You are on page 1of 1

Uzinduzi wa Jarida la CHAUKIDU

CHAUKIDU kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha


Dar es Salaam Tanzania, kinatangaza hafla ya
Uzinduzi wa Jarida la Kwanza la CHAUKIDU!
Pamoja na kujihusisha na maswala ya kuindeleza lugha ya Kiswahili,
WANACHAUKIDU pia wako mstari wa mbele katika nyanja za kiakademia.
Kwa mara ya kwanza, tuna furaha kukukaribisha ujumuike nasi kwenye
uzinduzi wa Jarida la Kwanza la CHAUKIDU lenye makala za kitaaluma!

Maelezo Muhimu:
Mahali: Hoteli ya Hyatt Regency Dulles Airport, VA
Muda: Saa sita hadi saa saba na nusu mchana
Siku: Jumamosi, tarehe 21 Aprili, 2018
Kiingilio: Hakuna Kiingilio kwa shughuli hii lakini ukitaka
kuhudhuria mawasilisho mengine – Kiingilio ni $ 100.

Usiku huo wa Jumamosi, karibu tumshangilie


MWANACHAUKIDU Profesa Alwiya Omar
akipata tuzo muhimu ya Walton Award!
Kiingilio: $50.00 – Pamoja na Chakula
Burudani: Jabali Afrika (Kenya/Congo)
Kwa Maelezo zaidi, piga simu: 217-493-3424 - Dr. Leonard Muaka