You are on page 1of 17

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

HALI YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2018

Januari, 2019

1
UTANGULIZI

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kutekeleza


jukumu lake la msingi la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya ikiwa ni
pamoja na huduma za kinga dhidi ya magonjwa yanayoambukiza (Malaria, Kifua Kikuu,
VVU na UKIMWI), huduma za kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama
magonjwa ya moyo, kisukari na saratani, huduma za chanjo ili kuwaepusha wananchi
na magonjwa yanayoweze kuepukika kwa chanjo, huduma za afya ya uzazi na mtoto
nchini ili kupunguza idadi ya vifo vya wanawake na watoto vinavyotokana na Uzazi,
kuimarisha upatikanaji wa damu salama. Aidha, Wizara imeendelea kuimarisha
upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vyote vya umma vya
kutolea huduma za za afya nchini na kuboresha upatikanaji wa huduma za kibingwa
lengo likiwa ni kusogeza huduma hizi karibu zaidi na wananchi na kupunguza rufaa za
nje ya nchi zisizo na ulazima. Kulingana na takwimu zilizokusanywa kutoka katika vituo
vya kutolea huduma za afya kupitia mfumo wa DHIS2, katika kipindi cha Januari hadi
Desemba 2018, hali ya huduma za Afya nchini ilikuwa imeimarika ambapo maeneo
mengi huduma zimeimarika na baadhi ya maeneo Serikali inaendelea kuyaboresha.

HALI YA HUDUMA YA AFYA NCHINI

1.0 HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO.

Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imeendelea kutekeleza Mpango


Mkakati wa ‘Kuboresha Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto wa umri chini ya
miaka mitano na Vijana’ wa Januari 2016 hadi Desemba 2020 unaolemga kusogeza
huduma bora za afya karibu na maeneo wanayoishi, ili hatimaye kupunguza vifo
vitokanavyo na uzazi, vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto walio na umri chini
ya miaka mitano. Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mkakati huo ni pamoja na
kuboresha huduma kwa wajawazito, huduma za wakati wa kujifungua na baada ya
kujifungua, huduma za watoto chini ya miaka mitano, huduma ya kuzuia maabukizi ya
VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), huduma za Chanjo, kuzuia
maambukizi ya malaria kwa wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano

1.1 Mahudhurio ya Wajawazito kliniki

Katika mwaka 2018, jumla ya wajawazito 2,086, 930 walihudhuria na


kuandikishwa Kliniki, ikilinganishwa na wajawazito 2,009,879 Mwaka 2017.
Mwongozo wa utoaji huduma za afya ya uzazi na mtoto unaelekeza wajawazito kuanza
huduma mapema kabla ya majuma 12 ya ujauzito na kuhudhuria kliniki angalau mara
nne katika kipindi cha ujauzito ili waweze kupata huduma zote muhimu. Wizara
iliendelea kuwahamasisha wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ambapo, katika
kipindi cha mwaka 2018 asilimia 25 ya wajawazito nchini waliweza kufanya
hudhurio la kwanza kabla ya majuma 12 ikillinganishwa na asilimia 18
mwaka 2017. Aidha, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wajawazito waliohudhuri

2
kliniki angalau mara nne imeongezeka katika kipindi cha mwaka 2018 na kufikia
asilimia 57 ikilinganishwa na asilimia 46 mwaka 2017. Mikoa ambayo bado kiwango
cha mahudhurio ya wajawazito kliniki yapo chini ni Mara 40%, Njombe asilimia 40,
Simiyu asilimia 41, Iringa asilimia 45, Tanga asilimia 46, Dodoma asilimia 47 na
Ruvuma asilimia 49. Vilevile, huduma ya kumkinga mama mjamzito dhidi ya Maleria
iliimarika ambapo asilimia 79 ya wajawazito walipatiwa kinga dhidi ya malaria katika
kipindi cha mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 66 mwaka 2017.

1.2 Huduma ya Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto

Huduma ya Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto iliendelea
kutolewa ambapo mwaka 2018 asilimia 97 ya wajawazito walipima VVU
ikilinganishwa na asilimia 95 mwaka 2017. Aidha, katika wajawazito waliopimwa
VVU, ni asilimia 3.9 waligundulika kuwa na VVU na kati ya hao waliogundulika
asilimia 99 walianzishiwa dawa za ART. Katika mwaka 2017 asilimia 4.2
waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kati yao asilimia 99 walianza dawa za
ART. Takwimu hizi zinaonyesha matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali
katika mapambano dhidi ya UKIMWI.
Wastani wa kiwango cha utoaji wa Huduma za kuzuia maabukizi ya VVU
kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto mwaka 2018

