You are on page 1of 9

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
MSINUNUE
e
g
n
u
b
a
W
eneo la mradi wa Gesi TPDC
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.104
51
Toleo No.

Limesambazwa
kwa Taasisi
naTaasisi
Idarana
zote
MEM
, 2015
Limesambazwa
kwa
Idara
zote MEM Tarehe - 23-29 Januari
Januari
28 - Februari 3, 2016

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA

Somahabari Uk.2

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli


Tanzania
(TPDC), Dkt.
James Mataragio
Mkurugenzi
MtendMkurugenzi Mkuu wa

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

aji wa TANESCO,
Mhandisi Felchesmi
Mramba

REA, Dk. Lutengano


Mwakahesya

GST yapata Tuzo Maalum ya SAG kutoka Marekani


JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

Soma
habari
Uk. 3

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya
News
Bullettin
hiiGhorofa
na Jarida
la(MEM)
Wizar
a yapepe:
Nishati
na Madini
au Fika
Ofisi
ya Mawasiliano
ya Tano
Barua
badra77@yahoo.com
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Msinunue eneo la mradi wa gesi TPDC


Na Veronica Simba

erikali kupitia Shirika la


Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC) imewataka wananchi
kujiepusha na ununuzi wa
maeneo yaliyotengwa kwa
miradiyenyemanufaakwaTaifahususan
Mradi wa kuchakata na kusindika gesi
asilia uliopo mkoani Lindi.
Taarifa iliyotolewa hivi karibuni
kwa Vyombo vya Habari na Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC,
imeeleza kuwa ni kinyume cha sheria
za nchi, mtu yeyote kununua, kujigawia
au kuvamia maeneo ya kiwanja Namba
1 kilichopo katika Kitalu A Likongo,

Manispaa ya Lindi kwani eneo hilo kwa


sasa linamilikiwa kisheria na Serikali
kwa ajili ya Mradi wa kuchakata na
kusindika gesi asilia.
Taarifa imeeleza bayana kuwa
hakuna malipo yoyote yatakayofanyika
kwa mtu yeyote atakayethibitika
kuvamia eneo husika kwa minajili ya
kujipatia kipato.
Aidha, Taarifa hiyo imeeleza kuwa
zoezi linaloendelea sasa ni la uhakiki
kwa waliokuwa wakazi katika eneo hilo,
kwa lengo la kujiridhisha na idadi ya
kaya ambazo zitaathirika na mradi huo
pamoja na mazao, ili walipwe fidia na
kuhamishiwa sehemu nyingine.
Ulipaji wa fidia utafanyika kwa
mujibu wa sheria za nchi. Nia na

mategemeo ya Serikali ni kuhakikisha


kila mkazi anapata haki yake kwa
wakati na kama anavyostahili kisheria,
imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zoezi la
uhakiki linatarajiwa kumalizika Januari
30 mwaka huu, na kwamba uhakiki
unaofanyika sasa ni kwa kuzingatia
ripoti ya tathmini iliyokwishafanywa
awali na Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Vilevile, taarifa imefafanua kuwa,
Januari 19 mwaka huu, TPDC ilifanya
kikao kazi na uongozi wa Serikali ya
Mkoa wa Lindi. Kikao hicho kilihusisha
Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa
Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri
za Mkoa wa Lindi na Wawakilishi wa

Kampuni za kimataifa za mafuta na


gesi ambazo ni wabia na TPDC katika
Mradi husika kwa lengo la kutoa elimu
na faida zitokanazo na mradi huo.
Imeelezwa kuwa, pamoja na
elimu hiyo, viongozi wa Mkoa wa
Lindi walitaarifiwa kuhusu uwepo wa
wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), Wizara ya Nishati
na Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi pamoja na
TPDC, ambao wanaendesha zoezi la
uhakiki wakishirikiana na wataalam wa
ardhi kutoka Halmashauri ya Manispaa
ya Lindi.

Wawekezaji wasio na uwezo


hawakubaliki- STAMICO
Na Coleta NjelekelaSTAMICO

hirika la Madini la Taifa


(STAMICO)
linaandaa
mwongozo wa majadiliano
katika miradi ya uwekezaji
katika mfumo wa ubia, ili
kudhibiti wawekezaji wababaishaji,
kuboresha mgawanyo wa hisa na kuleta
tija kwa Taifa.

Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti


na Uchorongaji Alex Rutagwelela
alisema hayo hivi karibuni, baada ya
kushiriki ziara ya Waziri wa Nishati
na Madini Profesa Sospeter Muhongo
alipotembelea Mgodi wa Makaa
ya Mawe wa Kiwira unaotarajiwa
kuzalisha umeme kiasi cha megawati
200.
Rutagwelela alisema mwongozo
huo wa majadiliano utajenga uwezo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akitoa


maelekezo kwa Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) baada
ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea Mgodi wa Makaa ya Mawe wa
Kiwira hivi karibuni. Wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO Alex Rutagwelela. Wa tatu kutoka
kulia ni Meneja wa Huduma za Kihandisi katika Mgodi wa Kiwira,
Mhandisi Aswile Mapamba.
wa wataalam wa Shirika hilo katika
kubaini wawekezaji wababaishaji na
wasio na uwezo wa kifedha, kiteknolojia
pamoja na uzoefu wa kutosha, katika
kutekeleza miradi ya ubia ikiwemo ya
utafiti na uchimbaji madini.
Wakati sasa umefika kwa
wataalam wa STAMICO kuendelea
kufanya kazi kwa bidii zaidi na
kuendesha majadiliano ya miradi ya
uwekezaji kitalaam zaidi; hatua hii
itawezesha kuachana na wawekezaji
wababaishaji wa ndani na nje ya nchi,
alifafanua Rutagwelela.
Hivi karibuni Waziri wa Nishati
Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Uchorongaji wa STAMICO, Alex
na Madini Profesa Sospeter Muhongo
Rutagwelela (wa kwanza kushoto) akipokea taarifa kuhusu Mgodi wa
alifanya ziara kwenye mgodi wa Kiwira
Makaa ya Mawe wa Kiwira, kutoka kwa Boazi Masatu (aliyeinama katika na kuitaka STAMICO kukamilisha
meza), wakati alipotembelea mgodi huo hivi karibuni. Wa pili yake ni
hatua za zabuni za kumpata mwekezaji
Meneja Mkuu wa Kampuni ya KCPL Evans Mponjoli na wa tatu kutoka mbia katika mradi husika ili uweze
kuanza mara moja na kuwanufaisha
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamuwe.

