenyewe, ni Uvuvi wa Bahari Kuu tu, tuliyokuwa hata hatuioni, ndio iliyopo Zanzibar. Na hiyo ilipatikana kwa vita, kwa ugomvi na kwa watu kununa. Hilo ni jambo ambalo lazima liondoke kwenye Katiba ya sasa. Vyenginevyo itakuwa hakuna ile faida ya Muungano kwa upande wa Zanzibar. “Hili la rasilimali ni muhimu sana, kwa sababu tunajiona leo tulivyo. Hivi sasa Zanzibar tuko kwenye mchakato wa suala la mafuta. Tumejikuta sisi tunalizungumza hivi sasa, lakini wenzetu wana wataalamu mpaka wa akiba wa masuala ya mafuta. Yaani timu yao imekamilika na wana wengine wa akiba wa hata kama wakitaka kuunda timu nyengine. Sisi Zanzibar ni wa kuokoteza tu. Hata ingelikuwa timu ya netiboli, haijatimia. Lakini hawa wametumia rasilimali za Muungano kuwasomesha watu wao. “Katika hilo pia jambo muhimu la kuzingatia ni la kuwa na fursa za kiuchumi. Hapa ni mahala ambapo tumeumia sana. Lazima tuhakikishe kuwa fursa zote za kiuchumi, hasa za kinchi, kila upande unakuwa nazo sawa.“

‘‘Bila ya kauli sawa, si Muungano bali ni ukoloni kasorobo’’

“N

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Benki Kuu, utakuta haziitambui Zanzibar kama ni nchi. Lakini je, hivi ndio ni kweli hatuwezi kuyaongoza mambo yetu mpaka tukamkabidhi mtu mwengine atuendeshee? “Labda Rais wa Muungano aliyepo leo tunamuamini, lakini vipi kesho akiingia yule wanayemwendesha Spika

ilikuwa nawaambia wenzangu kwamba Zanzibar tulitoka kwenye kuwa dola kubwa, kwa nini tuendelee kung’ang’ania kuwa manispaa? Hatuoni vibaya kutoka dola mpaka manispaa? Maana kwa hali iliyopo sasa, Zanzibar ni kigawe kidogo cha kisiasa cha Tanganyika. Soma sheria zote, ikiwemo ya

10

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Kalamu ya Bin Rajab

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

11

Uvundo wa Mji Mkongwe hauvumiliki tena
H
Na ahmed RAJAB
Wala Mji Mkongwe si mkongwe kama Lamu ulioanza kuwa mji mnamo karne ya 14 au pingine hata karne ya 12 na ulio kitivo kikubwa cha utamaduni wa Kiswahili. Mji Mkongwe umepitwa kwa umri pia na Lourenço Marques (siku hizi Maputo, mji ulioanza kujengwa karne ya 18 na ambao leo umeupiku Mji Mkongwe wenye vichochoro kama vyake). Maputo ya leo ni nadhifu zaidi na ina majengo mengi ya kisasa. Hata Moroni ulio kusini zaidi unasemekana ulianzishwa na mapema zaidi kushinda Mji Mkongwe, yumkini mnamo karne ya 10 na walowezi wa Kiarabu. Kabla ya Mji Mkongwe kuwa Mji Mkongwe kwanza kulikuwa na kijiji cha wavuvi. Walitangulia samaki, halafu yakaja mawe. Hayo mawe yalitumika kuujenga huu mji wa majumba ya mawe na vichochoro vilivyoshuhudia mengi na vyenye kuficha siri nyingi. AKUNA mengi yaliobadilika katika Mji Mkongwe tangu uanze kuvuta pumzi miaka kama 200 iliyopita. Majumba ndiyo yaleyale, vichochoro ndivyo vilevile, uchafu ndio uleule na harufu ndizo zilezile. Mengi ya majumba ya Mji Mkongwe yalijengwa karne ya 19 wakati ambapo nchi yetu ilikuwa na neema. Wakati huo Zanzibar ilikuwa ni dola kamili iliyokuwa kitivo muhimu cha biashara ya kimataifa katika kanda nzima ya Afrika ya Mashariki. Dola hiyo iliwavutia wengi — wa karibu na wa mbali. Waliopiga makasia na kuanza kuuona Mji Mkongwe majahazi yao yalipokuwa yakiyumbayumba juu ya mawimbi waliduwaa walipoyaona mandhari ya mji. Waliyakodolea macho huku wakiwa na papara majahazi yatie nanga ili wateremke bandarini. Mji Mkongwe ulikuwa na haiba ya aina yake ingawa haukuwa na ukale kama wa Mvita (Mombasa), mji unaonasabishwa na watawala wawili Mwana Mkisi na Shehe Mvita. Tayari Mvita ulikuwa mji wa biashara katika karne ya 12 kwani Al Idris, mwanajiografia mashuhuri wa Kiarabu, aliutaja kwenye maandishi yake mwaka 1151. Ibn Battuta, msomi na msafiri kutoka Morocco, alipokuwa anautembelea mwambao wa Afrika ya Mashariki aliwasili Mombasa mwaka 1331 na akalala huko usiku mmoja.

‘‘Mji wetu una harufu za ajabuajabu. Unaweza ukajaribu kuzikwepa kwa dakika mbili tatu lakini ukishavikata vichochoro viwili vitatu utakumbana nazo tena.’’
foliti. Tukizikimbia huku zinatufukuzia kule. Marikiti ndo hakusemeki. Wageni wanaotutembelea wanatusema. Wameanza kutusema tangu karne mbili zilizopita. Inaonyesha sisi wenyewe hatujali. Hatuoni haya; hatuoni aibu. Na wengi wetu ni Waislamu na tunaambiwa kwamba Uislamu ni unadhifu na hatoingia Peponi ila yule aliye nadhifu. Na unadhifu ni wa roho, wa vitendo, wa mwili na wa mazingira. Nadhani David Livingstone aliyeukanyaga Mji Mkongwe kwa mara ya kwanza 1866 alikuwa wa mwanzo kutukashif. Aliandika kwamba labda asiite tena Zanzibar bali aiite ‘Stinkibar’ (Mnukobar). Livingstone hakuwa akiielezea Zanzibar yote lakini akiuelezea Mji Mkongwe peke yake. Ukinuka siku hizo na unanuka hadi hii leo. Ndio maana wanaotutembelea wakirudi makwao hukimbilia kuandika kwenye tovuti na mablogi yao jinsi Mji Mkongwe unavyonuka. La ajabu ni kwamba kuna watu wanaolipwa mishahara kuhakikisha kwamba mji ni msafi. Wenzetu hao lazima waanze kuwajibika. Wasipofanya hivyo ZD Online itafanya wajibu wake wa kuwaandama na kuwafichua.

‘‘Ibn Battuta, msomi Ingawaje, hata wakati huo — miaka na msafiri kuto ka 200 iliyopita — ambapo Mji MkongMorocco, alipokuwa we ulipokuwa mpya na fakhari ya visiwa hivi mji huu ulikuwa ukituaianautembelea bisha. Na hadi sasa unatuaibisha. mwambao wa Afrika Mji wetu una harufu za ajabuajabu. Unaweza ukajaribu kuzikwepa kwa ya Mashariki aliwasili dakika mbili tatu lakini ukishavikata Mombasa mwaka 1331 vichochoro viwili vitatu utakumbana nazo tena. na akalala huko usiku Ni harufu za uvundo. Haziepukiki. mmoja..’’
Tumekuwa kama tunacheza nazo

Viongozi wapiga ngoma ichezwayo Z’bar
12

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

13

Matamshi ya Bi Waride, kwa niaba ya CCM, na ya Balozi Seif, kwa niaba ya Serikali, yalitosha kumtekenya Kamishna wa Polisi Zanzibar (CPZ), Mussa Ali Mussa. Yeye aliibuka na kutangaza rasmi kuwa wanamsaka Sheikh Ponda.

K

Na jabir IDRISSA

adhia ya Sheikh Ponda Issa Ponda mara hii imeanzia Zanzibar. Kwetu ndiko ilikotengenezwa kadhia hii mpya. Ni kazi ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Maneno ya uchonganishi waliotoa viongozi wa taasisi hizi mbili yalitosha kumtia ulamaa huyu wa Kiislamu katika mtihani mkubwa. Na kwa sababu ni kadhia iliyopikwa ikapikika, na hatimaye imeleta jibu kama walpishi walivyokusudia, ni ada kusema, ni kweli “Ngoma ikipigwa Zanzibar, wanaocheza huwa Mrima.” Nani hakumsikia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM/Zanzibar, Waride Abubakar Wakati alipomkandamiza Sheikh Ponda?

Kilimani, mjini Unguja, kwamba tayari walishaanza kumtafuta Sheikh Ponda ili wamhoji kuhusu maudhui ya hotuba zake alipokuwa Zanzibar. Aliulizwa alikuwa wapi kwa muda wote tangu Sheikh Ponda alipokuwa Unguja mpaka akaondoka kurudi Dar es Salaam? Mbona hakuwahi kutangaza kuwa Sheikh Ponda anasakwa akiwa bado Unguja? Kamishna akaulizwa kwa nini anatangaza “kumsaka” Sheikh Ponda akiwa ameshaondoka wakati alikuwa Zanzibar kwa kipindi chote cha ziara yake; tena akizunguka nchi huku na kule mchana kweupe; na akihutubia na kuhadhir msikiti huu na ule, kutoka Mjini Magharibi mpaka Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja? Kuna ushahidi wa kutosha kwamba katika ziara yake ya Unguja Sheikh Ponda hakufanya chochote kwa siri. Alihutubia hadharani ndani ya misikiti. Polisi, taasisi anayoiongoza Kamishna Mussa, ilituma askari wake kadhaa kufuatilia mihadhara ya Sheikh Ponda wakati wa maandalizi na wakati inafanyika. Nimeambiwa kuwa askari walikutwa maeneo ya misikiti ambako Sheikh Ponda angekwenda baadaye kuhadhir. Waliwauliza wenyeji wa misikiti na kutaka mawasiliano na viongozi wa misikiti iliyohusika. Walichukua majina ya viongozi wa shura za misikiti pamoja na namba zao za simu. Lakini hata wakati Sheikh Ponda alipowasili msikitini, akaingia ndani, akasali, akaanza kuhadhir, askari polisi walikuwa wamepiga kambi nje ya misikiti iliyohusika. Sheikh Ponda anazungumza na Waislamu ndani ya msikiti, wao askari wanalinda nje ili kusije kukatokea zahma yoyote ile ya kutiribua amani. Sheikh Ponda alidiriki kwenda gerezani Kiinua Miguu, Kilimani, kuonana na masheikh wenzake wanaoshikiliwa tangu Oktoba mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu. Katika wakati wote wa ziara yake, Sheikh Ponda hakufanya hata jambo moja kwa kificho. Sasa kama ni kumsaka Sheikh Ponda mbona Polisi walikuwa na muda mwingi wa kufanya hivyo? Kwa nini walikaa kimya na kuibuka ghafla baadaye alipokwishaondoka Zanzibar? Mwandishi mmoja wa khabari alikuwa na ujasiri wa kumuuliza Kamishna Mussa kama labda aliibuka kutangaza kuwa wanamsaka Sheikh Ponda kwa kuwa alikuwa ameshawasikia viongozi wa CCM wamem-

