You are on page 1of 11

MUHTAHSARI WA MIAKA 53 YA

MAFANIKIO YA KUJIVUNIA

AWAMU YA KWANZA

Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwalimu Julius Nyerere

Mafanikio ya Kijamii:

Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitatu ya Kwanza ulianzisha
shule za msingi, sekondari na ufundi ili kuandaa wataalam wa kusimamia
masuala ya utawala wa Tanganyika mpya.
Uanzishwaji wa Elimu ya Watu Wazima mwaka 1972.
Mafanikio ya Kisiasa:
Kuunda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwaka 1964.
Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano 1964 - 1969.
Azimio la Arusha 1967 lililojenga misingi ya usawa na maadili ya uongozi
katika nchi inayoamini katika siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
Mpango wa Maendeleo wa miaka 15 (1964 - 1980) na Mpango wa Pili wa
Maendeleo (1969 - 1974) na Mpango wa Tatu wa Maendeleo (1975 - 1980).
Azimio la Arusha lilipelekea nchi yetu kupata nchi marafiki kama vile China,
Urusi na Cuba, na matokeo ya uhusiano huo ni misaada, kwa mfano Reli ya
TAZARA.
Mwongozo wa TANU mwaka 1971 ulirekebisha maadili ya uongozi.
Uanzishaji Kikosi cha Kuzuwia Rushwa mwaka 1975
Muungano wa kipekee barani Afrika kati ya TANU na ASP kuunda CCM
mwaka 1977. Muungano huu wa vyama hivi viwili ulisaidia kuwaweka
karibu zaidi watu wa Bara na Visiwani ambao awali waliunganishwa na
Muungano wa mwaka 1964.
Mwaka huohuo 1977 Katiba ya Jamhuri ya Muungano iliandikwa na
kutangaza Tanzania kuwa nchi inayofuata siasa ya Ujamaa na yenye chama
Kimoja CCM. Katiba hiyo iliainisha mihimili mitatu ya Dola: Utawala, Bunge
na Mahakama.
Kushiriki mapambano ya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika.
Kulinda mipaka kikamilifu kwa kushinda Vita ya Kagera mwaka 1979.
Sheria ya Uhujumu Uchumi ilitungwa mwaka 1984 kuwabana wanyonyaji
na wahujumu wa uchumi wa Taifa, na baadaye kubadilisha kuwa Sheria ya
Makosa ya Uhujumu Uchumi.
Marekebisho ya Katiba ya mwaka 1977 yaliyofanyika mwaka 1984.
Mwalimu Nyerere ang'atuka kwa hiari yake mwenyewe.
Kuanzisha utaratibu wa rais kuongoza kipindi kisichozidi miaka 10 katika
wamu mbili za miaka mitano mitano.
Tanzania kama kiongozi wa mapambano dhidi ya ukoloni na ubaguzi wa
rangi barani Afrika na ilikuwa kiongozi wa Kamati ya Ukombozi Kunisi mwa
Bara la Afrika na ilisaidia harakati za uhuru nchini Msumbiji, Angola,
Namibia, Botswana, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Mafaniko ya Kiuchumi:

Mipango mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyobainishwa hapo juu.
Uwekezaji katika elimu ili kuandaa wataalamu wa kutumikia taifa.


Uanzishwaji Vijiji vya Ujamaa mwaka 1975vilivyowezesha kuwakusanya
wananchi kushi na kufanya kazi pamoja na kuharakisha upatikanaji wa
huduma na kuongez uzalishaji mali.
Matamko mbalimbali kama vile Kilimo cha Kufa na Kupona na Siasa ni
Kilimo kuhamasisha ushiriki na usimizi wa kilimo.
Uanzishwaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea kusaidia na kujenga uwezo
wa familia masikini.
Siasa za Kimataifa:
Msimamo imara uliopelekea Tanzania kuwa miongoni mwa vinara wa Nchi
Zisizofungamana na Upande Wowote.
Uenyekiti wa South-South Commission.
Kushiriki na kuchangia ripoti muhimu ya Challenge to the South mwaka
1980. Matokeo ya ripoti hiyo yalipelekea nchi zilizoendelea kukubali
kuundwa kwa Kituo cha Kudumu cha Ushirikiano kwa Nchi za Kusini
(South South Centre) mwaka 1995.
Ziara mbalimbali za viongozi wa kimataifa.
Mwalimu Nyerere kama mwanasiasa anayeheshimika kimataifa, suala
lililoifanya Tanzania pia kuheshimika kimataifa.