Watanzania.
Profesa Muhongo alisema mara
baada ya kumbaini mbia husika,
STAMICO haina budi kurudi mezani
na kujiridhisha kwa uhakika juu ya
uwezo wa mwekezaji huyo na uzoefu
katika kuendesha migodi ya makaa ya
mawe na uzalishaji umeme kwa makaa
ya mawe.
Mgodi wa Kiwira ulianzishwa
mwaka 1988 ukiwa na mashapo ya
makaa (Economical reserve) ya mawe
tani milioni 35.14, mashapo ya kisanifu
(Proved reserve) tani milioni 22.14 na
mashapo yanayoweza kuvunwa kwa
faida (Mineable reserve) tani milioni
14.64 za makaa ya mawe.
Mgodi huo unamilikiwa na Serikali
kwa asilimia 100 kupitia Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO).

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

GST yapata Tuzo Maalum


ya SAG kutoka Marekani

MEM

Tahariri
Na Badra Masoud

Tuepuke tamaa kuhodhi


maeneo ya Serikali

Katika Toleo hili, tumechapisha taarifa kutoka Shirika


la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kuhusu zoezi
la uhakiki kwa ajili ya kulipa fidia kwa waliokuwa wakazi
katika maeneo ya Mradi wa kuchakata na kusindika gesi
asilia.
Aidha, tumeandika habari inayotokana na taarifa
husika, yenye kichwa cha habari Msinunue eneo la Mradi
wa Gesi TPDC.
Katika taarifa hiyo, pamoja na mambo mengine, TPDC
imewaasa wananchi kujiepusha na ununuzi wa maeneo
ya Kiwanja Namba 1, Kitalu A Likongo, kilichopo
Manispaa ya Lindi kwani eneo hilo kwa sasa linamilikiwa
kisheria na Serikali kwa ajili ya Mradi wa kuchakata na
kusindika gesi asilia.
Taarifa imeeleza bayana kuwa haitawajibika kutoa
malipo kwa yeyote atakayethibitika kuvamia eneo husika
kwa minajili ya kujipatia kipato.Hii ni kwa sababu ni
kinyume cha sheria za nchi kwa mtu yeyote kununua,
kujigawia au kuvamia maeneo yanayomilikiwa kisheria na
Serikali.
Kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kutoka
kwa baadhi ya wananchi kuhusu Serikali kutowalipa
fidia ipasavyo pale inapochukua maeneo kwa ajili ya
kuendeshea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande mwingine, kuna taarifa kuwa kuna baadhi
ya wananchi wenye tabia ya kufanya udanganyifu kwa
kujimilikisha au kuhodhi maeneo isivyo halali ambayo
Serikali inayamiliki na kisha kudai fidia kutoka kwa
Serikali.
Udanganyifu huo wa baadhi ya wananchi huhusisha
pia kumilikisha watu wengine au kuwauzia maeneo
ambayo tayari Serikali imeyafanyia tathmini na kufanya
taratibu za fidia kwa wahusika.
Kutokana na hali hiyo, tunaunga mkono taarifa
iliyotolewa na TPDC ikiwataka wananchi kuwa makini
na kujiepusha na kununua ama kuhodhi isivyo halali,
maeneo ambayo yanamilikiwa kisheria na Serikali kwa
ajili ya kuendeshea miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Ikumbukwe kuwa maeneo yanayochukuliwa na
Serikali kwa lengo la kuendeshea miradi hiyo, ni kwa faida
ya Taifa zima kwa ujumla. Aidha, kufanya udanganyifu wa
aina yoyote kwa ajili ya kuhodhi maeneo hayo ili kujipatia
faida binafsi ni kosa kisheria na husababisha migogoro
isiyo ya lazima.
Tunawaasa wananchi waliokuwa wakazi wa maeneo
ya Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia huko Lindi,
watoe ushirikiano unaostahili katika zoezi linaloendelea
la uhakiki ili hatimaye waweze kulipwa fidia stahiki kwa
mujibu wa sheria.
Ikumbukwe kuwa lengo la Serikali siku zote ni kutenda
haki kwa wananchi wake, hivyo ushirikiano kutoka kwa
wananchi husika ni muhimu sana.
Serikali inatarajia kuwepo na uaminifu na ushirikiano
kutoka kwa wananchi wakazi wa eneo husika ili kwa
upande wake iweze kuhakikisha kila mkazi anapata haki
yake kwa wakati na kama anavyostahili kisheria.
Tuisaidie Serikali yetu kufanikisha malengo ya kuondoa
umaskini nchini mwetu kupitia utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa ufanisi.
Tuwe wazalendo na tuipende nchi yetu.

Na Samwel Mtuwa - GST

akala wa Jiolojia Tanzania


(GST)
umepata
tuzo
maalum ijulikanayo kama
Special Achievement of
GIS (SAG) kutokana na
utumiaji mzuri wa programu ya uchoraji na
uchakataji wa Ramani za Jiolojia ijulikanayo
kama ArcGIS kutoka kwa taasisi miliki ya
programu hiyo iitwayo Environment System
Research Institute (ESRI) yenye makao
makuu nchini Marekani.
Meneja wa Uchoraji Ramani na
Uchakataji taarifa za Jiosayansi wa GST,
Terence Ngole alisema hayo hivi karibuni
mjini Dodoma wakati akizungumza na Jarida
hili.
Ngole alisema kuwa GST imepata Tuzo
hiyo kwa mwaka 2015 kutokana na uzoefu
na ubingwa wa matumizi ya teknolojia ya
programu hiyo tangu mwaka 2004.
Aidha, alitaja sababu nyingine iliyochangia
GST kutunukiwa Tuzo hiyo kuwa, ni kuweza
kutumia leseni 29 za ArcGIS zilizogawanywa
katika sehemu mbili ambazo ni leseni 10
zinazotumiwa na watu wengi kwa wakati
mmoja pasipo kuingiliana (concurrent license)
pamoja na leseni 9 zinazotumiwa na mtu
mmoja tu (single use license).
Leseni hizo hutumiwa na GST katika
viwango vya aina Tatu ambavyo ni kiwango
cha juu, kiwango cha kati na kiwango cha
chini (Advanced, Standard & Basic).
Ngole aliongeza kuwa, utumiaji wa
programu hiyo katika hali ya ubora na
umakini katika pande zote yaani uchoraji na
uchakataji wa taarifa za jiosayansi (Maping
tool and Analytical tool) ni sababu nyingine ya
GST kupata tuzo hiyo.
Akifafanua kuhusu matumizi ya programu
husika, Ngole alisema kuwa inatumika
katika uchakataji na uchambuaji wa taarifa
za jiosayansi lakini kuna moduli nyingine ya
programu hiyo inayotumika kutunza taarifa
za jiosayansi.
Kuhusu faida zinazotokana na utumiaji
wa programu ya ArcGIS, Ngole alizitaja
baadhi ya faida kuwa ni pamoja na kuwezesha
uchoraji wa kisasa wa ramani za jiosayansi,
kuwezesha uchakataji na uhifadhi wa taarifa
za jiosayansi katika mfumo wa kisasa na
kuwezesha kusambazwa kwa taarifa kwa
wadau katika hali ya ubora zaidi yaani (GIS

based web-portal).
Alitaja faida nyingine kuwa ni pamoja
na programu husika kuwezesha wepesi wa
upatikanaji, usambazaji na ushirikishaji wa
taarifa za jiosayansi ukilinganisha na kipindi
cha miaka ya nyuma kabla ya matumizi ya
programu hiyo.
Tuzo za SAG zilianza kutolewa mwaka
2004 na hutolewa mwishoni mwa kila mwaka.
Katika Tuzo za Mwaka 2015, Kampuni 97
za Marekani na 77 kutoka nje ya Marekani
zilipata tuzo hizo katika sekta mbalimbali za
maendeleo kama vile gesi, umeme, madini na
mazingira.