laani kwa madai ya kuwachochea wananchi kuleta vurugu? Sheikh Ponda amegeuzwa mbuzi wa kafara. Viongozi wanashindwa kutekeleza majukumu yao lakini kwa kutaka kuficha udhaifu wao, wakaona hakuna isipokuwa kumsakizia yeye. Sina shaka yoyote kwamba kauli za kipuuzi zilizotolewa na viongozi wa CCM/Zanzibar ndizo zilizowasukuma walioko Bara kujiunga katika mchezo mchafu wa kutisha wananchi na kumtisha Sheikh Ponda kwa kuwa amejitokeza kuwa kiongozi wa harakati za Waislamu kudai haki zao zinazokandamizwa na serikali zilizopo madarakani. Uko wapi uongo wangu? Si imeonekana dhahiri shahiri kwamba mara tu viongozi wa Bara walipowasikia wenzao wa Zanzibar wakipiga jaramba la kumsakizia Sheikh Ponda nao wakaigiza nyimbo ile na kumtangazia ubaya? Alianza Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi. Aliibuka na kusema Sheikh Ponda akamatwe na kufikishwa mahakamani. Eti amevunja sheria na haiwezekani aachiliwe tu hivihivi. Polisi walewale waliokuwa ubavuni mwa Sheikh Ponda kwa wakati wote alipokuwa ziarani Zanzibar, wakageuka kituko na kuingia kwenye mtego wa watawala. Wakaanza kumfuatilia kila aendako. Kama vile Zanzibar, Kusini hadi Kaskazini, Mashariki hadi Magharibi, haikuwa sehemu nzuri ya kumkamata Sheikh Ponda, Polisi wakaona eneo mwafaka ni Dar es Salaam au Morogoro. Badala ya kumkamata katika utulivu, hasa kwa kuwa haijawahi hata mara moja kutokea Polisi kumhofia Sheikh Ponda kuwa anabeba silaha, wakaamua kumfuatilia kwenye makundi ya Waislamu wanaomtii. Wakamfuata Morogoro baada ya kubainika kuwa amealikwa kuhadhir wakati wa kongamano la Idi mjini Morogoro. Walijua atakuwepo ndio maana mapema walishurutisha kongamano lifanyike lakini bila ya yeye kuhutubia. Sasa kwani kongamano liliandaliwa na Polisi hata wapange nani na nani wazungumze na nani na nani asizungumze? Na tangu lini sheria hiyo imetungwa ya Polisi kuchagua wasemaji wa mkutano usiokuwa wao?
IMG© NAME SURNAME

Waride, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kiembesamaki, alisema siku chache tu baada ya Sheikh Ponda kuondoka Zanzibar alikokuwako kwa ziara ya wiki mbili, kwamba ulamaa huyo alikuja Zanzibar kwa lengo la kuwachochea wananchi wafanye maandamano dhidi ya serikali. Kauli yake ikatiwa nguvu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi. Alipokuwa anaufunga mkutano mrefu wa Baraza la Wawakilishi uliojadili na kupitisha bajeti ya serikali ya mwaka 2013/14, Balozi Seif alisema Sheikh Ponda alikuja Zanzibar kufundisha watu uasi dhidi ya serikali. Aliongeza kusema kwamba hotuba alizozitoa Sheikh Ponda alipokuwa Zanzibar zilijiegemeza kwenye chuki, uchochezi, na hamasa ya maandamano ili kuvunja misingi ya amani na utulivu iliyokwishajengeka. Balozi Seif alisema Sheikh Ponda ameonesha dhahiri kwa hotuba zake kuwa haitakii mema Zanzibar; akatoa tamko la kumpiga marufuku kuingia tena Zanzibar. Tena akahimiza wananchi wampuuze kwa kutosikiliza hotuba zake kwenye kanda. Matamshi ya Bi Waride, kwa niaba ya CCM, na ya Balozi Seif, kwa niaba ya Serikali, yalitosha kumtekenya Kamishna wa Polisi Zanzibar (CPZ), Mussa Ali Mussa. Yeye aliibuka na kutangaza rasmi kuwa wanamsaka Sheikh Ponda. Kamishna Mussa aliwaambia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar,

Ni nani anayalinda maslahi ya Zanzibar?

14

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Barza ya Jumba Maro

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

15

“Ningetaraji Dk. Shein angeongoza juhudi za kuisafisha Zanzibar nje ya nchi kwa kuangaza na mbinu za kibalozi na hilo liwe wazi wazi. Wenzetu hawasiti katika mambo kama haya. La, sivyo, Dk.Shein angetumia nafasi yake kuufikia ubalozi Uingereza kuhusu hilo.”
ungano, lakini kwa Mabadiliko ya 2010 Zanzibar imejitangaza kuwa ni “nchi” na kwa hivyo ikiwa nchi ina uchumi wake, ina watu wake na tabaan ina maslahi yake, tafauti na yale ya Tanzania Bara na Tanzania. Kwa mtizamo wowote uchumi wa Zanzibar ni uchumi shindani na ule wa Tanzania Bara na kwa hivyo kila upande unasaka njia zake na una wajibu wa kulinda njia hizo kwa maslahi yake, maana chumi zetu hazisemeshani, kama wasemavyo wachumi. Kuguswa kwa utalii ni kuguswa kwa uchumi wa Zanzibar. Kwa hivyo ningeitaraji Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kusimama kidete kuyalinda maslahi ya Zanzibar. Sisemi kuwa SMZ haikufanya kitu. Lakini niliitaraji ichukue hatua kubwa zaidi na pana zaidi. kuhusu hilo. Tatu ningetaraji kuona kampeni ya tukio hili ikipigwa ndani ya jiji la London, kwa Dk Shein kuona vipi Zanzibar inatumia Ubalozi wa Tanzania kutoa sura mbadala ya tukio hilo katika vyombo vya habari vya Uingereza. Kama Ubalozi huo upo kwa ajili ya pande mbili, inashangaza kuona haikuchukua hatua yoyote iliyoonekana na umma. Nne, kama Dk Shein ndiye mtetezi mkuu wa maslahi ya Zanzibar, kwa kujua kuwa si lazima linaloiumiza Zanzibar linawagusa wenzetu wa Tanzania Bara, pamoja na Rais Jakaya Kikwete kwenda kuwajulia hali waathirika wa tukio hilo ovu, ingefaa kabisa yeye Dk Shein awe mbele kutaka na ikibidi kudai hatua zichukuliwe kulinda taswira ya Zanzibar. Tano na mwisho kama Wizara ya Mambo ya Nje inapaswa kutumikia pande mbili za Muungano kwa ukamilifu, basi ilikuwa ni muhimu kwa Dk. Shein ambaye ndiye mlinzi wa maslahi ya Zanzibar aitake Wizara hiyo ichukue hatua ya kupunguza madhara kwa Zanzibar. Inasikitisha kumsikia Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akisema kuwa njia pekee ya kuzuia taswira ya Zanzibar kuchafuliwa ni kwa kuwakamata “wahalifu hao” na akiamini kuwa zawadi ya TShs 100 millioni itatosha kuwakamata. Je, Dk Shein naye akae kitako kimya kusubiri kukamatwa wahalifu hao na Zanzibar ikichafuliwa kwa ujumla na kuathiri sekta ya uchumi na kwa hivyo kutishia maelfu ya ajira? Nani alinde maslahi ya Zanzibar ni Serikali ya Muungano, au mtu aliyechaguliwa na Wazanzibari na kula kiapo kuilinda Zanzibar? Tutaraji kulindiwa na upande ambao pia ni washindani wetu kiuchumi na ambao unaweza kuwa na vipimo tafauti vya shida zetu?

ukio la Zanzibar kunangwa na kupakwa matope kwa ujumla wake kutokana na wasichana wawili wa Kiingereza kumwagiwa tindikali, limenifanya nifikiri kwa mara nyengine tena na kujiuliza ni nani anayepaswa kulinda maslahi ya Zanzibar? Wakati sote tunakubaliana tukio lile lilikuwa ovu, la kinyama na la kukosa ubinadamu, lakini bado mbele ya macho ya kimataifa halikuhusishwa tu na watu hao wawili waliotenda, lakini limehusishwa na Zanzibar nzima ikiwa ni pamoja na utu wake na uchumi wake.

T

ishi mkubwa duniani vikalenga bila kificho kuiathiri biashara ya utalii Zanzibar ambayo inachangia zaidi ya asilimia 60 ya uchumi wa Visiwa hivyo. Kwa sasa Zanzibar inapata watalii zaidi ya 200,000 kwa mwaka na Waingereza ni miongoni mwa wenye kuzitembelea kwa wingi fukwe na Mji Mkongwe. Tatizo nililoliona katika kadhia hii nzima ni kuwa sikujua ni nani mwenye wajibu wa kulinda maslahi ya Zanzibar. Na wiki mbili baada ya tukio hilo bado najiuliza na sijapata jawabu.

Kubwa kwa maana mtu wa kwanza ningetaka nimsikie akitoa sauti ya kulaani na kutoa mwongozo ni Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein. ingawa najua alifanya hivyo katika hotoba yake mbele ya Baraza la Idi lakini alichelewa kidogo. Hivi karibuni wavuvi wawili wa Taiwan walishambuliwa na askari wa Philippines na Waziri mmoja wa Philippines akatoa rambi rambi kwa niaba ya Serikali. Hilo likazua kashehe na kuonekana ni dharau, na Taiwan ikataka lazima tamko litolewe na Rais ndio suluhu ipatikane. Somo hapa ni kuwa kiongozi mkuu wa Zanzibar kila mara lazima ashauriwe juu ya mambo ambayo lazima ayatolee kauli yeye mwenyewe, tena bila ya kuchelewa na ikiwezekana siku hiyohiyo. Ningetaraji Dk. Shein angeongoza juhudi za kuisafisha Zanzibar nje ya nchi kwa kuanza na mbinu za kibalozi na hilo liwe wazi wazi. Wenzetu hawasiti katika mambo kama haya. La sivyo Dk. Shein angetumia nafasi yake kuufikia ubalozi wa Uingereza

Na ally SALEH

Vyombo vya habari vya Uingereza moja kwa moja vililihusisha tukio hilo na mvutano wa kidini na ugaidi. Vingine vilisema kuwa wasichana hao walishambuliwa kwa sababu wana asili ya Kiyahudi na vyombo hivyo vya habari  vilifanikiwa kuishawishi Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza kutoa tangazo la tahadhari kwa Waingereza wanaotaka kutalii Zanzibar. Vyombo hivyo venye nguvu na ushaw-

“Somo hapa ni kiongozi mkuu wa Zanzibar kila lazima ashauriwe juu ya ambayo lazima ayatolee kauli yeye mwenyewe tena bila ya kuchelewa na ikiwezekana siku hiyo hiyo.”
Zanzibar ni moja ya washirika wa Mu-

