Professional Documents
Culture Documents
PRESS RELEASE
Zanzibar 17 . 08 .201 7
Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao wa kijiji cha Kitogani kuwa kijiji chao kitakuwa
eneo la michezo kwani watafika watu kutoka ndani na nje ya n chi kwa ajili ya
kuutumia uwanja wao mpya unaoendelea kujengwa ambao tayari kwa awamu ya
kwanza umekamilika.
Dk. Shein alisema kuwa ujenzi wa kiwanja hicho ni utekelezaji wa ahadi aliyowaahidi
wananchi wa Kitogani baada ya wazee kutoa ombi lao la kujengewa uwanja vijana wao
na kusisitiza kuwa juhudi atazifanya katika kuhakikisha kiwanja kinakamilika katika
wakati wake wa uongozi .
Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa nia ya Chama chake cha CCM ni
kuimarisha michezo.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuvutiwa kwake na mas hindano ya riadha ya Wilaya
yaliyofanywa mnamo mwaka 2014 na mshindi alitoka Wilaya ya Kati katika kijiji cha
Ndijani na kuyapongeza mashindano hayo .