Meneja wa Uchoraji Ramani na


Uchakataji taarifa za Jiosayansi katika
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
Terence Ngole, akionesha tuzo maalum
ya SAG iliyotolewa na Taasisi ya
Environment System Research Institute
ya Marekani (ESRI) kwa mwaka 2015.

KWA HABARI PIGA SIMU


kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Mhariri Mkuu: Badra Masoud
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

NewsBulletin

Jitihada za Prof. Muhongo kuongeza


uzalishaji umeme ziungwe mkono

Waziri wa Nishati na Madini, akilakiwa na baadhi ya Askari wa Chuo Cha Magereza, Tukuyu alipofika
katika eneo hilo ambapo Kampuni ya ea- power iko kwenye mchakato wa kuzalisha umeme kutokana na
bwawa ambalo liko ndani ya eneo la Magereza. Nyuma ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mwalimu Zainabu
Mbusi.

Asteria Muhozya na
Rhoda James

http://www.mem.go.tz

nchini.
Prof. Muhongo alieleza kuwa
mbali na kuingiza umeme katika Gridi
ya Taifa, lakini pia kwa kushirikiana
vizuri na Shirika hilo kutakuwa na kasi
ya usambazaji umeme katika maeneo
ambayo miradi hiyo inaendeshwa na
hivyo kuongeza kasi ya usambazaji
umeme nchini kupitia TANESCO
au kupitia Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), jambo ambalo pia litawezesha
kutekeleza Ilani ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambayo inasema
hadi ifikapo mwaka 2020 , wananchi
waliounganishwa na umeme wafikie
asilimia 60 na kiwango cha uzalishaji
kifike megawati 4915.
Katika kuonesha kwamba, Profesa
Muhongo anamaanisha kile ambacho
pia kimeelezwa katika Dira ya
Maendeleo ya Taifa kuwa Tanzania
inakuwa miongoni mwa nchi zenye
Uchumi wa Kati ifikiapo mwaka
2025. Prof. Muhongo anataka Sekta ya
Nishati itoe mchango mkubwa kufikia
uchumi huo kwa kuwa rasilimali za
kufikia lengo hilo kupitia nishati zipo
kinachotakiwa ni dhamira, na kasi
ya kutekeleza kwa kuwa, awali Dira
ya Maendeleo ya Taifa ilieleza kuwa,
ifikapo mwaka 2015 uunganishaji
umeme ufikie asilimia 30; lakini
kutokana na utekelezaji madhubuti
wa dira hiyo kiwango hicho kilivukwa
kufikia asilimia 40 mwaka 2015.
Vivyo hivyo, Dira ya Maendeleo ya
Taifa inaeleza kuwa, ifikapo mwaka
2025 ifikie asilimia 50 na mwaka 2033
asilimia 70.
Prof. Muhongo
katika hilo
anaamini kwamba, nishati ya umeme
ni chachu kubwa ya maendeleo na
moja ya nyenzo kuu za ukuaji uchumi
>>Inaendelea Uk. 5

atika kudhihirisha kile


alichokuwa akikieleza
katika
ziara
zake
alipotembelea
miradi
ya kuzalisha umeme,
maeneo ya tafiti na miradi ya Makaa
ya Mawe hivi karibuni katika Mikoa
ya Njombe, Ruvuma na Mbeya,
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo akisisitiza mara
kadhaa kuhusu dhamira ya Serikali
ya kuhakikisha Tanzania inakuwa
na umeme wa kutosha kutoka
vyanzo mbalimbali vya Nishati
vinavyopatikana nchini ikiwemo Gesi
Asilia, Nishati Jadidifu, Maji, Makaa
ya Mawe, Jua, na Upepo.
Katika kila kituo cha kuzalisha
umeme au miradi ya umeme, Prof.
Muhongo hakuacha kulitaka Shirika
la Umeme Nchini (TANESCO),
kufanyakazi kwa karibu na Wazalishaji
Wadogo, Wa Kati na Wakubwa wa
umeme na kueleza kuwa, wazalishaji
hao watasaidia kuongeza kiwango
cha umeme nchini, jambo ambalo pia
litasaidia kuongeza kiasi cha umeme
katika gridi ya Taifa kwakuwa,
wazalishaji hao pia wataliuzia Shirika
hilo umeme badala ya Shirika hilo
kuwa mzalishaji pekee na hivyo
kuondoa changamoto ya nishati hiyo

Meneja Mkuu wa Kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia mabaki ya miti ya Miwati, Dkt. Rayeer
Singh (aliyenyoosha mikono), akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
na Ujumbe wake walipotembelea Kampuni hiyo.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

MAKALA

Jitihada za Prof. Muhongo kuongeza uzalishaji umeme ziungwe mkono

Waziri wa Nishti na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimweleza


jambo, Meneja wa Bwawa la kuzalisha umeme kwa Maji la Kihansi,
Mhandisi Pakaya Sakaya (wa Kwanza kulia), walipotembelea bwawa
la kuzalisha umeme la Uwemba, Njombe ambalo liko chini ya Bwawa
la Kihansi.
>>INATOKA Uk. 4
ambao una mchango mkubwa katika
kuongeza kipato cha mtu mmoja
mmoja na pato la taifa na uwezekano
wa kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka
2020 upo . Aidha, jambo hilo pia
lilisukuma ziara za Prof. Muhongo
kuangalia hali ya uzalishaji umeme
katika maeneo kadhaa ikiwemo
mabwawa ya kuzalisha umeme ya
Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu,
Hale, Kidatu , Pangani na pia
alitembelea mikoa ya Mwanza na
Kagera.
Ziara hizo pekee ni kiashiria
tosha kwamba, Prof. Muhongo
amedhamiria kuifanya Tanzania
inakua na umeme wa kutosha na
wa uhakika. Aidha, jambo hili pia
linadhihirika pale ambapo, katika ziara
hizo hakusita kuwataka wazalishaji
wadogo
kueleza
changamoto
zinazowakabili katika utekelezaji
wa majukumu yao, lengo likiwa ni
kuhakikisha Serikali inashirikiana kwa
karibu na wazalishaji hao waweze
kuzalisha, kuongeza viwango vyao
vya uzalishaji na hatimaye kuiuzia
TANESCO umeme wa bei nafuu
ambao pia hautakuwa mzigo kwa
wananchi.
Mifano hii ni michache tu kati ya
maeneo mengi aliyotembelea ambapo
aliitaka kampuni ya TANWAT
iliyopo Mkoani Njombe inayozalisha
umeme kwa kutumia Mabaki ya
Miti ya Miwati, kuongeza uwezo wa
uzalishaji kutoka Megawati 2.5 kufikia
10, huku akiitaka kampuni hiyo
kueleza changamoto zitakazozuia

