You are on page 1of 1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,
E-mail: press@ikulu.go.tz IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz
11400 DAR ES SALAAM.
Faksi: 255-22-2113425
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli


amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Taarifa iliyotolewa jioni hii na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi unaanza leo tarehe 01 Februari,
2018.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha
Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) kituo cha Arusha, na pia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa
Mafuta (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Paul Joel Ngwembe kuwa
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (DAG) kuanzia leo tarehe 01 Februari,
2018.

Kabla ya Uteuzi huu Bw. Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria


katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance
Regulatory Authority – TIRA).
Kufuatia uteuzi huu Mhe. Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju na aliyekuwa Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Mdemu kuwa Majaji wa
Mahakama Kuu kuanzia leo tarehe 01 Februari, 2018.

Wateule wote wataapishwa Jumamosi tarehe 03 Februari, 2018 saa 9:00 Alasiri.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
01 Februari, 2018