16

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Ghasia za Juni 1961, somo la historia kwa Wazanzibari
fasi soma kutoka Intaneti: Zanzibar Riot Report of June 1961“ utapata sura ya hali ya mambo ilivyokuwa wakati huo Mabishano yalikuwa baina ya vyama viwili vikuu vya siasa, Afro-Shirazi Party (ASP) na Zanzibar Nationalist Party ( ZNP au Hizbu). Viongozi na wanachama wa vyama hivyo walikuwa Wazanzibari na karibu wote ni Waislamu kama walivyokuwa wakaazi wa visiwa hivi ambao kwa miaka na dahari waliishi pamoja kwa salama na amani. koo na familia. Wanasiasa wa kambi zote mbili walikuwa wanasimama majukwaani, wengine wakiwa wasomi wenye elimu za juu za kidini na kidunia, wakikubali kuingizwa katika uchafu wa kusutana, kutukanana na kubezana. Kutostahamiliana kisiasa ndiko kulikotangulizwa mbele. Mara nyingine rangi ya mtu ndio ilikuwa utambulisho wake. Kipindi hicho kilikuwa cha aibu kwa visiwa vyetu. Wengi wa watu 68 waliouawa katika ghasia hizo za Juni1961 walikuwa wafuasi wa ZNP wenye asili ya Kiarabu. Na ingekuwa Balozi wa Uingereza (Resident, aliyekuwa na dhamana ya usalama), hajaamua kuwaita wanajeshi wa Kiingereza kutoka Kenya kuja kutuliza mambo, basi roho nyingi zaidi za watu wasiokuwa na hatia zingepotea. Mtaa niliokuwa naishi, Baraste Kipande, katika jimbo la uchaguzi la Darajani, ulikuwa mojawapo ya vitovu vya michafuko. Nikichungulia kutoka dirisha la chumbani kwangu, niliwaona wafuasi wa vyama vya ASP na ZNP wakirushiana mawe, wakitishana kwa kuoneshana mapanga, marungu, nondo na fimbo. Wengine kati yao ni watu waliocheza pamoja udogoni, waliokwenda shuleni pamoja, waliokuwa wakicheza pamoja karata, bao na dhumna mitaani. Kutoka kuwa binadamu mara wakageuka kuwa karibu sawa na wanyama, wanawindana.
Gwaride kubwa kabisa la kijeshi kuwahi kuonekana Afrika ya Mashariki tarehe 15 Februari 1965, Mnazi Mmoja, Zanzibar

Waraka kutoka Bonn

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

17

Na othman MIRAJI

J

UNI Mosi, 1961 na siku nane zilizofuata baadaye, nikiwa katika umri wa kubalPunde tu baada ya uchaguzi wa eghe, nilishuhudia michafuko mikubmwanzo wa mwaka 1957 ambapo wa baina ya Wazanzibari wenyewe kwa chama cha ASP kilikishinda kile cha wenyewe iliopewa jina la ‘Ghasia za Juni’. Wazanzibari 68 waliuwawa, 381 walijeruhi- ZNP, kwa ghafla Zanzibar iliyokuwa wa , baadhi yao vibaya sana, majengo mengi nuru ya uchumi na usomi katika yakaharibiwa na mali nyingi za watu zilipor- eneo la Afrika Mashariki, ilishuhudia watoto wake wakihasimiana, wa. wakichukiana na wakiombeana maovu. Biashara za Wazanzibari Kwa vile Wazanzibari wengi, hasa wale waliokuwa wafuasi wachama kimowaliokuwa na satua, walishindwa baaja zilisusiwa na Wazanzibari wenzidaye kujifunza kutokana na maafa hayo na kuchukua hatua mujarabu, yawezekana wao waliokuwa wafuasi wa chama kingine. Wakulima wadogo wadogo kuwa hiyo ndio sababu ya kuzidi kuweko walifukuzwa kutoka mashamba mgawanyiko miongoni mwa Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe. Mgawanyiko huo na wafanya kazi walipoteza ajira. visima vya maji vikawa vinatiwa ulipelekea kuweko Juni nyingine kadhaa vinyesi na mimea kukatwa, yote baaadye. ilikuwa kukomoana. Siasa za chuki Waliofaidika na michafuko hiyo hawakuwa na uhasama zikaenea hadi ndani ya Wazanzibari, bali watu wa nje. Ukipata na-

‘‘Wakoloni wa Kiingereza waliunda tume ya uchunguzi kutaka kujua sababu ya michafuko hiyo’

Mzee mmoja akitokea msikitini kusali adhuhuri alishtukia jiwe kubwa likimuangukia kichwani. Alianguka na kufa papohapo ubavuni mwa nyumba ilio jirani na kwetu, huku akishikilia tasbihi yake mkononi. Watu watatu tu walikwenda kumzika. Serikali ilitoa amri ya kuwazuia watu wasitoke nje ya nyumba zao. Wakoloni wa Kiingereza waliunda tume ya uchunguzi kutaka kujua sababu ya michafuko hiyo. Ripoti ya tume ilisema tu kwamba sababu ilikuwa mlolongo wa makosa ya Wazanzibari wenyewe walioshindwa kustahamiliana na kuvumiliana kisiasa. Japokuwa tume hiyo iliepuka kutaja kwamba nao Waingereza walichangia kuchochea kuwagawa Wazanzibari. Wazanzibari wengi waliliona tukeo la Juni kuwa la kipekee, la kupita tu na kwamba baadaye litasahauliwa. Walikosea. Miezi miwili baada ya michafuko hiyo Hayati Baba yangu alinipeleka Tanganyika kuendelea na masomo yangu, hivyo sijayashuhudia maafa mengine

yalioifika Zanzibar baada ya ghasia za mwaka 1961. Hebu nikupeni hadithi ya ndugu wawili, wanasiasa wa Kijerumani. Wa kwanza ni Bernhard Vogel, aliyekuwa waziri mkuu wa mkoa mmoja hapa Ujerumani na miongoni mwa viongozi wa Chama tawala cha Christian Democratic Union (CDU) katika miaka ya tisini. Wa pili ni kaka yake , Hans-Jochen Vogel, aliyekuwa katika uongozi wa Chama cha Social Democratic, (SPD), na aliyewahi kuchuana na Kansela Helmut Kohl wa chama cha CDU kupigania ukansele. Bernhard aliwahi kuulizwa ilikuwaje wao wawili waliopata malezi ya kikatoliki kutoka kwa wazee wao wakawa katika kambi za kisiasa zinazopingana, ndugu yake akiwa msoshalisti na yeye mhafidhina. Alijibu hivi: Mimi nampenda sana ndugu yangu Hans, lakini katika ushindani huu naona Helmut Kohl atakuwa kansela bora. Aliendelea kusema kwamba yeye na ndugu yake

wanaiona siasa kama wito wa kuwatumikia watu ili maisha ya wananchi yawe bora na kwamba kwao siasa si mradi wa kiuchumi au wa kutaka umaarufu wala si kufanya uhasama kuelekea yule aliye na mawazo tofauti na yao. Utu unatangulia siasa. Nilifahamu baadaye kwamba mtoto wa Hans-Jochen alikuwa akiishi na ami yake, Bernhard, katika mji wa Mainz anakosoma. Alisema Wajerumani wamejifunza kutokana na makosa makubwa walioyafanya kabla ya vita, kushindwa kustahamiliana na kuvumiliana nchini mwao na pia na mataifa mengine ya dunia. Mimi nilipoziona kanda za video za mikutano ya hadhara ya kisiasa huko Zanzibar hivi karibuni, wanasiasa wakiyatumia majukwaa kubezana na kushushiana heshima nilijiuliza; jee hii ni demokrasia tunayoitamani, na tunaelekea wapi? Nililikumbuka jinamizi la Juni 1961 na kuwakumbuka Wajerumani Bernhard na Hans-JochenVogel. Zote hizo ni historia, ni mafunzo kwangu na kwako.

18

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Ngurumo la Mkamandume

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

19

Muungano si tatizo pekee la Zanzibar
Je, kama mfumo huu wa Muungano ulikuwa ajali, ilikuwa ajali iliyoweza kuepukwa? Kwetu wengine, jibu lake ni “ndiyo”. Laiti kama kuelekea uhuru wa mwaka 1963, wakati wa zile ziitwazo “Zama za Siasa”, wanasiasa wa Zanzibar wangeliweza kujenga Mwafaka na Maridhiano ya Kitaifa. Wangelifanya hivyo basi pasingelifanywa Mapinduzi ya Januari 1964 na hatimaye kusingekuwa na Muungano. Kwa Zanzibar, Muungano ulikuwa nyenzo ya kuwalinda watawala walioingia madarakani baada ya Mapinduzi. Zanzibar inakabiliwa na matatizo mengine mengi na tena makubwa sana. Hayo ni matatizo ambayo hata kama Zanzibar isingelikuwa kwenye Muungano, bado yangelifanya libakie kuwa taifa lililo nyuma sana kimaendeleo mithali yalivyo mataifa mengine yaliopata uhuru wakati ule ule Zanzibar ilipopata wake. Kama kulivyo kwengine, hasa barani Afrika, Zanzibar pia kuna ufisadi unaofanywa na viongozi wa serikali, kuna ugoigoi wa kijamii na utovu wa nidhamu wa umma. Zanzibar hii leo ingepaswa iwe zilipo nchi kama Sudan, Misri na Ghana, kwa mfano, ambazo kwenye miaka ya ‘60 zilifanana sana na Zanzibar kwa uwezo wao wa kiuchumi, wingi wa wasomi, na nidhamu ya kijamii. Mkufu wa matatizo shingoni mwa Zanzibar ungeliitundika nchi hii hata kama isingelikuwa kwenye mfumo huu wa Muungano na Tanganyika. Hata nje ya Muungano, Zanzibar isingelikuwa taifa bora lau ingekuwa nao hawa wanasiasa waliobobea katika kufisidi mali ya umma – ardhi, majengo na fedha, ambazo zimegeuzwa kuwa mali ya viongozi hao na familia zao. Taifa ambalo lina raia wasiotambua haki na wajibu wao kwa nchi, ambao wanaweza kuiibia serikali, kuharibu mali ya umma au kutelekeza wajibu wao kwa kiwango tufanyacho kwetu, haliwezi kuwa zuri zaidi ati kwa kuwa liko huru nje ya Muungano.

Z

Na mohammed GHASSANI

anzibar ilifanya kosa kuingia kwenye mfumo huu wa muungano na jirani yake, Tanganyika. Kilichotokea Aprili 1964 ni “ajali ya kisiasa” kama zilivyo ajali nyingine zozote. Waswahili husema “ajali haina kinga”, lakini huko kutokuwa na kinga hakumaanishi kwamba ajali ni jambo zuri. Ajali zina madhara – majeraha, kuharibika mali na vyombo na hata vifo. Ndiyo maana mara baada ya ajali kutokea, jitihada huchukuliwa kurudisha hali ya kawaida, ingawa pia Waswahili haohao husema kuwa “lishalovunjika ni gaye”. Lakini gaye (upande wa nyungu au kaure) linaweza kufanyiwa marekebisho ya hapa na pale. Kwa miaka ikaribiayo 50 sasa, Wazanzibari wamekuwa wakijaribu kupambana na madhara ya ajali ya kisiasa iliyoipata nchi yao. Hiyo imekuwa miaka 50 ya kulifanya gaye lifae kuwa nyungu ya kupikia.

Hilo nalibakie hapo kwanza, maana halikuwa lengo la makala haya kuchambua chimbuko la Muungano. Itoshe tu kuthibitisha hoja kwamba Zanzibar iliingia kwenye mfumo huu wa Muungano kimakosa. Na kama lilivyo kosa lolote lile, ni busara kuliepuka. Kama halikuweza kuepukwa kabla ya kufanyika, basi hekima ni kupunguza madhara ya kosa hilo baada ya kufanyika na kujiepusha na mengine mfano wake. Na yako mengine, kwa hakika, baada ya kufanywa, huweza ‘kufanyuliwa.’ La mfumo huu wa Muungano tulio nao sasa, lilipaswa kuwa moja wao. Lakini je, hata kama hilo la kulifanyua kosa la mfumo wa Muungano likitokea, Zanzibar itakuwa imeyamaliza matatizo yake yote iliyonayo? Kwa hili, jibu ni “hapana” kwa sababu mfumo wa Muungano si tatizo pekee kwa Zanzibar, hata kama ni miongoni mwa matatizo hayo.

