You are on page 1of 15

HABARI

HabariZA
za
NISHATI
nishati&MADINI
&madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Toleo
No.138
51
Toleo No.

Limesambazwa
kwa Taasisi
naTaasisi
Idarana
zote
MEM
, 2015 23 - 29, 2016
Limesambazwa
kwa
Idara
zote MEM Tarehe - 23-29 JanuariSeptemba

Wabunge

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO -Uk2

WAZIRI MUHONGO
AAGIZA UTAFITI WA
KINA TETEMEKO
Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA
KAGERA
Somahabari Uk.2
UK
2

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini, anayeshughulikia
Madini Stephen Masele

Naibu Waziri wa Nishati na


Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,


Mhandisi Felchesmi
Mramba

Mkurugenzi Mkuu wa
REA, Dk. Lutengano
Mwakahesya

GESI YAPUNGUZA GHARAMA YA UZALISHAJI UMEME


JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4

>>>
UK. 4

Ofisi ya M awasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali


kwa ajili ya News Bullettin hii ya Wizar a ya Nishati na Madini
Ofisi ya Mawasiliano Serik alini inapokea habari za matukio mbalimbali
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
kwa
ajili ya News Bullettin
Jarida laGhorofa
Wizarya
a Tano
ya Nishati
au Fika hii
Ofisina
ya Mawasiliano
(MEM) na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22 2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263
au Fika Ofisi ya Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: badra77@yahoo.com

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

WAZIRI MUHONGO AAGIZA UTAFITI


WA KINA TETEMEKO KAGERA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akielezea


jambo wakati wa kikao na wataalam wanaofanya utafiti wa
tetemeko Mkoani Kagera (hawapo pichani).

Na Mohamed Saif

ataalam kutoka
Wakala wa
Jiolojia Tanzania
(GST) na Chuo
Kikuu cha Dar es
Salaam, wanaofanya utafiti baada
ya tetemeko la ardhi kutokea tarehe
10 Septemba, mwaka huu mkoani
Kagera, wametakiwa kuhakikisha
kuwa wanafanya utafiti wa kina ili
kubaini namna ambavyo miamba
ya maeneo husika ilivyo baada yab
Tetemeko, vilevile kuandaa ramani
mpya ya miamba katika maeneo
yatakayofanyiwa utafiti.
Agizo hilo limetolewa na Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alipofanya ziara

mkoani humo kwa lengo la kukagua


shughuli za utafiti wa tetemeko
zinazoendelea katika maeneo
mbalimbali mkoani humo.
Alisema kuwa, utafiti huo
utachukua muda mrefu kwani
hautafanyika mkoani Kagera pekee
bali utafanyika pia katika Mikoa ya
Geita, Mwanza, Shinyanga, Tabora,
Dodoma na baadaye nchi nzima.
Katika ziara hiyo, Waziri
Muhongo aliwaagiza wataalam hao
kuhakikisha wanatoa mafunzo ya
awali kwa umma hususan kwenye
maeneo yaliyoathiriwa zaidi na
tetemeko ili waelewe nini wanapaswa
kufanya endapo tetemeko litatokea.
Aliagiza elimu hiyo ianze
kutolewa siku ya Jumamosi, tarehe
24/9/2016 Saa 4 Asubuhi, huku

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa


Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza
jambo alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Kagera ili kujadiliana kuhusiana na
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja
Jenerali Mstaafu Salim Kijuu

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia)


akikagua eneo lililokumbwa na Tetemeko na kusababisha mpasuko
kwenye ardhi katika kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro ndani ya
Kitongoji cha Bilongo.
wakiandaa ratiba ya mafunzo hayo
kwa maeneo mengine na kuandaa
vipeperushi vyenye maelezo ya
kutosha kuhusu Tetemeko la
Ardhi kwa ajili ya kuwasambazia
wananchi.
Aidha, Profesa Muhongo
aliwaagiza wataalam hao, kuepuka
kutoa kauli zinazokinzana ili
kuepusha kuwachanganya
na kuwaletea hofu wananchi
waliokumbwa na kadhia hiyo na
kueleza kuwa Msemaji Mkuu wa
wataalam hao wanaofanya utafiti
husika ni Mtendaji Mkuu wa
GST, ambaye yupo mkoani humo
akishirikiana na wataalam kufanya
utafiti.
Mbali na hilo, Profesa Muhongo
aliagiza kuwa, ujengwe mnara
maalum katika eneo ambalo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter


Muhongo (wa pili Kulia) akizungumza wakati
wa ziara ya kukagua shughuli za utafiti wa
tetemeko zinazofanywa na timu ya wataalam
kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto
kwake ni Mtendaji Mkuu wa GST, Profesa
Abdulkarim Mruma ambaye ni kiongozi wa
timu ya wataalamu hao.

tetemeko hilo lilianzia katika kijiji cha


Kigazi, Kata ya Minziro, kilomita
88 kutoka Bukoba mjini ili iwe
kumbukumbu ya baadaye.
Eneo hili mliwekee alama,
muandike siku na muda ambao
tetemeko lilitokea, aliagiza Profesa
Muhongo.
Katika ziara hiyo, Waziri
Muhongo pia alikagua
miundombinu ya Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) ambayo
iliathiriwa na tetemeko la ardhi,
ili kubaini hatua zinazopaswa
kuchukuliwa kwa lengo la kuiboresha
na baadaye atakutana na Kamati
ya Maafa ili kuweka mikakati ya
kusimamia Shughuli za maafa na
namna bora ya kuwaeleza wananchi
jinsi ya kujihami kabla na baada ya
Tetemeko.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia


Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma
ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalam
wanaofanya utafiti wa tetemeko mkoani
Kagera akionesha kitovu cha tetemeko hilo
katika kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro
kilomita 88 kutoka Bukoba mjini kupitia
barabara ya Bukoba-Kyaka-Minziro.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