Na. Mkoa Mwaka Mwaka Na. Mkoa Mwaka Mwaka


2017 2018 2017 2018
1 Arusha 97% 97% 15 Mtwara 97% 98%
2 Dar Es Salaam 97% 96% 16 Mwanza 93% 97%
3 Dodoma 96% 98% 17 Njombe 92% 92%
4 Geita 95% 98% 18 Pwani 96% 97%
5 Iringa 93% 93% 19 Rukwa 99% 98%
6 Kagera 98% 98% 20 Ruvuma 96% 97%
7 Katavi 94% 97% 21 Shinyanga 96% 97%
8 Kigoma 95% 97% 22 Simiyu 96% 97%
9 Kilimanjaro 99% 98% 23 Singida 97% 98%
10 Lindi 95% 97% 24 Songwe 94% 96%
11 Manyara 99% 97% 25 Tabora 93% 98%
12 Mara 94% 98% 26 Tanga 97% 98%
13 Mbeya 92% 94% Kitaifa 96% 97%
14 Morogoro 96% 97%

Jedwali hapo juu linaonyesha kiwango (Asilimia) cha mwitikio wa Wajawazito kupima
VVU wakati wa ujauzito.

3
1.3 Huduma wakati na baada ya kujifungua

Takwimu zilizokusanywa kutoka katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini
zinaonyeshwa kumekuwa na ongezeko la wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya
ambapo katika mwaka 2018 asilimia 73 ya wajawazito walijifungulia katika
vituo vya afya ikilinganishwa na asilimia 70 mwaka 2017.
Wastani wa kiwango cha Wajawazito waliojifungulia katika Vituo vya Afya
mwaka 2018

Na. Mkoa Mwaka Mwaka Na. Mkoa Mwaka Mwaka


2017 2018 2017 2018
1 Arusha 63% 63% 15 Mtwara 70% 65%
2 Dar Es Salaam 54% 55% 16 Mwanza 76% 88%
3 Dodoma 62% 63% 17 Njombe 82% 66%
4 Geita 79% 95% 18 Pwani 96% 97%
5 Iringa 88% 71% 19 Rukwa 96% 100%
6 Kagera 66% 71% 20 Ruvuma 81% 74%
7 Katavi 88% 89% 21 Shinyanga 92% 98%
8 Kigoma 79% 92% 22 Simiyu 63% 63%
9 Kilimanjaro 59% 52% 23 Singida 75% 68%
10 Lindi 45% 62% 24 Songwe 70% 69%
11 Manyara 54% 49% 25 Tabora 73% 85%
12 Mara 75% 66% 26 Tanga 55% 57%
13 Mbeya 82% 75% Kitaifa 70% 73%
14 Morogoro 65% 65%

Jedwali linaonyesha kiwango cha wajawazito kujifungulia katika katika vituo vya
kutolea huduma za Afya kwa kila mkoa. Mafaniko haya yanatokana na maboresho
makubwa yanayofanyika katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo ukarabati
wa vituo vya kutolea huduma pamoja na upatikanaji wa dawa.

1.4 Huduma kwa Watoto Chini ya mwaka mmoja

Katika kipindi cha mwaka 2018 jumla ya watoto 1,568,832 walizaliwa


ikilinganishwa na Watoto 1,498,488 mwaka 2017. Watoto hao walipatiwa
huduma mbalimbali za chanjo ili kuzuia magonjwa yanayowaathiri Watoto ikiwemo
ugonjwa Kupooza, Kuharisha, Pepopunda, Pneumonia, homa ya ini na Surua. Katika
kipindi cha mwaka 2018 hali ya chanjo kwa Watoto nchini imeendelea kuwa katika kiwango
cha juu zaidi ya asilimia 85 ya kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya Duniani kama
inavyoonyeshaa katik hapa chini;

4
Wastani wa Hali ya chanjo kwa Watoto katika kipindi cha mwaka 2017 na
2018

105 102
99 99
100 97 97
96 96
95
91 90 90 90 90
90

85

80

75

70

65

60
OPV3 PENTA3 PCV3 Rota2

Mwaka 2017 Mwaka 2018 Lengo 2020

Jedwali hapo juu linaonyesha hali bora ya upatikanaji wa chanjo mhimu nchini.

2.0 HUDUMA YA TIBA NCHINI


Mwaka 2018 jumla ya mahudhurio ya wagonjwa ilikuwa 42,411,276 katika
vituo vya kutolea huduma za tiba nchini ikilinganishwa na 54,478,926 kwa
mwaka 2017 Kati ya hao wagonjwa wa wa nje (OPD) ilikuwa 41,052,012 na
wagonjwa wa kulazwa (IPD) ilikuwa 1,359,264. Takwimu hizi zinajumuisha wagonjwa
wa hudhurio la kwanza na mahudhurio ya marudio..
2.1 Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Halmashauri, Vituo vya
Afya na Zahanati katika ngazi ya msingi.
Katika mwaka 2018 jumla ya wagonjwa wa nje (OPD) ilikuwa 36,376,967 walipatiwa
huduma katika hospitalli za Halmashauri, hospitali nyingine, vituo vya afya na zahanati
ikiwa ni 18,194,619 hudhurio la kwanza na 18,182,348 mahudhurio ya marudio.
Mwaka 2017, jumla ya wagonjwa wan je (OPD) ilikuwa 47,650,158 ambapo
30,174,341 hudhurio la kwanza na 15,809,971 mahudhurio ya marudio. Wakati huo
huo wagonjwa wa Kulazwa mwaka 2018 walikuwa 404,659 ikilinganishwa na
wagonjwa 523,587 mwaka 2017