Taifa lenye kundi la wanasiasa wanaopigania kusalia madarakani hata kwa mtutu wa bunduki, wakipitia kwenye chaguzi zisizo huru wala zisizo za haki, haliwezi kusonga mbele kiuchumi, hata kama juu yake hakuna kizibo. Taifa ambalo lina usiri mkubwa sana kwenye mfumo wake wa kijamii, ambapo watoto wadogo wa kike na kiume huharibiwa na walimu, wazee, walezi na wakubwa wao, kisha likashindwa kuwachukulia hatua wahalifu hao kwa sababu yoyote ile iwayo, haliwezi kuzalisha vichwa vya kuliendeleza. Haya ni matatizo makubwa yanayoikabili Zanzibar. Na matatizo haya – kama yataendelea kuwapo hivi hivi – yasijengewe matumaini kwamba mara baada ya Zanzibar kutoka kwenye mfumo wa sasa wa Muungano, basi itaweza kusimama na kuwa taifa, nchi na dola huru yenye neema kufumba na kufumbua. Nirudie. Mimi ni mmoja wa wanaoamini kwamba Zanzibar ilifanya

kosa kuingia kwenye Muungano. Nimekiita kitendo hicho kuwa ajali ya kisiasa. Ndiyo, ilikuwa ajali, tena mbaya. Ajali haisifiwi wala haikaribishwi. Ajali hukosolewa na huepukwa. Lakini mwenendo wa mambo ndani ya Zanzibar yenyewe unaonesha kwamba nchi yetu bado ina matatizo mengine makubwa. Ni kwa kuyaweka sawa matatizo hayo tu, ndipo kuwa kwetu nje ya mfumo wa sasa wa Muungano kutakuwa na maana kwa maisha ya Mzanzibari wa kawaida. Na hilo la kuyaondoa matatizo hayo, halitakuwa jambo la siku moja, wala mbili. Utakuwa mchakato wa muda mrefu. Vuguvugu la umma kwenye mataifa ya Kiarabu limeibua hoja kwamba mataifa kama vile Misri, Tunisia na Libya, kwa mfano, sasa yanarudi hatua 100 nyuma kuliko pale yalipokuwa kabla wananchi hawajawapindua viongozi wao wakongwe. Kuna kitu kilikosewa, ambacho ni taaluma ya kuyasimamia matarajio ya umma. Nitaiita taaluma

hii expectology (public expecation management). Hapana shaka, haikuwa kwa Hosni Mubarak kuendelea kuwa Firauni wa Misri wala Zein Al-Abidin Ben Ali kuwa dikteta wa Tunisia, kama vile ambavyo si halali kwa Dodoma kuendelea kuwa mtawala wa Zanzibar. Lakini kuyadumisha mapinduzi ya umma wa Kiarabu, wanamkakati walipaswa kuutayarisha umma kwa kipindi kigumu cha kuyasimamisha mapinduzi hayo. Ya Zanzibar pia ni yayo. Bado Zanzibar haijawa na mageuzi makubwa yanayoonekana kuwa matarajio ya walio wengi. Ninachokusudia ni kuwa hata kama lengo ni kuwa na mfumo tafauti wa Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika, kuelekea huko wanamkakati walenge sasa kwenye taaluma ya expectology, inayojumuisha pia kuyatatua matatizo makubwa. ya ndani – angalau kwa kuanza leo kuyazungumzia kwa uwazi.

20

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

M

Bila ya Mkataba, hakuna Muungano wa haki
iongoni mwa sababu kubwa za ulazima wa kuandikwa kwa Katiba mpya sasa ni ukweli kwamba kwa takriban miaka yote ya uhai wake, Muungano huu haukuheshimu Mkataba uliouunda. za kwamba matatizo yanayoukabili Muungano huu yalikuwa ya kawaida tu na ambayo yangeliweza kufunikwafunikwa hapa na pale na kumalizika. Hilo limefanyika kwa muda wote wa miaka ikaribiayo 50, lakini halikufanikiwa. Hapa nitazungumzia ya jitihada butu za serikali za CCM kuonesha kwamba mambo yanaweza kukaa sawa, ilhali hayajawahi kukaa. Nao ni ule utaratibu wa vikao vya pamoja baina ya Serikali ya Muungano na ya Zanzibar kujadili “kero za Muungano”. Licha ya kujumuisha mabaraza ya mawaziri wa pande zote mbili, vikao hivi havina uhalali panapohusika msingi wa Muungano huu na ndio maana havina nguvu za kutatua kero yoyote ambayo, hata hivyo, imeundwa na wajumbe hao hao wa vikao kupitia sera ya CCM ya Muungano wa Serikali Mbili. Haviwashi wala havizimi kwa kuwa wajumbe wa vikao vyenyewe – upande wa Bara huongozwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na wa Zanzibar huongozwa na ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais – wanakutana wakiwa tayari wameshauvunja Mkataba wa kimataifa uliosainiwa na wawakilishi wa

Mkeka wa Mwana wa Mwana

21

Kwa kiasi kikubwa, Katiba ya 1977 imekuwa ikiyakhalifu makubaliano hayo ya kimataifa na, kwa hivyo, ni katiba iliyokwenda kinyume na msingi wake. Kutokana na hili, mbali ya mengine yote, ndiyo maana kuna ulazima wa kuandikwa kwa katiba mpya (na sio kuifanyia marekebisho iliyopo) kwa sababu hii ya sasa ni batili kwa kiwango ambacho Makubaliano ya Muungano yanahusika. Sababu ni kuwa Muungano huu haukuundwa, na katiba na wala hautakiwi kuongozwa na Katiba hiyo, bali Mkataba. Kile ambacho Katiba zote mbili, ya Muungano na ya Zanzibar, zilichotakiwa kukifanya, kilikuwa ni kuutafsiri Mkataba huo tu, na si vyenginevyo. Inapotokezea kuwa Katiba imesema kinyume na Mkataba wa Muungano, kama ambavyo Katiba ya sasa ya Muungano wa serikali mbili imekuwa ikifanya tangu kuundwa kwake, ni Katiba ambayo itakuwa imekosea na lazima irekebishwe mara moja kuondoa kosa hilo. Lakini kwa vile makosa hayo ni mengi mno, basi sasa yamechusha na yameipoka uhalali wote Katiba ya 1977. Ni bahati mbaya sana kwamba serikali za Chama cha Mapinduzi (CCM) zilikuwa zikijaribu kutueleRais Robert Nugabe

Na riziki OMAR
Tanganyika na Zanzibar wa wakati huo. Kikao chochote cha kuujadili Muungano huu kilitakiwa lazima kiakisi uwakilishi huo wa pande zinazohusika za Mkataba wenyewe. Kwa hivyo, ni kosa kubwa dhidi ya sheria zinazolinda mikataba ya kimataifa. Kwa hakika, ni hatua ya hatari kwa khatima njema ya Muungano huu, kwa ofisi za waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (ambayo Zanzibar ni sehemu yake) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (ambayo ni ya Zanzibar tu kama mwasisi mmojawapo wa Muungano wenyewe) kujadili mustakbali wa Muungano. Wanaostahili kuujadili na kuutolea maamuzi Muungano ni Serikali ya Zanzibar na mwenzake aliyetiliana saini Mkataba wa Muungano, ambayo ni Serikali ya Tanganyika. Viongozi wa Serikali hizo ndio walio-

kuwa washiriki wa mazungumzo ya kuunda Muungano kwa niaba ya nchi zao. Kilichotokea Aprili 1964 ni Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kukubaliana kuanzisha ushirika wao unaoitwa Muungano. Katika kulinda heshima za mataifa yao, viongozi hao waliweka saini Mkataba wa makubaliano yao, ambao una kila sifa ya kuwa Mkataba wa Kimataifa unaostahiki kuheshimiwa na pande zinazohusika. Kwa hivyo, ni upotoshaji wa makusudi kuuchukua mjadala wa nchi mbili zilizoungana na kuukabidhisha mikononi mwa vyombo visivyohusika na kuvipa vyombo hivyo mamlaka ya kufanya maamuzi yote. Kwa lugha rahisi ni kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu haina sifa ya kuuwakilisha upande wa pili wa Muungano, maana hii ni Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo Zanzibar ni sehemu yake. Ofisi hiyo – kama taasisi – ni taasisi ya Muungano, ambao ndio unaojadiliwa hapa, na si taasisi ya Tanganyika, ambayo inaambiwa haipo. Hii ni kusema kwamba, utaratibu huu wa pande mbili kukutana nako pia kulikuwa ni sehemu ya vizungumkuti vya CCM na serikali zake kwenye muundo

huu wa Muungano wa serikali mbili. Ni sawa na kukichukua kiumbe na kukiweka na mmoja kati ya waumbaji wake kukijadili kiumbe hicho. Kiumbe hapa ni Serikali ya Muungano na mmoja wa waumbaji ni Serikali ya Zanzibar, ambapo muumbaji mwengine (Serikali ya Tanganyika) husemwa kuwa hayupo. Wenye busara hawawezi kuamini kwenye vizungumkuti kama njia mwafaka na ya kudumu, ndio maana muundo wa Muungano wa Serikali Mbili ukaonekana wazi kwamba haufai. Tume ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba imependekeza, hatimaye, kile ambacho hasa kinautafsiri Mkataba wa

Muungano wa 1964, yaani Muundo wa Muungano wa Serikali Tatu. Kinyume chake, wale wanaotetea muundo wa sasa wa Muungano wanatuambia kwamba wanapenda kuendelea kufanya kizungumkuti hiki kwa makusudi, wakizikengeuka sheria za kimataifa, kama ile ya Common Law na Vienna Convention, ambazo hutakiwa kuongoza mikataba ya kimataifa kama huu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sisi wengine, hatutaweza kamwe kuwaunga mkono.

22

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

La Kusemwa Lisemwe

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

23

H

Zanzibar inavyoonewa na vyombo vya habari vya Bara

ivi karibuni  wasichana  wawili wa Kiingereza, Kristie Trup na Katie Gee, walimwagiwa tindikali na watu wawili wasiojulikana katika eneo la Shangani, Mji Mkongwe, Unguja. Mara tu baada ya kupatikana taarifa hizo zilizoishtua Zanzibar, kwa vile kitendo hiki cha kinyama hakiwezi kukubalika na jamii inayojali utu, zilisikika shtuma kali kwamba washambulizi walikuwa  wale wanaoitwa ‘Waislamu  wenye siasa kali’. Baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za nje na vya hapa nchini vilipaza sauti za kuwalaumu Waislamu. Vyengine, hasa vya nyumbani, vilitoa tahariri zilizoeleza kuwa Zanzibar haikaliki na watalii wameanza kuwa na khofu ya kutembelea Zanzibar. Sijui wataalamu hawa wa habari na baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi walifanya uchunguzi wakati gani hata wakagundua kuwa washambulizi ni vijana wa Kiislamu. Bila ya kutafuna maneno, hiki ni kielelezo chengine cha jinsi panapotafutwa sababu au kisingizio chochote kile cha kuwapaka matope Waislamu na dini yao. Hii sio mara ya kwanza  wala ya pili kutolewa kauli kama hizi zisizo na mshiko na zenye lengo la kuonyesha kuwa Zanzibar  wapo Waislamu wanaohusudu kufanya vitendo vya kijahili. Jengine ni kutaka kuiharibu sifa ya Zanzibar kama nchi ya watu wakarimu na wanaopenda wageni ili kuichafua sekta yake ya utalii inayotegemewa sana na uchumi wake. Kwanza tujiulize ni nini kilichopelekea kufikiriwa watu waliofanya unyama huo kuwa ni Waislamu au walikuwa na chapa inayoeleza “ Sisi ni Waislamu”? Vile vile nini kinachopelekea pasifikiriwe waliohusika kuwa ni watu wa dini

