You are on page 1of 2

National Team Main Sponsor

Release No. 130


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 22, 2014

TAIFA STARS KUPIGA KAMBI MBEYA
Kikosi cha Taifa Stars kinatarajia kuondoka keshokutwa (Julai 24 mwaka huu)
kwenda Mbeya ambapo kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya
marudiano dhidi ya Msumbiji.

Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki
Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika
wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai
31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya
mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa
Taifa wa Zimpeto.

MECHI YAINGIZA SHILINGI MILIONI 158
Mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas)
iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na
washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.

Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama
za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh.
74,432,095.

Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa
kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.

MUDA WA USAJILI WAONGEZWA KWA WIKI MBILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki
mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya
kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala ya Agosti 3 ya awali.

Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA

3
rd
Floor, PPF Tower, Garden Avenue / Ohio Street
P.O. Box 1574, Dar es Salaam, Tanzania . Telefax: + 255-22-2861815
E-mail: tanfootball@tff.or.tz . Website: www.tff.or.tz


National Team Main Sponsor



Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17
mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1
na 2 mwaka huu.

Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili
unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa
hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.

Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza
Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi
hiyo.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

You might also like