You are on page 1of 104

1

HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO


KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA
KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE,
DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015
Mheshimiwa Spika;
Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha
kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu
na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi
imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia
nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze
kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini,
shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na
shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi
rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari

mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama


salmini.

Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari

hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika


uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza
kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa
kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake
wakipewa nafasi wanaweza.
Mheshimiwa Spika;
Niruhusu pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati
kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kazi kubwa na nzuri
mliyoifanya. Mmetimiza ipasavyo wajibu wao wa Kikatiba
wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukuru
kwa ushirikiano wenu na msaada wenu.

Ni ukweli ulio

wazi kuwa bila ya ninyi Wabunge wetu na Bunge hili,


tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo tuliyoyapata.
Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima kubwa
mbele ya wananchi.

Mmeitendea haki demokrasia ya

Tanzania na kuliletea heshima kubwa Bunge letu nchini,


kikanda na kimataifa.
Mheshimiwa Spika;
Tarehe 30 Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa
nilielezea mtazamo wangu kuhusu nchi yetu na kutaja
majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya Awamu
ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele
hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16
Julai, 2010 wakati wa kuvunja Bunge hilo nilielezea
mafanikio tuliyopata na changamoto zilizotukabili katika
kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa kuzindua
Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya Serikali ya
Chama cha Mapinduzi katika kipindi changu cha pili cha
uongozi wa nchi yetu na kuahidi kuvitekeleza kwa ari zaidi,
nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama ilivyo ada, leo tunafikia
mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba kutumia fursa
hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali
na yale mambo ambayo tuliahidi na kupanga kufanya.

Umoja, Amani na Usalama


Mheshimiwa Spika;
Niliahidi kuwa katika kipindi cha uongozi wangu
nitafanya

kila

niwezalo

kuhakikisha

kuwa

Tanzania

inaendelea kuwa nchi moja na watu wake wanaendelea


kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya
tofauti zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na
ufuasi wa vyama vya siasa. Pia, kwamba nchi yetu
itaendelea kuwa yenye amani, usalama na utulivu.
Leo tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa
Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa wamoja.

Hata

hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapa


na pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi
yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta
chuki baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya Wakristo
na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya nchi na wengine.
Bahati nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa
Serikali zetu mbili wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja

na ushirikiano na viongozi wa dini na wa jamii na uelewa


wa

wananchi,

vimeliwezesha

taifa

letu

kushinda

changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi


zimethibitisha ubora wa mazungumzo.
kwamba

wanaozungumza

Ni kweli kabisa

hawagombani

na

wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.


Mheshimiwa Spika;
Niruhusuni, nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara
nyingine viongozi wakuu wenzangu, Makamu wa Rais, Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchi
wote kwa ushindi tulioupata katika kudumisha umoja wetu.
Hata hivyo, tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa
kwani watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu au na umoja
wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba hawajafaulu.
Huenda

wakajaribu

tena.

Tunachotakiwa

kufanya

ni

kuendelea kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.

Muungano Wetu Umeimarika Zaidi


Mheshimiwa Spika;
Nafurahi kwamba namaliza kipindi changu cha
uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na kuuimarisha
Muungano

wetu

adhimu

na

adimu

Barani

Afrika.

Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kufungua


Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande
zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi
wa Muungano wetu.

Nafurahi kwamba jambo hili

limefanyika chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais,


akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara
na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamu
yangu ya

kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika

awamu hii.
Mafanikio
mbalimbali

ya

yaliyopatikana
zamani

na

ni

makubwa.

mapya

Masuala

yamezungumzwa,

yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi.

Kwa mfano,

hadi mwaka 2005 zilikuwa zimebakia kero 13 za Muungano

zilizoainishwa na Tume ya Shelukindo, hivi sasa zimebaki


kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja unakamilishwa
kiutawala na tatu zimeshughulikiwa kwa ukamilifu katika
Katiba Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa
imefanyika na Katiba hiyo kupitishwa kungekuwa hakuna
kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo. Lakini kwa vile
kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea
kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na
kukubaliana tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya
mafuta na gesi. Ndiyo maana katika Muswada wa Petroli
hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia
uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.
Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa
kupitisha Muswada huo. Moja ya kero kubwa katika
Muungano tumeimaliza.

Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar

Mheshimiwa Spika;
Mtakumbuka

kuwa

nilizungumzia

kusononeshwa

kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo Zanzibar


wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia
kuuondoa. Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani
ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka
ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na
mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya
yote hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii
yamekuwa bora zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya
hapo.
Ni matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibar
watayadumisha mafanikio haya ili waendelee kuishi kwa
amani,

upendo

na

udugu.

Natambua

kuwepo

kwa

changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali


hiyo.

Jambo linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe

hayahusu muundo wa Serikali bali yanaletwa na watu


kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji wa

baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo


yanayoweza kumalizwa kwa wadau kukaa kitako na
kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.
Amani na Usalama
Mheshimiwa Spika;
Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama kwa sababu
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea
kutimiza ipasavyo jukumu lake la kulinda uhuru na mipaka
ya nchi yetu. Katika kipindi hiki tumewekeza sana katika
kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na zana za kisasa za kivita
na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu, Anga na
Majini. Utayari kivita wa jeshi letu ni mzuri tena wa hali ya
juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya juu.
Tumeboresha maslahi na makazi ya wanajeshi kwa kujenga
nyumba mpya za kuishi. Utekelezaji wa mpango wa
kuwajengea nyumba 10,000 unaendelea vizuri. Hadi hivi
sasa nyumba 6,064 zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati
yake nyumba 3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu

10

cha kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na


Usalama kwa kujiamini kwamba Tupo vizuri. Pamoja na
hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa
kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu
pale tulipopakusudia.
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya
kupambana na uhalifu ili kulinda usalama wa maisha na
mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka kuwa mwaka
2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi ya
ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba
yangu

Bungeni

waendelee

kwamba

kutamba.

Hali

hatutawaacha
ile

imedhibitiwa.

majambazi
Ingawaje

matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama


ilivyokuwa wakati ule.
Hali kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali
yamepungua kutoka 53,268 mwaka 2005 hadi 43,808 mwaka
2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi

11

kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.


Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za
barabarani. Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.
Niruhusuni niwatambue na kuwashukuru Inspekta Jenerali
(mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali (mstaafu) Said
Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa
uongozi wao mzuri.
Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali
katika utakelezaji wa mpango wa maboresho ya Jeshi la
Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu Saidi
Mwema,

IGP

mstaafu.

Jeshi

la

Polisi

kuwezeshwa kwa zana, vifaa na mafunzo.

linaendelea
Taratibu

zimekamilika za kulipatia Jeshi hilo magari ya kutosha ili


kuongeza ufanisi.
Pia, tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya
kuishi Maafisa na Askari.

Kwa ajili hiyo tumekarabati

baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba kadhaa


mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni.

Mipango

12

imekamilika ya kuwezesha ujenzi wa nyumba 10,000


ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa
nyumba za kuishi katika Jeshi la Polisi.
Mheshimiwa Spika;
Jeshi letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza
vizuri majukumu yake ya kulinda wafungwa na kurekebisha
tabia zao. Aidha, huduma za malazi, mavazi, chakula na
usafiri

kwa

Changamoto

wafungwa
kubwa

ni

zimeendelea
msongamano

kuboreshwa.
wa

wafungwa

Magerezani. Naamini mipango ya kujenga magereza mapya


na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo litaisha. Aidha,
mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika na
kutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na
kuishi maafisa na askari, hivyo kupandisha morali wao na
kuongeza ufanisi.
Jeshi la Kujenga Taifa
Mheshimiwa Spika;

13

Ahadi

yangu

ya

kuanzisha

upya

utaratibu

wa

kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria katika Jeshi la


Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana 38,200
wamekwisha

hitimu

mafunzo

hayo

wakiwemo

Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza sana Waheshimiwa


Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia
sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi.

Ni

matumaini yangu kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi


na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa pamoja kujadili namna ya
kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo. Naamini
zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila
matatizo yoyote.

Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza
dhamira yetu ya kujenga na kuimarisha utawala bora kwa

14

sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa rasilimali watu.


Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo
yale yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano
dhidi ya rushwa, maadili ya viongozi, ukusanyaji wa mapato
na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na mgawano
wa madaraka hati ya mihimili.
Bunge la Jamhuri ya Muungano
Mheshimiwa Spika;
Serikali imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili
mkuu wa dola wa Kutunga Sheria. Tulianzisha Mfuko wa
Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya Bunge toka
shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadi shilingi bilioni
173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili
kuwawezesheni

Wabunge

kuchangia

katika

kutatua

changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi wa


majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu
yake kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu
Kamati teule zilizoundwa.

15

Katika kipindi hiki miswada 163 imepitishwa, maswali


ya msingi 7,544 na ya nyongeza 22,632 yameulizwa na
kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya ni mafanikio
makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa
na kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa
chachu ya baadhi ya hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria
na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali. Kwa kweli mnastahili
pongezi nyingi.

Huwezi kutaja mafanikio ya Serikali ya

Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa Bunge hili.


Mchakato wa Katiba
Mheshimiwa Spika;
Kama sote tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa na
Bunge

hili,

mwaka

2013

tulianzisha

mchakato

wa

Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi yetu Katiba


mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba
mchakato

huo

ulituwezesha

kupata

Katiba

Inayopendekezwa ambayo imekidhi matarajio hayo. Narudia


kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

16

na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na nzuri


waliyofanya. Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni ambapo sote
tunasubiri maelekezo ya Tume ya Uchaguzi. Mimi naamini
iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa itaimarisha
zaidi taifa letu.
Vyama vya Siasa
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa
vikiendelea kuimarika na kujijenga nchini. Idadi ya vyama
vya siasa imeongezeka kutoka 18 hadi 24. Vyama vya siasa
vimefanya

shughuli

zake

kwa

uhuru.