5
2.2 Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa mwaka 2018

Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2018 Hospitali za Rufaa za Mikoa zilihudumia
jumla ya wagonjwa 3,526,503 ambapo wagonjwa wa nje walikuwa 3,054,318 na
wagonjwa wa ndani walikuwa 472,185 ikilinganishwa na wagonjwa 4,781,999
waliohudumiwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2017, ambapo wagonjwa wa nje
walikuwa 4,059,145 na wagonjwa wa ndani walikuwa 722,854 kama inavyoonesha
kwenye jedwali hapo chini.

Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa mwaka 2018

2017 2018
Na Jina la Hospitsli OPD IPD JUMLA OPD IPD JUMLA
1 Hospitali ya Rufaa Mount Meru 152,215 12,936 165,151 13,814 11,587 25,401
2 Hospitali ya Rufaa Songwe 12,866 3,513 16,379 3,244 3,979 7,223
3 Hospitali ya Rufaa ya Tumbi 166,890 9,257 176,147 105,697 7,415 113,112
4 Hospitali ya Rufaa Ligula 24,924 5,151 30,075 33,500 5,053 38,553
5 Hospitali ya Rufaa Sokoine 18,961 5,227 24,188 44,386 7,236 51,622
6 Hospitali ya Rufaa Dodoma 248,915 31,801 280,716 167,361 27,973 195,334
7 Hospitali ya Rufaa Morogoro 150,477 25,473 175,950 77,189 23,021 100,210
8 Hospitali ya Rufaa Njombe 26,310 5,153 31,463 30,650 5,268 35,918
9 Hospitali ya Rufaa Bukoba 333,039 13,373 346,412 188,159 13,319 201,478
10 Hospitali ya Rufaa Bariadi 36,999 7,642 44,641 35,561 7,098 42,659
11 Hospitali ya Rufaa Maweni 30,834 8,452 39,286 17,644 6,804 24,448
12 Hospitali ya Rufaa Mawenzi 106,717 8,735 115,452 97,316 6,209 103,525
13 Hospitali ya Rufaa Amana 221,144 16,456 237,600 217,023 10,791 227,814
14 Hospitali ya Rufaa Ruvuma 106,026 25,835 131,861 141,767 22,597 164,364
15 Hospitali ya Rufaa Musoma 54,998 12,274 67,272 56,770 11,250 68,020
16 Hospitali ya Rufaa Temeke 664,247 376,402 1,040,649 562,768 171,287 734,055
17 Hospitali ya Rufaa Mwananyamala 940,827 13,315 954,142 733,670 10,098 743,768
18 Hospitali ya Rufaa Singida 55,802 9,827 65,629 52,729 8,910 61,639
19 Hospitali ya Rufaa Shinyanga 46,024 12,390 58,414 31,981 10,910 42,891
20 Hospitali ya Rufaa Sekoutoure 116,277 23,043 139,320 119,588 22,146 141,734
21 Hospitali ya Rufaa Iringa 61,756 13,289 75,045 70,038 28,682 98,720
22 Hospitali ya Rufaa Katavi 43,935 10,409 54,344 27,232 7,530 34,762
23 Hospitali ya Rufaa Mbeya 196,479 32,420 228,899 21,330 3,663 24,993
24 Hospitali ya Rufaa Geita 29,306 10,603 39,909 21,014 10,070 31,084
25 Hospitali ya Rufaa Kitete 54,505 8,963 63,468 35,183 8,714 43,897
26 Hospitali ya Rufaa Manyara 15,421 1,299 16,720 13,314 1,706 15,020
27 Hospitali ya Rufaa Bombo 95,886 12,958 108,844 69,772 12,971 82,743
28 Hospitali ya Rufaa Sumbawanga 47,365 6,658 54,023 65,618 5,898 71,516
JUMLA 4,059,145 722,854 4,781,999 3,054,318 472,185 3,526,503

6
2.3 Mahudhurio ya wagonjwa katika Hospitali ya Taifa, Hospitali Maalum
na Hospitali za Rufaa za Kanda
Katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2018, Hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali
Maalum na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilihudumia jumla ya wagonjwa 2,103,147
ambapo wagonjwa wa kulazwa walikuwa 482,420 na wagonjwa wa nje walikuwa
1,620,727. Ikilinganishwa na idadi ya wangonjwa 2,046,769 kwa kipindi cha Januari
hadi Desemba 2017. Ambapo idadi ya wagonjwa wa kulazwa ilikuwa 711,766 na
wagonjwa wa nje 1,335,003. Mchanganuo wa idadi kwa kila Hospitali umeoneshwa
kwenye jedwali hapo chini.

