You are on page 1of 13

KITABU CHA UHIFADHI KWA JAMII KATIKA BAHARI YA HINDI NA 6

MIAMBA YA MATUMBAWE KATIKA BAHARI DUNIANI


NA Shawn Peabody
WALENGWA: WANAJAMII, WANAFUNZI MCHORAJI: NADY RATSIMBAZAFY

i e n c e A ss

Sc

ia

ti

on

WI

W e

Indian Oc ern st

n ea

MSA

ar

Wanyama wote wa baharini wanaweZa kugawanywa katika makundi mawili.

Wanyama wanaotumia muda wote wa maisha yao karibu na maeneo walipozaliwa na ambao kwa kawaida hawaendi mbali sana ni wanyama wakazi.

Na wanyama waliopo kwenye safu ya bahari wakisafiri umbali mrefu, wakati wote husafiri kujitafutia chakula chao na kwa nadra hukaa kwenye eneo moja kwa zaidi ya siku chache

Wanyama wakazi hukaa kwenye eneo moja kwa maisha yao yote.

Kama samaki wote wakazi wataondolewa kwenye eneo, hawawezi kurudi tena.

Samaki kutoka maeneo ya jirani hawatarudi kwa sababu waNAhofia kupita kwenye maeneo yaliyo wazi ya bahari ambapo hakuna sehemu ya kujificha.

Samaki wa kwenye safu ya maji huzunguka sehemu mbalimbali za dunia wakitafuta chakula wakati wote. Wanyama hawa hula kiasi kikubwa cha chakula kwa mda mfupi. Kama wakiishi eneo moja , wanaweza kula kila kitu kwa haraka na kukosa chakula.

Samaki wanaoishi kwenye safu ya maji ya bahari hupata chakula kwenye maeneo mengi duniani.

Kwenye maji ya baridi sana.

Karibu na miamba ya matumbawe

Na kwenye misitu ya mwani chini ya maji.

Endapo eneo moja limekufa na halina chakula.

Wanahamia mahali pengine.

Kwenye eneo lililokufa samaki wakazi hawapo.

Na samaki wa kwenye safu ya maji hawawezi kuishi maeneo hayo kwa muda mrefu, hivyo ni vigumu kuwakamata hapo.

Kama utaenda kwenye kina kirefu cha bahari mbali na miamba , unaweza kukamata baadhi ya samaki wanaoishi kwenye safu ya maji ya bahari.

Lakini kama miamba yote itakufa, samaki wa kwenye safu ya bahari hawatapita mara kwa mara, hata katika maji ya kina kirefu.

Samaki wa kwenye safu ya bahari wanahitaji matumbawe yaliyostawi ili waweze kuishi.

Matumbawe yaliyostawi ni kama migahawa kwa samaki wa kwenye safu ya maji kwa sababu husafiri sehemu mbali mbali za dunia kwenye mikondo ya bahari wakitafuta chakula. Miamba iliyokufa ni kama migahawa iliyofungwa.

10

Duniani kote watu wanavua kwenye bahari, wakiathiri miamba na misitu ya mwani sehemu ambazo samaki wa kwenye safu ya maji hutegemea kwa chakula.

Mingi ya migahawa hii duniani kote inaharibiwa na uvuvi wa kupita kiasi, njia haribifu za uvuvi na uchafuzi wa mazingira.

11

Wavuvi duniani kote wanaunganishwa na miamba na bahari za dunia.

Endepo mingi ya migahawa hii itafungwa kutakuwa hakuna samaki tena. Watu watakufa kwa njaa dunia nzima. Na vita vitalipuka kugombea chakula kilichobaki.

13

Lakini kama watu duniani kote watalinda rasilimali zao za bahari pamoja na maeneo tengefu na kwa kuondoa nnjia haribifu za uvuvi, tunaweza kuzuia mwisho huu mbaya.

Ili kulinda bahari duniani na mustakabali wa binadamu wote, inatupasa kufanya kazi pamoja. Kama kila mmoja atalinda miamba iliyo jirani naye ili isiharibiwe kutokana na njia haribifu za uvuvi na uvuvi wa kupita kiasi wote tutafanikiwa.

14