You are on page 1of 3

1

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Anwani ya Simu: POLISI TABORA
Fax: 026 2605489
Nambari za Simu: 026 2605478
Unapojibu tafadhali taja.

Ofisi ya:-
KAMANDA WA POLISI MKOA,
S.L.P. 23,
TABORA.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE
23/07/2014.
Ndugu waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora
linaendelea na operesheni ya kupambana na wahalifu na
wahalifu katika operesheni hiyo tumefanikiwa kama
ifuatavyo:-
KUJIFANYA ASKARI POLISI: Huko eneo la Mihogoni kata
ya Mbugani manispaa ya Tabora alikamatwa Mussa S/0 Mbeo
24yrs, mnyamwezi mkazi wa mbugani akijifanya ni askari
Polisi, baada ya kupekuliwa alikutwa akiwa na kitambulisho
feki kilichokuwa na majina ya MOSES R.KYOMO ID NO. F8452
D/C chenye picha yake. baada ya kuhojiwa mtuhumiwa
amekiri kutumia kitambulisha hicho kwa kutapeli wananchi.
Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.
KUPATIKANA NA SILAHA TATU AINA YA GOBORE. Katika
kijiji cha Kitunda kata ya Kipili wilaya ya Sikonge mkoa wa
Tabora askari wakiwa doria waliwakamata watuhumiwa
watatu ambao ni:-
1. PETER S/O PAULO, 48yrs, Mgogo, Mkulima, Mkazi Kipili Sikonge.
2. SULEMAN S/O IDDY, 19yrs, Mhaya Mkulima, Mkazi wa Kapumpa
Sikonge.
3. JUMA S/O SUDY, 46yrs, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi wa Kiwele
Sikonge.


2

wakiwa wanamiliki silaha aina ya gobore bila kibali.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya
upelelezi kukamilika.


KUKAMATWA WATUHUMIWA WA 4 NA POMBE YA
MOSHI LITA 295:- Huko wilaya kaliua na Igunga askari
wakiwa doria waliwakamata watuhumiwa wanne wakiwa na
pombe ya moshi lita 295 watuhumiwa hao ni:-
1. JOSEPH S/O SEBASTIAN, 48YRS, MSUKUMA MKAZI WA
UYUMBU.
2. MWAJUMA d/o RAMADHAN, 40YRS, MNYIRAMBA,
MKRISTO, MKULIMA WA IPUMBULIYA.
3. ROZALIA d/o SHIJA, 35YRS, MSUKUMA, MKULIMA,
MKAZI WA NKINGA.
4. ASHA d/o MARCO, 27YRS, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI
WA SIMBO.
Baada ya mahojiano watuhumiwa wamekiri kuwa ni wauzaji
wa pombe hiyo. Watuhumiwa wamefikishwa mahakamani.

KUPATIKANA NA DAWA ZIDHANIWAYO ZA KULEVYA
NA VIFAA VYA KUJIDUNGIA: - Huko maeneo ya
Chemchem na Isevya Manispaa ya Tabora waliwakamata
watuhumiwa 12 wakiwa wamejifungia ndani ya Guest House
ijulikanayo kwa jina la KENIOS baada ya kupekuliwa
walikutwa na sindano,nyembe na gram mbili ya madawa
yadhaniwayo ni heroin watuhumiwa hao ni :-

1. HAMISI S/O HATHUMANI@ MBAO, 39YRS, M/MWEZI,
MUISLAM, MKAZI WA CHEMCHEM.
2. ISSA S/O ABDALAH 22YRS MHEHE MKAZI WA
CHEMCHEM
3. ALLY S/O BAKARI 34YRS MYAO MKAZI WA NGAMBO.
4. DENSI S/O PETRO 34YRS MPOGORO MKAZI WA ISEVYA.
5. MRISHO S/O SHABANI 22YRS MNYAMWEZI MKAZI WA
CHEMCHEM.


3

6. RAMADHANI S/O MBADE 40YRS MNYAMWEZI MKAZI WA
ISEVYA.
7. HAJI S/O ABDALAH @ MUKI 40YRS MNYAMWEZI MKAZI
WA ISEVYA.
8. SAID S/O KASUMARI 24YRS MUHA MKAZI WA KIGOMA
UJIJI.
9. SHABANI S/O HARUNA 25YRS MUHA MKAZI WA KIGOMA
UJIJI.
10. DAVID S/O MALLE 43YRS MCHAGA MKAZI WA
ISEVYA.
11. RAMADHANI S/O HAMISI
12. PASCAL S/O ROBERT

watuhumiwa wakiwa wanapelekwa kituo cha polisi
waliwashawishi askari kuwapa rushwa ya Tshs 90,000/= ili
waachiliwe wasifikishwe kituoni. Baada ya mahojiano
watuhumiwa wamekiri kuwa ni watumiaji wa madawa hayo.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani muda wowote.

Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa wananchi kuzidi
kushirikiana nalo na kutoa taarifa za uhalifu na waalifu ili
kupunguza kabisa uhalifu mkoani kwetu. Pia watumiaji wa
pombe ya moshi na madawa ya kulevya kuacha mara moja
jeshi la polisi halitafumbia macho vitendo vyote vya kihalifu.

Imetolewa na:-

Suzan S. Kaganda ACP.
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.

You might also like