Idadi ya Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Kanda, Hospitali


Maalum na Hospitali ya Taifa Mwaka 2018

Na. HOSPITALI 2017 2018

OPD IPD JUMLA OPD IPD JUMLA

1 Hospitali ya Taifa Muhimbili 436,394 46,826 483,220 446,360 43,366 489,726

Taasisi ya Mifupa Muhimbili


2 171,732 7,450 179,182 203,357 8,315
(MOI) 211,672

Taasisi ya Moyo Jakaya


3 60788 3297 64,085 80228 3490
Kikwete 83,718

Taasisi ya Saratani Ocean


4 50,444 4,441 54,885 59,525 5,874
Road 65,399

Hospitali Benjamini Mkapa –


5 30865 2472 33,337 53553 2998
Dodoma 56,551

Hospitali ya Afya ya Akili


6 45,522 202,537 248,059 53,707 151,483
Mirembe 205,190

Hospitali ya Magonjwa ya
7 20635 818 21,453 26987 1012
Kuambukiza Kibong'oto 27,999

Hospitali ya Rufaa ya Kanda


8 187,574 30,177 217,751 249,224 44,170
Nyanda za Juu Kusini- Mbeya 293,394

Hospitali ya Kanda ya Ziwa –


9 138,664 211,161 349,825
Bugando 29,877 285,828
255,951
Hospitali ya Rufa ya Kanda ya
10 192,385 202,587 394,972 191,835 191,835
Kaskazini-KCMC 383,670

7
Na. HOSPITALI 2017 2018

2,103,147
JUMLA 1,335,003 711,766 2,046,769 1,620,727 482,420

2.4 Magonjwa kumi yaliyochangia vifo kwa mwaka 2018

Takwimu zilizokusanywa kupitia mfumo wa DHIS2 zimeainisha kuwa katika mwaka


2018 kumetokea jumla ya vifo 20,087 ikilinganishwa na vifo 19,693 mwaka
2017. Katika kipindi cha miaka yote miwili (2017 na 2018), homa ya mapafu
imeongoza kwa kusababisha vifo, ambapo kwa mwaka 2017, homa ya mapafu
imechangia asilimia 18.2 ya vifo vyote na mwaka 2018 imechangia kwa asilimia
12.9 ya vifo vyote. Mwaka 2018, ugonjwa usio wa kuambukiza (shinikizo la damu)
umejitokeza katika magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo ambapo
umechangia vifo kwa asilimia 1.9 ya vifo vyote.

Magonjwa Kumi yaliyochangia vifo kwa mwaka 2018

2017 2018

Idadi ya Idadi ya
Jina la Ugonjwa Asilimia Jina la Ugonjwa Asilimia
Na. Vifo Vifo

1 Homa ya mapafu 3,573 18.2 Homa ya Mapufu 2,590 12.9


2 Ugonjwa wa Moyo 1,904 9.7 Kukosa Pumzi (watoto) 1,269 6.3
3 Kukosa Pumzi (watoto) 1,658 8.4 Ugonjwa moyo 1,253 6.2
Kifo cha Mtoto Tumboni Kifo cha Mtoto Tumboni
4 (Ngozi imechubuka) 902 4.6 (Ngozi imechubuka) 766 3.8
Maambukizi katika damu
5 kwa watoto 710 3.6 Malaria 693 3.4
Kifo cha Mtoto Tumboni
6 (Ngozi haijachubuka) 625 3.2 UKIMWI 605 3
Kifo cha Mtoto Tumboni
7 Jeraha la Kichwa 597 3 (ngozi haijachubuka) 540 2.7
8 Kukosa pumzi 366 1.9 Magonjwa mengine 538 2.7
Maambukizi katika damu
9 Pumu 355 1.8 kwa watoto 496 2.5
10 Homa ya uti wa Mgongo 343 1.7 Shinikizo la Damu 382 1.9

3.0 Upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya
nchini

3.1 Hali ya Upatikanaji wa Dawa Muhimu


Hali ya upatikanaji wa Dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini
imeendelea kuimarika tokea kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya Tano. Hii ni

8
kutokana na Serikali kuongeza bajeti ya dawa kutoka Shilingi Milioni 31 mwaka
2015/16 hadi kufikia Shilingi milioni 251 mwaka 2016/17 na Shilingi 270 mwaka
2018/19. Hali hii imewezesha takribani vituo vyote vya kutolea huduma nchi kuwa na
dawa zote muhumu na kuwezesha wananchi kupata dawa karibu na maeneo
wanayoishi. Mwaka 2015 hali ya upatikanaji wa dawa ilikuwa asilimia 46 kutokana na
ongezeko la bajeti pamoja na usimamizi mzuri wa usambazaji dawa, mwaka 2016/17
hali upatikanaji wa dawa iliongezeka na kufikia asilimia 89 na mwaka 2018 ilifikia
asilimia 94 kwa dawa dawa muhimu zinazosambazwa na Bohari ya Dawa nchini
(MSD).
Wastani wa upatikanaji wa Dawa muhimu katika mikoa mwaka 2017 na mwaka
2018