‘‘Bila ya kutafuna maneno, hiki ni kielelezo chengine cha jinsi panapotafutwa sababu au kisingizo chochote kile cha kupakwa matope Waislamu na dini yao’
walipapurana na watu katika maeneo ya Mji Mkongwe. Gazeti hilo lilimnukuu rafiki mmoja wa wasichana hao, aliyekuwa nao Zanzibar akisema kuwa katika tukio moja wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani  wasichana hao waliwaudhi watu walipokuwa wanaimba hadharani wakati wa mchana. Dada mmoja aliudhika na kumpiga kibao Kristie. Rafiki mwengine wa wasichana hao alikiambia kituo cha televisheni cha  Channel 4 News cha Uingereza kuwa vijana wawili waliowamwagia hao wasichana tindikali walipita katika kundi la wazungu wengi. Vijana hao waliwaangalia vizuri hao wazungu na mmoja wao alionyesha kidole na mwenzake alipoinua kichwa kuitikia “Ndio”  ndipo walipomwagwa hilo tindikali. Je, matukio haya hayaonyeshi kama palikuwepo jambo hapa? Kwamba kitendo hicho kiliwalenga wasichana hao wawili tu kwa jambo ambalo lina taswira ya “kulipiza kisasi” au kutokana na tukio jengine la hapo awali? Hapa tujiulize kwa nini habari hii haitolewi maelezo na badala yake magazeti ya Bara hukurupuka tu kuwalaumu Waislamu na sio watu walioshukiwa kuwa na ajenda maalum ya kuwasaka wasichana hao? Ukiangalia hizo tahariri za Bara zinazoeleza kuwa Zanzibar haikaliki khasa za magazeti ya kampuni moja inayomilikiwa binafsi utaona wazi hapana kigezo cha uhakika kilichotumika kufikia uamuzi huu. Hapa tujiulize  kama matukio ya mashambulizi ndio kipimo cha kuamua eneo fulani halikaliki ni wapi pasikalike?  Bara au Visiwani? Matukio ya mashambulizi ya Bara ukiyalinganisha na ya Zanzibar ni mengi na ya hatari zaidi. Kwa mfano, tumeshuhudia Bara pakitokea mripuko kanisani huko Arusha. Ulipotokea mripuko huo na baadhi ya watu kuuawa na wengi kujeruhiwa lawama walitupiwa ‘Waislamu wenye siasa kali’. Hapo tena wakaanza kusakwa Waislamu na miongoni mwa waliotiwa nguvuni walikuwa raia wa nchi za Kiarabu waliokuwa watalii nchini. Hatimaye, Waarabu hao walionekana kuwa hawahusiki kivyovyote na shambulizi hilo. Hivi sasa wanaokabiliwa na mashtaka ya kuhusika na mripuko huo ni vijana wa Kikristo. Kwa nini hatuambiwi kuwa vijana hao ni ‘Wakristo wenye siasa kali’ kama wanavyoelezwa watuhumiwa wanaokuwa waumini wa dini ya Kiislamu? Kama ni matumizi ya tindikali katika kuwashambulia watu basi Bara nako pia mtindo huu umeshamiri. Je, tunayaonaje mashambulizi ya risasi zilizopigwa katika mkutano wa Chadema huko Arusha mjini, upigwaji nondo wa imamu katika msikiti mmoja wa Mbeya, mauaji ya waandishi wa habari Iringa na Kigoma na mashambilizi mabaya dhidi ya mwandishi mmoja wa habari jijini Dar es salaam. Halafu kuna hili tukio la karibuni la kushambuliwa Sheikh Issa Ponda huko Morogoro. Nalo hili ni tukio la kiusalama? Au ndio tuseme matukio yote haya sio makubwa na hayatishi kuliko ya  Zanzibar? Ukiitafakari hali halisi ilivyo utaona kwamba kama kuna eneo linaloweza kuwa lisilokalika kwa vile ni la hatari basi eneo hilo ni Bara na sio Zanzibar. Kwa kweli ni matendo kama haya yanayowafanya Wazanzibari wengi waamini kuwa  hawatendewi haki na baadhi ya ndugu zao wa upande wa pili wa Muungano.

‘‘Baadhi ya magazeti yanayochapishwa Tanzania Bara.
dhamira yao.’’

Kumekuwa na tabia iliyozoeleka ya vyombo vya habari vya Bara kuitangaza vibaya mno Zanzibar, hali inayotia wasiwasi wa

nyengine au wasiokuwa na imani yoyote ya kidini, bali ni majahali tu waliokuwa na lengo waliolijuwa wenyewe? Ungetaraji kuwa katika nchi yenye utawala bora na vyombo vya habari vinavyofuata maadili na uwajibikaji kwamba kwanza utafanywa uchunguzi kabla ya kuwahusisha na tukio hilo Waislamu au waumini wa dini yoyote ile, chama cha siasa au wengine wenye utashi wa jambo fulani. Kinachoshangaza ni kuona kuwa yapo magazeti ya nje ambayo yameibua mambo ambayo vyombo vingi vya habari na polisi humu nchini hawajayaeleza. Hayo magazeti ya kwetu labda yalifanya hivyo kwa makusudi au labda kwa vile undani wa suala hili haukutafutwa. Kwa mfano, gazeti la Uingereza la The Daily Telegraph la tarehe 12 Agosti liliandika kwamba mara mbili katika kipindi cha wiki moja kabla ya wasichana hao kumwagiwa tindikali

Na salim s SALIM

24

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Mazungumzo Baada ya Habari
na Rais Mstaafu Abeid Karume, Mzee Hassan Nassor Moyo na Kamandoo Dk. Salmin Amour. Je, na wao watasalimika na fukuza fukuza za CCM/Zanzibar? Bosi wa Othman Masoud ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na pia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Dk. Ali Mohammed Shein. Yeye ndiye aliyekisimamia kikao kilichopendekeza kumvua uanachama Mansoor. Akiwa Rais wa Zanzibar, Dk. Shein amenukuliwa mara kadhaa akisema hana msimamo juu ya Katiba Mpya. Lakini akiwa mwanachama na kiongozi wa CCM, msimamo wake ni wa kutaka Muungano uendelee kuwa na Serikali Mbili. Isitoshe, licha ya kuwa yeye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, Dk. Shein amekaririwa akisema haitambui Kamati ya Maridhiano, ambayo miongoni mwa mafanikio yake ni kuundwa kwa hiyo Serikali ya Umoja wa Kitaifa anayoiongoza. Haitambui Kamati hiyo iliyosimamia mazungumzo kati ya Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Amani Karume na kupigwa kura ya maoni iliyoidhinisha, hatimaye, mabadiliko makubwa ya Katiba ya Zanzibar na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Je, katikati ya khofu za wahafidhina wa Zanzibar juu ya khatima yao nje ya muundo wa sasa wa Muungano na madai ya mamlaka zaidi kwa Zanzibar, kuna nafasi yoyote ile ya kupatikana kwa mwafaka wa kwenda mbele kama Wazanzibari ndani ya CCM/Zanzibar? Jawabu ya Mwanasheria Mkuu

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

25

CCM/Zanzibar itaendelea hadi lini kuwala wanawe?
“uruhani wa Tanganyika ndio kasoro ya msingi. Kwamba imo ndani ya Muungano au haipo. Ipo, haipo. Lakini ikipanda kichwani ikatoa jina unaiona, inasema “nipo.”

Othman Masoud ni kwamba ndiyo, maana lile la “Kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar lilikuwa jambo zito zaidi kuliko mabadiliko ya muundo wa Muungano.” Othman Masoud anajulikana kuwa ni msomi na mwanasheria na sio kama mwanasiasa, na hivyo anashangaa kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wenye kuibeza Serikali ya Umoja wa Kitaifa na wanaokataa kukaa pamoja kuzungumzia Muungano wenye maslahi kwa Zanzibar. Mwanasheria Mkuu huyo alizidi kushangaa kuwa kuna wale wanaosema Serikali Tatu ni mzigo. Akiwasuta alihoji kwamba mzigo hasa ni muundo huu wa Serikali Mbili na ndio “utakaouvunja MuunganoHatujui CCM itawapokonya kadi wangapi wala hatujui wangapi watarudisha kadi kuwaunga mkono watetezi wao. Tusubiri kwani tutayashuhudia mengi katika kipindi hiki. Kitu kimoja kiko wazi: CCM imeshindwa kuelewa kwamba zama zinabadilika. Leo hii, si ajabu tena kumuona mwana-CCM na kiongozi wa juu Serikalini akiusema ukweli bila ya kutafuna maneno. Mansoor na Othman Masoud ni miongoni mwao na hatutarajii kama wao watakuwa wa mwisho. Kwa hivyo, CCM/Zanzibar itaendelea kuwafukuza wanachama wake na viongozi wa Serikali kwa kuukosoa muundo wa Muungano uliopo, maana imejihalalishia kuwa mtu hawezi kuwa mwana-CCM ndani ya CCM/Zanzibar kama anatetea muundo tafauti wa Muungano.

Lakini mbona ndani ya CCM/ Bara tumewahi kuwasikia wanachama na viongozi wake mbalimbali wakiukosoa mfumo uliopo, ambao ndio wa sera ya chama chao, na hawafukuzwi? CCM/Zanzibar ina tatizo la kutojiamini na kutowaamini Wazanzibari wenye uwezo. Kwa muda mrefu, Zanzibar haijawahi kuwa na Mwanasheria Mkuu aliye mahiri kama huyu wa sasa, lakini kwa mara nyingine tena nchi hii inapita katika kipindi kigumu. Uhafidhina ulio ndani ya mizizi ya CCM/Zanzibar hauchelei kuwaumbua Wazanzibari walio makini kama huyu, kwa maslahi tu ya wahafidhina wanaotaka kusalia madarakani chini ya ulinzi na kivuli cha Muungano wa Serikali Mbili. Lakini mwenyewe, Mwanasheria Mkuu, amekwisha lipasua jipu. Na, hakika, hakulipasua tu bali hata amelipatia dawa. “Hii ndio kasoro mama. Hii ndio kasoro kubwa. Hii ndio fitna ya Muungano. Huu uruhani wa Tanganyika. Mie naona niuite hivyo mtanifahamu zaidi. Hii kwamba uruhani wa Tanganyika ndio kasoro ya msingi. Kwamba imo ndani ya Muungano au haipo. Ipo, haipo? Lakini ikipanda kichwani ikatoa jina unaiona, inasema “nipo.” Naam, kadiri Tanganyika inavyoendelea kujificha nyuma ya pazia la Muungano wa Serikali Mbili, CCM/Zanzibar itaendelea yenyewe kuwala wanawe . Lakini ikitaka iache wanga huo wa kuwawangia wanawe, CCM/Zanzibar ikubali kubadilika kuufuata wakati, na wala sio kulazimisha kuubadilisha wakati.

