You are on page 1of 12

www.annuurpapers.co.

tz

Sauti ya Waislamu

Sheikh Simba alia kupuuzwa Makadhi wake Uk. 11

Serikali, Tume ya Katiba zalaumiwa Aliyosema Sheikh Mohamed Issa yametimia

Hali ya Sheikh mbaya gerezani

ISSN 0856 - 3861 Na. 1089 SHAWWAL1434, IJUMAA , SEPT. 6-12, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

ALIYEKUWA Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, Mansour Yussuf.

MZEE Moyo (kushoto) na Mohamed S. Riami "Eddy" wakiwa katika kongamano Bwawani.

Ustaarabu wa Kiislamu ni lulu


Na Mwandishi Wetu
USTAARABU wa Kiislamu ni hazina kubwa iliyojengwa na Misingi ya Dini ya Kiislamu, inayofaa kuenziwa kwa hali zote. Hayo yamebainishwa na Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga Kongamano juu ya historia na ustaarabu wa Kiislamu. Kongamano hilo lilifunguliwa Rasmi na Raisi wa Zanzibar Alhaj Dr. Ali Mohamed Shein, ambaye aliwahamasisha

Wimbo Sisi Sote wamliza Mansour


Karume, Maalim Seif wasema NO Membe atajwa kuhujumu Zanzibar Ni katika mambo ya Wakfu, Nje
Na Mwandishi Wetu
A L I Y E K U W A Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki, amejikuta akibubujikwa machozi alipopanda jukwaani na kuimbiwa wimbo wa Sisi Sote tumegomboka. Huo ulikuwa ni ule ummati wa Wazanzibari waliokusanyika katika ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Jumamosi iliyopita, wakiwa na kauli mbiu ya Zanzibar kwanza, wakiweka kando siasa za

Wa i s l a m u k u e n z i Ustaarabu uliokamilika w a Ta n g u A s i l i y a Watu wa Mwambao wa Afrika ya Mashariki na Kati. Ustaarabu wa Kuheshimika. Katika kongamano hilo

Inaendelea Uk.4

Inaendelea Uk.3

2
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786 Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: annuurpapers@yahoo.co.uk Ofisi zetu zipo: Manzese Tip Top Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

AN-NUUR

Hali ya Sheikh mbaya gerezani


Na Waandishi wetu, Zanzibar

Tahariri/Habari

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

TUMEARIFIWA kwamba ile m i s w a d a ya sheria ya marekebisho ya mabadiliko ya Katiba na suala la zima kuhusu kura ya maoni ya r a s i m u ya katiba mpya, inawasilishwa katika vikao vya Bunge linaloendelea mjini Dodoma hivi sasa. Miswada hiyo i n a wa s i l i s h wa k u j a d i l i wa n a wabunge ili kutoa nafasi k wa wa b u n g e kuchambua v i p e n g e l e v ya mbalimbali sheria hizo kuanzia uteuzi wa Kamati ya U t e u z i wa Bunge la Katiba, k u t i z a m a muundo na uwiano wa viongozi na wabunge katika Bunge la Katiba. Aidha kujadili juu ya mamlaka itakayosimamia kura za maoni

Tuchunge nafasi ya Zanzibar katika miswada ya sheria Katiba mpya

kuhusu rasimu hiyo na mambo m e n g i n e mbalimbali yanayohusiana na mchakato mzima wa rasimu ya Katiba mpya. Wakati Bunge l a J a m h u r i ya Muungano likipata nafasi ya kujadili suala hilo nyeti, ikumbukwe kuwa kuna chombo kingine cha kutunga sheria Zanzibar. Nacho si kingine bali ni Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. Baraza hili tunaona kuwa kama mdau muhimu wa mustakabali wa katiba mpya nchini, lina nafasi yake katika kujadili na kutoa mapendekezo yake juu ya miswada ya sheria ya mabadiliko haya ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

PAMOJA na taarifa r a s m i ya D a k t a r i kutoka Hospitali Kuu ya M n a z i M m o j a , Zanzibar inayoeleza hali ya afya ya Naibu Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI) Sheikh Azzan Khalid Hamdan ikidhoofika akiwa gerezani, Kiinuamiguu, mjini hapa, bado Serikali ya Zanzibar imeonekana kupata kigugumizi. Ta a r i f a h i y o inathibitisha kwamba hali ya Sheikh Azzan, anayeendelea kusotea gerezani kwa takriban mwaka mmoja sasa, akijumuika na

Maamiri wa JUMIKI na wale wa Jumuiya ya Maimamu ya Zanzibar (JUMAZA), hali yake imekuwa ikidhoofika kutokana na tatizo katika mfumo wake wa m a j i n d a n i ya figo kupata matatizo, kama walivyobaini m a d a k t a r i waliomfanyia uchunguzi hivi karibuni. Madaktari hao kupitia vipimo vya ultrasound wamebaini hitilafu hiyo na kupendekeza haraka iwezekanavyo Kiongozi huyo wa Kiislamu kupata matibabu ya haraka ikiwezekana nje ya Nchi. Ripoti ya Daktari

waliyoiona waandishi wa habari inathibitisha kuwapo kwa hitilafu hiyo inayoweza k u o n g e z a u k u b wa wa tatizo na kama wa l i v y o p e n d e k e z a wa t a a l a m u , i wa p o Kiongozi huyo hatapatiwa matibabu ya haraka. Haya ni matatizo ambayo ufumbuzi wa k e h a p a k we t u ni tabu kidogo waliofanikiwa wamepelekwa India au kwengineko na wasifanye mzaha, amekaririwa akisema mmoja wa wataalamu wa mambo ya afya ya jamii Nchini, mara alipoipiga macho ripoti hiyo ya kusikitisha.

Ubungo Islamic high School


P.o. Box 55105 Tel: 2450069, 0712 974428, fax: 2450822 Dar es salaam. E-mail: ipcubungoislamic@gmail.com

MAANDALIZI YA KUJIUNGA KIDATO CHA I, 2014 (PRE- FORM ONE ORIENTATION COURSE)
UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL inatangaza program maalum ya maandalizi ya kujiunga na kidato cha kwanza 2014. Program hii itaanza tarehe 16/09/2013 hadi tarehe 16/12/2013. Jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 9:00 Alasir. Masomo yatakayofundishwa ni:Elimu ya dini ya Kiislamu, English language, Lugha ya kiarabu, basic Mathematics na Computer. Fomu za Kujiunga zinapatikana shuleni BURE. Mlete mwanao apate Elimu yenye tija itakayomweze kujiunga na kidato cha kwanza. Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba: 0714 888 557/0712 974428 Wabllah tawfiq Mkuu wa Shule

Habari

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Inatoka Uk.1 CCM na CUF. Mara tu alipopanda jukwaani, ummati wa watu waliojazana katika ukumbi huo hadi kusababisha hali ya hewa kuwa nzito, ulisimama na kuimba wimbo huo mashuhuri unaoimbwa katika sikukuu za mapinduzi na mashujaa. Ni katika wimbo huo ambapo wanajeshi, wanamapinduzi, wazalendo na wananchi k wa u j u m l a wa n a t o a kauli, ahadi na kiapo cha kuipigania na kulinda nchi. Na hiyo ikalipua hamasa ya kutokurudi nyuma katika kupigania nchi pamoja na Dola ya Zanzibar yenye mamlaka kamili. Hapo ndio wengi wakaanza kutoka machozi huku Mansour akishindwa kujizuiya na kujikuta akilazimika kufuta machozi kwa vidole mwisho akatoa kitambaa. Hiyo ilitokana na ujumbe uliokuwepo katika wimbo huo ukihimiza ukombozi na kuwasifu walioikomboa Unguja kutoka kwa wakoloni ambapo sasa wanajiona wanalazimika kuipigania tena kurejesha hadhi na mamlaka yake. Pamoja na mengi aliyozungumza, lakini alichohimiza Mansour ni juu ya Wazanzibar kutokurudi nyuma kupigania mamlaka kamili ya nchi yao. Alisema, kwa kuwa mtumishi wa Serikali katika nafasi mbalimbali ameona dhulma na hujuma inayofanywa dhidi ya Zanzibar. Akigusia suala la mafuta na gesi, alionyesha jinsi ambavyo kwa muda mrefu Tanzania Bara imekuwa ikichimba gesi, lakini Zanzibar haipati kitu kutokana na pato hilo. Hata hivyo, ilivyokuja kwa Zanzibar kutafiti na kuchimba mafuta na gesi, vikwazo vingi vimewekwa ikidaiwa kuwa hilo ni jambo la muungano. Hata pale Zanzibar iliposema kuwa ipo tayari kutoa asilimia 60 ya pato la gesi kwenda Bara na Zanzibar kubaki na 40%, bado haikukubaliwa. Ndio hapo ikafika mahali wakasema kuwa inabidi wasimame imara kuhakikisha wanalitoa suala la mafuta na gesi katika mambo ya

Wimbo Sisi Sote wamliza Mansour


muungano. Kabla ya kusimama na kuzungumza Mansour, walitangulia wasemaji wengine akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya M a r i d h i a n o , M z e e Nassor Moyo ambaye aliwatahadharisha Wazanzibar juu ya fitna. Katika nasaha zake Mzee Moyo alisema kuwa kwa muda mrefu Zanzibar i m e k u wa k a t i k a f i t n a ambapo imeleta maafa ya kuuwana na kwamba sasa ni wakati wa kumaliza fitna hiyo. Alisema, Rais Mstaafu Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, washasema N0 (hapana) kwa mauwaji na siasa za chuki na uhasama, ndio maana walijenga mazingira ya kuleta Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Akasema kuwa wapo watu wasioitakia mema Zanzibar ambao wanataka daima wawaone Wazanzibar wakiuwana na kudumaa katika maendeleo. Na kwamba hao ndio watakaotaka kuleta fitna za vyama kuwatoa Wazanzibar katika agenda yao ya Mamlaka Kamili. Kwa hiyo akawataka kuwa macho, kuwa wamoja na kuhakikisha kuwa wanaitumia fursa hii ya kuandika Katika Mpya kuipata Zanzibar waitakayo. Kwa upande mwingine akasema kuwa umefika wakati wa kuichomoa na kuionyesha hadharani Serikali ya Tanganyika iliyojificha ndani ya Serikali ya Muungano, hali ambayo ndiyo inaendeleza jinamizi la kuikandamiza Zanzibar. Akigusia bila ya kusema kwa uwazi, alionyesha k u wa f i t n a Z a n z i b a r imekuwa ikiendelezwa na mtindo wa Chama tawala CCM kuiba kura na kunyakua madaraka kwa nguvu bila kujali kura za wananchi. Alisema, hata Rais Mstaafu Amani Karume aliligusia hilo pale alipowaambia wahafidhina wasio taka maridhiano kuwa hawana uwezo wa kumpa ushindi wa asilimia 60. Ushindi wetu Unguja mnaujua (unavyopatikana), alisema Mzee Moyo bila kufafanua n a k u n u k u u k a u l i ya