Viongozi

na

wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hata


maandamano kote nchini. Baraza la Vyama vya Siasa na
TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya kazi nzuri ya
kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.
Yamekuwa majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya
vyama vya siasa kwa masuala mbalimbali.

Matatizo na

changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi.

Ni

17

matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa


na kuimarishwa miaka ijayo.
Huu ni mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo
wahusika wakuu. Ni matumaini yangu kuwa vyama vya
siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi. Hii
itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa
uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu
Mheshimiwa Spika;
Habari kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu.
Tayari Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar
(ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwa ni
siku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya uchaguzi
huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa
mfumo mpya wa teknolojia ya Biometric Voters Register (BVR).
Hadi sasa zoezi la uandikishaji limekamilika katika mikoa 13
na linaendelea katika mikoa 11 na katika mkoa wa Dar es

18

Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza mwezi


huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari wamekwisha
andikisha hadi sasa wapiga kura milioni 11 kati ya lengo la
kuandikisha wapiga kura kati ya milioni 21 hadi 23.
Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu
wa kuiwezesha Tume kutimiza wajibu wake. Napenda
kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya
kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime tuhimize
watu wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki yao hiyo.

Uhuru wa Habari
Mheshimiwa Spika;
Mtakubaliana nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa
habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umepanuka sana.
Tanzania kuna magazeti ya kila siku 16 na kati ya hayo ya
Serikali ni 2 (Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya kila
wiki yapo 62.

Aidha, kuna vituo vya redio 115 na vya

19

televisheni 29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya


kuchapishwa au kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani
yangu kwamba ustawi wa demokrasia hutegemea sana
uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua
manufaa

ya

vyombo

vya

habari

kuelimisha

jamii,

kupambana na maovu na kuhimiza uwajibikaji.


Pamoja na hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua
hatua pale uhuru huo ulipotumiwa vibaya na kutishia
kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii au taifa. Au,
pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu
wetu wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa
kuutimiza.
Mheshimiwa Spika;
Katika kuongeza uwazi na mawasiliano na wananchi
mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya wananchi. Tovuti hiyo
imeshapokea hoja 117,243 na kati ya hizo zilizohusu Serikali
zilikuwa 78,258 na zote zimeshughulikiwa.

20

Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania


imeshahama kutoka mfumo wa analogia na kuingia kwenye
mfumo wa digitali.

Hii ni hatua kubwa muhimu kwa

maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo


nasikitika kuwa hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa
Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa Habari na Sheria ya
Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa
mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake
haukuweza kufika mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao
washughulike nayo katika Bunge la 11.

Vita dhidi ya Rushwa


Mheshimiwa Spika;
Vita dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia
njuga katika Awamu ya Nne. Tumepata mafanikio ya kutia
moyo katika mapambano dhidi ya rushwa ingawaje kazi
bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza,
tumetunga Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na

21

Kupambana na Rushwa ambayo imeongeza nguvu ya


mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya rushwa
iliongezwa kutoka 4 mpaka 24 na wigo wa wakosaji pia, kwa
kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya upelelezi na
uendeshaji mashitaka nayo imeimarishwa.
Tumeunda chombo kipya TAKUKURU badala ya
TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya kuzuia na
kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake.
TAKUKURU imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza
mapambano haya. Taasisi imeendelea kuimarishwa kwa
kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na
rasilimali

watu

na

mahitaji

mengine.

Tumeiwezesha

TAKUKURU kufungua ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.


Mheshimiwa Spika;
Maboresho haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma
za rushwa zinazofikishwa mahakamani kuongezeka kutoka
kesi 50 mwaka 2005 hadi 1,900 mwaka 2014. Jumla ya
shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali 97

22

wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi


mabaya ya ofisi zao baada ya ushahidi wa kijinai
kukosekana. Kwa upande wa kupambana na rushwa
kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya
Kudhibiti Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili
kutoa majibu ya kilio cha siku nyingi dhidi ya watu
wanaotumia fedha kununua kura.
Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali
Mheshimiwa Spika;
Nilieleza katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la
Tisa tarehe 30 Desemba, 2005 kuwa tutatoa kipaumbele cha
juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na nidhamu ya
matumizi ya Serikali.

Leo miaka kumi baadae ninaona

fahari tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali


yameongezeka kutoka shilingi bilioni 177.1 mwaka 2005
kwa mwezi hadi takriban shilingi bilioni 850.

Hii

imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutoka trilioni 4.13


mwaka 2005/2006 hadi trilioni 22.49 mwaka 2015/2016.

23

Isitoshe imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya


washirika wa maendeleo kutoka asilimia 42 ya Bajeti ya
Serikali mwaka 2005 hadi asilimia 15 mwaka 2014/2015 na
tumejipa lengo la kushusha zaidi hadi asilimia 8 mwaka
huu wa fedha wa 2015/2016.
Mheshimiwa Spika;
Mafanikio haya yametokana hasa na kazi kubwa
tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka ya Mapato ambao
wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza
kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa
mianya ya kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na
mamlaka nyingine za ukusanyaji mapato ya Serikali. Bado
ukusanyaji

wa

mapato

yasiyokuwa

ya

kodi

katika

Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara


zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo.
Huku kuendelee kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Spika;

24

Kwa upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na


mali za Serikali tulielekeza nguvu zetu katika kuimarisha
utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi wa hesabu za
Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,
tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa
Umma ili iweze kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti
wa sheria hiyo na kanuni zake. Kama mjuavyo sehemu,
kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi wa
bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni
jambo jema. Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.

Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali,
tumechukua hatua za makusudi za kuimarisha Ofisi ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi
Ofisi hiyo. Aidha, tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na

25

rasilimali watu.

Ofisi 8 za Mikoa zimejengwa na 2

zinaendelea kujengwa.
Nafurahi kwamba maagizo yangu kwa viongozi na
watendaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa zinasomwa,
zinajadiliwa

na

hatua

kuchukuliwa

kwa

kasoro

zilizoonekana. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali


imefanya kazi nzuri.
kuchukuliwa

hatua

Wezi na wabadhirifu wanaobainika


za

kisheria

mara

makosa

yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni


kwa muda wa kutosha.
Mheshimiwa Spika;
Niliamua pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali na kuwaweka Wakaguzi wa Ndani wote
wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka yake
na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria
na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma

26

zinaheshimiwa. Pia, katika ufuatiliaji na utekelezaji wa


mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa ukaguzi wa ndani na
ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali kuwa
nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu
zinazidi

kupungua

Serikalini.

Kwa

mfano

katika

Halmashauri za Wilaya na Miji, hati safi zimeongezeka


kutoka 56 mwaka 2006 hadi 150 mwaka 2014. Hati zenye
mashaka ni 13 na hakuna Hati isiyoridhisha.

Kazi ya

kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima


iendelezwe.

Maadili ya Viongozi wa Umma


Mheshimiwa Spika;
Katika

miaka

10

hii

tumeimarisha

mfumo

wa

kusimamia maadili ya viongozi. Tumefanya hivyo kwa


kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya kiongozi
na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya

27

Maadili na kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria


ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya 1995.
Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi na
familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la
Mali la kila mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa
kiongozi kuficha mali kwa mgongo wa mwenza wake au
mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kamati ya Maadili sasa si tu inapokea fomu na
kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi wa mali za viongozi na
kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali fedha. Hili
litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa ya
kimaadili wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili.
Sote tumeshuhudia kazi nzuri iliyofanywa na Baraza hilo
wakati wa sakata la Escrow.

Bado kazi ya kuimarisha

Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,


majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.
Muhimili wa Mahakama

28

Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi cha miaka 10 hii tumefanya jitihada
kubwa za kuimarisha mhimili wa Mahakama. Miongoni
mwa mambo mengine, tumefanya mambo muhimu kwa
madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa
jukumu lake la msingi la utoaji haki.
Kwanza, tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za
utawala. Tumeunda Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala. Hivyo basi,
Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki.
Mpaka sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa
makubwa kwa Mahakama kwani yameboresha utekelezaji
wa majukumu katika Mahakama. Pili, tumeanzisha Mfuko
wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika
kuendesha shughuli zake. Sambamba na hilo tumeongeza
bajeti ya Mahakama kutoka shilingi bilioni 36.6 mwaka
2006/07 hadi shilingi bilioni 87.6 mwaka 2014/15. Jambo

29

linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati ili


shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Spika;
Jambo la tatu, ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji
wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu Wakazi na
Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo.

Lengo letu ni

kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri.


Kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo
wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya Sheria. Hivi
sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama
hizo kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na
2015 tumeongeza Majaji wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005
hadi 16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka 37 hadi 81
katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya
Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo 5 na
katika Mahakama Kuu wapo 32 na kufanya jumla yao kuwa
37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu Wakazi 1,266 katika
ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao 534 sawa na asilimia

30

35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake


hivi sasa ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.
Mheshimiwa Spika;
Kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu
Mohamed Chande Othman Mahakama zimepiga hatua
kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.
Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na
kuamua mashauri yasiyopungua 220 kwa mwaka na kila
Hakimu Mkazi mashauri 250 na wale wa Mahakama ya
Mwanzo mashauri 260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo,
kuanzia Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015
yalifunguliwa mashauri 177,586 na Mahakama ilisikiliza na
kuamua

mashauri

179,962.

Maana

yake

ni

kuwa

zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma.


Bila shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia
kuwa historia katika kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza
sana Majaji na Mahakimu kwa kazi nzuri waifanyayo.
Kwa upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu,
wamekamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu za

31

Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama Kuu


Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya
Mahakama za Wilaya na 12 ya Mahakama za Mwanzo nayo
yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi unaendelea wa majengo ya
Mahakama Kuu 9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za Wilaya
9 na za mwanzo 25.
Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki
Mheshimiwa Spika;
Jambo lingine ambalo tumefanya katika nia ya
kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na kupunguza malalamiko ya
wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni kutenganisha
kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wa
mashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya
yote sasa watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashtaka ndiyo inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za
Mkurugenzi wa Mashtaka zimekwishafunguliwa katika kila
Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha, tumeboresha Ofisi
ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,

32

vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji


wa ofisi hiyo muhimu sana.