TAHARIRI

Septemba 23 - 29, 2016

SEMINA JOGMEC,
GST NA MEM

Poleni Watanzania
kwa Tetemeko la
Ardhi

Mnamo tarehe 10 Septemba, 2016, lilitokea tukio la


Tetemeko la Ardhi katika Mkoa wa Kagera ambapo
kwa mujibu wa taarifa ya Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), nguvu za mtetemo ni 5.7 kwa kutumia kipimo
cha Ritcher, ukubwa ambao umetajwa kuwa ni wa
juu sana.
Aidha, kutokana na tukio hilo, maeneo mengi
ya Mkoa wa Kagera ikijumuisha mji wa Bukoba
yamepatwa na madhara yakiwemo ya vifo, majeruhi,
nyumba kupasuka na nyingine kuanguka.
Kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya utafiti ya
GST, imeelezwa kuwa, chanzo cha tetemeko hilo ni
msigano wa mapande miamba katika uelekeo wa
Kaskazini kusini uliosababisha kuteleza kwa pande la
miamba kuelekea ulalo wa Mashariki.
Vilevile, baada ya tukio hilo kutokea, GST wametoa
taarifa mbalimbali kuhusu tukio hilo na kueleza kuwa,
tayari timu ya Wataalam ipo mkoani humo kwa
shughuli za Kitaalam ambazo zinahusiana na tukio
husika.
Miongoni mwa Wataalam hao ni pamoja na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
Profesa Justin Ntalikwa ambaye alipata wasaa wa
kutoa elimu ya namna ya kujikinga kwa wahanga wa
tukio hilo.
Miongoni mwa njia ambazo Prof. Ntalikwa
aliziainisha ni pamoja na kukaa maeneo ya wazi
wakati tukio kama hilo linapotokea, kuingia chini
ya uvungu au chini ya meza ambazo zipo imara na
kukaa katika kona za nyumba.
Aidha, pamoja na elimu iliyotolewa, Wakala huo
umeleeza kuwa, utaendelea kutoa taarifa zaidi juu ya
tukio hilo kulingana na matokeo ya tafiti zinazoendelea
kufanywa na wataalam hao kupitia vituo vya kupima
mitetemo vilivyopo maeneo mbalimbali nchini na
hususan kupitia Kituo cha Geita ambacho kipo jirani
na Mkoa wa Kagera.
Kutokana na tukio hilo, Wizara ya Nishati na
Madini inawapa pole wananchi wote walioathirika
na tukio hilo ambalo Wataalam wanaainisha kuwa ni
miongoni mwa majanga ya asili.
Aidha, Wizara inawasihi wananchi wote kuzingatia
elimu inayoendelea kutolewa kuhusu namna ya
kujikinga pindi matukio kama hayo yanapotokea.

Wadau mbalimbali waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Shirika la Umma


kutoka Japan linalojishughulisha na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC),
Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan,Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), pamoja na Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dar
es Salaam iliyolenga katika uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini nchini

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya


Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini, Profesa James Mdoe
akifungua Semina hiyo.

Meneja wa Maktaba na
Kumbukumbu za Jiolojia kutoka
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST),
Masota Magigita, akizungumza
kuhusu rasilimali madini nchini
wakati wa Semina hiyo.

KWA HABARI PIGA SIMU


kitengo cha mawasiliano

TEL-2110490
FAX-2110389
MOB-0732999263
Bodi ya uhariri
Msanifu: Lucas Gordon
Waandishi: Veronica Simba, Asteria Muhozya, Greyson
Mwase, Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James ,
Nuru Mwasampeta na Zuena Msuya

Five
Pillars of
Reforms
increase efficiency
Quality delivery
of goods/service
satisfAction of
the client
satisfaction of
business partners
satisfAction of
shareholders

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

GESI YAPUNGUZA GHARAMA


YA UZALISHAJI UMEME

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani


(mbele) akielezea juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za
upatikanaji wa nishati ya umeme nchini. Wengine katika picha ni
ujumbe kutoka Benki ya Dunia pamoja na Viongozi Waandamizi
kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake.

Na Rhoda James

meelezwa kuwa uzalishaji


wa umeme kwa kutumia gesi
asilia na maji umechangia
kwa kiasi kikubwa kupunguza
gharama ya uzalishaji wa
umeme nchini.
Hayo yameelezwa hivi karibuni
jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini, Dkt. Medard
Kalemani wakati wa kikao chake
na Ujumbe wa Benki ya Dunia na
baadhi ya watendaji wa Wizara na
Taasisi zake.
Akijibu baadhi ya maswali
yaliyoulizwa na Ujumbe huo, Dkt.
Kalemani alisema kuwa Serikali
imepunguza gharama ya uzalishaji
wa umeme baada ya ujenzi wa
mitambo ya kuzalisha umeme
kwa kutumia gesi asilia katika
sehemu mbalimbali nchini na hiyo
imepeleakea gharama za umeme
kushuka akitolea mfano kuwa, hapo
awali uniti moja ya umeme ilikuwa
ikinunuliwa kwa shilingi 298 kwa
wateja wa P1 lakini sasa ni shilingi
292.4.
Aliongeza kuwa hivi sasa
uwezo wa mitambo ya kuzalisha
umeme nchini umeongezeka hadi
MW 1,357.6 ambapo MW 607
zinatokana na gesi asilia, MW
566.7 unatokana na nguvu ya
maji na MW 183.9 ni mafuta na
tungamotaka.

Dkt. Kalemani aliieleza Benki


ya Dunia kuwa Serikali imekuwa
ikisimamia utekelezaji wa majikumu
ya TANESCO, kufuatilia madeni na
malipo yanayohusu Shirika hilo na
kudhamini TANESCO wakati wa
uombaji wa mikopo.
Aidha, kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa
TANESCO, Mhandisi Felchesmi
Mramba aliieleza Benki ya Dunia
kuwa hivi sasa huduma zinazidi
kuboreshwa kutokana na ukuaji wa
mahitaji ya umeme na kuongeza
kuwa Watanzania waliofikiwa
na huduma hiyo wameongezeka
kutoka asilimia 36 hadi asilimia 40.
Mhandisi Mramba aliongeza
kuwa, ongezeko hilo limechangiwa
na uboreshaji na ukarabati wa
miundombinu ya umeme , ujenzi
wa mitambo ya gesi asilia, udhibiti
wa wizi wa umeme na kuongeza
kuwa bado Serikali inaendelea
kuboresha huduma hiyo.
Dkt. Kalemani aliishukuru
Benki ya Dunia kwa niaba ya
Serikali kwa mchango mkubwa
inayotoa hususan upande wa
nishati ya umeme na kuahidi kuwa,
TANESCO itaendelea kuboresha
huduma zake kwa wananchi na
kueleza kuwa gharama za uzalishaji
wa umeme zinaendelea kushuka
zaidi ili kila Mtanzania aweze
kufikiwa na huduma hiyo kwa
wakati na kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird na Ujumbe


kutoka Benki ya Dunia wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na
Madini Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kikao hicho
kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara hivi karibuni jijini Dar es
Salaam.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James


Mdoe (kushoto) akimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati walipokutana na
Ujumbe wa Benki ya Dunia hivi karibuni.Wengine katika picha ni
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (wa pili kushoto), Kamishna wa Nishati, James Andilile
(wa tatu), Kamishna Msaidizi wa Umeme, Innocent Luoga (wa nne),
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
Mhandisi Felchesmi Mramba (wa tano) na Kaimu Mkurugenzi wa
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ,Boniface Gissima Nyamohanga.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

