You are on page 1of 2

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu: 255-22-2114512, OFISI YA RAIS,


2116898 IKULU,
E-mail: press@ikulu.go.tz 1 BARABARA YA
Tovuti : www.ikulu.go.tz BARACK OBAMA,
Faksi: 255-22-2113425
11400 DAR ES
SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli


leo tarehe 21 Agosti, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA),Bwana Shinichi Kitaoka
Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo hayo Bw. Kitaoka amempongeza Mhe. Rais Magufuli


kwa uongozi mzuri na wa mfano hususani katika kupambana na rushwa na
msukumo mkubwa anaoutoa katika maendeleo hususani katika kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Jitihada zinazosaidia kuimarisha uchumi na
kuboresha huduma za kijamii na kuahidi kuwa JICA itaendelea kuwa
mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania.

Bw. Kitaoka ambaye ni mara yake ya kwanza kuitembelea Tanzania kama


Rais wa JICA amemuahidi Rais Dkt Magufuli kuwa miradi yote ya maendeleo
ya nyuma na ya sasa inayotekelezwa kwa pamoja kati ya Tanzania na JICA
itamalizika kwa wakati ikiwemo mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Flyover)
wa TAZARA unaoendelea kujengwa hivi sasa,mradi wa ujenzi wa barabara ya
Mwenge - Moroco yenye urefu wa kilomita 4 nukta 3 pamoja na mradi wa
ujenzi wa daraja la Gerezani.

Tumefikia makubaliano mazuri kuhusiana na miradi tunayoendelea


kuitekeleza hapa nchini na wananchi watarajie kuona kazi zikifanyika kuanzia

1
mwezi june,mwakani hususani katika ujenzi wa daraja la gerezani na
mingineyo
Kwa upande wake Mhe. Dkt Rais Magufuli amemshukuru Rais huyo wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan Bw. Shinichi Kitaoka kwa uamuzi
wake wa kuja Tanzania na amemhakikishia kuwa Tanzania inatambua
mchango mkubwa ambao Japan inautoa katika maendeleo ya Tanzania
kupitia JICA, na kwamba itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano
wake na Japan katika masuala mbalimbali.

Mhe. Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kutoa fedha kwa ajili ya
kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ikiwemo upanuzi wa
barabara ya Mwenge Morocco, utakaoiwezesha barabara hiyo kuwa na zaidi
ya njia nane, ujenzi wa barabara ya TAZARA, ujenzi wa Daraja la Gerezani
njia nne, na barabara ya Bendera tatu hadi Kamata.

Tunathamini sana mchango unaotolewa na walipa kodi wa Japan kupitia


JICA katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini na ninakuomba
kuangalia uwezekano wa kufadhili na kujenga miundo mbinu na miradi
mbalimbali ya maendeleo katika Makao Makuu ya nchi Dodoma ambako
serikali imedhamiria kuhamia huko ili kuweka alama ya urafiki na mahusiano
mema yaliyopo kati ya Tanzania na Japan
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe.
Masaharu Yoshida,Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango Doto James,
Katibu Mkuu Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga na Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini Mhandisi Patrick Mfugale.

Emmanuel Buhohela,
Mwandishi wa Habari,Msaidizi wa Rais,
Dar es Salaam.
21 Agosti, 2017

You might also like