BAADHI ya washiriki wa kongamano la Bwawani. M h e s h i m i w a A m a n i Bernard Membe, aliondoa y a o n d o l e w e k w e n y e K a r u m e a k i w a a m b i a kipengele cha misaada ya Muungano ni Uraia na wa n a - C C M h a o k u wa Wakfu kutoka Mascut Uhamiaji, Sarafu na Benki yeye hayupo Ikulu kwa kwa vile tu misaada hiyo Kuu, Mambo ya Nje na ajili ya kusimamia fitna na i n g e k u w a i e l e k e z w e Usajili wa Vyama vya Siasa. mauwaji. Zanzibar. Mapendekezo hayo Mjumbe mwingine wa Akifafanua alisema, yalisomwa na Mwakilishi Kamati hiyo Eddy Riami u j u m b e w a M a s c u t wa Mji Mkongwe ambaye aliwahimiza Wazanzibar uliotembelea Tanzania, pia ni mjumbe wa kamati kusimama katika agenda p a m o j a n a m a m b o hiyo, Ismail Jussa katika m o j a t u : k u p i g a n i a m e n g i n e , w a l i t a k a Kongamano la Jumamosi utaratibu wa iliyopita. Zanzibar yenye mamlaka kuwekwa namna ya kutoa misaada Kila nchi mshirika kiamili. (kwa Zanzibar ) kupitia (Zanzibar na Tanganyika), Na kwamba wawafute taasisi ya Wakfu. ibakie na uraia wake na na kuwatupilia kwa mbali H a t a h i v y o , b a a d a mtu kuwa na uraia wa nchi viongozi wote wasiotaka y a t a r a t i b u z o t e mshirika ndiko kumpe kuona Zanzibar huru yenye kukubalika na kusubiri uhalali wa kuwa raia wa mamlaka yake kamili. kusainiwa makubaliano shirikisho. Alisema Jussa na Akizungumza kabla ( M e m o r a n d u m ) , ya kusimama Mansour, M h e s h i m i w a Wa z i r i kuongeza kuwa uchumi Makamu Mwenyekiti wa Membe alifuta kipengele si suala la Muungano hata katika Katiba ya sasa Kamati ya Maridhiano, cha Wakfu. na kwamba nyenzo za Mheshimiwa Abubakar Alisema, hata ukitizama kuendeshea na kusimamia Khamis Bakari alisema watumishi wa Serikali u c h u m i wa n c h i k wa k u w a k u n a m a m b o wakiwemo mabalozi katika maana ya sera za fedha yanafanyika makusudi kwa nchi za nje na Umoja wa na uchumi zimeendelea roho mbaya tu kuihujumu Mataifa, Zanzibar imekuwa k u d h i b i t i w a k u p i t i a ikipunjwa wakati inadaiwa Serikali ya Muungano. Zanzibar. Vyombo vikuu N a k w a m b a i l i kuwa hiyo ni Wizara ya vinavyosimamia sera hizo kuondokana na hali hiyo Muungano. N i k a t i k a h a l i h i y o ambavyo ni Benki Kuu ya ni lazima Tanganyika Mheshimiwa Abubakar Tanzania (BoT), Mamlaka isimame kama Tanganyika a mba ye ni Wa z i r i wa ya Mapato Tanzania (TRA) n a Z a n z i b a r i s i m a m e Kariba na Sheria (ZNZ) na Wizara ya Fedha ya k i v ya k e n d i o z i f a n ye na Mwakilishi wa Jimbo la Serikali ya Muungano muungano wenye haki Mgogoni, Pemba; alisema v i m e k u w a v i k i f a n y a sawa. k u w a k a t i k a m a m b o uamuzi na kuyatekeleza A l i s e m a , k a t i k a ambayo ni lazima yatiwe bila ya kuzingatia kuwa mfumo wa sasa ambapo katika Katiba Mpya, ni Z a n z i b a r i n a t e g e m e a Tanganyika imejificha pamoja na kuirejeshea uchumi wa utoaji huduma ndani ya Tanzania, hakuna Zanzibar mamlaka ya na haiwezi kuwa sawa na namna Zanzibar inaweza kuwa na Wizara yake ya uchumi wa Tanganyika ambao unategemea kupata haki yake. Mambo ya Nje. Akitoa mfano aligusia Wakati huo huo, Kamati rasilimali, alisema. Kwa upande mwingine hasara inayopata Zanzibar ya Maridhiano imetoa akasema kuwa suala la kwa kutokuwa na Mambo maoni yake ya Rasimu vyama vya siasa linapaswa ya Nje. ya Katiba ya Jamhuri ya Akasema, ni kiasi miezi Muungano wa Tanzania kuondolewa katika mambo miwili tu iliyopita ambapo k wa k u t a k a Z a n z i b a r ya Muungano ili Zanzibar Waziri wa Mambo ya ijitegemee karibu kwa kila na Tanganyika, kila moja iandikishe vyama vyake Nje na Ushirikiano wa kitu. Kimataifa Mheshimiwa M a e n e o i n a y o t a k a vya siasa.

Ustaarabu wa Kiislamu ni lulu


Inatoka Uk. 1 ilidhihirika wazi kuwa licha ya hujuma za makusudi za kuwadhoofisha Waislamu, Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu katika Mwambao wa A f r i k a M a s h a r i k i na Kati imeanzia mbali na iliyotambulika ulimwenguni. W a t a f i t i wameyabainisha hayo katika Kongamano hilo la Kimataifa la Siku tatu juu ya Historia ya Ustaarabu wa Kiislamu Afrika Mashariki na Kati, juma hili, lililofanyika maeneo ya Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Hilo ni kongamano la aina yake lililoandaliwa k w a p a m o j a k a t i ya Mamlaka ya Taifa ya Nyaraka na Makumbusho ya Oman (NRAA); Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Historia ya Kiislamu, Sanaa na Utamaduni (IRCICA); na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Watu mashuhuri na Viongozi wa Jumuiya na Taasisi mbali mbali za kitaifa na kimataifa, za Kiislamu, Watafiti, Wanataaluma na wasomi walijumuika katika Kongamano hilo. Hao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani (IOC) Dr. Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Afrika (AU (zamani OAU) Dr. Salim Ahmed Salim, Balozi wa Oman Nchini Sh. Saleh bin Suleiman Al Harthi, Mwenyekiti wa NRAA Dr. Hamed bin Mohammed Al Dhawyani na Makamu Mkuu wa SUZA, Prof. Idris Ahmad Rai. We n g i n e m i o n g o n i mwa watu mashuhuri waliohudhuria ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Bw. Omar Othman Makungu, M s h a u r i M a a l u m wa Raisi wa Burundi Dr. Muhammad Rukara Khalfan, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Ali Juma Shamhuna, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sh Saleh Omar Kabi, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar Bw. Said Ali Mbarouk, Raisi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi, n a K a t i b u M k u u wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sh. Ahmed Saud Al Siyabi. Wasomi na watafiti walitumia viashiria mbali mbali vya kuthibitisha ujio wa Ustaarabu wa Kiislamu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kusogea mbali zaidi katikati ya Bara la Afrika, tangu Karne za Awali za Hijria na Tarehe ya Kiislamu. Miongoni mwa viashiria hivyo ni Utafiti wa M a k u m b u s h o n a Nyaraka uliowasilishwa na Profesa wa Mambo ya Historia kutoka Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza, Dr. Timothy Insoll, ambaye amefananisha kwa ushahidi wa akeolojia wa vifaa vilivyotumika katika Mashariki ya Kati vilivyoshabihiana na vile ambavyo wakitumia watu wa tangu zamani katika Afrika ya Mashariki na Kati. Wataalamu, Dr. Farhat Jabir Profesa wa Mambo ya Taaluma ya Dini na Lugha ya Kiarabu wa Chuo Kikuu cha Tuni nchini Tunisia, Dr. Nahed Abdul Kareem wa Chuo Kikuu cha Sultan Kaboos nchini Oman, Dr. Mubarak Abdullah Al Rashdi Mkuu wa Idara ya Taaluma za Kiislamu Chuo Kikuu cha Sultan Kaboos Oman, Dr. Fouad Abdel Wahab Al Shami wa Chuo Kikuu cha Sanaa cha Yemen, na Dr. Rashid Hamad Al Husaini wa C h u o K i k u u c h a Sayansi cha Oman, pamoja na mambo mengine wameainisha umashuhuri wa Uislamu na Wasomi wa Kiislamu wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati waliotaheshimika ulimwenguni tangu asili na zama, kama dalili ya historia kubwa ya eneo hili katika Ustaarabu wa Kiislamu. Wataalamu, Dr. Mehmet Ipsirli wa Chuo Kikuu cha Fati nchini Uturuki, Dr. Ahmed Ibrahim Al Kindi wa Chuo Kikuu cha Sayansi nchini Oman, Dr Wafaa Al Drissi wa Chuo Kikuu cha Tunis, Dr Abuyaasir Kame wa Chuo Kikuu cha Eldoret nchini Kenya, na Sh. Muhana Khalfan Othman Al Kharousi Mtafiti na Mwandishi Mashuhuri wa Oman, walithibitisha heshima ya Ustaarabu wa Kiislamu Afrika Mashariki na Kati, ambapo hata Watawala Wakuu wa Dola ya Othman iliyokuwapo Andalus na Kostantania, Istanbul, Uturuki, waliwaheshimu Watawala wa Mwambao huu pamoja na kuwatumia mialiko ya heshima, kwenda kuonana nao. Ni mengi yaliyofichuka katika Kongamano hilo la Kihistoria katika mnasaba wa Ustaarabu wa Kiislamu Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Tanzania Bara, Mombasa Kenya, Uganda, Ufalme wa Baganda, Malawi, Mozambique Sofala, na Dola ya Asili ya Zanzibar, yakiwamo ya utamaduni wa asili ulioendana na Mila na Silka za Kiislamu na Bara Arabu. Wapo waliobainisha kwamba hata Ulimwengu wa Waarabu ulikuwa na mengi ya kujifunza kutokea maishani mwa Wa t u wa U k a n d a wa Afrika mashariki na Kati. Msisitizo wa Kongamnano hilo ni pamoja na haja ya waislamu kushikamana na kurejesha hadhi yao na ya ustaarabu wao uliojengeka kwa Misingi imara ya Dini ya Kiislamu pasi na kuyumbishwa na harakati za makusudi za kudhoofisha murua wa jamii za kiislamu, zikiwamo mbinu za utandawazi.

