You are on page 1of 2

TANGAZO

YAH: AJIRA ZA MAAFISA WATEKNOLOJIA WA AFYA (HEALTH LABORATORY SCIENTISTS) Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliwapangia Vituo vya kazi Maafisa Wateknolojia wa Afya kwa Waajiri mbalimbali nchini katika mwaka wa fedha 2012/2013. Wakati wa mchakato wa ajira ilibainika kuwa kuna baadhi ya wataalamu wa Maabara waliopangiwa kazi lakini hawana sifa za kuajiriwa kama Maafisa Wateknolojia wa Afya Daraja la II kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa mwaka 2009, Nyongeza Na. XI. Baada ya kupata taarifa hiyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliwaandikia Waajiri wote kutowaajiri wataalamu hao wa Maabara ambao hawakukidhi sifa za Muundo wa Utumishi wa Kada ya Maafisa Wateknolojia wa Afya. Kufuatia hali hiyo, baadhi ya wataalamu wa Maabara waliokataliwa kuajiriwa waliwasilisha malalamiko yao kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakidai kuwa, wanakidhi sifa za kuajiriwa kama Maafisa Wateknolojia wa Afya. Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii aliagiza Maabara ya Wataalamu wa Maabara wa Afya kukutana na wawakilishi wa wataalamu wa Maabara waliohitimu Mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine ambao ndio walioonekana kukosa sifa za kuajiriwa kama Maafisa Wateknolojia wa Afya. Kikao hicho kilifanyika tarehe 9 Januari, 2014 kikijumuisha wawakilishi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Baraza la Wataalamu wa Maabara wa Afya. Baada ya majadiliano katika kikao hicho, maamuzi yafuatayo yalitolewa; 1. Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka Vyuo vingine vinavyofanana na hivyo, hawana sifa za kitaaluma za kuwawezesha kufanya kazi katika Maabara za Afya

zinazohusika moja kwa moja na kumhudumia mgonjwa, yaani uchukuaji na upimaji wa vipimo vya mgonjwa. 2. Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka vyuo vingine vinavyofanana na hivyo hawana sifa za kisheria za kuwawezesha kusajiliwa au kupata leseni chini ya Sheria ya Baraza la Wataalamu wa Maabara wa Afya nchini. 3. Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka Vyuo vingine vinavyofanana na hivyo, wana uwezo mkubwa wa kufanya utafiti wa kisayansi katika maeneo husika na hivyo kutoa majibu ambayo yatatumika kwa madhumuni ya kisayansi na siyo kushughulika moja kwa moja na mgonjwa. Kutokana na maelezo haya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inasisitiza kuwa, wanaostahili kuajiriwa kama Maafisa Wateknolojia wa Afya ni wale wenye sifa zilizotajwa katika Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Na. 1 wa Mwaka 2009, Nyongeza XI. Kwa mujibu wa Waraka huu sifa ya kuajiriwa kama Afisa Wateknolojia wa Afya Daraja la II ni Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi katika fani ya Maabara, Radiologia, Macho, Viungo Bandia, Meno, na Dawa kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Mabaraza ya Taaluma pale inapohusika. Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni D.6(2) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009, Waajiri wanatakiwa kuwaondoa kwenye ajira walioajiriwa kama Maafisa Wateknolojia wa Afya ambao hawana sifa zilizoidhinishwa kwenye Waraka wa Maendeleo ya Utumishi wa Kada hiyo.

Katibu Mkuu WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

You might also like