Tanzania yaahidi mazingira mazuri


uwekezaji Sekta ya Madini
Teresia Mhagama na
Devota Myombe

anzania imeahidi kuendelea


kuboresha mazingira
ya uwekezaji katika
Sekta ya Madini kama
ilivyoainishwa katika Sera
ya Madini ya mwaka 2009.
Hayo yameelezwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Profesa James Mdoe
wakati wa Semina iliyoandaliwa
na Shirika la Umma kutoka Japan
linalojishughulisha na Mafuta, Gesi
na Metali (JOGMEC), Wizara ya
Uchumi, Biashara na Viwanda ya
Japan, Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), pamoja na Wizara ya Nishati
na Madini iliyofanyika jijini Dar
es Salaam. Semina ililenga kujadili
uendelezaji endelevu wa rasilimali
madini nchini.
Alisema kuwa, Dira ya Maendeleo
ya Mwaka 2025 imelenga katika

kuanzisha migodi mikubwa, ya kati


na midogo inayoendeshwa kwa
kuzingatia usalama na utunzaji wa
mazingira hivyo mazingira mazuri
ya uwekezaji yatavutia wawekezaji
wa ndani na nje ya nchi kuwekeza ili
kuendeleza Sekta ya Madini nchini.
Profesa Mdoe alisema kuwa
semina hiyo ililenga kupata taarifa
zilizohuishwa kutoka Japan na
Tanzania kuhusu shughuli za utafiti
na utunzaji wa mazingira katika Sekta
ya Madini nchini na kujadiliana juu
ya kuendeleza ushirikiano kati ya nchi
husika.
Semina hii ni muhimu kwani
Taasisi hizi zitajadiliana kuhusu
kuendeleza ushirikiano katika sekta
hii, kufahamu fursa za uwekezaji
kwenye Sekta ya Madini kwani wadau
kutoka Tanzania na Japan wataweza
kupata taarifa za utafiti kuhusu madini
yaliyopo nchini na pia Taasisi ya
JOGMEC itapata fursa ya kueleza
shughuli zake barani Afrika, alisema
Profesa Mdoe.

Meneja wa Kanzidata na Uchakataji


wa Taarifa za Jiolojia kutoka Wakala
wa Jiolojia (GST),Terence Ngole
akizungumza wakati wa Semina
iliyoandaliwa na Shirika la Umma
kutoka Japan linalojishughulisha na
Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC),
Wizara ya Uchumi, Biashara na
Viwanda ya Japan,Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), pamoja na Wizara
ya Nishati na Madini iliyofanyika
jijini Dar es Salaam iliyolenga katika
uendelezaji Endelevu wa Rasilimali
Madini nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia


Madini, Profesa James Mdoe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (Wa pili kutoka kulia),
Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje (Wa kwanza
kushoto),Watendaji kutoka Serikali ya Japan na JOGMEC wakati wa
semina iliyolenga katika uendelezaji endelevu wa rasilimali madini
nchini.

Akieleza kuhusu Sekta ya Madini


nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa
Sekta hiyo kwa sasa inachangia asilimia
3.5 katika Pato la Taifa na kueleza
kuwa asilimia hiyo bado ni ndogo
kwani lengo la Serikali ni kuona kuwa
Sekta hiyo inachangia mpaka asilimia
10 kufikia mwaka 2025.
Hata hivyo Profesa Mdoe alisema
kuwa ili sekta hiyo ichangie ipasavyo
katika Uchumi wa Taifa, itategemea
kutokushuka kwa bei ya bidhaa
zinazotokana na rasilimali madini na
uchumi wa Dunia kuendelea kukua
ili kampuni zinazojishughulisha na
utafiti na uchimbaji wa madini zipate
fedha kutoka Taasisi za kifedha duniani
ili kuanzisha shughuli za utafiti na
uchimbaji wa madini.
Aidha, Profesa Mdoe aliwaalika
wawekezaji kujenga vituo
vitakavyotumika katika shughuli za
uongezaji thamani madini nchini
kwani alisema kuwa uongezaji
thamani madini ndani ya nchi utasaidia
kuongeza ajira kwa wananchi,

ubadilishanaji wa teknolojia kutoka


nchi zilizobobea katika shughuli hizo
na kuwezesha ukusanyaji wa kodi
ambayo itasaidia katika shughuli
nyingine za maendeleo.
Awali Meneja wa Kanzidata
na Uchakataji wa Taarifa za Jiolojia
kutoka GST, Terence Ngole, alieleza
kuwa JOGMEC na GST walisaini
Mkataba wa Makubaliano mwaka
2010 ambapo ushirikiano kati ya
Taasisi hizo umesaidia kuongeza
utaalam na teknolojia katika utafiti wa
madini kupitia mafunzo mbalimbali ya
muda mrefu na mfupi yanayotolewa na
Shirika la JOGMEC.
Alisema kuwa, Semina hiyo
imeshirikisha wadau mbalimbali
kutoka Japan na Tanzania ambao
wanajishughulisha na Sekta ya Madini
na Mazingira na kwamba ni semina ya
kwanza kuendeshwa nchini na Shirika
la JOGMEC.

Kaimu Kamishna wa Madini,


Mhandisi Ally Samaje akieleza
jitihada za Serikali katika
kuendeleza Sekta ya Madini nchini
wakati wa Semina iliyoandaliwa
na Shirika la Umma kutoka Japan
linalojishughulisha na Mafuta, Gesi
na Metali (JOGMEC),Wizara ya
Uchumi, Biashara na Viwanda ya
Japan,Wakala wa Jiolojia Tanzania
(GST), pamoja na Wizara ya Nishati
na Madini iliyofanyika jijini Dar es
Salaam iliyolenga katika uendelezaji
Endelevu wa Rasilimali Madini nchini.

Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (wa pili kulia) akimsikiliza


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia
Madini, Profesa James Mdoe (hayupo pichani) akifungua Semina
iliyoandaliwa na Shirika la Umma kutoka Japan linalojishughulisha
na Mafuta, Gesi na Metali (JOGMEC),Wizara ya Uchumi, Biashara
na Viwanda ya Japan,Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), pamoja na
Wizara ya Nishati na Madini iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliyolenga
katika uendelezaji Endelevu wa Rasilimali Madini nchini.

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

Ujenzi wa Nyumba Kagera uzingatie


ushauri wa Wataalam- Profesa Muhongo
Na Mohamed Saif
Kagera

ananchi
waliokumbwa
na tetemeko la
ardhi mkoani
Kagera na nyumba
zao kuathiriwa, wameshauriwa
kutokuanza ujenzi wa nyumba
hizo hadi hapo wataalam
watakapotembelea maeneo yao na
kuwapatia ushauri kuhusu ujenzi
husika.
Wito huo umetolewa na Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo wakati alipofanya

ziara mkoani humo ili kukagua


shughuli za utafiti wa tetemeko
zinazoendelea kufanywa na
wataalam kutoka Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST) kwa kushirikiana na
wataalam kutoka Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Waziri
Muhongo alizungumza na wananchi
ambao walitaka kufahamu kitaalam
kama wanaweza kuendelea kujenga
nyumba zao ambazo ziliathiriwa na
tetemeko hilo.
Nyumba zetu zimeathiriwa
na tetemeko na hatujaanza
kurekebisha; Je kitaalam tunaweza
kuziendeleza?,aliuliza mmoja wa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto)


akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Kigazi, John Kilibwa aliyeuliza
maswali kuhusiana na Tetemeko.