Mwaka Mwaka Mwaka Mwaka


Na. Mkoa 2017 2018 Na. Mkoa 2017 2018
1 Arusha 91% 96% 15 Mtwara 88% 94%
2 Dar Es Salaam 92% 94% 16 Mwanza 90% 95%
3 Dodoma 87% 94% 17 Njombe 89% 94%
4 Geita 91% 95% 18 Pwani 87% 93%
5 Iringa 88% 94% 19 Rukwa 89% 93%
6 Kagera 95% 96% 20 Ruvuma 84% 94%
7 Katavi 89% 94% 21 Shinyanga 93% 96%
8 Kigoma 85% 94% 22 Simiyu 82% 94%
9 Kilimanjaro 91% 96% 23 Singida 93% 97%
10 Lindi 86% 92% 24 Songwe 90% 94%
11 Manyara 87% 94% 25 Tabora 82% 92%
12 Mara 88% 94% 26 Tanga 89% 95%
13 Mbeya 92% 97% 27 Kitaifa 89% 94%
14 Morogoro 88% 92%

3.2 Upatikanaji wa Damu Salama


Serikali imeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji wa Damu Salama ambapo katika
kipindi cha mwaka 2018 (January-Disemba) jumla ya chupa za damu salama 307,835
sawa na asilimia 85.5 ya lengo zilikusanywa ikilinganishwa na chupa 233,933
mwaka 2017. Chupa zote 307,835 zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu pamoja
na magonjwa makuu manne ambayo ni Ukimwi (HIV,) Homa ya Ini B na C (HBV, HCV)
na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa 262,283 sawa na asilimia 85.3 zilikuwa
salama na kusambazwa katika hospitali kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

4.0 MAPAMBANO DHIDI YA VVU/UKIMWI, MALARIA NA KIFUA KIKUU


Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI

4.1 Mapambano Dhidi ya VVU/UKIMWI

9
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania ina kuwa salaama kutokana na maambukizi mapya
ya VVU, kuwapunguzia makali ya virusi vya UKIMWI na kuzuia waathirika
wasishambuliwe na magonjwa nyemelezi, Sekta ya Afya ikishirikana na Wadau
inatekeleza mpango wa Kimatatifa wa 90-90-90 Mpango huo unazitaka nchi
kuwatambua wenye VVU kwa asilimia 90 ifikapo mwaka 2020 miongoni mwa
watanzania wote wanaoishi na VVU wanaokadiriwa kuwa 1,500,000 nchi nzima, hatua
ya pili ni kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya wanaogundulika kuwa na VVU wanaanza
dawa za ARV na kati ya wanaoanza dawa za ART asilimia 90 wanaimarisha kinga zao
za mwili ili kuzuia wasishambuliwe na magonjwa nyemelezi. Hadi kufikia mwisho wa
Mwezi Septemba 2018, Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI iliweza
kuwaandikisha katika tiba ya kufubaza virusi vya UKIMWI, jumla ya wagonjwa
1,087,382 kati ya hao watoto walikuwa ni 58,908. Idadi hii ya wagonjwa walio katika
tiba ni asilimia 72 ya watu 1,500,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini kote
ikilinganishwa na asilimia 70 mwaka 2017. Lengo la 90 ya pili ni kuhakikisha asilimia
90 ya waliokutwa na VVU wanaanzishiwa dawa za ART, lengo hili limefikiwa ambapo
Watanzania 1,068,282 sawa na asilimia 98.2 wanatumia dawa za ART na lengo la 90
ya tatu ni kuhakikisha asilimia 90 ya wanaoanzishiwa dawa za ARV kinga zao za mwili
zinaimalika (Viral road suppression), ambapo lengo hili limefikiwa kwa asilimia 87.

