You are on page 1of 1

TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

WANAFUNZI WASIO NA SIFA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa zoezi la
uhakiki wa sifa za wanafunzi wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya
Elimu ya Juu nchini kwa mwaka 2016/2017 limekamilika katika baadhi ya
vyuo. Katika kutekeleza zoezi hilo Tume imebaini kuwa kuna wanafunzi
ambao wamedahiliwa katika programu ambazo hawana sifa.

Orodha ya wanafunzi wasio na sifa imeshawasilishwa kwenye vyuo husika.
Hivyo, wanafunzi wote wanaondelea na masomo kwenye Vyuo vya Elimu ya
Juu nchini wanaweza kutazama matokeo ya uhakiki wao kupitia kiunganisho
(link) (Bonyeza Uhakiki wa Sifa za Udahili).

Tume inawaarifu wanafunzi wote ambao majina yao yameorodheshwa
wawasiliane na vyuo vyao ili kuthibitisha sifa zao kabla ya tarehe 28 Februari
2017. Wanafunzi ambao hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na Tume na
hivyo kukosa sifa za uanafunzi.

TCU inatoa rai kwa wanafunzi wote kutembelea tovuti ya Tume
(www.tcu.go.tz) mara kwa mara ili kupata taarifa mpya kuhusu uhakiki wa
sifa za wanafunzi.
Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
20/02/2017