You are on page 1of 3

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge unatarajiwa kuanza Jumanne tarehe 27
Januari 2015 na kumalizika tarehe 7 Februari 2015 Mjini Dodoma. Shughuli
zitakazokuwepo katika Mkutano huo ni kama ifuatavyo:
1.0 KIAPO CHA UTII
Kwa mujibu wa Kanuni ya 24, katika Mkutano wa Kumi na Nane wa
Bunge kutakuwa na Kiapo cha Utii kwa Mbunge ambapo Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, (Mb) ataapishwa baada
ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Mwita Werema.
2.0 MISWADA YA SHERIA YA SERIKALI:
Aidha, kwa Mujibu wa Kanuni ya 86 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,
jumla ya Miswada Mitatu (3) itasomwa na kupitishwa na Bunge. Miswada
hiyo ni:

(i) Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014


[The Tax Administration Bill, 2014] (Kupigiwa kura tu).
(ii) Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2013[ The
Statistic Bill, 2013] (Kamati ya Bunge zima na Kusomwa
mara ya Tatu)
(iii) Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa
Mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous
Amendments) (No. 2) Bill, 2014]
3.0 TAARIFA ZA CAG:
Pamoja na Miswada hiyo, Bunge pia litajadili Taarifa za Mdhibiti na
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi
na Tano wa Bunge kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Serikali
za Mitaa na Mashirika ya Umma kwa mwaka 2012/2013, ambapo pia
Serikali itatolea majibu baadhi ya Hoja.
4.0 TAARIFA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE
Kwa kuzingatia Kanuni ya 117 (15) katika Mkutano wa 18 wa Bunge,
Kamati za Bunge zitapewa nafasi ya kuwasilisha Taarifa za Mwaka za
Shughulii za Kamati na zitapangiwa muda wa kujadiliwa kwa kadri Spika
atakavyoelekeza.
5.0 TAARIFA YA KAMATI TEULE
Aidha, Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza na kuchambua
Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, Kilimo, Mifugo Maji na
Uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matuymizi ya Ardhi itapewa
nafasi ya kuwasilisha Taarifa yake, ambapo taarifa hiyo itajadiliwa
Bungeni.

6.0 MASWALI:
Jumla ya Maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa
ambapo ni wastani wa Maswali 15 kwa siku na maswali 10 kwa siku za
Alhamisi. Aidha katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuuinatarajiwa
kuwa jumla ya

Maswali 18 ya msingi yataulizwa na kujibiwa na Mhe.

Waziri Mkuu.
Aidha, Kamati ya Uongozi imefikira pia ratiba ya Mkutano wa kumi na tisa (19)
na Ishirini (20) ambapo imependekezwa kuwa Mkutano wa Kumi na tisa
utajadili Miswada yote ya Serikali iliyosomwa kwa mara ya kwanza na miswada
mingine itakayoonekana kuwa na umuhimu kabla ya Bunge kuvunjwa.
Mkutano huo wa Kumi na Tisa utafanyika tarehe za Katikati ya Mwezi Machi na
Kumalizika Mwanzoni mwa Mwezi Aprili, ambapo Mkutano wa Ishirini wa Bajeti
utafanyika tarehe za Mwanzoni mwa mwezi Mei na kumalizika tarehe 30 Juni
2015.
Ratiba Kamaili ya Mkutano wa Kumi na Nane (18) ya jinsi shughuli
zitakavyowasilishwa itatolewa mapema na kuwekwa katika Tovuti ya Bunge
ambayo ni www.parliament.go.tz

Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi Ndogo za Bunge
DAR ES SALAAM
22 Januari 2015

You might also like