Kuna haja ya kuendelea

kuongezea rasilimali fedha na vitendea kazi ili ufanisi


uongezeke zaidi.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora kwa kuiwezesha kwa nyenzo,
rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi katika
eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na
utumiaji wa mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi
mengi

zaidi

yanafikishwa

kwenye

Tume

na

mengi

yanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko


yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka 9,455 mwaka
2006 hadi

25,921 mwaka 2014 na uwezo wa Tume

kushughulikia

malalamiko

kwa

mwaka

umeongezeka

kutoka malalamiko 3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko


18,501 mwaka 2014.

33

Utendaji Serikalini
Maeneo ya Utawala
Mheshimiwa Spika;
Kwa nia ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha
mikoa mipya 4 ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavi na
wilaya mpya 19. Pia, tulianzisha Halmashauri 45, kata 1,432,
vijiji 1,949, Mitaa 1,379 na vitongoji 8,777. Nimeamua
kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya
na Wilaya sita kama ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi,
Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es Salaam, Songwe
mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani
Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwa
sasa tufanye haya.
Maslahi ya Wafanyakazi
Mheshimiwa Spika;
Serikali ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu
suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa Serikali. Karibu
kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha chini cha

34

mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara


kimeongezeka kutoka shilingi 65,000 mwaka 2005 hadi
shilingi 265,000 mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia
shilingi 300,000. Najua bado hakikidhi mahitaji lakini
ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki tumeongeza sana
mishahara

ya

wafanyakazi.

Vile

vile,

tumeendelea

kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutoka asilimia


18 mwaka 2005 hadi asilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu
ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa wafanyakazi. Vile vile,
tumewapandisha

vyeo

watumishi

233,876

na

kulipa

malimbikizo ya watumishi 422,348 ya kiasi cha shilingi


bilioni 384.8.
Mheshimiwa Spika;
Tumetekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa wilaya
jambo ambalo limelazimu kuongeza rasilimali fedha na watu
kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa ajili hiyo ruzuku
kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutoka shilingi bilioni
780 mwaka 2005/2006 hadi shillingi trilioni 4.69 mwaka

35

2015/2016.

Aidha,

tumeimarisha

utumishi

katika

Halmashauri kwa kuajiri watumishi wengi wa kada


mbalimbali.
Usawa wa kijinsia
Mheshimiwa Spika;
Mwaka 2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa
kuzindua Bunge la Tisa, kuwa tutaongeza ushiriki wa
wanawake katika shughuli na nyanja mbalimbali za maisha
ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi. Ninyi na
mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi
ya Wabunge wanawake imeongezeka kutoka 62 mwaka 2005
hadi 127. Hivi sasa hamsini kwa hamsini ni rasmi katika
Katiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya kwanza katika
historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika
mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.
Wanawake wameongezeka katika ngazi zote kuu za
uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri wanawake 10, Naibu
Mawaziri wanawake 5, Majaji wanawake 37 na Wakuu wa

36

Wilaya wanawake wako 53.

Kwa upande wa Makatibu

Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,


Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka. Katika
elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya
wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na
sekondari.

Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya

wanafunzi wa kike imeongezeka kwa kasi kutoka 10,039


mwaka 2005 hadi 78,800 mwaka 2014.

Hali ya Uchumi
Mheshimiwa Spika;
Wakati ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi
Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo
kujenga uchumi ulio imara na shirikishi. Hususan, nilisema
nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka
misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira,
kuongeza Pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika

37

miaka kumi iliyopita tumeendelea kusimamia kwa kiwango


kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi katika ngazi
ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.
Jitihada zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo.
Katika kipindi hiki, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa
takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa 10
ya Afrika na 20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa
kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara
tatu kutoka shilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia
trilioni 79.4 mwaka 2014. Hivyo basi, pato la wastani la
Mtanzania nalo limeongezeka kutoka shilingi 441,030
mwaka 2005 hadi shilingi 1,724,416 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Mauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola

za

Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani


bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu ya fedha
za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya

38

nchi

kutoka nje

kwa kipindi cha miezi

4.1 kama

tulivyopanga. Mfumuko wa bei ni asilimia 6.1.


Mheshimiwa Spika;
Kama mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira
ya Taifa ya Maendeleo ya hadi mwaka 2025. Mwaka 2010
tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long Term
Perspective Plan) wa (2010 2025) wa kuongoza utekelezaji
wa Dira kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake
katika Mipango mitatu ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila
mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za utekelezaji wa
Mpango wa Kwanza, (2011/12 2015/16) na kuandaa
mpango wa pili (2016/17 2021/22).
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
Mheshimiwa Spika;
Kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali
nilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na kusimamia
utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya

39

kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa


wakati. Tuliamua kuanza na sekta sita za Elimu, Nishati,
Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato ya Serikali. Baadae
sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji
ziliongezwa.
Katika kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa
wenye manufaa. Mambo katika sekta zilizojumuishwa katika
BRN yameanza kwenda vizuri. Changamoto yetu kubwa
imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa wakati
kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo isingekuwepo
mambo yangekuwa mazuri zaidi.
Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji
Mheshimiwa Spika;
Kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza
uchumi, kuzalisha ajira, kuongeza mapato na kupunguza
umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua hatua thabiti za
kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji wa

40

ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa


kuwekeza.
Mwaka 2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya
Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public
Private PartnershipPPP). Lengo letu ni kuweka mazingira
mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali
katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya
utaratibu huu ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza
katika baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi inaweza
kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu inaongeza kasi ya
maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha ambazo
inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine.
Juhudi zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji
zinaendelea kuzaa matunda mema. Kati ya 2005 na 2014,
Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi 7,159
yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya
miradi hiyo asilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani,
asilimia 23.41 ni wawekezaji wa kutoka nje na asilimia 27.18

41

ni miradi ya ubia baina ya Watanzania na wawekezaji wa


kigeni. Ajira 16,000 zilipatikana. Ukuaji huu wa uwekezaji
umeongeza mapato ya Serikali.
Kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda na Biashara
Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania inaongoza
Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. Ilipata Dola za
Marekani bilioni 2.142 sawa na asilimia 31.5 ya uwekezaji
wote katika Jumuiya yetu.
Sekta za Uzalishaji
Sekta ya Kilimo
Mheshimiwa Spika;
Kuendeleza kilimo ilikuwa ni moja ya mambo
tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha yetu kuu ni kutaka
kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima wapate
mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri
ili mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile
vile wao na taifa lijitosheleze kwa chakula.

42

Kwa ajili hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka


7 ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector
Development ProgrammeASDP). Katika Programu hiyo,
matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa
mdogo yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa
kuyatatua. Serikali pia ilianzisha mikakati, programu na
mipango mingine ya kuongeza msukumo katika kuleta
mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa
Kilimo Kwanza,

Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika

Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mpango wa


Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP),

Sera ya

Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu ya


Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika.
Mheshimiwa Spika;
Pamoja na hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya
kilimo kutoka shilingi bilioni 233.3 mwaka 2005/06 hadi
shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15. Kuongezwa kwa
bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na

43

pembejeo kuongezeka kutoka shilingi bilioni 7.5 mwaka


2005/06 hadi shilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/14.
Matrekta makubwa na madogo yameongezeka kutoka 7,491
mwaka 2005 hadi 16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo
matumizi ya jembe la mkono yamepungua kutoka asilimia
70 hadi asilimia 62. Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379
mwaka 2005 hadi 7,974 mwaka 2014.
Vituo vya utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali
fedha, watu na vitendea kazi. Aidha, tumeanza safari ya
kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha sekta
binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika
kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu
(Agricultural Seed Agency ASA) na kuongeza uzalishaji wa
mbegu bora kutoka tani 10,477.17 mwaka 2005 hadi tani
32,340 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi za Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda
mazuri. Tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na

44

chakula imeongezeka. Kwa upande wa mazao ya chakula


uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni 9.66 mwaka
2005 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili
limeliwezesha taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa
asilimia 125 mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 95
mwaka 2005.

Uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara

umeongezeka toka tani 427,738 mwaka 2005 hadi tani


569,054 mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta
umeongezeka karibu ya mara 4 toka tani 1,389.9 mwaka 2005
hadi tani 5,545.6 mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa matunda
nao umeongezeka toka tani milioni 1.2 mwaka 2005 hadi
tani milioni 4.4 mwaka 2014 na maua toka tani 5,862 hadi
tani 10,790.
Mheshimiwa Spika;
Upatikanaji wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa
mazao ya wakulima bado ni changamoto. Pia kuna tatizo la
upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao. Jitihada
zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala ya

45

kisasa

nchi

nzima.

Programu

ya

Mageuzi

na

Modenaizesheni ya Ushiriki ilianzishwa ili kutatua tatizo la


masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya kuanzisha soko la
bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.
Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa
SACCOS na kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa itatoa
mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya

mapinduzi ya

kilimo.

Mifugo
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanza
safari ya kuleta mageuzi katika sekta hii. Safari hiyo
tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya
Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya
sekta hii zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa
utekelezaji.

Katika kipindi hiki malambo 1,008, majosho

2,364 na maabara 104 za mifugo zimejengwa. Visima virefu

46

101

vimechimbwa,

malambo

370

na

majosho

499

yamekarabatiwa katika kipindi hiki cha miaka 10.


