You are on page 1of 8

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Simu: 255-22-2114512, 2116898 OFISI YA RAIS,
E-mail: press@ikulu.go.tz IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
Tovuti : www.ikulu.go.tz
11400 DAR ES SALAAM.
Faksi: 255-22-2113425
Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli


leo tarehe 28 Julai, 2018 amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa
Mikoa, Wizara na Wilaya.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho huo ili kujaza nafasi zilizo
wazi kufuatia baadhi ya viongozi kustaafu, kuteuliwa katika nafasi nyingine na
wengine kuachwa.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo;

1. Bw. ALLY SALUM HAPI (aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya


Kinondoni) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Anachukua nafasi ya AMINA MASENZA ambaye amestaafu.

2. Brigedia Jenerali MARCO ELISHA GAGUTI ameteuliwa kuwa


Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Anachukua nafasi ya Meja Jenerali
Mstaafu SALUM KIJUU ambaye amestaafu.

3. Bw. ALBERT CHALAMILA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa


wa Mbeya. Anachukua nafasi ya Bw. AMOS GABRIEL
MAKALA ambaye amehamishwa na kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Katavi.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu


RAPHAEL MUHUGA amestaafu.

4. Brigedia Jenerali NICODEMAS ELIAS MWANGELA


ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe. Anachukua nafasi
ya Luteni Mstaafu CHIKU GALLAWA ambaye amestaafu.

1
Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea
na nyadhifa zao kama kawaida.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa kama


ifuatavyo:

1. Bw. KESSY MADUKA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa


Mkoa wa Dodoma. Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA
MADENGE

2. Bw. ABOUBAKAR MUSSA KUNENGE ameteuliwa kuwa


Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam. Anachukua nafasi ya
Bibi THERESIA MMBANDO.

3. Bw. DAVID KAFULILA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa


Mkoa wa Songwe.

4. Bw. DENIS BANDISA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa


Mkoa wa Geita. Anachukua nafasi ya SELESTINE GESIMBA

5. Bibi. HAPPINESS SENEDA WILLIAM ameteuliwa kuwa


Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Anachukua nafasi ya Bibi.
WAMOJA DICKOLAGWA.

6. Bw. ABDALLAH MOHAMED MALELA ameteuliwa kuwa


Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

7. Bw. RASHID KASSIM MCHATA ameteuliwa kuwa Katibu


Tawala wa Mkoa wa Kigoma. Anachukua nafasi ya Bw.
CHARLES PALLANGYO.

8. Bw. MISSAILE MUSSA ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa


Mkoa wa Manyara.

2
9. Bi. CAROLINE ALBERT MTHAPULA ameteuliwa kuwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa MARA.

10. Dkt. JILLY ELIBARIKI MALEKO ameteuliwa kuwa Katibu


Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Anachukua nafasi ya ALFRED
LUANDA.

11. Bw. CHRISTOPHER DEREK KADIO ameteuliwa kuwa


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza. Anachukua nafasi ya
Kamishna wa Polisi Mstaafu CLODWING MTWEVE.

12. Bw. ERIC SHITINDI ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa


Mkoa wa Njombe. Anachukua nafasi ya BW. JACKSON
SAITABAU.

13. Prof. RIZIKI SALAS SHEMDOE ameteuliwa kuwa Katibu


Tawala wa Mkoa wa Ruvuma. Anachukua nafasi ya Bw.
HASSAN BENDEYEKO.

Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya kazi.

1. Bibi REHEMA MADENGE aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa


DODOMA, amehamishiwa katika Mkoa wa Lindi.

2. Bibi THERESIA MMBANDO aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa


DAR ES SALAAM amehamishiwa katika Mkoa wa Pwani.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu


Makatibu Wakuu kwa baadhi ya Wizara kama ifuatavyo;

1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. JOSEPH


BUCHWESHAIJA kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,

3
Biashara na Uwekezaji. Anachukua nafasi ya Prof. ELISANTE
Ole GABRIEL.

2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. ANDREW WILSON


MASSAWE kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. ELISANTE Ole


GABRIEL kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(Mifugo).

4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi kuwa


Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Mawasiliano)

5. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. EDWIN PAUL MHEDE


kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na


wengine kuhamishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;

1. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JERRY CORNEL MURO


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

2. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. FRANK JAMES


MWAISUMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido. Anachukua
nafasi ya Bw. DANIEL GEOFREY CHONGOLO.

3. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PATROBAS KATAMBI


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

4
4. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi MWANAHAMISI
ATHUMAN MUKUNDA kuwa Mkuu wa Wilaya ya BAHI.
Anachukua nafasi ya ELIZABETH SIMON KITUNDU.

5. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha kituo cha kazi Bw. DANIEL


GEOFREY CHONGOLO aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya
Longido kwenda Wilaya ya Kinondoni.

6. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bibi SARA MSAFIRI ALLY


aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwenda Wilaya ya
Kigamboni. Anachukua nafasi ya Bw. HASHIM SHAIBU
MGANDILWA.

7. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. SAID MKUMBA kuwa


Mkuu wa Wilaya ya Bukombe. Anachukua nafasi ya
JOSEPHAT PAULO MAGANGA

8. Mhe. Rais Magufuli amemhamisha Bw. JOSEPHAT PAULO


MAGANGA na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita. Anachukua
nafasi ya HERMAN CLEMENT KAPUFI.

9. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali PATRICK NORBERT


SONGEA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato. Anachukua nafasi
ya SHAABAN ATHUMAN NTARAMBE.

10. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. RASHID MOHAMED


MWAIMU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa. Anachukua
nafasi ya Kanali SHABAN ILANGU LISSU

11. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali SIMON M. ANANGE


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kasulu.

12. Mhe. Rais Magufuli amemteua Luteni Kanali MICHAEL


MASALAMA NGAYALINA kuwa Mkuu wa Wilaya ya

5
Buhigwe. Anachukua nafasi ya Brigedia Jenerali MARCO
ELISHA GAGUTI.

13. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. LENGAI Ole SABAYA


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

14. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. HASHIM SHAIBU


MGANDILWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa.
Anachukua nafasi ya Bw. JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI.

15. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ELIZABETH SIMON


KITUNDU kuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati. Anachukua nafasi
ya RAYMOND HIERONIMI MUSHI

16. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. JOSEPH JOSEPH


MKIRIKITI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang. Anachukua
nafasi ya SARA MSAFIRI ALLY.

17. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. MARY-PRISKA


WINFRED MAHUNDI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Anachukua nafasi ya Bibi. REHEMA MANASE MADUSA.

18. Mhe. Rais Magufuli amemteua Ndg. NGOLLO MALENYA


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga. Anachukua nafasi ya Bw.
JACOB JOSEPH KASSOMA.

19. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. MOSES JOSEPH


MACHALI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.

20. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. SEVERIN MATHIAS


LALIKA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela.

6
21. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILIS MESHACK
NYIMBO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana. Anachukua
nafasi ya MARY ONESMO TESHA.

22. Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. PHILEMON SENGATI


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu. Anachukua nafasi ya HADIJA
RASHID NYOMBO.

23. Mhe. Rais Magufuli amemteua Kanali LUCAS BONIPHACE


MAGEMBE kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe. Anachukua
nafasi ya ESTOMIH FRANCIS CHANG’AH.

24. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. ZAINAB RASHID


MFAUME KAWAWA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.
Anachukua nafasi ya Bw. MAJID HEMED MWANGA.

25. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi. JOKATE MWEGELO kuwa


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Anachukua nafasi ya Bibi.
HAPPINESS SENEDA WILLIAM.

26. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. SOPHIA KIZIGO kuwa


Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo. Anachukua nafasi ya Bibi.
LUCKINESS ADRIAN AMLIMA.

27. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. JASINTA VENANT


MBONEKO kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga. Anachukua
nafasi ya JOSEPHINE RABBY MATIRO.

28. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. RAHABU MWAGISA


SOLOMON kuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

29. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. PASACAS MURAGIRI


kuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida. Anachukua nafasi ya ELIAS
CHORO JOHN TARIMO.

7
30. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. KOMANYA ERIC
KITWALA kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.

31. Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi. KISA KASONGWA kuwa


Mkuu wa Wilaya ya Korogwe.

Tarehe ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Naibu


Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa itatangazwa baadaye.

Wakuu wa Wilaya wataapishwa na Wakuu wao wa Mikoa kwa utaratibu


utakaopangwa na Mikoa husika.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Julai, 2018