You are on page 1of 1

Na DERICK MILTON-SIMIYU

SERIKALI imesema watumishi wa umma ambao walikutwa na vyeti feki na baadaye wakakata
rufaa wakieleza vyeti vyao viko sahihi, hatima yao itajulikana mwishoni mwa mwezi huu,
uamuzi utakapotolewa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Dk. Laurian Ndumbaro, wakati akiongea na watumishi wa halmashauri sita za
mkoa wa Simiyu, wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani hapa.

Ndumbaro alisema hatua mbalimbali zinaendelea kwa wale wote waliokata rufaa kuhakiki upya
vyeti vyao kama kweli ni sahihi kama wao walivyoeleza wakati wanakata rufaa.

Mbali na kueleza hayo, Ndumbaro hakuweza kutaja idadi ya watumishi waliokata rufaa kati ya
wale waliokutwa na vyeti feki na kubainisha kuwa rufaa hizo zinapitiwa kwa umakini, ili kubaini
kama ni kweli au la.

Tunatarajia hadi kufikia tarehe 30, mwezi Juni mwaka huu, wale wote ambao walikata rufaa
baada ya kubainika wana vyeti feki tutatoa majibu ya rufaa zao, ambazo tulikuwa tunaendelea
kuzipitia kwa makini, alisema Ndumbaro.

Hivi karibuni Rais Magufuli aliwafukuza kazi zaidi ya watumishi wa umma 9,000, baada ya
kupokea ripoti kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, iliyoonyesha wana vyeti feki.

Mbali na hilo, katibu huyo alisema serikali inakamilisha hatua za mwisho kutangaza ajira
mbalimbali ifikapo Julai, mwaka huu, ili kuweza kujaza nafasi mbazo watumishi wake
wamefukuzwa kazi, kutokana na zoezi la vyeti feki.

Kwenye kikao hicho, kilichofanyikia katika ukumbi wa KKKT Bariadi, Katibu Mkuu huyo
aliwataka wakurugenzi wa halmashauri zote kuwachukulia hatua za haraka watumishi wa umma
ambao wamekuwa wakidhalilisha utumishi wa umma.

You might also like