uzalishaji huo kufikiwa. Vilevile, katika


Kituo cha kuzalisha umeme cha
Tulila, kinachomilikiwa na Watawa
wa Kanisa Katoliki wa Shirika la
Mtakatifu Agnes Chipole, Profesa
Muhongo aliwataka Wataalam wa
TANESCO kuendelea kuwapa
mafunzo wazalishaji hao kwa kipindi
cha mwaka mmoja ili waweze
kumudu vizuri zaidi shughuli za
uzalishaji umeme.
Prof. Muhongo alieleza umuhimu
wa wazalishaji hao kuliuzia Shirika
hilo umeme kwa bei nafuu akiamini
kwamba, unafuu huo wa bei
utaliwezesha Shirika hilo kujiendesha
kibiashara bila kutegemea ruzuku za
Serikali. Aidha, Prof. aliongeza kuwa,
ikiwa TANESCO itanunua umeme
kwa bei ghali, italazimika kuuza
kwa bei nafuu kuepuka kuwaumiza
watumiaji hususani wananchi jambo
ambalo linafanya shirika hilo kuwa
tegemezi.
Inawezekana kabisa kuna baadhi
ya wananchi wanadhani kuwa
Profesa Muhongo anavyozungumzia
wazalishaji wadogo anamaanisha
kwamba
TANESCO
watanyanganywa majukumu yake
ya kuzalisha na kusambaza umeme.
Dhana hiyo si kweli , taarifa
sahihi kuhusu jambo hilo ni kwamba,
upo Mkakati wa mwelekeo wa
kurekebisha sekta ndogo ya umeme
(EISI- RSR)
ambayo Mwezi
Juni 2014, Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ilipitisha na
kuchapisha mkakati wa mageuzi wa
Electricity Supply Industry Reform
Strategy and Roadmap (ESI-RSR)
2014 2025. Lengo la msingi wa

Prof. Sospeter Muhongo na Ujumbe wake, wakimsikiliza Mtaalam wa


Kituo cha kuzalisha umeme Tulila, kinachomilikiwa na Watawa wa
Kanisa Katoliki wa Shirika la Mtakatifu Agnes Chipole wakati wa ziara
yake.
mkakati huo ni kuboresha mazingira
ya uwekezaji wa sekta binafsi katika
nyanja za uzalishaji na usambazaji,
na kuongeza uunganishaji wa umeme
katika ngazi zote.
Utekelezaji wa mpango huo
ambao unatarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka kumi na
moja (11) umegawanyika katika
vipindi vikuu vitatu ambavyo ni muda
mfupi, wa kati na muda mrefu.
Mkakati wa muda mfupi ni
kutenganisha shughuli za Uzalishaji
ili zifanywe na Kampuni Tanzu ya
TANESCO. Umiliki wa uzalishaji,
usafirishaji na usambazaji chini ya
awamu hii itaendelea kuwa chini ya
Serikali, kama mbia moja.
Mkakati wa muda wa kati unahusu
kutenganisha sehemu ya usambazaji
kutoka kwenye usafirishaji. Katika
Awamu hii, Kampuni za uzalishaji,
usafirishaji na usambazaji zitaendelea
kuwa chini ya umiliki wa Serikali.
Mkakati wa muda mrefu
utahusisha Ofisi za Kanda kujihusisha
na usambazaji wa huduma za umeme
ambazo pia zitagawanywa kulingana
na uwezo wa kujiendesha. Katika
kipindi hicho cha muda mrefu,
kampuni binafsi za usambazaji
umeme zitaendelea kushiriki katika
shughuli za uzalishaji na usambazaji
umeme kwa ajili ya kuchochea
ushindani na ufanisi kwenye soko.
Aidha, ili kujua undani wa suala
hilo ni vema wadau wakapata fursa
ya kusoma mkakati wa mageuzi
ujulikanao kama Electricity Supply
Industry Reform Strategy and
Roadmap (ESI-RSR) 2014 2025
ambao unapatikana katika tovuti ya

wizara kwa anuani ya www.mem.


go.tz.
Aidha, ni vema tukatambua na
kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Wizara chini ya Profesa Muhongo
kwa kuwa anataka Tanzania yenye
umeme mwingi wa kutosha utakao
chochea ukuaji wa Viwanda kama
ilivyo Kaulimbiu ya Serikali ya
Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania
ya viwanda vikubwa na vidogo.
Mara baada ya ziara hiyo,
hatimaye tarehe 8 Februari, 2016,
Profesa Muhongo atakutana na
wazalishaji binafsi wadogo wa umeme
wa maji chini ya Megawati 20, lengo
la mkutano huo ni kuimarisha
ushirikiano, kutumia utaalam, uzoefu
na miundombinu ya TANESCO, na
kujadili namna ya kuongeza uzalishaji
wa mitambo ya wazalishaji wadogo.
Mkutano huo wa wazalishaji
wadogo unaotarajia kufanyika katika
bwawa la kuzalisha umeme kwa
maji la Mtera, unaonesha dhamira
safi aliyonayo Waziri Muhongo na
Wizara ya kuhakikisha kwamba
Tanzania inakuwa na umeme wa
kutosha ambao utakuwa kichocheo
cha ukuaji wa viwanda na shughuli
nyingine za kiuchumi zinazotegemea
nishati hiyo, ikiwemo kupanua wigo
wa ajira.
Hivyo, wananchi na wapenda
maendeleo hawana budi kuunga
mkono jitihada hizo za Wizara
ya Nishati na Madini badala ya
kuwanyooshea vidole viongozi
ambao wameonesha nia ya dhati ya
kuendeleza sekta ya Nishati ili iweze
kutoa mchango unaotarajiwa kwa
kizazi cha sasa na kijacho.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