AWAMU YA PILI

Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi

Mafaniko ya Kijamii:

Kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa katika Awamu ya Kwanza.
Kumudu vuguvugu kubwa la mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi duaniani.
Uboreshwaji wa sekta za afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara,
umeme, nk ili kukabiliana na changamoto zilizokuwepo muda huo.
Kuboresha na kudumisha ushirikiano na nchi za SADC, Afrika, Ulaya, Asia
na Amerika.
Ziara ya Mandela na Baba Mtakatifu Yohana Paulo wa Pili, kama uthibitisho
wa uhusiano mzuri na nchi za nje.
Ukurasa mpya wa mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Malawi kufuatia
Rais Bakili Mulizi kuingia madarakani.
Mafanikio ya Kisiasa:Mabadiliko makubwa ya Kikatiba mwaka 1992 kuruhusu mfumo wa siasa
za vyama vingi vya siasa.
Kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi,
mwaka 1995.
Kutungwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Namba 13, mwaka
1995 ambapo Sekretari ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa.
Mafanikio ya Kiuchumi:


Kuendeleza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wa nchi.
Mageuzi ya kiuchumi mwaka 1986 yaliyobadilisha mifumo na mipango ya
kiuchumi kujielekeza kwenye mfumo wa soko huria.
Kufungua milango ya biashara na kukaribisha wawekezaji wa ndani na nje.
Kutungwa sera ya Ubinafsidhaji wa Mashirika ya Umma mwaka 1992.
Ujenzi wa miundombinu ya barabara kuu na vijijini, chini ya mradi
kabambe wa barabara, Integrated Road Project
.Kuanzisha mchakato wa kufufa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

AWAMU YA TATU

Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa

Mafanikio ya Kijamii:

Kuendeleza falsafa za Awamu ya Kwanza na mageuzi ya kisiasa na uchumi
yaliyoanzishwa na Awamu ya Pili.
Uanzishwaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na
Mapngo wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) ili kuboresha elimu
ya msingi na sekondari. Mpinago hiyo ilipelekea ongezeko la idadi ya shule
na wahitimu.
Utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kama vile Mradi wa Maji
Kahama-Shinyanga kutoka chanzo cha maji cha Ziwa Victoria, na Mradi wa
Maji wa Chalinze.
Ujenzi wa mtandao mkubwa wa barabara kwa kiwango cha lami.
Ujenzi wa daraja katika Mto Rufiji (Daraja la Mkapa).
Uanzishwaji wa Mamlaka ya Barabara (TANROADS).
Ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo (Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es
Salaam).
Kuendeleza mahusiano mazuri na nchi nyingine duniani, mafanikio ni
pamoja na ziara ya Rais wa 42 wa Marekani Bill Clinton mwaka 2000,
ambapo pamoja na masuala mengine, Mkataba wa Masuala ya Anga kati ya
Tanzania na Marekani ulisainiwa.
Mafanikio ya Kisiasa:
Kuendelea kujenga taifa kwa misngi ya utawala bora na uadilifu.
Kuundwa Tume ya Rais ya kuchunguza Kero za Rushwa mwaka 1996,
ambayo ripoti yake ilipelekea Serikali kuandaa Makakati wa Kitaifa Dhidi ya
Rushwa na Mapngo wa Utekelezaji kwa lengo la kuziba mianya ya rushwa.
Kuandaa Mwongozo wa Kitaifa wa Utawala Bora mwana 1999.
Kutunga Sheria ya Kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
mwaka 2001.
Mchango mkubwa katika jitihada za usuluhishi wa migogoro kimataifa, kwa
mfano DRC, Burundi na Rwanda
Mafanikio ya Kiuchumi:
Kuendeleza na kuboresha uchumi.
Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, hususan yaliyokuwa yakiendeshwa
kwa hasara.
Kuimarisha miundombinu kulingana na mageuzi ya kiuchumi.
Maandalizi na zunduzi wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 iliyotoa
mwelekeo wa kisiasa, kiuchumi na kijamii iliyozinduliwa mwaka 1999.
Kutungwa Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma mwaka 2001
Kutungwa Sheria ya Manuniz ya Umma mwaka 2001 iliyopelekea kuundwa
kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma mwaka 2004.
Uanzishwaji wa programu mbalimbali za maboresho kwa ajili ya kuimarisha
utawala bora.
Kuanzisha miradi na mipango mbalimbali ya kuendeleza uchumi wa taifa,
kwa mfano MKURABITA na TASAF.

