JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Tele: +255 0262322761-5 Ofisi ya Bunge
Fax No. +2550262324218 S.L.P 941
Email:info@bunge.go.tz DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
________
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job
Ndugai amemtumia Salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mheshimiwa Freeman Mbowe
kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini 2000 -
2015, Mheshimiwa Philemon Ndesamburo kilichotokea leo Mkoani
Kilimanjaro.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mheshimiwa Philemon
Ndesamburo ambaye pia ni baba wa Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa
Lucy Owenya kilichotokea leo Mkoani Kilimanjaro, hakika ni pigo kubwa”
alisema.

“Natoa pole kwa Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Mbowe, ndugu,
jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu. Namuomba Mwenyezi
Mungu awape nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” aliongeza
Mheshimiwa Spika

Aidha, Mheshimiwa Spika amesema Marehemu atakumbukwa kwa
uchapakazi wake wakati akiwa mbunge hasa katika kutetea wananchi wa
jimboni kwake.

"Namkumbuka vyema Marehemu Ndesamburo na tuliingia Bungeni pamoja
mwaka 2000, alikuwa na mapenzi makubwa kwa wapiga Kura wake."
alisema Mheshimiwa Spika

Imetolewa na:
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano,
Ofisi ya Bunge,
Dodoma.

31 Mei, 2017.