wananchi.
Akijibu swali hilo, Waziri
Muhongo aliwashauri wananchi hao
kuwa na subira ili wataalam wakague
Nyumba zao na kuwashauri kabla
ya kuendelea na hatua ya ujenzi na
wakati huohuo aliwaagiza wataalam
ambao wako mkoani humo kufanya
zoezi hilo haraka.
Ni vyema mkawa na subira
kabla hamjafanya kitu ili wataalam
wapite kufanya ukaguzi pamoja na
kuwapatia ushauri wa kitaalam,
alisema Profesa Muhongo.
Aidha, Waziri Muhongo
aliwataka wananchi hao kuepuka
kusikiliza kauli za watu wasiokuwa

wataalam kuhusu tetemeko hilo


na badala yake aliwaasa wananchi
hao kufuatilia ushauri wa wataalam
wanaoendelea na shughuli za utafiti
katika maeneo yaliyoathiriwa na
tetemeko la ardhi mkoani humo.
Kutokana na maswali mbalimbali
aliyokuwa akiulizwa na wananchi
katika maeneo aliyotembelea, Waziri
Muhongo alimuagiza Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim
Mruma kutoa namba yake ya simu
ili wananchi watakaokuwa na
maswali yoyote au endapo kutatokea
hali ambayo hawaielewi waweze
kuwasiliana naye.

Moja ya nyumba ambazo zimeathirika kutokana na Tetemeko la


ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Waziri wa
Nishati na
Madini, Profesa
Sospeter
Muhongo
(kushoto)
akijadiliana
jambo na
Mtendaji
Mkuu wa
Wakala
wa Jiolojia
Tanzania,
Profesa
Abdulkarim
Mruma wakati
wa ukaguzi
wa shughuli
za utafiti wa
Tetemeko la
ardhi, mkoani
Kagera.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

Sekta ya Nishati yafanya Mageuzi Makubwa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia


Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kulia mbele)
akisikiliza mada iliyokuwa ikitolewa na Balozi Mkazi wa Norway nchini,
Hanne-Marie Kaarstad (hayupo pichani) katika Semina iliyofanyika jijini
Dar es Salaam, iliyolenga kukutanisha Wadau mbalimbali wa Nishati ya
Umeme na Taasisi za nishati ya umeme Nchini Norway.

Na Rhoda James

aibu Katibu Mkuu


wa Wizara ya
Nishati na Madini
anayeshughulikia
Nishati, Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo amesema kuwa,
Serikali ya Tanzania imefanya
mageuzi makubwa katika Sekta ya
Nishati ikiwa ni moja ya mikakati ya
kupunguza umaskini kwa wananchi
nchini.
Dkt. Pallangyo aliyasema
hayo hivi karibuni katika Semina
iliyofanyika katika Hotel ya Serena
jijini Dar es Salaam, lengo likiwa

ni kukutanisha Taasisi za Norway


na Wadau wa Nishati ya Umeme
nchini.
Akifungua Semina hiyo, Dkt.
Pallangyo alisema kuwa, Semina
hiyo ni fursa kwa Wadau wa Nishati
kujifunza na kubadilishana uzoefu
kwa kuwa nchi ya Norway ni
miongoni mwa nchi kubwa Duniani
ambazo zinazalisha nishati ya
umeme kwa kutumia nguvu ya maji,
gesi na mafuta.
Serikali ya Norway ina uzoefu
mkubwa katika Sekta ya nishati ya
umeme inayozalishwa kwa nguvu ya
maji kwa kuwa hadi sasa nchi hiyo

Naibu Katibu Mkuu wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,


Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo akisoma hotuba katika Semina
iliyowakutanisha Wadau wa Nishati ya Umeme na Taasisi za Nishati
za nchini Norway.
inazalisha nishati hiyo kwa kutumia
nguvu ya maji kwa asilimia 95,
alisema Dkt. Pallangyo.
Aidha, Dkt. Pallangyo alisemna
kuwa, ushiriki wa Taasisi binafsi
katika kuzalisha nishati hiyo ni
muhimu kwa kuwa Serikali yenyewe
haiwezi kufanya kila kitu.
Kwa upande wake, Balozi Mkazi
wa Norway Nchini, Hanne-Marie
Kaarstad alieleza kuwa, ushirikiano
wa nchi hizo mbili ni wa muda mrefu
kutoka miaka ya 1900 na kwamba
ushirikiano huo ni wa kipekee.
Balozi Kaarstad alisema kuwa,
katika Semina hiyo kampuni zaidi

ya 80 na Wadau mbalimbali nchini


walishiriki mkutano huo huku
Kampuni 14 za Norway zikishiriki.
Taasisi zilizoshiriki katika
semina hiyo ni pamoja na
Kampuni ya Norwegian Investment
Fund for Developing Countries
(NORFUND), Jacobsen Elektro,
Statoils Renewable Energy, Rift
Valley Energy, Viking Heat Engines
na Rainpower Norway. Nyingine ni
Bergen Engines, Multiconsult, W.
Giertsen Energy, Eltek, Standard
Hydro Power, Norsk Vind Energi,
Green Resources, SN power na The
International Centre for Hydropower.

Kamishna Msaidizi wa
Nishati anayeshughulikia
Umeme, Mhandisi Innocent
Luoga (wa pili kutoka kulia)
akielezea Sera ya Nishati
ya Tanzania kwa wadau
mbalimbali walioshiriki
Semina hiyo.Wengine katika
picha ni Viongozi Waandamizi
kutoka Taasisi za Wizara ya
Nishati na Madini.

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

SMMRP yakabidhi jengo la Madini Tunduru


Na Zuena Msuya,
Tunduru, RUVUMA,

izara ya Nishati
na Madini,
kupitia Mradi
wa Usimamizi
Endelevu wa
Rasilimali Madini (SMMRP)
imepokea jengo la Ofisi ya Afisa
Madini Mkazi wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma kutoka kwa
kampuni ya ukandarasi ya Mkongo
Contractors ili kuanza kutumika
na ofisi hiyo baada ya kufanyiwa
ukarabati .
Akizungumza mara baada
ya kupokea jengo hilo wilayani
Tunduru hivi karibuni, Msanifu
Majengo kutoka SMMRP, Joseph
Ringo alisema kuwa lengo la
ukarabati huo ni kuimarisha
shughuli za kiutendaji katika
uendelezaji wa shughuli za madini
wilayani humo pamoja na viunga
vyake kutokana na wilaya hiyo
kujikita zaidi katika uchimbaji wa
madini ya vito ya aina mbalimbali.
Aidha, Ringo alifafanua kuwa,
kama ilivyo dhamira ya mradi wa
SMMRP, kufanyika kwa ukarabati
katika jengo hilo kutawezesha Afisa
Madini Mkazi wa eneo hilo kufanya
kazi zake kwa ufanisi na hivyo
kufikia malengo aliyojiwekea katika