TMAA kuimarisha usimamizi wa mapato ya uchenjuaji wa marudio


Na Mwandishi wetu

akala wa Ukaguzi
wa
Madini
Tanzania (TMAA)
umekusanya wastani
wa shilingi milioni
40 kila mwezi kufuatia ukaguzi wa
uzalishaji na mauzo ya dhahabu
kutoka kwa wamiliki wa mitambo ya
uchenjuaji dhahabu wanaoyeyusha
mabaki (tailings) ya wachimbaji
wadogo.
Akizungumza na MEM Bulletin
hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Afisa
Mahusiano wa Wakala huo, Yisambi
Shiwa alisema ukaguzi wa aina hiyo
ulianza rasmi mwezi Agosti, 2012
katika mikoa ya Mwanza na Geita
kwa kushirikiana na Ofisi za Madini
katika maeneo husika.
Alisema TMAA ilibuni na
kuanzisha ukaguzi wa uzalishaji
na mauzo ya dhahabu kutoka kwa
wamiliki wa mitambo ya uchenjuaji
dhahabu wanaoyeyusha mabaki ya
wachimbaji wadogo kupitia mitambo
ya upembuaji wa marudio ya mashapo
ya wachimbaji wadogo ijulikanayo
kama vat leaching plants.
Ukaguzi huu uliiwezesha Serikali
kupata takwimu halisi za uzalishaji
kutoka kwa wahusika ambapo wastani
wa kilo 15 za dhahabu zilizalishwa
na kuiwezesha Serikali kukusanya
mrabaha wastani wa Shilingi milioni
40 kila mwezi, alisema.
Akizungumzia kuhusu mitambo
hiyo ya kuchenjulia dhahabu, Yisambi
alisema kadri siku zilivyopita watu
wengi zaidi walijenga mitambo husika
ya elution sehemu mbalimbali nchini
na hivyo kufanya idadi ya mitambo
hiyo kuongezeka kutoka mitambo 11
iliyokuwa ikikaguliwa mwaka 2012
katika mikoa ya Mwanza na Geita
hadi kufikia zaidi ya mitambo 100
inayokaguliwa hivi sasa.
Anasema kutokana na kuongezeka
kwa mitambo hiyo, uzalishaji
wa dhahabu umeongezeka hadi
kufikia wastani wa kilo 120 ambapo

mrabaha unaolipwa Serikalini nao


umeongezeka sawia hadi kufikia
takribani Shilingi milioni 320 kwa
mwezi.
Yisambi
alisema
teknolojia
ya uchenjuaji wa dhahabu kwa
kuyeyusha mabaki yatokanayo na
uchimbaji mdogo na kisha kutumia
carbon kuchenjua dhahabu (elution
column) iliingia nchini hususan kanda
ya Ziwa Viktoria ikitokea nchini
Zimbabwenaimewezeshawachimbaji
wadogo kuuza mabaki zao ambazo
tayari walikwishazichenjua na kwa
wachimbaji hao huhesabika kama
taka.
Alisema muunganiko huo wa
kimahitaji baina ya wachimbaji
wadogo na wa kati, uliongeza mfumko
wa shughuli za uchimbaji na biashara
ya madini katika mikoa mingi ya
Tanzania kwa kutumia teknolojia hiyo
mpya.
Aliongeza kuwa, baada ya
wachimbaji wa kati kuanza kutumia
teknolojia hiyo ya kuchenjua
marudio yaliyokuwa yameachwa
na wachimbaji wadogo na wa kati,
changamoto kubwa iliyojitokeza
ilikuwa ni jinsi ya kubaini na kudhibiti
mfumko huo wa uzalishaji.
Ili kukabiliana na changamoto
hiyo, Yisambi alisema Wakala ulibuni
utaratibu wa kudhibiti mapato ya
Serikali yatokanayo na biashara ya
dhahabu inayozalishwa kwenye
mitambo ya uchenjuaji wa marudio
katika Kanda ya Ziwa hususan katika
mikoa ya Geita na Mwanza.
Ili kudhibiti usafirishaji wa carbon,
Wakala uliandaa vibali maalum
kwa ajili ya kutumiwa kusafirisha
carbon kutoka vat leaching kwenda
kwenye elution plant; vibali hivyo
vinaainisha uzito wa carbon, kiasi
cha dhahabu kilichomo na mitambo
ambayo carbon hizo zinapelekwa
ikiwa ni pamoja na namba ya leseni ya
muhusika, alisema.
Aliongeza
kuwa,
kutokana
na hatua mbalimbali za udhibiti
zilizochukuliwa na Wakala kwa
kushirikiana na Ofisi za Madini, katika

Elution column zikiwa zimewekewa lakiri za Serikali

Marudio yakipakiwa kwenye gari tayari kwa ajili ya kupelekwa kwenye


matanki ya kuyeyushia dhahabu iliyopo ndani ya marudio hayo
kipindi cha mwezi Disemba 2015,
udhibiti huo umewezesha ukusanyaji
wa shilingi milioni 321.14 kama
mrabaha kutoka kwa wachenjuaji
wa marudio katika mikoa ya Geita,
Mwanza na Mbeya ambapo jumla ya
kilo 130 za dhahabu zilizalishwa.
Alisema, Wakala umeweza kufikia
mafanikio hayo katika kuwezesha
ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo
na shughuli za uzalishaji na biashara
ya madini nchini kutokana na kufanya
kazi kwa ushirikiano na weledi.
Vilevile, Yisambi alisema TMAA
imekuwa ikitoa elimu shirikishi kwa
wamiliki wa mitambo ya kuchenjua
dhahabu ili kuwaongezea uelewa wa
shughuli za Wakala na Ofisi za Madini
na vilevile kuhusu sheria, kanuni na
taratibu zinazopaswa kutekelezwa
na wamiliki wa mitambo hiyo kabla
na baada ya kuanzisha shughuli na
biashara ya madini.
Mafanikio yote hayo yametokana

na ubunifu na ushirikiano mkubwa


baina ya watendaji wa Wakala, Ofisi
za Madini pamoja na wananchi
waliowezesha upatikanaji wa taarifa
husika.
Akizungumzia
kuhusu
changamoto, alisema kuwa baadhi
ya wamiliki wa mitambo husika
sio waaminifu kwani wanafunga
na kuendesha mitambo hiyo kwa
siri kitendo ambacho kinaikosesha
Serikali mapato yake yatokanayo na
shughuli husika.
Aidha, alisema katika kukabiliana
na changamoto hiyo, Wakala
umeendelea kufanya kaguzi za
kushitukiza kwa kushirikiana na Ofisi
za Madini na vilevile anasema Wakala
unatoa wito kwa wananchi kufichua
na kutoa taarifa kwa Wakala, Ofisi ya
Madini au Polisi ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa kwa watakaogundulika
wakifanya shughuli hizo kinyume na
Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