Utekelezaji wa mpango wa 90-90-90 hadi kufikia Septemba 2018


% %
Na. Maeneo ya kipaumbele Takwimu Mpaka Takwimu Mpaka
Desemba,2017 Septemba,2018
Makisio ya Watu wanaoishi na
1 Virusi vya UKIMWI 1,400,000 1,500,000
Idadi ya Watu wanaopata 70 72
2 huduma 979,624 1,087,382
Idadi ya Watu wanaotumia 98.5 98.2
3 dawa 965,081 1,068,282
Asilimia ya kufubaza virusi
4 kwa watu wanaotumia dawa 94 87

4.2 Mapambano dhidi ya Malaria nchini


Mwaka 2018 idadi ya 5,769,837 waligundulika kuwa na ugonjwa wa malarea
ikilinganishwa na watu 5,595,916 mwaka 2017. Wakati huo huo matumizi ya kipimo cha
haraka cha malaria (mRDT) yakiongezeka kutoka asilimia 79 mwaka 2017 hadi kufikia
asilimia 86 mwaka 2018
Hali ya Malaria Nchini

2017 2018

Na. Mikoa
Jumla Malaria cases Jumla Malaria Cases
1 Arusha 4221 5870
2 Dar Es Salaam 377828 293239

10
3 Dodoma 49294 75660
4 Geita 264480 366177
5 Iringa 16906 19375
6 Kagera 637175 454146
7 Katavi 67302 88711
8 Kigoma 649122 667968
9 Kilimanjaro 8422 8122
10 Lindi 329130 224872
11 Manyara 8239 11484
12 Mara 225707 210214
13 Mbeya 83940 100265
14 Morogoro 310630 356049
15 Mtwara 462903 400311
16 Mwanza 328165 341198
17 Njombe 19668 17122
18 Pwani 289795 328175
19 Rukwa 96397 108537
20 Ruvuma 425566 312655
21 Shinyanga 163300 218898
22 Simiyu 87445 51365
23 Singida 30434 55831
24 Songwe 25525 27263
25 Tabora 336201 547564
26 Tanga 298121 478766
Kitaifa 5595916 5769837
Jedwali hapo juu linaonyesha idadi ya wagonjwa wa Malaria kimkoa

4.3 Mapambano dhidi ya Kifua Kikuu Nchini


Wizara kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya iliendelea na mapambano dhidi ya
ugonjwa wa kifua kikuu ambapo katika mwaka 2018 jumla 47,967 waligundulika kuwa
na vijidudu vya Kifua kikuu ikilinganishwa na wagonjwa 44,714 waliogunduliwa mwaka
2017. Tatizo la ugonjwa wa Kifua Kikuu umeendelea kuwa tatizo takribani mikoa yote
nchini kama inavyoonyesha katika jedwali hapa chini.

Idadi ya Wagonjwa wa Kifua kikuu na ukoma waliogundulika mwaka 2017


na 2018

Mwaka Mwaka Mwaka Mwaka


Mkoa
Na. Mkoa 2017 2018 Na. 2017 2018
1 Arusha 3,522 4,037 15 Mtwara 2,124 2,722
2 Dar Es Salaam 14,235 15,366 16 Mwanza 4,087 4,627
3 Dodoma 3,303 3,337 17 Njombe 1,381 1,363
4 Geita 2,941 3,842 18 Pwani 2,374 2,918
5 Iringa 1,689 1,521 19 Rukwa 864 881
6 Kagera 2,158 2,192 20 Ruvuma 1,509 1,452
7 Katavi 520 544 21 Shinyanga 2,533 2,444
8 Kigoma 1,119 1,176 22 Simiyu 1,404 1,282

11
9 Kilimanjaro 2,509 2,812 23 Singida 1,709 2,049
10 Lindi 1,155 1,674 24 Songwe 1,020 942
11 Manyara 2,625 3,445 25 Tabora 2,243 2,244
12 Mara 2,164 2,121 26 Tanga 2,716 2,773
13 Mbeya 3,765 3,270 27 Kitaifa 44,714 47,967
14 Morogoro 3,009 2,630

4.4 Huduma kwa Wagonjwa wa TB wanaogundulika kuwa na HIV 2017 na


Mwaka 2018
Katika kuimarisha tiba dhidi ya Kifua Kikuu na VVU, wagonjwa wote wanaogundulika
kuwa na kifua kikuu, hupimwa kama wanamaambukizi ya VVU. Hii inawawezesha
wagonjwa kutibiwa TB na VVU. Katika kipindi cha mwaka 2018 asilimia 99 ya
wagonjwa waliogundulika kuwa na maambukizi ya Kifua Kikuu walipimwa
VVU ambapo asilimia 31 kati yao walikutwa na VVU ikilinganishwa na mwaka
2017 ambapo asilimia 97 ya wagonjwa wa TB waliopima VVU kati yao
asilimia 34 waligundulika kuwa na VVU. Aidha kwa wale waliogundulika kuwa na
VVU asilimia 93 walianzishiwa dawa za ARV. Kiwango cha maambukizi ya VVU kwa
wagonjwa walio na TB kiko juu sana hivyo Sekta ya Afya inahakikisha kuwa wagonjwa
wote wanaogundulika kuwa na VVU/UKIMWI wanaanzishiwa dawa za ART. Kama
inavyoonyesha katika Jedwali lifuatalo
Wastani wa Wagonjwa wa TB na HIV kwa pamoja walioanzishiwa dawa za
ARV mwaka 2017 na Mwaka 2018

