You are on page 1of 2

;/0 Tanzania Football Federation

Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA


Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shaurimoyo Road P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815 E-mail: tanfootball@tff.or.tz . Website: www.tff.or.tz

Release No. 002 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Januari 7, 2014 SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA JAN 13 Semina ya waamuzi na makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inafanyika Januari 13 na 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ndiye anayetarajiwa kufungua semina hiyo. Wakati huo huo, Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kimemwalika Rais Malinzi kuwa mgeni rasmi kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Chuoni itakayochezwa kesho (Januari 8 mwaka huu) saa 2 usiku Uwanja wa Amaan. MAKOCHA WA LESENI B WAKABIDHIWA VYETI Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amekabidhi leseni B kwa makocha walioshiriki kozi iliyofanyika mjini Zanzibar mwaka jana. Jamhuri Kihwelo alipokea leseni hiyo inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa niaba ya washiriki wengine tisa waliofuzu mafunzo hayo. Makocha wengine waliofuzu kozi hiyo iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy Mkhonta kutoka Swaziland ni Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma Mohamed, Gulam Abdallah Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban Ramadhan, John Simkoko na Hemed Suleiman Ali. Hivi sasa Tanzania ina makocha 40 wenye leseni B za CAF baada ya wengine 31 kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika mapema mwaka juzi jijini Dar es Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza kutoka Zambia. Boniface Wambura Mgoyo Ofisa Habari na Mawasiliano

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

You might also like