Ukarabati na ujenzi wa majosho umeongeza idadi
kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi 3,637 mwaka 2015.
Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi
6,041 mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo
kutoka kituo 1 mwaka 2005 hadi vituo 8 mwaka 2015 na
kuwezesha ngombe 955,360 kuhamilishwa katika miaka 10
hii.
Mheshimiwa Spika;
Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi
tuliyoyajenga yamewezesha viwanda vya kusindika nyama,
maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda vya
kusindika maziwa vimeongezeka kutoka 22 mwaka 2005
hadi 74 mwaka 2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya
mifugo vimeongezeka kutoka viwanda 6 mwaka 2005 hadi
80 mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tani milioni
1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na

47

machinjio ya kisasa 9 vimejengwa katika kipindi hiki.


Usindikaji wa ngozi pia umeongezeka kutoka vipande
790,000 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78 mwaka 2014.
Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)
umefikia marobota 957,860 ikilinganishwa na marobota
178,100 mwaka 2005.
Safari yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji
kwenda kwenye ufugaji imeanza. Vijiji vingi vimeandaa
mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo vimetenga
maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji
vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo
ya malisho mbali na mazao ya wakulima. Pia, tuhimize
uhamilishaji kama mlango wa kuingilia kwenye kuboresha
kosafu za mifugo yetu.
Uvuvi
Mheshimiwa Spika;
Wakati nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005
nilisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele

48

kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika kutekeleza hayo


tumefanya yafuatayo. Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya
Mifugo na Uvuvi. Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili
kuwawezesha wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa bei
nafuu zaidi. Tatu, tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi sasa
vina uwezo wa kudahili wanafunzi 1,215 ikilinganishwa na
wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii imetuwezesha kuongeza
wagani wa uvuvi kutoka 103 mwaka 2005 hadi 540 mwaka
2014. Nne, tumeongeza sana juhudi za kupambana na uvuvi
haramu ili kutunza mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia
kuvuliwa au kuuawa kwa samaki wadogo.
Tumeimarisha maabara ya Taifa ya Samaki pale
Nyegezi kwa vifaa vya kisasa na wataalamu ili iende na
wakati. Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza ufugaji
wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka
kutoka 13, 011 mwaka 2005 hadi 20, 325 mwaka 2014.
Uvuvi haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi
yameongezeka kutoka shilingi bilioni 351.6 mwaka 2005

49

hadi shilingi trilioni 1.8 mwaka 2013. Bado tuna kazi kubwa
ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato ya
wavuvi na taifa.
Utalii
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za
kuiendeleza sekta hii muhimu. Tumeongeza kutangaza
vivutio vya utalii vya nchi yetu katika masoko makubwa
duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani wa asilimia 7.1
na imechangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.
Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii 612, 754 mwaka
2005 hadi watalii 1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitanda
katika mahoteli imeongezeka kutoka 15,828 hadi 21,929.
Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za Marekani
milioni 823.05 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani bilioni 2
mwaka 2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka
32,673 hadi 686,130 na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka

50

165,883 hadi 1,318,109. Haya ni mafanikio makubwa na ya


kujivunia.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la
ujangili wa wanyamapori hasa wa ndovu kutokana na
kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei kuwa
kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la
ujangili lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu nchini
na dunia nzima. Tukaamua kuchukua hatua za kuidhibiti
hali hiyo. Tumefanya operesheni tatu kukabiliana na tishio
hili. Ya kwanza, iliendeshwa na Idara ya Wanyamapori na
Misitu

wakishirikiana

na

TANAPA

na

Ngorongoro

Conservation Area. Hii hasa ilihusu kupambana na ujangili


katika hifadhi na mapori ya Kaskazini mwa Tanzania.
Mafanikio makubwa yalipatikana.
Mheshimiwa Spika;
Operesheni ya pili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi
katika hifadhi na sehemu nyingine za Tanzania. Operesheni

51

Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata mafanikio. Na ya tatu,


Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya ulinzi
na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi
zimesaidia sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo
yake katika sensa ya ndovu iliyofanyika mara ya mwisho,
ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na mapori mengine ina
muelekeo mzuri.
Kuundwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA)
yenye mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia sekta ya
wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano
ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani,
naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.
Viwanda
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea
kukua kwa kasi nzuri ya kutia moyo. Viwanda vikubwa, vya
kati na vidogo vimeongezeka kutoka 11, 544 mwaka 2005
hadi viwanda 51,224 mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005 na

52

2014 na miradi 751 imepewa leseni za kudumu na BRELA ya


kuanzisha viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda katika
Pato la Taifa umefikia asilimia 7.3

mwaka 2014 kutoka

asilimia 6.8 mwaka 2005. Mchango wa viwanda kwenye


mauzo ya nje umeongezeka kutoka asilimia 9.3 mwaka 2005
hadi asilimia 23.3 mwaka 2014.
Tunategemea ukuaji mkubwa wa viwanda katika
Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka 5 kutokana na
misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza.
Ujenzi wa kiwanda cha chuma kule Liganga na makaa ya
mawe cha Mchuchuma, unatarajiwa kuanza mwaka huu na
kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza
baada ya taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika.
Hivi ni viwanda vya msingi na mama ambavyo vitachochea
kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi kwa jumla.
Madini
Mheshimiwa Spika;

53

Sekta ya Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa


kuingiza fedha nyingi za kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia
upya sera, sheria na mikataba ya madini iliyokuwepo na
kutengeneza

sera

na

sheria

mpya.

Halikadhalika,

tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo


hatimaye yalizaa marekebisho ya mikataba yao na hivyo
kuboresha maslahi ya taifa.
Kufuatia marekebisho hayo, makampuni husika ya
madini yanalipa kodi ya mapato. Bila ya hivyo huenda
mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi. Kutumika
kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na
kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato ya
Serikali. Aidha, tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini
Tanzania (TMAA) ambao umewezesha kukagua mahesabu
ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na
kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa
makampuni hayo.
Mheshimiwa Spika;

54

Mabadiliko haya pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji


katika sekta hii yamewezesha mchango wa sekta ya madini
katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia 2.9 mwaka
2005 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2014. Thamani ya
mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka kutoka Dola
za Marekani milioni 655.5 mwaka 2005 hadi kufikia Dola za
Marekani bilioni 1.794 mwezi Desemba 2014. Mambo
yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu isingeshuka
katika kipindi hiki.

Mheshimiwa Spika;
Serikali ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezesha
Shirika letu la Madini (STAMICO) kuanza tena kazi ya
utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia kampuni zake
tanzu.

STAMICO

kwa

kupitia

kampuni

yake

ya

STAMIGOLD imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje.


Vilevile, tumejiunga na Mpango wa Uwazi wa Uvunaji wa
Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika kuongeza

55

uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika


ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye makampuni ya
madini.
Katika kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa
nayo ni Migodi ya dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga) na
New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka
(Ruvuma).

Aidha,

miradi

mikubwa

mingine

imeendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi


ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Mradi wa
Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa
Mchuchuma (Njombe). Pia, ajira rasmi kwenye migodi
mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517
mwaka 2005 hadi waajiriwa 15,000 mwaka 2014.

Hali

kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi wa


bidhaa na huduma hapa nchini (local procurement) kutoka
Dola za Marekani milioni 230.41 mwaka 2005 hadi Dola za
Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.
Mheshimiwa Spika;

56

Katika kipindi hiki pia, tumetenga maeneo 8 kwa ajili


ya wachimbaji wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha
wachimbaji wadogo kuchimba madini bila bughudha.
Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya
uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili
ya

wachimbaji

wadogo.

Tumeanzisha

mfuko

wa

kuwakopesha wachimbaji wadogo pale Wizarani ili kutoa


fursa

kwa

wachimbaji

wadogo

kupata

mikopo

ya

kuendeleza shughuli zao.

Nishati
Mheshimiwa Spika;
Wakati naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania
ilikuwa inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababisha
upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na upungufu
mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha
umeme kukosa maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha
watu zaidi ya milioni 3,776,000 na kukodisha mitambo ya

57

kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni tuliamua kuchukua


hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa
kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya
mawe, mionzi ya jua na upepo.
Ujenzi umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi
kutoka Mtwara na Songo Songo litakaloongeza kiasi cha gesi
kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji wa megawati
3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya
kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam.
Umeme huo utakidhi mahitaji ya umeme sasa na miaka
kadhaa ijayo.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme Vijijini
(REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya
kusambaza umeme kwa vijiji 5,336 kati ya vijiji 12,423 nchini.
Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa na ile ya
mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata umeme
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 40 mwaka 2015. Uamuzi

58

uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa kukusanya fedha


kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta ya petroli,
utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza umeme vijijini.
Gesi Asilia
Mheshimiwa Spika;
Tumepata mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi
asilia. Kuanzia mwaka 2010 nchi yetu imepata bahati ya
ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari kuu. Mpaka sasa
zimegundulika futi za ujazo trilioni 47.08. Ukijumlisha na
futi za ujazo trilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40
iliyopita kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali
ya gesi asilia nchini ni futi za ujazo trilioni 55.08. Kazi ya
utafutaji

inaendelea

na

wataalamu

wanasema

kuwa

Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazo trilioni 200.


Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni kikubwa na
kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa kuipatia dunia
nishati hii.

59

Gesi asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri


itaiwezesha nchi yetu na watu wake kupata maendeleo
makubwa na kuondokana na umaskini. Ni fursa ya aina
yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha
kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake.
Lakini, ili hayo yaweze kufanyika hapana budi pawepo
usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu za mnyororo wa
thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji, uuzaji wa
gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali
ghafi ya viwanda upande mmoja.

Upande mwingine

inategemea sana matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na


rasilimali hiyo.
Mheshimiwa Spika;
Ni kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo
yanakuwa hivyo ndiyo maana tumetunga Sera ya Gesi Asilia
na kuwasilisha katika Bunge hili ile Miswada miwili yaani
wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato ya
Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa

60

kuipitisha

Miswada

hii

nami

nitaitia

saini

mara

nitakapoletewa.
Usafirishaji na Uchukuzi
Barabara
Mheshimiwa Spika;
Serikali ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu
kwa uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji na
uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na barabara, reli, bandari,
usafiri wa majini na usafiri wa angani. Tumeendeleza kazi
ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa
mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na
zile zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kazi
ya ujenzi inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po
pote nchini kwenda Dar es salaam unafika siku hiyo hiyo,
tofauti na ilivyokuwa zamani watu walichukua zaidi ya siku
moja.

Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa

Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.

61

Katika mkakati wetu wa kupanua mtandao wa


barabara za lami nchini, tulitambua barabara za urefu wa
kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami. Baadae
tuliongeza barabara nyingine na kufikisha kilomita 17,742
katika mpango huo.

Utekelezaji wake upo katika hatua

mbalimbali. Tayari ujenzi wa kilomita 5,568 kwa upande wa


barabara kuu na kilomita 535 kwa barabara za mijini
umekamilika.

Ujenzi

wa

kilomita

3,873

unaendelea.

Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara


za urefu wa kilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana
fedha ujenzi uanze. Baadhi ya barabara hizo zimo katika
bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za urefu wa
kilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu
wa kina.
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki pia, madaraja madogo 7,200 na
makubwa 12 yamejengwa na mengine 16 yapo katika hatua
mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja makubwa

62

yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa


ni daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja
haya yalikuwa miongoni mwa matano yaliyopangwa
kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa
Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani
la Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003.
Kwa upande wa vivuko, tumeongeza vipya 15 na kufikisha
idadi ya 28 kote nchini mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika;
Tumeongeza sana fedha katika mfuko wa barabara
kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/06 hadi shilingi
bilioni

866.63

mwaka

2015/16.

Hii

itasaidia

katika

matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga


nyingine mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha
barabara za udongo na changarawe wilayani na vijijini
ziweze kupitika wakati wote. Katika kipindi hiki barabara

63

za changarawe zimeongezeka kutoka kilometa 9,424 hadi


kilometa 22,089.
Mheshimiwa Spika;
Katika miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani
magari, bajaji na pikipiki imeongezeka kutoka 1,696,088
mwaka 2005 hadi 3,313,254 hivi sasa.

Ongezeko hili

linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri


limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi
nchini. Katika jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa
zaidi na Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali
kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa baadhi ya
barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) na
sasa tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine
(flyovers). Tulianzisha matumizi ya treni katika reli za
TAZARA na TRC kusafirisha abiria.

Hivi sasa reli hizo

zinasafirisha abiria milioni 2,804,269 kwa mwaka ambao


wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa

64

kuendeleza matumizi ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa na


tumeanza kuutafutia fedha.
Usafiri wa Reli
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta
ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili reli zetu za TAZARA
na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa zinakabiliwa na
matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na
uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli
hizi ambazo kila moja inaweza kusafirisha tani milioni 5
kwa mwaka zinasafirisha kati ya tani 200,000 na 300,000 tu.
Hivyo basi, mizigo mingi husafirishwa kwa barabara na
kutishia uhai wa barabara ambazo tumezijenga kwa
gharama kubwa.
Kwa upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya
Dar es Salaam na Tabora unakaribia kukamilika na
utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza. Wakati huo huo
mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa

65

(standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza


mwaka huu kutegemea kukamilika kwa majadiliano na
mabenki yaliyoonyesha utayari wa kutukopesha pesa za
ujenzi.
Mheshimiwa Spika;
Azma yetu ya kufufua reli ya TAZARA nayo
tumeiwekea

mkakati.

Sisi

na

Zambia

tumekubaliana

kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa


matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki
zetu wa China nao wamekubali kutusaidia katika mipango
yetu hiyo. Ni matumaini yangu kuwa safari hii tutapata
ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo yanayoathiri ufanisi wa
reli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na ustawi wa
uchumi wa nchi zetu na watu wake.
Bandari
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha na kuimarisha huduma katika bandari ya
Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa. Mwaka 2014

66

bandari yetu ilihudumia tani milioni 14.4 ukilinganisha na


tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia
tani milioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwa saa 24 na
kasi ya kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka
sana na wizi umepungua sana. Hata wale walioacha
kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.
Mheshimiwa Spika;
Kuanza kutumika kwa mfumo wa Single Customs
Territory unaorahisisha upakuaji na upakiaji mizigo ya nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza zaidi ufanisi.
Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao
wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.
Kuongezeka kwa usafirishaji wa mizigo inayopita
nchini kuna faida kwani sekta ya usafirishaji inachangia
zaidi ya asilimia 15 ya pato la taifa. Hali kadhalika, ujenzi
wa gati za 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam
unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya
makasha kuongezeka kutoka makasha 600,000 hadi makasha

67

1,200,000. Mipango ya kuboresha bandari za Mtwara, Tanga


na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu na ujenzi wa
bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania kunufaika na
fursa ya jiografia yake.
Usafiri wa Anga
Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya
kuwekeza kwenye ukarabati, upanuzi na ujenzi wa viwanja
vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo
wa kuhudumia kutoka ndege 7 hadi 30 hivi sasa. Aidha
tunajenga jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo lenye
uwezo wa kuhudumia abiria milioni 3.5.

Ujenzi huo

unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.


Kukamilika kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa
Julius Nyerere kuhudumia abiria milioni 6 na ndege nyingi
zikiwemo ndege kubwa za kisasa za Airbus 380.
Mheshimiwa Spika;

68

Vile vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja wa


Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa sekta
ya utalii ya ukanda wa kaskazini. Uwanja mpya wa ndege
wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi sasa
unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja
vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora,
Mwanza na Bukoba.
Ujenzi,

upanuzi

na

ukarabati

huu

tulioufanya,

umechangia sana katika ongezeko kubwa la safari za ndege


na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini zimeongezeka
toka safari 78 mwaka 2005

zilizokuwa zinatolewa na

kampuni 29 za usafiri wa ndege hadi safari 175 zinazotolewa


na kampuni 55 mwaka 2014. Aidha, abiria wanaoondoka na
kuwasili katika viwanja vya ndege wameongezeka kutoka
2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013.
Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka
kwa kasi kubwa.
Mheshimiwa Spika;

69

Jambo ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la


kufufua Shirika letu la Ndege. Tumefanikiwa kulifanya lisife
lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata kwenye ile hali
yake ya zamani.

Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu

mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa


Menejimenti imepewa jukumu la kuandaa mpango wa
biashara unaoeleweka na unaokopesheka, kisha Serikali
itaona namna ya kulisaidia shirika.

Utabiri wa Hali ya Hewa


Mheshimiwa Spika;
Sambamba na hayo, tumeboresha huduma za utabiri
wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa imepatiwa vifaa
vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa utabiri
unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata cheti
cha utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya
taarifa zake kutambuliwa kimataifa.

70

Mawasiliano
Mheshimiwa Spika;
Tumepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya
habari na mawasiliano. Tumejenga Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano wenye urefu wa kilometa 7,560 unaounganisha
miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara isipokuwa mkoa
mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na Pemba, ujenzi
wake utakamilika mwezi ujao. Katika Awamu ya Pili, Mkoa
wa Simiyu na wilaya zote nchini zitaunganishwa.
Ujenzi wa mkongo huu umechangia katika kuongeza
ubora na kasi ya mawasiliano, na kushusha gharama za
mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simu
zimeshuka kutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005
hadi shilingi 34.92 mwaka 2014 na gharama za

intaneti

zimeshuka kutoka wastani wa shilingi 36,000 kwa Gigabyte


moja mwaka 2005 hadi wastani wa shilingi 9,000 kwa
Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014.

Hii imeshusha pia

71

gharama za biashara kwa kurahisisha mawasiliano na


malipo kati ya mabenki na kwa njia ya mtandao na simu.
Kwa upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka
laini milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 28 mwaka 2014.
Watu wanaotumia intaneti wameongezeka toka milioni 1.6
hadi milioni 9.3 mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya
simu kumewezesha watumiaji milioni 12.3 kupata huduma
ya fedha kupitia simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na
Aprili 2014 jumla ya miamala milioni 972.6 ilifanyika yenye
thamani ya shilingi trilioni 28. Huu ni wastani wa zaidi ya
shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania
kuongoza duniani kwa huduma hii.
Mheshimiwa Spika;
Tulitambua

kuwa

makampuni

binafsi

ya

simu

hayapendi kuwekeza vijijini ambako biashara si kubwa kama


mijini.

Kwa

kutambua

umuhimu

wa

huduma

ya

mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo


huo. Kwa sababu hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano

72

kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha kata na vijiji vyote


nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo
umekwisha wezesha jumla ya kata 52 na vijiji 314 kufikiwa
na huduma hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano
kupitia Mfuko huo zinaendelea kwa kata nyingine 163 zenye
vijiji 922, ambapo wananchi milioni 1.2 watanufaika.
Mheshimiwa Spika;
Tumechukua hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya
kodi inazibwa na kwamba makampuni yanalipa kodi stahiki
kwa

kununua

na

kufunga

mtambo

wa

Kusimamia

Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha


Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu halisi
za mawasiliano yanayofanywa. Tangu kuanza kutumika kwa
mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza kukusanya
shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo zisingepatikana.
Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika ya Mashariki
kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda digitali. Karibu

73

tutakamilisha kwa mikoa yote. Tunazipokea nchi kadhaa


zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji wa zoezi hili.
Ardhi na Makazi
Mheshimiwa Spika;
Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na
kuboresha makazi ya watu. Sote tunafahamu kuwa makazi
ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la kuboresha
huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio
makubwa. Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu
zaidi na wananchi kwa kuanzisha Kanda nane za kusimamia
upangaji,

upimaji

na

utoaji

hatimiliki.