Na. Mkoa Mwaka Mwaka Na. Mkoa Mwaka Mwaka


2017 2018 2017 2018
1 Kilimanjaro 95% 89% 15 Shinyanga 94% 98%
2 Simiyu 95% 92% 16 Rukwa 94% 96%
3 Mbeya 93% 87% 17 Mara 78% 59%
4 Dodoma 95% 93% 18 Manyara 86% 94%
5 Kigoma 79% 68% 19 Kagera 96% 95%
6 Katavi 62% 96% 20 Singida 83% 80%
7 Morogoro 90% 95% 21 Songwe 95% 91%
8 Mwanza 95% 94% 22 Njombe 94% 92%
9 Tanga 91% 91% 23 Pwani 94% 92%
10 Lindi 98% 92% 24 Iringa 93% 93%
11 Tabora 86% 92% 25 Geita 97% 97%
12 Mtwara 58% 98% 26 Arusha 95% 98%
13 Dar Es Salaam 98% 96% Kitaifa 93% 93%
14 Ruvuma 97% 97%

Jedwali hapo juu linaonyesha mafanikio makubwa ya Mpango wa Taifa wa kutoa


matibabu ya ART kwa wangonjwa wote wa TB wanaogundulika kuwa na VVU/UKIMWI.

12
Kitaifa zaidi ya asilimia 93 ya wagonjwa wote wa TB wliogundulika kuwa na VVU
walianzishiwa dwa za ART
5.0 Magonjwa ya Mlipuko

Tanzania imeendelea kuwa salama licha ya tishio la kuwepo kwa Ugonjwa wa Ebola
katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Wizara imechukua tahadhari za kulinda
mipaka yake. Hivyo, hakukuwa na mgonjwa yeyote aliyegundulika kuwa na Ebola nchini
kwa mwaka 2017 na 2018.
Aidha, Serikali imeendelea na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu
ambapo Mwaka 2018 kulikuwa na wagonjwa 4,706 na vifo 84 ikilinganishwa na
wagonjwa 4,626 na vifo 93 mwaka 2017.
Kwa upande wa Ugonjwa wa Dengue watu 226 waliathirika mwaka 2018
ikilinganishwa na watu 65 mwaka 2017. Hakuna kifo kilichosababishwa na ugonjwa
huu.
Vilevile kulikuwa na wagonjwa 6 wa Chikungunya ambao walipatiwa matibabu mwaka
2018 na hakuna kifo kilichotokea.
HALI YA UGONJWA WA KIPUNDUPINDU KWA MWAKA 2017 NA 2018
2017 2018
Vifo vilivyotokana

Vifo vilivyotokana
na kipindupindu

na kipindupindu
wagonjwa wa

wagonjwa wa
kipindupindu

kipindupindu
Idadi ya

Idadi ya
Mkoa

1 Arusha 0 0 1892 33
2 Dodoma 277 8 593 21
3 D'salaam 296 4 0 0
4 Geita 0 0 0 0
5 Iringa 353 7 88 1
6 Kagera 0 0 0 0
7 Katavi 180 1 0 0
8 Kigoma 525 13 176 2
9 Kilimanjaro 1 1 47 1
10 Lindi 0 0 0 0
11 Manyara 48 4 75 0
12 Mara 115 0 0 0
13 Mbeya 1,260 17 0 0
14 Morogoro 341 10 56 0
15 Mtwara 0 0 0 0
16 Mwanza 0 0 0 0
17 Njombe 13 0 0 0

13
ko
2017 2018

a
18 Pwani 82 3 0 0
19 Rukwa 161 8 922 14
20 Ruvuma 247 8 374 3
21 Shinyanga 0 0 0 0
22 Simiyu 0 0 0 0
23 Singida 53 0 0 0
24 Songwe 725 4 484 9
25 Tabora 7 1 0 0
26 Tanga 168 2 0 0
Jumla 4,852 91 4,707 84

6.0 Vituo vya kutolea huduma za afya nchini


Hadi kufikia Desemba 2018, jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya vilifikia 7,768
kutoka vituo 7,435 mwaka 2017 sawa na ongezeko la vituo 333 kwa mwaka. Katika
vituo hivyo Serikali ilikuwa inamiliki asilimia 71 ya vituo vya kutolea huduma;
Mashirika ya dini asilimia 12, Taasisi za Serikali (Parastatal) asilimia 3 na vituo
binafisi asilimia 15. Wakati ambapo hospitli zilikuwa asilimia 3, Vituo vya afya
asilimia 11 na Zahanati asilimia 86.
Umiliki wa Vituo na Aina ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya Nchini Mwaka 2018