kuwahudumia wadau wa madini


katika eneo husika.
Vilevile, alisema kuwa, ukarabati
wa jengo hilo umefadhiliwa
na Serikali ya Tanzania kwa
kushirikiana na Benki ya Dunia
ambao umejumuisha vifaa vya kisasa
ikiwemo kuunganishwa na mfumo
mpya na wa kisasa wa TEHAMA
ambao unarahisisha utunzaji wa
kumbukumbu za wadau wa madini
tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kwa upande wake, Ofisa Madini
mkazi Tunduru, Mhandisi Fredrick
Mwanjisi aliupongeza mradi wa
SMMRP kutokana na kuboresha
na kuzijengea uwezo ofisi za madini
nchini jambo ambalo litaboresha
shughuli za uendelezaji wa rasilimali
za madini.
Hata hivyo Mhandisi Mwanjisi
ameushauri mradi husika kutumia
muda mfupi katika kutekeleza
shughuli za ukarabati na ujenzi wa
majengo mbalimbali kwa lengo la
kuendeleza rasilimali madini.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi
Rasilimali Watu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Joyceline Lugora,
amewataka maafisa madini wakazi
na wa Kanda zote nchini kutunza
miundombinu ya majengo hayo
ili kuondoa gharama za ukarabati
wa mara kwa mara ikiwemo
kuhakikisha unafanyika ukarabati
endapo kunatokea uharibifu.

Mkurugenzi Msaidizi RasilimaliWatu wa Wizara ya Nishati na


Madini Joyceline Lugora (wa pili kushoto mbele) akikabidhi funguo
za jengo la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilayani Tunduru mkoani
Ruvuma kwa Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Nyasa,
Mhandisi Fredy Mahobe, (wa pili kulia mbele).

Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini,Wasanifu majengo


pamoja na Wakandarasi waliojenga jengo la ofisi ya Madini Mkazi
Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma katika picha ya pamoja mbele
ya jengo la Ofisi ya Madini Tunduru. Mstari wa mbele kutoka
kulia ni Msanifu majengo wa SMMRP, Joseph Ringo, Mkurugenzi
Msaidizi Rasilimali Watu, Joyceline Lugora, Mkuu wa Kitengo cha
Tehama Fransis Fungameza, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda
ya Ziwa Nyasa, Mhandisi Fredy Mahobe.
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wilayani
Tunduru mkoani Ruvuma, jengo hilo limejengwa na Mradi wa
Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) unaofadhiliwa
na Benki ya Dunia.
Msanifu Majengo wa
SMMRP , Joseph Ringo
akitia saini hati za
makabidhiano ya jengo la
Ofisi ya Afisa Madini Mkazi
Wilani Tunduru mkoani
Ruvuma, (kulia) huku
akishuhudiwa na Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda
ya Ziwa Nyasa, Mhandisi
Fred Mahobe (wa pili kulia)

Mkurugenzi wa Kampuni ya umeme ya Nyasa, Aleluya Samata


(aliyeshika wire) akitoa maelezo kwa Watendaji wa Wizara ya
Nishati na Madini,Wasanifu majengo pamoja na Wakandarasi
waliojenga jengo la ofisi ya madini Mkoa wa Ruvuma katika wilaya
ya Tunduru kuhusu namna ya jengo hilo litakavyotumia umeme wa
jenereta pindi umeme unapokatika.

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

TANZANIA GEOTHERMAL DEVELOPMENT COMPANY LIMITED


GEOTHERMAL DEVELOPMENT PROJECT

ENERGY SECTOR
(INDIVIDUAL CONSULTANT)
REQUEST FOR EXPRESSIONS OF INTEREST
FOR
PROVISION OF CONSULTANCY SERVICES FOR PREPARATION OF PROJECT
PROPOSAL DOCUMENT AND M&E SYSTEM MANUAL FOR THE PROJECT
Project ID No.: P-TZ-FA0-012
Bid No.:PA/131/2016-17/C/06
22ndSeptember, 2016
1. The United Republic of Tanzania has received
financing from the African Development Bank toward the
cost of the Geothermal Development Project, (Recommended
by the Investment Plan for Tanzania, April 21st 2013) and
intends to apply part of the agreed amount of this grant
for payments under the contract for Consultancy Services
for Preparation of Geothermal Energy Development Project
Proposal Document and M&E Manual for the Project.
2. The main objective of the consultancy services is
to provide technical support to the Government, through
the Ministry of Energy and Minerals and Tanzania
Geothermal Development Company Limited (TGDC) by
preparing a comprehensive project proposal document with
recommendations for addressing the high upfront risks in
the early stages/phases of geothermal development; and
propose a system for assessing the progress of performance
of the project.
3. The Tanzania Geothermal Development Company
Limited (TGDC)now invites eligible and qualified Individual
Consultants to indicate their interest in providing the
specified services. Interested consultants must provide
information indicating that they are qualified to perform the
services by submitting their academic qualification, reference
of similar assignments and experience in similar condition.

4. Expressions of Interest (EoI) in one (1) original plus


two (2)copies must be enclosed in a sealed envelope properly
addressed and delivered to the Secretary, TGDC Tender
Board, Mt. Meru Building, 2nd Floor, Mandela Road,
P.O.BOX 14801, Dar es salaam at or before10.00 hours
local time on Friday 07th October, 2016. The envelopes
containing the Expression of Interest shall be enclosed in
a single envelope and marked Expression of Interest for
Consultancy Services for Preparation of Geothermal Energy
Development Project Proposal Document and M&E Manual
for the Project.
5. The opening of Expression of Interest (EIO) shall take
place immediately after the deadline for submission, at the
address indicated under Para4 above. Applying individual
consultants are invited to attend the opening ceremony.
6. A consultant will be selected in accordance with the
procedures set out in the African Development Banks Rules
and Procedure for the Use of Consultants, which is available
on the Banks website at http://www.afdb.org. Borrowers
are under no obligation to shortlist any consultant who
expresses interest.
7. Any request for clarification with regards to this
Expression of Interest shall be addressed to the undersigned.
The client shall respond to clarifications received not less
than one (1) week before the deadline for submission.
8. Faxed, Emailed and late submitted expression of
interest shall not be accepted for evaluation irrespective of
the circumstance.

