You are on page 1of 2

BENKI YA KCB TANZANIA KUTOA RUZUKU YA TSHS 85 MILIONI KWA

WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI

KCB Bank Tanzania.


Taarifa kwa umma
12 Juni 2019.

Benki ya KCB Tanzania leo imezindua awamu ya pili ya programu yake


ya 2jiajiri katika warsha iliyofanyika katika makao makuu yabenki hiyo
jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo iliyohudhuriwa na baadhi ya walengwa
wa programu ya 2jiajiri, wafanyakazi wa Benki ya KCB, waandishi wa
habari na wadau mbali mbali umeendelea kuonyesha dhamira ya dhati
ya benki hiyo katika kumnyanyua mwanamke wa Kitanzania.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2016, programu ya 2jiajiri imefanikiwa


kuwawezesha wanawake 256 wa Kitanzania katika sekta ya biashara
kwa kuwapa mafunzo mbali mbali na kuwapanulia wigo wa masoko ili
kukuza mitaji na uwezo wa kibiashara.

2jiajiri kwa Mwaka 2019 inafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya
kwanza ililenga katika kutoa mafunzo nadharia kwa wanawake 256
katika nyanja za kurasimisha biashara, usimamizi wa fedha na mafunzo
ya kuongeza mauzo na kukuza soko la biashara zao. Aidha wanawake
115 kati ya 256 walipitia mafunzo kwa vitendo katika nyanja mbali mbali.

Awamu ya pili ambayo imezinduliwa leo tarehe 12 Juni 2019 inatarajia


kutoa ruzuku ya TSH 5,000,000.00 kwa washiriki wa programu hiyo
ambao wamekamilisha na kufuzu awamu ya kwanza ya programu ya
2jiajiri. Jumla ya walengwa 17 watapitia mchujo ili kuhakikisha ustahili
wa na matumizi sahihi ya ruzuku hiyo ili kukuza biashara zao.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi.


Christine Manyenye alisema japo ruzuku hiyo haina marejesho, Benki ya
KCB itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wapokeaji ili
kuhakikisha wanawake hao wanafikia malengo yao ya kibiashara.
Aidha Bi. Manyeye aliainisha vigezo ambavyo wapokeaji wanatakiwa
kukidhi vikiwemo kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya Benki ya
KCB na matawi yake nchi nzima, lazima mpokeaji awe amekamilisha
mafunzo ya kinadharia na vitendo katika awamu ya kwanza, awe
muendesha akaunti ya 2jiajiri iliyo hai na awe mwenye cheti na leseni
halali ya usajili wa biashara.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Bhoke Mukoji Mhini, Mkurugenzi


Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya East Coast iliyo Kibaha ambaye ni
mmoja wa walengwa wa programu ya 2jiajiri alisema kwamba hajawahi
kuona dhamira ya dhati katika kumuwezesha wanawake wa Kitanzania
na kuwa Benki ya KCB na 2jiajiri ni mfano wa kuigwa na taasisi
nyingine. “KCB Bank na mpango wa 2jiajiri umenyanyua ufito wa
uwekezaji kwa jamii.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati


iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua
na kuenea katika nchi 6 za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda,
Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika
kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na
wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki
Afrika Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam,


Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya
KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua
milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika
kukuza sekta ya fedha nchini.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi


ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale
inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika
Mashariki.