You are on page 1of 1

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo : N G O M E
Simu ya Mdomo : DSM 22150463
Telex
: 41051
Tele Fax
: 2153426
Barua pepe
Tovuti

Makao Makuu ya Jeshi,


Sanduku la Posta 9203,
DAR ES SALAAM, 27, FEB15

Taarifa kwa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa
taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27
Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,
Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo
ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha
ndegevita kuwaka moto.
Hata hivyo, rubani wa ndgevita hiyo Meja Peter Lyamunda
alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya
ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa
maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa
kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya
kawaida .
Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na
shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta
madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundo mbinu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0783-309963

You might also like