General Manager,
Tanzania Geothermal Development Company Limited,
Mt. Meru Building, 2nd Floor, Mandela Road,
P.O.Box 14801, Dar es Salaam,
Tel; +255 (0) 687 833 855
Emails; gm.tgdc@tanesco.co.tz; info.tgdc@tanesco.co.tz

10

Habari za nishati/madini

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

CURRENT TRENDS
By Raphael B.T. Mgaya

LNG VALUE CHAIN AND MARKETS-PART I


Introduction
Tanzania has embarked into the
initial processes for the development
of tens of billions of the US Dollars
liquefied natural gas (LNG) project.
LNG project will be the largest project
in terms of capital investment ever
undertaken in the history of our nation
and it will indeed remain so for the
quite some time. Upon its completion,
the LNG project will have significant
impact in the economy of our country
and the livelihood of the people.
Thousands of jobs will be created
as a result of the project and the
Government will earn more foreign
currency and revenues in general than
ever before. To put it in context, the
LNG project will cost more than 24
times the cost for the Songosongo/
Mtwara via Somanga Fungu to Dar
es Salaam Gas pipeline which I/is in
operation and 10 times the UgandaTanzania Crude Oil Pipeline currently
in the initial stages!.
The scale of this LNG project
necessitates that as a nation we must
muster our resources, both financial
and human and focus our energy and
thing and plan strategically to make
sure that everything is done right. For
this reason, the author considers it
prudent at this juncture to share this
information with the stakeholders
and the public at large so that to create
awareness that has never been so badly
needed.
LNG Fundamentals
Large quantities of natural gas
are located in countries where local
demand and/or market prices are low.
At the moment the lucrative markets
for LNG are in countries like Japan,
Korea, India, China and the Western
European countries. In most cases, the
need for LNG is driven by the growing
demand for electric power.
The distance between these
countries is substantial, which makes
delivery by pipelines too expensive.
The need to transport gas in distant
markets led to the development of
the liquefied natural gas (LNG)

technology in the 1960s which


involves cooling natural gas to
259F (-162C), the boiling point of
methane, liquefying the gas and in
the process reducing its volume by a
factor of about 625. LNG can then be
transported in specially designed and
insulated ships to a special purpose
receiving terminal in the market
country. At the market country, the
LNG is offloaded to insulated storage
tanks and then either transported by
special tanker trucks to regional storage
tanks or re-gasified and delivered via
pipelines.
The LNG value chain, from

liquefaction processes is the cooling


of the treated gas as it passes through
a series of heat exchangers that are
cooled by refrigerants. In principle,
the LNG Plant works like a giant
refrigerator.
There are a number of liquefaction
technologies available but the more
popular ones are the C3-MR and
the AP-X Processes offered by the
ConocoPhillips Optimized Cascade
System and Air Products.
The ConocoPhillips Optimized
Cascade System
The ConocoPhillips technology
was first used in the Alaska LNG
plant, built in 1969, and has been

Fig.1:The LNG value chain from supply to market


production to market, is a substantial
integrated undertaking because all
of its components must exist and be
aligned both legally and commercially
for a project to be viable. The
components are shown in Fig. 1.
LNG Industry Units
Liquid Quantities
LNG plant capacity is usually
specified in million metric tonnes per
year (mt/y or mtpa). A metric tonne is
equivalent to 1000 kg. The LNG ship
and storage tank capacity is usually
measured in cubic meters of liquid
(m3).
Liquefaction Technologies
The foundation of the various

re-engineered for larger capacity by


Bechtel in recent years and became
popular again. This technology has
been used in LNG plants in Trinidad,

Egypt, Equatorial Guinea, Angola,


Papua New Guinea and Australia.
The Atlantic LNG in Trinidad
installed a single Optimized Cascade
LNG train which began deliveries in
1999. Its capacity is 3.0 mtpa. It has
since added three more trains with
a combined capacity of 11.8 mtpa
bringing the total output to 14.8 mtpa.
Air Products Processes
Air Products has developed a
number of LNG technologies over
the years which have become the
most widely used in the industry. Its
more recent process for smaller plants,
referred to as the CH4 MCR process,
consists of two heat exchangers: a
propane pre-cooling heat exchanger,
that drops the temperature of the inlet
gas to the boiling point temperature
of propane; followed by the mixed
component refrigerant (MCR) heat
exchanger that drops the temperature
to that of LNG.
A typical LNG facility using
Air Products technology is the one
installed in Yemen that started up
in 2009. It has two trains with a
combined capacity of 6. 7 mt/y.
LNG Storage Tanks
LNG storage tanks come in
various sizes from 100,000-200,000
m3 of capacity. These tanks need to
be insulated to minimize heat transfer
from the atmosphere that will cause
the LNG to warm up and vaporize.
The tank size must be large enough
to fill large LNG ships during loading
>> CONT. PG. 13

Fig.2: LNG Storage Tanks

The author is an advocate of the Superior Courts in Tanzania and subordinate courts save the Primary Courts. He currently works as a
Senior Legal Officer for the Ministry of Energy and Minerals. He holds LLB (Hons.) (Dar); LLM (Intl law) (Warwick); LLM (Oil and Gas law)
(RGU Aberdeen); MBA (Mzumbe); CLE (Mississippi).
He can be reached through: raphael.mgaya@gmail.com
DISCLAIMER:
Views expressed herein are entirely authors views and should not be associated with his employer.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

11

By Eng.Gilay Shamika
Engineer & Gemologist TMAA
Email: gshamika@tmaa.go.tz
Phone: +255 762 715 762

Aquamarine Gemstone in Tanzania

Picture 1:
Cut and
Polished
Aquamarine

quamarine is a
member of the
beryl family and
ranges in color
from an almost
colorless pale blue to blue-green.
The most prized color is a deepblue aqua color and gets its name
from Latin words meaning water
(aqua) and sea (marine).
Aquamarine is the modern
March birthstone as adopted
by the American National
Association of Jewelers in 1912.
It is also suggested as a gem
to give on the 16th and 19th
wedding anniversaries. The most
valuable aquamarines come
from Brazil, but it is also mined
in Kenya, Nigeria, Madagascar,
Zambia, Tanzania, Sri Lanka,
Pakistan, Afghanistan and
Russia.

In Tanzania Aquamarine
ismostly available at Ruvuma:
Tunduruand Manyara: Mbulu
Geology
The process of forming
aquamarine is almost entirely
dependent on the presence of
two components: beryl and iron.
Beryl is largely comprised
of beryllium aluminum
cyclosilicate. In its purest form
it is clear. When iron is present,
beryl takes on a blue color, and
is then known as Aquamarine.
Beryl is primarily located
in deposits known as granitic
pegmatites, which are large
structures comprised of
interlocking minerals and
rocks. Granitic pegmatites
are especially high in granite
deposits.

Picture 2: Rough Aquamarine

When beryl deposits are


forming in the presence of iron
it is likely that the crystallization
process will result in aquamarine
gemstones. As the beryl crystals
form, iron is essentially trapped
insidefusing with them. If
little or no other impurities are
present these processes result in
aquamarine gems. When other
impurities are present the beryl
may form into emeralds.
Colour Ranges:
Aquamarine color ranges
from light blue to dark blue and
blue-green. If deep greenit is
called Emerald.

gem varieties, including Emerald,


Morganite and Heliodor.
Heat treatment:
Some gemstones are heated
to high temperatures to enhance
the color and/or clarity of a
stone. Aquamarines are often
heat treated to change light color
aquamarine to get the desired
dark blue aquamarine. This
results in a permanent color
change.
Aquamarine Confuse with:
Topaz, Kyanite, Tourmaline
and Zircon.

