You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amekamilisha ziara
yake ya kikazi ya SIKU TANO mfululizo aliyoifanya katika Wilaya ya
Ngorongoro yenye lengo la kujitambulisha kwa wananchi wake, kufahamu
changamoto na fursa zilizopo pamoja na kukagua miradi ya Maendeleo.
Katika ziara hiyo iliyokua na mafanikio makubwa Mhe. Gambo alitembelea
Tarafa zote tatu ambazoni Sale, Loliondo na Ngorongoro kwenye Kata za
Ngarasero, Pinyinyi, Oldonyosambu, Digodigo, Samunge, Olorien,
Soitsambu, Ololosokwani, Piyaya, Nainokanoka pamoja na Kata ya Endulen.
Pia alifanya mikutano ya hadhara kwenye kila kata ili kusikiliza kero za
wananchi.
Aidha kupitia ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliweza kukutana na wafanyakazi wa
Taasisi za Serikali zinazotoa huduma katika Wilaya ya Ngorongoro,
Makapuni ya Utalii yaliyowekeza katika Wilaya hiyo, Baraza la wafugaji,
taasisi binafsi pamoja na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
Kupitia ziara hiyo ya kazi Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo alibaini na kutoa
maelekezo katika maeneo yafuatayo:
i.
Ugonjwa wa ajabu wa kutapika damu kwa wakazi wa Kata ya
Pinyinyi uliosababisha vifo vya watu 21, ambapo Mkuu wa Mkoa
alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa kuleta wataalam kufanya tafiti
na kupata ufumbuzi wa tatizo hilo na mpaka ziara inamalizika
wataalamu toka Wizara ya Afya na Taasisi ya Utafiti ya magonjwa
ya binadamu (NIMR) walikua wameshafika kwenye kata hiyo kwa
ajili ya utekelezaji wa maagizo hayo. Pia alimuagiza Mkurugenzi
kuboresha Zahanati ya Kata hiyo iliyopo mpakani mwa Kenya na
Tanzania yenye umbali wa zaidi ya Km 120 kutoka makao makuu ya
Wilaya.
ii.

Kutokuwa na mawasiliano ya mitandao ya Simu katika Tarafa


ya Sale na baadhi ya Kata za Ngorongoro; ambapo Mkuu wa Mkoa
1

ameahidi kukutana na makampuni ya Simu hasa yale


yaliyoelekezwa kufikisha huduma za simu maeneo ya vijijini ili
waweze kufikisha huduma hiyo maramoja.
iii.

Matumizi mabaya ya Fedha za Umma; Kutokana na hili Mhe.


Gambo aliwasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya
Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhifu wa fedha za uchaguzi pamoja
na miradi mingine ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Tsh 500
milioni. Watumishi hao ambao ni Mwekahazina Bw. Evans
Mwalukasa, Mwanasheria Bw. Sembeli Siloma pamoja na Afisa
Uchaguzi Bi. Hadija Mkumbwa. Sambamba na hilo Mhe. Gambo
amezuia watendaji wa kata kuhudhuria vikao vya Baraza la
madiwani kwa kuwa si wajumbe halali wa Kikao hicho na ambapo
hadi sasa wamesababishia Halimashauri hasara ya Tsh 132
milioni. Aidha amemuagiza katibu Tawala Mkoa wa Arusha
kumuandikia Katibu Mkuu Tamisemi ili awarudishe aliyekuwa
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Ngorongoro Bw. John Kulwa Mgalula
na Afisa Mipango Bw. Louis Chambi pamoja na Mhandisi Eng.
Maziku kuja kujibu tuhuma zinazowakabili. Rc Gambo amechukua
hatua hizo mara baada ya kupokea taarifa ya kamati aliyoiunda
kabla ya ziara hiyo.

iv.

Madeni ya Walimu; Mkuu wa Mkoa aliagiza Halmashauri kulipa


madeni ya walimu kwa kutuimia fedha za ndani ili kupunguza
madeni yao. Aidha Rc Gambo alishangazwa kuona Halimashauri
inadaiwa Million Tatu na laki Nane na walimu wa Sekondari
Wilayani Ngorongoro na Halimashauri kusema inasubiri fedha
kutoka Serikali Kuu. Alimuelekeza Mkurugenzi Mtendaji kulipa mara
moja kwa kuwa hicho kiasi ni kidogo.

v.

Usafiri wa Madiwani; Mkuu wa Mkoa alitoa maagizo ya


kusitishwa mara moja utaratibu wa Halimashauri kutuma gari za
Serikali kumfuata kila Diwani nyumbani kwake maana taratibu
hazisemi hivyo. Badala yake Mkurugenzi afanye jambo hilo kwa
kufuata Sheria na Taratibu. Pia alimuelekeza Mwenyekiti wa
Halimashauri hiyo kutumia gari ya Serikali mara mbili kwa wiki
kama taratibu zinavyotaka. Aidha, fedha zitakazookolewa kwa
utaratibu huu zielekezwe katika kupunguza madeni ya walimu
wilayani hapo.

vi.

vii.

Changamoto za huduma duni za afya, Elimu na maji; Mkuu


wa Mkoa aliwataka Halmashauri kwa kushirikiana na wadau
kuboresha huduma hizo na kuhakikisha wanajenga Vituo vya Afya
badala ya zahanati ili wakina mama waweze kujifungua salama.
Mhe Gambo alichangia bati zaidi ya 500 na fedha zaidi ya
Tsh Mil. 3,000,000 ili kushughulikia matatizo hayo. Aidha, alisema
hali ya usimamizi wa miradi ya Maji ni mbaya sana hivyo
Halimashauri ijipange upya kusimamia miradi hiyo.
Migogoro ya Ardhi inayotokana na kutopimwa kwa vijiji
hivyo na kukosekana kwa mpango wa matumizi bora ya
ardhi; Mhe Gambo ameagiza uongozi wa Wilaya, kukaa pamoja na
wawekezaji, Sekretarieti ya Mkoa na wadau wengine kumaliza
migogoro kwa kujadiliana changamoto hizi na kuzipatia ufumbuzi
wa kudumu.

viii.

Migogoro na wawekezaji; Mkuu wa Mkoa aliagiza wananchi


kushirikishwa katika kila hatua ya uwekezaji (Bottom up approach)
ili kuwepo na maridhiano baina ya wawekezaji na wananchi wa
meneo husika.

ix.

Uhifadhi hasa katika eneo la Ngorongoro na Loliondo; mkuu


wa Mkoa
alitaka kuwepo mpango wa uhifadhi ambao
hautaathiriwa na mifugo wala ongezeko la idadi ya watu na kuwepo
na mikakati wa kudhibiti ongezeko la mifugo ndani ya Kreta ya
Ngorongoro.

x.

Chakula cha Njaa; Rc Gambo alisema Serikali itakaa kuona


namna bora ya kupitia matamko mbalimbali yaliyotolewa na
viongozi wa awamu iliyopita ya kuwapatia Wananchi magunia
kumi bure kwa kila Kaya ili kumaliza tatizo la njaa. Pia alisema
Serikali ya Mkoa itakaa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ili
kuangalia namna bora ya kuboresha mpango wa chakula cha bei
nafuu kutoka NFRA.

xi.

Baraza la wafugaji; Mkuu wa Mkoa alisema ni muhimu baraza la


hilo kufanyiwa upembuzi yakinifu katika mambo yafuatayo:
Kuangalia kama Baraza hilo linafanya kazi kwa kuzingatia Sheria
na Taratibu
Kama malengo yaliyokusudiwa kuanzisha Baraza hilo yanafikiwa

Ufanyike ukaguzi kwa matumizi ya Fedha walizopewa kwa kipindi


cha miaka mitano maana malalamiko ya matumizi mabaya ya
fedha yamekuwa mengi.
Ikumbukwe kwamba Baraza Hilo la wafugaji la Ngorongoro
linapewa zaidi ya TSH 2.5 Billion kila mwaka fedha ambayo ni zaidi
ya mapato ya ndani ya Halimashauri ya Ngorongoro alisisitiza
Mhe. Gambo.
xii.

Rc Gambo pia aliagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro


kukamilisha ahadi yake ya Madawati 2000 kwa kumalizia haraka
madawati 1500 yaliyobakia ili kusiwe na mtoto yeyote anaye kaa
chini Wilayani Ngorongongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha alihitimisha ziara yake kwa kuwataka Madiwani


na Wataalam kila mmoja kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na Taratibu, pia
aliahidi kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kutafuta
ufumbuzi wa haraka wa changamoto zinazoikabili Wilaya ya Ngorongoro.
Imetolewana:

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari