You are on page 1of 23

NCHI YETU

Jarida laSanaa
Utamaduni, Mtandaoni
na Michezo

TOLEO NA.6 Limeandaliwa na Idara ya TOLEO MAALUM: JULAI-AGOSTI, 2017


Habari-MAELEZO

Hoima-Tanga
Ni Safari ya Kihistoria, Tunatekeleza

www.maelezo.go.tz
i Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Bodi ya Uhariri
Mwenyekiti
Dkt. Hassan Abbasi
Mkurugenzi-Idara ya Habari-MAELEZO
Wajumbe
Rodney Thadeus
John Lukuwi
Elias Malima
Jovina Bujulu
Lilian Lundo

Wasanifu Jarida
Hassan Silayo
Benedict Liwenga

Huduma zitolewazo MAELEZO


1.Kuuza picha za Viongozi wa Taifa na matukio muhimu
ya Serikali.
2.Kusajili Magazeti pamoja na Majarida
3.Kukodisha ukumbi kwa ajili ya mikutano na Waandishi
wa Habari.
4.Rejea ya Magazeti na Picha za Zamani
5.Kupokea kero mbalimbali za wananchi.

Jarida hili hutolewa na:


Idara ya Habari-MAELEZO
S.L.P 8031
Dar es Salaam-Tanzania
Simu : (+255) 22 -2122771
Baruapepe:maelezo@habari.go.tz
Blogu: blog.maelezo.go.tz
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO ii
TAHARIRI
AMANI IMEREJEA BURUNDI,WAKIMBIZI RUDINI MKAJENGE NCHI YENU
Hivi Karibuni Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli, katika ziara ya kikazi katika mikoa ya kanda ya
ziwa akiwa wilayani Ngara, alitoa wito wa kuwataka wakimbizi raia wa Burundi kurejea nyumbani kwa kuwa
hali ya usalama nchini humo imetengemaa.

Wito huo wa Mheshimiwa Rais uliungwa mkono pia na Rais wa Burundi Mheshimiwa Pierre Nkurunziza
ambaye alikuwa Mkoani Kagera kwa ziara ya siku moja kwa mwaliko wa Rais Magufuli.
Katika wito wake huo, Rais Magufuli aliweka bayana kuwasiwafukuzi wakimbizi hao bali nawashauri tu
kurejea nyumbani kwa hiari yenu kwa kuwa nimethibitishiwa na Rais Nkurunziza kuwa hali nchini Burundi ni
shwari.

Tunaunga mkono wito wa Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kuzingatia kuwa kuwepo nchini kwa raia hao
wa Burundi ni kutokana na hali ya usalama nchini mwao kuwa hatarishi hivyo walikuja Tanzania kunusuru
maisha yao.

Tanzania ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ina wajibu wa kuwapokea wakimbizi kama
zinavyowajibika nchi nyingine wanachama ili kuwanusuru na kuwahifadhi raia wanaokimbia nchi zao
kutokana na machafuko ya kisiasa na majanga yanayofanana na hayo.

Kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza wajibu huo ambapo imekuwa
ikiwapokea raia wa nchi mbalimbali wanaokimbia vita, machafuko, migogoro inayotishia amani na
usalama wao na hata wale wanaokimbia ukandamizaji katika nchi zao.

Katika kufanya hivyo, Tanzania imekuwa ikitumia rasilimali zake nyingi kuwasaidia raia hao hata kama
kumekuwepo na usaidizi kutoka jumuiya ya kimataifa. Ni vyema kila Mmoja kufahamu kuwa kuwepo kwa
wakimbizi nchini kumekuwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi, kimazingira na kijamii.

Tunapenda kukumbusha kuwa ilifika wakati katika kilele cha migogoro katika nchi jirani, katika Wilaya ya
Ngara, mkoani Kagera wakimbizi walikuwa wengi kuliko wenyeji na wakati fulani kambi kubwa kabisa ya
wakimbizi duniani ilikuwa Tanzania.

Kwa hivyo, wito wa Mheshimiwa Rais kuwataka wakimbizi kurejea nyumbani wakati huu hali ya usalama
ikiwa imetengemaa nchini Burundi umezingatia hali halisi ya nchi zote Burundi na Tanzania.

Kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa kuna wakimbizi wapatao 247, 000 kutoka nchini Burundi katika makambi
ya wakimbizi ambayo mengine yao yapo katika mpaka kati ya nchi hizi mbili.

Katika wito wake huo Rais Magufuli aliiagiza pia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kusitisha mara moja
kuwapa uraia wakimbizi kutoka Burundi. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2006 na 2007
wakimbizi 160, 000 raia wa Burundi walipewa uraia wa Tanzania na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka hadi
kufikia 200,000.

Kupatiwa uraia wa Tanzania wakimbizi hao raia wa Burundi ni muendelezo wa hisani na ukarimu wa
watanzania kwa ndugu zao wa kiafrika na zaidi kutekeleza wito wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
kuwataka waafrika waoneshe ukarimu zaidi kwa waafrika wenzao.

Tanzania imetekeleza wajibu wake na watanzania wameonesha ukarimu wao kwa raia hao wa Burundi
kwa kuwapokea kwa mikono miwili na kuwapa kila aina ya msaada na ushirikiano waliohitaji wakati wote
wakiwa nchini.

Wahenga walinena kupeana ni kikoa toa na wewe upewe basi ni matarajio ya watanzania wote kuwa
raia hao wa Burundi nao wataitikia wito wa marais wetu na kukumbuka uungwana wa wenyeji wao na kwa
kurejea nyumbani kwa hiari yao ikiwa ni nia mojawapo ya kuonesha shukrani zao kwa ndugu na marafiki
zao wananchi wa Tanzania.
1 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Hoima-Tanga:Ni Safari ya Kihistoria,


Tunatekeleza

Lakini pia ni bomba Haikushangaza kuona katika


Na Dkt. Hassan Abbasi linaloendelea kuiweka Tanzania hotuba yake ya utangulizi,
na Uganda katika nafasi ya akitumia lugha adhimu ya

M iaka mitano iliyopita


maisha ya wakazi 4,000
hivi wa rasi ya Chongoleani nje
kimkakati zaidi kiuchumi na
kisiasa katika ukanda wa
Afrika Mashariki na duniani.
Kiswahili mara kadhaa, Rais
Yoweri Museveni alikumbusha
mengi ya historia na kuuita
kidogo ya jiji la Tanga, huenda uzinduzi huo kuwa: ni
yalikuwa kama maisha ya Kwa viongozi wakuu wote, uthibitisho wa undugu wa
wakazi wengine wa Pwani ya akiwemo Makamu wa Rais, Watanzania na Waganda.
uvuvi na uvunaji wa chumvi. Mama Samia Suluhu Hassan
na hata Waziri Mkuu, Kassim Shujaa wa mradi huo akatajwa
Wakati maisha ya wakazi wa Majaliwa, walipopata fursa kutoka kinywani mwa Rais
Chongoleani yakiendelea adhimu ya salaam katika uzinduzi Museveni alipotoa siri akisema:
kuwa hivyo, kwa sadfa tu, hali huo, hawakusita kuonesha Nafuu kubwa za kodi
ni kama hiyo kwa ndugu zao bashasha yao na sura ya kuwapa tulizopewa na Rais Magufuli
umbali wa takribani kilometa matumaini wana Chongoleani kama vile kodi ya ongezeko
1500 katika ukanda wa Pwani na wenzao wa Hoima. la thamani na nyingine nyingi
ya Ziwa Albert huko Uganda. ni uamuzi wa kukumbukwa.
Kwa furaha zaidi Mama
Kisha jambo moja linatokea: Samia alihitimisha salaam Huenda waliokuwepo pia
ugunduzi wa mafuta katika zake kwa kusisitiza pia msisitizo walishangazwa na bashasha
Ziwa Albert sasa unakwenda wetu wa kila siku kuwa katika nyingi zilizopamba uzinduzi
kuyabadili maisha yao, maendeleo hakuna siasa huo hasa kwa viongozi
uchumi wao na historia yao. na ahadi kwa wananchi ni wakuu. Ipo sababu na sadfa
moja tu: TUNATEKELEZA. nyingine muhimu kuhusu kisa
Ni mradi unaofungua historia cha Chongoleani na Hoima.
kwa Uganda kupata bomba Ni uzinduzi uliojaa historia,
la kwanza lakini ni historia kumbukizi ya undugu Nayo ni: licha ya nchi hizi kungaa
nyingine kwa Tanzania katika na kushuhudiwa mara katika ripoti ya Quantum
miundombinu ya mabomba, kadhaa wakitajwa viongozi Lab taasisi ya Uingereza kwa
baada ya lile la mafuta la wakuu waasisi wa pande Tanzania kuwa ya kwanza
Tanzania-Zambia na la gesi hizi mbili kama Mwalimu kuvutia wawekezaji na Uganda
la Mtwara-Dar es Salaam. Nyerere na Mzee Obote. kuwa ya pili katika EAC, viongozi
Inaendelea Uk. 2
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
2
Inatoka Uk. 1

wetu hawa wana uzalendo mambo ili mradi uje kwetu. vitabaki pia kuwa jambo
unaotokana na kulelewa vyema. Haijapata kutokea, ndio neno la kukumbukwa, na kama
Marais vinara wa mradi huu Mzee la kuhitimisha la Rais Magufuli kutakuwa na wakati murua
Museveni na Mzee Magufuli alipokuwa akieleza faida za wa kumbukizi hii ni pale somo
wote ni zao la malezi mema mradi huo kwa Watanzania kutoka wimbo huo lilivyomfanya
kutoka Chuo Kikuu mashuhuri akionesha namna uzinduzi huo tu Mhe. Rais kuwakutanisha
katika ukanda huu na duniani tayari ulivyoifanya Chongoleani viongozi vijana wawili Ruge
cha Dar es Salaam (UDSM). na Tanga kufurika na kungaa. Mutahaba na Paul Makonda
na wakapeana mikono.
Viongozi hawa pia pale UDSM Kibwagizo cha Ishi na Mimi
wamesoma taaluma zilizokuwa kutoka kwa wasanii nyota Hivi ndivyo safari ya kihistoria na
muhimu kuamua mradi huu. wa wakiongozwa na Mrisho iliyosheheni bashasha ilivyoanza
Wakati Museveni alianzia sheria Mpoto Mjomba kilitosha Pwani ya Chongoleani,
kisha akahamia darasa la kuwathibitishia viongozi safari ya kazi, na safari ya
sayansi ya siasa, Mzee Magufuli wanasayansi hao kuwa kilometa 1,445 itakayoishia
alisoma sayansi ya kemia. hawakukosea kufikia mradi katika Pwani ya Ziwa Albert.
huu na kilikuwa ukumbusho
Sayansi ya siasa na sayansi ya tosha kwa wananchi juu ya Ni safari itakayopita katika
kemia zilikuwa muhimu katika umuhimu wa kuishi salama na nyakati za kiza, mwanga,
kuamua kwa nini mradi huu mradi huo, kuutunza na kuuenzi. baridi, joto na jua kali, milima
upitie Tanzania na si kwingineko. na mabonde lakini kama
Wakati Ishi na Mimi walivyosema wasanii wetu na
Ndio maana naye aliposimama ikihamasisha mapenzi kwa walivyosisitiza Marais wetu ni
kuhutubia katika mradi huo, mradi huo, huenda uzinduzi safari tunayopaswa kuishi nayo.
Rais Magufuli, alishadidisha wa Chongoleani ukawa
dhana hii ya sayansi za siasa na changamoto kwa wasanii
kemia kusaidia kufikiwa mradi wenzao wa kundi la Wagosi
Nafuu kubwa za kodi
huu na akatoa siri aliposema: wa Kaya ambao huenda tulizopewa na Rais
Pamoja na Mzee Museveni baada ya awali kuimba wakihoji Magufuli kama vile
kuwa ndugu wa Watanzania Tanga kunani mbona kila kitu
lakini katika mradi huu kimekufa sasa watalazimika
kodi ya ongezeko la
alifuatwafuatwa sana kutaka kupitia upya mashairi yao. thamani na nyingine
mradi usije Tanzania. Lakini nyingi ni uamuzi wa
namshukuru kwa kusimamia Na mwishowe uzindushi wa
udugu huo. Na sisi ilibidi bomba Chongoleani na
kukumbukwa
kuchomekea baadhi ya kibwagizo cha Ishi na Mimi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais


wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi
mbalimbali wa Serikali.
3 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Dondoo Muhimu Kuhusu Mradi wa


Bomba la Mafuta Hoima-Tanga
M radi huu wa Bomba la
Kusafirisha Mafuta Ghafi
kutoka Hoima nchini Uganda
Bomba la Gesi Asilia kutoka
Madimba Mtwara
Kinyerezi Dar es Salaam
hadi
TULLOW Oil ya Uingereza na
China National Offshore Oil
Corporation (CNOOC) ya
hadi Bandari ya Tanga, Tanzania na Bomba la kusafirisha China. Bomba hili litakuwa na
unajulikana kama East African mafuta kutoka Tanzania urefu wa kilometa 1,445 kutoka
Crude Oil Pipeline (EACOP). hadi Zambia (TAZAMA). Hoima Uganda hadi Bandari
ya Tanga Tanzania. Makisio
Mradi wa Bomba la Kusafirisha Hali ya tambarare katika ardhi ni uwepo kwa mapipa bilioni
Mafuta ghafi kupita Tanzania ya Tanzania hivyo gharama 6.5 (reserve) na yanayoweza
ulitangazwa na Rais wa Jamhuri za utekelezaji kuwa rahisi. kuchimbwa ni kuanzia mapipa
ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Bilioni 1.2 -1.7 (recoverable).
Museveni wakati wa mkutano Tamko la Pamoja
wa 13 wa Ushoroba wa Kaskazini Tamko la pamoja la kukamilika Gharama
ambapo alieleza kuwa, Bomba kwa majadiliano ya vipengele Ujenzi wa Bomba hili la mafuta
hilo la mafuta kutoka Hoima vya Mkataba kuhusu utekelezaji utagaharimu jumla ya Dola za
Ziwa Albert nchini Uganda wa Mradi husika lilisainiwa Marekani Bilioni 3.55 na litakuwa
litapita katika ardhi ya Tanzania tarehe 21 Mei, 2017 jijini Dar es na urefu wa kilomita 1,445
kwenda Bandari ya Tanga. Salaam na Rais wa Jamhuri ya ambapo litasafirisha mapipa
Muungano wa Tanzania Mhe kati ya laki mbili (200,000) na laki
Aidha, sababu zilizochangia Dkt. John Pombe Magufuli na mbili na kumi na sita elfu (216,000)
bomba hilo kupita Rais wa Jamhuri ya Uganda kwa siku. Kati ya kilomita hizo,
ni nchini pamoja na; Mhe. Yoweri Kaguta Museveni. kilometa 1,149 zitajengwa
Ubora wa bandari ya Tanga ndani ya ardhi ya Tanzania.
ambayo imeonekana kuwa Kusaini Mkataba
bora zaidi ukilinganisha Waziri wa Katiba na Sheria Faida za mradi huu
na bandari nyingine Afrika wa Tanzania, Profesa Ujenzi wa Mradi huu
Mashariki kwa kuwa ina Paramagamba Kabudi unatarajiwa kuzalisha ajira
kingo za asili (naturally pamoja na Waziri wa Nishati zaidi ya 11,000 za muda
sheltered) na kina kirefu na Maendeleo ya Madini mfupi na za kudumu
cha futi 25 kwenda chini wa Uganda, Mhandisi Irene Kuchochea utafutaji wa
hivyo kupunguza muda Muloni tarehe 26/5/2017, mafuta nchini Tanzania
na gharama za ujenzi kwa walisaini mkataba wa na nchi jirani hususani
kuwa uchimbaji wa kina INTERGOVERNMENTAL katika maeneo linapopita
hauhitajiki. Aidha, bandari AGREEMENT ( IGA)- yaani bomba la mafuta.
hiyo itakuwa na uwezo Mkataba wa Ushirikiano kati ya Kuimarisha matumizi ya
wa kupakia mafuta katika Serikali ya Uganda na Tanzania bandari ya Tanga na hivyo
kipindi cha mwaka mzima. kwa ajili ya utekelezaji wa kuongeza mapato ya Serikali
Miunganiko wa njia ya reli ujenzi wa bomba la kusafirisha kutoka katika bandari hiyo
ya Tanga hadi reli ya kati. mafuta ghafi (crude oil) kutoka pamoja na kupatikana
Miundombinu ya barabara Hoima nchini Uganda hadi mkuza utakaoweza kutumika
nyingi ambayo haipo katika Bandari ya Tanga- Tanzania. siku za baadaye kwa shughuli
njia Mbadala za nchi Jirani. nyingine za maendeleo.
Usalama na uzoefu wa Utekelezaji Ujenzi wa barabara mpya,
Tanzania katika ujenzi wa Mradi huo mkubwa uboreshaji wa barabara
mabomba yakiwemo utatekelezwa kwa ushirikiano wa zilizopo na madaraja katika
Bomba la Gesi Asilia kutoka Serikali za Uganda na Tanzania maeneo linapopita bomba.
Kisiwa cha Songo Songo na pia utahusisha kampuni Kufungua Mkuza
mpaka Ubungo-Dar, za TOTAL E & P ya Ufaransa, wa Miundombinu
Inaendelea Uk. 4
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
4
Inatoka Uk. 3

unaounganisha nchi
za Maziwa Makuu
zisizopakana na bahari na
na
Njia ya Bomba la Mafuta
Kutoka Hoima (Uganda)
hivyo kuipa bandari ya Tanga
fursa ya biashara mpya.

hadi Tanga (Tanzania)


Fursa wakati wa ujenzi
Karakana za
ukarabati wa mashine
mbalimbali na magari.
Huduma za Sheria.
Mawasiliano na kandarasi za
kusambaza vifaa vya ujenzi
na usafirishaji wa mabomba.
Huduma ya vyakula.

Njia ya bomba la mafuta ghafi


Bomba hili litaingilia Mkoa
wa Kagera kutoka nchini
Uganda na kupita katika
Mikoa ya Geita, Shinyanga,
Tabora, Singida, Dodoma na
Manyara hadi bandari ya
Tanga. Bomba hili linatarajia
kukamilika mwaka 2020.

Watumiaji wengine wa bomba


nje ya Tanzania
Nchi zinazotarajiwa kutumia
bomba hilo kwa miaka ijayo
ni pamoja na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Sudan
Kusini, Burundi na pia nchi
nyingine za Afrika Mashariki.

Eneo itakapojengwa gati Gati


Itajengwa nje kidogo ya mji
wa Tanga katika eneo la
Chongoleani.

Shughuli za Utafiti
Zoezi la utafiti wa nchi kavu na
baharini limefanywa. Tayari
sampuli za udongo na maji
zimekwishapatikana kwa ajili
ya uchunguzi wa takwimu
mbalimbali za kihandisi.
Maeneo sita (6)
yamekwishachimbwa visima
vya sampuli za udongo
katika awamu ya kwanza.
Utafiti wa njia nzima ya
bomba unaendelea kwa
kuanza kuwashirikisha wadau
wote wa Mikoa ambayo
bomba litakapopita.
5 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Inatoka Uk. 1

UCHUMI WA TANZANIA WAZIDI KUIMARIKA


Na Bushiri Matenda-MAELEZO

L
wa
icha ya kuyumba kwa uchumi
na kuongezeka kwa mfumuko
bei duniani, Tanzania
imeendelea kuongoza kwa
ukuaji wa uchumi miongoni
mwa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambapo takwimu
za Benki Kuu ya Tanzania
(BOT) na Shirika la Fedha la
Kimataifa (IMF) zimetaja uchumi
wa Tanzania kuwa imara.

Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) na Msemaji
Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan
Abbasi alibainisha hayo
wakati akitoa ufafanuzi kwa
Waandishi wa Habari Wiki
iliyopita Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
kuhusu hali ya uchumi nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi
alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi mbele ya
Uchumi wa Tanzania kwa miaka
mitatu mfululizo sasa bado uko
Waandishi wa Habari Wiki iliyopita Jijiji Dar es Salaam.
katika ukuaji usiopungua asilimia
7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa za taasisi ya Quantum Global kazi maoni hayo ya IMF na Benki
juu katika ukanda wa Afrika Research Lab ya Uingereza ya Dunia na kwamba mabadiliko
Mashariki ambapo Rwanda kuhusu Farihisi ya Uwekezaji Afrika makubwa yamefanyika katika
inakua kwa asilimia 6, Uganda ambazo zilionesha Tanzania kupambana na rushwa na
asilimia 5 na Kenya asilimia ikiongoza miongoni mwa nchi kudhibiti mapato ya Serikali
6.4, alisema Dkt. Abbasi. za Afrika Mashariki na ya nane ambapo ukusanyaji wa mapato
Barani Afrika, ikiwa imepanda umeongezeka kutoka wastani
Alieleza kuwa sambamba na kutoka nafasi ya 19 mwaka 2015. wa shilingi bilioni 925 kwa
ukuaji wa uchumi, Tanzania mwaka 2015 hadi shilingi trilioni
imeendelea kudhibiti mfumuko Mashirika ya Kimataifa kama 1.069 kwa mwaka 2016/17
wa bei ambapo taarifa ya IMF, Benki ya Dunia katika ripoti ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.
hivi karibuni zilizotolewa na zao za hivi karibuni yamesisitiza
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kuwa uchumi wa Tanzania ni Dkt. Abassi ambaye pia ni
zinaonesha kuwa mfumuko imara na wamesifu mageuzi Msemaji Mkuu wa Serikali,
wa bei nchini umeshuka makubwa yanayofanywa na alieleza kuwa kutokana na
kutoka asilimia 6.1 mwezi Mhe. Rais Dkt. John Pombe uchumi wa Tanzania kuwa
Mei hadi kufikia asilimia 5.4 Magufuli, alieleza Dkt. Abbasi imara kumeiwezesha Serikali
mwezi Juni mwaka huu. na kusema kuwa mashirika hayo kufanya maboresho makubwa
yameitaka Serikali iendeleze katika sekta mbalimali zikiwemo
Aidha, Mkurugenzi Dkt. Abbasi mapambano zaidi dhidi rushwa afya, elimu, miundombinu na
alieleza kuwa katika eneo la na udhibiti wa mapato ya Serikali. nishati ambapo katika sekta ya
mazingira bora ya uwekezaji, afya Serikali imetenga shilingi
Tanzania imeendelea kufanya Alieleza kuwa Serikali ya Awamu trilioni 1.077 kwa mwaka wa
vizuri ambapo alitoa takwimu ya Tano imeendelea kufanyia fedha 2017/18 kulinganisha na

Inaendelea Uk. 3
Inaendelea Uk. 6
Jarida la Nchi Yetu 2016
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
Tuimarishe Uchumina
Limeandaliwa wa Viwanda
Idara kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO 6
Inatoka Uk. 5 uchumi imara, Tanzania
imeendelea kutekeleza
miradi mbalimbali mikubwa
ya maendeleo ikiwemo ile ya
umeme, maji, reli ya kisasa,
barabara na pia mradi wa ujenzi
wa bomba la mafuta kutoka
Hoima nchini Uganda mapka
Tanga nchini Tanzania, ambapo
mradi huu unatekelezwa kwa
pamoja na nchi hizo mbili.

Uchumi wa Tanzania kwa


miaka mitatu mfululizo
sasa bado uko katika
ukuaji usiopungua asilimia
7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji
wa juu katika ukanda wa
Taarifa kutoka Benki ya Dunia ikionesha nchi ambazo uchumi Afrika Mashariki ambapo
wake unakuwa kwa kasi Rwanda inakua kwa
shilingi bilioni 796 zilizotengwa kufikia shilingi bilioni 475 na asilimia 6, Uganda asilimia
mwaka fedha 2016/17. kwa mwaka 2016/17 bajeti ya 5 na Kenya asilimia 6.4,
mikopo ya elimu juu iliongezeka
Alieleza kwa kwa upande hadi kufikia shilingi bilioni 483.
alisema Dkt. Abbasi.
dawa na vifaa tiba, Serikali ya Alieleza kuwa kutokana na
Awamu ya Tano imeendelea
kutekeleza ahadi yake kwa
kuongeza fedha katika ununuzi
wa dawa ambapo katika
kipindi cha miaka mitatu fedha
za ununuzi wa dawa na vifaa
tiba zimeongezea kutoaka
shilingi bilioni 30 mwaka 2015/16
mpaka kufikia shilingi bilioni 261
katika bajeti ya mwaka 2017/18.

Katika kuhakikisha Watanzania


wengi wanaelimika, Serikali
imeendelea kutoa elimu bure
kuanzia darasa la kwanza
hadi kidato cha nne ambapo
takribani shilingi bilioni 18
hutumika kwa mwezi na
zinawafikia walengwa na kwa
wakati, alieleza Dkt. Abbasi

Dkt. Abbas alingeza kuwa


wakati Serikali ya Awamu ya Muonekano wa Juu wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni
Tano inaingia madarakani kiungo muhimu cha ukuaji wa Uchumi
kulikuwa na shilingi bilioni 341
kwa ajili ya mikopo ya elimu
ya juu lakini Rais John Pombe
Magufuli akaongeza hadi
7 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Tanzania Yapaa Kimataifa Usafiri wa Anga


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Tanzania kupitia Mamlaka


ya Usafiri wa Anga
Tanzania (TCAA) imefaulu
ukaguzi wa kimataifa wa
The International Civil
Aviation Organization
(ICAO) kwa kupata asilimia
64.7 juu ya viwango vya
Kimataifa vya asilimia 60.

Mkurugenzi Mkuu wa
mamlaka hiyo Hamza Johari
anaeleza kuwa mara ya
mwisho Tanzania ilikaguliwa
mwaka 2013 na kupata
asilimia 37 ambapo kwa sasa
imeweza kufaulu kwa zaidi Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga (TCAA) Bw. John Chacha akipokea tuzo ya Kimataifa ya
ya asilimia zinazohitajika.
Usafiuri wa Anga iliyotunukiwa na Shirika ;la Kimataifa la Usafiri
wa Anga Duniani (ICAO) na Rais wa Shirika hilo
Kwa kuwa nchi imeweza Dkt. Olumuyiwa Aliu.
kufaulu na kuongeza alama
za ufaulu kwa asilimia 100 na na sekta ya utalii nchini. nyingi kwa wakati mmoja
itatunikiwa cheti na nishani Bw. Johari anasema kuwa jambo ambalo litavutia
ya Rais wa ICAO mwishoni TCAA inafunga rada nne ndege nyingi kuja nchini na
mwa mwaka 2017, katika Uwanja wa Ndege hatimaye kukuza utalii na
anasema Mkurugenzi huyo. wa Kimataifa wa Julius kuongeza mapato ktika sekta
Nyerere (JNIA), Kilimanjaro ya usafiri wa anga na utalii.
Johari alizitaja faida za International Airport (KIA),
kutunukiwa cheti na Shirika Uwanja wa Ndege wa Mkurugenzi huyo anafafanua
hilo la ICAO ni pamoja na Kimataifa wa Songwe na kwa kusema kuwa TCAA
nchi kuaminika kimataifa, Uwanja wa Ndege wa inaendelea kudhibiti vyuo
kuongezeka kwa ndege za Kimataifa wa Mwanza. vyote vinavyotoa elimu
kimataifa kwa kuwa Tanzania katika sekta ya anga kwa
inakuwa imeaminika Ufangaji wa rada hizo kuvipatia ithibati na vyeti
kimataifa katika usalama wa utaongeza usalama na pamoja na kuboresha Chuo
anga na pia kuvutia zaidi kuhakikisha zaidi katika cha Usafirishaji nchini (NIT)
watalii kuja nchini kutokana viwanja hivyo vya ndege kwa lengo la kupunguza
kuongezeka kwa safari na pia kuongeza ufanisi gharama za kupeleka
za ndege nchi na hivyo katika kuongoza ndege Watanzania kusoma fani
kuongeza mapato kwa TCAA ambapo zitakuwa na ya urubani nje ya nchi.
uwezo wa kuongoza ndege
Inaendelea Uk. 8
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO 8
Inatoka Uk. 7

Akizungumzia mashirika ya za kimaandishi kwa shirika Johari anaeleza kuwa


ndege nchini, Mkurugenzi husika, Baraza la watumiaji Serikali ya China itaipatia
huyo ameyataka mashirika na kwa mkurugenzi mkuu Serikali ya Tanzania Dola
hayo nchini kufuata wa mamlaka ya usafiri wa za Kimarekani milioni moja
sheria na miongozo anga alifafanua Bw. Johari. kupitia Shirika la Anga
mbalimbali zilizowekwa Duniani ili kuweza kuboresha
na sekta ya anga nchini. Katika jitihada za kuboresha baadhi ya miundombinu
sekta ya anga nchini, katika Sekta hiyo.
Aidha, Bw. Johari anawataka
watoa huduma katika
sekta ya anga kuwajibika
ipasavyo endapo watumiaji
wa huduma hiyo watapata
tatizo kwa makosa ya
uzembe wa shirika husika.

Iwapo mtumiaji wa huduma


ya usafiri wa anga atapata
tatizo la ucheleweshaji wa
ndege anatakiwa alipwe
dola 6000, upotevu wa mizigo
anatakiwa alipwe dola 1500,
kama ni ajali mtoa huduma
anapaswa kulipa dola 120,000 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini
na kuendelea na mtumiaji
Kuwait ,Mhandisi Yousef Al Fozan (kushoto) wakibadilishana hati za
wa huduma ya usafiri wa makubaliaono ya Usafiri wa Anga baina ya Kuwait
anga atatakiwa kutoa taarifa
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
9 Tuimarishe Uchumi na
Limeandaliwa waIdara
Viwanda kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO

Mfumo wa Kielektroniki Waokoa


Mabilioni Serikalini
Na. Frank Mvungi-MAELEZO

Serikali inatarajiwa kuokoa


mabilioni ya fedha kutokana
na kuanza kwa matumizi
ya Mfumo wa Kielektroniki
ulioboreshwa katika
kuandaa Mipango, Bajeti
na Ripoti, ambapo kabla
yakuboreshwa kwa mfumo
huu wastani wa kiwango
cha fedha kilichotumika
ilikuwa ni milioni 50 kwa kila
Halmashauri kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa


Mipango wa Halmashauri ya
Wilaya ya Songea Mkoani
Ruvuma Bw. Shaban Millao Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha Kutoka mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya
Sekta za Umma (Public Sector Systems Streghthen PS3.) unaofadhiliwa na Shirika
wakati wa mafunzo maalum la Maendeleo la Kimataifa la Marekani (USAID) Bw. Gemini Mtei akizungumza
kuhusu mfumo huo wa wakati wa mafunzo hayo hivi karibuni Mjini Mtwara.
kuandaa Mipango na Bajeti
za Mamlaka ya Serikali za Gharama za kuchapisha 9.25, fedha ambazo sasa
Mitaa (PlanRep) yaliyofanyika vitabu vya bajeti na Mipango zitaweza kuelekezwa katika
Mjini Mtwara na kuwashirikisha katika Halmashuri zetu kwa miradi mbalimbali ili kwaletea
Waganga Wakuu, Makatibu wastani ni shilingi milioni 4 kwa wananchi maendeleo.
wa Afya, Maafisa TEHAMA, kila mwaka hivyo unaweza
Maafisa Mipango, Wahasibu ukaona kiasi cha Fedha Millao alifanunua kuwa
na Wachumi kutoka katika kitakachookolewa kwa kuwa mfumo huo unawawezesha
Mikoa ya Lindi, Mtwara, mfumo wa sasa utakuwa Maafisa Mipango kutekeleza
Ruvuma na Dar es Salaam. wa kielektroniki ambao majukumu yao popote pale
sasa unaondoa gharama na utasaidia kuimarisha
Fedha zitakazookolewa ni zile zilizokuwa zinatumika mawasiliano katika ngazi
zilizokuwa zikitumika kulipa awali katika mchaka zote za Serikali kwa kuwa
watumishi wa Halmashauri huu, amesisitiza Millao. upatikanaji wa taarifa
na Mikoa masurufu ya mbalimbali kuhusu mipango
safari, gharama za mafuta Kutokana na mfumo huu ya Idara na Halmashauri
ya magari, uchapishaji wa mpya wa Kielektroniki, Serikali kwa ujumla utakuwa rahisi
nyaraka mbalimbali wakati imeweza kuokoa shilingi na wenye kuendana
wa mchakato wa kuandaa milioni 50 kwa kila Halmashauri na mahitaji ya wakati.
bajeti pamoja na uwasilishaji na hivyo kwa Halmashauri Aliongeza kuwa mfumo
wake, ambapo kwa sasa 185 zilizopo nchini, tafsiri huu mpya wa Kielektroniki
kazi hii itafanyika katika yake ni kwamba sasa Serikali umejikita katika kutusaidia
mfumo wa kielektroniki. inaokoa zaidi ya shilingi bilioni kupanga, kuandaa bajeti
Inaendelea
Inaendelea
Uk.Uk.
8 10
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
10
Inatoka Uk. 9

Washiriki wa Mafunzo ya mfumo wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep)
wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa, mafunzo hayo yalihusisha Waganga Wakuu, Mkatibu wa Afya,
Maafisa TEHAMA,Maafisa Mipango, Wahasibu na Wachumi.

na kutoa ripoti ya utekelezaji Kwa upande wake Mratibu mtizamo wa pamoja katika
hali itakayosaidia kuongeza wa PS3 Manispaa ya Mtwara mageuzi haya yanayolenga
tija na usimamizi wa rasilimali Mikindani Bw. Amon Mkocha kuwainua wananchi wa
zinazoelekezwa katika amebainisha kuwa kila kipato cha chini kwa
huduma za jamii kutoka Halmashuri imetoa watumishi kuwapa huduma bora.
na na bajeti iliyopangwa watano waliopatiwa
katika mwa kahusika. mafunzo ya mfumo huo wa Serikali ya Tanzania na USAID
kielektroniki utawapa fursa kupitia mradi wa uimarishaji
Wito wangu kwa Serikali ni wananchi kushirikiki kamilifu wa Mifumo ya Sekta za
kuwa Mikoa na Halmashuri katika kujiletea maendeleo Umma (PS3) imeandaa
zotezitaunganishwa katika na itakuwa rahisi kupima mafunzo haya kwa watumiaji
mfumo huu ambao utaleta matokeo ya mipango husika. wake nchi nzima, Mafunzo
mapinduzi makubwa katika yanatolewa na Wakufunzi
sekta zote za hudu ma za Mfumo huu unalazimisha kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI,
Jamii ikiwemo elimu na kila mtumishi kutimiza wajibu PS3, Wakala ya Serikali
Afya, amesisitiza Millao wake katika eneo lake na mtandao, Ofisi ya Rais Utumishi
Pia Millao alipongeza Ofisi hakutakuwa na visingizio tena na Utawala Bora, Wizara ya
ya Rais TAMISEMI kwa katika kuandaa mipango, Fedha nay Mipango, Wizara
kushirikiana na Mradi wa PS3 kuandaa bajeti, kutekeleza ya Afya na unatarajiwa
unaofadhiliwa na Shirika la na kutoa ripoti kwa wakati. kutumiwa na watumiaji
Maendeleo ya Kimataifa 1500 watakaofundishwa
la Marekani (USAID) amesisitiza Mkocha. matumizi ya mfumo huo.
kwa kufanikisha kuwepo Akifafanua Mkocha
kwa mfumo wa Kitaifa amesema kuwa ni wa kati
utakaochochea maendeleo muafaka kwa watumishi wote
hasa kwa wananchi wa Vijijini. katika Halmashuri kuwa na
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
11 Tuimarishe Uchumi wa
Limeandaliwa Viwanda
na Idara kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO

UWEKAJI JIWE LA MSINGI UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI


HOIMA (UGANDA) - TANGA (TANZANIA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Samia Suluhu Hassan akimpa mkono Rais wa Uganda Yoweri
Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Kaguta Museveni wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la
mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania. Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akiongea wakati
Magufuli akiongea wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa bomba
msingi la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Nchini Uganda hadi
Hoima Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania. Tanga Nchini Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni (mwenye Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakiwa
kofia) wakifunua kitambaa kuashiria kuwekwa kwa jiwe la msingi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
la mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima
Nchini Uganda hadi Tanga Nchini Tanzania.
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
12

KATUNI NA MSAMIATI WA LEO

6
Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na
13 Tuimarishe Uchumi na
Limeandaliwa waIdara
Viwanda kwa Maendeleo Yetu
ya Habari-MAELEZO

TANZANIA JULAI & AGOSTI

Rais Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo
mafupi mara baada kufungua mradi wa ukarabati na kutoka Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia kuhusu
upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora. mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya
Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati
alipoutembelea Agosti 1, 2017.

Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan
Kabudi ambaye anaongoza Timu ya Tanzania akionyesha kitabu chenye ripoti ya nchi kuhusu
katika majadiliano na Kampuni ya Barrick Gold Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika
Corporation baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya kujipima kwa vigezo vya Utawala Bora (APRM)
mazungumzo hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. mara baada ya kuzindua taarifa hiyo.
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
14

NCHI YETU KATIKA HISTORIA

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Rais wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Nyerere akipokea maelekezo kutoka Mwenyekiti akiweka mchanga kwenye tofali wakati akizindua
wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) wakati moja ya jengo enzi za uongozi wake
akikabidhiwa baiskeli ya kwanza iliyotengenezwa na
kiwanda cha Taifa cha Baiskeli.

Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Rais wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Nyerere akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto
wa Usambazaji Maji wa Kijiji cha Ujamaa Butiama za Milenia(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher
wakizindua mradi wa maji wa Mambongo Mkoani
Morogoro.
15 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

JKCIYaokoa Bilioni Tatu za Wagonjwa wa Moyo


Na Agness Moshi-MAELEZO

T aasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI)
ya

imefanikiwa kutoa matibabu


kwa wagonjwa wa moyo
hapa nchini na kuokoa
kiasi cha shilingi bilioni
3.07 ambazo zingetumika
kama wagonjwa hao
wangepelekwa nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa taasisi hiyo,
Prof. Mohamed Janabi
alipokuwa akizungumza na
baadhi ya Wabunge kutoka
nchini Uganda ambao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
walikuja nchini kuona na Ummy Mwalimu (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya
makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya
kujifunza jinsi taasisi hiyo Kikwete hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa
inavyotoa huduma zake. Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Kwa miaka mingi tatizo la kuwa ni pamoja na upasuaji wabunge wa Uganda Bi.
ugonjwa wa moyo limekuwa wa wazi, kubadilisha mishipa,Cecilia Barbara alieleza
likigharimu wagonjwa na kuweka betri za moyo kufurahishwa kwake
Serikali pesa nyingi kwa ajili ya kubwa na ndogo na kutoa na ubora wa huduma
matibabu nje ya nchi kama ushauri kwa wagonjwa. zinazotolewa katika taasisi
vile India na Afrika ya Kusini, hiyo hasa jinsi ilivyoweza
ambapo imekuwa ni vigumu Akizungumzia aina ya kupunguza gharama za
kwa wananchi wa kipato wagonjwa wanaowatibu, matibabu kwa wagonjwa
cha chini kumudu gharama Prof. Janabi alisema kuwa wa moyo wanaotoka katika
hizo, amesema Prof. Janabi. wanatoa huduma kwa watu nchi za Afrika Mashariki.
wote kuanzia daraja la chini
Prof.Janabi alisema kuwa kwa watu wenye kipato Tunahitaji kubadilishana
taasisi hiyo imefanikiwa kidogo na kuendelea. Mbali mawazo kama wana Afrika
kutumia shilingi bilioni 1.65 na kuhudumia wagonjwa wa Mashariki, kwasababu kwa
badala ya shilingi bilioni hapa nchini taasisi ya Moyo kuja hapa tumegundua tuna
4.72 ambazo ni sawa na ya Jakaya Kikwete inatoa vifaa na uwezo wa kupunguza
kupunguza takribani asilimia huduma kwa wagonjwa gharama za matibabu ya
65 ya gharama za matibabu kutoka nchi mbalimbali moyo na tunategemea
kama wagonjwa hao zikiwemo Uganda,Comoro, kuanzisha mradi kama
wangepelekwa nje ya nchi. Yemen , Kenya na Jamhuri huu nchini Uganda japo
ya Kidemokrasia ya Congo. itatuchukua muda kufikia
Alizitaja baadhi ya huduma hatua iliyofikiwa na
za magonjwa ya moyo Kwa upande wake kiongozi Tanzania, Alisema Bi.Cecilia.
zinazotolewa na taasisi hiyo wa msafara wa huo wa
Inaendelea Uk. 16
Limeandaliwa
Limeandaliwa
na Idara
na Idara
ya Habari-MAELEZO
ya Habari-MAELEZO 14
16
Inatoka Uk. 15 wa nne kwa mwaka 2016.

Wahenga walisema kuwa


Ya kale ni dhahabu, ingawa
Rais mstaafu wa awamu
ya nne Dkt. Jakaya Kikwete
amemaliza muda wake
lakini bado anakumbukwa
kwa jitahada zake za dhati
za kufanikisha kuwepo
kwa taasisi hiyo ambayo
imekua msaada mkubwa
siyo tu kwa Tanzania bali
Afrika Mashariki kwa ujumla.

Tumefanikiwa
kutumia shilingi
Wataalam wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya bilioni 1.65 badala
Kikwete (JKCI) na wataalam kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika
ya Nchini Marekani wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha ya shilingi bilioni 4.72
kurekebisha mapigo ya moyo. ambazo ni sawa na
kupunguza takribani
Taasisi ya Moyo ya Jakaya uuguzi ambapo imesaidia asilimia 65 ya gharama
Kikwete (JKCI) ilianzishwa kupunguza idadi ya wagonjwa za matibabu kama
mwaka 2014 ikiwa na jukumu waliokua wakipelekwa tungepeleka wagonjwa
la utoaji wa matibabu kwa nje kwa matibabu kutoka kutibiwa
wagonjwa wa moyo, kutoa 160 kwa mwaka 2012 nje ya nchi.
mafunzo kwa wanafunzi hadi kufikia wagonjwa
wa udaktari, ufamasia na

Serikali, Sekta Binafsi Kuendelea Kuimarisha Sekta ya Afya


Rais Mstaafu wa
Na. Immaculate Makilika -MAELEZO Awamu ya Tatu

S
Benjamin Mkapa
erikali kwa kushirikiana na
akimkabidhi
sekta binafsi imeendelea Hati za Umiliki
kuimarisha sekta ya afya wa nyumba 50
nchini kwa kujenga nyumba za Watumishi
za watumishi wa sekta wa Afya kwa
Waziri wa Afya,
hiyo, vituo vya afya pamoja
Maendeleo ya
na Zahanati mbalimbali ili Jamii, Jinsia,
kusaidia wananchi kupata Wazee na Watoto
huduma za afya kwa urahisi. Ummy Mwalimu
katika uwanja
wa michezo wa
Mapema mwezi huu, Taasisi
Mazaina Chato
ya Mkapa inayosimamiwa mkoani Geita.
na Rais Mstaafu wa Awamu
ya Tatu Benjamin William
Inaendelea Uk. 17
17 Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO

Inatoka Uk. 16 dawa za kuongeza damu


anasisitiza Waziri Ummy.

Wakati akihutubia wananchi


katika makabidhiano
hayo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania John
Pombe Magufuli ameishukuru
Taasisi ya Mkapa na Mfuko
wa dunia wa kupambana
magonjwa ya kifua kikuu,
ukimwi na malaria kwa kutoa
pesa zilizojenga nyumba
kwa watumishi wa sekta ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe afya katika mikoa 17 nchini.
Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Benjamin Mkapa wakati Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Kwa upande wake, Rais
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa
akihutubia wananchi wa Chato mkoani Geita. Mstaafu wa Awamu ya Tatu
Benjamini William Mkapa
Mkapa, imetimiza azma Wazee na Watoto Ummy aliyekuwa mgeni rasmi katika
hiyo muhimu kwa kukabidhi Mwalimu anavyoeleza kuwa shughuli hiyo ameushukuru
nyumba 50 za watumishi Serikali imedhamiria ifikapo Mfuko wa Dunia wa
wa afya katika mikoa ya mwaka 2020 asilimia 60 ya kupambana magonjwa
Geita, Kagera na Simiyu. Watanzania wapate huduma ya kifua kikuu, Ukimwi na
kupitia bima ya afya tofauti na Malaria kwa kushirikiana na
Akifafanua kuhusu nyumba sasa ambapo ni asilimi 28 tu
Serikali na Taasisi yake kwa
hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa ndio wanapata huduma hiyo
miaka 14 sasa na kuiomba
taasisi hiyo Dk. Ellen Mkondya nchini kuptia bima ya afya.
kuendelea kushirikiana
Senkoro ameeleza kuwa
na wadau wengine
nyumba hizo ni sehemu ya Waziri Ummy, aliongeza wanaopigana na maradhi
nyumba 450 zilizojengwa na kuwa Wizara yake ni kati
ikiwemo Taasisi ya Mkapa
taasisi hiyo nchi nzima tangu ya wizara zilizotengewa ili kuendelea kuimarisha
mpango ulipoanzishwa bajeti kubwa kwa mwaka
sekta hiyo katika utoaji
mwaka 2012 zikiwa na 2017/2018 na kwa kupitia
huduma kwa Watanzania.
thamani ya shilingi bilioni 26.5. fedha hizo wataboresha
huduma za afya nchini ikiwa Taasisi ya Benjamini Mkapa
Taasisi imekabidhi nyumba ni pamoja na kuimaimarisha
ambayo ilianzishwa mwaka
50 katika mikoa ya Geita (20), huduma na afya ya mama
2006, imetoa ajira 1,100
Simiyu (20), na Kagera (10) na mtotona kupunguza kwa wataalamu wa afya,
kwa ajili ya wafanyakazi wa vifo vitokanavyo na uzazi.
imefundisha vyuo 43 vya
sekta ya afya ili kuwezesha
afya nchini, imefadhili
huduma za afya kupatikana Pia kwa mwaka huu wanafunzi 949 wanaosoma
kwa saa 24 kwa kuwa tutaboresha vituo vya afya
masuala ya afya ambapo
watumishi wataishi karibu na 170 nchini, tutajenga benki
826 wakiwa wanasubiri ajira
hospitali alisema Dk. Senkoro. za damu za mikoa katika
katika taasisi za sekta hiyo
mikoa 10, na kuhakikisha sambamba na kujenga vituo
Sekta hii adhimu pia itanufaika kuwa hakuna mwanamke
11 vya upasuaji nchini nzima.
kwa kupatiwa vifaa tiba atakayefariki kwa sababu
na mahitaji mengine kama ya kuvuja damu, na kukosa
ambavyo Waziri wa Afya, dawa ya kuzuia ya kifafa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, cha mimba pia tutatoa
Limeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
18

Marufuku ya Mimba za Utotoni Italinda Maadili


Na Judith Mhina-MAELEZO

Hivi karibuni Rais wa Jamhuri


ya Muungano wa Tanzania
alitoa agizo la kupiga
marufuku kwa mwanafunzi
atakayepata ujauzito kurudi
shuleni, kwa lengo la kulinda
maadili ya jamii ya Kitanzania.

Maelekezo hayo aliyatoa


alipokuwa katika ziara Mkoa wa
Pwani alisema. Ndani ya utawala
wangu kama Rais, hakuna
mwanafunzi atakayepata
mimba atarudi shuleni. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwasalimia wanafunzi wa Sekondari mara baada ya
Hebu tuangalie agizo la kuhutubia wakazi wa Sengerema, wakati wa ziara
ya Kanda ya Ziwa
Rais, ambapo kwa yeyote
anayejua sheria na maadili
ya mwanafunzi wa shule ya masomo, kuwa na maadili na Mashirika ya kimataifa, lakini
msingi au sekondari, basi agizo hatimaye aje awe kiongozi tukumbuke kila Taifa duniani
hili limezingatia maelekezo ya na mama bora katika jamii. lina maadili yake na hapa ni
kitabibu na afya kwa mjamzito, muhimu kujikumbusha maadili
kabla na baada ya kujifungua. Watanzania walio wengi ya Mtanzania na kuepuka kuwa
wanazitambua sababu za watu wa kuiga kila uchwao
Sheria ya Elimu ya mwaka 1987 ongezeko la mimba za wanafunzi, kwa kisingizio cha usasa.
na kanuni zake, pamoja na kuwa ni; mila potovu, kubakwa,
marekebisho ya mwaka 2002 kutengana kwa wazazi na kuacha Tuangalie sababu za msingi za
inasema Ni marufuku kwa watoto wanatangatanga bila kiafya ambazo mimi na wewe
mwanafunzi akipata ujauzito uangalizi, umbali mrefu kutoka na Watanzania walio wengi
kurudi shuleni, sheria hii bado nyumbani kwenda shule, wanazijua. Kanuni za Afya
ipo na haijafutwa, hivyo kutokuwa na mabweni kwa zinaelekeza mwanamke yeyote
hakuna sababu za msingi za wasichana ambao hupanga anapotaka kubeba ujauzito ni
kutetea uovu wakati sheria ipo. nyumba mitaani na kurubuniwa vema apime na kujua hali yake
na wanaume, kufuata mkumbo ya afya, kufuata kanuni na
Ni muhimu kutambua kuwa, wa marafiki wenye tabia miongozo ya afya bora, ikiwa
Rais Magufuli ni mzazi, baba mbaya, umaskini wa familia, ni pamoja na kuhudhuria kliniki,
na kiongozi wa nchi, ambaye tamaa ya wasichana mfano:, kula chakula bora, kujikinga
ana uchungu kama mzazi kula vizuri, kuvaa vizuri, starehe na malaria, pia magonjwa
mwingine yeyote, ambaye na mengineyo kama hayo. ya kuambukiza. Kwa bahati
akiona binti amepata ujauzito mbaya hivyo vyote mwanafunzi
na kukatisha ndoto za maisha Serikali imezifanya kazi hawezi kuvifanya, hii inapelekea
yake. Kwa hiyo tamko ni changamoto nyingi na bado ongezeko la vifo vya wajawazito
dhahiri yamelenga kumtakia inaendelea kuzifanyia kazi na watoto wachanga.
mema mtoto wa kike, azingate zilizopo, ikishirikiana na Asasi
Zisizo za Kiserikali, wafadhili na Waziri wa Afya na Ustawi wa
Inaendelea Uk. 19
19
Inatoka Uk. 18

Jamii Bibi Ummy Mwalimu,


amethibitisha hilo wakati wa
kupokea nyumba 50 za afya
zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin
Mkapa, katika Mkoa wa Geita
ambapo amesema; Katika
vizazi hai 100,000 wakina mama
506 hupoteza maisha wakati wa
kujifungua na kati ya watoto
wachanga 1,000 wanaozaliwa
wakiwa hai, 25 hufariki dunia
kati ya siku 25 hadi 28. Tatizo la
mimba za utotoni limeongezeka
nchini kutoka asilimia 23 mwaka aandikishwe na aanze shule. kufanya watoto wa kike kitega
2010 hadi kufikia asilimia 27 uchumi wajue wanajichimbia
mwaka 2016/17 hii ikiwa na Mzazi ambaye hampeleki mtoto kaburi. Sheria haitawaacha
maanan kuwa tatizo ni kubwa. wake shule sheria imeelekeza wafanye watakavyo, mtoto ni
kukamatwa na kuchukuliwa Taifa la kesho, lazima aandaliwe
Tatizo la mimba shuleni sio la hatua za kisheria, hivyo hii ili aje alitumikie Taifa lake.
Tanzania peke yake, mifano inaashiria watoto wote kwa
dhahiri mwaka 2015 Mkoa wa asilimia kubwa wapo shule, Ili kuhakikisha kuwa
Rukwa, idadi ya wanafunzi tofauti na miaka ya nyuma tunawaepusha wanafunzi na
waliopata mimba shule za msingi wakati wa uchangiaji wa elimu. mimba za utotoni ni lazima,
walikuwa 2,785 na sekondari 22, wazazi, walezi, walimu, wanafunzi
nchini Afrika ya Kusini wanafunzi Haki ya mtoto ni pamoja na na jamii kwa ujumla tukubaliane
15,000 walipata ujauzito na kunyonya maziwa ya mama tuwe na maadili katika kulea
nchini Marekani wanafunzi kuanzia siku 0 mpaka miezi 6, watoto wetu, aidha tutumie
300,000 laki tatu walipata binti anayepata ujauzito akiwa imani zetu za dini, kuwa karibu na
ujauzito. Hivyo tatizo ni kubwa, mwanafunzi anamkosesha watoto, tumshirikishe Mwenyezi
ila tunaweza kulimaliza iwapo mtoto mwenzie haki zake, Mungu katika kila jambo.
wazazi, wanafunzi, walimu, jamii mtoto anahitaji chanjo zote
kwa ujumla na serikali kila mmoja mpaka afikishe miaka mitano na Tufate ushauri wa viongozi
atakapotimiza wajibu wake. upendo wa mama kwa mtoto wetu wa dini, tuache kuiga
maana akiukosa atadhirika mambo ambayo sio ya
kwa sasa Watanzania kwa kiasi kikubwa kisaikolojia. Kitanzania na kuacha mila zote
tumeiachia Serikali ihangaike zinazopelekea kumchochea
peke yake haiwezi kufanikiwa Kwa wanafunzi ni vema mtoto kuanza mahusiano ya
bila ushiki wa wote. wakatambua fursa hii, ya elimu kimapenzi na wanaume au
bure na kuitumia kwa lengo wanawake. Tukizingatia hayo,
Takwimu zinaonesha dhahiri lililokusudiwa. Wanafunzi wawe tutaweza kumaliza tatizo
tukiweza kuzuia wanafunzi wa na huruma na wazazi ambao la mimba kwa wanafunzi.
shule za msingi na sekondari wanaopenda mtoto asome,
kupata ujauzito wakiwa shuleni, maana kuna wazazi wengine
nchi itakuwa imepunguza idadi ndio chanzo cha kumshawishi
kubwa ya mimba za utotoni. mtoto apate ujauzito ili aachishwe
Maana sera ya elimu bure shule na kuolewa. Mzazi mwenye
inamtaka kila mtoto wa Tanzania kutaka mahari ili atajirike au
mwenye umri wa kwenda shule,
LIMEANDALIWA NA

Idara ya Habari-MAELEZO
S.L.P 8031
Dar es Salaam-Tanzania
Simu : (+255) 22 -2122771
Baruapepe:maelezo@habari.go.tz
Tovuti: www.maelezo.go.tz
Blogu: blog.maelezo.go.tz

@TZ_MsemajiMkuu Msemaji Mkuu wa Serikali MaelezoTv