Habari/Tangazo

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Msisitizo huo pia ulikwenda sambamba na wasia wa makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akilifunga Kongamano hilo, akasema Ustaarabu wa Kiislamu ni hazina kubwa iliyojengwa na Misingi ya Dini ya Kiislamu, inayofaa kuenziwa kwa hali zote. Kongamano hilo lilifunguliwa Rasmi na Raisi wa Zanzibar Alhaj Dr. Ali Mohamed Shein, aliyewahamasisha waislamu kuenzi Ustaarabu uliokamilika w a Ta n g u A s i l i y a Wa t u w a M w a m b a o wa Afrika ya Mashariki na Kati, Ustaarabu wa Kuheshimika.

Bismillahir Rahmanir Raheem

KIGAMBONI /KIGOGO

CU.124

CHUO CHA UALIMU

CU.130

NAFASI ZA MASOMO
UALIMU: STASHAHADA (E Moja Na S Moja) GRADE 3A ( Div. IV-27) CHEKECHEKEA (Div. IV- 28 na Kuendelea)
(2013-2014)

TEACHERS COLLEGE

Note: Nafasi za Udhamini kwa waliopata viwango Ngazi ya Diploma na Cheti. Wahi, Nafasi Chache!
(Asiyekuwa na Viwango anaruhusiwa kusoma Ualimu huku anarudia Mitihani) Secretarial Studies, Records Mgt, Project Planning & Mgt, ICT, Simplified Accountancy, Computer Applications
Kozi za Biashara

0715-860120 / 0654- 580924

Habari za Kimataifa

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Assadi akishambuliwa kutaibuka vita vya ukanda mzima


DAMASCUS R a i s wa S y r i a B a s h a r a l Assad, ametahadharisha kwamba iwapo yatafanyika mashambulizi yeyote dhidi ya nchi yake kutoka Mataifa ya Magharibi, basi itarajiwe kuibua vita vya kanda nzima. Aidha ameongeza kuwa iwapo Marekani na Ufaransa zitaamua kuishambulia Syria, machafuko na ghasia vitapanuka zaidi na kusababisha hatari ya kuzuka vita eneo zima linalozunguka nchi hiyo (Mashariki ya Kati). Rais Assad pia ametoa changamoto kwa Washington na Paris kwamba, kama kweli mataifa hayo yana ushahidi wa madai kwamba Damascus imetumia silaha za sumu, basi na mataifa hayo yaonyeshe na kuthihirisha ushahidi huo. Bila shaka kauli ya Rais Assad inakuja kufuatia madai ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ambaye alishaeleza kuwa Marekani ina ushahidi kwamba serikali ya Syria imetumia silaha za sumu kuwaangamiza raia wake. Kauli ya Rais Assad imeungwa mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, Jumatatu iliyopita, pale alipozungumza na vyombo vya habari Moscow, ambapo aliitaka Marekani kutoa ushahidi wa uchunguzi wake uliodai kuwa serikali ya Syria inatumia silaha za sumu nchini Syria. Kwa upande mwingine, Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein D e h q a n , a m e s e m a Te h r a n iliitahadharisha Marekani miezi nane iliyopita, juu ya kupelekwa waasi wa Syria. Urusi tayari imeshasema kuwa ina ushahidi wa kutosha, unaothibitisha kuwa waasi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani na rafiki zake, ndio waliotumia gesi ya sumu dhidi ya wananchi na jeshi la serikali ya nchi hiyo. Kuhusu madai ya Marekani

Urusi waitaka Marekani kuonyesha ushahidi wake


kuwa ina ushahidi unaothibitisha kwamba silaha za kemikali zimetumika nchini Syria, afisa huyo wa UN amesema kuwa, Umoja wa Mataifa ni taasisi pekee inayoweza kutoa maoni kwa uhakika na kwa uwazi kuhusu suala la kutumiwa au kutotumiwa silaha za sumu nchini Syria na kwamba kwa sasa njia za kijeshi dhidi ya Syria hazipaswi kuzingatiwa. Baada ya kushindwa kupata uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa, Obama amesema kuwa Marekani itaishambulia Syria pale Congress itakapoafiki suala hilo. Wakati hali ikiwa hivyo, timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa iliyokuwa ikichunguza silaha hizo huko Damascus bado haijatangaza ripoti yake. Hata kabla ya kutangazwa ripoti ya UN baada ya wiki mbili za kuanza uchunguzi wa madai kuwa serikali ya Damascus ndiyo iliyotumia silaha za kemikali, Marekani imeamua kutangaza kuwa itaishambulia Syria. Hayo yanajiri huku ikifahamika kwamba Marekani na washirika wake wa Magharibi pamoja na baadhi ya nchi za Kiarabu, katika miaka miwili iliyopita wametumia mamilioni ya dola kuwapa silaha za kisasa waasi wa Syria ili kuangusha serikali ya Damascus. Imeelezwa kwamba lengo la kundi hilo la Wamagharibi na Waarabu lilikuwa kudhoofisha jeshi la Syria, na hivi sasa silaha za kemikali linatumiwa kama kisingizio cha mwisho cha kukabiliana na serikali ya Damascus. Fikra za walio wengi zinatawaliwa na swali kwamba, ni kwa nini Marekani inashabikia kuishambulia Syria hata kabla ya kutangazwa ripoti ya Umoja wa Mataifa? Na je, Marekani inaweza kuhalalisha vipi misimamo yake hiyo ya kindumilakwili?

Ukabila waitesa Kenya


TAKRIBAN watu elfu sitini wamelazimika kuyakimbia makazi yao nchini Kenya, kufuatia mapigano ya kikabila. Shirika la Msalaba Mwek u ndu la K en ya limetangaza kuwa, kufuatia kuibuka mapigano ya kikabila n c h i n i h u m o , wa t u wanaokadiriwa kufikia elfu sitini wameukimbia m j i wa m p a k a n i wa Moyale na kukimbilia nchi jirani ya Ethiopia. Afisa mmoja wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ameziambia duru za habari kwamba, baada ya mapigano ya kikabila yaliyozuka Ijumaa iliyopita huko Kaskazini mwa Kenya, vijiji tisa vimesalia bila wakazi b a a d a ya wa t u wa k e kukimbia, huku nyumba arobaini zikichomwa moto kufuatia mapigano hayo. Katika hali nyingine, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, amemshambulia vikali Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga akimtaka kuufyata ulimi wake kama hana jipya la kuwaambia wananchi. Rais Kenyatta alikuwa akimjibu Bw. Odinga, ambaye alisema serikali inatoa vyeti vya kumiliki ardhi kwa wakazi wa pwani wakati wakuu wa serikali hiyo ndio wezi nambari moja wa ardhi katika eneo hilo. Kenyatta amemwambia Odinga asahau masuala

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (kushoto), Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga.

Rais Kenyatta na Raila wazidi kulumbana


ya siasa na aisaidie serikali kutatua matatizo ya ardhi na kama hawezi anyamaze kimya. Rais Kenyatta aliongeza Waziri Mkuu huyo wa zamani anapayuka ovyo na kwamba, bado anasumbuliwa na jinamizi la kushindwa kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa Machi 4. Vita vya maneno kati ya Bw. Odinga na wakuu wa s e r i k a l i , h u s u s a n Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto, vimeendelea kwa muda s a s a h u k u b a a d h i ya wachambuzi wakisema Odinga anajaribu kuvutia wanahabari ili nyota yake ya kisiasa isififie haraka.

Nyumba za Waislamu Myanmar zateketezwa Polisi Misri watuhumiwa kumnyanyasa Badie


PHINON PEIN Mamia ya Waislamu nchini Mynamar, wamebaki bila makazi baada ya Mabudha we n ye m i s i m a m o mikali kuchoma moto nyumba na maduka yao katika eneo lenye machafuko la Sagaing. Maafisa wa eneo hilo wamesema kuwa, zaidi ya watu 300 wanahifadhiwa katika shule baada ya genge la Mabudha wenye misimamo ya kibaguzi ya kihafidhina kuchoma moto nyumba na maduka yao. Hii ni mara ya nne vurugu za kuwashambulia Waislamu zinatokea huko katikati na kaskazini mwa Myanmar kwa mwaka huu pekee. Vurugu kama hizo zilitokea mwaka uliopita katika jimbo la magharibi la Rakhine, ambapo karibu Waislamu 200 wa kabila la Rohingya waliuawa. Hayo yanajiri huku serikali ya nchi hiyo ikishindwa kuzuia mashambulizi hayo na jamii ya kimataifa ikiendelea kupigia kimya jinai hizo wanazofanyiwa Wa i s l a m u n c h i n i Myanmar.
CAIRO Wakili wa Wanaharakati wa Ikhwanul Muslimin nchini Misri, amesema polisi nchini humo wamemnyanyasa k i o n g o z i wa k i r o h o wa wanaharakati hao Mohamed Badie, wakati ilipomkamata. Wa k i l i M u h a m m a d Gharieb amesema, Badie a l i va m i wa n y u m b a n i k wa k e , a k a p i g wa n a kutolewa matusi na kwamba, alipoteza meno yake kutokana na kipigo alichopewa na polisi hao Kwa upande mwingine k e s i ya k u h u k u m i wa v i o n g o z i n a wa f u a s i 64 wa Harakati ya Ikhwanul Muslimin ya

Misri na pia wafuasi wa rais aliyepinduliwa Muhammad Musri, imefanyika Jumatatu yawiki hii katika mkoa wa kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Watu hao wanashitakiwa kwa tuhuma za kufanya uchochezi uliosababisha kushambuliwa askari jeshi na pia kuhujumiwa makanisa katika mkoa wa Suez. Tangu Julai 3 mwaka huu, Misri imetumbukia katika machafuko na ghasia baada ya jeshi kufanya mapinduzi ya kumuondoa madarakani Muhammad Mursi, rais wa kwanza aliyechaguliwa na wananchi kidemokrasia nchini humo.

Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Iraq kutoruhusu anga yake kutumiwa kuishambulia Syria


MSEMAJI wa Waziri Mkuu wa Iraq Ali al Mousawi, amesisitiza kuwa nchi hiyo inapinga mashambulizi dhidi ya Syria na kwamba haitaruhusu anga yake kutumiwa katika mashambulizi yanayoweza kufanywa dhidi ya nchi jirani ya Syria. Ali al Mousawi, amesema hayo kufuatia msimamo wa hivi karibuni wa Marekani na Uingereza wa kutaka kuishambulia Syria na kuongeza kwamba, katiba ya Iraq hairuhusu ardhi yake kugeuzwa sehemu ya kushambulia nchi nyingine. Wakati hayo yanaripotiwa, Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema kwamba hakuna ushahidi kwamba jeshi la Syria limefanya shambulizi la silaha za kemikali kusini mwa nchi hiyo. Putin amesema hayo katika mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa U i n g e r e z a D a v i d Cameron. Jumatatu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov, pia aliionya Marekani kuishambulia kijeshi Syria akisema, matokeo yake yatakuwa na athari mbaya na ya muda mrefu, sio tu katika eneo la Mashariki ya Kati bali pia kaskazini mwa Afrika kwa ujumla. Kuingilia kwa namna yeyote kijeshi nchini Syria bila kuithinishwa na Baraza la Usalama la UN, kutakuwa ni kuvunja sheria ya kimataifa. Lavrov aliwaeleza waandishi wa habari jijini Moscow mapema wiki hii. Viongozi wa Washington, Uingereza, Ufaransa na Istanbul wametaka hatua za k i j e s h i k u c h u k u l i wa kumwadhibu Rais Bashar Al-Assad kwa kile walichokiita ametumia sialaha za sumu. H a t a h i v y o wa k a t i mataifa hayo yakitangaza nia ya kutaka kuinguilia mzozo wa Syria kijeshi bila hata ya udhibi ya UN, bado wakaguzi wa silaha za sumu wa UN ndio kwanza wameanza kazi yao na bado hawajathibitisha iwapo kuna matumizi ya silaha za sumu wala kubainisha ni upande gani unaotumia silaha hizo kato ya pande

Blix aitahadharisha Marekani kuhusu Syria

madai ya kuweko

MKUU wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Hans Blix. mbili zinazozozana za waasi na serikali. Viongozi wa Mataifa ya Magharibi wanatoa maelezo yanayoonyesha kuwa hawatasubiro matokeo ya ukaguzi, tayari wameamua kila kitu alisema Lavrov. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague alisema Uingereza imeshawishika kuwa Rais Assad yupo nyuma ya shambulio la Agost 21 na wameshakubaliana na Marekani na Ufaransa katika kujibu mapogo. Waziri wa mambo ya Nje wa Uturuki, Ahmet Davutoglu naye alisema nchi yake itaungana na muungano wa mataifa hayo dhidi ya Syria iwapo UN itashindwa kuchukua hatua. Rais Assad ameshajibu misimamo ya mataifa hayo aliyoiita kuwa ni nonsense, wakati alipokuwa akifanya mahojiano na gazeti la Izvestia la Urusi mapema wiki hii. Urusi ambayo imekuwa ikitumia kura yake ya veto kwenye Baraza la Usalama la UN kuzua mikakati ya kuiadhibu Syria, wiki hii imeitaka Marekani kutorudia makosa ya siku za nyuma kama yale ya kuivamia Uraq mwaka 2003. Marekani na washirika wa k e wa l i i s h a m b u l i a Uraq bila ya udhini ya U N , b a a d a ya U r u s i , Ujerumani na Ufaransa kukataa kuivamia nchi hiyo kijeshi kumuondoa Saddam Hussein. Bw. Lavrov alisema Wizara ya Mambio ya Nje ya Urusi imeshafanya mazungumzo na John Kerry, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Yule wa Uingereza, na kwamba mazungumzo yao yalionyesha kuwepo dalili za Waasi kufanya mashambulizi ya kuitia hatiani serikali ya Assad. Katika hatua nyingine, Mkuu wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, Hans Blix, amesema kitendo cha kutaka kuishambulia Syria kwa kutegemea

silaha za maangamizi ya halaiki ni kurejea makosa ya huko nyuma ya viongozi wa Washington. H a n s B l i x amewatahadharisha viongozi wa Marekani kuhusu nia yao ya kutaka kuishambulia kijeshi Syria, akisema kuwa hawapaswi kuwa na haraka katika suala hilo. Mwaka 2003 mkaguzi hyo alitahadharisha kuwa madai yaliyokuwa yakitolewa na Marekani kuhusu silaha za kemikali huko Iraq si ya sahihi baada ya timu yake iliyokuwa umepewa majukumu ya kufanya u c h u n g u z i j u u ya madai ya Marekani na washirika wake kwamba serikali ya Saddam Hussein inamiliki silaha za maangamizi.

Bw. Blix amesema kwamba Marekani na marafiki zake wanapaswa kwanza kutoa fursa kwa wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wao k u h u s u m a d a i ya kutumiwa silaha za kemikali huko Syria, kabla ya kuchukua hatua yoyote ile. Serikali ya Syria imewaruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kulitembelea na kulifanyia uchunguzi eneo la Ghouta al S h a r q i ya , a m b a l o nchi za Magharibi zinadai kuwa silaha za kemikali zimetumiwa. Mkuu huyo wa zamani wa wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Mashariki ya Kati, amesisitiza kuwa Rais Barack Obama wa Marekani hapaswi kuchukua hatua dhidi ya Syria bila ya suala hilo kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. (irib.ir)

TANGAZO

UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO UNAPENDA KUWAARIFU WADAU WAKE WOTE KUWA BWANA. JUMA SAKATAI SIO MFANYAKAZI WA CHUO TENA TANGU TAREHE 02/09/2013. HIVYO BASI CHUO HAKITAHUSIKA NA SHUGHULI AU MAWASILIANO YOYOTE YATAKAYOFANYWA NAYE AU KUPITIA KWAKE. AFISA UHUSIANO CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO 05/09/2013

Tuseme ukweli kuhusu mgogoro wa Misri


Na Madole Rashidi KATIKA kipindi cha kama wiki mbili sasa yameandikwa na kusemwa mengi juu ya kadhia inayoendelea nchini Misri. Haya yamekuwa yakiandikwa kutoka katika mirengo tofauti tofauti kutegemea dhamira ya mwandishi au chombo husika cha habari. Naandika makala haya huku msingi wake mkuu ukiwa ni kutoka katika makala za takribani wiki mbili zilizopita katika matoleo ya gazeti la Raia Mwema, toleo namba 312 la Agosti 2127, 2013 yenye kichwa cha makala Mabavu ya kijeshi hayawezi kutuletea kheri iliyoandikwa na mwandishi mashuhuri, Ahmed Rajab. Makala nyingine ni ile katika toleo namba 313 la Agosti 28-September 3, 2013 ya gazeti hilo hilo iliyoandikwa na Sheikh Abdallah Bawaziri yenye kichwa cha makala Amani itarejea Misri kwa nguvu ya umma?. Katika makala zote mbili, hakuna pahala ambapo waandishi wetu wamejadili kwa kina chanzo cha mgogoro wa Misri na kama kuna la kujifunza kama taifa. Kwa hakika ninachokiona ni maandishi yenye kueleza historia tu ya Misri tena sana kuanza kwa uongozi wa Gamal Abdel-Nasser (na kumbe wangeweza kwenda nyuma zaidi na pengine hii ingetusaidia kujua kwanini Misri leo iko pale). Kimsingi nakubaliana na waandishi wetu, Ahmed Rajab na Sheikh Bawaziri katika makala zao kwamba Misri kihistoria ni nchi ya karne nyingi sana zilizopita. Imeshuhudia harakati nyingi sana za kisiasa na hata zile ka kidini na kwa maana hii imetajwa hata katika vitabu vya dini ya Kikristo ona ya Kiislamu. K a t i k a h i s t o r i a ya harakati za kisia nchini Misri mengi yameandikwa sina haja ya kuyarudia na kwa hili nampongeza sana mwandishi Ahmed Rajab. Kwa namna anavyoandika historia ile huweza kumsisimua m s o m a j i ye y o t e y u l e Historia inatuambia kuwa kitabia Qutb alikuwa ni mwenye kupenda sana kusoma hata wakati tu ana umri wa miaka 12 tayri alikuwa anamiliki m a k t a b a ya k e n d o g o yenye vitabu vipatavyo 25. Hivyo alivinunua kwa kudunduliza pesa kidogo k i d o g o k wa m u u z a j i aliyejulikana kwa jina la Amsaaliah. Katika miaka ya 1950, Qutb alirudi Misri akitokea huko Marekani alikokwenda kujifunza masuala ya mitaala ya elimu. Ni katika wakati huo ambapo (akiwa Marekani) ambapo mtazamo wake juu ya mfumo wa maisha unaomwongoza binadamu ulibadilika. Alipowasili Misri na baada ya kustaafu shughuli za umma, ndipo alipojiunga na chama cha Udugu wa Kiislamu mwaka 1951 na kushika nyadhifa za juu kabisa katika chama hicho. Lengo kuu likiwa ni kufanya mapinduzi na kuiongoza Misri kutoka katika dimbwi la Jahilliyah (jamii isiyo maadili, isiyo na mfumo mzuri wa maisha). Mgongano kati ya Qutb na Nasser ni wa kiitikadi. Wawili hao walikuwa wakishirikiana kwa karibu mno, kwani Muslim Brotherhood waliamini katika mapinduzi ya kuungoa utawala wa kifalme amboa ulikuwa ndio kibaraka wa ubepari nchini humo. Na matumaini mapya yakajengeka kwa viongozi wa udugu wa kiislamu na wafuasi wao kwamba sasa ni fursa ya kuijenga Misri mpya itakayoongozwa na sheria za Kiislamu. Na miaka ya 1952, vugu vugu la maofisa huru wa jeshi (free officers movement ) lililokuwa likongozwa na Nasser lilifanya mapinduzi na kushika hatamu za uongozi. Nasser aliyavunja matumaini ya Udugu wa Kiislamu kwa kuzidi kuipeleka Misri katika dimbwi la Jahilliya. Nasser aliutumuia urafiki wao kwa manufaa yake na ya kikundi chake cha maofisa huru na kwa maana hii aliunda kundi lingine la siri lililoitwa Tahreer (lenye maana ya uhuru) ili lifanye kazi ya Inaendelea Uk, 10

Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

WAANDAMANAJI nchini Misri.

mzalendo na au mpenzi wa historia na kumfunza vya kutosha. Makala haya yanalenga kuutazama mgogoro wa Misri katika nyanja nyingine ambayo kwa namna moja ama nyingine, a m b a y o k wa s a b a b u wanazozijua waandishi wetu haijajadiliwa vya kutosha Nini chanzo cha mgogoro wa Misri? Binafsi nautazama mgogoro wa Misri katika nyanja au mrengo mwingine kwamba ni mgogoro unaotokana na kusigana kwa mifumo miwili ambayo yote inalenga kushinda kundi kubwa katika jamii. Hali hii imedumu kwa muda mrefu tu, na sasa ni wakati ambao imeshindikana kuficha maradhi haya ya kuoneana kijicho baina ya mifumo hiyo miwili. Mifumo hii ni ipi? Kwanza ni mfumo wa Uislam chini ya mwamvuli wa Ikhwani Al Muslmyin (Udugu wa Kiislam). Msingi mkuu wa mfumo huu ni kuongoza Misri na dunia nzima kwa kufuata sheria za Allah (s.w). Juhudi hizi za udugu wa Kiislamu kushinda sehemu kubwa ya jamii ya Wamisri si za jana wala za juzi, hizi ni juhudi za muda mrefu pengine nyuma kabisa ya mwaka wa 1928 ambapo ndio chama cha udugu wa Kiislamu kiliasisiwa na mwasisi wake Hassan Al Bana. Mfumo huu umeasisiwa katika kitabu cha dini ya