Na salim s SALIM

K

wa kuwatimua kutoka CCM Wazanzibari kindakindaki kwa sababu ya hoja zao za kuitetea Zanzibar, CCM/Zanzibar inajiweka kwenye kundi la washtakiwa wanaotetewa mahakamani, lakini wenyewe wakisema: “Hatutaki kutetewa, wacha tufungwe.“ Shinikizo za kutaka Mansoor Yusuf Himid afukuzwe uanachama zilianza kwa nguvu wakati ambapo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Othman Masoud Othman, akisema anaunga mkono msimamo wa Tume ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba wa kuwa na Muungano wa Seri-

kali Tatu, huku akiupinga vikali ule wa Serikali Mbili akisema kuwa huo utauvunja Muungano. Tayari Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar, unaoongozwa na vijana wenye misimamo mikali ya kutupwa ya kihafidhina, umemtaka Mwanasheria Mkuu huyo ajiuzulu mwenyewe ama watafanya maandamano ya kumlazimisha ajiuzulu. Lililomponza Mansoor ni lilelile analoliunga mkono Mwanasheria Mkuu. Na ndilo lilelile lililowafukuzisha kazi Rais Aboud Jumbe na Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na wenzake. Othman Masoud anaweza

akawa si mwanachama wa CCM, lakini anaitumikia serikali inayoongozwa na CCM, chama ambacho sera yake ni kuendelea na muundo huu wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili kwenda Moja. Je, naye atatolewa kikoa? Mwanasheria Mkuu ana msimamo mmoja kama Mansoor. Naye pia anautetea mfumo wa Muungano wa Serikali Tatu utakaokuwa na maslahi kwa Zanzibar – “mfumo ambao utaiondoa Zanzibar kuwa manispaa, mkoa, wilaya au jimbo la Tanganyika“ – kwa lugha nyepesi, Zanzibar yenye mamlaka kamili. Zanzibar yenye mamlaka kamili anayoililia Mwanasheria Mkuu, ndiyo pia inayoliliwa

26

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Waraka Maalum

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

27

Zanzibar pia ni nyumbani pa WakrIsto
Na Mwandishi Maalum
hiyo.  Baada ya kuimarisha utawala wake kisiasa, kiuchumi na kijeshi, Sayyid Said akaanza kuwakaribisha wageni wengine katika makao yake makuu, Zanzibar.  Aliwaruhusu watu wa dini zote kuendesha shughuli zao za kidini walivyopenda. Japo alikuwa Mwislamu mwenye imani kamili, Sayyid Said alionesha mfano bora wa uvumilivu juu ya mahitajio  ya kidini ya waumini wa dini nyingine.  Warithi wake nao wakaufuata utaratibu wa mzee wao kwa kuruhusu kuanzishwa mahekalu ya Kihindu, makanisa mawili – moja la Kikatoliki na jengine la Kiprostanti, sehemu za mazishi za Maparisi wafuasi wa dini ya Zoroastriani na misikiti kwa kila madhehebu makuu au madogo ya Kiislamu katika mji mmoja. Baada ya Wareno kurudi nyuma, Wakristo kidogo tu wa jamii ya Magoa ndio waliobakia Zanzibar. Wakristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia ibada zao lakini waliweza kuihuisha jumuiya yao kwa kufanya ibada zao binafsi kwa faragha.  Baadaye katika miaka ya 1800 makundi ya watu kutoka Ulaya yalianza kuingia Zanzibar yakiwajumuisha Wamishionari waliokuwa wakipitapita mara chache na wachungaji katika meli bandarini.  Katika mwaka 1844, Wamishionari zaidi waliwasili Afrika ya Mashariki kwa kupitia Mchungaji wa Kilutheri, Joseph Krapf, na wafuasi wawili ambao walifanya kazi kwa ajili ya Jumuia ya Kimisheni ya Kanisa la Kiingereza. Wakiwa wanafanya kazi Mombasa, walitembelea Zanzibar na miaka michache baadaye walichapisja kamusi zuri la Kiswahili na Kiingereza, ingawa hawakuwahi kuanzisha kanisa visiwani Zanzibar. Katika Septemba 1860, Abbe Favat aliyekuwa mhubiri maarufu wa Kikristo aliyetokea Ufaransa, alitiliana saini mkataba na Seyyid Said wa kumruhusu ayahamishe makao makuu yake kutoka kisiwa cha Reunion hadi Zanzibar. Kufikia mwezi Desemba, kikundi chake cha “mapadri wawili wasio watawa na watawa sita wa kike” (“Filler de Marie”) walikuwa wakiishi katika makazi ya watawa ambayo pia yalikuwa na kanisa dogo hapo Shangani.  Jengo hili la watawa linasemekana lilijengwa mwaka 1860, lakini ujenzi huu inawezekana ulikuwa ni wa matengenezo makubwa ya nyumba iliyokuwepo kabla.  Kanisa dogo katika jengo hili lilikuwa ni kanisa la kwanza lililojengwa Zanzibar kwa miaka 200. Baadaye Sultan Majid, mwanawe Sayyid Said, wakati wa enzi yake aliwaruhusu Wafaransa hao kufungua duka mjini Zanzibar, hatua iliyotafsiriwa kama juhudi za Sultan huyo kuweka “uwiano wa nafasi kubwa waliokuwa nayo Waingereza visiwani Zanzibar kwa kuwakaribisha wapinzani wao wakuu wa Kizungu.”  Wamishionari wa Kifaransa walikuwa makini kuepuka matatizo yoyote Zanzibar “kwa kutambua uhalisi wa maisha ulivyo ndani ya nchi ya Kiislamu ya Zanzibar, kuanzia mwaka 1862 wafuasi wa Holy Ghost Order, waliamua kujikita katika maeneo maalum kama ya elimu, shughuli za uchungaji kwa jumuiya ndogo ya mjini ya Magoa Wakatoliki na walifungua hospitali ya mwanzo ya Kizungu iliyopendekezwa na Sultan mwenyewe. 

U

kristo una historia ndefu Zanzibar. Uliletwa kwa mara ya mwanzo na Wareno.  Wareno wakielekea juu kutoka kusini baada ya kufanikiwa kuizunguka Rasi ya Matumaini Mema – Cape of Good Hope – katika mwaka 1488 walifanya jaribio la nguvu la kudai bandari, njia za biashara na raslimali kiasi cha maili 2,000 za mwambao wa Afrika. Baada tu ya kuwasili Zanzibar, walianzisha Ujumbe wa Kanisa Katoliki na kituo cha biashara ndani ya mji wa Zanzibar katika mwaka 1499. Kwa miaka 200 iliyofuatia, Wareno walihodhi njia za baharini za Afrika ya Mashariki na walijitahidi kuanzisha msururu wa makazi katika eneo lote la mwambao.  Mabaki ya makazi yao bado yanaweza kuonekana karibu na Fukuchani Kaskazini Unguja na kisiwani Pemba.  Ngome Kongwe, ambayo ipo karibu na bandari ya Unguja, ilijengwa juu ya eneo lilipokuwepo kanisa la mwanzo la Kikatoliki, baada ya kutekwa na jeshi la Omani.  Inasemekana jeshi hilo liliitwa na wenyeji wa Unguja na Pemba kuwasaidia kuwang’oa Wareno waliokuwa makatili na madhalimu. Mnamo mwaka 1841, mbabe wa kivita wa Kiomani, Sultan Seyyid Said bin Sultan al-Busaid, alivutiwa sana na visiwa vya Zanzibar, na kwa hivyo alihakikisha anayahamishia huko makao makuu yake . Kuanzia hapo Oman na maeneo yote yaliyokuwa chini ya himaya yake yakawa yanatawaliwa kutokea Zanzibar, kwani ndio uliokuwa mji mkuu wa himaya

‘Baada ya Wareno kurudi nyuma, Wakristo kidogo tu wa jamii ya Magoa ndio waliobakia Zanzibar. Wakristo hawa hawakuwa na kanisa la kufanyia ibada zao lakini waliweza kuihuisha
Juu ya ukarimu wa watu wa Zanzibar, Wazanzibari hawakuwa na azma yoyote ya kufuata dini ya wageni hawa wapya.  Wamishionari wa Kikatoliki walilielewa hili, lakini waliamini kwamba kundi kubwa la wafuasi wapya wa dini hii ya Kikiristo lingeliweza kupati-

jumuiya yao kwa kufanya ibada zao binafsi kwa faragha.’
kana Tanganyika, masafa mafupi baada ya kuuvuka mlango bahari wa Zanzibar. Hivyo, walipeleka ujumbe mdogo Bagamoyo mwaka 1868 na kwa sehemu kubwa walitumia nafasi walizonazo Zanzibar kama ni makao makuu ya kuzidisha harakati zao ndani ya ardhi ya Bara. Hivyo ndivyo Ukristo ulivyosambaa Bara ukitokea Zanzibar. Ndio maana sababu za mashambulizi ya karibuni dhidi ya Wakristo kisiwani Unguja zilizotangazwa na

vyombo vingi vya habari ndani na nje ya Tanzania hazina mashiko ya kihistoria. Tanbihi: Makala haya yameandikwa kwa msaada mkubwa wa makala “Wakristo wa Zanzibar“ inayopatikana kwenye mtandao wa www.zanzibarhistory.org. Msomaji anashauriwa kuisoma makala nzima kwenye kiungo hiki: http://www.zanzibarhistory.org/wakristo_wa_zanzibar.htm

28

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Ladha ya Beti

Barua za Wasomaji

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

29

N

N’na Jini Aniwina
Tushapiga makafara, na kusoma tawasuli
 Jini bado yu imara, hana hata mushkeli
 Aniletea madhara, anitesa kweli kweli
 Hataki kutoa jina Tukasoma na rukia, visomo vilo vikali
 Yu kichwani asinzia, wallahi hata hajali 
Atucheka nadhania, atuona madhalili
 Katu hakutoa jina Magwiji mlo nyumbani, nadhani mwanisikia
 Wa Chambani na Bumbwini, wa Ole na Nungwi pia
 Muje mutie ubani, mwenenu nateketea
 Mumng’oe aondoke

Ushauri wa bure kwa Mansoor
Mhariri

na jini aniwina, ananipanda kichwani
 Hataki kutoa jina, ananipa mtihani
 Visomo tushavisoma, haongei asilani
 Hataki kutoa jina Hataki kutoa jina, ya kwamba yeye yu nani
 Nani aliemtuma, na kaja kwa shida gani
 Maluuni aniwina, mwaka wa arobaini
 Hataki kutoa jina Tushaupiga uganga, wa kofi na kufukiza
 Wakakutana waganga, jinale kumuuliza
 Lakini jini apinga, yu nami aniumiza Kagoma kutoa jina

I

Suleiman Hakum Mpendae - Zanzibar

S

Zenji Ninakulilia
Walopewa madaraka, kutwa wamo vikaoni
 Kujitia hangaika, na kujivisha huzuni
 Kubwa wanalolitaka, waonekwe tiviini
 Si kwa shidazo watani Meli zinapopinduka, tasikia hotubani
 “Sote tunasikitika, kwa hii kubwa huzuni”
 Mapesa yakachangishwa, kwa jina la masikini
 Watu wako ya watani Mapesa huyachangisha, kutoka nje na ndani
 Mabilioni ya pesa, yakaishia hewani
 Watuwo waathirika, ‘kaambulia vipeni
 Tadhlili ya watani Watuwo wadhalilika, wanotaka kukuhami
 Magerezani kuswekwa, na kuitwa mahaini
 Kosa kubwa walitaka, hadhi yako ya zamani
 Hawajatoka watani Ni mengi yanofanyika, ya dhuluma ya watani
 Zenji ishafisidika, dhulma ndio sukani
 Yote ningeyaandika, ningeweza natamani
 Ila siwezi watani

auti yanikauka, kuulilia watani
 Machozi yapukutika, pukupuku mashavuni
 Kifua chatatalika, chakatikia kwa ndani
 Kwa kulilia watani Dola iloimarika, ndivyo ‘likuwa zamani
 Mashariki Afrika, kusiwe na mpinzani
 Wageni wakavutika, kuja weka maskani
 Sasa uwapi watani Wageni walivutika, kuja weka maskani
 Walitoka Amerika, Uchina na Arabuni
 Wahindi na Sri Lanka, Zenji pakawa nyumbani
 Nasononeka watani Watani nasononeka, hikuona hilakini
 Mamlakayo kupokwa, ukawa huna hunani
 Na watuwo wateseka, kukimbia watamani
 Huzuni kubwa watani Watu wako wateseka, kuhajiri watamani
 Majumba yaporomoka, hakuna wa kuyahami
 Walopewa madaraka, yaishia matumboni
 Yasikitisha watani

