You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


JESHI LA POLISI TANZANIA




PRESS RELEASE
28/07/2014
MAJAMBAZI 10 HATARI WAKAMATWA NA SILAHA/BUNDUKI NANE MMOJA
MWANAMKE ANAYEJUA KUTUMIA SMG
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limefanikiwa kukamata mtandao
hatari wa majambazi wapatao kumi (10) mmoja wao akiwa ni mwanamke anayeshiriki
kikamilifu wakati wa matukio ya ujambazi. Majambazi hao wamekamatwa katika msako
mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam katika harakati za kuhakikisha kwamba maisha
na mali za wakazi wa Dar es Salaam vinalindwa kikamilifu. Katika msako huo
watuhumiwa walipekuliwa katika miili, makazi, na maficho yao na wakakamatwa na
jumla ya silaha 8 kama ifuatavyo.
1. SMG NO. 13975 ikiwa na risasi 11 na magazine 2
2. SMG 1 haikuwa na magazine na namba hazisomeki.
3. BASTOLA 1 aina ya LUGER yenye namba 5533K
4. BASTOLA 1 aina ya BROWNING yenye namba TZACR83494 S/No.7670
Na risasi 6 ndani ya magazine.
5. S/GUN PUMP ACTION na risasi 55
6. MARCK IV iliyokatwa mtutu na kitako yenye magazine 1 na risasi 4
7. BASTOLA 1 yenye namba A963858 browning ambayo ina risasi 1
8. SMG 1 ambayo iko kwa mtaalam wa uchunguzi wa silaha (Balistic)
9. SHOT GUN TZ CAR 86192 ilitelekezwa baada ya msako

Majina ya watuhumiwa ni ifuatavyo:-
1. MAULIDI S/O SEIF MBWATE miaka 23, mfanyabishara, mkazi wa Mbagala
Charambe.
2. FOIBE D/O YOHANES VICENT miaka 30, hana kazi, mkazi wa Mbagara
Kibondemaji.
3. VICENT S/O OGOLA KADOGOO miaka 30, mkazi wa Mbagara Kibondemaji
4. SAID S/O FADHIL MLISI miaka 29, dereva wa Bodaboda, Mkazi wa
Gongolamboto
5. HEMEDI S/O AWADHI ZAGA miaka 22, dereva wa Bodaboda, mkazi wa
Gongolamboto
6. MOHAMED S/O IBRAHIM SAID miaka 31, Fundi welder mkazi wa Kigogo.
7. LUCY MWAFONGO. Miaka 41, mama lishe mkazi wa Vingunguti Ukonga
8. RAJABU S/O BAHATI RAMADHANI, miaka 22, Mkazi wa Kariakoo
9. DEUS JOSIA CHILALA miaka 30, Mgonga Kokoto Kunduchi , mkazi wa Yombo
Kilakala.
10. MARIETHA D/O MUSA miaka 18, mkazi wa Yombo Kilalakala
Mwanamke pekee katika kundi hilo anayejulikana kwa jina la FOIBE D/O YOHANES
VICENT ameshiriki katika matukio ya uporaji wa kutumia silaha, mauaji, n.k. na yeye
mwenyewe alikuwa akitumia bunduki aina ya SMG. Katika baadhi ya matukio wananchi
walioshuhudia matukio haya wamekuwa wakitoa taarifa kwamba alikuwepo mwanamke
aliyekuwa akifyatua risasi na hatimaye polisi walifanikiwa kumkamata akiwa na
wenzake katika kundi hilo.
Licha ya kukamatwa kwa mtandao huu hatari Jeshi la Polisi linaendelea na misako ya
mitandao mingine ya ujambazi kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu. Hivyo
tunawashukuru wananchi kwa namna walivyoendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi
katika kutokomeza uhalifu. Majambazi hao watafikishwa mahakamani baada ya
Mwanasheria wa Serikali kupekua majalada yao ya kesi mbali mbali.
MITAMBO NA VINGORA KATIKA TAWI LA STANBIC BANK KARIAKOO
VYAWAKIMBIZA/KUWAKURUPUSHA MAJAMBAZI KABLA YA KUKAMILISHA
DHAMIRA YA KUPORA FEDHA ZA BANK
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanzisha msako mkali wa kuwatafuta
majambazi watano ambao jana tarehe 27/7/2014 saa 8.00 mchana walifika katika benki
ya Stanbic Tawi la Kariakoo lililoko mtaa wa Swahili. Watatu kati yao waliingia ndani ya
benki hiyo wakiwa na mifuko mikubwa wakijifanya ni wateja waliopeleka fedha nyingi
katika benki hiyo. Watu hao watatu walipoingia ndani walianza kulazimisha kuvuka
wigo wa wateja wa kawaida na kutaka kuingia kwa nguvu kwenda kupora fedha.
Stanbic Bank ina mitambo ya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na vingora vya
tahadhari. Vingora hivyo vilianza kulia kwa sauti kubwa nje na ndani ya benk hiyo hali
iliyowatia kiwewe wahalifu hao. Waliamua kurudi nje kwa kasi ambapo kulikuwa na gari
aina ya Noah na pikipiki moja ambazo hazikusomeka namba kwa haraka na
wakatoweka baada ya kufyatua risasi hewani na kuwatisha watu waliokuwa nje na
ndani ya Benk. Baada ya kuondoka majambazi hao iligundulika kwamba mmojawao
alichota kwa mkono kiasi cha fedha ambazo mteja alizileta kwa madhumuni ya
kuziweka katika Tawi hilo. Baada ya kutoroka majambazi hao waliterekeza mifuko
mikubwa ambayo walitegemea kubebea fedha watakazopora katika benk hiyo ambayo
imehifadhiwa kama kielelezo na ndani ya mifuko hiyo waliweka kokoto na uchafu
mwingine kwa madhumuni ya kuwadanganya walinzi na watumishi wa benk kwamba
walikuwa wamebeba fedha za kuweka benki.