Uamuzi

huu

umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata hati


miliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati 164,275 zimetolewa,
vijiji 10,500 vimepimwa na kati yake vijiji 10,341 vimepatiwa
hatimiliki.
Mheshimiwa Spika;
Tumetunga Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji
wa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni

74

pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba (Mortage Finance)


na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa
kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria
hizi kwa ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi
kupata mikopo ya kujenga au kukarabati nyumba zao na
kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya jengo.
Mabadiliko hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba
kukua kwa kasi kubwa na majengo na nyumba za kisasa
kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es Salaam ya
leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la
Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii nayo imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenzi
wa nyumba katika kipindi hiki.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa watumishi wa serikali kuwa na
nyumba mwaka 2008 tulianzisha Mfuko wa Mkopo kwa
watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya
shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi 1,169. Pia, tumeanzisha

75

Kampuni ya Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa


umma ambayo tayari imeanza kazi.
Mheshimiwa Spika;
Ninayo furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia
yameendelea kuwa bora. Takwimu za Sensa ya Watu na
Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi ya nyumba
zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 46
mwaka 2002 hadi asilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha
nyingine nyumba zilizoezekwa makuti na nyasi zimezidi
kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia moyo na
hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.
Utafiti
Mheshimiwa Spika;
Jambo lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni
eneo la utafiti. Hili ndilo eneo ambalo ilitalivusha taifa letu
kwenda katika maendeleo makubwa zaidi. Niliamua Serikali
ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli za utafiti
ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu. Niliamua

76

kuwa Serikali ianze safari ya kutenga fedha za kutosha kwa


ajili ya utafiti. Tulianza na shilingi bilioni 10 na kuendelea
kuongeza mwaka hadi mwaka na kufika shilingi bilioni 60
mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi kufikia asilimia 1
ya bajeti ya Serikali na hatimaye asilimia 1 ya pato la Taifa
kwa ajili ya shughuli za utafiti.
Mheshimiwa Spika;
Kwa kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi
wetu 344 wamepata ufadhili wa masomo ya shahada ya
Uzamili na 173 wa shahada ya Uzamivu. Miradi 70 ya utafiti
imefadhiliwa, kati ya hiyo 22 ni ya kilimo. Fedha hizi pia
zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
kuanzisha viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha
vijana wetu kubuni na kuvumbua teknolojia zenye manufaa
kwa maendeleo ya jamii na taifa. Wamezalisha ajira na
kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni mfano
mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.
Huduma za Jamii

77

Elimu
Mheshimiwa Spika;
Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa mwaka
2005 nilisema kuwa, Hakuna Taifa lililopata maendeleo
bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza elimu nchini
itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka kumi
bajeti ya sekta ya elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko

za

sekta nyingine zote. Mwaka huu 2015 bajeti ya elimu


imefikia shilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa na shilingi
bilioni 669.5 za mwaka 2005.
Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani
ya miaka 10 hii ni ya kutia moyo. Tumeongeza shule za
msingi kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,538 mwaka 2015
na

wanafunzi

wameongezeka

kutoka

7,541,208

hadi

8,202,892. Upanuzi huu umewezesha asilimia 98 ya watoto


wanostahili kupata elimu ya msingi sasa kuandikishwa.

78

Kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi


tumeongeza Shule za Sekondari kutoka Shule 1,745 mwaka
2005 hadi Shule 4,753 mwaka 2015. Idadi ya wanafunzi
imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056
mwaka 2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi
vimeongezeka kutoka 184 mwaka 2005 hadi 744 mwaka 2015
na wanafunzi katika vyuo hivyo wameongezeka kutoka
40,059 hadi 145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio
makubwa sana.
Kwa nia ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua
hatua thabiti za kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu,
vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya kujifunzia na
kufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,
Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi
ya walimu wa Shule za Msingi kutoka 135,013 mwaka 2005
hadi 202,752 mwaka 2015, na walimu wa Shule za Sekondari
kutoka 18,754 mwaka 2005 hadi 88,908 mwaka 2015. Uhaba
wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa

79

kutosha. Tuna upungufu wa walimu 20,141 wa masomo wa


sayansi na hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu
za kusomesha walimu wa sayansi vyuoni zilizopo, katika
miaka michache ijayo tatizo hili nalo tutalipatia ufumbuzi.
Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014
kimeanza kudahili wanafunzi 5,000 wa ualimu wa masomo
ya sayansi.
Mheshimiwa Spika;
Kwa upande wa maabara za sayansi, katika shule za
sekondari za kata tayari maabara 5,979 zimejengwa na
nyingine 4,410 ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wa
vifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa
vitabu

tumeweza

kuboresha

upatikanaji

wake

kwa

mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka uwiano wa 1:5


mwaka 2005 hadi 1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari
uwiano ni 1:2 ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.
Mheshimiwa Spika;

80

Katika

kipindi

hiki

pia

tumeshuhudia

upanuzi

mkubwa wa elimu ya juu nchini. Idadi ya vyuo vikuu


imeongezeka kutoka vyuo 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka
2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha
Dodoma na cha Nelson Mandela cha Arusha ambavyo
vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Tumeanza
mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha
Kilimo kule Butiama. Vyuo hivi ni fahari ya nchi yetu kwani
tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe bila msaada kutoka
kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi ya
wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi 40,719 mwaka
2005 hadi 218,959 mwaka 2014.
wanaonufaika

na

mikopo

nayo

Idadi ya wanafunzi
imeongezeka

kutoka

wanafunzi 16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi 99,590


mwaka huu.
Afya
Mheshimiwa Spika;

81

Tumepata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa


kuboresha na kupanua huduma ya afya nchini. Tuliazimia
kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa
kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na
kuimarisha vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya
kutolea huduma za afya 2,175 vimejengwa. Kati yake
hospitali 19, vituo vya afya 168 na zahanati 1,883
zimejengwa.
Tumeimarisha

hospitali

ya

Taifa

ya

Muhimbili,

Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na Wilaya kwa


kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,
Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa ya
Afya ya Jamii ambayo inatumika kama maabara ya
Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC. Tumeimarisha
maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya
uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina
uwezo wa kubaini virusi vya Ebola jambo ambalo miezi
michache iliyopita tulikuwa tunapeleka sampuli Nairobi.

82

Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza kufanya uchunguzi


wa mwenendo wa figo na ini.
Mheshimiwa Spika;
Tumeboresha huduma ya Afya ya Kinywa katika
Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga mashine 26 za kisasa
za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza meno
bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa
kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashuri 91. Hivi
sasa hospitali 136, vituo vya afya 63 na zahanati 3 zinatoa
huduma hiyo nchini.
Tumeanza kupata mafanikio katika dhamira yetu ya
kujenga uwezo wetu wa ndani wa kuchunguza na kutibu
maradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya fahamu
ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa
mfano, tangu Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale
Muhimbili

wagonjwa

wakiwemo

692

71,963

waliofanyiwa

wamepatiwa
upasuaji.

matibabu
Watu

hao

83

wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu


utaongezeka sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.
Mheshimiwa Spika;
Tumebadilisha utaratibu wa kusambaza dawa kutoka
Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba
kutoka shilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadi shilingi
bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na
Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya
wameongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2005 hadi asilimia
19 mwaka 2014.
Katika kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika
kupambana

na

maradhi

makubwa

ya

kuambukiza

yanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha


kampeni ya kupambana na malaria nchi nzima kwa
kubadilisha dawa ya kutibu malaria na kugawa vyandarua
26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa akina
mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia
dawa ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda

84

ya ziwa. Matokeo ya jitihada hizo ni kupungua kwa


maambukizi ya malaria kwa asilimia 51 na vifo kwa
asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua
viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya
kutokomeza malaria hapa nchini ni ya uhakika.
Mheshimiwa Spika;
Juhudi

zetu

katika

kupambana

na

ukimwi

zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya ukimwi kutoka


asilimia 7.7 mwaka 2005 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012.
Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka
kutoka 365,189 mwaka 2005 hadi 25,468,564 mwaka 2014.
Aidha, tumewezesha vituo 5,244 na asilimia 97 ya vituo
vyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya kuzia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mheshimiwa Spika;
Kati ya mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa
wanafunzi katika vyuo vya afya kutoka 3,025 mwaka 2005
hadi 11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho wataalamu wa

85

afya 55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya kada


mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya madaktari
imeongezeka kutoka madaktari 1,048 mwaka 2006 hadi
madaktari 2,325 mwaka 2014. Halikadhalika, madaktari
wasaidizi wameongezeka kutoka 1,223 hadi 1,914, wauguzi
kutoka 15,961 hadi 22,942 wataalamu wa Maabara kutoka
1,277 hadi 2,378 mwaka 2014. Hivi sasa uwiano wa Daktari
kwa wagonjwa ni 1:6,666 ikilinganishwa na 1:35,714 mwaka
2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa wagonjwa umeshuka
kutoka 1:2,347 mwaka 2005 hadi 1:2,008 mwaka huu.
Mheshimiwa Spika;
Tumeendesha kampeni ya kuboresha lishe nchini na
kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Lishe (2011-2016). Kwa ajili
hiyo mwaka 2013 tulizindua Programu ya Uongezaji wa
Virutubishi. Matokeo ya jitihada zetu hizo yameanza
kuonekana. Udumavu umepungua toka asilimia 44 mwaka
2005 hadi asilimia 35 mwaka 2014 na uzito pungufu toka
asilimia 17 hadi asilimia 13.

86

Kwa jumla juhudi zetu za kuboresha huduma ya afya


zimezaa matunda ya kuridhisha. Wastani wa umri wa kuishi
wa Mtanzania umeongezeka toka miaka 49 mwaka 2005
hadi miaka 62 hivi sasa. Vifo vya watoto wachanga
vimepungua toka vifo 68 kwa kila vizazi hai 1000 hadi vifo
21 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2014. Vifo vya watoto
chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 112 kwa kila
vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi vifo 54 kwa kila vizazi hai
1000 mwaka 2014, na vifo vya akinamama wajawazito
vimepungua toka vifo 578 kwa vizazi hai 100,000 hadi vifo
432 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2012. Haya ni mafanikio
ya kutia moyo ingawaje bado tunatakiwa kuendeleza juhudi
zaidi mara dufu ili vifo vipungue zaidi na zaidi.
Maji
Mheshimiwa Spika;
Serikali ya Awamu ya Nne imefanya juhudi kubwa
katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na
salama na usafi wa mazingira

katika kipindi hiki.

87

Tumekamilisha miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa 8,


Wilaya 6 na Miji midogo 2. Aidha, miradi katika miji
mingine 13 ya mikoa, 27 ya Wilaya na Miji midogo
inaendelea

kutekelezwa.

Utekelezaji

wa

miradi

hii

umewezesha kiwango cha upatikanaji maji mijini kufikia


wastani wa asilimia 86 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia
73 mwaka 2005. Na kwa Vijijini imefikia asilimia 67.6
Mwaka 2014 ukilinganisha na asilimia 53 mwaka 2005.
Tumevuka lengo letu la kuwapatia maji asilimia 65 ya
wakazi wa vijijini.
Aidha, miradi inayoendelea kutekelezwa hivi sasa
itakapokamilika katika mwaka huu wa fedha upatikanaji wa
maji mijini utafikia asilimia 90 ambalo ndilo lengo la Ilani ya
uchaguzi ya CCM. Vijijini inaweza kufikia asilimia 70
ambayo ni juu ya lengo la asilimia 65.
Aidha, tumeboresha huduma za uondoaji wa maji taka
katika miji ya Tanga, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa,
Songea, Tabora na Morogoro. Uboreshaji huu wa huduma za

88

utoaji wa maji taka ni mwanzo mzuri katika kuhakikisha


kwamba tunakuwa na mipango mizuri ya maji taka mijini.
Uwezeshaji wa Wananchi
Mheshimiwa Spika;
Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ilikuwa ni moja ya
dhima kuu ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.
Katika kutekeleza dhamira hii, Serikali imeendeleza kwa
mafanikio makubwa mifuko ya kutoa mikopo kwa vijana,
wanawake, wajasiriamali wadogo na kuanzisha fursa
nyingine mpya. Watu wengi wamenufaika na wao wenyewe
kuwa chachu ya kuzalisha ajira, kupunguza umasikini na
kuinua hali za maisha ya watu walioguswa na fursa
zilizopatikana.
Tumeiwezesha

Benki

ya

Wanawake

kuanza

na

kuendelea kutoa huduma. Kama mjuavyo niliamua Serikali


ichangie mtaji wa mwanzo na inaendelea kuchangia mtaji
huo. Tayari Benki hiyo imeshakopesha watu 125,000 na kati
yao wanawake ni asilimia 82. Hali kadhalika, nilifanya

89

uamuzi wa makusudi wa kuifufua Benki ya Rasilimali (TIB).


Dhamira yangu ni kutaka iwepo Benki ya maendeleo
itakayotoa mikopo ya muda mrefu na wa kati kwa
wawekezaji

wazawa.

Hii

itawezesha

kuanzisha

na

kuendesha shughuli za viwanda, madini, utalii na biashara


kwa urahisi.
Tumeiwezesha Benki ya Rasilimali kwa mtaji, rasilimali
watu na vitendea kazi na kuifanya iwe moja ya benki ya
kutumainiwa

nchini.

TIB

imeshatoa

mikopo

kwa

makampuni 365 yenye thamani ya shilingi bilioni 512.


Aidha, imetoa mikopo kwa miradi 201 yenye thamani ya
shilingi bilioni 156 kupitia dirisha dogo la kilimo. Natoa
pongezi maalum kwa viongozi na watumishi wa Benki ya
Rasilimali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya katika
kipindi hiki kifupi. Naomba waendelee na moyo huo kwa
maslahi ya nchi yetu.
Mheshimiwa Spika;

90

Tumetimiza ahadi yetu ya kuimarisha ushirika nchini


kama nguzo kuu ya kuunganisha nguvu za wanyonge
kujiletea maendeleo. Katika kipindi hiki, idadi ya Vyama vya
Ushirika vya aina mbalimbali nchini imeongezeka kutoka
5,832 mwaka 2005 hadi 9,604 mwaka 2015.
Kwa upande mwingine, Vyama vya Akiba na Mikopo
(SACCOS), vimeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka vyama
1,875 mwaka 2005 hadi 5,559 mwaka 2014. Akiba, hisa na
amana za wanachama zimeongezeka kwa zaidi ya mara tano
kutoka Shilingi bilioni 85.6 mwaka 2005/2016 hadi Shilingi
463 bilioni mwaka 2014 na mikopo kwa wanachama imekua
mara 13 toka shilingi bilioni 65.7 hadi shilingi bilioni 893
mwaka huu. Kwa hakika haya ni mafanikio makubwa ya
kujivunia.

Watu

wengi

wamewezeshwa

kupunguza

umasikini wao na wengine kuondoka katika lindi la


umasikini.
Sanaa na Michezo
Mheshimiwa Spika;

91

Niliahidi kusaidia kukuza michezo na sanaa nchini.


Kwa upande wa michezo niliahidi kuwa Serikali italipia
makocha.

Nilitimiza ahadi yangu kwa michezo ya soka,

netiboli na ngumi. Kwa upande wa riadha tuliwapeleka


wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa
maandalizi ya mashindano ya kimataifa. Timu yetu ya taifa
ya soka haijafanya vizuri sana. Kwa upande wa soka
tulianza kupata matumaini lakini baadae yakafifia. Timu
yetu ya taifa ya soka haijafanya vizuri sana pamoja na
kubadili makocha. Hata vilabu vyetu pia havifanyi vizuri.
Kwa kweli lazima Watanzania tukae chini na kujiuliza kwa
nini hatufanyi vizuri na tufanye nini tufanikiwe.
Mheshimiwa Spika;
Nilifanya uamuzi wa kurejesha michezo mashuleni
pamoja na mashindano ya michezo kwa shule za msingi na
sekondari (UMISHUMTA na UMISETA). Nia yetu ni kutaka
vipaji vya michezo vya vijana viibuliwe wakiwa bado

92

wadogo na kuendelezwa. Uamuzi huu umerejesha uhai na


matumaini kwamba siku za usoni tutaona matunda yake.
Kwa dhamira hiyo hiyo, kwa kushirikiana na Kampuni
ya Symbion Power na Klabu ya Soka ya Sunderland kituo
cha

kuandaa

wanamichezo

wadogo

kinajengwa

pale

Kidongo Chekundu, Dar es Salaam. Kituo hiki kinatarajiwa


kuwa tayari ifikapo mwezi Septemba, 2015.

Kikitumiwa

vizuri huenda ikawa ndiyo mwanzo wa safari ya uhakika ya


kuendeleza

soka

hapa

nchini.

Tukifanikiwa

Kidongo

Chekundu, vituo vingine kama hivyo vinaweza kuanzishwa


sehemu nyingine nchini na wadau mbalimbali.
Mheshimiwa Spika;
Tumepata mafanikio ya kuridhisha kwa upande wa
sanaa za filamu na muziki. Vijana wetu wa tasnia hizi
wamekuwa wanafanya vizuri kiasi kwamba leo hii Bongo
Flavor na Bongo Movie zimevuka mipaka ya Tanzania.
Zinaitangaza sanaa ya Tanzania, lugha ya Kiswahili pamoja
na nchi yetu. Vijana hawa wameitoa kimasomaso Tanzania

93

na kutufutia unyonge tunaopata kwenye michezo. Tasnia


hizi zimeajiri vijana wengi, wanalipa kodi na wanasaidia
sana katika kuhamasisha na kufikisha ujumbe kwa mambo
muhimu katika jamii.
Mheshimiwa Spika;
Kwa nia ya kutaka kuendeleza ujuzi, mbinu na maarifa
kwa wasanii wetu mwaka wa jana niligharimia timu ya watu
wazoefu wa fani za muziki na filamu kutoka Marekani kuja
nchini kutoa mafunzo ya muda mfupi. Ninafanya mipango
waje tena kwani mafunzo ya mara kwa mara yatawaimarisha
wasanii wetu.
Kwa wasanii wa muziki niliwatimizia maombi yao ya
kutaka kuwa na mastering studio.

Kwa wote nimefanya

jitihada kubwa ya kutafuta majawabu kwa tatizo sugu la


kupata malipo ya haki kwa kazi wazifanyazo. Tumetunga
Kanuni ambazo zimewezesha kazi za wasanii kutambuliwa
na kulindwa. Halikadhalika, tumeweza kuanza utaratibu
mpya wa kusambaza kazi za wasanii ambapo wao wenyewe

94

wana

sauti

nazo.

Nitajitahidi

katika

kipindi

kifupi

kilichobaki niyasukume kwa kasi masuala yaliyosalia ili


niwaache wasanii wetu mahali pazuri.

Nataka wapate

malipo ya haki kwa vipaji vyao na jasho lao ili wainue hali
zao za maisha.

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa


Mheshimiwa Spika;
Wakati nalihutubia Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba
2005 niliahidi kwamba Serikali itafanya kila iwezalo
kuhakikisha Tanzania inakuwa na uhusiano mzuri na
mataifa mengine duniani, na mashirika ya kimataifa
na

kikanda.

