You are on page 1of 2

PIMA UKRISTO WAKO

1. KIPIMO CHA UBINAFSI


- Ubinafsi ni hali ya mtu kujifikiria na kujipenda yeye mwenyewe. Hali ya mtu kutaka kuvuta
umakini wote kwake.
- Mtu mbinafsi hufanya kila anachofanya ili kutaka kutambulika na watu na kutaka
kuonyesha umwamba wake mbele za watu.
- Mtu mbinafsi hupenda kujitutumua ili kutaka kuonyesha umuhimu wake na heshima yake
mbele za watu.
- Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana
mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. – Mathayo 6:1
- Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama
katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia,
Wamekwisha kupata thawabu yao. – Mathayo 6:5
- Ubinafsi ni tabia ambayo wakati mwingine watu wanaweza wasiione moja kwa moja
kwako, lakini moyo wako unajua fika kama una ubinafsi au la.
- Kwa mfano wewe ni mwalimu, je furaha yako ipo katika kule kuonekana kwamba
umefundisha vizuri sana au katika kuona watu wanafaidika na maisha yao kubadilika
kutokana na mafundisho yako?
- Unaweza hata ukawa unamtumikia Mungu au unamtafuta Mungu lakini kwa malengo ya
kibinafsi kama vile kushindana na watu wengine, kutaka nawe uonekane una upako, kutaka
kuonekana unajua sana maandiko n.k. Shauku yako kubwa ni kutaka kuonekana na watu.
- Kwa kifupi, mtu mbinafsi anasumbuliwa na kitu kimoja kikubwa, ‘WATU
WANANIONAJE’
- Ubinafsi huonekana katika namna zifuatazo
- Hali ya kutaka kushindana na wengine
- Kutafuta kuonekana mbele za watu
- Kutotambua mchango wa wengine au kutopenda kupongeza na kuwakubali wengine
wanapofanya vizuri kuliko wewe
- Kutopenda kuona wengine wanasifiwa
- Kutofurahishwa na mafanikio ya wengine
- Kutotaka kuwapa wengine nafasi
- Kutopenda kukosolewa, kutaka kuonekana muda wote uko sahihi
- Kusumbuliwa sana na maisha ya hadharani kuliko maisha yako ya sirini.
- Kujifikiria wewe Zaidi kuliko watu wengine
- Kupenda kuonekana mkamilifu
- Kujitafutia utukufu
- Mtu mbinafsi anajiabudu. Mtu mbinafsi amejifanya kuwa mungu wake mwenyewe. Mtu
mbinafsi analinda mwonekano wake mbele za watu (Public Image) kwa gharama yoyote ile.
- Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu
na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. – Wafilipi 2:3

KWA NINI KIPIMO CHA UBINAFSI?


- Ukristo unaanzia kwenye kifo cha ubinafsi
- Ukristo ni uhai wa Kristo ndani ya mwamini.
- Kwa hiyo, ni lazima wewe ufe ili Kristo aishi kupitia wewe.
- Ukristo siyo kujaribu kujonyesha wewe bali ni kumruhusu Kristo aonekane kupitia wewe.
- Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani
yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu,
ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. – Wagalatia 2:20
- Ukristo haupo katika wewe kujaribu kuishi ‘kikristo’ bali kumuacha Kristo awe hai ndani
yako, aishi ndani yako na adhihirike katika mwili wako, na yote haya yanafanyika kwa
Imani.
- Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. – Wafilipi 1:21
- Maisha ya ukristo ni maisha ya Kristo na siyo maisha yetu.
- Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. –
Wakolosai 3:3
- Ukristo ni umoja na Kristo. Ukristo ni kuishi kwa uhai wa Kristo, Roho wa Kristo, Neno la
Kristo, Imani ya Kristo na Mawazo ya Kristo.
- Ukristo ni kukubali kufa na kumucha Kristo aishi kupitia mwili wako. Ni kukubali
kuutumia mwili wako kama chombo cha kumdhihirisha Kristo.

SWALI: Je, katika yote unayofanya, unataka uonekane wewe au aonekane Kristo?

You might also like