Kipwerere katika Mzimu wa Watu wa Kale, kile kitabu maarufu cha mwandinaonekana ile misingi ya kulindana, shi gwiji wa Zanzibar, Mohamed Said kuweka siri na kujiweka kuwa wao La kufanya ni kusimamia nadharia ya Abdalla (Bwana MSA). ni wa mfano kwa namna ambayo kutaka Zanzibar iwe huru, aendelee Mwalimu Julius Nyerere aliiweka, kujitapa kuwa yeye ni mwanachaHakuna aliyeyafahamu maelezo ya haipo tena kwenye CCM ya leo. Itikadi ma halisi wa CCM na kujinasibisha Kipwerere pale alipopanda kichwani, imepotea na sasa ni ’burtangi’ – kien- na baba yake na mchango wa mzazi hadi pale Bwana MSA alipoyatafsiri dacho arijojo kuelekea kwenye waya wake huyo kwa chama cha Afro maana ya kiza alichokieleza Shetani za umeme – tena zile zenye umeme Shirazi. Aiwache historia imhukumu. huyo ya “Nyekundu na Kiza“. mkubwa. Asichopaswa kufanya ni kutajaruki, “Kiza ni mauti,“ Bwana MSA akaelezea Kwa nini nikasema hayo? CCM wali- asiwapige pande wenzake wa CCM na “na nyekundu ni damu“. Na kweli, wahi kuwasema sana Chama cha asiende popote pale wala asiuwachie likaja kusibu aguo lake kwa kuonekaWananchi (CUF) juu ya suala la wakati umhukumu. na Bwana Ali Bomani kauliwa na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid, kukatwa kichwa na kupakatishwa na kuonyesha kuwa wao, CCM, wana Nini kitachomtokea akifanya au akia- boga mikononi mwake na kichwa utaratibu madhubuti wa kutatua cha kufanya hivyo? kutoonekana. tafauti zao za ndani. Lakini sasa, Atakuwa mshindi na atawashinda hao na wao wanaelekea huko huko. maadui zake, kwani wimbi la maba- Hadithi hii ukiiunganisha na kinWalichokifanya CUF na wao wanaki- diliko sasa linavuma Tanzania kwa achoendelea kwenye uongozi wa tenda. jumla — Bara na Visiwani — huku CCM, basi utaona kuwa nako ni “kiza nchi ikielekea katika kipindi cha mpito na kwekundu“. Yaliyobaki, maliza Sasa wanataka kumfukuza Mansoor ambamo khatima ya taifa inaelekea mwenyewe. Yusuf Himid. Hapa naomba nimpe kwenye kiza na kati yake kuna ndugu yangu Mansoor ushauri wa uwekundu. Kipara Msoko, bure wa mambo ambayo anapaswa Mpendae - Unguja kuyafanya na yale anayopaswa kuy- Hayo, kama alivyosema Shetani

aepuka endapo CCM watathubutu kumfukuza.

Hili si la kwetu
Mhariri, Ipo haja ya kuyatazama matukio haya kwa jicho la pili. Maana baadhi ya matukio hayo kama vile mauaji ya kinyama na mashambulizi ya viongozi wa dini na watu wengine si sehemu ya dasturi za watu wa mwambao. Kuna

Hamad Hamad

 Copenhagen - Denmark

30

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Tufungue Kitabu

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

31

Karamu ya Jumba Maro
K
Na mohammed GHASSANI
Matokeo yake yakawa ni yaleyale ya mjumbe wa Jumba Maro. Mjumbe aliyekuwepo Zanzibar alikuwa ni gazeti la Dira, mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambalo lilijitolea kuandika na kuchambua masuala mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa yaliyohusu khatima ya Zanzibar. Lakini nalo likaandamwa hadi likafungiwa moja kwa moja na serikali, huku mhariri wake mkuu, Marehemu Ali Nabwa, akigeuzwa mkimbizi kwa kutangazwa si raia katika nchi ya mababu na mabibi zake. Mjumbe kaemewa. Baada ya ushairi huo kuifungua hadithi, mwandishi ameanza kwa kitendawili cha kuingia nyoka katika chumba cha Bwan’ Tajir, ambacho kwa namna kilivyojengwa hakukuwa na uwezekano wowote wa nyoka huyo kufika huko. Kuingia kwa nyoka huyu kulimshtua sana Bwan’ Tajir kiasi ya kwamba alimtoa kazini nokoa wake mkuu kwa kuwa uchunguzi wa barza aliyoiunda kuchunguza mkasa wenyewe ulibaini kuwa nyoka aliingia kwa uzembe wa nokoa huyo. Tafrani ya kuingia kwa nyoka katika chumba cha Bwan’ Tajir ndiyo inayotuunganisha na kiini cha hadithi yenyewe. Kwamba sio tu kuwa Bwan’ Tajir alikuwa akimuogopa nyoka huyu binafsi, lakini pia alikuwa amekusudia kupika karamu kubwa na kuwaalika watu wazima wote wa mji kuja kula kwake, katika kasri lake. Kwa hivyo, kwa upande mmoja kujitokeza kwa habari hii kungelisababisha watu wengi kusita kuja katika karamu hiyo kwa kukhofia usalama wao. kwa upande mwingine kujitokeza kwa habari hii kungewapa watu picha halisi kwamba naye Bwan’ Tajir ni mwoga na kwake kunapenyeka,. Na fahari ya Bwan’ Tajir ni “kuwa watu wote kabisa washiriki katika karamu yake, wale wanywe fadhila zake” (uk. 92), bila ya kuushuku woga wake na ugoigoi wa himaya yake. Mwandishi anatuonesha kuwa, hata hivyo, Bwan’ Tajir si mtu wa fadhila kiasi hicho. Hana ukarimu jambo. Kupitia nong’ono za watu, tunajifunza kuwa huyu ni mtu bakhili na mwenye tabia ya uchoyo mno kiasi ya kwamba hutia ndizi na dagaa katika mifuko yake ya suruali ili asiombwe. Swali ambalo watu walikuwa wakijiuliza ni vipi angeliweza kuwakirimu watu wa mji mzima? Hatimaye karamu inapikwa na kuliwa, lakini, kama ilivyokhofiwa tangu mwanzo, karamu hiyo ilikuwa na mapungufu kibao kiasi ya kwamba haikuwa halali hata kidogo kusema kuwa ilikuwa ‘karamu ya mji’. Wengi wa watu walikosa hata tonge moja ya biriani huku wachache wakiwa wamekula zaidi ya sahani moja. Na hata hao waliopata kula, wengi wao walikuwa ni watoto na sio watu wazima wa mji kama ilivyoahidiwa mwanzoni. Hao watu wazima waliokoseshwa, walikuwa wamekoseshwa katika mazingira ya kutatanisha na kusikitisha kabisa. Kwa mfano, mwandishi anatwambia kuwa kuna wengi waliokataliwa kuingia katika ukumbi wa dhifa kwa kuwa bawabu hakuzitambua kadi zao za mwaliko. Ati zilikuwa na rangi tafauti na kadi alizoagizwa kupokea. Kuna wengine walikuwa na kadi zenye rangi ndizo, lakini walikataliwa kuingia kwa kuwa herufi za majina yao ni tafauti na wanavyoyatamka. Katika ukurasa wa 93, bawabu anamuuliza mwenye kadi: “Mbona umeniambia jina lako Ahmed na humu limeandikwa Ahmad?” Mwenye kadi anajitetea kuwa si yeye aliyeandika kadi hiyo, bali ni karani wa Bwan’ Tajir. Anasema kwamba hata yeye alimwambia na mapema karani huyo juu ya kukosewa kwa herufi moja kwenye jina lake, lakini karani alimhakikishia Ahmed kuwa hapatokuwa na taabu yoyote ile: siku ya karamu, atakula tu. Lakini leo hii bawabu anamwambia Ahmed: “…hutaramba karamu….saa ya kutazama makosa imekwisha. Kazi yangu ni kutazama kadi sahihi. Asiyekuwa nayo haingii”. Na kweli Ahmed, na wenziwe wa mfano wake, hawakuruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa karamu. Kwa hali hii watu wazima wengi wa mji wakakosa kula karamu waliyoandaliwa na Bwan’ Tajir. Ilikuwa kana kwamba huu ulikuwa ni mpango uliofanywa makusudi na Bwan’ Tajir na wasaidizi wake, maana hata watu hawa walipolalamika kuwa wamekoseshwa karamu, hakuna mwenye mamlaka aliyewasikiliza. Hata Shawishi Mkuu, ambaye ndiye aliyekabidhiwa jukumu la uandazi, alipoambiwa kuhusu hilo, alisema haiwezekani kuwe na watu waliokosa chakula ilhali biriani huko ndani ilikuwa ya ‘kupigia mbwa’. Watu walipomuapia kuwa wao hawajaramba kitu, aliwanuka viganja vyao. Alipoona ni kweli havinukii harufu yoyote ya machopochopo, akawaruka hapo hapo: “Waongo hawa. Wamekula kisha wakaenda kunawa na wanataka kudanganya kula mara mbili”. Masikini watu wazima wale, wakasawijika kwa kuambiwa kuwa wanazua ili wajilie mara mbili ilhali hata hiyo moja hawakuipata. Hivi ndivyo karamu ya Bwan’ Tajir ilivyoishia. wa vile kitabu cha Jumba Maro si riwaya yenye hadithi moja refu, bali mkusanyiko wa hadithi nyingi fupi fupi, tutachambua moja tu kati ya hadithi 12 zilizomo, tukiamini kuwa itatusaidia kuuona undani wa ‘Jumba’ lote. Hadithi iliyopewa jina la Karamu, kama zilivyo nyingine, inaanza na ushairi uitwao Mjumbe Kaemewa. Ushairi huu unasimulia masaibu yaliyompata mjumbe aliyetumia kalamu yake kuandika mambo ya kweli ili watu wake waelewe kile khasa kilichotokea. Lakini kumbe hakujua kwa kufanya hivyo alikuwa anakosana na wakubwa. Matokeo yake ni kwamba mjumbe huyu aliadhibiwa kwa kuwekwa jela na kukatwa kidomodomo chake. Zanzibar kulikuwa na mjumbe kama huyu ambaye naye aliamini kuwa kwa kuandika ukweli, alikuwa anaisaidia jamii yake kufahamu mambo na hivyo kuifanya isimamie ukweli siku zote. Lakini naye pia alikuwa anawakera wakubwa.

32

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

Michezo
Mwandishi aligundua kitu kimoja cha ki-Majham pekee: kinapotokea kitu katika mazungumzo kinachomkuna husema ‘awii’. Mwandishi akizungumza na Abdul Majham nyumbani kwake Mwandishi: Je unakumbuka mwaka uliozaliwa? Majham: Miye sikumbuki lakini labda uwaulize wale niliocheza nao watu kama kina Sayyid Ali Soud, lakini ninachoweza kukisema kuwa ninafahamu fika kuyajuwa yaliokuwa yanaendelea kwenye Vita Vikuu vya Pili wakati huo ni mtoto wa makamo naenda chuoni kusoma Qur’an.