Kiislam na waaminio kwao huuona kama ndio mfumo s a h i h i wa k u o n g o z a maisha ya mwandamu duniani hapa. Watafanya kila wawezalo kuhakisha hilo. Lakini kwa upande mwingine mfumo wa pili ni huu wa Ubepari chini ya mwamvuli wa demokrasia iliyojengwa katika misingi ya haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria uwazi na uwajikaji nakadhalika. Na hata hivyo sina haja ya kuandika mengi (kwani mengi yameshaandikwa) kuhusu mfumo huu wa demokrasia ambao kwa kiasi kikubwa umeshindwa katika maeneo mengi kusimamia hizo haki za binadamu. Makala haya yanalenga kuutazama mgogoro wa Misri sana kupitia mfumo wa kwanza, ambao kwa namna fulani haujajadiliwa kwa mapana na marefu. Kwa hiyo lengo la makala haya ni kuujadili mgogoro huo katika mrengo mwingine. Anaandika Sheikh Bawaziri katika makala yake kuwa Misri baada ya mapinduzi ya 1952 na Gamal Abdel Nasser kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo kulikuwa na upinzani mkubwa baina ya serikali ya N a s s e r n a c h a m a cha Udugu wa Kiislam kilichokuwa kikiongozwa na Sayyid Qutb kwa wakati huo, wawili hawa;Rais Nasser na Qutb. Walikuwa

wakitofautiana katika mambo mengi... Je haya mambo mengi yawafanyayo watofautiane n i ye p i ? H a p a n d i p o ninapojenga dhana ya kwamba mgogoro wa Misri ni mgogoro kati ya mifumo miwili inayosigana kama nilivyoeleza hapo juu, yaani mfumo wa Kiislamu kuuondosha mfumo wa ubepari wa Magharibi na vivyo hivyo mfumo wa ubepari wa Magharibi kuuondosha mfumo wa Kiislamu, yote hayo kupitia mawakala wao wa Demokrasia na wa Udugu wa Kiislamu. K u p a t a u n d a n i wa msingi wa dhana hii hatuna budi kuingia ndani kidogo kuona, je, wawili hao ni akina nani? Walikutana vipi? Na walichotofautiana ni kipi? Hapa hatuna budi kutazama historia zao kwa ufupi. Mwaka 1906 oktoba 9 katika kijiji cha Musha alizaliwa kijana aliyejulikana kwa jina la Sayyid katika familia ya mwanaharakati wa kisiasa, Qutb. Alipata elimu yake ya mrengo wa Kimagharibi katika miaka ya 1929 and 1933. Vile vile amewahi kuwa mtumishi katika Wizara ya Elimu ya nchini Misri katika miaka ya 1939 na historia inatuambia kwamba miaka ya 1948 hadi 1950 aliishi nchini Marekani akisomea mfumo wa elimu wa nchi hiyo katika chuo cha Colorado (kwa sasa Chuo Kikuu cha Colorado Kaskazini).

Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Mauaji ya Misri, ni wakati wa kusimamia Uislamu!


Said Rajab

JESHI la Misri limeendelea kufanya maangamizi ya wananchi wasio na hatia, katika jaribio lake la kuwaondoa mitaani waandamanaji wanaopinga kung'olewa madarakani kijeshi kwa Rais aliyechaguliwa kidemkorasia, bwana Mohammed Morsi. Inasemekana zaidi ya watu 2000 wameuawa na vikosi vya usalama katika kipindi cha wiki moja tu, ambapo kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, wengi wao ni wanawake, watoto, vijana na wazee ambao walikutwa na m a j e r a h a ya r i s a s i vifuani na vichwani. Vikosi vya usalama nchini Misri vimetenda uhalifu mkubwa ambao haujawahi kufanywa hata na maadui wakubwa wa Waislamu. Wa m e c h o m a m o t o hospitali ya dharura katika eneo la Rab'a Al Adawiyah wakati miili ya watu waliokufa na wale waliojeruhiwa ikiwemo ndani. Nadhani lengo lao lilikuwa ni kufuta ushahidi wa uhalifu walioufanya. Hali hii inaonyesha kiwango cha unyama na ukatili kinachoweza kufanywa na viongozi wa mapinduzi ya Misri dhidi ya Siasa za Kiislamu nchini humo. H a wa n a h o f u h a t a kidogo kwa uhai wa wananchi wao wenyewe, wala heshima kwa wale waliotangulia mbele ya haki! Lakini, jambo la wazi kabisa, ni ule utayari wa jeshi la Misri kuendeleza umwagaji damu na maangamzi ya watu wanaopigania haki yao iliyoporwa mchana kweupee, hatua ambayo inatukumbusha m a a n g a m i z i yanayofanywa na

WAANDAMANAJI nchini Misri M a ya h u d i d h i d i ya waliobeba bendera ya akhira kwa uovu wao. Waislamu wa Palestina. Uislamu. Huu ni utawala Wamemwaga damu Kufuatia mauaji hayo mpya wa kijeshi. Na i s i y o n a h a t i a y a ya kihalifu, Rais wa hawa ni viongozi wa Waislamu, wanaendesha Serikali ya mpito ya Misri m a p i n d u z i a m b a o vita dhidi ya dini ya akatangaza hali ya hatari wanaendeleza unyama. Mwenyezi Mungu na kwa kipindi cha mwezi Wako tayari kumwaga wanatumikia maslahi m m o j a . Wa n a d h a n i damu isiyo na hatia ili ya Marekani badala ya ndani ya kipindi hicho, k u f a n ya m a p i n d u z i wananchi wa Misri: wataweza kuwaua y a o y a o n e k a n e "Na mwenye na kuwapondaponda yamefanikiwa. kumuua Muislamu kwa waandamanaji ili W a n a k u w a kukusudia, basi malipo w a s a l i m u a m r i n a wakali kama simba ya k e n i J a h a n n a m , kukubali utawala mpya wanapokabiliana kijeshi humo atakaa milele; wa kidhalimu. na raia wao wenyewe, na Mwenyezi Mungu U t a w a l a a m b a o lakini wanyonge kama a m e m g h a d h i b i k i a Jenerali Al Sisi, akibebwa vifaranga kwa maadui n a a m e m l a a n i n a na Marekani, anataka wao halisi, ambao ni amemuandalia adhabu kuuweka nchini Misri Mayahudi na mataifa kubwa" Qur (4:93). baada ya kumpindua ya Magharibi. Wanakula Na Mtume wa Mohammed Morsi, njama pamoja nao Mwenyezi Mungu ambaye amechaguliwa kuhujumu taifa lao amesema: "Kumuua na wananchi wa nchi wenyewe! Wamekuwa M u i s l a m u m m o j a hiyo. wa l i n z i h o d a r i wa ni vibaya zaidi kwa M a p i n d u z i y a maslahi ya maadui hata Mwenyezi Mungu kama Januari 25 mwaka 2012, kwa damu ya ndugu kuangamiza Dunia yote" yaliyomng'oa Hosni zao! (Tirmidhi). Mubarak, ambayo Wa n a p i g a v i t a Kauli mbiu ya viongozi yalidumu kwa siku Uislamu kwa jina la wa mapinduzi nchini 18, yalisababisha vifo "kupambana na ugaidi", Misri ni "kupambana vya takriban watu 365, wakati Mayahudi walio na ugaidi", ambapo wakati kwa siku moja jirani nao, ambao ndiyo kuwapiga vita 'Ikhwan tu Serikali kibaraka ya maadui wao wakubwa, Misri imeua zaidi ya wa k i wa s a l a m a n a Muslimin' ni kichaka mara mbili ya idadi hii! wenye uhakika. Vipi chao tu cha kupambana Watu 638 wameuawa h a w a w a h a l i f u n a n a Ui s l a m u . L a ki ni ndani ya masaa 24 tu! wasaliti, waliomwaga wanasahau kwamba I n a o n e k a n a h a y a damu ya Wamisri wasio Uislamu nchini Misri ni mauaji ya kisasi na hatia, wanaweza una mizizi mirefu, na y a n a y o t u f a n y a kuleta ushindi kwa haiwezekani kung'oa tukumbuke utawala wananchi wa Misri? mizizi ya Uislamu nchini wa Hosni Mubarak, Hawa ni wahalifu na humo. Misri ni nchi ya ambaye alikuwa na wauaji! Na Mwenyezi Waislamu. Insha'Allah, iko siku chuki kubwa dhidi ya Mungu atawaadhibu m f u m o wa k i k a f i r i raia wake, hususan wale hapa duniani na kesho

unaotawala Misri, ambao unasimamiwa na Marekani na washirika wake wa Kimagharibi utakoma, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mfumo wa Kiislamu utasimama! Mfumo ambao siyo demokrasia, siyo usekula na wala haushirikiani na Ukafiri kwa namna yoyote ile. Jambo la msingi ni kwa Waislamu wa Misri k u t a m b u a k wa m b a kuzingatia maagizo na taratibu za Mwenyezi Mungu, ndiyo njia pekee ya kujipatia ushindi na heshima. Misri inahitaji Uislamu katika utawala na siyo tu Waislamu kuongoza mfumo wa kisekula. Suala hapa siyo nani anaingia madarakani, bali ni mfumo gani unatawala nchi hii ya Waislamu. Kufuatia kupinduliwa kwa Rais Mohammed Morsi na darsa iliyopatikana, Waislamu wa Misri wana kazi ngumu ya kuung'oa utawala wa kidhalimu kutoka kwenye mizizi na matawi ya k e . Wa n a h i t a j i k a kupambana na kuleta mapinduzi kamili ya Kiislamu. Hawana sababu tena ya kujificha kwenye vichaka vya demokrasia wala usekula. Wameshaona madhara yake, na Waislamu hawaumwi na nyoka mara mbili kwenye shimo moja: "Mwenyezi Mungu Amewaahidi wale walioamini miongoni m we n u n a k u f a n ya vitendo vizuri, kuwa Atawafanya makhalifa katika ardhi kama Alivyowafanya makhalifa wale wa l i o k u we p o k a b l a yao, na kwa yakini Atawasimamishia dini yao Aliyowapendelea, n a At a wa b a d i l i s h i a amani baada ya hofu yao. Wawe wananiabudu, hawanishirikishi na chochote. Na watakaokufuru baada ya hayo; basi hao ndiyo wavunjao amri zetu" Qur(24:55).

9
Na Abdulkarim S. Msengakamba

Habari

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013 Amir wa jumuiya wilaya ya Temeke Ust. Saad Ahmed Salim aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuwapatia chumba kitakachotumika kuhifadhia vifaa vya kazi za kila siku za Jumuiya hiyo sambamba na kuhifadhi dawa, a m b a z o h u wa p a t i a wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo. Kufuatia ombi hilo, Naibu Meya Juma Mkenga, aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kuangalia uwezekano wa kutenga chumba kimoja kwa ajili ya shughuli za kihuduma za Jumuiya hiyo. Amir huyo alisema jumuiya ya Waislamu kitengo cha afya na ustawi wa jamii JAI, ni Taasisi isiyo ya serikali ambayo ina zaidi ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwake. Taasisi hiyo inafanya kazi zake bega kwa bega na watumishi wa serikali katika kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii katika maeneo ya Hospitalini na majumbani. Alielezea kuwa Jumuiya hiyo inatambua hali halisi ya maisha ya Mtanzania na kupanda gharama za m a t i b a b u , d a wa n a vifaa mbalimbali vya tiba, hivyo kwa dhati kabisa kwa kutumia kauli mbiu zake zaHuruma-Upendo, imekusudia kutoa huduma zote stahiki kwa wagonjwa wa jinsia zote, madhehebu yote waliopo mawodini na majumbani. Amir Salim, aliongeza kuwa jumuiya yao hutoa huduma zake kila siku ambazo ni kuwaombea dua na kuwafariji wagonjwa, kuwanunulia dawa zinazokosekana mahospitalini, kuwafanyia usafi katika hali zote stahiki, k u wa p a t i a c h a k u l a kwa nyakati zote, h u s u s a n i k wa wa l e ambao hawama ndugu, jamaa, ambao inatubidi kuwahudumia kwa kwa hali na mali. Katika zoezi hilo, jumla ya unit 300 za damu zilikusanywa.

AN-NUUR

WAISLAMU kupitia Jumuiya ya Akhlaaqul Islaam (JAI), kitengo cha Afya na Ustawi wa Jamii mwishoni mwa w i k i wa m e c h a n g i a damu kwa wagonjwa, katika zoezi lililofanyika katika hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam. Tu k i o h i l o lilihudhuriwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Juma Mkenga, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Sofia Mjemwa. Binafsi nimefarijika sana kuona muamko huu wa Waislamu kwa jamii, nimefurahishwa na akina mama ambao wamejitokeza katika zoezi hili, wanastahili kuungwa mkono na jamii kwa ujumla kwa kitendo hiki, ni mfano mzuri unaostahiki kuigwa na akina mama wengine popote katika jamii yetu. Alisema Naibu Meya huyo. Aidha aliikumbusha jamii kwa ujumla umuhimu wa kuchangia damu kwa hiyari, kwani kitendo hicho ni cha kuokoa maisha ya wagonjwa wenye kuhitajia huduma hiyo ya damu. N a ye D r . S t a n l e y Lwiza, wa hospitali y a Te m e k e a k i t o a shukurani zake kwa Waislamu hao alisema, hospitali yake wa inathamini mchango na misaada pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na wanajumuiya wa JAI. Kwa upande wake, Meneja maabara wa hospitali hiyo Grace Maliva, alisema muitikio ulionyeshwa na Waislamu hao ni mkubwa na kushauri elimu zaidi ya kuchangia damu inahitajika kutolewa katika jamii ili kuwajengea moyo zaidi wa kujitolea. Alisema takwimu zinaonesha kuwa wanaohitaji damu zaidi ni akina mama, ambao kutokana na uhaba wa damu hupoteza maisha kwa kukosa huduma

Wachangia damu hospitali Temeke

ZOEZI la uchangiaji damu likiendelea hospitali ya Temeke.

hiyo. Alisema takribani akina mama zaidi ya wanne hupoteza maisha kwa siku kwa kukosa damu. Wa k a t i m w i n g i n e hulazimika kukamata watu kwa ajili ya kutoa damu bila ya kujali

mpango wa damu salama, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu, lakini hulazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama hususani wa pale wanapojifungua ambapo hupoteza damu kwa wingi sana.

Hata hivyo aliwaasa kina mama kuhamasika kujitokeza zaidi katika mazoezi ya kuchangia d a m u k wa n i a k i n a mama wenzao ndio wahitaji wakubwa wa huduma hiyo. Katika risala ya Jumuia hiyo iliyosomwa

10
Hodi hodi mhariri, si wa gazeti la giza, Bali wa letu AN-NUUR, lenye angavu mwangaza, Kuna jambo nafikiri, naomba kulidokeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Uvivu niwape siri, tunaouendekeza, Wa kushindwa kufikiri, hali ya kuwa twaweza, Nd'o unotuathiri, pamwe na kutudumaza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Wengi likizo nadhari, zetu tumeziwekeza, Wachache wanotughuri, kadiri wanavyoweza, Badala wanafikiri, yetu nasi twafatiza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kheri wakiita shari, nasi nyuma twafatiza, Shari wakiwamba kheri, kadhalika twachagiza, Kwa mgando tafakuri, vyovyote watugeuza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Waizushapo habari, papo hapo twaimeza, Mia kwa mia twakiri, pasi hata kuchunguza, Kadhalika kufikiri, twameza na kueneza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Twajiona maayari, kwa puya kuhanikiza, Sote yatatuathiri, madharaye nawajuza, Kwazo ikifuka nari, sote yatuteketeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Tuchukue tahadhari, kwa kutokuhanikiza, Tumezeshwazo habari, pasi kwanza kuchunguza, Kwanini zetu fikari, likizo twaziwekeza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kwa uvivu kukhitari, wa kutokujizoeza, Kila mtu kufikiri, kadiri anavyoweza, Taifa la tafakuri, muhali kutengeneza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Ni yako sasa hiari, kujali au kubeza, Lengo langu kushauri, na si kukung'ang'aniza, Ila ni kubwa hatari, endapo utapuuza, Uvivu wa kufikiri, utajatuangamiza. Kaditamati akhiri, nimefika kueleza, Akali ya kufikiri, leo yanatosheleza, Kalamu ya tafakuri, haina la nyoongeza, Utajatuangamiza, uvivu wa kufikiri. ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Mashairi/Makala

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

UVIVU WA KUFIKIRI !

Tuseme ukweli kuhusu mgogoro wa Misri


InatokaUk. 7

IMERUDI ULINGONI !!!


1.Imerudi ulingoni, idhaa yetu nchini, Imerudi ulingoni, kwa Bara na Visiwani, Imerudi ulingoni, nyote ninakujuzeni, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 2.Imerudi ulingoni, idhaa ya waumini, Imerudi ulingoni, kipenzi cha waumini, Imerudi ulingoni, si nyingine ni IMANI, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 3.Imerudi ulingoni, natoa kwenu ilani, Imerudi ulingoni, wiki jana si zamani, Imerudi ulingoni, mijini na vijijini, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 4.Imerudi ulingoni, kwa habari za yakini, Imerudi ulingoni, zisizo na walakini, Imerudi ulingoni, zimridhizo Manani, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 5.Imerudi ulingoni, kwa elimu ya yakini, Imerudi ulingoni, iso shaka maishani, Imerudi ulingoni, yenye jazaa ufuni, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 6.Imerudi ulingoni, kwa za kheri burudani, Imerudi ulingoni, Imerudi ulingoni, si za rajimi shetani, Imerudi ulingoni, zidakhilizo nirani, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. 7.Imerudi ulingoni, idhaa yetu IMANI, Imerudi ulingoni, lengo ni kukujuzeni, Imerudi ulingoni, kalamu naweka chini, Isharejea hewani, REDIO yetu IMANI. REDIO yetu IMANI, isharejea hewani. ABUU NYAMKOMOGI. MWANZA.

kukichafua chama cha Udugu wa Kiislamu ili atakaposhika madaraka brotherhood kilichokuwa maarufu sana miongoni mwa Wamisri kiwe na cha kusema. Lakini hakuna siri itakayodumu milele. Na ikafika wakati ambao Qutb na Muslim Brotherhood ya k e wa k a t a m b u a walikosea kushirikiana na Nasser na ndipo ulipokuwa mwisho wa uhusiano wao. Nasser akafanya juhudi nyingi tu kumshawishi kwa nafasi kadhaa serikalini ili Qutb arudi ila ikashindikana, Nasser amenukuliwa akisema; We will give you whatever position you want in the government, whether it's the Ministry of Education, Ministry of Arts, or any position you want. Na kwa hiyo mwaka 1954 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa wanachama wa Udugu wa Kiislam. N i wa k a t i a m b a o Qutb alikamatwa na kufungwa jela kwa tuhuma za kupanga mauaji dhidi ya Nasser, kamata kamata hiyo iliwaandama mpaka wafuasi wengine kama akina Zainabu Ghazal waliokuwa kunyume na serikali yake. Kwa maana hii, tofauti kati ya Nasser na Qutb ni ya kimtizamo, historia inatuambia kwamba Qutb anaamini kuwa jamii yeyote ile ambayo uongozi wake haufuati sheria ya Mwenyezi Mungu haiwezi kuwa ya K i i s l a m u h a t a kama wao wanajiita ni Waislam, na wanasali, wanfunga na wanahiji. Qutb anasema; Thus, a society whose legislation does not rest on divine law (shari'at allah) is not Muslim, h o we ve r a r d e n t l y its individuals may proclaim themselves Muslim, even if they pray, fast, and make the pilgrimage. Na mwaka 1966 ikawa ndio mwisho Sayyid Qutb ambaye a l i h u k u m i wa k i f o