Varieties:
Aquamarine is the variety of
Beryl. Beryl also contains other

Gemological Properties of Aquamarine


Gem group
Refractive Index (RI)
Specific Gravity (SG)
Hardness (Mohs Scale)
Toughness
Stability to light

Unit of Measure
Beryl
DR 1.577 to 1.583
2.72
7.5 to 8.0
Medium
Unstable

Treatment and Grading of Aquamarine


Heating: To improve color or clarity appearance. Lattice
diffusion: This is a process of heating Aquamarine to very high
temperature in the presence of a coloring agent. The aim is either to
increase colour appearance, remove color or change to other colour.
Aquamarine Grading Explanation
A
Vivid Pure dark-blue or blue-green
Colour
B
Deep dark-blue or blue-green Colour
C
Deepdark-blue or blue-green colour
with windowand impurities
TraditionalGrading
Gem quality
A
Near Gem
B
Industrial/Low quality
C

Habari za nishati/madini

12
NewsBulletin
YALIYOJIRI MKUTANO WA WAZIRI MUHONGO
NA WAFANYAKAZI WA TANESCO MKOA WA
KAGERA, TAREHE 22 SEPEMBA, 2016
http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

Profesa Muhongo alisema kuwa Mradi wa Umeme


Vijijini Awamu ya Tatu (REA III), ni mradi mkubwa na wa
kipekee na kwamba lengo ni kuhakikisha ndani ya miaka
5 Vijiji vyote vya Tanzania vinapata huduma ya umeme.
Wakandarasi 8 waliokuwa wakisambaza umeme vijijini
katika miradi ya REA Awamu ya II, hawataruhusiwa
kufanya kazi kwenye REA III kwa kuwa walifanya vibaya
na hawakufikisha malengo kwenye REA II.
Bajeti ya usambazaji umeme vijijini Awamu ya Tatu
(REA III) ni zaidi ya shilingi Trilioni moja.

Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo
(kulia) akimsikiza
Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Jiolojia
Tanzania (GST),
Abdulkarim Mruma
(mwenye kipaza
sauti) wakati Pofesa
Muhongo alipokutana
na Wafanyakazi wa
Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO)
mkoani Kagera.Wa
kwanza kushoto
ni Meneja wa
TANESCO- kanda ya
Ziwa, Mhandisi Amos
Maganga, na wa pili
kushoto ni Meneja
wa TANESCO mkoa
wa Kagera Mhandisi
Francis Maze.
Ameagiza Bodi ya TANESCO kwa kushirikiana na
Menejimenti kuhakikisha inatatua suala la vibarua katika
Shirika hilo. Alisema haiwezekani mtu akawa kibarua kwa
zaidi ya miaka 5.

Kasi ya usambazaji Umeme nchini itaongezeka


maradufu.
Amewataka watumishi kujiepusha na vitendo vya
rushwa ikiwemo kuepuka mazingira yanayoweza
kusababisha kuwepo kwa rushwa.
Amewaagiza kuhakikisha matatizo na malalamiko ya
wateja yanashughulikiwa kwa wakati.
Ameliagiza Shirika hilo kufungua Ofisi vijijini hususan
kwenye maeneo yenye watumiaji wengi wa umeme ili
kuwaepushia usumbufu wananchi.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani


Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (hayupo pichani) wakati alipokuwa mkoani humo kukagua
athari za tetemeko la ardhi katika miundombinu ya umeme.
Tetemeko hilo lilitokea mkoani Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (kulia) akizungumza wakati alipokuwa
akikagua miundombinu ya umeme katika eneo la
Kyaka na Kibeta mkoani Kagera baada ya kutokea
tetemeko la ardhi mkoani humo tarehe 10 Septemba,
2016.Wengine katika picha ni Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Abdulkarim
Mruma (wa tatu kushoto), Meneja wa TANESCOkanda ya Ziwa, Mhandisi Amos Maganga ( wa pili
kushoto) na wa kwanza kushoto ni Meneja wa
TANESCO mkoa wa Kagera Mhandisi Francis Maze.

NewsBulletin

Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

MIRADI YA TEDAP, BACKBONE


YAONGEZA KIWANGO CHA UMEME

13

LNG VALUE
CHAIN AND
MARKETS >> FROM PG. 10
and to accommodate large on-shore LNG storage
tanks during offloading (Fig. 2).
LNG Ships

Kamishna Msaidizi wa Nishati


nayeshughulikia Umeme
Mhandisi, Innocent Luoga

LNG ships have been in existence for many


years but their carrying capacity has been
increased in recent years to accommodate the
larger train sizes. The standard ship carries
138,000 - 145,000 m3. In order to optimize the
sale of LNG to the long distance UK and Japan
markets for instance, companies like Nakilat
commissioned the construction of two larger size
vessels the Q-Flex with a capacity of 210,000
m3 and the larger Q-Max at 260,000 m3.
LNG ships have two major designs: the

Miundombinu ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 400 (Backbone)

Fig. 3: LNG Ship with Technigaz


Membrane technology

Fig. 3: LNG Ship with Technigaz


Membrane technology

Baadhi ya mitambo ya umeme katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme kilichopo mkoani
Singida. Kituo hiki ni moja ya vituo vilivyoboreshwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa
miundombinu ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga (Backbone)

Na mwandishi wetu

amishna Msaidizi wa Nishati


anayeshughulikia Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga
amesema kuwa utekelezaji wa
miradi ya umeme ya Tanzania
Energy Development Access Program (TEDAP)
na Miundombinu ya Kusafirisha Umeme ya
Msongo wa kV400 (Backbone) imewezesha
ongezeko la kiwango cha upatikanaji umeme
nchini.
Mhandisi Luoga aliyasema hayo Ofisini
kwake jijini Dar es Salaam wakati wa Mahojiano
Maalum na Kampuni ya Uandaaji vipindi
ya True Vision na kueleza kuwa, miradi hiyo

inayofadhiliwa na Benki ya Dunia na wadau


wengine wa maendeleo imewezesha ongezeko
la upatikanaji wa umeme huo kutoka asilimia 7
mwaka 2011, 36 mwaka 2014 hadi asilimia 58 ya
sasa.
Vilevile, amesema kuwa, miradi hiyo
inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali
nchini, itawezesha kuinua uchumi wa Tanzania
kutokana na umeme huo kutumika katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.
Serikali inajivunia matokeo hayo kupitia
miradi hiyo, kwanza imeongeza kiwango cha
upatikanaji umeme nchini na kutoa uhakika
wa kutekeleza mipango yetu ya baadaye ya
usambazaji umeme nchini, alisema Mhandisi
Luoga.

Technigaz Membrane technology shown in Fig.


3 and the Moss Spherical technology shown
in Fig.4. Each of these LNG containers must
accommodate the expansion and contraction
that occurs within the LNG containment system
when the temperature rises after the cargo is
unloaded at a receiving terminal and becomes
cold again as LNG is loaded at a supply port.
This requires specially design materials such as
invar, a nickel steel alloy that expands minimally
in the presence of temperature fluctuations.
Conclusion
LNG technology is important because
it makes possible the transportation of large
volumes of natural gas to distant markets which
would otherwise not be possible using the
conventional means of pipeline transportation.
For LNG project to be economically viable there
must be enough reserves to justify the investment
in the project. Our country is blessed to be one
of the countries in the world with natural gas
discoveries that make the development of LNG
project a reality within reach.

