You are on page 1of 2

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serengeti Breweries yatangaza mabadiliko ya uongozi wa juu


Dar es Salaam, 17 Juni, 2019: Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti
Breweries Limited (SBL) imemteua Mark Ocitti kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuchukua
nafasi ya Helene Weesie anayeondoka.

Helene amekuwa na SBL kwa miaka minne kuanzia mwaka 2015, kipindi ambacho kampuni
imeweza kuzindua bidhaa muhimu zilizosababisha ukuaji wa biashara kwa kiasi kikubwa
ikiwa ni pamoja na kampuni kupata tuzo za ubunifu na kuongezeka kwa uwekezaji. Helene
anaondoka kwenda kuchukua nafasi nyingine ndani ya Diageo barani Ulaya. Akiwa nchini
Tanzania atakumbukwa, bali na mambo mengine, kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya ndani
ya nchi.

Mkurugenzi mtendaji mpya, Mark Ocitti, kwa sasa anahudumu


katika nafasi sawa na hiyo katika kampuni ya Uganda Breweries
Limited (UBL) ambayo pia ni sehemu ya kampuni mama ya East
Africa Breweries Limited (EABL) inayoongoza kwa uzalishaji wa
vinywaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ocitti, chini ya
uongozi wake, UBL imeweza kupiga hatua kubwa katika
utendaji wake na kupelekea kukua kwa biashara.

Akizungumzia uteuzi wa Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa


Mtendaji Mkuu wa EABL, Andrew Cowan amesema: “Mark
Mark Ocitti amefanya mageuzi makubwa katika biashara yetu nchini
Uganda; ameongeza nafasi yetu kiushindani na kukuza faida ya UBL
kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Sina shaka kwamba kutokana na uzoefu wa uongozi
wa Mark, maono, pamoja na mipango mikakati yake shupavu, itaifanya biashara ya SBL,
inayokua kwa kasi kukua hata zaidi.”

…Mwisho…

Kuhusu SBL
Ikiwa imeanzishwa kama Associated Breweries mwaka 1988, Kampuni ya Bia Serengeti
(SBL) ni moja ya kampuni kubwa za bia nchini Tanzania, ambapo aina zake za bia
zinachangia zaidi ya asilimia 20 ya bidhaa hizo katika soko. SBL inaendesha viwanda vitatu
vilivyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara yake imekua na kuimarika zaidi na
asilimia 51 ya hisa mwaka 2010 zilizochukuliwa na Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki

Mark Ocitti
(EABL) zimeshuhudia ongezeko la uwekezaji katika kukua zaidi na hivyo kusababisha
kuongezeka kwa fursa zaidi za ajira kwa watu wa Tanzania.

Aina za bia zinazozalishwa na SBL ambazo zimepata tuzo kadhaa za kimataifa ni pamoja
na Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout,
Uhuru na Kick.

SBL pia ni wazalishaji vinywaji vikali vinavyofahamika duniani kama vile Johnnie Walker
Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream..

………………………………………………………………………………………………………………………………………………

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na;

John Wanyancha
SBL Corporate Relations Director
Tel: 0692148857
Email: john.wanyancha@diageo.com

2|Page