Watu Hospitali Aina ya vituo


Taasisi za Binafsi Umiliki wa vituo 3%
Dini 15%
2% Vituo vya
Afya
11%

Mashirika
ya Dini
12%
Serikali
71%
Zahanati
86%

7.0 Idadi ya Wananchi waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya


(NHIF)
Haadi kufikia Desemba mwaka 2018, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na jumla ya
wanachama wachangiaji wamefika 899,654 na ikihudumia jumla ya wanufaika 4,219,192 sawa
na asilimia 8 ya Watanzania wote. Kwa upande mwingine hadi kufikia Mfuko wa Afya ya Jamii

14
(CHF) unahudumia wanufaika 13,506,330 sawa na asilimia 25 ya Watanzania wote
ukilinganisha na asilimia 24 kwa kipindi kama hicho mwaka 2017. Aidha kwa ujumla wake NHIF
na CHF inahudumia wanufaika 17,725,522 sawa na asilimia 33 ya watanzania wote. Idadi ya
Wanachama wa NHIF kwa aina ya uanachama ni kama inavyoonyesha kwenye Jedwali hapo
chini.
Idadi ya Wanachama wachangiaji hadi 31 Desemba 2018

Idadi ya Wanachama wachangiaji hadi 31 Desemba 2018

(% ya Idadi ya
Aina ya Wanachama 2017 2018
wanachama)

Watumishi wa Umma 594,473 568,079 63

Wanafunzi 83,766 147,075 16

Mashirika Binafsi 38,413 59,486 7

Toto Afya Kadi 34,000 82,271 9

KIKOA 28,055 28,609 3

Viongozi wa Dini 4,661 7,480 0.80

Wanachama Binafsi 1,516 3,284 0.40

Wahe. Madiwani 3,799 2,496 0.30

Wahe. Wabunge 394 394 0.00

Ushirika Afya 480 0.10

Jumla 789,077 899,654

UKUAJI 14%

15
8.0 HITIMISHO

Kutokana na takwimu hizi ni Dhahiri kuwa Sekta ya Afya imepata mafanikio makubwa
katika mwaka 2018 na hii ni kutokana na jitihada za Serikali ya awamu ya Tano chini ya
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuwekeza kwenye afya za watanzania.
Katika mwaka huu wa 2019, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI
na wadau itaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha upatikanaji wa
huduma bora za afya kwa wananchi. Mikakati hii ni pamoja na;

 Kuendelea kutekeleza afua mbalimbali katika kuimarisha afya ya uzazi na mtoto


ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi wa mpango, utoaji wa chanjo, elimu kuhusu
mahudhurio ya kliniki na lishe bora kwa kuongeza idadi ya watoa huduma za afya
ya uzazi na mtoto wenye ujuzi, kuhakikisha dawa na vifaa tiba vya kutosha vipo
katika vituo vinavyotoa huduma za afya ya uzazi na mtoto, na kuboresha vituo
vinavyotoa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa kuweka miundombinu
inayohitajika (vyumba vya upasuaji, maji, umeme nk).
 Wizara imeanzisha Kada ya Watoa huduma za afya katika ngazi ya jamii. Ikiwa na
matarajio makubwa kuwa watumishi hawa watakaa na wanachi katika maeneo yao
na kuwa na jukumu la kuwahamasisha wananchi kuwa na tabia za kupima afya zao
na kuwaandikisha wazazi wote na Watoto katika rejesta zao ngazi za jamii ili
waweze kuwafuatilia kuhakisha wanapata huduma zote muhimu. Vilevile watakuwa
na jukuku la kuihamasisha jamii kuanza huduma za wajawazito mapema ili hatimaye
wapate huduma zote wao pamoja na Watoto watakaozaliwa, ikiwa ni pamoja na
kuelimisha vijana suala la makuzi na afya bora.
 Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwa ni
pamoja na kuendelea na ujenzi wa vituo vya afya ambapo katika mwaka 2018
maboresho yalifanyika katika vituo 318 kutoa huduma za CEmONC na hivyo kufikia
vituo 325 kati ya vituo vya afya 527 sawa na asilimia 61.7 ya vituo vyote vya afya
nchini. Aidha Serikali itaendelea na ujenzi wa hospitali za wilaya, ujenzi wa hospitali
katika mikoa ambayo haina hospitali za rufaa za mikoa.
 Kuendelea kuimarisha huduma za upatikanaji wa Damu salama
 Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya wateja wenye mahitaji ya huduma za
afya wanazipata katika ngazi ya msingi yaani kwenye zahanati na vituo vya afya.
Hivyo Serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuimarisha huduma katika ngazi
hiyo ili kuboresha afya za wananchi
 Kuendelera kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vyote vya kutolea
huduma ya afya nchini.
 Kuimarisha huduma katika ngazi ya Rufaa ili kuhakikisha huduma za kibingwa
zinasogezwa karibu na wananchi na kupunguza rufaa za nje ya nchi.
 Kuimarisha upatikanaji wa wataalam wa afya katika ngazi zote za kutolea huduma.

16
 Kuboresha huduma za kinga kwa kuanza kutumia wahudumu wa afya katika ngazi
ya jamii.

17