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

33

ya Umeme pale Public Works Department (PWD) na nilifanya kazi hapo kwenye miaka ya 1950 hadi kufikia Mapinduzi. Halafu nikawa nafanya kazi katika Shirika la Umeme na nimefanya kazi hapo hadi kufikia kustaafu. Mwandishi: Baada ya kuzungumzia maisha yako kwa jumla hebu tugeukia michezo. Kitu gani kilikuvutia kucheza soka, hoki (mpira wa magongo) na kriketi (cricket)? Majham: Nimeanza kucheza soka nikiwa na umri wa miaka sita na nilikuwa hodari wa kupiga chenga tangu umri huo. Ninapocheza na watoto wenzangu kila mtu huvutiwa namna ninavyochukua mpira na kuwapiga chenga wenzangu. Nilipokuja kuona filamu ya Garincha pale Ofisi ya Filamu ya kina Mohammed Kassim, hapo ndipo ikawa nikichocheo kikubwa kwangu kuwa nakokota mpira na kuhesabu wachezaji, ingawa Mwalimu wetu ‘Mr. Mazal’, huyu ni Ahmed Iddi Mjasiri. alikuwa hapendi kumuona mtu anakaa na mpira kwa muda mrefu. Mwandishi: Majham wewe ni mzaliwa wa Malindi, verejee ukachezea Vikokotoni? Majham: Ukweli miye sipendi mambo ya kifahari wala kujiweka mbelembele. Miye mambo yangu ni kutopenda mambo ya kifakhfakh. Kwa sababu hizo ndio nikenda Vikokotoni, ingawa nilicheza muda mfupi katika timu inayoitwa Hadhrami. Haya mambo ya Hadhrami yawache kwani yana hikaya refu. Mwandishi: Kwa nini isiwe Kikwajuni, Mwembeladu, Miembeni? Majham: Miembeni au Kikwajuni zama hizo kulikuwa ni sawa kwa leo kama upo maeneo ya Mwanakwerekwe,. Doooh, ingekuwa taabu kwangu. Mwandishi: Taabu ya nini? Majham: Uwwih, alaaa, [kacheka sana bila ya kutaka kuendeleza]. Mwandishi: Ulianza kuchezea Gos-

sage mwaka gani? Majham: Nakumbuka nilianza kucheza Gossage 1952 nakupa na hiyo picha uone . Nilikuwa na kina Mzee Mwinyi(Mpiringo) Mzee Ahmed Islam, Seif Rashid, Maulidi Mohamed (Machaprala) na wengineo. Tulicheza Nairobi tulikuwa washindi wa pili. Tuliwafunga Waganda na Tanganyika, tulilala kwa Kenya na ukweli Kenya ikitupa tabu sana, kwani wakitumia nguvu za hali ya juu na sisi tulikuwa na wachezaji wachache ambao wakitumia nguvu. Sisi mchezo wetu ni dama, mfano wa Brazili. Unaweka karata kwenye bao, unaanza nyuma unafika kati, unachezewa kidogo, unapelekwa wingi, unawekwa kati, haooo, tunarudi, huo ndio mtindo wetu. Kenya wao pasi tatu wako golini. Kutoka hapo niliendelea kuchaguliwa kwenye timu ya Gossage mpaka mwaka wa 1968 ndio nikamalizia kucheza timu ya taifa. Nimecheza na kina Kassim bin Mussa, Sururu, Khalid Kessi, Boti mkubwa wa Malindi, nikaja nikacheza na vijana kina Boti mdogo, Abdimout Ajmi, Saad, Hijja Saleh, Seif Rashid, Seif Nassor (Mshumaa). Kisha nilikuwa na fowad nikistaladha kucheza nao, huku Ahmada Mwanga, huku Mossi Kassim, Mkweche kushoto, Ahmada Mwanga na mfalme wa hewani Mohammed Kassim, uwwih, alaaa. Hapo nakwambia kigoma tukikipiga, waulize Warusi waliokuja na kuzifunga timu zote za Afrika Mashariki na kuja hapa tukenda suluhu nao, Warusi hawajaweza kuamini, siku hiyo mpate Ahmada Mwanga na Mkweche watakuelezea kigoma tulivyokipiga, ilikuwa kila mtu anazungumza juu ya game hii. Kikosi cha timu ya Gossage ya Zanzibar mwaka wa 1952 Mwandishi: Mchezo gani unaoukumbuka na hutousahau? Majham: Gossage Zanzibar mwaka wa 1966, timu yetu ilikuwa 1. Bobea. 2. Sleiman Amour 3. Tindo 4. Ahmed Himidi London 5. Majham 6. Kitwana Rajab 7. Mossi Kassim, 8.Moham-

Majham: Lulu Iliyotupwa
Wengi wanamjua kwa jina lake la mkato: Majham. Kuna wanaomwita ‘Pele wa Zanzibar’. Angelikuwa amezaliwa Ulaya, Marekani au hata Amerika ya Kusini hii leo angelikuwa anaenziwa. Hakujaaliwa bahati ya akina Boby Charlton, Geoff Hurst, Johan Cruyff, Platini, Pele, Blokhin, Hadji, Latto, Tostao, Gerson, Romario. Angelijaaliwa bahati hiyo basi angelikuwa fahari ya nchi yake kwani zama zake Majham alikuwa amebobea katika michezo miwili — soka na hoki (mpira wa magongo). Viwanja vya soka vikimjua, viwanja vya hoki vikimtambua. Siku hizi ukimtafuta Majham hutompata kwenye viwanja vya soka wala vya hoki. Kwanza vya hoki haviko tena Zanzibar kwani hoki haichezwi tena nchini mwetu. Mchezo huo ulipigwa marufuku baada ya Mapinduzi ukionekana kuwa ni spoti ya kibwanyenye. Siku hizi ukimtaka Majham itakubidi wende Mchangani. Zikate kona mbili tatu hadi nyumbani kwake. Ukibahatika utamkuta amekaa barazani. Saa zote anakuwa mpweke hapo barazani kwake akitafuta rubaa la washabiki wa spoti wa kuweza kuzungumza naye. Ingawa ni mpweke hataki kujinasibisha na chochote kile. Hii leo Majham — jina kamili Abdul Majham Omar — amekuwa mfano wa lulu iliyotupwa. Pamoja na uzee, ana umri wa miaka 79, Majham siku hizi ni dhaifu, ganzi ya miguu inamsumbua na haoni sawasawa.

Mwandishi: Itakuwa labda una umri wa miaka 9 hivi wakati huo wa Vita Vikuu vya Pili vya dunia? Majham: Zaidi, labda miaka 11 au 12. Mwandishi: Nikifanya mahesabu unafikia umri wa miaka 79. Majham: Nakubaliana na wewe. Mwandishi: Nielezee maisha yako kwa mukhtasar? Majham: Mimi ni mzaliwa wa mtaa wa Malindi na ndipo nilipokulia. Nalianza masomo yangu ya Qur’an chuo cha Maalim Jeledi Nilisoma hapo mpaka nikahitimu na huku nikiendelea na masomo ya msingi katika skuli ya Gulioni. Naikumbuka Gulioni na nina masikitiko kuwa jengo la skuli hiyo halipo. Nawakumbuka baadhi ya walimu wetu ambao walikuwa sio walimu wenye kusomesha lakini walikuwa ni wazazi wetu. Unaposomeshwa na Maalim Burhan au Maalim Buda au Maalim Badi unajikuta kuwa upo na sehemu ya wazazi wako. Sijabahatika kusoma na kufika mbali, nalimaliza masomo hapo Gulioni skuli nilipofika chumba cha 5. Mwandishi: Baada ya masomo ya msingi ulikuwa unafanya nini? Majham: Zamani sio leo, kila mtu alikuwa ni mzee. Nilitafutiwa kazi [na wazee] na kupata kazi sehemu

34

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

ZANZIBAR DAIMA ONLINE AGOSTI 23-07 SEPT

35

kwanza kucheza kombe la klabu la Afrika ilikuwa ni Cosmopolitan chini ya Mwalimu Mansour Magram. Tulicheza na timu ya Somalia tulikwenda suluhu 1-1 pale kiwanja cha Ilala Dar-es-Salaam na tukashindwa kwenda Somalia kwa mbinu za FAT kutotaka twende. Silisahau hili. Tupo klabu tunasubiri safari na mabegi yetu tunaambiwa hamna safari. Tulikuweko pale kina Abdimout, Msuba, Msomali, Emil Kondo, Marandu, Abuu, Kitwana Douglas, Masiku, Rajabu, Iddi Balozi, Makanda. Tulikuwa tuelekee Somalia zikafanywa hila na haya yanakwenda na kujirejea. Jengine, kama unavyoniona nipo mgonjwa. Nashukuru nimepata kuonana na Rais [Ali Mohamed Shein] nikaambiwa nitapatiwa matibabu nje ya nchi, lakini hadi leo hakuna lilofanyika na hali yangu ya kiafya inakwenda chini. Aidha namshukuru Waziri Mohammed Aboud na ile kamati ya mtoto wa muuza magazeti [Farouk Karim] na wewe mwandishi naambiwa umo, kufanyisha mchango wakuweza kunisaidia nashukuru sana, sana. Wito wangu Serikali ijuwe sisi tulilitumikia Taifa basi tuangaliwe kama wenzetu huko Ulaya na kwengineko. Tumetupwa useme kanda la usufi, puuuu

Timu ya Zanzibar katika kombe la Gossage 1952

med Kassim. 9. Peter 10. Ahmada Mwanga 11. Maalim Seif Nassor (Mshumaa). Tulifungwa na Kenya, tukalala kwa Tanganyika na tukenda suluhu na Uganda. Natamani kungekuwa na filamu yake ungeona namna tunavyocheza. Yule kocha wa Tanganyika aliwahi kusema lau ningeipata timu hii ya Zanzibar ningekuwa juu. Kikosi cha timu ya Zanzibar kilichocheza Gossage 1966 Mwandishi: Tuzungumzie hoki (mpira wa magongo) na kriketi (cricket). Majham: Kriketi sijacheza. Nilijaribu nikaona mchezo haunifai, kwani unachukua muda mrefu, lakini

mpira wa magongo nilicheza baada ya kushauriwa kuwa nitasaidia hoki ambayo ilianza kupotea baada ya Mapinduzi. Nikasema kuwa nipo tayari lakini naogopa kucheza mbele, nikapendekezwa nicheze golikipa na nikakubali. Ukipa wangu ulikuwa nachanganya na utaalamu wa soka nikawa natoa pasi nacheza kijanja, nikapata sifa nikawa nachaguliwa timu ya taifa miye, kijana Islam Ahmed Islam nimecheza mpira na babake, halafu huyu Daktari Mohamed Jidawi tukicheza pamoja timu ya Taifa ya Tanzania. Umetaja kriketi, nikipenda kuwaangalia vijana wawili wazalendo wakichezea Comorian, Zaghalouli na Ahmed Himidi. Wakikutana hao, basi utaona raha. Zaghalouli anapi-

ga mipau, mipira kaokote jumba la Makumbusho, lakini Ahmed Himidi kutwa yupo kiwanjani anazuia tu, akiwapa taabu kwelikweli warushaji mipira. Mbona leo umeazimia kutaka kuniliza? Leo wapi… nchi hii watu wakicheza futuboli, hoki, kriketi, tenis hata gofu. Michezo yote imekufa isipokuwa soka. Kuna wachezaji kama Ahmed Himidi London akicheza michezo yote hio, sio kucheza tu, lakini akichaguliwa katika timu ya taifa kwa kwa kile mchezo. Mwandishi: Unanyongeza? Majham: Nyongeza ninayo. Kwanza mbona hujaniuliza kuwa timu ya

Timu ya Zanzibar katika kombe la Gossage mwaka 1966 Mwandishi wa Zanzibar Daima kushoto akizungumza na Abdul Majham

Sign up to vote on this title
UsefulNot useful