MAKALA

PROFESA MUHONGO:
UMEME NI INJINI YA UCHUMI
Na Mohamed Saif

kiwa ni takriban mwezi mmoja


tangu ameapishwa kuwa waziri
wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo amekuwa
gumzo kubwa kwa juhudi na
kasi yake katika kuhakikisha tatizo la
umeme nchini linamalizika.
Mara tu baada ya kuapishwa,
Profesa Muhongo alikutana na
Menejimenti ya Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na kutaka
majawabu ya kisayansi ya maswali
makuu manne ambayo alisema
yatasaidia katika kutatua tatizo la muda
mrefu la nishati ya umeme nchini.
Maswali ambayo yaliulizwa ni:
kwa namna gani tatizo la kukatika
umeme mara kwa mara litamalizika;
pili ni vipi wamejipanga kuhakikisha
kunakuwepo na umeme mwingi,
wa kutosha na wa uhakika; tatu
ni vipi watahakikisha gharama za
umeme (bei) zinapungua kutokana na
matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha
umeme na swali la nne ni kwamba
vipi wamejipanga kuondokana na
malalamiko ya wateja katika kutoa
huduma bora kwa wananchi.
Mbali na maswali hayo, Waziri
Muhongo aliwaagiza kuandaa
mkakati madhubuti utakaotumika
kuhakikisha makusanyo ya mapato
yatokanayo na huduma ya nishati ya
umeme yanaongezeka mara mbili ya
malengo yaliyokuwapo awali.
Alisema wananchi wanahitaji
umeme wa bei nafuu ili waweze
kujikwamua na umasikini huku
akieleza kwamba ni wakati mwafaka
suala hilo likatazamwa kwani bei ya
huduma ya umeme ikishuka bidhaa
nyingine pia zitashuka.
Profesa Muhongo alisema lengo la
Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda na ili
kufikia azma hiyo, anasema inatakiwa
kuwepo na umeme mwingi na wa
uhakika.
Vilevile
Profesa
Muhongo
aliwataka watendaji hao kujieleza ni
kwanini umeme umekuwa ukikatika
mara kwa mara ikiwa ni pamoja
na kuwataka waeleze wao kama
Menejimenti ya Shirika hilo ni hatua
zipi ambazo tayari wamezichukua
kuhakikisha hali hiyo haijirudii.
Siku ya pili baada ya kuapishwa
kwake, Waziri Muhongo alianza
ziara ya kukagua miundombinu na
mitambo ya uzalishaji umeme ambapo
alieleza umuhimu wa kutembelea
maeneo hayo na kujionea hali halisi
iliyoko kwenye maeneo ya uzalishaji
umeme nchini.
Kukaa ofisini hakuwezi kutatua
tatizo la umeme nchini; nimeamua
kufanya ziara nchi nzima ili kukagua
hali halisi ya uzalishaji wa umeme,
alisema.
Waziri Muhongo alianza ziara
yake ya kukagua vyanzo vya kuzalisha
umeme kwa nguvu ya maji ambapo
alitembelea Kituo cha Hale, New
Pangani vya Mkoani Tanga na siku

hiyo hiyo alitembelea kituo cha


Nyumba ya Mungu cha Mkoani
Kilimanjaro.
Baada ya hapo Waziri Muhongo
aliendelea na ziara yake kwa
kutembelea Mikoa ya Morogoro na
Iringa ambapo alikagua uzalishaji
umeme katika vituo vya Mtera,
Kihansi na Kidatu na kujionea hali ya
mitambo ya kuzalisha umeme katika
vituo hivyo pamoja na hali halisi ya
maji kwenye mabwawa ya vituo hivyo.
Katika majumuisho ya ziara yake
katika vituo hivyo vya kuzalisha
umeme vilivyotajwa hapo juu, Waziri
Muhongo alisema amebaini kwamba
sababu kuu iliyopelekea kupungua
kwa kina cha maji katika mabwawa
hayo ni mfumo duni wa umwagiliaji
usio zingatia taratibu za matumizi
sahihi ya maji.
Alisema mfumo wa umwagiliaji
unaotumika kwenye mashamba
yanayotumia maji ya mito inayotiririka
kwenye mabwawa ya kuzalisha
umeme ni wa kienyeji sio wa kitaalamu
na hivyo aliagiza matoleo ya maji ya
kumwagilia kwenye mashamba hayo
yafungwe.
Kufuatia agizo hilo, tayari
imeelezwa kuwa kina cha maji
kwenye mabwawa husika kimeanza
kuongezeka; hata hivyo Waziri
Muhongo ameelekeza kuacha maji
hayo yaongezeke ili kuwa na uzalishaji
umeme wenye tija zaidi kwa kipindi
chote.
Suala lingine ambalo Waziri
Muhongo aliliwekea mkazo katika
ziara zake ni taratibu za manunuzi ya
mitambo ya kuzalisha umeme ambao
alionyesha kutoridhishwa nao.
Waziri Muhongo amelitaka
Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), kuwa makini wakati
wa kuingia mikataba na Wakandarasi
ili kuepuka kuuziwa mitambo hafifu
na kusababisha hasara na migogoro
isiyo ya lazima.
Agizo hilo limefuatia ukaguzi
wake kwenye mitambo ya kuzalisha
umeme ambapo alikuta mitambo
kadhaa ikiwa imeharibika na hivyo
kushindwa kuzalisha umeme na huku
baadhi ya mitambo ikiwa haina muda
mrefu tangu imefungwa na mingine
imesimama kutokana na kukosa
ukarabati.
Katika kituo cha kuzalisha umeme
cha Hale ilielezwa kwamba kituo
kinayo mitambo miwili ambayo
ilifungwa mwaka 1964 ikiwa na
uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi
cha megawati 21 ambapo kila mtambo
(kati ya mitambo miwili) katika kituo
hicho una uwezo kuzalisha umeme
wa kiasi cha megawati 10.5.
Kilichomshangaza
Waziri
Muhongo ni kwamba ukarabati wa
kwanza wa mitambo hiyo ulifanyika
mwaka 1986 na kuwa ilipofika mwaka
2008 mtambo mmoja uliharibika na
hivyo kusababisha mtambo mmoja tu
kufanya kazi.
>>Inaendelea Uk. 8

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akikagua vipuli


vilivyoharibika vya mitambo ya kuzalisha umeme ya Nyakato ya jijini
Mwanza.

Baadhi ya mitambo ya kuchakata Gesi Asilia ya Kituo cha Madimba


ambacho kilitembelewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo.

Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta uliopo


katika kituo cha Nyakato cha jijini Mwanza.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin

MAKALA

http://www.mem.go.tz

Profesa Muhongo: Umeme ni Injini ya Uchumi


>>INATOKA Uk. 4

Akionekana
kukasirishwa
na
taarifa hiyo, Profesa Muhongo alihoji
ni kwanini ukarabati wa mtambo huo
umechukua muda mrefu na hivyo
kuagiza mtambo huo kufungwa haraka
ili uweze kuzalisha nishati ya umeme.
Hali kama hiyo alikutana nayo
alipotembelea kituo cha kuzalisha
umeme cha Somanga Fungu cha Kilwa,
Mkoani Lindi ambapo alikuta mtambo
mmoja kati ya mitatu iliyopo kituoni
hapo umeharibika na haufanyi kazi
tangu mwaka 2012 na huku kituo hicho
kilizinduliwa rasmi mwaka 2010.
Halikadhalika waziri Muhongo
alifanya ziara kwenye kituo cha kuzalisha
umeme cha Nyakato, mkoani Mwanza
chenye uwezo wa kuzalisha megawati
60 ambapo alijionea mitambo mitatu
kati ya mitambo kumi imeharibika na
huku kituo hicho kikiwa kimezinduliwa
mwezi Novemba mwaka 2013.
Profesa
Muhongo
alisema
alichogundua tangu ameanza ziara
ya kukagua mitambo ya kuzalisha
umeme maeneo mbalimbali nchini ni
kuwa Shirika hilo linaonekana kutumia
watu wa kati katika kununua mitambo
yake na vilevile ukarabati wa mitambo
haufanyiki inavyopaswa.