Kutokana na tukio hili tunahimiza benki zote kuchukua tahadhari za kiusalama ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha kwamba wanaingia mkataba wa kulindwa na Jeshi la Polisi,
kuweka vifaa mbali mbali vya ulinzi vikiwemo vingora (alarms), CCTV Camera na
mashine za kugundua (metal detectors) mtu anapoingia na silaha au kitu kingine cha
hatari kama visu, mitarimbo n.k.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU
TAHADHARI YA KIUSALAMA KUELEKEA SIKUKUU YA IDD EL HAJI
2014.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeweka mikakati ya mpango kazi kama
ifuatavyo:-
Limepanga kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama ikiwa ni
pamoja na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni binafsi za ulinzi, Vikosi vya
uokoaji wakati wa majanga, na vikundi vya Ulinzi Shirikishi ili kuhakikisha kuna
udhibiti wa matukio ya uhalifu au fujo zinazoweza kujitokeza.

Tumejipanga kutumia Kikosi cha FFU kikijumuisha askari na magari ya
washawasha, Askari wa Mbwa na Farasi. Kikosi cha Polisi Wanamaji nacho
kitakuwepo. Pia Vikosi vya Kuzuia Dawa za Kulevya, askari wa kawaida (GD),
askari wa Usalama Barabarani, na askari Makachero. Wote hawa wamepewa
maagizo maalum ya kuchukua hatua kabla matukio ya uhalifu hayajajitokeza na
sio kungoja tukio lifanyike. Kwa mantiki hiyo, dalili zozote za uvunjifu wa amani
litashughulikiwa pasi na ajizi.

Zitakuwepo doria za Miguu, doria za pikipiki na doria za miguu katika barabara
zote muhimu.

Wananchi wanashauriwa kusherehekiea siku ya Idd El Haji katika ngazi ya familia
au kukusanyika katika mitaa kwa amani wakisherehekea.

Aidha kutokana na sababu za kiusalama na matishio mbalimbali katika ukanda
wa Afrika ya Mashariki, Jeshi la Polisi limepiga marufuku disko toto katika kumbi
mbalimbali kutokana na sifa za kumbi hizo kutokidhi viwango vya kiusalama.

Wananchi wanapoona dalili zozote au maandalizi ya uvunjifu wa amani watoe
taarifa mapema iwezekanavyo katika vituo vya Polisi vya karibu ili hatua
zichukuliwe kwa haraka.

Madereva wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja
na kutoendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi, wasiwe walevi, magari au
pikipiki zenye sauti kali/zenye kuleta mshtuko nazo ni marufuku.

Aidha, Kikosi cha Polisi Wanamaji (Marine Police) kitafanya doria kwenye fukwe
za Bahari na maeneo yote ya Bahari jijini Dar es Salaam. Patakuwepo Helkopta
ya Jeshi la Polisi ikifanya doria kuzunguka jiji la Dar es Salaam na askari wa
Kikosi cha Mbwa na Farasi nao watahusika na doria.

Polisi watatoa ulinzi katika fukwe za bahari, kwa kuweka vituo vya Polisi vya
muda vinavyohamishika (Mobile Police Station) ili kutoa msaada wa haraka pindi
unapohitajika. Pia askari wa kutosha watakuwepo kuhakikisha wananchi
wanasherehekea kwa amani.

Aidha, kwa urahisi wa mawasiliano wananchi wasisite kutoa taarifa za uhalifu
kwa namba muhimu za simu zifuatazo:
1. RPC ILALA: Mary Nzuki SACP 0754 009 980 / 0754 339 558
2. RPC TEMEKE: Kihenya wa Kihenya SACP 0715 009 979/ 0754 397 454
3. RPC KNDONI: Camillius Wambura ACP 0715 009 976 / 0684 111 111


NAWATAKIA NYOTE HERI YA IDD EL FITR 2014.


S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

You might also like