You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

R.P.C
Namba ya simu 2502572
Fax -+255252503734
E-mail: rpc.mbeya@tpf.com
tanpol.mbeya@gmail.com
Unapojibu tafadhali taja

Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
S. L. P. 260,
MBEYA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 27.11.2015.

MZEE WA MIAKA 70 AUAWA KWA KUPIGWA NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA
WILAYANI RUNGWE.

MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA MAGARI MAWILI
KUGONGANA NA KISHA KUPINDUKA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MZEE WA MIAKA 70 MKAZI WA KIJIJI CHA MPELANGWASI WILAYA YA RUNGWE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWANYAPU MWAKASEGE ALIKUTWA AMEUAWA KWA
KUPIGWA MCHI KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NJE YA NYUMBA YAKE MNAMO TAREHE 26.11.2015 MAJIRA
YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPELANGWASI, KATA YA MATWEBE, TARAFA
YA PAKATI, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, WATU HAO AMBAO BADO KUFAHAMIKA WALIMVAMIA USIKU MAREHEMU
AKIWA AMELALA PEKE YAKE NA KUMTOA NJE NA KUMUUA. MWILI WA MAREHEMU
ULIKUTWA HAUNA NGUO HUKU UKIWA NA JERAHA LA KICHWANI.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU
ALIKUWA ANATUHUMIWA KUWA NI MCHAWI. UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA
NI PAMOJA NA MSAKO MKALI WA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA
KISHIRIKINA KWANI ZINA SABABISHA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII. AIDHA ANATOA
WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:

MTU MMOJA MKAZI WA SAE JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ERNEST MWAKAJE
[45] ALIFARIKI DUNIA BAADA GARI ALILOKUWA AKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.940
CQN AINA YA TOYOTA COASTER IKIENDESHWA NA DEREVA GABRIEL MWANGOSI [30]
MKAZI WA SOWETO KUGONGANA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T. 414 CMR AINA YA
HOWO TIPPER IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE WATSON CHARLES BIMBIGA HUKO
ENEO LA TAZAMA - PIPELINE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.11.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO
KATIKA ENEO LA TAZAMA – PIPE LINE, KIJIJI NA KATA YA INYALA, TARAFA YA TEMBELA,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.
AIDAHA KATIKA AJALI HIYO, WATU WATANO WALIJERUHIWA KATI YAO WAWILI MWANAUME
NA MWANAMKE WALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA NA WENGINE AMBAO NI ABIRIA
WATATU BADO WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA AMBAO NI 1. GABRIEL
MWANGOSI 2. JONAS ALBERT [24] NA 3. SHUKRANI MANAYARI [30].
CHANZO CHA AJALI NI GARI AINA YA HOWO KUTAKA KUYAPITA MAGARI MENGINE BILA
KUCHUKUA TAHADHALI. DEREVA WA GARI AINA YA HOWO ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO. UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA DEREVA HUYO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA, ALAMA NA
MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.