WAANDAMANAJI nchini Misri. kwa kunyongwa na aliyekuwa mshirika wake mkuu Gamal Abdel Nasser. Suala la msingi hapa ni kuwa Udugu wa Kiislamu wanaitaka Msiri itakayoongozwa na sheria za Kiislamu wakati hawa wengine wanataka Misri ya kisekula, Misri ya kidemokrasia ya Magharibi. Hii ndio tofauti kubwa baina ya mifumo hiyo mawili. Kwa muda wa nusu karne sasa kundi l e n y e m r e n g o wa Udugu wa Kiislamu limekandamizwa mno. Juhudi nyingi zimefanyika kuzifuta fikra za Udugu wa Kiislamu lakini imeshidikana, na pengine ni kwa sababu waliwekeza mawazo yao katika watu, waliwekeza katika mafunzo na hivyo yataishi milele. Hapa nitapishana kidogo mtazamo na mwandishi Sheikh Bawaziri ambae yeye anaandika kuwa Misri imegawanyika katika makundi matatu makuu. Kundi linalomuunga mkono Morsi (raisi a l i ye p i n d u l i wa n a aliyechaguliwa kwa uchaguzi huru), kundi linalompinga Morsi na kundi pekee la Jeshi. Nayaona Makundi mawili tu pale Misri, kundi linalounga mkono sera za Ikhwani Al Muslimyn na kundi l i n a l o u n ga m ko n o ubeberu wa Magharibi kwa kujivika kilemba cha demokrasia, nalo hili linaundwa na Jeshi na wananchi huku kila mmoja akifanya nafasi yake. Na ndio maana nakubaliana na Sheikh Bawaziri katika makala yake ya tarehe 30 Agosti katika gazeti la kisiwa yenye kichwa cha makala ni nani aliyeweka mipaka hii katika Demokrasia?, Bawazir anaandika; Maandamano yaliyofanywa na wapinzani wa Morsi yalionekana ni halali, hakuna bunduki iliyoelekezwa kwao na wala hakuna yeyote aliyedai kwamba ni magaidi. Lakini maandamano ya wafuasi wa Morsi waliotaka raisi wao arejeshwe madarakani, hayo hayakuonekana kuwa ni nguvu ya umma. Bali waandamanaji hao walionekana kuwa ni magaidi wanaoipinga serikali iliyowekwa madarakani na mtu mmoja tu kwa nguvu ya jeshi. Kwa mtizamo huu kinachoendelea Misri ni msuguano baina ya mifumo miwili ya Uislam na Ubeberu. Lakini vile vile nakubaliana na Sheikh Bawazir katika makala yake hayo kwamba hofu ya mfumo wa ubeberu ni Uislam wa aina yoyote ile, Uislam siasa kali, siasa poa siasa zozote zile! Na hatima yake ni kuangusha dola lolote lenye mrengo huo. Kimsingi serikali ya Morsi isingeweza k u f a n ya l o l o t e l a maana ndani ya kipindi ilichokuwa madarakani, au ndani ya kipindi ambacho ingekuwa madarakani, iwe kuindeleza Misri kiuchumi au kujenga sera zake za Udugu wa Kiislamu. Ingeliichukua Misri miaka mingi k u f a n i k i wa k a t i k a moja kati ya hayo. Kwanini? Kiuchumi, Misri bado ni tegemezi na imekuwa ikipokea misaada mingi tu kutoka serikali za magharibi. Ambayo nayo ilifutwa bada ya M o r s i k u i n g i a madarakani. Lakini pia ni ngumu Misri iliyojaa rushwa na dhulma kupiga hatua ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, si kazi ndogo kuusafisha mfumo uliotamalaki katika kila kona ya nchi. Na hata kiitikadi, ingelichukua pia muda mrefu wa kwa Morsi kuzijenga sera zake za udugu wa Kiislamu. Kwani hali ilivyo sasa ni kama nusu kwa nusu, hii ingeifanya s e r i k a l i ya M o r s i kuwekeza nguvu ya ziada katika kuliendea lengo hilo (kama kweli ndio lengo la Udugu wa Kiislamu). Sasa hofu yote hii ni ya nini? Nguvu yote hii ni ya nini? Wanaoumia ni wananchi wasio na hatia yoyote ile. Ni wakati kwa dola za Magharibi kuwasikiliza wamisri wanataka nini kupitia hiyo hiyo demokrasia. (madoler@hotmail. com-0717 003 530).

11

SHAWWAL 1434, IJUMAA

SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

Sheikh Simba alia kupuuzwa Makadhi wake


Na Shaban Rajab

Serikali, Tume ya Katiba zalaumiwa Aliyosema Sheikh Mohamed Issa yametimia


jijini Dar es Salaam. Aliilaumu serikali kwa kutowatambua Makadhi hao na vilevile kupuuza m a o n i ya Wa i s l a m u ya kutaka Mahakama ya Kadhi na wadhifa wa Kadhi kutambuliwa kikatiba ndani ya rasmu ya Katiba. Alisema licha ya jamii ya Waislamu na taasisi zao kuwasilisha maoni yao kwa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya, ya kutaka kuwepo mahakama ya Kadhi inayotambulika kikatiba, bado Tume hiyo imepuuza maoni yao kiasi cha kukosekana katika rasimu hiyo ya katiba mpya. Hata hivyo lisisitiza kwamba bado atajitahidi kuwasilisha maoni zaidi juu ya suala hilo. Itakumbukwa kwamba Julai mwaka jana akiwa Dodoma, Mufti Simba huyo huyo katika hali ambayo haikuratajiwa na Waislamu wengi nchini, ghafla alitangaza kumteua Kadhi Mkuu na wasaidizi wake wawili na baada ya hapo, aliwateua Makadhi wengine 14 wa mikoa huku akiahidi kuteuwa Makadhi wengine wa mikoa iliyosalia na wa Wilaya. Katika uteuzi huo, Sheikh Abdallah Mnyaki alitangazwa kuwa Kadhi Mkuu wa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Masheikh Abubakar Zuberi na Alli Muhidini, walitangazwa kuwa ndio wasaidizi wa Kadhi Mkuu. Uteuzi huo ulifanyika baada ya kumalizika kwa kikao cha siku mbili kilichowakutanisha Masheikh wa Bakwata wa Mikoa na Wilaya kutoka Tanzania Bara. Baada ya kuchaguliwa, Sheikh Mnyaki, Mufti Simba aliwataka Waislamu kuwa na umoja pamoja na kushiriki zoezi la Sensa na kuwataka wa p u u z e k a u l i a m b a z o zimekuwa zikitolewa na taasisi za Kiislamu na badala yake aliwataka Masheikh kumpa ushirikiano Kadhi Mkuu ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu. N i j a m b o l i l i l o wa z i kwamba, wakati Mufti Simba na Bakwata kwa ujumla wanachukua hatua ya kuasi Kamati iliyoridhiwa na Waislamu, walitambua kuwa Makadhi hao wasingekuwa na nguvu zozote za kisheria zaidi ya kubaki na majina yao tu huku wakiishia kupuuzwa sio na serikali tu, bali hata na Waislamu wenyewe. Tu j i k u m b u s h e t u kwamba kabla ya Mufti Simba kuchukua hatua

QURAN surat Munafiqun aya ya kwanza inasema, Wa n a p o k u j i a wa n a f i k i husema: Tunashuhudia ya kuwa, kwa yakini wewe ni Mtume wa mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wake na Mwenyezi Mungu anashuhudia ya k u wa h a k i k a wa n a f i k i ni waongo, (wanasema wasiyoyasadiki). Aya hii aliinukuu Katibu wa Jumuia ya Wanazuoni wa Kiislamu nchini (Hayat) Sheikh Mohammed Issa, wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya Mufti wa Bakwata, Sheikh Issa Shaaban Simba, kutangaza kuteua Kadhi na wasaidizi wake Julai mwaka jana mjini Dodoma. Baada ya kunukuu aya hiyo, Sheikh Issa alifafanua kwamba, awali wakati Mufti Simba anawateua wajumbe wa Kiislamu kuunda Kamati ya kushughulikia mchakato wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini, aliwaeleza baadhi ya wajumbe hao kwamba anamfahamu vizuri Sheikh Simba, kwamba si kiongozi wa kuaminika katika kufanya maamuzi kwani anaweza kubadilika wakati wowote. Alisema anamfahamu vizuri kwa sifa hiyo tangu alipokuwa Sheikh wa Bakwata mkoa wa Shinyanga. Sheikh Mohamed Issa alisema kutokana na tabia hiyo ya Mufti, aliwahakikishia baadhi ya wajumbe wa Kamati ile kuwa hawatafika pale walipokusudia kwa kuwa Mufti atawageuka. Maneno hayo ya Sheikh Mohammed Issa, aliyatoa b a a d a ya M u f t i S i m b a kutangaza kuteua Makadhi mjini Dodoma Julai mwaka jana, wakati Kamati ya Kushughulikia Kurejeshwa mahakama ya Kadhi nchini ikiwa haina taarifa jambo lililowashangaza Waislamu wengi. I k i wa n d i o u m e t i m i a mwaka mmoja tangu Mufti Simba, alipoamua kuipuuza Kamati ya pamoja ya Waislamu iliyokuwa imepewa jukumu la kushughulikia mchakato wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini na kuamua kuteua Makadhi wake, sasa anaililia serikali kwa kutowatambua kisheria Makadhi aliowateua. Mufti Simba alitoa malalamiko hayo wakati walipozungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita

h i y o ya h a r a k a , a wa l i iliundwa Kamati ya pamoja iliyojumuisha viongozi mbalimbali wa taasisi za Kiislamu nchini na wajumbe kutoka serikalini chini ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwa ajili ya kushughulikia mchakato mzima wa kuanzishwa Mahakama ya Kadhi nchini. Wajumbe wa Kiislamu walitaka mahakama hiyo iendeshwe kwa gharama za serikali kwa kuwa Waislamu nao ni walipa kodi na sehemu ya jamii ya Tanzania inayohitaji huduma ya kijamii ya serikali. Aidha walitaka mahakama hiyo ipewe nguvu kisheria kwa kutambuliwa na katiba ya nchi ili isije kupuuzwa na kudharauliwa kwa kukosa nguvu za kisheria. Wajumbe wa Kiislamu walitambua kuwa iwapo hilo lisingefanyika, basi mahakama hiyo isingeheshimiwa na hukumu za mashauri yake yasingeheshimiwa pia kwakuwa yasingetambuliwa kisheria. Hata hivyo Maaskofu walikuja juu na kusisitiza kwamba hawawezi kukubali serikali kutumia fedha za watu wa imani zote hudumia Waislamu pekee na kuongeza, mahakama ya kadhi kutambuliwa na katiba ni sawa na kuisilimisha n c h i h i v y o h a wa k u b a l i kuanzishwa mahakama hiyo. Waislamu nao walihoji kuwa, kama kanisa na serikali wanatambua hilo, iweje serikali hiyo hiyo ikasaini mkataba kati yake na Kanisa wa mwaka 1992, ambao unairuhusu serikali kutoa fungu la fedha za walipa kodi wakiwemo Waislamu, kwenda kwa makanisa kwa ajili ya kugharamia huduma zinazotolewa na kanisa. Hoja hizo na msiamo wa Maaskofu uliifanya serikali kupiga danadana suala la kuanzishwa mahakama ya Kadhi hadi leo. Itakumbukwa kwamba mwezi Juni mwaka jana, Serikali ilisema uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi itakayoshughulikia migogoro na masuala mbalimbali ya ustawi wa Waislamu nchini umefikia katika hatua nzuri. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo wakati akijibu hoja za wabunge zilizojadili kwenye hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2012/2013. A l i s e m a i t a a n z i s h wa wakati wowote baada ya maandalizi kukamilika na

MUFTI wa Bakwata, Sheikh Issa Shaaban Simba.


kwamba, utekelezaji wake uko katika hatua nzuri baada ya kamati ndogo iliyoteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, yenye wawakilishi wa Waislamu na Serikali imetoa taarifa yake ya mwanzo ya namna ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi. Waziri Pinda alibainisha wazi kwamba mambo yatakayoshughulikiwa na mahakama hiyo ni pamoja na mashauri ya ndoa na talaka, mirathi, wosia, usuluhishi wa migogoro ya Kiislamu, hiba/zawadi/ tunu, wakfu na malezi ya watoto na kwamba, Mahakama hiyo haitahusika na mashauri ya jinai. Waziri Mkuu alisema bungeni kwamba Kamati Kuu inayojumuisha viongozi wa waumini wa Dini ya Kiislamu na Serikali chini ya Uenyekiti wake, kimsingi imekubaliana kwa kauli moja uanzishwaji wa Mahakama hiyo Nchini itakayokuwa nje ya mfumo wa serikali. Aliongeza kuwa kulikuwepo na umuhimu na dhamira ya kweli ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara. Pinda alikuwa akijibu hoja za wabunge waliotaka kufahamu maendeleo ya Mahakama hiyo, wakitaka Serikali itimize ahadi yake hiyo ambayo ipo katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Wabunge hao walikuwa ni Hamad Rashid Mohammed, Rashid Ali Abdallah, Ahmed Juma Ngwali na Hussein Nassor Amar. Aidha alisema katika kikao chao cha mwisho cha pamoja kati ya Serikali na ujumbe wa wawakilishi wa Kiislamu, kilichofanyika Machi mwaka jana kwamba, walikubaliana kuwa baadhi ya wajumbe kutoka upande Waislamu na Serikali wakafanye ziara ya mafunzo katika nchi za India, Uingereza, Kenya na baadaye Zanzibar ili wakajifunze n a m n a ya k u r a t i b u n a kuendesha Mahakama za Kadhi katika nchi hizo, ambazo zina Mahakama za Kadhi kwa muda mrefu. Alisema wataalamu wa kuanzisha mahakama hiyo watakwenda nchini Kenya, India, Uingereza na Zanzibar kujifunza jinsi ya kuanzisha chombo hicho na kwamba, ziara hiyo itagharamiwa na serikali. Hata hivyo wakati hali i k i wa h i v y o , k a b l a ya kufikiwa makubaliano ya kuanzishwa mahakama hiyo, Mufti Simba na Masheikh wa Mikoa Bakwata walikutana mjini Dodoma na kutangaza uteuzi wa makadhi. Mufti Simba alifanya hivyo bila hata kuwasiliana na kamati ya wawakilishi wa Waislamu katika kujadili suala hilo na kuvuruga mchakato mzima ya k u a n z i s h wa M a h a k a m a ya Kadhi inayotambulika kikatiba na mchakato mzima ukaishia hapo. Hadi leo si Mufti Simba wala Waziri Mkuu Pinda aliyezunfgumzia kuanzishwa mahakama ya Kadhi tena.

12

AN-NUUR
MAKALA

SHAWWAL 1434, IJUMAA SEPT. 6-12, 2013

AN-NUUR

12

SHAWWAL 1434, IJUMAA

SEPT. 6-12, 2013

Na Bakari Mwakangwale
SERIKALI imetanabaishwa k u ya t a f u t i a u f u m b u z i wa k u d u m u m a d a i ya Waislamu nchini ambayo yamewasilishwa kwa nyakati tofauti ili kuepusha msuguano uliopo sasa. Hayo yamesemwa na Ustadhi Suleiman Daud, akiongea na An- nuur, a k i z u n g u m z i a h a l i ya mvutano baina ya Serikali, Masheikh na Waislamu unaondelea sasa. Ust. Daud, alisema hali iliyopo sasa inatokana n a S e r i k a l i k u s h i n d wa kuyatafutia ufumbuzi m a d a i y a Wa i s l a m u na sasa wanapoamua kuitahadaharisha wanasakamwa kwa uchochezi. Hali hii inatokana na Serikali inayojinadi kuwa ni sikivu na adilifu, lakini inapuuza kabisa kuyafanyia kazi madai ya Waislamu na kujaribu kutaka kuwaziba mdomo kwa kutumia vyombo vya dola, jambo a m b a l o n i h a t a r i k wa mustakabali wa Taifa hili. Alisema. Ust. Daud, alisema kimaumbile binaadam, a n a p o h i s i k u o n e wa n a akafikisha malalamiko yake sehemu husika ili apate ufumbuzi kisha akapuuzwa na kufikia hatua akashindwa kuona wapi apeleke madai na malalamiko yake, hufika mahali akasema, sasa basi, liwalo na liwe. Ust. Daud, aliye Amir wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Kamati ya Kuendeleza Uislamu, alisema hivi sasa madai ya Waislamu Serikali yanaonekana kuwa ni uchochezi kabla hata kuyajadili au kuyafanyia utafiti. Ust. Daud, alisema ikiwa madai ya Waislamu ni uchochezi bila shaka ( Wa i s l a m u ) w o t e watafunguliwa mashitaka. Alisema, kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii, Waislamu wana haki na wajibu wa kutendewa haki kama ambavyo Serikali inavyowatendea makundi mengine. Amir Daud, alisema Waislamu wana kumbukumbu kuwa waliunda makundi yaliyowawakilisha Wa i s l a m u k u wa s i l i s h a madai yao Serikalini moja

Serikali itende haki

Tanzania Muslim Hajj Trust Safari ya Hijja 2013 Uandikishaji unaendelea gharama za Hijja ni dola za Kimarekani $ 4200. Safari ni tarehe 5 na 7 Octoba, na Kurudi Tarehe 27 na 28 Octoba, 2013. Wahi kujiandikisha Sasa. Uandikishaji wa Hijja Zijazo 2014, 2015 kwa Kulipia kidogo kidogo, unaendelea. Simu: 0717 000 065, 0784 222 911, 0754 304 518, 0754 498 888 Au kupitia Tovuti yetu. www.hajjtrusttz.org. ya madai ya Waislamu na jinsi wanavyopuuzwa na kusababisha yote hayo mfano wa kadhia hiyo ya Wanafunzi wa Ndanda. Akahoji, ikiwa Serikali inapelekewa matatizo ya raia wake ili iyatafutie ufumbuzi, wao (Serikali) hawataki h a t a k u f a n ya m j a d a l a , wanategeme Masheikh hao wakisimama jukwaani mbele ya Waislamu watasema nini. Alisema, kupitia MoU, Serikali inatoa mabilioni ya pesa kuyapa Makanisa kwa ajili ya kuendeshea miradi yao, ilihali Serikali inajua kuna makundi mengine ya kiraia lakini imeyapuuza na kuidhinisha kinyemela kundi hilo moja kupewa pesa hizo. Waislamu, wamekuwa wakihoji siku zote suala hili, majibu yake ni kuonekana kuwa ni wachochezi, na sasa ili Masheikh wasiseme haya, Serikali inaona ufumbuzi wake ni kuwapigwa risasi. Alisema Amir Daud. Alisema, si hayo tu kuna tukio la kuuwawa Waislamu katika kadhia ya Msikiti wa Mwembechai, pamoja na Waislamu kupeleka madai yao ili iundwe Tume huru ya kuchunguza mauaji hayo, Serikali imewapuuza. Akizungumzia madai ya Waislamu Serikalini kuhusu Baraza la Mitihani la Taifa, Amir Daud, alisema Waislamu wamelalamika muda mrefu juu ya namna vijana wa Kiislamu wanavyo felishwa, lakini alidai pia walipuuzwa.

Ustadhi Suleiman Daud.


kwa moja achilia mbali madai wanayoyatoa kupitia majukwaani na makongamano. Alisema, mwaka 1998, Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, lilifikisha madai ya Waislamu Serikalini, dai la msingi lilikuwa ni kutaka kufahamu au kupata ufafanuzi kutoka Serikalini juu ya Tume ya Majeshi ya Kanisa Katoliki Nchini. Mpaka sasa Serikali haijatamka kauli yoyote juu ya suala hili, ukihoji haya unaambiwa unachochea, unahatarisha amani ya nchi. Alisema Amir Daud. Akasema, mwaka 1999, Halimashauri Kuu ya Waislamu, iliorodhesha madai ya Waislamu, na mapendekezo ya njia stahili ya kuchukua ili kuondoa s i n t o f a h a m u b a i n a ya Waislamu na Serikali yao, madai haya alifikishiwa kwa Rais wa wakati huo Mzee Benjamin Mkapa. Lakini Rais huyo wa awamu ya tatu, alitoa majibu kuwa matatizo ya Waislamu ni ya kihistori, hivyo alidai kuwa ina maana kwamba hawezi kuvuruga historia ya kupuuzwa Waislamu nchini. Amir Daud alikumbusha kwamba Mwaka 2011 lilifanyika Kongamano katika ukumbi wa Diamond Jubilee, lililokusanya Waislamu wa nchi nzima, chini ya Kamati Maalum ya Makongamano ya Mfumokristo. Alisema, Kamati hiyo ilitoa kitabu chenye orodha ya madai ya Waislamu, na kwamba karibia ofisi zote za Serikali zilifikishiwa kitabu hicho, kuanzia Ofisi ya Waziri Mkuu mpaka Wa b u n g e wa B u n g e l a Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mpaka leo hakuna kiongozi yeyote wa Serikali au Mbunge aliyesimama kutoa au kutaka ufafanuzi dhidi ya madai hayo ya Wa i s l a m u . S a s a k a t i k a hali kama hii unategemea Waislamu wafanye nini. Alisema Amir Daud. Alisema, madai ya Waislamu kwa ujumla ni ya msingi kwa mustakabali wa Taifa hili, lakini yanakaliwa kimya ama kupuuzwa, kisha akasema, Serikali husimama na kujinadi kuwa ni sikivu na adilifu, akahoji ni uadilifu gani huo wa kupuuza madai ya moja ya kundi katika makundi ya raia wake. Alisema, katika kadhia ya wanafunzi wa Kiislamu wa Shule ya Sekondari Ndanda, k u f u k u z wa S h u l e k wa sababu za chuki ya udini, Serikali iliwaita viongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, kuzungumzia kadhia hiyo. Alisema Masheilkh chini ya Amir Mussa Kundecha, waliitikia wito huo wakiwa na orodha

UN yamkaribisha Rais Rohani mkutano Baraza Kuu


NEW YORK Naibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Masuala ya Kisiasa, Jeffrey Feltman, amekaribisha uamuzi wa k u s h i r i k i R a i s H a s s a n R o h a n i wa Iran katika mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi ujao. Feltman amesema hayo alipokuwa akizungumza na Muhammad Mehdi Akhoundzadeh, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughuliakia masuala ya kimataifa na Sheria. Feltman pia amesifu ushirikiano wa siku za nyuma na wa sasa kati ya Iran na taasisi hiyo ya kimataifa katika kulinda mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, masuala ya wakimbizi, kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya, kushirikiana na

Urusi yatoa tahadhari kwa Marekani

Rais Hassan Rohani wa Iran. Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan na Iraq. Kwa upande wake, Akhoundzade, amesisitiza juu ya ulazima wa kuendelezwa ushirikiano wa Iran na Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro inayoendelea katika eneo la Mashariki ya Kati, hasa mgogoro wa Syria.

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

You might also like