Ilipaswa wataalamu wafanye


uchunguzi wa mitambo na kujiridhisha
kabla mitambo hiyo haijaletwa nchini; na
pia msisubiri hadi mitambo inaharibika
ndiyo mnafanya ukarabati, alisema.
Alisema haoni sababu ya Shirika hilo
kununua mitambo yake kutoka kwenye
kampuni ambazo hazina viwanda vya
kutengeneza mitambo husika wakati
zipo kampuni mahiri duniani zenye
kutengeneza mitambo bora.
Hawa inaonekana wanatumia watu
ambao hawatengenezi mitambo na
ndio maana tunashuhudia tunauziwa
mitambo hafifu ambayo katika kipindi
kifupi tangu imeanza uzalishaji baadhi
imeharibika, alisema.
Mbali na suala la umakini kwenye
ununuzi, Profesa Muhongo alisema
wataalamu wanapaswa kufuata taratibu
za uendeshaji wa mitambo na hivyo
aliwaasa kuwa makini muda wote
wakati wa kuendesha mitambo hiyo.
Baada ya kujionea hali halisi ya
umeme maeneo aliyotembelea, Waziri
Muhongo alikutana na watendaji
kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya
Wizara ya Nishati na Madini hususan
zinazojishughulisha na masuala ya
nishati ya umeme.
Baada ya tathmini ya uzalishaji
umeme, Profesa Muhongo amesema

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara


baada ya kuapishwa alifika Makao Makuu ya Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na kuzungumza na Menejimenti ya Shirika hilo. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
unahitajika uwekezaji mkubwa katika kwamba wawekezaji wanakaribishwa
uzalishaji umeme ili kuwa na umeme katika uzalishaji umeme kwa kutumia
mwingi na wa uhakika na hivyo kueleza vyanzo mbalimbali.

Fomu za kuomba huduma ya umeme ziwepo


kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa- REA
Na Zuena Msuya Singida.

kupata fomu hizo kwa urahisi na


kupunguza malalamiko, alisema
Dkt. Mwakahesya.
Vilevile
Mkurugenzi
huyo,
aliwataka wananchi waishio katika
vijiji ambavyo viko katika miradi
ya REA kuchangamkia fursa hiyo
kwa kuwa huduma hiyo ya umeme
hutolewa kwa bei nafuu tofauti na
kuunganishiwa huduma hiyo moja

kwa moja na TANESCO.


Katika hatua nyingine, Dkt.
Mwakahesya
aliwaasa
vijana,
kutumia nishati ya umeme kwa
kujipatia kipato kwa kujiajiri kwa
kufanya kazi zinazotumia nishati
hiyo kama vile kuchomelea vifaa vya
chuma, kuuza vinywaji baridi na hata
shughuli za muziki ili kupunguza
uhalifu na vilevile kuepuka kujiingiza

kurugenzi Mkuu wa
Wakala wa Nishati Vijijini
(REA), Dkt. Lutengano
Mwakahesya ameshauri
kuwa fomu za kuomba huduma ya
kuunganishiwa umeme ziwekwe
katika ofisi za Serikali za Mitaa ili
kuwaondolea adha ya kutembea
umbali mrefu wananchi kufuata fomu
hizo.
Ushauri huo aliutoa hivi karibuni
Mkoani Singida kwenye ziara yake
ya kukagua miradi ya Umeme Vijijini
inayotekelezwa na wakala huo na
kusimamiwa na Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO).
Dkt. Mwakahesya alisema kuwa
hatua hiyo itahamasisha wananchi
kujiunga na huduma ya umeme
wa REA kwa kuwa itawaondolea
usumbufu wa kutembea umbali mrefu
kufuata fomu hizo katika ofisi za
TANESCO ambazo alisema nyingine
zipo maeneo ambayo inamlazimu
mwananchi kutumia gharama kubwa
hadi kufika eneo husika.
Fomu hizi ni bei ndogo, ni shilingi
elfu sita tu; lakini unakuta mwananchi
anatumia zaidi ya fedha hiyo kwa
ajili ya nauli kufuata fomu; sasa
TANESCO iangalie namna ambavyo Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
itaweza
kuwasaidia
wananchi Dkt. Lutengano Mwakahesya

katika makundi mabaya ya mitaani.


Eneo ambalo umeme umefika
maendeleo huwa makubwa sana kila
mmoja hujitahidi kuutumia ili kubadili
maisha yake na hata wale wasiokuwa
nao pia wananufaika kwa kupata
huduma za haraka zinazotumia
umeme kama kusaga nafaka; vijana
wamekuwa wabunifu wakubwa
katika matumizi ya umeme sasa ni
vyema wale waliojiunga na huduma
hiyo watoe ushauri kwa wengine ili
kukuza ajira za vijana, alisema.
Dkt. Mwakahesya aliongeza kuwa
sera ya Taifa inaeleza kuwa kufikia
mwaka 2025, Tanzania itakuwa katika
uchumi wa kati kutokana na kuwepo
kwa umeme wa uhakika kutoka katika
vyanzo mbali vya umeme na hivyo
kila Mtanzania ajitahidi kuendana
na kasi ya sera hiyo ili kuharakisha
Maendeleo ya Taifa.
Katikaziarahiyo,Dk.Mwakahesya
aliambatana na Mkurugenzi wa
Ufundi wa REA, Mhandisi Bengiel
Msofe pamoja na Afisa Mahusiano
wa wakala huo, Jaina Msuya ambapo
walitembelea miradi mbalimbali ya
REA katika mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha, Singida, na Manyara ambapo
wakandarasi wanaotekeleza miradi
hiyo wametakiwa kukamilisha kama
walivyokubaliana.