Leo,

miaka

10

baadae

napenda

kuwahakikishia kuwa ahadi yetu tumeitekeleza, tena vizuri


kuliko tulivyotegemea. Tanzania ni rafiki wa kila nchi na kila
shirika la kanda na kimataifa. Hadhi yetu katika uso wa

95

kimataifa imepanda sana. Tunaheshimiwa, tunasikilizwa,


tunathaminiwa na kuaminiwa na mataifa makubwa na
madogo.
Katika kipindi hiki tumetembelewa na wageni wengi
mashuhuri kutoka mabara yote. Tumeweka historia kwa
kutembelewa mfululizo na Marais wawili wa Marekani
yaani Rais George W. Bush mwaka 2008 na Rais Barack
Obama mwaka 2013, na Marais wawili wa China Rais Hu
Jintao mwaka 2009 na Rais Xi Jinping mwaka 2013. Pia
tulitembelewa na Wafalme, Marais, Mawaziri Wakuu na
Mawaziri kutoka nchi za Mabara yote duniani. Aidha,
tumetembelewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais
wa Umoja wa Ulaya, Rais wa Benki ya Dunia n.k.
Tumeshirikishwa katika shughuli nyingi na mikutano
mingi. Nimepata fursa ya kushiriki katika mikutano
mbalimbali
kuwakilisha

ya

kimataifa

Afrika.

pamoja

Nimewahi

na

miwili

kushiriki

na

ya

G8

kupewa

dhamana ya uongozi katika kamati na Tume kadhaa za

96

Afrika na dunia. Nimewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa


Afrika (2008), Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi za
Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Mjumbe wa
Danish Africa Commission, Mwenyekiti wa ALMA.

Hivi

karibuni nimeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja


wa

Mataifa

Kupendekeza

Namna

Bora

kwa

Dunia

Kushughulikia Majanga ya Afya.

Mheshimiwa Spika;
Katika kipindi hiki tumefungua Balozi mpya 5 katika
nchi za Oman, Malaysia, Brazil, Uholanzi na Comoro. Hii
inafikisha idadi ya Balozi zetu kuwa 35. Pamoja na ufinyu
wa bajeti jitihada zimekuwa zinafanyika kuboresha huduma
kwa Balozi zetu na wanadiplomasia wetu. Tumejenga jengo
la Ubalozi New Delhi na kununua majengo ya ofisi ya kitega
uchumi

Washington

DC,

New

York

na

Ufaransa.

Tumeanzisha Kurugenzi ya Diaspora katika Wizara ya


Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ili

97

kuwashirikisha

Watanzania

waishio

ughaibuni

katika

maendeleo ya nchi yetu.


Ushirikiano wa Kanda
Mheshimiwa Spika;
Tanzania imeendelea kuwa mwanachama mwaminifu
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, Umoja wa Afrika
na Umoja wa Mataifa. Tumepiga hatua kubwa katika
kuimarisha

na

kuendeleza

utengamano

wa

Afrika

Mashariki. Katika miaka 10 hii tumefanikiwa kukamilisha


utekelezaji wa Umoja wa Forodha tarehe 1 Januari, 2010 na
tarehe 1 Julai, 2010 tulianza utekelezaji wa Soko la Pamoja
ambao unaendelea hivi sasa. Tumetia saini Itifaki ya Umoja
wa

Sarafu

Novemba

2013

ambayo

utekelezaji

wake

unaendelea vizuri. Matunda ya utekelezaji wa utengamano


kiuchumi yameanza kuonekana. Kwa mfano, mauzo yetu
katika soko la Afrika Mashariki yameongezeka kutoka
bidhaa zenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 161
mwaka 2005 hadi bidhaa za Dola za Marekani bilioni 1.2

98

mwaka 2014. Uwekezaji nchini Tanzania kutoka nchi


wanachama

wa

Jumuiya

ya

Afrika

ya

Mashariki

umeongezeka toka miradi 35 yenye thamani ya Dola za


Marekani milioni 39.5 hadi miradi 244 yenye thamani ya
Dola za Marekani milion 676.5. Haya yote ni mafanikio
makubwa.
Mheshimiwa Spika;
Kuhusu Umoja wa Maendeleo wa Nchi za Kusini Mwa
Afrika (SADC). Tumeendelea kushiriki kwa ukamilifu katika
shughuli za umoja huo. Tumeshiriki kwenye kutafuta
suluhisho la Visiwa vya Comoro, Madagascar, Zimbabwe na
DRC.
Salamu za Kuaga
Mheshimiwa Spika;
Tulipanga kufanya mengi na tumefanikiwa mengi,
lakini

hatukuweza

kuyamaliza yote

kwa

sababu

ya

changamoto mbalimbali na kubwa zaidi ni uhaba wa


rasilimali fedha na wakati mwingine rasilimali watu na

99

vitendea kazi. Hata hivyo tumeweza kutekeleza zaidi ya


asilimia 88 ya ahadi zetu zilizomo kwenye Ilani za Uchaguzi
ya Chama cha Mapinduzi na mipango ya Serikali.
Siku moja nikiwa Marekani mwandishi mmoja wa
habari aliniuliza, je, utakapomaliza uongozi wako utapenda
Watanzania wakukumbuke kwa lipi? Nikamjibu, nitapenda
Watanzania waseme, Rais Kikwete alitukuta kuleee! na
sasa anatuacha hapa palipo juu. Mimi na ninyi ni
mashahidi kuwa tulipo leo ni bora zaidi ya kule tulipokuwa
jana.
Changamoto za nchi haziishi kila siku zinaibuka mpya.
Kila ukimaliza moja inazaa changamoto nyingine. Hivyo
ndivyo ilivyokuwa kwa baba wa taifa ambaye naye
hakumaliza changamoto zote, ndivyo ilivyokuwa kwa Mzee
Mwinyi na hivyo ndivyo alivyoniachia Rais Mkapa. Nami
namwachia anayekuja, naye afanye yake na yatakayobakia
atamwachia atakayemfuatia. Jambo linalonipa faraja ni kuwa

100

nami nimetoa mchango wangu kwa maendeleo ya nchi yetu


na watu wake.
Shukrani
Mheshimiwa Spika;
Nitakuwa

mchoyo

wa

fadhila

nisipokushukuru

Mheshimiwa Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Ghalib Bilal


kwa msaada wako, ushauri wako na ushirikiano wa karibu
ulionipatia katika kipindi hiki cha miaka 5. Nakutakia kila
la heri katika maisha yako baada ya mimi na wewe kumaliza
kipindi chetu cha uongozi. Namshukuru Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt.
Ali Mohamed Shein, ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano katika kipindi changu cha
kwanza. Nakushukuru kwa ushirikiano wako mkubwa,
msaada wako na ushauri wako wa hekima na busara ambao
umewezesha mafanikio tuliyoyapata katika kujenga nchi
yetu na katika kuimarisha muungano wetu.

101

Kwa namna ya pekee namshukuru Mheshimiwa


Mizengo Kayanza Pinda, Waziri Mkuu na Kiongozi wa
shughuli za Serikali Bungeni kwa kazi nzuri na ya kutukuka
uliyoifanya katika kipindi cha miaka 8.

Umepita katika

misukosuko mingi, na wakati mwingine umebebeshwa


lawama isiyokuwa yako. Daima umeonyesha ukomavu,
uimara

na

kutotetereka.

Napenda

pia

kumtambua

Mheshimiwa Edward Lowassa ambaye katika kipindi kifupi


alichokuwa Waziri Mkuu alifanya kazi kubwa na nzuri.
Nawashukuru

pia

Mawaziri,

Manaibu

Mawaziri,

Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa


Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Watendaji na
watumishi wote wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa
mchango wao katika kufanikisha majukumu ya Awamu ya
Nne. Mmenisaidia sana. Kwa kweli mafanikio haya
tunayozungumza leo yameletwa na juhudi zenu.
Nawashukuru viongozi wa dini, asasi za kiraia na
vyombo vya habari kwa kuniunga mkono mimi na Serikali

102

yangu na kwa mchango wenu muhimu.

Nawaomba

muendelee kuilea amani ya nchi yetu na watu wake.


Nakishukuru Chama changu, Chama cha Mapinduzi
kwa kuniamini, kuniunga mkono na kunisaidia kwa karibu,
katika miaka yote hii kumi. Wakati wote CCM imekuwa
pamoja nami na Serikali. Kimetoa uongozi wa nchi na
kuisimamia Serikali kutekeleza Ilani.
Mwisho lakini sio mwisho wa umuhimu, naishukuru
sana familia yangu. Namshukuru mke wangu Bi. Salma
Kikwete kwa mchango wake mkubwa ulionipa utulivu wa
kutekeleza majukumu yangu. Upo msemo kwamba, kwa
kila mwanaume mwenye mafanikio, yuko mwanamke,
nawaambia ni kweli. Shukrani zangu, pia, kwa wanangu na
wajukuu zangu kwa kunivumilia pale walipomkosa baba
yao na babu yao.

Karibuni mambo yatakuwa tofauti

mtaniona mara kwa mara kiasi kuwa huenda mkanichoka.


Hitimisho
Mheshimiwa Spika;

103

Ninapoagana na Bunge letu natambua kuwa baadhi ya


Wabunge mnarudi kutetea viti vyenu nawatakia kila la
kheri. Nimewahi kuwa Mbunge, hivyo naelewa hofu na
mashaka mliyonayo. Mwenyezi Mungu awape utulivu na
subira.

Nawatakia mapumziko mema kwa wale ambao

mmeamua kustaafu. Wale wanaogombea Urais waliomo


humu nawatakia kila la kheri, na nawashukuru kwa
kuonyesha nia ya kunipokea mzigo huu mzito. Nawatakiwa
heri katika matamanio yenu.
Kwa

ndugu

zangu

Watanzania

wenzangu,

nawashukuruni kwa kuniamini na kunichagua mara mbili


kuwa kiongozi wa nchi yetu. Nawashukuru kwa kuniunga
mkono wakati wote wa uongozi wangu. Mmenipa heshima
kubwa

ambayo

sitakaa

nisahau

maishani

mwangu.

Ninamaliza kipindi changu cha uongozi nikiwa nawapenda


sana na nitaendelea kuwapenda mpaka siku Mwenyezi
Mungu atakaponiita. Nitawa-miss kama mtumishi na
kiongozi wenu mkuu lakini tutakutana kwa urahisi zaidi

104

nikiwa raia. Baada ya hotuba yangu ndefu, sasa natangaza


kuwa Bunge la 10 limevunjwa rasmi, lakini linabakia kuwa
hai mpaka tarehe itakayotangazwa rasmi kwenye Gazeti la
Serikali kwa mujibu wa Katiba.
Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni kwa kunisikiliza!