AWAMU YA NNE:

Rais wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mafanikio ya Kijamii:
Kupanua na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa na uhuru wa
kutoa maoni.
Upanuzi wa sekta ya elimu kuanzia ya msingi, sekondari kila kata, vyuo na
vyo vikuu.
Ongezeko kubwa la shule la sekondari za serikali na za binafsi.
Ongezeko la vyuo na vyuo vikuu, kwa mfano Chuo Kikuu cha Dodoma,
kikubwa kuliko vyote Afrika Mashariki na Kati.
Ongezeko la zahanati, vituo vya afya na upanuzi wa hospitali za rufaa na
mikoa, sambamba na mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya afya.
Maendeleo katika sekta ya maji, kwa mfano kukamilisha mradi wa maji wa
Kahama-Shinyanga ulioanza kutekelezwa katika Awamu ya Tatu.
Uhusiano mzuri na nchi za nje, uliopelekea ziara za viongozi wa mataifa
makubwa duniani, Rais Obama wa Marekani, na mtangulizi wake Rais
George W. Bush na Rais Hu Jintao wa China.
Kupitisha Sheria ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya
mwaka 2007 iliyoipa TAKUKURU Mamlaka zaidi ya kushughulikia makosa
ya rushwa. Taasisi hiyo sasa ina Ofisi kila wilaya.
Sheria ya Kuanzisha Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa ilipitisha mwaka
2008.
Kuweka kipaumbele katika kuendeleza na kuimarisha michezo.
Kutoa uhuru mpana zaidi kwa vyombo vya habari.
Mafanikio ya Kisiasa:

Kufungua milango ya uhuru zaidi kwa lengo la kupanua demokrasia.
Kuridhia na kuingia katika utaratibu uliowekwa na Umoja wa Afika, wa
kujitathmini katika nyanja za Utawala Bora, Kupambana na Rushwa na
Utawala Bora, mwaka 2009.
Kuongeza idadi ya wanawake kwenye nafasi za juu za uongozi, na
kuwezesha wanawake wengi kuteuliwa akiwemo Dkt Asha-Rose Migiro
aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2006.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 uliokuwa wa huru na haki.
Kupitisha Sheria ya Gharama za Uchaguzi Namba 6, mwaka 2010.
Kupanua muundo wa Mahakama na kuongeza idadi ya majaji, kuwajengea
uwezo na kuwapatia vitendea kazi.
Kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kati ya CCM na CUF huko Zanzibar
baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, na kumaliza mgogoro wa kisiasa
Visiwani humo uliodumu kwa muda mrefu.
Kuweka historia kwa kumteua mwanasiasa wa chama cha upinzani, James
Mbatia, kutoka NCCR- Mageuzi, kuwa mmoja wa wabunge 10 wanaoteuliwa
na Rais.
Mafanikio ya Kiuchumi:


Jitihada za kuendeleza programu za maboresho katika nyanja za uchumi.
Vipaumbele katika kuendeleza sekta za kilimo na ujenzi wa miundombinu
ya barabara kuu na za mikoa, mambo yaliyobainishwa katika Mkakati wa
Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania (MKUKUTA II).


Kufanya mapitio ya Dira ya Maendeleo ya Taifa mwaka 2025.
Kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano, mwaka 2011, ili
kuimarisha na kuendeleza shughuli zinazochangia kukuza uchumi na
kuwezesha taifa kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati ifikapo mwaka
2025.
Kupitia Sera ya madini ili kuliongezea taifa mapato kutoka katika sekta ya
madini.
Dhana ya Kilimo Kwanza ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na
biashara.
Kuwapatia wakulima pembejeo na kuwapeleka wataalam wa ugani kwa
wakulima ili kusaidia maendeleo ya kilimo.
Kuweka msisitizo katika utunzaji na matumizi ya maliasili za kitaifa.
Kuweka umuhimu katika utunzaji mazingira, sambamba na kuimarisha
utunzaji na usimamizi wa vyanzo vya maji.
Kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, wa kikanda na wa kimataifa.
Rais Jakaya Kikwete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
mwaka 2008. Akiwa Mwenyekiti wa Umoja huo, Rais Kikwete alishughulikia
matatizo makubwa ya kisiasa, kama vile mgogoro wa uchaguzi nchin
Kenya, matatizo ya kisiasa nchini Somali, Sudan, Chad, Comoro na Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo.
Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume Maalum ya
Afrika.
Mchango mkubwa wa Rais Kikwete katika mijadala mbalimbali ya kimataifa.
Kufuta Sheria ya Kuzuwia Rushwa, Namba 16, ya mwaka 1971 na k
utungwa Sheria ya Kuzuwia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya
mwaka 2007, iliyoongoza makosa ya rushwa kutoka manne hadi 24.