9
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TAN

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

NDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC)

SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI


TANZANIA (TPDC)
TAARIFA KWA UMMA

ZOEZI LA UHAKIKI KWA AJILI YA KULIPA FIDIA KWA WALIOKUWA


TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA

WAKAZI KATIKA MAENEO YA MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA


NATURAL GAS
- LNG)LA
MKOANI
LINDI
A AJILI YA KULIPA FIDIA(LIQUEFIED
KWA WALIOKUWA
ZOEZI
UHAKIKI
KWA AJILI YA KULIPA FIDI

EO YA MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKAWAKAZI KATIKA MAENEO YA MRADI WA KUCHA


Shirika la ASILIA
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) zitokanazo na mradi huu ili kuweza kujiandaa na Nia na mategemeo ya Serikali
ni kuhakikisha
kila
GESI
GESI
ASILIA
linatoa taarifa kwa umma juu ya zoezi linaloendelea fursa na changamoto zinazoambatana na mradi.
mkazi anapata haki yake kwa wakati na kama
NATURAL
GAS
- LNG)
MKOANI
LINDI
(LIQUEFIED
NATURAL GAS - LNG) MK
la uhakiki
kwa ajili
ya kulipa fidia
kwa waliokuwa
Pamoja na elimu hiyo Viongozi wa Mkoa
wa anavyostahili kisheria.

wakazi katika maeneo ya Kiwanja Na. 1 Kitalu A Lindi walitaarifiwa uwepo wa wataalamu kutoka
Likongo, Manispaa ya Lindi. Itakumbukwa kwamba Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Wizara ya Nishati na Serikali kupitia TPDC inatoa wito kwa wananchi
oli Tanzania
(TPDC)
linatoa
taarifa
Shirika
ya
la na
Maendeleo
ya Petroli
(TPDC)
mwezi Desemba
mwaka 2015
TPDC ilitoa
taarifa ya kwa
Madini,umma
Wizara yajuu
Ardhi,
Nyumba
Maendeleo kujiepusha
na ununuziTanzania
wa maeneo ya kiwanja
Na.1- linatoa
kupata hati miliki ya ardhi tajwa kwa ajili ya mradi ya Makazi na TPDC ambao wanaendesha zoezi la Kitalu A Likongo, Manispaa ya Lindi kwani eneo
kwa ajili
ya ya
kulipa
fidia
waliokuwa
zoezi
katika
linaloendelea
uhakikikwakwa
ya kulipa
huu. Baada
kupata hati
miliki,kwa
sheria inaelekeza
uhakikiwakazi
wakishirikiana
na wataalam
wa ardhi kutoka la
hili limetengwa
miradi ajili
yenye manufaa
kwa Taifafidia kw
mmiliki kuwalipa wahusika fidia kulingana na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
na hivyo kujigawia au kuvamia itakuwa ni kinyume
Kitalu tathmini
A Likongo,
Manispaa
ya wa
Lindi. Itakumbukwa
maeneo ya KiwanjachaNa.
1nchi.
Kitalu
A Likongo,
itakayofanywa na
Mtathmini Mkuu
sheria za
Ni vema ikaeleweka
kuwa hakuna Manisp
Serikali.
Zoezi hili la uhakiki linategemea kumalizika tarehe malipo yeyote yatakayofanyika kwa mtu yeyote
30 Januari
2016.
Nia
ni ya
kujiridhisha
na idadi Desemba
ya atakayethibitika
kuvamia eneo
hili kwa
minajiliilitoa
ya
waka 2015 TPDC ilitoa taarifa ya kupata
hati
miliki
kwamba
mwezi
mwaka
2015
TPDC
taar
Tarehe 19 Januari 2016, TPDC ilifanya kikao kazi kaya ambazo zitaathirika na mradi huu pamoja na kujipatia kipato.
na uongozi
wa ya
Serikali
ya Mkoa wa
Lindi.
Kikao mazao,
ili walipwe
fidia na kuhamishiwa
sehemu
di huu.
Baada
kupata
hati
miliki,
sheria
inaelekeza
ardhi
tajwa kwa
ajili ya mradiImetolewa
huu. na;
Baada ya kupata h
hiki kilihusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa nyingine (resettlement). Ikumbukwe kuwa tayari
Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa tathimini ilishafanywa na Wizara ya Ardhi, Nyumba
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji,
dia kulingana
na tathmini
na Mtathmini
mmiliki
kuwalipa
kulingana
na tathmini it
Lindi na wawakilishi
wa kampuni itakayofanywa
za kimataifa za na Maendeleo
ya Makazi
hapo awali
hivyo uhakikiwahusika
Shirika lafidia
Maendeleo
ya Petroli Tanzania,
mafuta na gesi (IOCs) ambazo ni wabia na TPDC unaofanyika sasa ni kwa kuzingatia ripoti ya tathmini
P.O.Box 2774,
Mkuu
Serikali.
katika mradi wa LNG. Lengo kuu la kikao kazi hicho hiyo ya mwanzo. Ulipaji
wa wa
fidia utafanyika
kwa
Dar-es-Salaam.
ilikua ni kutoa elimu juu ya mradi wa LNG na faida mujibu wa sheria za nchi.
Tanzania.

C ilifanya kikao kazi na uongozi wa Serikali ya Mkoa


Tarehe
wa 19 Januari 2016, TPDC ilifanya kikao kazi na uong

Maonesho ya 5 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha


yenye aina mbalimbali za vito zikiwemo
a Lindi na wawakilishi wa kampuni za kimataifa
wa za
Halmashauri
mkoa
wa Lindi
na wawakilishi wa
Tanzanite, za
Ruby,
Sapphire,
Tsavorite,
Rhodolite,
Spessartite,
zo ni wabia na TPDC katika mradi wa LNG. Lengo
mafuta
kuu na
gesi (IOCs)
ambazoTourmaline,
ni wabia na TPDC katika
Chrysoberyl na Almasi yanatarajiwa kuvutia

tibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi


Lindi. Kikao hiki kilihusisha Katibu Tawala wa Mkoa, Waku

toa elimu juu ya mradi wa LNG na faida zitokanazo


la kikao
na kazi hicho ilikua ni kutoa elimu juu ya mradi wa

100 za wafanyabiashara
a na fursa na changamoto zinazoambatana na mradi.
mradiZaidi
huu ya
ili kampuni
kuweza kujiandaa
na fursa na na
changamoto z
wachimbaji madini ya Vito kutoka Tanzania na
nchi zingine za Afrika Mashariki, Kati na Kusini;

ngozi wa Mkoa wa Lindi walitaarifiwa uwepo


Pamoja
wa
na elimu hiyo Viongozi wa Mkoa wa Lindi

is, TAKUKURU, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara


wataalamu
ya
kutoka Ofisi ya Rais, TAKUKURU, Wizara ya N

na
ya wanunuzi
500 kutokayazaidi
ya nchi
o ya Makazi na TPDC ambao wanaendesha zoezi
Ardhi,
la zaidi
Nyumba
na Maendeleo
Makazi
na25TPDC am
ulimwenguni

aalam wa ardhi kutoka Halmashauri ya Manispaa


uhakiki
ya wakishirikiana na wataalam wa ardhi kutoka Ha
Lindi.

Jisajili na Ushiriki Sasa!!!


Wasiliana na: Kamati ya Maandalizi AGF
Simu: +255 784352299 or +255 767106773
Barua pepe: info@arushagemshow.com
:ama Ofisi za Madini za Kanda

Yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini


kwa kushirikiana na
Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA)