1

SARUFI NI NINI
Kimsingi, sarufi ni kanuni ama sheria ambazo hutawala ubunifu, ufasaha na matumizi ya
lugha fulani. Sheria zinazotawala uumbaji na matumizi yalugha huegemea mno mambo
kama vile:
 Maumbo ya maneno
 Ufasaha wa maneno
 Matumizi ya maneno
 Miundo ya sentensi.
Dhima ya sarufi
Dhima ni sawa na wajibu. Dhima ya sarufi ni pamoja na:
 Kuongoza uundaji wa maneno
 Kuongoza uainishaji na wa maneno
 Kuelekeza usanifishaji wa lugha
 Kudhibiti matumizi ya lugha ili kukamilisha mawasiliano
MIHIMILI (NGUZO) YA SARUFI
Haya ni maneno ambayo ndiyo msingi mkuu wa lugha ya Kiswahili. Kila neno lina kazi
yake maalum ya kutekeleza ili kuafiki ufasaha. Maneno haya ni:
 NOMINO
Ni maneno ambayo hutumika kutajia na kutambulia :
 Watu ,wanyama

2

 Mahali
 Vitu
Zipo aina sita za nomino
 Maalumu / pekee
 kawaida - jumla
 za wingi
 za dhahania
 vitenzijina
 za jamii
 za pekee /maalum
 hutaja mtu au mahali
 lazima zianze kwa herufi kubwa
majina ya watu
Hasani, Ali, Kenyatta, Maulidi, Issa Hayatou
Sifa za Mungu
Kahari, Karima, Dayani, Raufu, Maulana, Rahimu, Jalali
majina ya mahali
Bara kama Afrika, Uropa na Marekani
Nchi kama Kenya, Tanzania na Uholanzi
Miji kama Arusha, Dodoma na Mwanza

3

Mito kama Rufiji, Tana na Nzoia
Milima kama Kilimanjaro, Elgon na Longonot
Maziwa kama Turkana, Nakuru na Tanganyika
majina ya miezi
Januari, Machi, Juni, Septemba na Disemba
majina ya siku
Jumapili, Jumatatu, Jumatano, Alhamisi na Ijumaa

ukwasi. daktari wanyama. aghalabu hujumuisha nomino katika ngeli ya ya-ya maziwa . simba. urembo * werevu. ujinga. uzembe  za vitenzijina huundwa kwa kupachika kiambishi ``ku’’ mwanzoni pa kitenzi mifano: Kucheza kwingine kunawaudhi wavyele . utamu. mkono. kuku. mafuta. ndege mtu.macho  za wingi huonyesha nomino zinazopatikana katika hali ya wingi pekee. makini  za dhahania hutaja vitu vinavyoonekana kwa fikra na dhana tu ni hali isiyoweza kupimika ila kukadirika tu mifano: * uchoyo. madini. utajiri * uchoraji. mali haki. weledi. ng’ombe mwili. ubora * uzuri. kitabu.Ni majina yasiyoanza kwa herufi kubwa isipokuwa mwanzoni pa sentensi . kalamu. msichana.4 b) za jumla au kawaida . ubaguzi. kisigino. maisha. marashi.aidha hujumuisha nomino za makundi yasiyobainika waziwazi mpira.

5 Kusoma kwangu ni bora Kuimba kwake kunapendeza kupika kwetu ni kuzuri kuchora kwao ni duni kufundisha kwake kunalipa  za jamii hutaja vitu au watu katika makundi mifano: umati wa watu genge la mabaharia mzengwewa maharamia kikoa cha waimbaji thurea ya nyota safu ya milima .

2. nyembamba. 1. Itiliwe maanani kwamba hakuna kivumishi ambacho kitatumiwa kwa shughuli ambazo si zake (isipokuwa kiwakilishi). mbali zaidi. watiifu. sura. Hutumiwa kueleza kitalifa au umbali wa nomino kwa kutegemea alipo msemaji ama msikilizaji. kimo. mrefu. kubwa. vya kuonyesha Aidha huitwa vionyeshi au viashiria.6 KIVUMISHI Ni maneno ambayo hutoa habari zaidi kuhusu jina linalozungumziwa. karibu. 1.hapa. kitu kilivyo au kinavyofikiriwa kuwa ( dhana ). Kijiko kichafu hakifai kuliwa wali.pale. Hurejelea mahali tatu. ni maneno ambayo hueleza sifa za nomino kwa kuegemea mambo kama vile: tabia. mbali kidogo. 1. vya sifa Kimsingi. jamii. Mifano: nzuri . mtamu. hodari. .hapo na 3. kichafu. safi. Maji safi ni bora kwa afya. imani. mkaidi. Mkate mtamu ulilika haraka. Hutoa habari za jinsi kitu au mtu alivyo ama anavyofikiriwa kuwa Vipo vivumishi aina kadhaa kwa kutegemea kazi au hamsini zilizopo. mrembo. shujaa. Gari kubwa limeegeshwa uchochoroni. fupi. mwaminifu Nguo nzuri itauzwa ghali. bingwa. maumbile. jema. mweupe. hawafu.

(pale) ngamizi ile .(hapo) kochi hilo .ghorofa hizo njia hiyo .ngamizi zile mgahawa ule.7 vya karibu .nyuta zile. maji yale – maji yale kulima kule – kulima kule ugali ule – ugali ule .mawele hayo vya mbali .vyerehani hivyo uele huo .(hapa) mtoto huyu – watoto hawa chakula hiki – vyakula hivi gari hili – magari haya uji huu – uji huu.njia hizo maji hayo kuandika huko cherehani hicho .migahawa ile uta ule .ndwele hizo uwele huo .makochi hayo ghorofa hiyo . nguo hii – nguo hizi uzi huu – nyuzi hizi mbacha huu – mibacha hii ulezi huu – malezi haya kuimba huku shambani hapa chumbani humu – vyumbani humu vya mbali kidogo .

vya kumiliki Aidha huitwa vimilikishi.mikorosho ile kabati lile . hubainisha ni nani mwenye kumiliki nomino inayotajwa.8 chai ile – chai ile mkorosho ule .makabati yale kichwani kule kichwani mle kichwani pale 1. Hurejelea nafsi tatu ambazo ni: NAFSI 1 2 3 UMBO KIWAKILISHI KIKANUSHI KIMILIKISHI Mimi ni si Sisi tu hatu -etu Wewe u hu -ako Nyinyi m ham -enu Yeye a ha -ake Wao wa hawa -ao (Mimi) – angu (sisi) – etu (wewe) – ako (nyinyi) – enu -angu .

Swali la hamsini ni tata. vya idadi Haya ni maneno ambayo hutekeleza majukumu ya kufafanua: idadi kamili au halisi (hesabu) Wachezaji watatu walituzwa.vyakula vyetu gari lako – magari yenu uta wake – nyuta zao nguo yangu – nguo zetu mkono wako – mikono yenu shambani pake – shambani pao 1.9 (yeye) – ake (wao) – ao Mifano: changu wangu – changu wetu chakula changu. Vijiko sita vimepotea jikoni. Mikate ishirini na miwili ilipotea Magonjwa matatu yamekuwa sugu nafasi ya jina katika orodha Taifa la kwanza lilikuwa Urusi. Magari manne yatauzwa. Mchezaji wa tatu barani ni Farouq Nchi ya pili duniani ni Hispania. Karatasi ya kumi ni mswaki. . Mwanafunzi wa kumi nchini ni Mapenzi.

10 idadi isiyoweza kuhesabika wala kubainika kikamilifu. Magari machache hayana vidhibiti mwendo. . Alinipa unga kidogo nikashukuru. Mboga ni haba sokoni siku hizi. Watu wengi wanampenda Mtimkuu kuwa shehe.

Maneno haya hutaka kuulizia habari kuhusu idadi ya vitu machungwa mangapi? mikunga wangapi? Vyerehani vingapi? Nguo ngapi? Magonjwa mangapi? bayana ya vitu a) vya mzizi -pi Mitume wapi? Vyungu vipi? Mikono ipi? Sindano zipi? Ugonjwa upi? Mkate upi? Sarahangi yupi? Shambani kupi? b ) visivyoambishwa Alitaka kalamu gani? Walitaka mipira gani? Kamba ile ni ya mchungaji gani? Shangangi hili ni la nani? Ametumwa na nani? . viulizi Haya ni maneno yanayotumiwa kutaka kujua habari fulani.11 1.

vya pekee Ni maneno ambayo hutoa maelezo kuhusu nomino kwa njia ya kipekee. Vivumishi vya pekee ni sita katika idadi. Huchukua viambishi vya majina ama vya ngeli kuleta ufasaha -ote . halisi na maalum. Aidha huitwa vivumishi halisi.12 Anataka nini? Gari linabeba nani? sababu ya tukio fulani mbona Kassim aliadhibiwa? Kwa nini mwalimu hakufika jana? Atanyang’anywa gari kwa nini? Mbona Eden hakai na wenzake? namna au jinsi ya utokeaji wa jambo Alichezaje mechi ya jana? Ataenda vipi shuleni? Liliharibikaje gari la Ali? Mpira ulitoboka vipi? Vya wakati Mpira ulianza lini? Ndege itaondoka lini? Wageni watafika lini? Mkutano utaanza saa ngapi? Nguo zilioshwa saa ngapi? 1.

13 Huonyesha ukamilifu katika utokeaji wa jambo Huchukua viambishi vya majina ama ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula chote – vyakula vyote Mkate wote – mikate yote Gari lote – magari yote Nyumba yote – nyumba zote Ugonjwa wote – magonjwa yote Ukuta wote – kuta zote Shambani kote – shambani kote Kichwani pote – kichwani pote -o-ote Huleta dhana ya hiari katika uteuzi na maamuzi Huchukua viambishi vya majina ama ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula chochote – vyakula vyovyote Mkate wowote – mikate yoyote Gari lolote – magari yoyote Nyumba yoyote – nyumba zozote Ugonjwa wowote – magonjwa yoyote Ukuta wowote – kuta zozote .

14 -enye Huleta dhana ya kumiliki Huchukua viambishi vya majina ama ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula chenye ladha – vyakula vyenye ladha Mkate wenye sukari – mikate yenye sukari Gari lenye abiria – magari yenye abiria Nyumba yenye ufa – nyumba zenye nyufa Ugonjwa wenye maambukizi – magonjwa yenye maambukizi Ukuta wenye ua – kuta zenye maua Shambani kwenye miti – mashambani kwenye miti -enyewe Huleta dhana ya kujitegemea na kuwapo kwa dhahiri ya uhusika Huchukua viambishi vya majina ama ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula chenyewe kina ladha – vyakula vyenyewe vina ladha Mkate wenyewe hauna sukari – mikate yenyewe haina sukari Gari lenyewe limejaa abiria – magari yenyewe yamejaa abiria Nyumba yenyewe inao ufa – nyumba zenyewe zina nyufa Ugonjwa wenyewe huambukiza – magonjwa yenyewe huambukiza Ukuta wenyewe una ua – kuta zenyewe zina maua .

15 -ngi Huleta dhana ya kuwapo katika hali iliyozidi ya kawaida na katika wingi tu Huchukua viambishi vya majina/ ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula kingi kimepikwa – vyakula vingi vimepikwa mikate mingi itaoza magari mengi hayana vidhibiti kasi nyumba nyingi hazina nyua magonjwa mengi yamekosa tiba mwafaka kuta nyingi zina nyufa mikunga wengi huvuliwa usiku. -ngine Huleta dhana ya ziada katika mahitaji ama matumizi Huchukua viambishi vya majina/ ngeli kwa kutegemea nomino husika Chakula kingine – vyakula vingine Mkate mwingine – mikate mingine Gari jingine/ lingine – magari mengine Nyumba ingine/nyingine – nyumba zingine/nyingine Ugonjwa mwingine – magonjwa mengine Ukuta mwingine – kuta zingine/nyingine .

16 1. radidi kimsingi hivi ni viashiria ambavyo huradidiwa (hukaririwa ama kurudiwa) hutumiwa kushadidia jambo Fulani katika usemi mtoto huyu huyu – watoto hawa hawa chakula hiki hiki – vyakula hivi hivi gari hili hili – magari haya haya uji huo huo – uji huo huo nguo hiyo hiyo – nguo hizo hizo uzi huo huo – nyuzi hizo hizo mbacha ule ule – mibacha ile ile ulezi ule ule – malezi yale yale kuimba kule kule – kuimba kule kule chumbani mle mle – vyumbani mle mle 1. visisitizi kimsingi hivi ni viashiria ambavyo huradidiwa (hukaririwa ama kurudiwa) hutumiwa kutilia mkazo jambo fulani katika usemi mtoto yuyu huyu – watoto wawa hawa chakula kiki hiki – vyakula vivi hivi gari lili hili – magari yaya haya uji uo huo – uji uo huo nguo iyo hiyo – nguo zizo hizo uzi uo huo – nyuzi zizo hizo mbacha ule ule – mibacha ile ile ulezi ule ule – malezi yale yale kuimba kule kule – kuimba kule kule .

. Aghalabu hili hushamiri mno katika ngeli ya a – wa. Kwenye sentensi yenye nomino mbili katika usanjari. Kimatumizi.17 chumbani mle mle – vyumbani mle mle 1. Viunganifu vya –a Kiunganifu –a huleta dhana ya uhusiano baina ya nomino na nyingine na kuujenga katika misingi hafifu ya kumiliki. vya nomino Nomino hutumiwa kutoa maelezo ya nomino nyingine. hutegemea mno viambishi vya majina ama ngeli kulingana na nomino husika. nomino ya pili hutoa ufafanuzi wa nomino ya kwanza na hivyo kuwa kivumishi cha sifa. Mifano Mtoto wa mama – watoto wa mama Chandarua cha kaka – vyandarua vya kaka Mkono wa mualisaji – mikono ya waalisaji Kabati la nguo – makabati ya nguo Nguo ya harusini – nguo za harusini Ubavu wa mgonjwa – mbavu za wagonjwa Hewa ya sumu – hewa ya sumu Kuimba kwa mutribu – kuimba kwa watribu Uyoga wa nyikani – uyoga wa nyikani Unyoya wa ndege – manyoya ya ndege Mafuta ya taa – mafuta ya taa 1.

tenga. Mwanajeshi mkimbiaji alishinda nishani ya dhahabu. funga. Mwalimu mwimbaji alituzwa. Mifano ya vitenzi ni kama vile: Pika. Mifano: Mtimkuu aliandika waraka Mvua inanyesha kidindia Mkono wake umemwuma sana Gari litambebea viazi Badi alikuwa akiimba Mvua imekuwa ikinyesha . KITENZI Kitenzi ni neno ambalo hutoa taarifa kuhusu tendo linalofanyika au litakalofanywa na kiumbe. chora. soma. lima. Kiongozi salihina anawaongoza raia kwa haki. Vitenzi vya aina hii aghalabu huitwa vitenzi vikuu. Mwanafunzi mchoraji hufanikiwa aushi yake. Aidha huitwa kiarifu. Daktari jasusi ameshtakiwa. inga. ota. iba. sema. unda AINA ZA VITENZI 1. imba.18 Mifano Askari mhubiri ameondoka. kata. Waziri mchezaji hupendwa na raia. Vitenzi halisi huchukua viambishi mbalimbali ili kutekeleza majukumu ainaaina. panda. Vitenzi vikuu(T) Zipo sentensi ambazo zina kitenzi kimoja. piga.

19 Garimoshi litakuwa likiondoka Mufti atakuwa akihutubu .

Aghalabu kitenzi kisaidizi huja kabla ya kitenzi kikuu katika sentensi. kivumishi au kielezi na nomino. vya wakati na vya hali Mifano Kuwa kwisha kuweza kutaka ngali kupata kubidi kulazimu Iddi amekuwa mkaidi zaidi ya mwanambuzi Pwagu yule angetaka kujiua Maria angali mtoni Maziwa yamekwisha kumwagwa Zandiki anaweza kubadilika? .20 1. kiwakilishi. Vitenzi hivi viko katika makundi mawili Vikamilifu Huchukua viambishi vya ngeli. Mifano: Walikuwa wakidhulumiwa sana Kaidi hatakuwa amempa Ali hakuwa akimweleza Tulikuwa tukiimba mashairi Sadiki angali anamsubiri Zandiki Musa hawezi kuandika sentensi sahihi Juma atafika kuwafundisha waimbaji 1. Vitenzi vishirikishi (t) Haya ni maneno ambayo hutumiwa kudhihirisha uhusiano kati ya nomino. kivumishi au kielezi kingine. Vitenzi visaidizi(Ts) Kitenzi kisaidizi hutumika pamoja na kitenzi kikuu katika sentensi ili kukamilisha taarifa inayokusudiwa.

Mifano ni si yu li ndi ki Simba ndiye mfalme wa jangwa Maimuna si mtukutu Cherehani ki sebuleni Embe li mezani Mbwa yu kizimbani Nguo i mkobani 1. Havichukui viambishi vya wakati ama hali.21 Vipungufu Hivi huchukua viwakilishi vya nafsi pekee. wakati na hali ya vitenzi hivi huwa sawa Vitenzi sambamba aghalabu huwa ni vitenzi halisi viwili au kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu Mifano Sadiki alicheza akichechemea T T Mcheja analima akiimba T T Mkonokono alikuwa akiwatibu T T . Vitenzi sambamba Hivi ni vitenzi viwili au zaidi vinavyotumika katika sentensi moja Vitenzi sambamba hufuatana katika usanjari kwenye sentensi Vitenzi sambamba hutoa maana halisi ya tendo Nafsi.

‘kitendo kilitokea wakati gani?’ . Kielezi aidha huitwa kisifa.22 Salihina angali anasali T T  KIELEZI Kielezi ni neno ambalo hutoa maelezo zaidi kuhusu utokeaji wa kitendo fulani. Kitendo kilitokea lini? Haya ni maneno ambayo hutaja na kubainisha wakati wa kitendo. Mifano Samba aliimba vizuri Kanzu ya shehe ilishonwa vibaya Kaidi alijibu kijinga Mandela alipigana kishujaa Garimoshi litapita haraka Huimba mara kwa mara Angesafiri kwa matwana Mtimkuu anampenda sana 1. kitendo kilitokea vipi? Huitwa vielezi vya namna au jinsi. Hivi huitwa vielezi vya wakati kwa jinsi yanavyojitahidi kujibu swali. Hutarajiwa kujibu swali. Kielezi hujibu maswali kama vile: 1. Kitendo kilitokea vipi? Hivi hutoa dhahiri ya namna ama jinsi kitendo kilivyotokea.

Huitwa vielezi vya mahali Mifano Gari lilianguka mtaroni Watoto wanacheza uwanjani Maji yalibebewa mtungini Ibada ilifanyiwa maabadini Meli ya mizigo ilizama baharini Wageni walilala hemani Mchopozi mwenyewe hulala korongoni pale darajani Saa yangu iliharibikia sandukuni 1. Huitwa vielezi vya nomino . Kitendo kilitokea wapi? Haya ni maneno ambayo hueleza mahali palipotokea kitendo husika. Kitendo kilihusika na nini? Haya ni maneno ambayo hueleza kitu ama mtu aliyepokea kitendo kinachohusika.23 Mifano Halima alifika jana Nguo zitaoshwa leo Kabati litaundwa asubuhi Kiti kilivunjika jioni Safari ingalianza alfajiri Wageni waliondoka saa thenashara Mchezo ulitia nanga alasiri Mtihani ulifanywa mwezi uliopita Uchaguzi utaandaliwa mwaka ujao 1.

Mifano Maziwa yalimwagika yote Magari yalifwata huku Machungwa yalioza mengi Karimu alilima pakubwa Maji yalienea kote Matwana yatapitia kwenu 1. Kitendo kilitokea mara ngapi? Hivi hueleza idadi ya utokeaji wa kitendo kinachotajwa. Huitwa vielezi vivumishi.24 Mifano Hemedi alivunjika mkono Gari liliangukia nyumba Nguo zilianikiwa kijakazi Ukuta ulijaa nyufa Wanafunzi wote waliletewa maziwa 1. Kitendo kilikuwa na sifa gani? Haya ni maneno ambayo hudhihirisha uvumi unaozingira kitenzi. Aidha huitwa vielezi vya idadi Mifano: Mvua aghalabu hunyesha maeneo haya Juma aliitwa mara tatu ndipo akaitika Shangazi alipita hapa mara nyingi Matatu yameonywa kwa mara ya mwisho Gari lile ndilo lililofika la kwanza Mwizi mwenyewe alikatwa mguu mara nne .

25 .

Kiunganishi katika sentensi huwasilisha maana na dhana mahsusi Vipo viunganishi ambavyo vinaweza kuwa mwanzo wa sentensi na vingine ni sharti viwe katikati ya sentensi. Kivumishi Neno ambalo kimsingi ni kivumishi linaweza kuchukua majukumu yote ya jina na kuyatekeleza kikamilifu katika sentensi. Neno lenyewe si nomino ila huchukua na kutekeleza majukumu yote ya nomino katika sentensi. Kiwakilishi pia huitwa kijina ama kibadala Viwakilishi huweza kuwa na maumbo mbalimbali 1. Mifano minghairi bighairi kefu ingawa almuradi madhali seuze lakini lau na ijapokuwa japo maadamu ili angaa angalau bali mbali na Wananchi wengi humpenda waziri wa utamaduni japo ana kiburi Kibago changu kilivunjwa bighairi ya sababu maalum Juhudi alicheza vizuri ingawa hakutuzwa Wagonjwa wote watahudumiwa maadamu tabibu yupo Mvua ilinyesha angaa kutupunguzia vumbi Tanzania iliipiku Uganda seuze Rwanda  KIWAKILISHI Kiwakilishi ni neno ambalo huwakilisha nomino katika sentensi.26  KIUNGANISHI Hili ni neno ambalo huunga neno na neno. Maziwa haya yamechina mengine mazuri yataletwa Yote yaliyonunuliwa yatauzwa . wazo na jingine ama wazo na jingine.

ni - tu- u- m- a- wa- Mifano nilimpigia simu jana asubuhi tunayaosha magari ya walimu wetu ukifika mapema nitakutuza msingalikibomoa kibanda mngalienda hasara alikuwa akiimba alipochukuliwa wameliziba korongo lililowaangamiza wanyama howa .27 Mengi yaliyooza yametupwa Hiki kipya kitatumiwa leo Wa kwanza kufika atatuzwa vizuri Matatu mekundu yatawafaa sana Ngapi kubwa zitawatosha wageni? 2. Nafsi Nafsi huru Nafsi isiyoambishwa na chochote. mimi sisi wewe nyinyi yeye wao mimi nitacheza mpira sisi tuliimba mashairi wewe ungefika mapema nyinyi nyote mlishindwa mchezoni yeye mwenyewe asingalijenga nyumba wao wakifika tutashukuru Nafsi tegemezi Nafsi huweza kuwakilishwa kwa silabi zinazoambishwa kwenye kitenzi.

Kirejeshi ambaKirejeshi amba.kinaweza kutumiwa kutekeleza majukumu yote ya nomino katika sentensi kama kibadala ama kijina. Mifano Ambaye atakibeba kigoda atatuzwa Ambacho kilinunuliwa hakishoni vizuri Ambao ulichezwa jana ulitoboka Ambayo yangenywewa na mtoto yameganda Ambako kulikuwa kukijengwa kutakuwa kwangu Ambayo yanatisha ni ukimwi Ambapo pana miti ni hatari kujenga .28 3.

kusuta.Kuonyesha mshangao kumbe! – kuonyesha mshangao au kukosa hakika ya jambo ah! – ajabu! – salale! – huonyesha hali ya kupumbaa kefule! – kefle! – aka! – ebo! – huonyesha hali ya kuudhika au kusinywa .29  KIHUSISHI Kihusishi ni neno ambalo huonyesha uhusiano baina ya nomino na nomino. tukio na tukio ama tukio na wakati Uhusiano huo unaweza kuwa wa karibu ama mbali Mifano chini ya juu ya awali ya kando ya kabla ya kwa na nyuma ya mbele ya ubavuni pa baada ya kwenye ndani ya Paka ameingia ndani ya nyumba Gari liliegeshwa mbele ya nyumba Maji yalitiwa katika chupa Maria analala chini ya gari Bendera itawekwa kwenye mlingoti Mvua ilinyesha halafu ya ngurumo za radi Mafua yamezidi tangu ujio wa kipupwe Maria angetembea ubavuni pa baba yake Kikao kiling’oa nanga awali ya dua kusemwa KIHISISHI Kihisishi ni neno ama fungu la maneno ambalo hutumiwa kuonyesha hisia katika usemi Hisia zenyewe zinaweza kuwa za kufurahi. kubeza. hali na hali. kuridhika ama kuajabia jambo fulani Alama ya mshangao hutumiwa ili kudhihirisha hisi Mifano lo! . kuudhika.

Marahabaa! Fanaka amefuzu udaktari. Kumbe! Nilidhani ni rafiki kumbe ni hasimu.kuonyesha huruma hewaa! – marhabaa! – kuonyesha kuridhika na jambo Lo! Kaidi amempiga baba yake. Ah! Mvua inanyesha ya pilau? Ajabu! Maria nafikiri atamshinda Kauleni? Aka! Hata Wigan pia inaishinda timu ya Baba? . Salale! Ati Kenya imeshinda Uturuki? Kefu! Unajinaki kwa kijigari chako? Maskini! Maulidi amechomewa nyumba.30 maskini! .

hali ya tukio na njeo yake ili kujibu swali. Viambishi awali Hivi hupatikana kabla ya mzizi wa kitenzi. lini? . Ki-jiko _ vi-jiko m-kono _ mi-kono u-bavu _ m-bavu ki-pofu _ vi-pofu *gari _ ma-gari u-limi _ ndi-mi m-toto _ wa-toto u-gonjwa _ ma-gonjwa n-guo _ n-guo Viambishi vya ngeli Hivi hupatikana mwanzoni pa fungutenzi.31  VIAMBISHI Kiambishi ni mofimu (silabi) ambazo huunda neno. Vipo viambishi vya aina mbili 1. Hutumiwa kuonyesha umoja ama wingi wa majina. hali na njeo Hivi hudhihirisha hasa wakati wa tukio. Mzizi wa kitenzi ni sehemu ya kitenzi isiyobadilika kama vile piga pig-ia pig-wa pig-ika pig-ana viambishi awali viko katika mikondo mitano bayana. a-naimba _ wa-naimba ki-livunjika _ vi-livunjika li-naoshwa _ ya-naoshwa i-liraruka _ zi-liraruka u-tazuiwa _ ya-tazuiwa u-meiva _ u-meiva u-takatwa _ i-takatwa u-taanguka _ zi-taanguka ya-litosha _ ya-litosha Viambishi vya wakati. Viambishi vya majina Hivi huwa kwenye mianzo ya majina. Aidha huambishwa kunako mzizi wa kitenzi ili kukamilisha maana. Hivi hutambulisha ngeli ya nomino husika.

32 mifano a – li –kuja li – me – anguka ya – nge – mwagika u – na – katika zi – ngali – shonwa ku – singali – tengenezwa ki – ta –enda a – ka – tufukuza u – ki – mwangamiza hu - waua Viambishi virejeshi vya –o Hivi huwa ni vibadala vya kirejeshi ambaHurejelea kitenda/mtenda au kiima Aghalabu huja baada ya kiambishi cha wakati Mifano Gari ambalo lilianguka > gari li – li – lo – anguka Mkonokono ambaye amefika > mkonokono a – li – ye – fika Cherehani ambacho kinashona > cherehani ki – na – cho – shone Mkate ambao utanunuliwa > mkate u – taka – o – nunuliwa Kalamu ambayo inaandika > kalamu i – na – yo – andika Kuta ambazo zilibomoka > kuta zi – li – zo . kitendewa/mtendewa ama shamirisho. Hutegemea ngeli na jina linalohusika Aghalabu huchukua viambishi vya ngeli Mifano Gari li – li – lo – mw – angusha > magari ya – li – yo – wa – angusha Mtoto a – li – ye – ki – vunja kiti > Watoto wa – li – o – vi – vunja viti .bomoka Shambani ambapo alijenga > shambani a – li – po – jenga Kipofu ambaye amepona > kipofu a – li – ye – pona Viambishi viwakilishi vya shamirisho Hivi huwa vya kusimama badala ya kitenda/mtenda.

e – ka > tendwa > tendana > tendeka .li .w – a Watabeb – a – na Zilishon .funika mkate > nguo zi – li – zo – i .zi .shona Nguo i – li – yo – u .vyo .33 Mkono u – li – o – li – kata embe > Mikono i – li – yo – ya – kata maembe Ugonjwa u – li – o – m – lemaza magonjwa ya – li – yo – wa – lemaza > Cherehani ki – li – cho – i – shona > vyerehani vi .funika mikate b) Viambishi tamati Hivi hupatikana baada ya mzizi wa kitenzi Huwa na sura mbalimbali Viambishi virejeshi vya –o Hivi huwa ni vibadala vya kirejeshi ambaHurejelea kitenda/mtenda au kiima Huleta dhana ya mazoea katika utokeaji Mifano Gari ambalo lilianguka > gari liangukalo Mkonokono ambaye amefika > mkonokono afikaye Cherehani ambacho kinashona > cherehani kishonacho Mkate ambao utanunuliwa > mkate ununuliwao Kalamu ambayo inaandika > kalamu iandikayo Kuta ambazo zilibomoka > kuta zibomokazo Shambani ambapo alijenga > shambani ajengapo Kipofu ambaye amepona > kipofu aponaye Viambishi vya mnyambuliko Hivi hudhihirisha kauli ya kitenzi yani kitenzi kiko katika mnyambuo gani Mifano Lilimwanguk – i – a > tendea Kinaund .

34 Yalikat – i – wa Huandik – ia – na > tendewa > tendeana Tuliwabeb – e – sha > tendesha Waliimb – i – shwa > tendeshwa Viambishi tamati viulizi Hivi mara nyingi huwa ni vya kuegemea mzizi wa kitenzi kwa nia ya kuulizia: Namna ya utokeaji Alicheza .je? Waliimba .je? Zilifuliwa .ni? Lilivunja – ni? Itafunika – ni? Palipandwa – ni? Walipikiwa – ni? Walifulia – ni? Mahali pa kutokea kitendo Aghalabu huchukua kiambishi –pi Lilikwama – pi? Kilipatikana – pi? Yalimwagwa – pi? .je? Lilianguka .je? Nomino iliyopokea kitendo Wataka .je? Palipitika .

35 Atalima – pi? Amehamia – pi? Inapandwa – pi? Tanbihi: Ikumbukwe kuwa viambishi tamati hasa viulizi hutumika katika sanaa wala katika maandishi natharia haihalisi. .

Kimsingi. Wakati uliopita Vitendo katika wakati huu huwa ni vya wakati ama kipindi cha awali (kitambo cha mapema) Kitendi husika aghalabu ni mapisi ama historia Huwakilishwa na silabi –li.gari halikukarabatiwa Jumba kubwa lilijengwa .na kukanushwa na –ha*kuTanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.maji hayakumwagika Mpira ulitoboka .jumba kubwa halikujengwa Nguo nyingi zilishonwa . zipo nyakati tatu katika Kiswahili na hali mbalimbali kwa kutegemea utokeaji wa kitendo husika.moto haukuzimwa asubuhi Kuimbwa kwake kulitusisimua .nguo nyingi hazikushonwa Moto ulizimwa asubuhi . cha sasa au cha baadaye.36  NYAKATI Wakati ni kipindi maalum cha muda.mpira haukutoboka Gari lilikarabatiwa . 1.kuimba kwake hakukutusisimua Zipo hali mbalimbali ambazo hubainika kwa kutegemea utokeaji wenyewe. Kipindi hiki kinaweza kuwa ni cha mapema au awali. Hali timilifu Kitendo kinachozungumziwa kina kipindi kifupi tangu kutokea kwake.chakula hakikupikwa Maji yalimwagika . . Mifano Chakula kilipikwa .

nyumba hazijabomolewa Ukuta umejengwa Tarakilishi imepotea . Mifano: Mtoto amelala .mihadarati haijaharibu vijana Shambani pamelimwa . Huwakilishwa na –ngali.mtoto hajalala Chombo kimeoshwa . Hali tegemezi Hudhihirisha uhusiano baina ya vitendo viwili katika kutokea kwake.dawati halijavunjika Mwembe umekatwa . Hutokea kwamba kufaulu kwa kitendo cha pili kulitegemea pakubwa ufanisi wa kitendo cha kwanza. Huwakilishwa na –me.tarakilishi haijapotea Ugonjwa umesambaa . Huleta dhana ya majuto kwa kutofaulu kwa kitendo cha pili kwa sababu ya kukosa kufaulu kwa kitendo cha kwanza.chombo hakijaoshwa Dawati limevunjika .magonjwa hayajasambaa Mihadarati imeharibu vijana .shambani hapajalimwa Tanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.na hukanushwa na –singali- .kuta hazijajengwa .mwembe haujakatwa Nyumba zimebomolewa .na kukanushwa na –ha*jaTanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.37 Ipo hakika na ithibati ya kutokea kwake.

Nguo zisingalichafuka zisingalioshwa Ubavu ungaliumia angalilia sana .Mkate usingalioza usingalitupwa .38 Mifano: Angalikuja ningalimpa msaada Kiti kingalianguka kingalivunjika Mkate ungalioza ungalitupwa Sikio lingaliraruka lingalishonwa . Mifano: Mvua ilikuwa ikinyesha alipofika . Huwakilishwa na kuwepo kwa -kuwa -kiHukanushwa kitenzi kisaidizi ha*kuwa peke yake Tanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.Mkutano haukuwa ukikamilka alipoitwa - Gari halikuwa limeegeshwa lilipolipuka .Ubavu usingaliumia asingalilia sana Maji yangalimwagika ningalipigwa .Kiti kisingalianguka kisingalivunjika .Maji yasingalimwagika nisingalipigwa Ugonjwa ungalimshika angaliaga .Mvua haikuwa ikinyesha alipofika Mchezo ulikuwa ukiendelea risasi ilipolia .Asingalikuja nisingalimpa msaada . Hudhihirisha na kubainisha kitendo kilichotokea baada ya cha kwanza.Ugonjwa usingalimshika asingaliaga Hali ya maendelezi au sadfa Huleta dhahiri ya kuwepo kwa vitendo viwili katika kutokea kwake huku kitendo cha pili kikifuata cha kwanza na kujiikuta katika kuendelea kwa pamoja.Mchezo haukuwa ukiendelea risasi ilipolia Muziki ulikuwa ukiendelea walipoingia .Sikio lisingaliraruka lisingalishonwa Nguo zingalichafuka zingalioshwa .Muziki haukuwa ukiendelea walipoingia Mkutano ulikuwa ukikamilka alipoitwa Gari lilikuwa limeegeshwa lilipolipuka .

Maji hayakuwa yamejaa alipopiga mbizi Wageni walikuwa wamewasili alipoingia .Hasani hakumpiga wala hakumwumiza Gari lilianguka likawajeruhi .na hukanushwa na wala Mifano: Aliniita nikaenda akanituma . i.haikunyesha. cha pili na vingine. sikuloa wala sikuugua Ulitoboka ukashonwa na ukachezwa . Huibua dhana ya kuwa msemaji yuko katika hali ya kushuhudia kitendo kikitokea Huwakilishwa na silabi –na.Wageni hawakuwa wamewasili alipoingia Hali ya masimulizi Huweka wazi vitendo viwili au zaidi vilivyotokea. o na u husalia nazo hata katika ukanushi. Huwakilishwa na silabi –ka. hakunipiga wala hakuniumiza Ilinyesha nikaloa hadi nikaugua . sikuenda wala hakunituma Hasani alimpiga akamwumiza .Hakuniita.Gari halikuanguka wala halikuwajeruhi Alinishika akanipiga na akaniumiza .na hukanushwa na ha*i Vitenzi vinavyoishia irabu –a hubadilika na kuishia irabu –i.Mkonokono hamtibu mgonjwa .hakunishika.Haukutoboka. Vitenzi vinavyoishia kwa e. haukushonwa wala haukuchezwa b) Wakati uliopo Huonyesha kuwa kitendo ama vitendo viko katika muda wa sasa. mifano: Mkonokono anamtibu mgonjwa . Tanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.39 Maji yalikuwa yamejaa alipopiga mbizi . Utokeaji wenyewe huwa katika mfululizo kiasi cha kubainisha cha kwanza.

Mwalimu hatatufundisha kesho Mkeka utauzwa asubuhi .na kukanushwa na ha.Mipira yote haishonewi jijini Arusha Ugonjwa wa ukimwi unatisha jamii .Ukuta wenyewe hautapakwa rangi Wakati ujao una hali mbalimbali kwa kuzingatia utokeaji wenyewe. .Kibago kipya hakitapakwa rangi Maji yote yatamwagika sakafuni .Ugonjwa wa ukimwi hautishi jamii Kidole kimoja kinavunja chawa . Hali ya kuendelea ama sadfa Huleta dhahiri ya kuwepo kwa vitendo viwili katika kutokea kwake huku kitendo cha pili kikifuata cha kwanza na kujikuta katika kuendelea kwa pamoja.Mtambaachi hanyinyiriki nyasini Mvua inanyesha nyingi .Mvua hainyeshi nyingi Mashamba yanapaliliwa na wakulima .Hakimu hawahukumu wahalifu Mtambaachi ananyinyirika nyasini . Mifano: Mwalimu atatufundisha kesho .Kabanguo jipya halitanunuliwa Nyumba zote zitashonewa ndani Ukuta wenyewe utapakwa rangi Nyumba zote hazitashonewa ndani . Kitendo husika kiko katika muda wa baadaye.Timu ya taifa haichezi vizuri Mipira yote inashonewa jijini Arusha .Tabibu hafikirii jinsi ya kutibu uele c) Wakati ujao Wakati huu hurejelea kitendo ambacho kipo katika hali ya kusubiriwa.kuambishwa kwenye kiarifu.Kidole kimoja hakivunji chawa Tabibu anafikiri jinsi ya kutibu uele .Miji yetu hailindwi na wanajeshi Timu ya taifa inacheza vizuri .Mashamba hayapaliliwi na wakulima Miji yetu inalindwa na wanajeshi .40 Hakimu anahukumu wahalifu .Maji yote hayatamwagika sakafuni Kabanguo jipya litanunuliwa . Huwakilishwa na silabi –ta.Mkeka hautauzwa kesho Kibago kipya kitapakwa rangi .

Wanafunzi hawatakuwa wakijiandaa Wakulima watakuwa wakipanda miti . Hutokea kwamba kufaulu kwa kitendo cha pili kutatetegemea pakubwa ufanisi wa kitendo cha kwanza.Nguo zote hazitakuwa zikipigwa pasi Ugonjwa wowote utakuwa ukizuiwa . Mifano: Waziri atakuwa akihutubu mkutanoni . Huleta dhana ya majuto kwa kutofaulu kwa kitendo cha pili kwa sababu ya kukosa kufaulu kwa kitendo cha kwanza.na hukanushwa na –singe- . Huwakilishwa na –nge. Huwakilishwa na kuwepo kwa -kuwa -kiHukanushwa kitenzi kisaidizi ha*takuwa peke yake Tanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama ngeli ya nomino husika.Mchezo hautakuwa ukiendelea mchana Gari litakuwa likipakwa rangi nyeupe .Gari halitakuwa likipakwa rangi nyeupe Nguo zote zitakuwa zikipigwa pasi .Waziri hatakuwa akihutubu mkutanoni Mchezo utakuwa ukiendelea mchana .Wakulima watakuwa wakipanda miti Hali tegemezi Hudhihirisha uhusiano baina ya vitendo viwili katika kutokea kwake.41 Hudhihirisha na kubainisha kitendo kilichotokea baada ya cha kwanza.Ugonjwa wowote hautakuwa ukizuiwa Njia zote zitakuwa zikifungwa usiku .Njia zote hazitakuwa zikifungwa usiku Wanafunzi watakuwa wakijiandaa .

42 Mifano: Angekuja ningemsaidia kununua .Mhazigi asipokuja hawatatibiwa Njia zikitengenezwa uchumi utakua .na hukanushwa na –sipo- ha* Tanbihi Alama * inaashiria kuwa nafasi hiyo huchukuliwa na kiambishi cha jina ama cha ngeli ya nomino husika. Mifano: Mhazigi akija watatibiwa .Njia zisingetengenezwa tusingeshukuru Shambani kungelimwa kungefaa - Shambani kusingelimwa kusingefaa Mazingira yangetunzwa tungeishi - Mazingira yangetunzwa tungeishi Hali ya masharti Huleta uhusiano baina ya vitendo viwili na kutokea kwake.Njia zisipotengenezwa uchumi hautakua Gari likianguka litakarabatiwa .Ugonjwa usingekingika asingekuwa hai Njia zingetengenezwa tungeshukuru .Gari lisipoanguka halitakarabatiwa Mazingira yakiwa safi afya itaimarika .Blanketi lisingeraruka tusingeadhibiwa Marashi yangemwagika angelia - Marashi yasingemwagika asingelia Ugonjwa ungekingika angekuwa hai . Huleta dhana ya masharti kuwa ili kitendo cha pili kifaulu ni sharti cha kwanza kiwe kilifaulu Huwakilishwa na silabi –ki.Asingekuja nisingemsaidia kununua Kiti kingevunjika ningeanguka - Kiti kisingevunjika nisingeanguka Blanketi lingeraruka tungeadhibiwa .Mazingira yasipokuwa safi afya haitaimarika Ukimwi ukizuiwa tutaishi salama - Ukimwi usipozuiwa hatutaishi salama .

Wakati usiodhihirika Kitendo kinachotajwa hakina dhahiri ya wakati Huchukuliwa kuwa kitendo hicho kipo katika hali ya kuendelea Huwakilishwa na irabu –a na hukanushwa kwa misingi ya wakati uliopo Katika kukanusha.na hukanushwa kwa kutanguliza neno huwa --Katika kukanusha.Magari huwa hayapiti hapa mara nyingi Chakula chetu hupikwa mapema - Chakula chetu huwa hakipikwi mapema Watoto watundu huadhibiwa - watoto watundu huwa hawaadhibiwi Rais hutoa zawadi kila mara - Shule nyingi hutoa huduma za dezo - Rais huwa hatoi zawadi kila mara Shule nyingi huwa hazitoi huduma za dezo 3.43 Ajira ya watoto ikikoma watasoma .Ajira ya watoto isipokoma hawatasoma Dawa za kulevya zikiuzwa tutaumia - Dawa za kulevya zisipouzwa hatutaumia Maziwa yakimwagwa tutakasirika . huchukua mtindo wa ha*i Mifano: Ukimwi waua wengi - Ukimwi hauui wengi Maji yamwagika kupita kiasi - Maji hayamwagiki kupita kiasi .Maziwa yasipomwagwa hatutakasirika Zipo hali nyingine ambazo hazidhihiriki kuwa ni za wakati gani hasa. 2. Hali ya mazoea Huleta dhana ya kitendo kuwa na mazoea ya kutokea mara kwa mara Huwakilishwa na silabi hu. huchukua mtindo wa huwa + ha*i Mifano: Mvua hunyesha kila Januari - Mvua huwa hainyeshi kila Januari Magari hupita hapa mara nyingi .

44 Magari yasababisha ajali niani - Magari hayasababishi ajali njiani Kenya yashindwa na Tanzania - Kenya haishindwi na Tanzania Ukuta wa Yeriko wabomoka Ukuta wa Yeriko haubomoki - Mazingira yawekwa safi mjini Punda ashtakiwa kwa kuua - Ufisadi waangamiza Kenya Mazingira hayawekwi safi mjini Punda hashtakiwi kwa kuua - Ajali zahujumu juhudi za polisi - Ufisadi hauangamizi Kenya Ajali hazihujumu juhudi za polisi JEDWALI LA WAKATI NA HALI MBALIMBALI KIKANUSHI HALI KIKANUSHI Uliopita ( -li-) Ha-ku Timilifu (-me-) Ha-ja Yalimwagika hayakumwagika yamemwagika hayajamwagika Tegemezi (-ngali-) -singali- yangalimwagika yasingalimwagika Kuendelea (kuwa + ki) Ha-kuwa –ki- Yalikuwa yakimwagika Hayakuwa yakimwagika Masimulizi (-ka-) Ha-ku + wala Alinipa nikachukua Hakunipa wala sikuchukua WAKATI Uliopo (-na-) Ha-i zinaoshwa hazioshwi Ujao (-ta-) Ha-ta Tegemezi (-nge-) -singe- utaliwa hautaliwa Ungepikwa ungeliwa Usingepikwa usingeliwa Masharti (-ki-) -sipo.ha- .

45 Usiodhihirika (a) Chapikwa yashonwa Ha-i Hakipikwi haishonwi Ikinyesha tutapanda Isiponyesha hatutapanda Kuendelea (-kuwa + ki) Ha-kuwa + ki Itakuwa ikijengwa Haitakuwa ikijengwa Mazoea (hu-) Huwa ha-i Yai hupikwa Yai huwa halipikwi Nguo hushonwa Nguo huwa haishonwi .

mikunga jumba .ilikuwa ikiuzwa .mihogo jembe .mikalatusi uele .vimepikwa ukisongwa .ukisongwa linaoshwa .mitume jani .kutawavutia itashonwa .majina muhogo .zitashonwa yananukia .yananukia palijengwa - palijengwa kunalimwa - kunalimwa mtaoshwa .kalamu daktari – madaktari ukuta .mikonga gari . Viambishi vya ngeli aliondoka .vichwa jokofu .mtaoshwa ungejengwa .mbavu chambo .ingeangamizwa kimepikwa .vyambo ugonjwa .yanaoshwa kutawavutia .mawele jina .zingejengwa ungalitibika . Viambishi vya majina mtoto – watoto nguo .majembe kichwa .majani mkunga .mikeka uwele .ndwele mkeka .waliondoka ingeangamizwa .kuta kipini – vipini ubavu .majumba mkonga .magonjwa mkalatusi .yangalitibika ulikuwa ukiuzwa .magari mwiro .majokofu mtume . yapo mambo ambayo ni lazima yaangaziwe Baadhi ya mambo haya ni pamoja na: 1.miro 1.46 UMOJA NA WINGI Katika kuangalia uhalali wa umoja ama wingi katika lugha ya Kiswahili.nguo kipofu – vipofu kalamu .

47 .

uwanjani kwetu tunda bovu . Virejeshi –o Virejeshi –o vina asili ya amba.kalamu nzuri shambani pazuri .vyumba vipya kuimba kwema .ambayo inauzwa ambacho kimepotea – ambavyo vimepotea ambayo yalichemka – ambayo yalichemka ambao unauma – ambayo inauma ambao utasongwa .ambazo zingalishonwa ambapo pamelimwa – ambapo pamelimwa ambao ukibomoka . vivumishi umoja na wingi wa vivumishi aidha hutegemea viambishi vya majina au ngeli mbuzi mkubwa .ambao utasongwa ambalo lingeanguka – ambayo yangeanguka ambako kunavutia .shambani pazuri ubao mpana .mikate mitamu uji mtamu - uji mtamu chumba kipya .kuimba kwema kalamu nzuri .mifukoni mweusi .mbao pana uwanjani kwangu .matunda mabovu mfukoni mweusi ugonjwa mbaya .ambayo yatasambaa 1.mbuzi wakubwa miraa kali - miraa kali mkate mtamu .48 1.ambazo zikibomoka ambamo mngeingia .ambako kunavutia ambayo ingalishonwa .na hutegemea ngeli husika ambaye alitoka – ambao walitoka ambayo inauzwa .ambamo mngeingia ambao utasambaa .magonjwa mabaya .

49 .

50

KUKANUSHA
Kukanusha ni kukana, kukataa, kupinga ama kukinza jambo linalosemwa
Kukanusha huhitaji uelewa na ufahamu mwafaka wa nyakati, halina njeo aina
Katika kukanusha, ni silabi ya wakati, hali ama njeo inayobadilika peke yake, hasa kunako
kiarifu.
Mifano:
Chakula kililiwa - chakula hakikuliwa
Mkahawa umefungwa - mkahawa haujafungwa
Kiwiko kinauma sana - kiwiko hakiumi sana
Embe litakatwa vibaya - embe halitakatwa vibaya
Mvua ingalinyesha tungalipanda - mvua isingalinyesha tusingalipanda
Nguo ingeshonwa ingevaliwa - nguo isingeshonwa isingevaliwa
Mkutano ulikuwa ukiendelea tulipowasili - mkutano haukuwa ukiendelea tulipowasili
Uji utakuwa ukikorogwa nitakapoondoka - uji hautakuwa ukikorogwa nitakapoondoka
Sadiki aliniita, nikaenda na akanituma - Sadiki hakuniita, sikuenda wala hakunituma
Garimoshi hupita hapa kila Ijumaa - Garimoshi halipiti hapa kila Ijumaa
Bei ya vyakula yapanda kila leo - Bei ya vyakula haipandi kila leo
Alipofika tuliondoka - Alipofika hatukuondoka

 MATUMIZI YA –kiSilabi –ki- ikiwa katika sentensi huweza kutumika kuleta hali mbalimbali kama
vile:
1. kiambishi cha jina

51

silabi –ki- hutumiwa kuonyesha viambishi vya majina
huonyesha umoja wa majina
mifano:
kiatu - viatu

kigoda - vigoda

kibago - vibago

kijaluba - vialuba

kiboko - viboko

kiduko - viduko

kipofu - vipofu

kibwiko - vibwiko

kibogoyo - vibogoyo

kithembe - vithembe

2. kiambishi cha ngeli
kiambishi –ki- aidha hutumika kama kiambishi cha ngeli cha ngeli ya ki - vi
hutumika kutambulisha ngeli ya nomino husika kwenye fungutenzi
mifano:
chakula kinapikwa – vyakula vinapikwa
chombo kimeoshwa – vyombo vimeoshwa
kibago kiliuzwa jana – vibago viliuzwa jana
kijiko kitapotea – vijiko vitapotea
kitanda kikivunjika wataanguka – vitanda vikivunjika wataanguka
kigoda kingalipotea angalilia – vigoda vingalipotea wangalilia
chambo kingeliwa angeshikwa – vyambo vingeliwa wangeshikwa
chumba kilikuwa kikioshwa – vyumba vilikuwa vikioshwa
3. hali ya masharti
kiambishi –ki- pia hutumiwa kuibua dhana na hali ya masharti katika utokeaji na
ufaulishaji wa vitendo vinavyotajwa
kinapotumiwa palipo na vitenzi viwili, huweka masharti kuwa ili kitendo cha pili
kifaulu, ni lazima cha kwanza kifaulu.

52

Mifano:
Akija nitafurahi – Wakija tutafurahi
Chakula kikipikwa atakila – Vyakula vikipikwa watavila
Mkono ukiumia utatibiwa – Mikono ikiumia itatibiwa
Gari likikwama litavutwa – Magari yakikwama yatavutwa
Nguo ikishonwa itauzwa – Nguo zikishonwa zitauzwa
Ubavu ukivunjika utaungwa – Mbavu zikivunjika zitaungwa
4. hali ya sadfa(maendelezi)
kiambishi –ki- pamoja na kitenzi kisaidizi –kuwa huleta hali ya sadfa katika
utokeaji wa
vitendo viwili ingawa kipo kilichotangulia kutokea.
Mifano:
Alikuwa akioga alipozimia
Kilikuwa kikiundwa kilipovunjika
Mpira ulikuwa ukichezwa ulipotoboka
Basi lilikuwa likienda kwa kasi wakati wa ajali
Maji yalikuwa yakiongezwa walipoanza kuogelea
Mihadarati imekuwa ikiuzwa sana Mombasa
Mvua itakuwa ikipusa tutakapong’oa nanga
Abiria watakuwa wakiandamana gari litakapopita
Ajira za watoto zingalikuwa zikishughulikiwa kisheria
Nguo zingekuwa zikitolewa bure
5. hali ya maelezo (mfanano)
Silabi –ki- hutumiwa vilevile katika kutoa maelezo kuhusu jinsi kitendo
kilivyotokea na hujikuta ikiwa ki ya kielezi

Mifano: Kijigari chake kilikwama njiani Iddi anaringia nani na kijiduka chake kama kizimba? Kijumba chake kama kibanda cha kuku Kikoba chake kimechakaa Kijibaiskeli kile hakina thamani sasa Kijisaa cha Maria hakionyeshi muda vizuri Watu wana majitanda naye Zandiki hulalia kijitanda Kigombe chake cha maziwa ni gofu tu! 7.huchukua nafasi ya neno kama Mifano: Alipigana kishujaa Alijibu maswali kitaalam Walifanya kazi kitumwa Mtoto yeyote asifanyishwe kazi kipunda Mihadarati huuzwa kiharamu Ndoa za mapema ni mambo ya kishirikina Alizungumza nami kibiashara Ajira za watoto ni jambo la kinyama Maulidi alizungumza kilevi Watu wanaowakeketa mabinti wanawatenda kinyama 6.hutumika kunako nomino. ukanusho wa wakati uliopo hali ya kutendeka . kiambishi –ki.53 Maelezo haya pia tunaweza kuyaita kwamba ni ya kulinganisha ama ya tashbihi Silabi –ki. hali ya udogo Katika kuonyesha dharau ama udogo wa nomino.

54 Katika kukataa yanayosemwa katika wakati uliopo hali ya kutendeka.hakiliki Yanamwagika – hayamwagiki Uwanja unafyekeka – uwanja haufyekeki Maji yanazoleka – maji hayazoleki Kitabu kinasomeka – kitabu hakisomeki Mchezo unachezeka – mchezo hauchezeki Njia za kusini zinapitika – njia za kusini hazipitiki Mlima Kilimanjaro unapandika – mlima Kilimanjaro haupandiki Waathiriwa wa ukimwi wanateseka – waathiriwa wa ukimwi hawateseki Anapachika udongo – hapachiki udongo Kasri la gavana linajengeka – kasri la gavana halijengeki . silabi –ka hugeuka na kuwa –ki Mifano: Anabebeka – habebeki Kinalika .

Matumizi ya –kwa.ni pamoja na: 1.55  MATUMIZI YA KWA Kwa ni kiunganishi ambacho huleta dhana tofauti katika sentensi ni lazima kufahamu unalotaka kusema ili wasikilizaji wapate kuelewa kwa ufasaha unalozungumzia. Kwa ya sababu Hutumiwa kuyakinisha sababu ya kitendo fulani kutokea Hujibu swali. kwa nini? Mbona? . kwa ya kitumizi Hutumika kuonyesha kifaa kilichotumika katika kutekeleza kitendo kinachosemwa Mifano: Alinikata kwa kisu – Walitukata kwa visu Kitabebwa kwa gari – Vitabebwa kwa gari Nyama itachemshwa kwa seredani – nyama zitachemshwa kwa seredani Alizungumza kwa simu – Walizungumza kwa simu Ndovu aliuawa kwa risasi – Ndovu waliuawa kwa risasi Shamba linalimwa kwa trekta – Mashamba yanalimwa kwa matrekta Mti umekatwa kwa msumeno – Miti imekatwa kwa misumeno Ujumbe husambazwa kwa gazeti – jumbe husambazwa kwa magazeti Mwanajeshi alifika Kismayu kwa jahazi – Wanajeshi walifika Kismayu kwa majahazi Walevi alipigana kwa kijiti – Walevi walipigana kwa vijiti Mpunga ulitwangwa kwa mchi – Mipunga ilitwangwa kwa michi 2.

Kwa mahali Huonyesha mahali panapotajwa kuwa ni pa mtu fulani Mifano: Amelala kwa Juma Mtoto mzuri alitumwa kwa babu Miti mizuri ilipandwa kwa mjomba Nyumbani kwa shangazi kuna mikorosho Mgonjwa ataenda kwa daktari Karim Mlingoti uliotiwa kwa Hasani umevunjika Salihina angeenda kwa kasisi angefaulu Gari lilikwama kwa Ali Risasi zilisikika kutoka kwa Kauleni 4.56 Mifano: Timu yetu ilishinda kwa bidii zao Alifukuzwa chuoni kwa wizi wake Wanapigana kwa shamba la miwa Alihukumiwa kwa wizi wa mali ya umma Walifungwa kwa kuajiri watoto wadogo Mipaka ya nchi itafungwa kwa mihadarati iliyojaa Shirika la bima lilifungwa kwa visa vya ufisadi Nyumba ilibomoka kwa nyufa za kutani Chombo kinazama kwa kuvuja maji Ndizi zilioza kwa joto jingi Nyama itatupwa kwa kuvunda Dawa ingetengenezwa kwa samli 3. Kwa ya pamoja .

watu watatu kwa kumi ni wagonjwa Katika mitaa ya mabanda. Kwa ya jinsi Huonyesha namna au jinsi gani kitendo fulani kilitokea . wasichana kumi kwa mia wamedhulumiwa kimapenzi 6. Kwa ya sehemu ya kizima (akisami) Hutumiwa kuonyesha kuwa idadi inayotajwa ni sehemu tu ya nzima Huleta dhana ya akisami Mifano: Kumi kwa ishirini Hamsini kwa mia Mmoja kwa watatu Wanafunzi kumi kwa kumi na watano Takriban abiria kumi kwa hamsini hujifunga mikanda salama Karibu wanafunzi sita kwa kumi wameathirika na mihadarati Themanini kwa mia ya wavutaji bangi huugua saratani bila fahamu Katika umati.57 Huonyesha kuwapo vitu pamoja katika mseto wa aina yake Mifano: Ugali kwa nyama Chai kwa mahamri Uji kwa muhogo Wasichana kwa wavulana Wazee kwa vijana Walimu kwa wazazi Maembe kwa machungwa Madaktari kwa wauguzimikate kwa maandazi 5.

58 Mifano: Walipita kwa haraka Jamila hutembea kwa maringo Walijibizana kwa sauti kalikali Walicheza kwa kiburi Maria alijibu maswali kwa ujasiri mkubwa Mashabiki wa Asenali waliimba kwa vishindo Nilinyang’anywa gari langu kwa nguvu Matapeli huzungumza kwa upole sana wanapofanya hila Mwajuma alinifukuza kwa dharau Mvua ilinyesha kwa wingi nchini kote 7. Kwa ya kimilikishi Huonyesha mahali panapotajwa ni mali ya mtu anayesemwa Mifano: Miembe ilipandwa kwangu Magari ya kwetu hupita alfajiri kila Jumamosi Njia za kwenu mjomba zina mashimo sana Nilipita kwako alasiri nikakukosa Nyumbani kwake kuna mbwa wakali kwelikweli Nchini kwao kuna uraibu mkubwa wa mihadarati .

imbeni . Kuyakinisha Silabi ni hutumika katika kuyakinisha jambo linalosemwa kwa vile inavyoleta muktadha wa ukubalifu Mifano: Sadiki ni motto mtiifu sana Nairobi ni mji mkuu wa nchi ya Kenya Kabumbu ni mojawapo wa michezo maarufu Ukimwi ni ugonjwa hatari mno Ajira za watoto ni tisho kubwa kwa kizazi cha halafu Mkandaa ni chai isiyokuwa na maziwa Tasfida ni maneno ya adabu Malenga ni mtunzi wa mashairi Mkonokono ni mganga wa sumu ya nyoka 2.choreni Imba .simameni Chora .hutumika kurejelea miktadha mbalimbali kwa kutegema mahali inapowekwa katika sentensi husika 1. Amri kwa wengi Silabi –ni inapotiwa mwisho wa kitenzi.59  MATUMIZI YA –NISilabi –ni. hugeuka na kuleta muktadha wa amri kwa watu wengi Mifano: Simama .

someni tuhumu .huwa kiwakilishi cha nafsi tegemezi Nafsi inayowakilishwa ni ya kwanza umoja (mimi) Mifano: Nilikipasua kibuyu Nimeliegesha gari kando ya barabara Ninayachota maji ya kufulia Nitapinga sana ajira za watoto Ningalimwona ningalimtuma Sumbawanga Ningejua wanatumia mihadarati ningewashtaki kituoni Nikiyatunza mazingira nchi yangu itakuwa safi Nilikuwa nikipiga jelbe aliponivamia Chakula nilichokipika kililiwa chote Gari lililonibeba lilitokea mjini .sukumeni Kata .bembeeni tembea .60 Kimbia . Kiwakilishi nafsi Katika fungutenzi.lieni cheza .chezeni 3.kateni Soma .taghafalini bebmbea .kimbieni Beba .pigilieni taghafali .tuhumuni hujumu .tembeeni lia .bebeni Sukuma .hujumuni pigilia . silabi ni.

61 Maji yaliyoniletea kichocho ni ya kisimani Walioniuzia mihadarati wameshikwa Aliyeniajiri ananinyima haki yangu ya maisha 4. Mahali Nomino yoyote inapoambishwa –ni mwishoni hugeuka na kuwa mahali na ikahama ngeli asilia na kujumuika katika ngeli ya pa-ku-mu pamoja na kwamba hugeuka na kuwa kielezi cha mahali. Mifano: Shambani anakoishi Mtoni alikoenda Chumbani anamolala Msituni walipofyeka Kichwani palipoumia Pipani walimotia maji Mezani penye vitabu Stanini kwenye katara Kitini nilipokaa Mgongoni anapopaka dawa Bustanini kwenye maua Puani penye pini Shuleni kulikojaa nyasi Mijini kwenya mihadarati hakufai Nyumbani alikoajiriwa mtoto si kuzuri Walichezea uwanjani Gari lilianguka mtaroni Wanafunzi waliingia darasani Maria alienda sokoni .

hawasukumani Yanavutana .62 5. Kiulizi Silabi –ni huwekwa mwisho wa kitenzi na kuibua dhana ya kiulizi Hutumiwa kama kiambishi tamati kiegema cha kiulizi Mifano: Walani? Wachekani? Mwaimbani? Yualiani? Achimbani? Atafanyani? Aliadhibiwani? Aliyeshinda atatuzwani? Waliopigania uhuru walipewani? Wanaogombana watakani? Nchi yetu inagombaniani Kusadikika? Tanbihi: Mbinu hii ya uandishi isitumiwe katika uandishi natharia hasa insha 6.hayavutani Mnakatana .hatupigani Wanasukumana . Kikanushi cha kauli ya kutendana. kutendeana na kutendeshana Katika kukanusha vitenzi katika kauli za kutendana.hamkatani . kutendeana na kutendeshana silabi –ni huwekwa mwisho wa kitenzi Sentensi hizi huwa katika wakati uliopo Mifano: Tunapigana .

hawakatani mchezo Wanachekeshana wao .hawabebeani mizigo Tunapigiana simu .majembe yanayolima hayagongani Wanabebeana mizigo .hawachekeshani wao .hatulishani keki Wanakatazana mchezo .hatupigiani simu Tunakatana makataa .63 Tunaandikiana barua – hatuandikiani barua Majembe yanayolima yanagongana .hatukatani makataa Tunalishana keki .

64  MATUMIZI YA –POSilabi –po. Kilipoanguka palikuwa na tope jingi Yalipokwama palijaa heroe.hutumiwa kurejelea wakati wa tukio Mifano: Alipofika tuliondoka Iliponyesha tulianza shughuli za upanzi Linapoanguliwa hutoa kifaranga Zinapooshwa hutakata ghaya Yalipomwagika walilala njaa Mihadarati inapotumiwa humfanya mraibu kuwa mtumwa Mazingira yanapotunzwa nchi hukua . Walipobomoa patazibwa kwa mawe. Wakati Silabi –po.ikitumiwa katika sentensi. Jumba lilipojengwa palikuwa makao ya wakoloni. Alipouficha mkuki pamejulikana. Alipofyeka patatumika kulishia wageni. huleta ama huibua dhana mbili: 1.hutumiwa kurejelea mahali pa tukio Aghalabu ngeli inayohusika ni pa-ku-mu Mifano: Alipojenga pana kinamasi. Panapowasumbua waashi kujenga ni mwambani. Mahali Silabi –po. 2.

65 Tunapoyahifadhi maji kilimo kitakuwa Tunapodumisha ndoa za mapema tunaangamiza nchi .