14

Habari za nishati/madini

Septemba 23 - 29, 2016

NewsBulletin
http://www.mem.go.tz

HABARI PICHA
Baadhi ya Watendaji
wa Wizara ya Nishati
na Madini na Taasisi
zake wakimsiliza
Meneja wa Kampuni ya
Kuzalisha Umeme wa
Jua ya JUSUNG kutoka
Korea Kusini, Justin Yi
alipokuwa akiwasilisha
mapendekezo yao
kuhusu kuwekeza
kwenye Nishatiya
Umeme. Kikao hicho
kilifanyika Makao
Makuu ya Wizara jijini
Dar es Salaam. Katikati
ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini
anayesimamia Nishati,
Dkt.Mhandisi Juliana
Pallangyo.
Makamu wa Rais wa
Kampuni ya Kuzalisha
Umeme Jua ya JUSUNG
kutoka Korea Kusini,
Yong-Woo Shin akisaini
kitabu cha Wageni
ofisini kwa Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini
anayesimamia Nishati,
Dkt.Mhandisi Juliana
Pallangyo. Pembeni yake
ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na
Madini anayesimamia
Nishati, Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo.

Naibu Katibu Mkuu


wa Wizara ya
Nishati na Madini,
Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo
(Katikati) akiwa
katika picha ya
pamoja na Makamu
wa Rais wa Kampuni
ya Kuzalisha
Umeme Jua ya
JUSUNG kutoka
Korea Kusini,YongWoo Shin (Kushoto)
pamoja na Meneja
wa Kampuni hiyo
Justin Yi (Kulia).

15
NewsBulletin
China yaonesha nia kuwekeza Mradi
wa Umeme Mchuchuma Makambako
Habari za nishati/madini

http://www.mem.go.tz

Septemba 23 - 29, 2016

Na Veronica Simba

hirika linalosimamia Gridi


ya Taifa nchini China,
kupitia Kampuni yake
tanzu ya umeme (China
Electric Power Equipment
and Technology Co., Ltd CET),
limeonesha nia ya kuwekeza kwenye
sekta ya nishati nchini, hususan
katika Mradi wa kusafirisha umeme
wa msongo wa kilovolti 400 kutoka
Mchuchuma hadi Makambako.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika
hilo, katika nchi za Tanzania na
Kenya, Dkt Zhang Xiang, aliyasema
hayo Septemba 22 mwaka huu,
alipokutana na uongozi wa Wizara
ya Nishati na Madini pamoja na
wataalam kutoka Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na Shirika la
Maendeleo la Taifa (NDC), katika
kikao kilichofanyika Makao Makuu
ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha mapendekezo ya
uwekezaji katika Mradi husika, Dkt
Xiang, aliyeambatana na Meneja
Miradi wa Shirika hilo, Zhu Debing,
alisema kuwa nchi ya China kupitia
Shirika lake, ina uwezo, utaalam na
uzoefu mkubwa katika uwekezaji
wa aina mbalimbali kwenye sekta
ya nishati; hivyo endapo Serikali
ya Tanzania itaridhia uwekezaji
husika, utatekelezwa kwa mafanikio
makubwa.
Dkt Xiang alitaja baadhi ya sifa
za CET ambazo zinaipa vigezo vya
kuwekeza katika sekta husika kuwa
ni pamoja na uzoefu wa kutekeleza
kwa ufanisi miradi mikubwa ya
nishati katika nchi mbalimbali duniani
zikiwemo Ethiopia, Misri, Brazili,
Uturuki, Pakistan, Myanmar, Urusi na
China.
Aidha, alisema kuwa CET
inatumia teknojia ya kisasa kabisa na

Viongozi na Wataalam waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa
mapendekezo ya uwekezaji katika Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 400 kutoka
Mchuchuma hadi Makambako, uliokuwa ukifanywa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Gridi la Taifa la
China, katika nchi za Tanzania na Kenya, Dkt Zhang Xiang, katika kikao kilichofanyika hivi karibuni, jijini
Dar es Salaam.
ya hali ya juu katika utekelezaji wa
miradi yake ambayo inajumuisha pia
utoaji wa mafunzo katika miradi ya
umeme ya aina zote.
Vilevile, Dkt Xiang aliongeza
kwamba, Kampuni ya CET inao
uwezo wa kutoa suluhisho la
uwezeshaji kifedha kufanikisha miradi
mbalimbali ya umeme.
Kwa upande wake, Kamishna
Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia
Umeme, kutoka Wizara ya Nishati
na Madini, Mhandisi Innocent Luoga
aliwaeleza wawakilishi hao kutoka
Shirika la Gridi la China kuwa, Serikali
ya Tanzania imedhamiria kwa dhati
kuboresha upatikanaji wa umeme kwa
wananchi wake; hivyo, Shirika hilo
linakaribishwa kuwekeza katika Mradi
husika.

Mtaalam kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Godwill Wanga


(Kulia), akichangia katika Kikao hicho. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi
wa Shirika la Gridi la Taifa la China, katika nchi za Tanzania na Kenya,
Dkt Zhang Xiang na katikati ni Meneja Miradi wa Shirika hilo, Zhu
Debing.

Mhandisi Luoga alisema kuwa,


Mradi wa usafirishaji umeme wa
Mchuchuma hadi Makambako ni
miongoni mwa Miradi muhimu sana
inayotegemewa kuboresha sekta ya
umeme kwa kuhakikisha kunakuwepo
na umeme wa uhakika na wa kutosha
kwa Watanzania.
Aliwataka wawakilishi hao
kutoka Shirika la Gridi la China,
kuwasilisha wizarani mchanganuo wa
mapendekezo ya namna gani Mradi
husika utafadhiliwa ili yajadiliwe kwa
pamoja na wataalam wa Wizara kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha,

TANESCO na NDC na kukubaliana


kuhusu utaratibu utakaofaa kutumika
kufadhili Mradi.
Awali, akichangia katika kikao
hicho, Mhandisi Mwandamizi kutoka
Wizara ya Nishati na Madini, Leonard
Masanja, aliwahakikishia wawakilishi
hao kutoka CET kuwa Tanzania
ina historia nzuri ya amani hivyo
wasipoteze muda mwingi kufanya
utafiti kuhusu mazingira ya uwekezaji
nchini bali wajikite kukamilisha
mchakato wa uwekezaji katika sekta
husika kama walivyopendekeza.

Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi


Innocent Luoga, akifuatilia kwa makini, uwasilishaji wa mapendekezo
ya uwekezaji katika Mradi wa kusafirisha umeme wa msongo
wa kilovolti 400 kutoka Mchuchuma hadi Makambako, uliokuwa
ukifanywa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Gridi la Taifa la China,
katika nchi za Tanzania na Kenya, Dkt Zhang Xiang, (hayupo
pichani), katika kikao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

You might also like